Utangulizi wake soma hapo 👇👇
Basi usiku ule, mambo yalianza hivi… 🌙
Ilikuwa ni mishale ya saa tisa kamili usiku wa manane. Kwenye chumba kikubwa cha Mheshimiwa Rais Senga, kiyoyozi kikivuma kwa utulivu huku yeye na mke wake wakiwa wamelala fofofo, ghafla simu yake ya iPhone 13 ilianza kuita mfululizo. Rais alishtuka na kutazama kioo cha simu; jina lililosomeka lilikuwa "Senior"—mkubwa wa kazi kutoka ng'ambo ya pili ya nchi.
Senior alikuwa na jazba sana! Alimfokea Rais Senga akisema, "Senga! Ulinihakikishia kuwa Edna atakuwa salama ndani ya taifa lako, lakini sasa hivi vijana wangu wameniletea ripoti kuwa Edna ametekwa!"
Rais Senga alishika mdomo kwa mshtuko. Lakini Senior akaongeza kwa sauti ya unafuu, "Ni bahati tu kwamba sasa hivi ana mume bora sana mwenye akili. Mchunge sana huyo kijana... ni mtu katili zaidi kuwahi kutokea duniani!"
Kijana huyo aliyeitwa mume wa Edna hakuwa mwingine bali ni Roma.
Lakini ukiachana na maneno ya Senior, ukienda kule soko la Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam, Roma alijulikana kama mbeba mizigo na msukuma mkokoteni wa kawaida sana; fukara lakini mchapakazi na mwaminifu mno.
Siku hiyo, baada ya kusomba saruji na mizigo ya akina Mama Nasra, Roma aliingiza buku kumi na tano yake halali. Akaenda kupata ugali na nyama ya mbuzi kwa Mama Joshua akisindikizana na rafiki yake Juma.
Roma alikuwa amepanga chumba kimoja kwenye nyumba ya urithi ya Juma. Kwenye nyumba hiyo kulikuwa na mdada mrembo, mwalimu wa chekechea anayeitwa Najma (mdogo wake Juma). Najma alikuwa amezama kwenye lindi la mapenzi mazito kwa Roma, lakini kaka yake, Juma, alikuwa akimzuia akisema Roma ni fukara asiye na malengo.
Mambo yalianza kuharibika usiku ule walipoenda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa mrembo Rose pale Club B, maeneo ya Chalambe. Rose, ambaye alikuwa bosi wa ile Club, alikuwa akimzimia sana Roma. Alimtumia Roma kijimemo cha siri aende chumbani kwake.
Roma alipoingia, alimkuta Rose akiwa nusu uchi, amevaa khanga moja tu baada ya kutoka kuoga. Rose alimbembeleza sana ampe hata nusu saa ya kimapenzi, lakini Roma—kwa kutumia nguvu kubwa ya kiume na kihisia—alijinasua na kumkataa Rose katakata kisha akatoka nje!
Hata hivyo, mwili wa Roma ulikuwa umeshamshika mshawasha mkubwa. Akajiambia, "Hapana, leo siwezi kulala hivi hivi, lazima nitafute kahaba yeyote niende naye ghetto."
Akanyoosha miguu hadi JR Hotel, hoteli iliyosifika kwa kuwa na machangudoa wa bei ghali. Akiwa pale bar, macho yake yakatua kwenye meza moja ambapo alikuwa amelala mwanamke mmoja mrembo aliyekuwa amezika kichwa chake mezani kutokana na ulevi chakari.
Roma akasogea, akaukusanya mkoba wa yule mwanamke, akambeba mzima mzima begani kama gunia la misumari na kuelekea nje.
Kumbe, pale hotelini kulikuwa na wanaume watatu waliokuwa wakimvizia yule mwanamke. Wale jamaa walishtuka, kiongozi wao akasema, "Shit! Huyu fala ni nani anayejiamini hivi? Mfuateni haraka!"
Roma alipakia yule mwanamke kwenye bajaji, na wale jamaa wakaanza kuwafukuzia nyuma kwa gari aina ya Lexus Dualis. Kwa bahati nzuri, dereva wa bajaji alikuwa mwenyeji wa vichochoro vya Chalambe, akakata kona za chocho na kuwapoteza wale watu.
Roma alimfikisha yule mdada ghetto kwake, akavua nguo, na kufanya naye mapenzi mazito kwa zaidi ya dakika sitini huku yule mwanamke akiwa hajitambui kabisa.
Asubuhi ilipofika saa kumi na mbili na nusu, mwanamke yule alishtuka. Alijitazama na kujikuta yuko uchi wa mnyama kwenye chumba asichokijua. Machozi yalimtoka kwa uchungu. Alivaa nguo zake haraka, akachukua nguo yake ya ndani akaingiza kwenye mkoba, na kukimbilia nje ambapo alipanda bodaboda na kutoweka.
Roma alitoka nje akimkimbilia na kumwambia, "Hey sista, umesahau malipo yako!"
Kumbe pale nje, Najma alikuwa akishuhudia kila kitu! Moyo wa Najma uliungua kwa wivu na maumivu, akakimbilia ndani akilia. Juma naye alifurahi sana, akajua sasa dada yake atamchukia Roma.
Juma akasaza umbea kwa wapangaji wote (akina Mama Debora) kuwa Roma ameingiza kahaba ghetto. Hata hivyo, Najma alilia, lakini upande mmoja wa moyo wake ulikuwa bado unampenda Roma.
Siku tatu mbele, Najma alipika wali na mapaja ya kuku akamwekea Roma chumbani kwake. Juma alipogundua, alikasirika sana kuona yeye amewekewa wali wa choroko huku Roma akiwekewa kuku. Kwa hasira, Juma akachukua kufuli kubwa akaenda kufunga mlango wa chumba cha Roma ili akirudi amfukuze kabisa.
Lakini Roma hakuwa amerudi nyumbani kwa siku mbili, kwa sababu gani?
Siku iliyotangulia mchana, akiwa anakula ugali kwa Mama Joshua baada ya kupiga kazi ya saruji, gari kubwa la kifahari aina ya V8 nyeupe lilisimama. Alishuka mwanamke mmoja mrembo aliyevaa suti ya bluu anayeitwa Suzzane.
Suzzane alimfuata Roma na kumwambia kwa sauti ya kujiamini, "Kuna mtu muhimu sana anataka kuonana na wewe."
Roma alimaliza msosi wake taratibu, kisha akaingia kwenye lile gari.
Suzzane alimpeleka Roma hadi kwenye hoteli ya kifahari ya Grand Palace. Wakapanda lifti hadi floor ya 18, chumba namba 708.
Walipoingia ndani, Roma alimkuta mwanamke mmoja aliyevaa suti nyeupe ya gharama akiwa amewapa mgongo akitazama dirishani.
Yule mwanamke aligeuka taratibu na kumtazama Roma usoni. Roma alipouona ule uso, macho yalimtoka, akashtuka na kupiga kelele ya nguvu,
“Kahabaaa…!!!”
Hapo ndipo alipogundua kuwa yule mwanamke bosi mwenye ukwasi mkubwa ndiye yule yule "kahaba" aliyemtoa bikra kule ghetto kwake Bias!
Ukisoma hii simulizi huachi, itakuchekesha, itakutoa machozi, itakupa msisimko na kila aina ya matukio, kwanzia mapenzi, biashara na mengineyo mengi.
Kuisoma nitatute watsapp 0687 151 346
Au unaweza kuisoma sehemu kubwa bure kabisa akupitia jukwaa letu la fasihinet , tembelea: www.fasihinet.com kisha search simulizi ya nilimdhania kahaba kumbe bikra.
Au gusa link hapo chini au kwenye comment
https://fasihinet.com/novels/23/
HII NDIO TAMTHILIA YA ROMA YA NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
Siri za ulimwengu ndani ya simulizi
Singanojr · Dakika 4 za kusoma ·
