SEHEMU YA 7: Pazia Linapofungwa: Nani Hasa Anashika Remote ya Dunia?

Giza la Vault ya mwaka 1895 lilionekana kuwa zito zaidi huku sauti ya Arturo Sosa—yule Papa Mweusi—ikitoka kwenye spika ndogo za kompyuta ya Elena kwa utulivu wa kutisha. Uso wake kwenye skrini ulikuwa hauna chembe ya wasiwasi, kama mchezaji wa chess anayejua kuwa amemkamata mpinzani wake katika hatua ya mwisho ( Checkmate ).Gabriel alikuwa amesimama imara, kidole chake kikitetemeka juu ya kitufe cha Enter . Bonyeza moja tu ya kitufe hicho ingesambaza zile Cryptographic Keys za akaunti za siri…