KARATA YA MAUAJI
KARATA YA MAUAJI
NI KIPI SIASA IMETUAHIDI? KIFO, UKOMBOZI AU MAPINDUZI? KUWA SEHEMU YA HISTORIA YA UHURU WA MAPINDUZI YA KISIASA. KARATA YA MAUAJI ✅ Kwenye ulimwengu wa kibebari dunia haina ukoloni tena wa watu weupe kutawala sehemu mbali mbali za dunia watu weusi ndio ambao wanawatawala wenzao lakini kwenye utawala wa hawa watu sio kila mtu anapendezwa na mambo ambayo wanayafanya. Tanzania ilikuwa ni moja ya mhanga wa jambo hili. Ilikuwepo serikali ambayo ilikuwa inatawala kwa mabavu na kufanya yale ambayo wahusika waliona kwamba yanawafaa kwa maslahi yao binafsi. Watu wengi hawakuwa wanajali huenda kwa sababu hawakuwa na taarifa juu ya nini kinaendelea chini lakini kwenye kundi kubwa la watu wasiojali huwa kuna watu kadhaa wenye kujali kuhusu taifa lao. Tanzania ilikuwa inaendeshwa na watu kadhaa ambao walitengeneza mfumo wa kutawala milele ndipo wakaibuka watu wa siri ambao walihitaji kubadilisha mfumo huo wa kidhalimu kwa kuhitaji kumuweka madarakani kiongozi wa upinzani kwa sababu waliona ndiye ana mwelekeo sahihi na mfumo wa watawala wa chama tawala unatakiwa kuondolewa madarakani kwa nguvu. Kwahiyo watu hao wakaanzisha umoja wa siri kuweza kufuta jumla mfumo wa serikali ila wamuweke kiongozi wa chama cha upinzani madarakani kwa mara ya kwanza. Jambo hili linasababisha machafuko makubwa na mauaji ya watu wengi ndani ya nchi akiwemo mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa na mkuu wa majeshi mwisho wa siku CIA wanahusika Moja kwa Moja ndipo jambo hili linachukua sura mpya Tanzania inaingia gizani na kwenye umwagaji wa damu. KARATA YA MAUAJI- Sio simulizi tu bali unaenda kuyaishi maisha ya KISIASA kwenye ulimwengu wa kufikirika, unaenda kuwa moja ya sehemu ya fikra za ULIMWENGU wa kutisha wa kisiasa hivyo isome simulizi hii ili ujue nini hatima ya maisha yako ya kisiasa kwenye dunia ya kufikirika. Mawasiliano yangu ya WhatsApp na kawaida ni +255621567672 Email: [email protected]
295
50

CH

ongoing
Chaguo langu ni wewe
Chaguo langu ni wewe
Simulizi kutoka kwa Tatu Kiondo
458
1

CH

ongoing
Passpoti ya Gaidi
Passpoti ya Gaidi
Simulizi kutoka kwa mtaalamu Richard Mwambe
466
1

CH

complete
Kitanzi cha mwisho
Kitanzi cha mwisho
Simulizi kutoka kwa Halfan Sudy only preview chapter
242
1

CH

ongoing
Queen Monica
Queen Monica
Simulizi kutoka kwa mtunzi mahili patrick Ck.
274
1

CH

ongoing
Farida
Farida
Imeandikwa na Halfani Sudi chanzo internet archives.
253
1

CH

ongoing
Vipepeo weusi
Vipepeo weusi
Simulizi hii imeandikwa na Habib B Anga
227
1

CH

ongoing
Bahari ya Hindi
Bahari ya Hindi
Simulizi hii ni kutoka kwa mwandishi Yonna source internet archives
423
4

CH

complete
Gamboshi
Gamboshi
soma simulizi ya kijini imeandikwa na mtunzi ERICK SHIGONGO
460
1

CH

complete
Fumbo
Fumbo
PUA za Leila ziliipokea harufu ya manukato iliyopozwa na kiyoyozi, mara baada ya kufungua mlango na kuingia ofisini. Chini, sakafu ilifichwa na zulia la sufi. Juu, taa zenye rangi anuwai zililizunguka dari mithili ya nyota zipendezavyo anga. Nusu ya kila dirisha ilifunikwa kwa mapazia ya rangi ya samli ilhali nusu ya pili ikikingwa na vioo. Mvuto wa ofisi na umaridadi wa samani zake, vilipambanua haiba na tajriba ya bosi anayeimiliki. Alitembea taratibu, akiyapita makochi yaliyopangwa kwa kuizunguka meza ya vioo katikati ya ofisi. Mama Mbegu alikuwa ameketi nyuma ya meza ya duara, akiendelea kuperuzi kompyuta yake. Hata Leila alipomsabahi, bado hakujikalifisha kunyanyua uso wake, aliishia kuitika salamu hali macho yameganda kwenye kioo cha kompyuta. Leila akiwa amesimama asijue la kufanya, ndipo aliinua uso, akivua miwani na kuitenga mezani, na kwa mkono wake wa kushoto akamwashiria aketi. Kisha, akajitengeneza wigi lake, lenye mchanganyiko wa rangi nyeusi na kahawia, lililofunika kichwa pamoja na masikio, na kushuka hadi usawa wa mabega. Alipomaliza, akavitenga viwiko vya mikono juu ya meza kiasi cha kufanya bangili na pete za dhahabu kumeremeta. Leila alivuta kiti kimoja, kati ya viwili vilivyopangwa mbele ya meza. Hata baada kuketi, bado alijihisi kama bado amesimama. Mapigo ya moyo yalimgomea kutulia. Kitendo cha kuitwa ofisini na mama Mbegu, ilikuwa ni sawa na mwanafunzi kuitwa na mwalimu wa nidhamu ofisini – ambapo kwa kawaida huwa haiingi yeyote bali kuna walakini. “Enhe, una matatizo gani na Seba?” mama Mbegu alimrushia swali. Japo sauti yake ilikuwa tulivu na isiyo papara, walakini ilijaa shari. “Hakuna tatizo, bosi,” Leila alijibu kwa indhari, huku akiminya macho yake kiudadisi. Mama Mbegu alipandisha nyusi juu huku macho yake makubwa yaliyokolea wanja wa chini, akiyazungusha tamthili ya mtoto mwenye degedege. “Unajua, muda niliopanga kuzungumza nawe ni dakika tano tu,” alisisitiza huku akiinua mkono kutazama saa, “na mpaka sasa umekwishatumia dakika mbili. Sasa, usipokuwa makini, nazo zitakwisha kabla sijajua cha kukusaidia. Umenipata?” “Ndio bosi.” “We ndiye msaidizi wa Seba, na mlipaswa mwende pamoja Kanada, kikazi. Nimeambiwa uligoma kusafiri naye, na bado unasema hakuna tatizo!” Kimya kifupi kilitanda wakati wakitazamana. Leila aliinamisha macho chini, akihisi baridi ya hofu ikimzizima maungoni. Hakuwa amepanga kumwambia mtu yeyote kuhusu chochote baina yake na Sebastian. Lakini kwa kuhofia kisirani cha mama Mbegu, alifunua kinywa, “Seba amenikasirikia, bosi.” Mama Mbegu aliachia ucheko hafifu, japo sauti iliyotoka haikuwa ya cheko halisi, bali ni kama madebe mabovu yaliyonyeshewa mvua. “Kwa hiyo unasubiri nikuulize hadi sababu ya ugomvi wenu?” “Hapana, bosi,” Leila alijibu haraka na kuendelea, “Seba alianzisha tabia mbaya. Kila mara alipoingia ofisini, alianza kunishikashika bila ridhaa yangu. Nikamwambia sipendi hiyo tabia. Akaacha. Ghafla, siku hiyo nilikuwa nimeinama kabatini nachuk–” “Eh! Eh! Makubwa haya,” mama Mbegu alidakia huku tabasamu la ugwadu likijijenga usoni mwake. “Kwa hiyo mwenzetu kushikwa tu mpaka uandikiwe barua ya maombi?” Kama ipo walau chembe ya aibu machoni mwa mama Mbegu, ingelihitajika darubini kuweza kuiona. Leila alipoinua uso kumtazama kwa tahayari, alikutana na uso mkavu usio na soni. Akaishia kuvuta pumzi nyingi na kuzitoa taratibu. “Lakini bosi, nilikwishamweleza na akanielewa. Mimi ni mke wa mtu. Mume wangu akijua itak–” “Atajuaje? Utaenda kumwambia? Au amekufunga Bluetooth mwilini?” Leila hakujibu. Akainamisha kichwa chini. Mama Mbegu aliinuka kitini. Akasimama na kujitengeneza kivazi chake; blauzi ya rangi ya hudhurungi iliyodariziwa kwa riboni za kahawia, na kubandikwa vishikizo vyeusi vilivyofunikwa kwa papi pana juu yake, viliupendezesha mwonekano wake. Sketi ya rangi ya damu ya mzee, iliyoishia juu ya magoti iliruhusu miguu yake minene kuonekana vizuri, kadri alivyopiga hatua kuelekea kwenye korido ndefu iendayo maliwatoni. Alipoifikia meza ndefu ya mninga iliyobanwa ukutani kando kando mwa korido, alisimama na kushika chupa ya chai. Akajimiminia kahawa kwenye kikombe kidogo. Akarudi nayo mezani. “Seba anarudi leo usiku, na kwa taarifa nilizonazo, tayari anayo barua yako mkononi,” alisema huku akiweka kikombe cha kahawa mezani. “Hakuhitaji tena kazini.” Leila alihisi misuli ya tumbo ikikakamaa. Ngurumo mithili ya radi zilirindima tumboni mwake. Taratibu, jasho likaanza kutengeneza chemchemi makwapani. “Bosi nakuomba nisai–” Mama Mbegu alimnyooshea kiganja kumzuia asiendelee kuzungumza. Akaketi na kusema, “Unaelewa namna nifanyavyo kazi na Seba. Hatuingiliani kwenye maamuzi. Nilipokutafutia nafasi ya kazi, nilimsisitiza mama Mainda akwambie kuwa, jukumu la kuipigania na kuilinda nafasi yako si langu tena. Nadhani alifanya hivyo. So, sitokuwa na mahali pengine pa kukupachika endapo Seba ameamua kukutimua.” Leila alimeza funda la mate na kufanya koromeo lake kucheza saka-mke-wangu. Ndani ya muda mfupi, tayari uso ulimshuka mithili ya mbuzi anayesubiri kuchinjwa. Tangu mzee Dominic Mbegu, mmiliki wa kampuni ya Crops Investment Limited, alipougua kiharusi na kushindwa kutimiza majukumu yake, mama Mbegu kwa kushirikiana na Sebastian Mbegu, mdogo wake mzee Mbegu, walisimamia na kuendesha kampuni. Mafanikio ya kampuni chini ya usimamizi wao, yalichagizwa na namna walivyolindana na kwa kila mmoja kuchunga mipaka waliyowekeana. Mama Mbegu akaendelea, “Leila, bahati ikibisha hodi mlangoni, unainuka kwenda kuifungulia – usisubiri hadi na mlango ijifungulie.” Leila aliinamisha kichwa huku mikono ameifumbata mapajani wakati mama Mbegu akizungumza. Alipoinua kichwa kutaka kusema neno, tayari alikuwa amechelewa.
222
1

CH

complete
Jinsi jini lilivyonitumia kumwaga damu
Jinsi jini lilivyonitumia kumwaga damu
Ulikuwa ni usiku wa manane, usiku ambao nilijikuta nipo makaburini peke yangu huku nikiwa sina nguo hata moja. Nilikuwa uchi wa mnyama. Niliitazama maiti iliyokuwa mbele yangu juu ya kaburi moja ambalo sikuweza kulifahamu kuwa lilikuwa ni kaburi la nani. Kutokana na uchakavu wake, yawezekana muhusika alizikwa miaka mingi iliyopita. Maiti ile Ilikuwa ni ya mwanamke nisiyemfahamu aliyeonekana kujeruhiwa vibaya kwa kukatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake. Ile damu iliyokuwa ikiendelea kuchirizika mahali pale iliweza kunithibitishia kuwa muuaji aliyefanya mauaji yale bila shaka aliyafanya muda mfupi uliopita. Hofu kubwa ikaanza kunitawala moyoni na kila nilipojaribu kuyakwepesha macho yangu yasiendelee kuishuhudia maiti ile nilishangaa kuona macho yakiendelea kuishangaa tu bila kutoka. Ghafla! Mingurumo pamoja na sauti za ajabu zikaanza kusikika mahali pale. Sikujua sauti zile za kutisha zilikuwa zinatokea wapi ila kwa uwoga wangu nikajikuta nimeketi chini huku nikijaribu kuyaziba masikio yangu yasiendelee kuzisikia sauti zile za ajabu. Lahaula! Haikuwa kama nilivyotegemea, badala ya masikio yangu kuyazuia yasiweze kuzisikia sauti zile za ajabu sasa ikawa kama ndiyo nimezikaribisha sauti zile walau ziweze kusema chochote. “Haaa! Haaa! Haaa! Haaa!” nilizisikia sauti za watu zikicheka huku zikiwa zinajirudiarudia masikioni mwangu. Ghafla! Nikaanza kukisikia kishindo cha mtu ambaye alikuwa akitembea kuja mahali nilipokuwepo. Nilipogeuka kumtazama huyo mtu aliyekuwa ananifuata ajabu sikumuona. Nikazidi kuogopa mno! Kijasho chembamba kikaanza kunitoka huku nikitetemeka kwa hofu. Sikujua nilikuwa mahali pale kwa lengo gani na ni kwa nini nilikuwa nikiishuhudia ile maiti ikiwa juu ya kaburi huku ikiwa inachirizika damu. Wakati nilipokuwa nikishangaa kuwepo mahali pale hasa katika nyakati kama zile za usiku mara nikamuona kwa mbali mwanamke mmoja ambaye alikuwa akinifuata huku akiwa amevaa sanda iliyokuwa imeufunika mwili wake kasoro sehemu ya uso wake tu. Alitisha mno kutazama hasa katika giza lile. Nikatamani kukimbia lakini kila nilipojaribu kufanya hivyo nilishindwa. Aliponikaribia, aliniita jina langu kisha akaanza kucheka huku sauti ya kicheko chake ikijirudiarudia kama sauti ya mwang’wi. “Wewe ni nani na umenijuaje jina langu?” nilimuuliza kwa sauti ya hofu huku nikimsihi asinidhuru. “Haaa! Haaa! Haaa! Haaa! naitwa Mulhaty,” alijitambulisha kisha akaunyoosha mkono wake wa kulia kuielekezea ile maiti iliyokuwa imelala juu ya kaburi halafu akawa kama kuna maneno anayanena kwa sauti ya chini ambayo sikuweza kujua ni maneno gani. Niliushuhudia mwanga mkali ukitokea katika mkono wa Mulhaty ukielekea mahali maiti ilipo. Ni kama kitendo cha dakika mbili nikashuhudia maajabu mengine tena. Ile maiti ikatoweka juu ya lile kaburi. Sikumbuki ni nini kilitokea ila nilijikuta nikitokea sehemu nyingine kabisa tofauti na pale makaburini tulipokuwa. Nikabaki kinywa wazi huku nikiendelea kuishangaa miujiza ambayo katika maisha yangu sikuwahi kuwaza au kutegemea kama kuna siku nitakuja kuishuhudia kwa macho yangu.
215
1

CH

complete
MNYORORO WA DAMU
MNYORORO WA DAMU
HADITHI: MNYORORO WA DAMU MTUNZI: RAJONCE JOHN WHATSAPP:0673049321 UMRI: 18+ SEHEMU YA KWANZA. Mvua kubwa yenye ngurumo na radi nzito zenye kuogofya ziliunguruma zikionesha hasira kali yenye kumtafuta wa kummeza, radi zilipiga kwa sekunde na kuliacha giza litawale kisha zilirejea na kupiga upya, hazikutoka patupu kwani zilipasua vipande vipande miti mirefu ndani ya msitu mkubwa wa asili wa Tabo, katika hali hiyo ya hewa mbaya na giza lenye kutisha alionekana mwanamke mmoja akiwa amebeba mtoto mkononi. Mwanamke huyu alikuwa amelowana mwili mzima kutokana na matone mazito ya mvua ambayo hayakuonesha huruma yeyote juu yake, yalimchapa kisawasawa, hakuwaza kusimama akili na moyo bado vilimdai kwenda mbele zaidi ili kujiokoa yeye na mwanae, hakujua ni wapi anaelekea lakini hakuacha kwenda, miiba ilimchoma miguuni na kumwachia maumivu makali lakini bado aliendelea kwenda, katikati ya msitu huu hakuwa na mwingine wa kumlilia msaada zaidi ya Mungu wake, machozi yalimtiririka lakini hayakufika hata mashavuni yalichanganyikana na matone ya mvua kali iliyokuwa inapiga, licha ya kumkumbatia kwa nguvu mwanae ili kumwongezea joto, bado mtoto aliendelea kulia na kukohoa, kikohozi kikavu kutokana na baridi kumwingia kwenye mapafu, mwanamke huyu na mtoto aliembeba mkononi walikuwa kwenye wakati mgumu sana. Akiwa katika hali ya hofu kuu, akihema kwa nguvu mpaka kudunda kwa mapigo ya moyo wake aliyasikia kwa ukubwa, aliamua kujihifadhi chini ya mti ambao ulikuwa na matawi mengi na makubwa yaliyobana vizuri, angalau matone ya mvua yalikuwa yanashuka kwa idadi ndogo, bado baridi iliwatetemesha yeye na mtoto wake. "Si unasikia sauti ya mtoto akilia, atakuwa hapa hapa, hajaenda mbali huyu mwanamke" "Tuharakishe tumkamate, ni lisaa limoja limebaki kufikia saa nane usiku muda wa kutoa kafara" "Pita kulia, mimi napita kushoto kwa yeyote atakae mwona hakikisha hatuponyoki tena" "Sawa sawa" Maongezi ya watu hao yalisikika kwenye masikio ya mwanamke huyu, watu hao ndio walikuwa wanamtafuta yeye na alitakiwa kukamatwa kabla ya kufika muda wa kutoa kafara, kwamba yeye ndio kafara yenyewe aiseeh haya tuone. Maneno yalikuwa makali yalipenya moyoni kama mkuki wa moto, alimtazama mwanae alimwonea huruma,hakupaswa kupitia haya aliyokuwa anapitia, hakutaka kuliruhusu wazo la kukubali kujikamatisha kirahisi kwani hilo halikua na mwisho mzuri kwake wala kwa mtoto aliembeba, alimbeba vizuri mtoto na kuchomoka mbio bila kutazama nyuma, kishindo cha miguu yake kiliwashtua watesi wake, walijua ni mwendo wa mchakamchaka nao walianza kumfuatia kwa nyuma, alikuwa akikimbia kwa kubana vidole vyake kwa nguvu juu ya ardhi, akijizuia kuanguka baada ya kuteleza, mbinu hii ilimsaidia kusogea mbele zaidi tofauti na watu waliokuwa wakimfuata kwani walianguka zaidi ya mara tatu na wao walisimama juu na kuendelea kumkimbiza. Mwanamke alikuwa makini kuipekenyua njia kwani kosa moja, angejikuta mikononi mwa watu hao wabaya ambao alikuwa akiwakimbia kwa nguvu zake zote, milio ya magari iliongezeka kila alipokuwa anakimbia, akili ya haraka ilimtuma kwamba ameikaribia barabara, mwanga wa matumaini ulijipenyeza katikati ya ufa mdogo, baada ya hatua kumi na tano, tayari alikuwa barabarani akiwasihi madereva wa magari yaliyokuwa yanapita kwenye barabara hiyo wasimame na waweze kumpatia msaada, hakuna dereva ambae alijaribu kukanyaga breki na kusimama kutoa msaada kwenye pori hilo, macho na akili zao ziliwatuma kuwa huo ni mtego, hakuna ambae alitamani wema wake ugeuke majuto ya kudumu kwenye maisha yake, mwanamke huyo alichorwa picha ya haraka kuwa ni sehemu ya mpango mwovu wa majambazi, hivyo madereva walizidi kuongeza mwendo na kulipita eneo hilo pasipo kutazama nyuma. Mwanamke aliamua kujitosa katikati ya barabara aliamua kuchagua kifo cha kugongwa na gari, ikiwezekana yeye na mwanae wafe mara moja kuliko kuangukia kwenye mikono ya watu waliokuwa wanamkimbiza, kama madereva wa magari walishindwa kumwokoa kwenye hiyo hatari bhasi wamwokoe kumuwaisha kaburini. Hii ilikua nukta ya mwisho ya maamuzi magumu. Watu watatu waliovalia makoti marefu meusi yaliyoficha mpaka vichwa vyao, walishangazwa na maamuzi hayo, walitamani kuwapata wawili hao wakiwa hai lakini hakuna aliekuwa tayari kuingia katikati ya barabara kuwaokoa na kwenda kuwafanyia kile ambacho walitaka kukifanya, waliishia kupunga mikono wakimsihi dereva wa gari aliekuwa katika mwendo wa kishada afanye namna ya kuwakwepa wawili hao. Gari lililokuwa linakuja, dereva wake alikanyaga breki ya haraka, gari lilikuwa kwenye mwendokasi liliseleleka, mwanamke alifumba macho kupokea matokeo ya maamuzi yake lakini gari lilisimama sentimeta chache na halikumgonga, mwanamke aliachia pumzi mzito baada ya kugundua bado yuko hai alianza kuomba msaada hapo hapo, watu wenye makoti walimfikia haraka, walimkamata na kuanza kumvuta kumpeleka ndani ya msitu, mwanamke huyu aliendelea kulia huku akiomba msaada kwa watu waliokuwa ndani ya gari. Gari ilisogezwa pembeni ya barabara kidogo, kisha mlango wa kushoto wa gari ulifunguliwa, lilitangulia buti refu kisha ulifuatia mwili, alikuwa mwanaume, miguu yote miwili ilipokuwa chini, alikuwa anawatazama watu hao, alitembea hatua ndefu ndefu za haraka alipowakaribia watu hao, waligeuka nyuma mmoja alikuwa amemkamata mwanamke na wawili walichomoa visu virefu kwa lengo la kumkabili mtu huyo ambae aliingia kati akitaka kuicheza ngoma, walikuja wawili kwa kasi wakijiona wana uwezo na nguvu ya kumkabili mtu huyo na kumtoa kiherehere chake, pambano lilikuwa kati, walikuja na kurusha mikono yao yenye visu, alikwepa mkono mmoja na mwingine aliukamata kwa nguvu, aliukunja kwa nguvu na kuupeleka zaidi ya mahali pake pa kuhimili. "Paaaaaaaaaa" sauti ya kuvunjika kwa mfupa ilisikika ikiambatana na ukelele wa maumivu alivutwa mbele alisogea alipigwa kikumbo kizito alianguka chini na kuramba matope, mwingine alitaka kutumia mwanya wa kugeuziwa mgongo alikuja kwa lengo la kumchoma kisu mgongoni, zoezi lilishindikana mwanaume alikuwa na hisia kali zenye kunusa hatari unaweza zani ana macho kisogoni alimuwahi kwa kumkamata mkono kisha alipeleka kwa nguvu kichwa chake kilitua kwenye uso wa jamaa, kofia ilivuka, mwanaume hakumwachia aliendelea kumpelekea vichwa mara tatu, jamaa alidebweda alipoachiwa alikwenda chini moja kwa moja. Mwanamke alianza kujiondoa kwa nguvu mikononi mwa aliemshikia kisu, ulikuwa ni mwendo wa kushindana nguvu, mwanamke alisukumwa kwa nguvu na kuanguka chini, mtoto hakuwa mikononi mwake, jamaa lilimfuata mtoto na kumkamata mkononi. "Shemeji tafadhali sana naomba usimuue mtoto wangu nakuomba, nakuomba sana shemeji angu" mwanamke aliomba akiwa amepiga magoti mbele ya aliemwita shemeji. Alieitwa shemeji hakujibu bali alizungumza maneno kwa lugha ambayo aliifahamu yeye kisha alipeleka kwa nguvu kisu kwenye upande wa kushoto ulipo moyo wa mtoto, alikiingiza kisu chake kwa nguvu sana. Kisha alimtupa mtoto chini baada ya kuona yule mwanaume alieshuka kutoka kwenye gari alikuwa anamfuata kwa kasi yenye hatua ndefu ndefu. Jamaa alianza kukimbia pasipo kutazama mbele, alijikwaa kwenye mzizi wa mti, alianguka chini, tayari mwanaume alimfikia, mkononi alikuwa na kisu. "Nitakupa pesa zozote utakazo, tafadhali usiniue, naomba usiniueeeeeeee" jamaa aliomba, pasipo kukumbuka dakika chache zilizopita aliombwa kwa maneno hayo hayo lakini alijifanya kiziwi asiesikia. Mwanaume alimkamata kwa nguvu alimshusia ngumi tatu nzito kisha alimpelekea kisu shingoni, kisu kilitokea upande wa pili wa shingo, alitupa tupa miguu na kufa. "Tuondokeee" mwanaume alimwambia mwanamke akiwa ameubeba mwili wa mwanae akilia, mwanamke alikuwa akimtazama tu, hakuwa na nguvu zozote. "Naomba uniue, nataka kufaaaaa, nataka kumfuata mwanangu, niueeeeeeeeeee eeeeeeh eeeh" mwanamke huyo alilia sana, katikati ya kilio alikuwa anaongea maneno yenye uchungu, alikuwa amelala huku akiwa amemkumbatia mwanae kwa nguvu, hakuona sababu ya kuendelea kuishi kama amempoteza mtoto ambae alifanya kila namna kukimbia umbali mrefu ili aweze kumwokoa lakini imeshindikana na wabaya wake wamefanikiwa kupita na maisha ya mtoto. Mwanaume aliubeba mwili wa mtoto kisha alimfuata mwanamke huyo alimkamata mkono kwa nguvu na kwenda nae mpaka kwenye gari. Dereva wa gari aliwasha gari na kuondoka mahali hapo kwa kasi. Walifanikiwa kumwokoa mwanamke lakini hawakuweza kuyaokoa maisha ya mtoto, mwanamke alikuwa analia wakati wote, kwa pamoja walimwonea huruma mama huyo lakini hakuna alieweza kumsemesha kitu, walimwacha aendelee kulia angalau ashushe machungu aliyobeba moyoni. “kumbe ni wewe nishusheni nasema nishusheni” mwanamke huyo alianza kupiga kelele kama mtu aliechanganyikiwa baada ya kuiona sura ya mtu aliemsaidia hakutaka kuendelea kukaa ndani ya gari hilo, alipiga kelele huku akiupiga mateke mlango wa gari ili ufunguke. Licha ya kufanya hayo si dereva wala alietoa msaada ambae alifungua kinywa chake na kuzungumza, kwanini mwanamke huyu alipiga kelele namna hiyo na huyo mwanaume ni nani kwenye maisha ya huyo mwanamke. Mpendwa msomaji majibu yetu yote yanapatikana ndani ya sehemu ya pili ya kigongo hiki kipya kabisa kinachokwenda kwa jina la Mnyororo wa damu, mwandishi wako ni mimi Rajonce John.
383
1

CH

complete
Penzi La Kweli Lilio Msurubisha Hansi😔💔
Penzi La Kweli Lilio Msurubisha Hansi😔💔
Ni Simulizi Ya Maisha Yangu Halisi Nilye Poteza Kila Kitu😔 Hadi Kumkosea Mungu Wangu💔 Lakini Nikageuza Maumivu Kuwa Nguvu Yamafanikio😎
376
2

CH

ongoing
DYLAN
DYLAN
Hadithi ya maisha ya mwanaume kijana anayerudi nyumbani kutoka masomo nje ya nchi. Anakutana na visa vingi ndani ya familia yake vinavyopelekea awekwe katikati ya migogoro na matukio yenye kuvuruga amani anayohitaji ili moyo wake utulie.
504
43

CH

complete
RAHA IKO KILELENI
RAHA IKO KILELENI
Simulizi ya Kijasusi Ambayo chanzo kikuu cha yote ni Mapenzi
615
6

CH

ongoing
KIZAZI DHALIMU
KIZAZI DHALIMU
Kisa ni kati ya vijana wa wawili wa kike wanaomshindania kijana mmoja wa kiume
674
20

CH

complete
THE JOURNALIST
THE JOURNALIST
AMANI KILONZO!!!!!... Ni jina ambalo lilikuwa alama ya ushindi, lilikuwa ni jina maarufu ambalo kila mwandishi wa habari pamoja na waandishi wote walikuwa wakilichukulia kama jina la mfano. Jina maarufu kutoka kwa mwanaume aliyetokea kwenye maisha ya kimasikini haswa, familia ambayo haikuwa na uhakika hata wa kula mlo mmoja tu ndiye ambaye alikuwa shujaa wa habari Tanzania. AMAN KILONZO alizaliwa yeye na dada yake tu EPIPHANIA KILONZO. Mwanaume huyu alikuwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi, mzalendo na mtu aliye lipenda mno taifa lake hivyo hakuwa tayari kuvumilia ushenzi na ukatili wa mamlaka jambo ambalo lilipelekea yeye kuripoti na kudai alikuwa na ushahidi wa mauaji ya watu ishirini na sita ambayo yalifanyika ndani ya hifadhi ya taifa ya Mikumi, Morogoro. Hiyo ilikuwa safari nzuri ya kufa kwake kwa sababu nyuma ya hayo, kulikuwa na Siri nzito ambazo hakupaswa kuwa nazo ila kwa bahati mbaya alizipata. Alishuhudia mdogo wake akiwa mfu, mwanamke asiye na nguo hata moja kwenye mwili wake baada ya kubakwa. Kama kaka aliapa kuwashughulikia wale wote ambao walihusika na ushenzi huo ila kwa bahati mbaya hata yeye baada ya hapo hakuwahi kuonekana tena mpaka ulipo okotwa mwili wake. Kupotea kwake kulianzisha safari nyingine ya mwandishi WILLIARD NZITU ambaye aliandika kitabu kiitwacho TONE LA DAMU, kitabu hicho baada ya kutoka tu kilipigwa marufuku na serikali na wale wote ambao walikinunua waliuawa lakini kuna mtu mmoja alifanikiwa kubaki na nakala moja akaificha vizuri kwa siri. Sababu za kufungiwa kitabu hicho ni Williard kuandika siri za mambo ambayo yalifanya role model wake AMAN KILONZO kuweza kuuliwa hivyo hata yeye hakuwa Salama kwa watu hao. Uhatari ambao aliutengeneza ulikuwa mbaya kwake, jina lake lilikuwa zaidi ya kirusi hivyo hata yeye alitakiwa kupotezwa. Baada ya waandishi hao wawili nguli kupotea, ilipita miaka mitano ndipo akaibuka mwandishi mwingine, bwana huyu alitafutwa na watu wasio julikana ambao walimpatia siri nzito ambazo zingemfanya kuingia kwenye maisha ya hatari tofauti na yale aliyokuwa anayaishi mwanzo. RASHID MAZINDE ndilo lilikuwa jina lake, alikuwa mwanaume mmoja mstaarabu sana, mtu wa MUNGU sana ambaye aliishi akiitegemea Kalamu yake hivyo hakuwa na makuu na mtu. Lakini habari mbaya ni kwamba bwana huyo alidaiwa kuwa na kurasa ambazo zilitisha kwenye maisha yake. Kurasa za maisha yake ya nyuma alikuwa amezizika na hakuna binadamu ambaye alikuwa hai alikuwa anazijua kwa imani yake yeye. Rashid Mazinde alidaiwa kuhusika kwenye mauaji ya watu zaidi ya mia-tano wakiwemo matajiri wakubwa duniani mia-moja lakini hakuna mtu alikuwa anazijua kurasa hizo. Sasa hao ambao walimtafuta walizijulia wapi? Hizo siri kwanini walimpa yeye na walitaka azifanyie nini? Zilihusiana vipi na mwandishi wa habari za kiuchunguzi AMAN KILONZO? Huyu ndiye binadamu ambaye anaenda kutulia muda wetu kuweza kuzigusa hizi kurasa tujue kuna nini ndani yake.... Simulizi hii inaitwa THE JOURNALIST (TONE LA DAMU)....karibu tone namna hilo Tone La Damu linavyo husiana na huyo mwandishi. SIMULIZI HII EPISODES ZAKE ZOTE UTAZIPATA HAPA HIVYO NUNUA COIN ZA KUTOSHA UWEZE KULISOMA MOJA YA MAANDIKO BORA YA KISIASA NA KIJASUSI KUWAHI KUANDIKWA HAPA TANZANIA. UNAWEZA KUNICHEKI WhatsApp au kawaida kwa namba 👇 +255621567672 Email yangu: [email protected] Langu jina FEBIANI BABUYA. Wasalaam.
1065
102

CH

complete
Pendo zawadi ya  umvumilivu
Pendo zawadi ya umvumilivu
Rafaeli anaingia chuo bila kujua kwamba nyumbani amempa ujauzito mfanyakazi wao wa ndani aliyejulikana kwa jina la Magreth. Kutokana na ujauzito huo, na kwa kuwa hataki kumchanganya Rafaeli kimasomo, Magreth anakimbilia kijijini kwao bila kumwambia mtu yeyote kuhusu hali yake. Rafaeli akiwa chuoni anakutana na wanawake watatu kwa nyakati tofauti na kuanzisha nao mahusiano. Hata hivyo, kati ya wanawake hao anatokea kumpenda Nifani kwa moyo wake wote — vivyo hivyo Nifani naye anatokea kumpenda sana Rafaeli. Wakiwa katika penzi zito, wanaahidiana kuoana mara tu baada ya chuo. Upande mwingine, Magreth anahudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na kugundulika kwamba mimba yake imeota nje ya mfuko wa uzazi. Daktari anamshauri aitoe ujauzito huo kwa sababu ya uwezekano wa kupoteza uhai wake wakati wa kujifungua. Lakini Magreth anakataa kutoa ujauzito huo, akiamini kwamba huo ndio njia pekee ya kuonyesha mapenzi yake kwa Rafaeli. Je, penzi la chuo kati ya Rafaeli na Nifani litafikia hatima ya ndoa? Na je, Magreth atathibitisha kweli mapenzi yake kwa Rafaeli licha ya kubeba mimba inayohatarisha uhai wake?
630
4

CH

ongoing
INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
*FIVE POISONED SERIAL KILLERS (THE TOXIC)* Hili ni kundi la wauaji watano hatari sana. THE TOXIC Neno TOXIC ni kifupi cha majina yao hao wauaji watano, herufi hatari na mhimu zaidi ni X ambayo ni utambulisho wa mwanaume aliyefutiwa kumbukumbu zake zote Kisha akawekewa kumbukumbu mpya kichwani na majina ya watu Tisa tu ndio anawakumbuka. Hawa watu watano ni wa Siri sana kiasi kwamba hata serikali na mamlaka hazitambui uwepo wao isipokuwa watu wachache. INAHUSU NINI? SIMULIZI NI YA KIJASUSI/KIPELELEZI NA MAPIGANO. Jaji mkuu anapokea simu usiku akipewa onyo la kutomhukumu mtuhumiwa mmoja ambaye amekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya raisi wa nchi ambaye ni rafiki yake mkubwa. Kwenye simu hiyo anaambiwa kama akienda kinyume basi yeye na familia yake watauawa. Akiwa na uchungu wa raisi kuuawa jaji analipuuzia agizo hilo na kumpatia hukumu ya kunyongwa huyo mfungwa. Anarudi nyumbani na kuvamiwa, inauawa familia yake yote kuanzia binti yake, mkewe mjamzito na yeye mwenyewe. Lakini kabla ya yeye kufa, anampigia simu mdogo wake ambaye anaishi Marekani na kumwambia kwamba wanauawa. Mdogo wake ni mwanafunzi wa Chuo bora duniani cha HARVARD. Taarifa hizo zinamrudisha mwanaume huyo Tanzania. Uwepo wake hauonekani kuwa hatari kwa sababu ni kijana ambaye historia yake haina mambo mengi lakini wahusika hawaujui ukweli..... JASON ambaye ndiye mdogo wa jaji mkuu ni moja ya viumbe hatari zaidi kuwahi kutengenezwa duniani. Huyu ndiye kiongozi mkuu wa Siri wa kikosi hatari cha wauaji watano yaani FIVE POISONED SERIAL KILLERS na ni kiongozi wa siri wa moja ya taasisi za kiusalama Afrika. Baada ya kurudi Tanzania anatoa miezi sita tu ya wahusika ambao wameua familia yake kujitokeza aweze kuwasamehe lakini hakuna ambaye anatokea. Mwanaume huyu anaanza kufanya mambo ya kutisha sana ambayo yanalifanya taifa zima kuingia gizani kwenye zama za kutisha na mauaji ya kutisha. Sasa huyu JASON ni nani? Alitengenezwa na nani? Kwa lengo lipi? Kundi lake la FIVE POISONED SERIAL KILLERS (TOXIC) lina sababu zipi za kuwepo? Marekani alikuwa anatafuta nini? Majibu yake yote utayapata ndani ya simulizi hii inayoitwa INNOCENT KILLER (THE REVENGE) yaani MUUAJI ASIYE NA HATIA (KISASI) Kwa namna yoyote ile usipange kulikosa hili andiko maana utajutia mno. TWENDE PAMOJA MWANZO MPAKA MWISHO. Mwandishi ni mimi FEBIANI BABUYA WhatsApp namba yangu: +255621567672 lakini pia unaweza kupiga kawaida au kutuma sms nitaupata ujumbe wako. Email: [email protected]
1017
135

CH

complete
ENDLESS FATE
ENDLESS FATE
Hatma! Hatma ni mwisho, mwisho wa kila kitu kilichowahi kuwa na mwanzo. Kama hatma iliandikwa basi lazima itafika! Mambo ya kutisha, mateso, machafuko na mengineyo mengi kama hayo, yanamfanya mlengwa wa hatma kuhisi hakuna ukomo wa yaliyo tabiliwa kuwa na mwisho. Nadir sporah, anafikiri ni mtu wa kawaida kama walivyo wengine, kumbe zama zilizopita zilimtaja, zilimhusudu, zilimuheshimu. Anabeba hatma ya Dunia ya wanadamu. Anaishi maisha ya kawaida bila kujua asili au chimbuko la ubini wake, anajaribu kutafuta asili yake, anakutana na mambo ya kutisha na kustaajabisha sana mengine ni kutoka kwa watu wake wa karibu alio wazoea mno. Kila kitu alichokuwa anafanya kwenye maisha yake kilipangwa toka kale. Usikose simulizi hii itakayo kushangaza na kukuacha mdomo wazi.!!!
959
4

CH

ongoing
Mwisho wa Dunia kimya kimya
Mwisho wa Dunia kimya kimya
JINA RASMI LA SIMULIZI: Mwisho wa Dunia Kimya Kimya --- MUHTASARI WA SIMULIZI (DESCRIPTION): > Dunia inaendelea kuzunguka. Serikali zinafanya siasa zao. Wapendanao wanatafuta furaha. Lakini chini ya pazia la amani, kuna mkakati wa kishetani unaoendelea—mpango unaotishia kuandika upya historia ya mwanadamu. Najim Kifu, mwanaume kutoka Kigoma, mtaalamu wa historia na mjasusi wa zamani aliyejificha kwenye kivuli cha kawaida, anavutwa tena kwenye dunia aliyojaribu kuisahau. Ujumbe wa siri kutoka kwa mtu aliyedhaniwa kuwa amekufa unamrejesha kwenye njia ya damu, usaliti, na upendo wa ajabu. Anapogusa faili moja la kale, gurudumu la matukio linaanza kugeuka kimya kimya—na yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kusikia kelele zake. Katika safari yake, atakutana na nguvu ambazo hazielezeki, atapenda na kuchukiwa, atasalitiwa na kuokolewa, na hatimaye kulazimika kuchagua: aokoe dunia au aokoe moyo wake. Hii ni hadithi ya ujasusi, fantasy, historia, ujambazi, mapenzi—na hatari ambayo dunia haijui inakuja… kimya kimya.
562
17

CH

ongoing
Queen of the Long Con
Queen of the Long Con
Alisalitiwa, akawekewa mtego, na kutupwa kwenye jehanam ya mateso-lakini sasa anarejea kulipa kisasi. Brenda Nyaki alikuwa na kila kitu-kazi yenye mafanikio, mchumba aliyempenda, na maisha yaliyojaa matumaini. Lakini mzunguko wa hatima usiotarajiwa ulimtupa gerezani kwa kosa ambalo hakulitenda, na kila alichokijenga kikaporomoka. Akiwa amesalitiwa na mfumo wa haki pamoja na watu aliowaamini, Brenda analazimika kujifunza kuishi gerezani-na kupambana ili kuibuka mshindi. Akiwa na akili ya kipekee, uzuri, na dhamira isiyotetereka, Brenda anatoka gerezani akiwa mwanamke aliyebadilika kabisa. Kutoka kuwa msichana asiye na hatia hadi kuwa mjanja wa hali ya juu anayejua kudanganya na kuwazidi ujanja wale waliomhujumu. Akiwa anasafiri katika miji mikuu ya dunia, akijihusisha na njama za kimataifa na mchezo hatari wa udanganyifu, Queen of the Long Con ni hadithi ya kusisimua simulizi ya msichana mrembo, jasiri, genius, na mwanamke anaetumia kila mbinu kuhakikisha anabaki kuwa juu.
600
5

CH

ongoing
The Shortcut: 12 Life-Changing Lessons from the Best Self-Help Books of All Time
The Shortcut: 12 Life-Changing Lessons from the Best Self-Help Books of All Time
Let’s be honest-reading is hard for most people. In a world full of distractions, few can finish even one book a year, yet inside those unread pages are the life stories of people who’ve failed, fought, and ultimately won. Reading is how we borrow decades of wisdom in just a few hours. It's how we avoid the mistakes others made on their way to greatness. Inside the greatest self-help books are blueprints drawn from real experiences of billionaires, spiritual seekers, thinkers, warriors, and world-changers. When you read them, you don’t just gain knowledge; you gain direction. Kajembe Jr. is a critical thinker and lifelong learner who has spent thousands of hours reading, analyzing, and extracting wisdom from the world’s most impactful books. Though still a student of life, in The Shortcut he distills life-changing lessons from twelve masterpieces, so you don’t have to read them all to change your life. What if you could transform your life by learning from the 12 greatest minds in self-help, without reading 12 entire books? The Shortcut is your fast-track to personal mastery, combining the most powerful lessons from the best-selling self-help books of all time. In this single, inspiring volume, Kajembe Kajembe Jr. distills decades of wisdom into 12 transformative lessons that will help you: ✔ Build powerful habits and break the ones holding you back ✔ Master your mindset, energy, and emotional clarity ✔ Unlock financial intelligence and a lasting wealth mindset ✔ Cultivate deep focus, resilience, and authentic relationships ✔ Reclaim your time, purpose, and inner peace Whether you're just beginning your personal growth journey or searching for a fresh spark, this book is your ultimate guide. From the disciplined clarity of Atomic Habits to the timeless wonder of The Alchemist, each chapter delivers clarity, action, and momentum. You don’t need more books on your shelf. You need the right lessons, at the right time. This is your shortcut.
636
39

CH

complete
Learn to Differentiate Between Needs and Desires to Make Growth
Learn to Differentiate Between Needs and Desires to Make Growth
Usiishi kwa Matakwa Yako, Ishi kwa Mahitaji Yako" (Live by Your Needs, Not by Your Desires) In a world driven by constant pressure to "want more," this book invites you to take a bold step back — and live intentionally. "Usiishi kwa matakwa yako, ishi kwa mahitaji yako" is not just a title — it’s a mindset shift. This eBook explores the difference between what we desire and what we truly need to live a fulfilled, peaceful, and purposeful life. Through honest reflections, relatable real-life examples — like how a discarded pen taught a timeless lesson — and practical insights, you'll learn: The dangers of chasing endless wants How to identify your true personal and spiritual needs Why simplicity can lead to clarity and peace The hidden value in things and knowledge we often overlook How to regain control of your time, mind, and energy "Not everything that feels useless is truly without value. Sometimes, it's just not the right time." Whether you're feeling overwhelmed by modern life or searching for deeper meaning, this book will challenge your perspective and help you rebuild your life — not on fleeting desires, but on lasting essentials.
519
3

CH

ongoing
Her Side of Silence
Her Side of Silence
Her Side of Silence Je, unadhani kimya kinaweza kuwa kisasi kikubwa? Zara Mwinyi ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na pia mhadhiri wa lugha mwenye utulivu wa ajabu. Anajulikana kwa busara zake, uvumilivu wake, na uwezo wake wa kuwasoma watu bila kusema neno. Lakini maisha yake yanabadilika ghafla mumewe, Imran, mwandishi wa habari maarufu wa vita anapopotea na kutangazwa kuwa amekufa. Miezi kadhaa baadaye, Imran anarudi akiwa hai… akiwa na mwanamke binti kigoli anayeitwa Dalia, mwenye ujauzito wake. Badala ya hasira, Prof. Zara anawakaribisha nyumbani kwake kwa upole na ukarimu wa kutisha. Lakini hapo nyumbani matukio ya jabu yanaanza kutokea. Dalia akiwana mimba yake anaanza kuota ndoto za ajabu. Imran anaanza kuishi kwa mashaka kana kwamba kuna mtu anatishia uhai wake. Na Zara? Kwa utulivu kabisa anaandika kwenye journal yake - maneno ambayo yanabadilisha kila kitu unachodhani unajua. Hadithi hii ya mivutano ya kihisia, usaliti wa kimyakimya, na akili inayozama taratibu, itakuacha ukijiuliza maswali kibao: ni nani mwathirika halisi? Na je, kweli tunakumbuka mambo yalivyokuwa… au tunatamani yangekuwa hivi?
502
9

CH

ongoing
Utamu wa shemeji
Utamu wa shemeji
Chombezo ya mapenzi 18+
1582
15

CH

complete
KIBIRITINGOMA
KIBIRITINGOMA
Anaitwa Frola, Mitaa ikampa jina la Bebe. Mungu alipomuumba kama mwanamke, akamuongezea na tunu ya kuwa mrembo. Urembo wake ukamtokomeza kwenye ukahaba, baadaye ukamuopoa huko na kumfanya mlimbwende maarufu Afrika mashariki na kati, Urembo ukamtumbukiza kwenye dimbwi zito la utapeli... Ukamsafirisha mbali mpaka kwenye anga ambazo hakuwahi kutegemea kufika hapo kabla. Zawadi aliyopewa ikagaeuka kuwa laana. Kuna nini humu kitabuni? Ni mkasa ambao hautakuacha mtupu kwa burudani yake. Ni yuleyule mwandishi aliyebarikiwa na Mungu, GODLOVE KABATI.
638
0

CH

ongoing
The End of the Beginning (Mwisho wa Mwanzo)
The End of the Beginning (Mwisho wa Mwanzo)
Mwisho wa Mwanzo Riwaya ya Kifantasia ya Kiswahili ya Kipekee na Isiyosahaulika Na Kajembe Kajembe Jr Katika dunia ambapo muda hujikunja kama karatasi, na damu hubeba nguvu za kale, mvulana mmoja mwenye miaka kumi na sita anagundua kwamba yeye ni mwili wa mwisho wa roho elfu moja mia tisa tisini na tisa — kila moja ikiwa ni mtaalamu wa enzi tofauti, mwenye uwezo wa kupindua maumbile, akili na hatima. Yeye ni wa 2000. Na yeye ndiye wa mwisho. Sasa, katika enzi ambapo falme zinaanguka, teknolojia za kale zinaamka, na vita vya kiroho vinafufua mipaka ya kweli na maono, JackXavier lazima afumbue siri ya nguvu zake, akikumbana uso kwa uso na makosa ya mababu zake — akihusiana na sauti zisizosemwa, kumbukumbu ambazo si zake, na kivuli cha unabii uliofutwa karne nyingi zilizopita. Atasafiri kwa wakati, atazungumza lugha za vizazi vilivyokufa, atatawala vipengele vya ulimwengu na kuweza kuamrisha elements kama moto, upepo, udongo, chuma, na maji, lakini hatakuwa na mwongozo zaidi ya sauti ndani ya moyo wake. Na mwisho wake hautakuwa uchaguzi rahisi. Atakubali kuandika historia upya... au kuvunja mzunguko wa milele? Mwisho wa Mwanzo ni safari ya ndani ya roho, vita vya kizazi kwa kizazi, na wito wa kupaza sauti ya kimya ambacho dunia imekataa kukisikia kwa muda mrefu.
797
7

CH

ongoing
Shattered Evil: Light And Shadow
Shattered Evil: Light And Shadow
Miaka kumi na sita iliyopita, mtoto mdogo alipotea katika mazingira ya kutatanisha, katikati ya mchana kweupe, akiwa ndani ya shule ya msingi jijini Dar es Salaam. Hakuacha alama. Hakukuwa na ushahidi. Hakukuwa na majibu. Taifa lilishtuka. Serikali ilituma vikosi. Kamera zilichunguzwa. Lakini mtoto huyo alimezwa na giza lisiloeleweka. Watu wengine walisema labda ni uchawi Alipelekwa mahali palipo nje ya uelewa wa binadamu—ulimwengu wa siri uliojaa nguvu zisizosemwa, mafunzo ya hatari, na maamuzi ambayo yangebadili maisha yake milele. Alirudi akiwa mtu mwingine. Si mtoto tena—bali mwanaume mwenye nguvu, aliyejificha kwenye kivuli cha jina la Liam jina lake jipya ambalo alipewa na mmoja wa master wake Sehemu alio pelekwa Liam ni nje kabisa ya uelewa wa kidunia si kila mtu anaweza kufifa kuingia kwake kuna kifaa malumu ambavyo ndio hutumika kama funguo Katika kurudi kwake kuitafuta familia aliyosahau, hatima inamtupa katikati ya jiji lenye kelele, uongo, na siasa chafu—na hapo ndipo anapokutana na , binti tajiri mwenye ushawishi mkubwa Ni baridi. Ni mwenye akili. Na ni mgumu kumpenda mtu asiye na historia inayoeleweka. Lakini moyo haujui mantiki. Na vivuli vya zamani vinamfuata liam—wakati majibu ya ukweli juu ya kutoweka kwake yanaanza kujifungua taratibu.
8580
13

CH

ongoing
Mjini kati ya miujiza
Mjini kati ya miujiza
Mjini Kati ya Miujiza ni safari ya kijana wa kawaida, Ebenezer, anayeishi katika jiji la kisasa lililojengwa juu ya misingi ya kale iliyosahaulika. Ndani ya mitaa yenye pilikapilika za maisha ya kila siku, kunatiririka nguvu ya ajabu ambayo wengi hawaioni—isipokuwa waliochaguliwa na damu, urithi, na hatima. Ebenezer hajui kuwa ndani ya damu yake, kuna nguvu ya kale iliyolala kwa karne nyingi. Wakati ukuta wa chumba chake unaanza kung’aa, na sauti za kale zinamuita kwa jina, anajikuta akivutwa katika ulimwengu wa uchawi, maadui wa kivuli, na siri za familia yake ambazo zimezikwa kwa muda mrefu. Riwaya hii inaleta mguso wa fantasy ya kisasa, ikiwa imejaa fumbo, vita vya kiroho, na mashindano ya nguvu kati ya nuru na giza. Ni hadithi ya ukuaji, mapambano ya ndani, na kusimama imara katika dunia ambayo ukweli wake umefichwa nyuma ya pazia la kawaida. Karibu kwenye safari ya Ebenezer—ambako giza si adui pekee, na nguvu si zawadi bali mzigo.
652
13

CH

ongoing
Kwa Ajili ya Upendo
Kwa Ajili ya Upendo
Kupitia nguvu ya mapenzi wanajikuta wakikomboa mji wa Dodoma
811
21

CH

complete
Shamba la hela
Shamba la hela
Katika maisha yake ya kawaida ya kila siku ya utafutaji. Kijana Feruzi anajikuta akikosea kona na kuangukia pua dhidi ya watu hatari... Watu ambao wanailinda siri kubwa...siri nyeusi. Siri ya shamba kubwa la hela. Kulikoni?! Karibu tuzifunue pamoja kurasa za riwaya hii. Riwaya bora kutoka katika mkono wa kaka Godlove Kabati.
1176
28

CH

complete
KIkao cha haki
KIkao cha haki
Haujawahi kuwa mchezo salama kabisa. Ni mchezo ambao kama ukiucheza na hujui kanuni zake...basi utapata majuto na maumivu. Wengi wameutungia nyimbo na mashairi. Tukayaimba Wengine wameuandikia hadithi na riwaya, kwa lugha nzuri za kifasihi na sarufi. Tukazisoma. Hawa wengine wameuigizia tamthilia na filamu. Tukazitazama. Lakini bado hatukupata maana halisi na jibu la huu mchezo. Ni kama fumbo gumu ambalo halijawahi kuwa rahisi kufumbua. Ni kitendawili kigumu ambacho hata ukipewa mji uende na hurudi na majibu yake bado ungeshindwa tu. Ni mchezo wa mapenzi. Yaliyowakuta hawa wapendanao wawili. Kila mmoja ana hadithi yake ya kusikilizwa. Kilifanyika kikao.. Hatutamlaumu mwanamke baada ya kuisikia hadithi ya upande mmoja tu wa mwanaume. Tutataka pia kuisikiliza hadithi ya mwanamke.. Hii ndio haki! Hii ni simulizi fupi ya mapenzi, ambayo hakika haitakuacha mtupu baada ya kuisoma. Utaburudika, utaelimika na zaidi utapata hekima kubwa kuhusu mahusiano. Karibu tukisikilize kwa pamoja KIKAO CHA HAKI!
745
5

CH

complete
Nafsi zilizotelekezwa
Nafsi zilizotelekezwa
Mwaka 1991, ni mwaka ambao umoja wa nchi za Kisovieti ulidondoka baada ya kushindwa kwenye vita baridi dhidi ya watu wa Magharibi hususani Marekani. Baada ya vita hiyo kuisha kulikuwa na sababu nyingi sana zilizo wafanya washindwe ikiwemo utaifa na mchango wa nchi za magharibi. Kwa madhara makubwa ambayo yalipatikana, nchi ya Urusi ilikaa chini kufanya tathmini ili kujua ni wapi walifanya makosa mpaka jambo hilo likatokea nchini mwao. Moja kati ya sababu kubwa ambazo walizipata ni kufeli kwa shirika lao la kijasusi la KGB kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kiusalama kwa asilimia miamoja, waliamini kwamba huenda kama shirika hilo lingekuwa imara mapema na kutekeleza majukumu yake kwa usahihi basi wangeishinda vita hiyo. Sasa mjadala ukawekwa mezani, walishindwaje? Ndipo ikanukia harufu ya usaliti ndani yao, iligundulika kwamba ndani ya shirika lao kuna watu ambao walikuwa wasaliti na usaliti wao ndio ambao ulifanya shirika hilo kuyumba na kufeli. Sasa wasaliti walikuwa nani na nani? Jina ambalo lilitokezea kwenye makablasha yao ni jina la mwanamke wa miaka ishirini na mitano (IRINA ESPANOVICH). Sasa IRINA ni nani na alitokea vipi kwenye hiyo orodha ya wasaliti? IRINA ESPANOVICH alikuwa ni jasusi mbobevu ndani ya shirika hilo, Moja kati ya wapelelezi ambao waliaminika mno kiasi kwamba akapata bahati ya kuolewa na moja kati ya maafisa wakubwa ndani ya shirika hilo la KGB. Kuolewa kwake na kiongozi mkubwa wa shirika hilo ikawa nafasi ya yeye kupata taarifa nyingi na za siri za shirika hilo kwa njia ya kawaida ama kuziiba kwa sababu huyo mwanaume alikuwa akiishi naye nyumba moja. Sasa kwenye ule mchakato wa kuwatafuta wasaliti, waligundua kwamba kuna akaunti ndani ya Urusi ilipokea mabilioni ya fedha kutoka ndani ya nchi ya Marekani na walipo jaribu kuichunguza akaunti hiyo ili wajue sababu ya msingi ya pesa nyingi kiasi hicho kutumwa kwa mtu ambaye taifa lake lilikuwa vitani na nchi hiyo ni ipi! Ndipo wakagundua kwamba akaunti hiyo ilikuwa inamilikiwa kwa siri na mwanamke huyo IRINA ESPANOVICH. Baada ya kuunganisha doti, wakagundua kwamba hizo pesa zilitoka ndani ya shirika la kijasusi la Marekani CIA ambalo wengi huwa wanaamini kwamba ndilo shirika namba Moja kwa ubora zaidi duniani kutokana na kuwa na bajeti kubwa ya uendeshwaji wake. IRINA alipokea pesa nyingi ambazo hata angefanya kazi miaka mia-moja asingeweza kuzipata, CIA wamtumie pesa kama nani? Ikahitimishwa kwamba huyo ndiye msaliti ambaye alikuwa akiwauza kwa CIA ndiyo maana walifeli hivyo ikatolewa amri kwamba asakwe popote alipo, akamatwe, ateswe kisha auawe mrembo huyo. Bahati ikawa upande wake, mlinzi mkuu wa mumewe akampatia taarifa kwa simu kwamba Maam you are to be killed (unatakiwa kuuawa) hawa watu wanajua kila kitu hivyo KIMBIA (RUN). Alikuwa hatarini hivyo hakuwa na muda wa kupoteza akapotea haraka, KGB hawakumpata mwanamke huyo hivyo ukaanza msako wa kimya kimya kwa sababu waliogopa kuziweka taarifa hizo wazi kwani zingewavua nguo kwa kuonekana ni wazembe mpaka yote hayo yanatokea na hawana taarifa! Hawakutaka aibu wakaamua kuifanya siri kumtafuta huyo DOUBLE AGENT IRINA ESPANOVICH. Kupotea kwake Urusi mikononi mwa KGB ambao walimpachika jina la LUNATIC GIRL, ukawa mwanzo wake wa kuingia ndani ya nchi ya Tanzania. Kwanini iwe Tanzania? IRINA alipiga hesabu zake akagundua kwamba kama angeenda nchi kubwa hususani ambazo zina usambaaji wa taarifa haraka wangekuja kumpata tu siku moja hivyo alihitaji kuishi sehemu ambayo hata KGB wenyewe wasingeidhania kwamba anaweza kuwepo na ile amani ambayo imetawala Tanzania ikamvutia kuishi hapa kwani ingekuwa ni ngumu kuja kujulikana kwamba yupo hapa. Yes, mpango ulikuwa sahihi sasa Tanzania angeishije na angeweza vipi kujilinda? Ukawa mwanzo wa kuanzisha jamii ya Siri ambayo aliiita LUNATIC SOCIETY, jina ambalo alipewa na KGB kwa usaliti wake. Kumbuka alikuwa mgeni hivyo asingeweza kuianzisha jamii hiyo mwenyewe ikamlazimu kumtafuta mtu. Macho yake yakadondokea kwa Novack Nyangasa, mdogo wa raisi wa Tanzania ambaye aliamini angekuwa na nguvu ya kumpeleka anapo pataka yeye. Alimshawishi mwanaume huyo kwa urembo wake na kumpa mpango mzima juu ya utajiri ambao wangeenda kuutengeza, Novack akatokwa na mate ya uchu, akakubali. Jamii hiyo ikaanzishwa kwa nguvu ya mdogo wa raisi ambapo waliwasajili watu wakubwa; wanasiasa wakubwa, maprofesa, wanafalsafa, madaktari bingwa, wafanya biashara wakubwa na kila ambaye walimuona anafaa. Baadae raisi akazipata habari, akachukia sana na kumuita mdogo wake IKULU. Akamtaka aifute jamii hiyo kwa mwezi mmoja tu pekee, huo mwezi ukatumika kummaliza yeye, raisi akawekwa kati akatakiwa kufa ili jamii hiyo iwepo. Moja kati ya mipango mikakati ambayo waliiweka ili kujilinda ni kuanzisha chuo cha kuwatengeneza vijana hatari kwa ajili ya ulinzi na kufanya kazi yao kwa nguvu pale ambapo ingebidi, zoezi hilo likatua mikononi mwa jasusi wa zamani wa Tanzania ambaye aliachana na kazi hiyo baada ya kuhusika na mauaji ya watu wengi sana, NIKOLAI GIBSON. Mwanaume huyo kwenye moja ya mazao yake alifanikiwa kumtengeneza kijana wa kuitwa YOHANI MAWENGE, bwana mdogo ambaye alimuokota Tandale kwa Tumbo akililia mapenzi na kutaka kujiua kisa uchi wa mwanamke. Alimfunza namna ya kuwa mwanaume akampa begi la pesa akale maisha kwa mwezi mzima, alale na wanawake warembo ambao aliishia kuwaona kwenye runinga ili ushamba umtoke kisha baada ya hapo alikuwa na kazi naye. Alitengenezwa kikawa kiumbe cha kutisha na Kazi yake ya kwanza ikawa kwenda kumuua mcheza KAMARI mmoja huko BAMBALI Senegal na alitakiwa kurudi na bilioni 30 zilizokuwa mkononi mwa bwana huyo..... Huyu tuna mengi ya kuyasoma kwake ni mhimu sana. Ukawa mwanzo wa mwanamke huyo wa KGB kuitawala Tanzania kwa miaka takribani thelathini. Lakini baadae Moja kati ya makosa makubwa ambayo waliyafanya ni kumuua mwanasayansi aliyedaiwa kuwa binadamu mwenye akili zaidi nchini. NAFSI ZILIZO TELEKEZWA ni zipi na za nani? Kulikuwa na utata wa maisha ya mwanaume Edison, bwana ambaye hakuwa na kumbukumbu na kwenye mfuko wake alikuwa anatembea na picha ambayo walidai ni ya mkewe, bwana huyu alikuwa akishangaa kwa sababu yeye binafsi hakuwa na kumbukumbu yeyote kama aliwahi kuwa na mke au familia. Kitu cha kushangaza kwa EDISON ni kwamba alikuwa anatafutwa ili auawe kuliko hata pesa inavyo tafutwa na maskini mpaka yeye mwenyewe akawa anashangaa. Hali hiyo ilimlazimu kwenda kuishi maisha ya chini sana huko Kigogo Mwisho ili awe salama kwani hakuna ambaye angempata kirahisi akiwa kwenye maisha ya kifukara huko lakini usiku mmoja mvua ikiwa inanyesha akiwa ndani ya kijumba kibovu kwenye mkeka, akapokea simu ambayo ilimtaka atoweke eneo hilo kwa dakika kumi na tano vinginevyo angekufa. Aliduwaa ila hakuwa na namna aliondoka haraka ila kabla hajafika mbali akavamiwa na wanaume wa kutisha ambapo alimuua mmoja akafanikiwa kutoroka. Safari yake ikawa ni kwenda kwa mlezi wake ambaye ndiye alimpa taarifa hiyo na ndiye alimtaka akaishi huko Kigogo mapaka mambo yakae sawa ili akampe ukweli wa kwanini anatafutwa sana? Kufika kwa huyo mlezi wake ambaye alikuwa ni mchungaji wa KKKT pale Mabibo Mwisho karibu na hosteli za wanafunzi wa NIT, alimkuta mtu huyo yupo kwenye hatua za mwisho za uhai wake. Hakumwambia kitu zaidi ya kumtaka aende nyumbani kwake kwenye banda la mbwa akachukue kitabu ambacho kingemfunulia ukweli kwamba yeye ni nani, kwanini hana kumbukumbu, maisha yake kabla yalikuwaje na kwanini anatafutwa sana na watu ambao yeye alidai hawajui! EDISON alishangaa baada ya kuambiwa kwamba anatafutwa kwa kuhusika na mauaji ya makomando TISA wa kikosi maamulu cha KOM (KILL ON MISSION).akabaki ameduwaaaa!!!!!!! Ilishawahi kukukuta kwenye maisha yako ukatakiwa kumuua mama yako mzazi kwa mkono wako mwenyewe? Hilo ni jambo baya na gumu lakini Yes, kuna mwanaume alitakiwa kumuua mama yake aliye mzaa ili nchi iwe salama. Je huyu naye hatima yake ilikuwaje? Kuna uhusiano gani kati ya hizo NAFSI ZILIZO TELEKEZWA, IRINA ESPANOVICH na EDISON? Unataka kumjua zaidi IRINA ESPANOVICH? Unataka kuijua kiundani LUNATIC SOCIETY? Unataka kujua uhalisia wa maisha ya EDISON kabla na baada ya hapo? Hizo nafsi ZILIZO TELEKEZWA ndizo hizo za makomando TISA (9) ambao alidaiwa kuwaua au kuna mengine nyuma ya mlango wa siri? Ungana nami kwenye simulizi yangu bora zaidi kuwahi kuiandika kwa mkono wangu.... 1. Storyline yake ni kali sana 2. Dialogue (majibizano) yake ni kali sana. 3.Haitabiriki kabisa (huwezi kutabiri kinacho tokea baadae) 4.Lakini pia ina actions kali mno. Mwandishi ni Mimi FEBIANI BABUYA KARIBU UWEZE KUZIGUSA KURASA HIZI HAPA HAPA KWA KUTUMIA Coin.
1229
106

CH

complete
DOSARI
DOSARI
Mwanamke mmoja kijana asiye na maisha yenye uwezo wa hali ya juu anajikuta ndani ya changamoto nzito zaidi kwenye maisha yake baada ya mzazi wake kuugua na kukosa njia ya haraka kuweza kumsaidia. Akiwa peke yake na kuishiwa na namna ya kuleta suluhu, anatafuta msaada mahali ambapo panamwingiza matatani zaidi ya matarajio anayojipa ya kuleta suluhisho. Upande mwingine wa kisa hicho, mwanaume tajiri mwenye familia nzuri na maisha yaliyotulia anakutana na masaibu mazito ghafla sana yanayovuruga amani yote aliyokuwa nayo moyoni. Ni mikazo kutoka kwenye matatizo hayo inayomfanya ashindwe kujua ni jambo gani sahihi analotakiwa kufanya ili asonge mbele na kuyafanya yaliyomkuta kuwa mapito, lakini inamwia ugumu sana kufanikisha jambo hilo, na maamuzi anayochukua yanabadili kabisa mpangilio wote wa maisha aliotaka kuwa nao mwanzoni. Katikati ya hayo yote, kuna visa na mikasa yenye kusisimua sana inayozileta hatma za wawili hao pamoja, na kutokea hapo maisha yao yanaelekea kwenye mkondo usionyooka kutokana na mambo mengi yanayowazunguka kuyatia maisha yao vikwazo na dosari nyingi. Fuatilia kisa hiki chenye kusisimua na kujenga sana. DOSARI...
1374
20

CH

ongoing
Siku za mwisho- (The darkness of an angel)
Siku za mwisho- (The darkness of an angel)
SIKU ZA MWISHO!!!!! Je wewe ni mdau wa IDAIWE MAITI YANGU? Je wewe ni mdau wa SAFARI YA GAVIN LUCA? Kama jibu ni ndiyo kwanini usiisome SEHEMU YA MWISHO ya mtiririko wa simulizi hizi iitwayo SIKU ZA MWISHO - GIZA LA MALAIKA (THE DARKNESS OF AN ANGEL?)........ Hii simulizi ni sehemu ya mwisho au season 3 ya IDAIWE MAITI YANGU ambazo zimetoka kwa collection kama ifuatavyo 1. IDAIWE MAITI YANGU 2. SAFARI YA GAVIN LUCA - LIONELA (THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA) 3. SIKU ZA MWISHO - GIZA LA MALAIKA kwa kiingereza THE DARKNESS OF AN ANGEL Collection hii inaihusu familia ya GAVIN LUCA na mwanae wa pekee LIONELA GAVIN LUCA. Hivyo kama uliisoma IDAIWE MAITI YANGU ukapata maswali ambayo yalijibiwa kwenye SAFARI YA GAVIN LUCA kisha 👇 SAFARI YA GAVIN LUCA ikatuachia maswali mengi ambayo yanajibiwa ndani ya SIKU ZA MWISHO. Hivyo hakikisha unaisoma hii collection nzima ili uweze kuipata hatima nzima ya maisha ya familia Moja kubwa sana na ya Kitajiri barani Afrika, familia ya GAVIN LUCA. SIKU ZA MWISHO (GIZA LA MALAIKA)- THE DARKNESS OF AN ANGEL..... Ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya mwendelezo wa IDAIWE MAITI YANGU na SAFARI YA GAVIN LUCA (THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA).... Humu utajua hatima ya familia ya GAVIN LUCA na mwanae wa pekee LIONELA na hatima ya zile nguvu zao. Kwenye SAFARI YA GAVIN LUCA uliona JABARI akionekana msaliti, hivyo kama unataka kujua sababu nyuma yake kwamba kwanini alimsaliti mkewe wa ndoa? Basi hii ndiyo sehemu sahihi ya kupata majibu yako. JABARI alituacha wote mdomo wazi baada ya kumuoa LIONELA kisha akaanza kuua familia ya LIONELA Lakini mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Kenya (NIS) alikuwa na ajenda gani hatari kwa Tanzania na familia ya GAVIN ? KAA NA MIMI TWENDE SAWA MUDA HUU UANZE KULISOMA MOJA YA ANDIKO BORA SANA KUWAHI KUTOKEA TANZANIA. FEBIANI BABUYA
1575
122

CH

complete
THE IMMORTAL BOND (Kifungo Cha Milele)
THE IMMORTAL BOND (Kifungo Cha Milele)
The Immortal Bond ni riwaya ya mapenzi ya kiajabu inayomfuata Yolanda Mekkanan, mchawi mwenye nguvu ambaye aliishi kwa karne nyingi, na Michael Nsebo, mwanaume aliyetokea kumpenda kwa dhati kupita Kiasi. Mwaka 1622, wakati wa kilele cha majaribio ya wachawi wa Salem, Yolanda anatuhumiwa kwa uongo kutumia uchawi kuleta tauni ya mafua kwa watu zaidi ya maelfu na kuhukumiwa kifo. Ingawa hukumu yake ya kifo inapitishwa, roho yake inafungwa duniani kwa uchawi wa kale, ikimpa kutokufa (immortality). Akilazimika kuishi kupitia nyakati mbalimbali, akitazama wale anaowapenda wakiwa wazee na kufa, bila kuweza kupata amani ya kweli. Karne baadaye, Yolanda anakutana na Michael Nsebo, mwanaume ambaye anahisi kuwa naye na mahusiano yasioeleweka. Anapomfahamu zaidi, anatambua kwamba Michael ni mfululizo mpya wa mapenzi yake ya kwanza na pekee, mwanaume ambaye hapo awali alipigana kumwokoa kutoka kwenye hukumu ya kifo. Lakini Michael, asiyejua chochote kuhusu maisha yake ya hapo awali, anajitahidi kuuelewa mvuto wake mkubwa kwa Yolanda na kumbukumbu za ajabu zinazojitokeza kila wanapokuwa pamoja. Yolanda na Michael wanapotafuta njia katika uhusiano wao mpya, adui wao was zamani anajitokeza ambaye amekuwa akimfatilia Yolanda kupitia Nyakati tofauti tofauti(different time zones), akitafuta kisasi. Riwaya hii inaunganisha pamoja mada za hatima ya wapendanao(themes of fate), kuzaliwa upya(reincarnation), na mapambano kati ya wema na uovu wakati Yolanda anapopigania kujinasua kutoka kwenye mzunguko wa hasara na hatimaye kudai upendo ambao umekuwa ukimkwepa kwa karne nyingi. Kwa mchanganyiko wake wa mazingira ya kihistoria na ya kisasa, The Immortal Bond ni hadithi pana ya upendo unaovuka wakati, ukithibitisha kwamba upendo wa kweli ni wa milele.
1080
40

CH

ongoing
FOR YOU
FOR YOU
Vijana wawili mapacha kutoka katika familia ya Meja wa kijeshi, wanajikuta ndani ya sintofahamu baada ya jambo lisilotazamiwa kusababisha miili yao iingiliane. Na katikati ya hayo yote, kuna kisa Cha usaliti ndani ya Serikali ya nchi yao kinachopelekea familia yao kubomoka na umwagaji mwingi wa damu isiyo na hatia kwa sababu ya tamaa na migogoro inayoletwa na watu wenye pupa. Lakini ili kutimiza ahadi aliyoweka kwa ajili ya pacha wake, pacha mmoja anafanya kila lililo ndani ya uwezo wake akiwa na mkono unaomsaidia kupambana na maadui wao wote ili kukomesha matendo maovu yanayosababisha maumivu kwa wengi. Safari yake kutimiza hilo inakuwa na vikwazo vingi hasa kwa kuwa anakutana na mkazo wa kufanya yaliyo sawa ingawa kwa njia zinazoacha maumivu kwenye pande zingine muhimu kwa maisha yake. Yote hayo na mengine mengi ni ndani ya hadithi hii tamu na yenye kusisimua sana; FOR YOU. Ahadi ni damu.
624
54

CH

ongoing
JIJI LA KAMARI
JIJI LA KAMARI
JIJI LA KAMARI ( GAMBLING CITY) INTRO........... Usiku wa kiza kinene ambacho kilikuwa kinasindikizwa na mvua ambazo hazikuwa na mpaka wa kuweza kuzielezea vyema, alionekana mwanaume mmoja akiwa ndani ya nguo zake nyeusi tii na begi jeusi usiku huo huku mwili wake ukiwa umefunikwa na koti kubwa jeusi pia ambalo lilikuwa refu kiasi kwamba lilivuka mpaka magotini. Mikono yake ilifunikwa na gloves nzito nyeusi pia ambapo mkono wake wa kulia ndio ambao alikuwa ameutumia kuweza kushika begi lake mkononi akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka haraka huku akiwa makini mno kuonyesha wazi kwamba alikuwa anatakiwa kulifikisha begi hilo salama kabisa sehemu ambapo lilikuwa linahitajika kuweza kufika. Akiwa kwenye mwendo wake huo wa haraka, wakati amefika katikati ya barabara ndogo ambayo ilikuwa imezungukwa na majengo marefu na pembeni yake kukiwa na vichochoro vingi, alihisi kwamba eneo hilo ni kama lilikuwa na mtu au watu wengine ukiacha yeye hivyo alizidisha hali ya umakini kwa hapo ambapo alikuwa amesimama. Masikio yake yalimtekenya vizuri mithili ya funguo zinapokuwa zinazamishwa kwenye kufuli na kumpa taarifa hiyo, alikuwa ni mtu wa kuutumia mlango wake wa sita wa fahamu huo wa hisia kwa umakini mkubwa hivyo alikuwa na uhakika kwamba hisia zake zisingeweza kumsaliti kamwe kwani alikuwa akijiamini kwenye jambo hilo akawa na uhakika kwamba kulikuwa na ugeni ndani ya hilo eneo. Alisimama na kutulia ili kuweza kujua kwamba huyo mgeni alikuwa anatokea upande upi huku akiwa ameyafumba macho yake kuweza kujipa hali ya utulivu zaidi kwenye masikio yake. Akiwa bado amesimama hapo alihisi kama kuna kitu kilikuwa kinakuja kwa kasi sehemu ambayo alikuwa amesimama hivyo aliinama kwa kasi mithili ya radi ya mvua. Wakati anainama alipishana na shoka ambalo lilienda kukita kwenye ukuta mmoja wa jengo la pembeni. Aligeuka haraka ila wakati anageuka alitumia muda mrefu ambao ulimpa nafasi mtu ambaye alikuwa ameingia hapo kufanya kile ambacho alikuwa anakitaka. Alihisi kifua kinamuwasha mithili ya mtu aliye tafuna pilipili kichaa maana spidi ambayo mvamizi aliitumia kumkita hapo kifuani haikuwa ya binadamu mwenye mifupa ya kawaida bali alikuwa ni mashine haswa kama namna umeme unavyo safiri kwenye zile njia zake. Alipokea mishindo ya haraka na mabuti makali hali iliyofanya begi kumtoka mkononi huku ikionekana wazi kwamba mabuti hayo yalitokea kwa mtu ambaye alidhamiria kabisa kumuua ndiyo maana hakumpa hata nafasi ya kuweza kumtazama maana mvamizi huyo uso wake ulifunikwa kwa kitambaa cheusi na hata mvamiwaji hakupata hiyo nafasi ya kumtazama kwa ukaribu. Mwanaume huyo licha ya kurushwa mbali na mabuti hayo hali ambayo ingemfanya auvunje mgongo wake kwa kujibamiza kwenye kuta za mawe mazito za majengo ambayo yalikuwa pembeni, hakuwa fala kufa kijinga namna hiyo. Mkono wake ndio ambao aliutumia kukita kwenye kuta hizo na sio mgongo ambao ulitua ukutani kwa nguvu kubwa. Kasi ambayo alitua nayo kwa mkono wake ililifanya koti lake kujivuta kidogo na kwenye mkono wake ikaonekana alama ya tatoo (tatuu) ambayo ilisomeka kama 001. Baada ya kujichomoa hapo ndipo aligeuka na kumuangalia mtu ambaye alionekana alihitaji kumuua, mtu huyo alikuwa kwenye mavazi meusi kama yeye na koti kama lake, yaani kiufupi wote walikuwa wamevaa sawa ila utofauti wao ni kwamba mvamiwaji alivaa kofia aina ya pama kichwani ila mvamiaji alikuwa amejifunika tu kitambaa kwenye uso wake hivyo sura yake haikuwa ikionekana kabisa. Baada ya hapo ulipigwa mkono wa hatari mpaka umeme ulipo katika ghafla ndipo mvamiwaji alitulia akiwa makini maana hakuwa akimuona mtu ambaye alitakiwa kumshambulia huku akiwa amepigwa vibaya na umeme huo kukatika alishukuru japo ilikuwa ni hatari maana angeweza kuuawa bila kujua mhusika yuko wapi ila aliamini kwamba angepata dakika chache za kupumzika maana bila hivyo ni lazima angekufa. Akiwa anaangaza kwa umakini huku na huko umeme ulirudi tena ghafla na ndipo alipo gundua kwamba ndani ya eneo hilo hapakuwa na mtu mwingine zaidi yake, mvamizi alikuwa ameondoka muda mrefu ila chini palikuwa na karatasi nyeupe ambayo ilikuwa imesainiwa kwa damu huku ikiendelea kunyeshewa na mvua. Aligeuka na kuangalia pale ambapo begi lilikuwa limedondokea ili kujua usalama wake ila kwa bahati mbaya begi halikuwepo kabisa eneo hilo, alishtuka sana akionyesha hofu ya wazi moyoni na kwenye uso wake hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuisogelea ile karatasi ili aweze kusoma kile ambacho kilikuwa kimeandikwa. “KAMARI YANGU YA MWISHO, NDIYO KAMARI YAKO YA KWANZA” hayo ndiyo maneno ambayo yalikuwa yameandikwa hapo. Aliogopa sana baada ya kuisoma huku akionekana wazi kwamba mikono yake ilikuwa inatetemeka wakati huo. Hiyo ilikuwa ni kauli ambayo alikuwa anaitumia mwanaume mmoja ambaye alimuua yeye mwenyewe kwa mkono wake miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita huko nyuma, huku begi ambalo lilionekana kuwa na nyaraka mhimu mno likiwa limepotea kizembe. Inawezekanaje mwanaume ambaye alimuua kwa mkono wake mwenyewe bado awe hai? Hilo begi lina nini mpaka mtu ambaye alisemekana kwamba alikufa aweze kupotea nalo? Nini maana halisi ya JIJI LA KAMARI na jiji hilo lina mambo yapi na siri zipi labda? Unategemea kukutana na nini humu ndani? Mimi nashika kalamu yangu sasa nakaa mezani, kazi yako wewe ni kuhakikisha unaenda nayo nukta kwa nukta ili uweze kuifunua kila kurasa kuweza kuzisoma serikali tatu kwa wakati mmoja ndani ya JIJI LA KAMARI. Kalamu ni yangu mwenyewe; FEBIANI BABUYA.
876
88

CH

complete
Niliemdhania kahaba kumbe bikra
Niliemdhania kahaba kumbe bikra
Roma mbeba mizigo ndani ya soko la Mbagala Rangi Tatu anamdhania Edna Kama mwanamke anaejiuza ,baada ya mwanadada huyu kuwekewa dawa ya usingizi kwenye kinywaji na maadui zake katika ulimwengu wa Biashara akiwa ndani ya hoteli na Roma anambeba Edna na kumpeleka Geto kwake na afanya nae mapenzi. Edna kwa Mara ya kwanza analala na Roma pasipokujitambua na kupoteza usichana wake ,baada ya tukio Hilo anaamua kuolewa na Roma kwa mkataba wa Miezi sita ili kuepuka kuolewa na mwanaume asiempenda ,baada ya Roma kufunga ndoa na Edna anakuja kugundua kuwa mke wake anamiliki kampuni kubwa Nchini huku akiwa na utajiri wa kutisha. Edna anamuona Roma kama mtu asiyekuwa seriasi na maisha kutokana na aina ya mfumo wa maisha yake ,maisha ya kuwa na wanawake wengi swala linalomkasirisha Edna. Edna anajitahidi kuweka ukaribu na Roma ili kujua sababu ya mume wake macho yake kubadilika Rangi anapokuwa na hasira na kuwa ya kijani huku akiwa na roho ya ukatili mno Idara na mamlaka za kiusalama Nchini zinashangazwa na uwezo wa Roma wa kuzungumza Lugha zaidi ya ishirini na mbili na wanaanza kutafuta taarifa zinazomuhusu Roma lakini licha ya kupata taarifa inayoonyesha Roma kusomea ndani ya chuo kikubwa Duniani Cha Harvard wanakosa taarifa zingine zinazomuhusu Roma na kuishia kujiuliza Roma ni Nani haswa
4111
490

CH

complete
MIMI NA MIMI
MIMI NA MIMI
Simulizi yenye kusisimua kuhusu maisha halisi ya mwanaume kijana wa kitanzania anayekwenda likizo kutafuta wakati mzuri. Huko anakutana na watu, visa, na mikasa inayomfanya abomoe na kujenga aina ya utu unaofaa mbali na ulealiokuwa nao mwanzo. Na anapotafuta furaha anayoitaka, anakuja kuipata mahali ambapo hakutarajia kabisa, ingawa kwa magumu na mabaya mengi anayohitaji kupitia ili kuweza kuistahili furaha hiyo. Yote ni ndani ya MIMI NA MIMI.
6659
157

CH

ongoing
CHANGE (BADILIKO)
CHANGE (BADILIKO)
Ni hadirhi inayohusu wanawake wawili wanasheria walio marafiki wa damu, wanapokutana na mwanaume aliye na maisha yaliyojaa siri nzito sana zinazokuja kuingiliana na maisha yao pia mpaka kupelekea hali zenye utata mwingi kuwazunguka. Wakiwa na utayari kukumbana na changamoto zinazoletwa na mikasa mingi yenye kutatanisha, je wataweza kufaana na mabadiliko yatakayoletwa na matokeo ya visa hivyo? Yote ni ndani ya CHANGE... BADILIKO.
730
27

CH

ongoing
INVISIBLE
INVISIBLE
Ni hadithi yenye kusismua inayomhusu mwanaume kijana anayejitahidi kuishi maisha rahisi na yenye usawaziko, lakini yanampa mkondo tofauti kabisa kwa kumwingiza katika hali yenye utata inayofanya maisha yake yote yabadilike. Na anakutana na changamoto nyingi zinazomhitaji atende kwa njia ambazo hakuwahi kuwazia kabla, lakini ndiyo zinamwongoza kuifikia tamati yenye kuridhisha kutokana na yanayomzunguka kumjenga zaidi kimtazamo, na kiutu. INVISIBLE.
1021
36

CH

ongoing
BADO NINAISHI
BADO NINAISHI
BADO NINAISHI. Inamhusu mwanaume mmoja ambaye alikuwa ni kiongozi wa genge la kihalifu ambalo lilikuwa linaitwa SARAFU KUMI NA TANO. Mwanaume huyo alikuwa anasakamwa na mamlaka za usalama ndani ya taifa la TANZANIA kwa miaka kumi bila mafanikio. Ndipo alitumika mwanamke mrembo ANELIA BATON ambaye alimwingiza mwanaume huyo kwenye HONEY TRAP kwa kupitia kikosi hatari kutoka ndani ya shirika la kijasusi kiitwacho HOLY TRINITY, walifanikiwa kumpata mwanaume huyo. Alihukumiwa kifungo cha miaka sitini gerezani na baada ya hapo angenyongwa. Alipelekwa ndani ya gereza hatari la DOMINIC, huko alikutana na tajiri mmoja ambaye alikuwa amejificha ili kuyalinda maisha ya mwanae ambaye alitekwa. Tajiri huyo alikutana na mwanaume huyo aliye itwa REMMY CLAUDE na kumuomba akamuokoe mwanae yeye anyemsaidia kumtorosha gerezani. Walifikia makubaliano mwanaume akatoroshwa gerezani. Huko uraiani alienda kumtafuta mtoto wa kiongozi huyo lakini wakati anafanikisha hilo tajiri huyo alikuja kupata habari kwamba mfungwa huyo aliye Mtorosha gerezani hakufungwa kwa bahati mbaya bali ilikuwa ni mipango yake yeye ili akutane na tajiri huyo. Alishangaa sana ilikuwaje mtu ajitoe kafara kufungwa gerezani kwa sababu yake? Ndipo akaja kugundua kwamba Remmy alikuwa anautafuta umoja wa watu ambao hawakuwa wakifahamika na tajiri huyo ndiye mtu pekee ambaye angemsaidia kuwajua wote ndani ya umoja huo. Anakuja kushtuka akiwa amechelewa, mwanaume huyo alikuwa amempata mwanae tayari na kupotea naye hali ambayo ilileta maafa makubwa sana na kulilazimu shirika la kijasusi kuanza na moja kumtafuta. SARAFU KUMI NA TANO halikuwa pambo bali ilikuwa idadi ya wanafamilia ambao waliuawa kikatili takribani miaka ishirini iliyokuwa imepita ila kwa bahati mbaya mtu mmoja alifanikiwa kuishi. Sitaki nikumalizie uhondo. Unataka kujua huyo Remy ni nani? Kwanini alijitoa sadaka kwenda gerezani? Huo umoja una nini hasa ndani yake na unaongozwa na nani? Nini hatima ya maisha ya Remy Claude? Hili ni moja kati ya andiko ambalo litakufanya ujivunie sana kuyasoma maandishi. SIMULIZI HII INAPATIKANA HAPA HAPA HIVYO TWENDE SAWA PAMOJA ILI UWEZE KUYAGUSA MAISHA YA BWANA REMMY CLAUDE TUPATE KUMJUA NI NANI HASWA NA ANAHUSIANA VIPI NA TITLE YA BADO NINAISHI AU ASHRAFU NDILO JINA LANGU ✍️🔥
1352
100

CH

complete
THE REVENGE SEASON 1 (DERICK)
THE REVENGE SEASON 1 (DERICK)
Kijana mdogo Derrick anaapa kulipa kisasi Kwa watu wote walio husika na mauaji ya wazazi wake pamoja na mdogo wake wa kike, anapambana kadili ya uwezo wake na anafanikiwa kuwatambua watu hao na kuanza kumuangamiza mmoja baada ya mwengine
646
10

CH

ongoing
Safari ya Kweka – Kutoka Umasikini hadi Uongozi wa KGC
Safari ya Kweka – Kutoka Umasikini hadi Uongozi wa KGC
Katika kijiji cha Mwika, kilichopo mlimani Kilimanjaro, alizaliwa kijana mmoja aliyepewa jina Joseph Kweka. Alikuwa mtoto wa pekee wa Mzee Petro Kweka na Mama Anna Kweka, wakulima wa kawaida waliotegemea kahawa na ndizi kuendesha maisha yao. Tangu utotoni, Joseph alikuwa tofauti. Alikuwa na udadisi usio wa kawaida kuhusu vitu vya kielektroniki, na mara nyingi alionekana akichunguza redio ya baba yake, akijaribu kuelewa jinsi inavyofanya kazi. Katika mazingira yenye changamoto, ambako shule za kata zilikuwa na uhaba wa walimu na vifaa, Joseph alijitahidi sana katika masomo yake, akiamini kuwa elimu ilikuwa tiketi yake ya kutoka kwenye maisha ya kawaida na kuelekea ndoto kubwa. Alikuwa na ndoto ya siku moja kuwa mjasiriamali mkubwa katika sekta ya teknolojia, ingawa wengi waliona mawazo yake kama ndoto zisizowezekana. Baada ya safari ndefu ya masomo, aliingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea Teknolojia ya Habari (IT). Huko, alikutana na changamoto mpya—maisha ya jiji, ushindani wa wanafunzi wengine, na ugumu wa kifedha. Lakini, kila changamoto ilikuwa fursa kwake. Alianza kutengeneza programu ndogo ndogo za biashara, akijifunza mbinu za ujasiriamali kwa vitendo. Baada ya kuhitimu, Joseph alifanya maamuzi magumu—badala ya kutafuta kazi kwenye kampuni kubwa, aliamua kujenga biashara yake mwenyewe. Akiwa na mtaji mdogo, akaanzisha Kweka Group of Companies (KGC), kampuni iliyolenga kutoa suluhisho za kidigitali kwa biashara ndogo na kubwa. Njia yake haikuwa rahisi: alikumbana na vikwazo vya kifedha, usaliti wa washirika wa biashara, na changamoto za kibinafsi. Katika safari yake, alihusiana na watu waliompa msaada na wengine waliomvunja moyo. Alipitia mapenzi ya ujana yaliyojaa matumaini na huzuni. Mahusiano yake na wazazi wake nayo yalipitia majaribu, hasa pale walipoona akipambana na biashara badala ya kazi ya ofisini yenye uhakika. Hii ni hadithi ya kujitoa, maono, na ushindi dhidi ya vikwazo. Ni safari ya kijana wa kawaida aliyethubutu kuwa tofauti—aliyepigana kutoka kijiji cha Mwika hadi kuwa mfanyabiashara maarufu wa teknolojia nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Karibu kwenye safari ya Joseph Kweka, safari ya mafanikio iliyojaa mafunzo, vikwazo, na ushindi.
733
12

CH

ongoing
I want to die judge (Nataka kufa hakimu)
I want to die judge (Nataka kufa hakimu)
I want to die judge ni hadithi ya kijana mmoja aliyeitwa Jamal, ambaye alishuhudia tukio la kutisha ambapo familia yake yote iliuawa kwa ukatili na wanaume wawili. Jamal aliona mwanaume mmoja akikata kichwa cha baba yake na kuondoka nacho mbele yake. Kilicho msaidia Jamal kubaki hai ni msaada kutoka kwa mtu ambaye hakujua alitokea wapi. Baadaye aligundua kuwa huyo mtu alikuwa jasusi kutoka idara ya usalama wa taifa. Jamal alipelekwa wilayani Kyela, jiji la Mbeya, ambapo aliishi kwa miaka saba pembeni mwa mlima Livingstone akifanya mazoezi makali ambayo hakuelewa kwa nini yalifanywa. Baada ya miaka saba, alikabidhiwa mkufu ambao aliambiwa ulinde kwa maisha yake yote, hata kama inahitajika afe ili kulinda mkufu huo (mkufu ndio chanzo cha kila kitu kilichotokea baadaye). Hapo ndipo safari ya kurudi mjini ilipoanza. Jamal alikuzwa na kuwa kamanda mkubwa ndani ya jeshi la Tanzania chini ya usimamizi wa mkuu wa majeshi. Lakini alikumbana na matatizo makubwa alipoanza kufuatilia kundi moja lililojulikana kama M96 OWNER'Z, ambalo lilihusishwa na mauaji ya familia yake. Baadaye, Jamal alishitakiwa kwa kuua makamu wa rais wa Tanzania, ingawa ukweli ulidhihirika baadaye kwamba makamu huyo alikuwa hai. Ilikubaliwa kuwa Jamal alifungwa gerezani kwa kosa la kumwua makamu huyo ambaye alikuwa bado yupo hai. Jamal alipata nafasi ya kutoka gerezani kwa kushirikiana na serikali, lakini aliambiwa atakubaliana na suala la kumrudisha mwanasheria mkuu wa Tanzania, ambaye alikuwa ametekwa huko Medellín, Colombia. Mwanasheria huyo alikuwa ndiye aliyesababisha Jamal afungwe gerezani. Jamal alikubali kumleta mwanasheria huyo, lakini baada ya kumaliza kazi hiyo, alijikuta akitekwa na kupangwa kuuawa kwa sababu alikuwa anajua siri nyingi za serikali na viongozi wa juu waligopa kuwa angeweza kuwaumbua. Jamal alipigwa risasi zaidi ya kumi na mwili wake kutupwa baharini. Baada ya mwaka mmoja, kiumbe cha kutisha kilichoingia mjini kilianza kuwashambulia wale wote waliotekeleza unyama dhidi ya Jamal. Katika ulimwengu wa watu wenye nguvu, alitokea mwanamke aitwaye Catherine, ambaye alidaiwa kuwa mtoto wa mkuu wa kambi ya MAKOMANDO nchini Cuba. Mwanamke huyu alikuwa na nguvu kubwa, na dunia iliamini kuwa hakuna aliyeweza kusimama mbele yake. Jinsi Catherine alivyovuka mipaka ya nchi na kuingia kwenye maeneo ya hatari? Hii ni hadithi ya kutisha—unataka kujua nini kilijificha nyuma ya mauaji ya makamu wa rais na kifo chake kilichosemekana? MASWALI YANAYOHITAJI MAJIBU Kuna nini ndani ya kundi la M96 OWNER'Z? Je, ni nini kilichofichwa nyuma ya mauaji ya makamu wa rais na yeye kuwa hai, ikiwa ulimwengu wote ulijua kuwa amekufa? Mwanasheria mkuu ni nani na kwanini alitekwa Medellín, Colombia? Vipi Jamal alionekana kuwa muuaji wa makamu wa rais na madaktari walithibitisha kifo chake hadharani? Mkuu wa majeshi ni nani na kwanini hakumtetea kijana wake? Jamal alikufa baharini baada ya kupigwa risasi kumi—ni kweli? KUMBUKA Yule aliyeondoka na kichwa cha baba yake, Jamal, ndiye mwanaume aliyeingia Ikulu, akamwua Rais na kuondoka akiwa amepigwa risasi moja tu. Na ndiye huyohuyo ambaye alimpiga mwanaume mwingine aliyetaka kumwokoa, kisha akamkata sehemu zake za siri na kuwarushia mbwa wale. Hadithi hii ni ya kutisha. Ikiwa ulikuwa unawaza maisha yako kuwa ya huzuni, hakikisha unapata nafasi ya kuisoma hadithi hii bora ambayo haijawahi kuandikwa hapo awali. Tuliza akili zako, achana na kila kitu kwa muda huu, kwani ikiwa utachanganya mambo mengi, hautaelewa, na utaishi kwa mashaka. Hii ni hadithi bora na ya ajabu ya Bux the Story Teller. Magic fingers, kalamu ni yangu mwenyewe; Bux the Story Teller. Jina langu naitwa FEBIANI BABUYA.
1242
100

CH

complete
Solo King: Ancient legacy, Dark Majesty
Solo King: Ancient legacy, Dark Majesty
Hapo zamani, kabla ya historia kuandikwa, aliishi mtu mmoja ambaye alivuka mipaka ya asili. Alikuwa mchawi mwenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani, aliyefikia upeo wa juu lakini jina lake lilisahaulika, na urithi wake ulipotea kwa muda mrefu. Kitu kimoja kilichobaki ni kitabu cha kale, kilichoandikwa kwa lugha zilizozungumzwa zamani, lugha ambazo sasa ni za kihistoria. Kitabu hicho kilijulikana kama FORBIDDEN GRIMOIRE, na kilikuwa na masalia ya maarifa yake pamoja na nguvu zisizo za kawaida. Karne zilipita, falme zilikuja na kupita, dunia ilibadilika, na uchawi ukawa ni hadithi tu za kusadikika. Lakini hatima haikupotea. Kijana mmoja aitwaye Jimmy anakuja kubeba hatima yake bila kujua. Usikose simulizi hii ya kusisimua, yenye matukio ya ajabu na mabadiliko ya nguvu. Inamhusu kijana machachari aitwaye Jimmy, anavyopitia changamoto na majira, na jinsi anavyotoka kuwa dhaifu hadi kuwa mwenye nguvu kubwa.
7765
44

CH

ongoing
Safari ya Gavin Luca- Lionela
Safari ya Gavin Luca- Lionela
Idaiwe Maiti Yangu Season 2 ✅ Gavin Luca Katika Idaiwe Maiti Yangu, tulimfahamu Gavin Luca, lakini alibaki kuwa na hali ya kutatanisha. Hatukujua kama alikufa au alifanikiwa kuishi. Zaidi ya hayo, hatukuweza kugundua hatima ya nguvu zake wala mustakabali wa mtoto wake katika zile nguvu. The Odyssey of Gavin Luca inakuja kutoa majibu ya maswali haya yote. Tutajua kilichotokea wakati ule, nini kilitokea kwa Gavin Luca, na ni nini kinatarajiwa kutokea siku zijazo. Lionela, mtoto pekee wa Gavin Luca, anakuja kuwa kiumbe mwenye nguvu nyingi duniani, akitambua ukweli kwamba baba yake alikuwa mfu. Lakini je, ni kweli alikufa? Hatujapata uthibitisho wa kifo chake, na hakuna ishara ya uwepo wake. Kama alikufa, kwa nini hakukuwa na dalili yoyote ya upanga wake au alama nyingine za uwepo wake? Kama alifanikiwa kuishi, alifanikiwaje kutoka kwenye hali hiyo? Alipo wapi sasa, na ni nini hatima yake? Nini Kinaendelea Kuikumba Familia Hiyo Maarufu na Tajiri? Je, kuna mtu alisahaulika katika The Immortals, au kuna siri nyingine nyuma ya pazia? Nakaribisha kutazama hii simulizi inayofuata! Hautakiwi kuikosa simulizi hii kwa gharama yoyote ile. Kabla ya kuisoma hii, hakikisha umesoma Idaiwe Maiti Yangu, kwani ni sehemu ya kwanza ya hadithi hii. Idaiwe Maiti Yangu inapatikana hapa Fasihinet, ikiwa imekamilika kabisa. Kazi Kwako ✍️ Twende Sawa ✅ WhatsApp: +255621567672 Wao wananiita Bux the Storyteller. Jina langu ni Febiani Babuya. Wasalaam.
1981
121

CH

complete
Mikasa ya ajabu nilioishuhudia kwa macho yangu
Mikasa ya ajabu nilioishuhudia kwa macho yangu
Kwanza kabisa, nianze kwa kusema kuwa nina mikasa miwili ya kipekee ambayo nimewahi kuishuhudia kwa macho yangu na kuifanya kwa mikono yangu mwenyewe. Mkasa wa kwanza unahusu mimi na ndugu zangu, ulitokea nikiwa na miaka 14 - 15, mwaka 2000 - 2001, huko mkoani Mara, wilaya ya Tarime, Tanzania. Mkasa wa pili unanihusu mimi pia, na ulitokea nikiwa mtu mzima, kuanzia mwaka 2012 hadi 2018. Huu ni mkasa wa maisha ya kitajiri, uliohusisha nguvu za giza. Kuna nyuzi kadhaa ambazo nimekuwa nikizisoma za watu mbalimbali wakisimulia visa na mikasa ya maisha yao au ya jamaa zao, ambayo waliwahi kupitia. Hivyo, nikajiona kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuleta simulizi za maisha yangu ili kuwafundisha na kuwaonya vijana wenzangu, hasa wale wenye tamaa ya kupata mali kwa njia niliyoifanya mimi. Naomba wale vijana waache mara moja, kwa sababu mwisho wake unaweza kuwa kifo mikononi mwa shetani. Ingawa mimi niliponea chupuchupu.
771
0

CH

ongoing
Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa
Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa
Naitwa Rojaz, nikiwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita katika familia yetu. Nimezaliwa kwa wazazi ambao walikuwa na ndoto ya kuona watoto wao wanapata elimu bora na kufikia malengo yao. Hii ni ndoto ya kila mzazi, kwani hakuna mzazi anayewalea watoto wake bila kutamani kuona wanapata mafanikio katika masomo yao. Nimeweza kufika kidato cha nne, lakini matokeo yangu hayakuwa mazuri. Nilijikuta nikikosa majibu ya moja kwa moja kuhusu sababu ya kushindwa kwangu. Hata hivyo, najua kuwa uzembe wangu na uzembe wa wenzangu shuleni ulifanya niwe na matokeo duni. Wakati wengine walijitahidi na kuzingatia masomo yao, mimi niliwekeza muda wangu kwenye michezo isiyo na tija. Hii haimaanishi kuwa nilidhihaki elimu, bali mazingira yangu na familia yangu ya kipato cha chini yalichangia katika changamoto nilizokutana nazo. Elimu yangu, kuanzia kidato cha kwanza, ilitegemea michango ya familia, marafiki, na misaada kutoka kwa shangazi au mamdogo. Kwa kifupi, nilikulia katika familia duni, lakini hiyo haikunizuia kutoka kwa juhudi yangu ya kuboresha maisha yangu.
942
2

CH

ongoing
IDAIWE MAITI YANGU
IDAIWE MAITI YANGU
GAVIN LUCA Ndilo jina ambalo limeishikilia Idaiwe Maiti Yangu. Hili ni jina la mwanamume mmoja ambaye anatusafirisha mpaka Kenya, ndani ya msitu wa Mau, ambako ndiko kila kitu kinapoanzia. Mwanzo wa simulizi hii unaanza na mwanaume huyo akiwa ametekwa na makomando wa Jeshi la Tanzania. Aliteswa vikali, kisha akauawa kwa kupigwa risasi baada ya kuchomwa moto. Lakini muda mfupi baadaye, jambo la ajabu lilitokea. Mtu mwingine aliingia katika eneo hilo na kuwaua makomando wote, isipokuwa mwanamke mmoja tu aliyenusurika, aitwaye Sarah Martin. Sarah alishangazwa sana kumwona mwanamume huyo, kwani alikuwa ndiye yuleyule waliyemuua dakika chache zilizopita. Inawezekanaje? Idaiwe Maiti Yangu itatupatia majibu sahihi. Gavin Luca alikuwa akitafutwa na mamlaka za usalama kwa miaka mingi, mpaka alipokuja kujitokeza hadharani. Kutokea kwake kulisababisha maafa makubwa ndani ya Afrika, yakiwemo mauaji ya zaidi ya marais wawili. Mwanaume huyu anatoka katika familia yenye historia ya kutisha na utata mkubwa. Hatimaye, akawa kiumbe wa ajabu kabisa kwenye dunia ya watu wenye mabavu. Gavin Luca pia aliaminika kuwa na nguvu zisizo za kawaida, ambazo alipata huko China. Kurejea kwake kulianza enzi mpya ya utawala wa familia yake ndani ya Afrika nzima. Sasa Gavin Luca ni nani? Alitokea wapi? Kwa nini alitafutwa kwa miaka mingi? Ni nguvu za aina gani alizokuwa nazo? Na kwa nini alionekana akiwa hai baada ya kuuawa? Hii ni simulizi moja bora sana kuwahi kuandikwa hapa Tanzania. Twendeni sawa, tukazifunuue kurasa za kiumbe huyu wa ajabu. NB: Simulizi hii ni ya kutunga tu. Haina uhalisia wa maisha ya mapenzi, ujasusi, siasa, usaliti, uzandiki, watu, mauaji, nguvu za ajabu, na yote yaliyoandikwa humu ndani.
1392
105

CH

complete
JUMBA JEUSI
JUMBA JEUSI
JUMBA JEUSI...... SIASA NI KAMARI....Je NANI HUIBUKA MSHINDI? JUMBA JEUSI ni andiko ambalo linaangazia siasa kwa ujumla wake.... Inaangazia namna viongozi duniani wanavyo yatumia madaraka kuhadaa watu lakini pia kufanya mambo ya kutisha... JUMBA JEUSI ni sanaa ya siasa ndani ya maandishi....utajifunza namna wananchi wanavyo danganywa na wanasiasa, namna wanasiasa wanavyo yafanya mambo ya kutisha nje ya macho ya kawaida ... Je wananchi wanapaswa kufanya nini kuhakikisha wanaikimbia hiyo hali na kuyapigania maslahi ya mataifa yao? Kumbuka tu kwenye kundi la wajinga wengi ambao wanadanganywa na wanasiasa huwa wanaibuka watu werevu, sasa watu hao huwa hawataki kwenda na ule ubaradhuli wa wanasiasa na mambo huwa yanaanza kubadilika hapo kwa sababu wanasiasa huwa hawawapendi watu wa namna hiyo..... Unahisi inakuaje kwenye mtanange wa namna hiyo baina ya watu werevu ambao wanaamua kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kuwapigania wengi na mataifa yao? NI WAKATI SAHIHI WA WEWE KUYAPATA MAJIBU KWA KULISOMA ANDIKO HILI. KWA LEO NAKULETEA SEHEMU YAKE YA KWANZA Bux the storyteller CIAO
1658
101

CH

complete
Chanzo Ni Yeye
Chanzo Ni Yeye
Simulizi ya kubuni ya kijana wa mtaani aitwaye Ayubu ambaye kwa sababu zisizojulikana anajikuta akiwa na maadui wengi bila kuwatambua....kuna chanzo cha yote tafadhali ungana na mimi mwandishi wako Machokulenga TZ
860
25

CH

ongoing
Gereza la Hazwa
Gereza la Hazwa
Mvua ilimwagika kwa nguvu, upepo mkali ukiparaganya miti na radi zikilipuka mithili ya mapigo ya ngoma za kuzimu. Huu si msitu wa kawaida—ni Elnino, kichaka kinachokomeza roho za wasiotarajia, hata mchana ukiwa na giza lisilo na mwisho. Lakini usiku huu, kivuli kilikuwa kinakimbia kwa kasi isiyoelezeka, miguu yake ikizama kwenye tope zito. Uso wake ulikuwa umefunikwa na nywele chafu na ndevu ndefu, macho yake yakiangaza hofu isiyoelezeka. Alikuwa akitoroka—lakini kutoka kwa nani? Nyuma yake, wanaume sita walimsakama. Wanne walikuwa wamevaa mavazi ya kininja, wakipotea na kurejea kwenye giza kama manyoya yanayorushwa na upepo, huku wawili wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi. Hakukuwa na huruma katika macho yao—mauti pekee ndiyo aliyoyajua. Kisu kikubwa kiliruka kwa kasi kuelekea shingo yake, kikapita kwa milimita chache tu. Punde, alikata mwelekeo na hakuwapo tena. Mmoja wa wawinda wake alisimama, akisikiliza kwa makini—lakini upepo ulisambaza sauti kila upande, ukivuruga hisia zake. Walielekezana kimyakimya: "Muaue." Lakini ghafla… tone la jasho likamdondokea mmoja wao. Akakoki bastola, akaiinua juu, akifyatua bila kusita. Hakuna kilichompata mtu huyo wa kutisha, aliyejirusha kutoka juu ya mti kwa kasi isiyoelezeka. Mikono yao ilikutana kwa sekunde chache, mapambano ya mwili kwa mwili yakaanza juu ya mti. Risasi sita zilifyatuka—hakuna hata moja iliyompata. Mlio wa mifupa ukasikika. Shingo ya askari mmoja ilikatika kwa sekunde chache tu. Mwili wake ukaanguka huku damu ikimwagika kwa kasi. Mwanaume huyo mchafu hakuwa na muda wa kusherehekea ushindi. Kisu kikubwa kilikuwa kimetua mgongoni mwake, kikamdhoofisha—lakini hakuwa tayari kufa. Mbele yake kulikuwa na maporomoko makubwa yasiyo na mwisho. Nyuma yake, waninja wanne na askari mmoja wamesimama, wakimtazama kwa macho baridi. Hakuhangaika kugeuka… alijirusha kwenye giza la maporomoko. "He is not human, he’s completely a devil." "But no survive, he is no more there." "Let's go and take Donald’s body." Walidhani kuwa msako wao umeisha. Lakini walikosea… Mwanaume huyu alikuwa mfungwa wa miaka 10 katika gereza ambalo hakuna aliyewahi kutoroka kwa miaka 200. Gereza ambalo hakuna mfungwa anayejua lilipo. Lakini leo, mtu mmoja yuko nje. Nani huyu? Ni kwa nini wanamtaka afe? Na je, kweli ameangamia kwenye maporomoko hayo...?
2255
116

CH

complete
Mapenzi na kisasi
Mapenzi na kisasi
Simulizi inaelezea nguvu ya mapenzi na kisasi kwa mtu anayetaka kuondoa furaha yako ya mapenzi
1388
16

CH

complete
Damiani
Damiani
Damiani mhitimu wa chuo kikuu cha uhasibu , anahitimu masomo yake na kurudi kijijini kwao kwa ajili ya kusubiria upepo wa ajira lakini katika hali ya kutokutegemea mama yake kipenzi anapigwa risasi mbili za kifuani na kufa hapo hapo na hio inatokana na kumpatia msaada mwanaume ambae hamfahamu mwenye asili ya ulaya (mzungu ) ambae na yeye alikuwa kwenye hatua ya mwisho ya kupoteza uhai wake kwani alikuwa na jeraha la risasi tumboni ,lakini mzungu huyo kabla ya kupoteza maisha anamkabidhi damiani nyaraka bila kumpa maelekezo ya aina yoyote ile . Damiani anajikuta anajenga chuki na kisasi kwa watu waliohusika na mauaji ya mama yake , anajiapiza kuwatafuta mahali popote pale na kulipiza kisasi , katika harakati za kuwatafuta wabaya wake anajikuta akifahamu siri nzito iliokuwa nyuma ya kifo cha ghafla cha raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , anapata waraka ulioachwa na raisi huyo uliopewa jina la KAULI YA MWISHO YA RAIS KABLA YA KIFO CHAKE . JE UNAFIKIRI ATAFANIKIWA KULIPIZA KISASI CHAKE ? JE NI KAULI GANI YA MWISHO ALIO ACHA MHESHIMIWA RAISII KABLA YA KIFO CHAKE ?. simulizi hii imekamilika , mwandishi ataiweka hapa hivi punde .
1660
3

CH

complete
Shetani rudisha akili zetu
Shetani rudisha akili zetu
Ni kipindi cha mwaka mmoja tangu nirudi nchini Tanzania nikitokea nje ya nchi, ambako niliishi kwa zaidi ya miaka ishirini. Kwa lugha nyepesi, tangu nikiwa mdogo maisha yangu yote yalikuwa nje ya nchi — na siyo katika taifa moja tu, bali katika mataifa mbalimbali, kwenye mabara tofauti tofauti. Sababu ya kurudi Tanzania, nchi ambayo nina kumbukumbu chache sana za utoto wangu, ilikuwa kutafuta asili yangu, wazazi walionileta duniani, lakini vilevile kutafuta utulivu na amani ya maisha. Nimepitia mengi sana nikiwa nje ya nchi — mambo ambayo kwa mtu wa kawaida hayawezi hata kufikiriwa. Kwanza kabisa, nilifika Tanzania kwa siri sana. Hata marafiki zangu niliowaacha nje ya nchi sikuwataarifu kuwa nilikuwa nasafiri kwenda nchi gani ya Afrika. Hivyo, hata nilipoingia jijini Dar es Salaam, sikutaka kuishi maisha niliyozoea huko nje; nilitaka kuishi maisha ya kawaida, ili nijifiche dhidi ya watu wanaonifahamu. Ndiyo, unaweza kushangaa. Ukweli ni kwamba nina maadui wengi sana wanaonitafuta kila kona, na yote hayo yanatokana na historia yangu ya maisha — kuanzia nilivyokuwa mdogo, nilivyojikuta nikiwa nje ya nchi, hadi kazi nilizowahi kufanya huko. Basi nilipanga chumba maeneo ya Gongo la Mboto, chumba cha kawaida sana ambacho hakikuwa hata na choo ndani. Nilinunua godoro la kawaida na kulitandika chini, nikinunua pia mahitaji madogo madogo. Kwa ufupi, niliishi kama kijana anayeanza maisha ya kujitegemea. Kwa ukweli, kuanzia hapo niliishi maisha ya kawaida. Nilianza kutumia ujuzi wangu nilioupata nje ya nchi — kuwa fundi na hata mwalimu wa tuition. Yote hayo yalikuwa kwa ajili ya kujitafutia kipato cha kuweza kumudu maisha. Unaweza kushangaa, lakini ukweli ni kwamba nina pesa nyingi sana — nina utajiri unaozidi hata wa Bill Gates au Elon Musk mwenyewe. Lakini kutokana na aina ya utajiri huo, ambao nilipata kwa njia zisizo za kawaida, sikutaka kutumia fedha hizo. Nilihitaji, kwa mara ya kwanza, kutumia hela ambazo ninazipata kwa njia halali. Ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu niingie nchini Tanzania, hatimaye nilikuwa nimezoea jiji. Watu wengi waliniita kwa majina ya huduma nilizowapatia — wapo waliokuwa wananita fundi, wengine mwalimu, na hata wengine mwanafunzi mwenzao. Basi bwana, siku moja nikiwa napekua pekua mtandao wa JamiiForums — mtandao ambao nilikuwa nikiupenda hata nikiwa nje ya nchi — niliona tangazo kwenye jukwaa la mahusiano. Lilikuwa tangazo la kawaida sana, lililoonekana kama mzaha. Tangazo lenyewe lilikuwa la mwanamke aliyekuwa akitafuta mwanaume wa kuigiza kuwa mpenzi wake, kwa malipo ya mwezi. Halikuwa na maelezo mengi zaidi ya kichwa cha habari hicho. Mwanamke huyo aliandika tu sifa za mtu anayemtaka — awe mwenyeji wa jiji la Dar es Salaam, dini yoyote, umri usiozidi miaka thelathini, asiwe na watoto, na awe na urefu wa wastani. Watu wengi, mara baada ya kuona tangazo hilo, walilidharau. Walianza kulidhihaki kwa kusema, “Ni Mtanzania gani hasa, mwanamke, anayeweza kutafuta mpenzi wa kumlipa?” Wengi walianza kumtusi na kumzushia maneno ya kashfa. Upande wangu, nilifurahishwa na maoni hayo yote. Hata hivyo, mimi nilikuwa na mtazamo tofauti — pengine kutokana na uzoefu wangu nikiwa nje ya nchi. Kwa namna tu tangazo lilivyokuwa limeandikwa, niliamini kabisa kwamba mhusika alikuwa serious. Kitu kilichonivutia zaidi, ambacho pia kilifanya wengi wadharau, ni kwamba mwanamke huyo aliweka wazi kiasi cha mshahara: shilingi laki saba kwa mwezi. Kwanza nililipuuza, lakini siku ya pili nikajikuta kuna sauti ndani yangu ikisema, “Jaribu kuomba, pengine ni kweli.” Basi nikafanya hivyo. Niliandika maelezo yangu mafupi — jina langu, Hamza Mzee, umri wangu, na mwonekano wangu wa kuchanganya damu ya Mwafrika na Mzungu. Baada ya siku kama mbili, nikiwa nimeshasahau kabisa kuhusu tangazo hilo, asubuhi moja nilipokea simu kutoka kwa namba mpya. Nilipoipokea, mtu alijitambulisha kama ndiye aliyeweka tangazo kwenye mtandao. Ee bwana eeh! Kwanza kabisa, sauti yake ilikuwa ya mwanamke, na kwa sauti hiyo tu niliweza kuhisi ni mwanamke mzuri kupindukia. Hisia zangu hazikunikosea. Licha ya kushangazwa na ukweli kwamba nilitafutwa kwa ajili ya usaili wa kuwa boyfriend feki, nilivutwa kabisa na sauti yake tamu. Maelezo kutoka kwa mwanamke huyo yalikuwa mafupi na wazi. Aliniambia nimechaguliwa kwa ajili ya usaili wa kazi hiyo, na kama niko tayari nifike kesho yake kwenye hoteli moja kubwa jijini Dar es Salaam. Bila kusita, nilikubali — nikiwa na shauku na maswali mengi kichwani. Kwa ufupi, siku iliyofuata nilifika katika hoteli hiyo ambayo ilikuwa na mandhari tulivu na harufu ya kifahari. Sikuwa na wasiwasi — maeneo kama hayo nilikuwa nimezoea. Ni kwamba tu, baada ya kurudi nchini, niliamua kuishi maisha ya kimasikini. Hapo ndipo nilipokutana na mwanamke mrembo sana aliyejulikana kwa jina la Regina. Niwaibie siri — yule mwanamke mwenye sauti tamu aliyeniambia nifike kwenye usaili hakuwa Regina! Kukutana na Regina ndio mwanzo wa maisha yangu ya nyuma kunianza kuniwinda tena. Ndipo maadui zangu walipoanza kupata taarifa kuhusu nilipo, wakaanza kunifuatilia — na walipopata habari kwamba nina mpenzi, hata kama ni wa feki, ndipo walipopata nguvu zaidi.
38605
475

CH

ongoing
Masaa mawili ya kumbukumbu
Masaa mawili ya kumbukumbu
Kijana Masumbuko ambae anaonekana kuwa na uwezo usiowa kawaida , uwezo wa kumfanya mtu kufanya kile anachokitaka yeye kwa kumkonyeza machoni huku akishidnwa kujua uwezo wake unatokana na nini , anaianza safari kutokea mkoani Tanga kuelekea mkoani Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta maisha kama ilivyo kwa vijana wengi ambao wanaamini kuishi ndani ya jiji la Dar es salaam ndio njia rahisi ya kutoboa kimaisha. Kama ilivyokuwa jina lake hakuwa na maisha mazuri wala pesa yoyote mfukoni ya kumuwezesha kufika jijini Dar es salaam, kitu pekee ambacho alikuwa nacho na kujiamini anaweza kukamilisha safari yake hio ni uwezo wake wa kumpumbaza mtu kwa kumwangalia usoni kwa kile ambacho yeye anakiita kwamba ni masaa mawili ya kumbukumbu zake. Hatimae kwa uwezo wake huo wa ajabu anafanikiwa kula na kushiba na kupanda basi ambalo linamfikisha jijini Dar es salaam burea kabisa. Ndani ya jiji la Dar es salaam anakutana na Peter kijana msomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam , kutokana na namna ambavyo wamekutana wanajikuta wanakuwa marafiki wa kubwa na Peter anamxchkua Masumbuko na kwenda kuishi nae. Peter ni mtoto wa Irene mwanadada ambae kazi yake ni uchangunduo kazi ya kuuza mwili wake kwa kufanya mapenzi na wanaume tofauti tofauti na kujipatia hela. Irene miaka mingi nyuma akiwa katika harakati za kazi hio , anajikuta anapata mteja tajiri afahamikae kwa jina la Samir, katika hali ya kushangaza tofauti na siku zote ambazo amefanya kazi Samiri anampatia Mimba Irene. Irene anagoma kutoa ujauzito kwa hofu ya kukosa kizazi baadae , hivyo anafanya maamuzi magumu na kulea ujauzito huo na licha ya kujua Samniri hawezi kukubali ujauzito wake anachukua maamuzi ya kijasiri na kwenda kumwambia kama amepata ujauzito wake na hawezi kuutoa kwasababu yta kuogopa kukosa mtoto baadae. Samiri anamfukuza Irene nyumbani kwake na kumwambia hatambui ujauzito huo , lakini licha ya hivyo mke wake Samiri afahamikae kwa jina la Shani anagundua juu ya swala la Irene kubeba ujauzito wa Samiri na jambo hilo linamchukiza sana na kuogopa kwa kudhania kwamba licha ya Samiri kukataa ujauzito huo mbeleni anaweza akamtafuta mtoto wa Irene na kumrisha mali za familia. Kutokana na hilo anaandaa mpango na kukodi mtu wa kumfatilia Irene kila siku na kumpa taarifa zake , miaka kadhaa mbele Peter anazaliwa na anafafikisha umri wa miaka saba na Shani anamtengenezea Irene ajali na anapoteza maisha. Peter anampoteza mama yake bila ya kujua wazazi wake na maisha yanaanza upya anafauafuru vizuri kwenda kidatoi cha kwanza ana anapata ufadhili kwa kampuni ya misaada ya F and R foundation , kampuni ambayo inaongozwa na baba yake Samiri na Peter anafanikiwa kutetea ndoto zake kama ilivyo kwa watoto wengi wenye uwezo na anafdika chuo. Siku moja akitoka kufana ununuzi wa simu katika mall za Mlimani City anajikuta kushangazwa na urembo wa binti mmoja ambae alikuwa akiingia katika maduka hayo kwa jili ya kufanya ununuzi, kitendo cha kushangaa anajikuta simu yake inakwapuiliwa na vibaka na kutokana na tukio hilo linamkiutanisha na Masumbuko ambae anamwahidi Peter anao uwezo wa kwenda kumrudishia simu yake kama tu atamslipa kiasi cha hela. Peter anashangazwa na masumbuko lakini mwisho wa siku anakubaliana na Masumbuko kwseli anafaikiwa kumrudishia Peter simu yake
2892
3

CH

complete