WAKUU KWEMA,

Leo ndani ya nusu saa, nimenunua bando la shilingi 500 mara nne, jumla ya shilingi 2,000, lakini kila bando limeisha ndani ya dakika 10 tu

Simu yangu haina programu nyingi. Nimezuia matumizi ya data kwenye background na hata kuzima arifa za programu zote. Kwa matumizi yangu ya kawaida, bando la shilingi 500 hudumu karibu saa 24 kwa kuchat tu WhatsApp na kuchungulia chungulia Facebook na Instagram, huku MB nyingine zikibaki. Hata hivyo, hali niliyokutana nayo jana na leo ni tofauti kabisa na uzoefu wangu wa kawaida.

Kama mmoja wa walio umizwa na ubovu huu najutia matumizi mabaya ya hela, hii hela ninge nunua hata miogo ya buku na pepsi baridi kisha jero ninge tumia tu kwenye internet nikamaliza siku kibabe.

hali hii inanifanya nihoji ufanisi na uwazi wa mifumo ya huduma za intaneti. Inawezekana kukawa na hitilafu ya mtandao au sababu nyingine inayohitaji uchunguzi, uwezekano wa matatizo haya yapo sitashangazwa airtel wakija kudai ni vifaa vyetu ndio tatizo na sio mifumo yao mibovu mibovu lakini wateja wanastahili maelezo ya wazi kuhusu huduma wanazolipia.

Moja ya changamoto za mifumo ya intaneti tuliyoizoea nchini ni ukosefu wa uwazi wa kutosha kuhusu matumizi ya huduma tunazonunua.

Mtumiaji anaweza kununua kifurushi cha data na kukiona kikiisha haraka bila kuwa na njia rahisi ya kuthibitisha ni kiasi gani kimetumika, kimetumika na programu zipi, au kama kuna tofauti kati ya matumizi halisi ya simu na makato yanayooneshwa na mtoa huduma.

Hali hii inazua swali muhimu: Je, tunawezaje kuwa na uhakika kwamba tunapata thamani kamili ya huduma tunazolipia ikiwa hatuna taarifa za kutosha za kuthibitisha matumizi yetu? Bila mifumo imara ya uwazi na ufuatiliaji, mteja anaweza kupata hasara bila kujua chanzo chake. Hatuwezi kupuuza uwezekano wa kuwepo kwa mizengwe unaoweza kuendelea nyuma ya pazia, unaoweza kuwaumiza watumiaji, bila kuwa na njia madhubuti za kugundua na kuthibitisha kinachoendelea.

Ndiyo maana ninaona umuhimu wa kujenga suluhisho la kiteknolojia litakalompa mtumiaji uwezo wa kufuatilia matumizi yake ya intaneti kwa uwazi. Kupitia programu maalumu, mtumiaji ataweza kuona kiasi cha data alichotumia, kutambua programu zinazotumia data nyingi na kuelewa matumizi yake kwa kulinganisha na bajeti yake.

Lengo ni kumwezesha kila mtumiaji kufanya maamuzi sahihi, kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima na kuwa na taarifa zinazomsaidia kulinganisha matumizi yanayooneshwa na simu yake na taarifa za mtoa huduma. Hii ni hatua muhimu kuelekea uwazi, uwajibikaji na ulinzi wa watumiaji wa huduma za kidijitali.

Maono yangu

kila solution linakuja kutokana na tatizo

Nina maono ya kujenga mfumo wa kisasa wa huduma za intaneti unaotumia teknolojia za kidijitali na miundombinu ya mawasiliano ya kizazi kipya, kwa lengo la kupanua upatikanaji wa intaneti ya kasi na gharama nafuu nchini Tanzania.

Maono yangu ni kuona baadhi ya Watanzania wenye kipato cha chini wakipata huduma za intaneti bure, huku wengine wakipata huduma hizo kwa gharama nafuu. Ninaamini teknolojia inapaswa kuwawezesha wananchi, si kuwa kikwazo kwa maendeleo yao.

Tanzania inahitaji suluhisho bunifu, miundombinu ya kisasa na mifumo inayowapa watumiaji udhibiti na uwazi zaidi inayo endana na dira yake ifikapo 2050, Hatupaswi kuishia kulalamikia changamoto; tunapaswa pia kujenga teknolojia zinazoweza kuzitatua.

Jiandae! Nina maono ya kuleta suluhisho jipya la huduma za intaneti nchini Tanzania, lenye lengo la kutoa muunganisho wa kasi, gharama nafuu na uwazi zaidi kupitia teknolojia za kizazi kipya ukiachana na hizi za miaka ya 90 huko zilizopo.

Intaneti bora ni haki ya kila Mtanzania.

Mdau, je, umewahi kukutana na tatizo kama hili ?