SEHEMU YA 2: Usiku wa Siri Ndani ya Jiji la Roma

Sauti ya hatua za viatu vizito kwenye korido ilizidi kuwa karibu na mlango wa ofisi ya Profesa Gabriel. Moyo wake ulikuwa ukidunda kifuani kama ngoma ya kivita. Alijua hana muda. Huku akitambaa sakafuni kwenye giza, alizikusanya zile karatasi za siri zilizotawanyika na kuzisukumia haraka ndani ya mkoba wake wa ngozi. PAAA! Mlango wa ofisi yake haukugogwa; ulipigwa teke kubwa na kuanguka ndani. Watu wawili warefu, waliojifunika nyuso zao kwa masks nyeusi, waliingia wakiwa na tochi zenye mwanga mkali wa…