Sehemu 33: Mikono ya Siri Kwenye Umoja wa Mataifa (UN)
Unapofikiria kuhusu chombo chenye mamlaka makubwa zaidi ya kisheria na kidiplomasia duniani, jibu la haraka huwa ni Umoja wa Mataifa (UN) . Makao Makuu ya UN yaliyopo jijini New York yanajulikana kama uwanja ambapo mataifa makubwa yenye nguvu za kijeshi na kinyuklia kama Marekani, Urusi, na Uchina huchuana vikali kulinda maslahi yao kupitia kura na kura za turufu (veto). Hata hivyo, kuna mchezaji mmoja wa kipekee ambaye hana jeshi, hana kura ya turufu ya wazi, na hahesabiki kama mwanachama kamili…