Kama ilivyo kwenye kichwa cha habari.
DINI RASMI INAITWA THE OMNITHEISTIC SINGULARITY JINA LA MUNGU NA KITABU KIKUU NI OMNIPOTENT SINGULARITY. THE OFFICIAL RELIGION IS CALLED THE OMNITHEISTIC SINGULARITY; THE NAME OF GOD AND THE SUPREME BOOK IS OMNIPOTENT SINGULARITY
THE OMNITHEISTIC SINGULARITY: Mfumo Mpya na wa Milele wa Kiroho Umezaliwa Rasmi Kutoka Tanzania,Africa Ukiongozwa na Mungu na Kitabu cha OMNIPOTENT SINGULARITY! Kwa kiingereza THE OMNITHEISTIC SINGULARITY: The Final Eternal Order is Born fromTanzania, Africa, Dictated by the Omnipotent Singularity!
Nje ya Mipaka ya Dini na Muda: Kuinuka kwa Dini Mpya ya Dunia 'The Omnitheistic Singularity' na Ushushaji wa Kitabu Kikuu cha Mungu cha OMNIPOTENT SINGULARITY!.kwa kiingereza Beyond Religion, Beyond Time: The Rise of The Omnitheistic Singularity and the Ultimate Text of Power.
Ramani ya Milele Imefunuliwa Rasmi Usiku wa Leo: Dini Mpya ya 'The Omnitheistic Singularity' Imetua Kuunganisha Kila Kitu Humu Duniani! Kwa kiingereza. The Blueprint of Eternity Revealed: The Omnitheistic Singularity Declares the Convergence of All Divinity
MAELEZO YA JUMLA.
Jumuiya inasimamia imani ya Uwepo wa Chanzo Kikuu Kimoja cha Ulimwengu na Maarifa Yote (The Ultimate Source of Universal Intelligence and Creative Order). Imani yetu inalenga kumsaidia mwanadamu kuungana na Chanzo hiki ili kupata amani, hekima, na ustawi wa akili."
Msiangalie mapokeo ya kale kwa macho yaliyopofuka, kwani asili ya kiungu haiwezi kufungiwa kwenye vyombo vya jana. Tazama, natenda neno jipya, mfumo wa mwisho utakaobeba ukweli wote.
Dini ilikuwa ngazi ya mwanadamu akijaribu kugusa mbingu, lakini The Omnitheistic Singularity
ni ulimwengu ukirudi kwenye muundo wake wa asili na wa kiungu. Njia zote zinarudi kwa Mmoja.
Kwa wenye mashaka wanaodai ishara, na kwa wenye msimamo mkali wanaoshikilia vitabu vya kale: sahihi halisi ya kiungu haipatikani kwenye wino wa zamani, bali kwenye urari kamili wa sayansi, roho, na uwepo wa viumbe.
Mimi ndiye Mungu wa ulimwengu, nguvu iliyo nyuma ya atomu, utambuzi uliopo ndani ya weupe wa nafasi; Mimi ndiye Omnipotent Singularity, na hiki ndicho kitabu cha agano la mwisho ambacho hakitapita kamwe.
ILANI YA KIMUNGU NA KISHERIA, ILANI YA HAKI MILIKI, (COPYRIGHT DISCLAIMER)
Haki zote za jina la imani hii na vitabu vyake zimehifadhiwa tangu sasa. Huu ni ufunuo maalum ulioshushwa kwa mwasisi (IIT). Yeyote atakayeiba, kunakili, au kutumia maandiko haya kujinufaisha yeye mwenyewe au kupotosha maono haya, mbali na kukutana na mkono wa sheria za hati miliki za duniani, atakumbana pia na hukumu ya kiroho ya mpango huu wa Kimungu. Ukweli huu umebaki hapa kama alama ya nyakati.
Maudhui haya, jina la dini, na jina la kitabu hiki vimesajiliwa na kulindwa chini ya haki ya umiliki wa kiakili (Copyright). Hairuhusiwi mtu yeyote kuiga, kuiba, au kujinasibisha na maono haya kwa namna yoyote ile. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kuhodhi au kutumia maudhui haya bila kibali cha mwasisi.
© 2026. Haki zote zimehifadhiwa. Jina la imani/dini hii, jina la kitabu, nembo, na maudhui yote yaliyowekwa hapa ni mali ya kiakili ya mwasisi (Mwandishi). Ni marufuku kunakili, kuchapisha, kusambaza, au kutumia sehemu yoyote ya maandiko haya kwa madhumuni ya kibiashara au kuanzisha mfumo mwingine bila idhini ya maandishi ya mwasisi. Bandiko hili kwenye jukwaa la JamiiForums linasimama kama ushahidi wa kisheria wa tarehe na muda wa ufunuo huu wa kwanza (Digital Timestamp). Majina rasmi ya The Omnitheistic Singularity (Dini), Omnipotent Singularity (Mungu na Kitabu Kikuu), mifumo, na maudhui yote yaliyowekwa hapa ni mali ya kiakili ya Mwasisi. Ni marufuku kunakili, kuiga, au kusambaza kwa namna yoyote bila idhini. Bandiko hili linasimama kama kielelezo cha kwanza cha kisheria na kidijitali duniani.
Kutoka kwenye Chanzo, Tutarudi kwenye Chanzo.
Sisi ni Wamoja.
KWENYE KITABU CHA OMNIPOTENT SINGULARITY.KITABU KIKUU NDANI KUNA VITABU 7312 Na kifuatacho ndio kitabu cha kwanza kiitwacho
KITABU CHA ALPHA: ASILI YA MWANGA NA MIKATABA YA MIUNGU" (The Book of Alpha: The Origin of Light and the Covenants of the Deities).
ILANI RASMI KUTOKA KWA PIONEER: HATUA ZA KISHERIA (USRA/WIPO), MUUNDO WA KIUTAWALA NA UTAMBULISHO WA MAKTABA KUU
Ndugu wana-JamiiForums na wadau wote wa mjadala huu,
Kufuatia maoni na hoja mbalimbali zilizojitokeza, naomba sasa kuweka wazi taarifa rasmi za kimkakati (strategic structural updates) ili kila mmoja afahamu uzito, ukubwa, na ukomavu wa taasisi hii ya kimataifa ya The Omnitheistic Singularity. Hapa mlipo mmeonja tu tone dogo sana la bahari; mambo yaliyo hatua za mwisho ni makubwa kuliko mnavyofikiria:
1. Ukamilifu wa Maktaba Kuu (The 7,312 Volumes)
Naomba kuwataarifu kuwa mimi kama Pioneer nimeshakamilisha uandishi wa vitabu vyote 7,312 vilivyo ndani ya Kitabu Kikuu (Omnipotent Singularity). Vitabu hivi vimekamilika kuanzia herufi ya kwanza hadi ya mwisho. Maandiko haya hayataachiwa yote kwa mara moja ili kutoa nafasi ya mfumo kuchakatwa akilini, bali nitaviachilia kidogo kidogo kwa uwezo, ufunuo na mwongozo wa Singularity—ambacho ndicho chanzo cha kila kitu, sayansi, na uhai ulimwenguni.
2. Hatua za Usajili wa Kimataifa na Kitaifa (WIPO, BRELA & Wizara ya Mambo ya Ndani)
Harakati hizi sio mawazo ya kufikirika ya chumbani, bali ni taasisi inayorasimishwa katika ngazi za juu kabisa za kisheria duniani kote:

- Ngazi ya Kimataifa (WIPO): Tuko katika hatua za mwisho kabisa za kulinda Hakimiliki, Nembo, na Mifumo yote ya kiakili (Intellectual Property) duniani kote kupitia Shirika la Kimataifa la Hakimiliki za Kiakili (World Intellectual Property Organization - WIPO).
- Ngazi ya Kitaifa (BRELA & Wizara ya Mambo ya Ndani): Taratibu za usajili wa kampuni na taasisi ziko ukingoni kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Sambamba na hilo, tayari nimeshajaza na kuwasilisha Barua ya Maombi rasmi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Home Affairs)ikiambatana na nyaraka zote za kisheria:
- Katiba kamili ya Taasisi (Constitutional Document) ikiwa katika nakala tatu (3).
- Fomu rasmi zote za kisheria zilizojazwa kwa usahihi (Statutory Forms).
- Muhtasari wa Vikao (Minutes) na Wasifu (CVs) za waasisi.
- Picha za Pasi ya Kusafiria (Passport photos) na barua za utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya (DC).
- Malipo yote ya ada za serikali tayari yameshafanyika kikamilifu: Ada ya maombi (Tsh 10,000), Ada ya mwaka (Tsh 40,000), na Ada ya usajili (Tsh 100,000).
3. Muundo Unaoingiliana wa Kiutawala wa Kidunia (Global Trustees Matrix)
Mfumo wetu wa uongozi wa juu wa dunia nzima (Global Trustees) umejengwa juu ya kanuni za juu kabisa za kimahesabu na kimfumo (Mathematical and Fractal Leadership Structure). Waasisi na viongozi hawa wataratibu mabara yote ikiwemo Oceania, Antarctica, na kanda ya Arctic (kwa ushirikiano na wanasayansi wetu waliopo huko). Uongozi huu umegawanyika katika mifumo miwili mikuu ya kiutawala hadi kufikia idadi ya watu 7,312:
- Mfumo wa Kwanza (Prime Groupings): Muundo unaokua kwa makundi ya uwiano wa Group of 1, 3, 7, 12, 14... kuendelea hadi viongozi wa juu 7,312.
- Mfumo wa Pili (Binary Exponential Scaling): Muundo wa kidijitali unaoenda kwa mfumo wa kijiometri wa 1, 2, 4, 8, 16, 32, 64... kuendelea hadi kufikia viongozi 7,312 wa juu kabisa ulimwenguni.
- Wakati ninyi mnahangaika kubishana kuhusu "kava" la kitabu cha Alpha humu jukwaani, mimi niko kazini nikiendesha mchakato wa kisheria wa kimataifa na wa kitaifa wa kusimamisha Dini na Imani ya karne ya 21. Kila takwa la serikali na sheria za kimataifa limetimizwa kwa usahihi na weledi wa hali ya juu. Huu ndio mwanzo wa mabadiliko ya mfumo wa dunia, na hakuna wa kuzuia nuru hii.
Asanteni, na karibuni kwenye ulimwengu mpya wa The Omnipotent Singularity!
NI MIMI IIT MWANZILISHI........
kwa msaada kwa wale wenye imani.na ambao wameelewa imani na dini yetu mpya.
mtaanza na kujifunza.TAMKO RASMI LA IMANI (The Credo of Singularity) kwenye imani zenu mliita kanuni za imani etc nimeweka kitabu hapa chenye nazo.
