Peter Gerald Scully ni raia wa Australia, akitokea jijini Melbourne. Alipokuwa mtu mzima, alianza 'kujitafuta' ili naye 'atoke' kimaisha. Akagusa hiki kikafeli, akagusa kile kikafeli.

Siku moja, akapata wazo, japo la kitapeli. Akalitazama lile wazo, akaona linaweza kumpatia pesa nyingi, japo kwa njia za kitapeli. Akainama, akacheka, akasema: "Sina jinsi. Nataka pesa. Nitaanzisha kampuni. Nitaiita The Key Result. Itakuwa ni uwekezaji wa masuala ya nyumba."

Kijana akaanzisha kampuni. Kwa muda mfupi, akakusanya pesa za watu. Mwaka 2011 'arobaini' zake zikafika. Alikuwa ameshatapeli karibia dola za ki-Marekani milioni mbili, hapo sio chini ya shilingi bilioni tano za ki-Tanzania.

Ile tu anataka aanze kula maisha, 'manjagu' wa Australia wakamweka kwenye 'rada' zao! Wakasema kijana usitutanie. Vumbi likatimka. Kijana Peter akatoroka nchi. Huku nyuma akaacha kesi yenye makosa 117 ya utapeli! Mh! Makosa 117 wangemwua aisee!

Watu wakawa wamelizwa pesa zao namna hiyo. Wakabaki wanalia.

Shida ikaja kwamba, sio polisi wala nani aliyejua Peter ameenda wapi. Peter alikuwa ametoroka kwa umakini sana.

Kwa siri sana, Peter alikuwa ameenda hadi nchini Ufilipino. Akatafuta maeneo ya ndani-ndani kabisa aweze kujificha kisawasawa. Akaenda kusini mwa Ufilipino, akajichimbia maeneo ambapo watu masikini sana wanaishi. Akawa anaishi mkoa uitwao Mindanao, na pia akawa akiishi kwa siri miji ya Cagayan de Oro, Surigao, na Malaybalay.

Mpaka hapa, pengine Peter angesema hivi: "Nimeiba pesa za watu, na nimefanikiwa kutoroka. Ngoja nitafute mashamba huku nianze kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa. Niliowatoa machozi wanatosha. Acha nisiongeze laana."

Lakini Peter hakuwaza hivyo. Nyerere alisema ukila nyama za watu utaendelea kuzila tu. Kuna saa utazi-miss, maana kwako ni nyama tamu. Shetani na malaika wake Petiro Scully.

Badala Peter aachane na uovu, akaishia kusema: "Bado ninataka pesa nyingi. Tena kwa njia yoyote. Kama ni kuua watu nitaua hata dunia nzima! Nachotaka ni pesa nyingi!"

Peter alikuwa na roho ya aina yake. Akapata wazo lingine, wazo ovu mno. Muda mfupi ujao, alikuwa tayari kuiliza dunia nzima. Na wala hajali. Na kweli, Peter amejua kutuumiza. Peter ni moja ya watu wenye akili nyingi, lakini ni mtu mpumbavu kuwahi kukanyaga hii dunia! Furaha yake ni pale mtalia wote. Na mkilia sana ndio mnazidi kumchekesha. Wazo la Peter lilikuwa ovu mpaka shetani akaita karamu kuzimu. Najuta hadi kwa nini akaitwa Peter.

Alifanya hivi: alichukua mihela yake ya wizi. Akajenga studio nzuri, safi kabisa, akaiwekea teknolojia za hali ya juu za mitandao. Peter ana akili na ujuzi mwingi. Tofauti ni kwamba ni kwamba ana njaa ya kikatili kupindukia. Yupo tayari kuchinja na kuuza moyo na figo hata kama ni za mtoto wake mwenyewe!

Ili uelewe wazo la Peter, ngoja nikupe elimu kidogo, japo sio ngeni sana kwako.

Najua unajua intaneti. Ni kama hii hapa unasoma whatsapp, facebook, google, instagram, youtube, na kwingineko kwa kutumia simu au kompyuta yako.

Lakini, kuna ile intaneti ambayo 'ipo chini' yake, ambayo hujawahi kuiingia. Inaitwa Deep Web. Lakini tena sikia vizuri: ndani ya Deep Web kuna ule Mtandao Giza unaoitwa Dark Web. Huku ndio kwenyewe sasa!

Najua wengi mnajua hii Dark Web, angalao kwa kusikia tu. Huko, huingii tu kama tu unavyofanya, kuwasha data na kuanza kuperuzi mtandaoni. Pamoja na kwamba ndani ya Dark Web kuna vitu vizuri ambavyo inalazimu vipatikane huko tu, lakini unapotaja Dark Web unataja mahali ambapo shughuli chafu duniani hufanyika.

Hapa unazungumzia vitu kama biashara haramu za kuuza watu, biashara za uuzaji haramu wa silaha, miamala haramu ya fedha, makampuni ya kitapeli, ufisadi wa malundo makubwa ya fedha na mambo kama hayo.

Huku ndani ya Dark Web (Mtandao Giza) kuna data nyingi kuzidi haya ambayo yanapatikana kwenye hii intaneti ya kawaida tunayoingia kila siku!

Ndani ya Dark Web ni sehemu salama kwa magendo yote unayojua duniani. Ni mtandao ambao umesukwa kwa namna ambayo mtu anapoingia anaweza kuweka 'layer' za kificho kwa namna ambayo kamwe hawezi kujulikana ni nani.

Utaishia kuona uozo na uozo lakini hakuna jinsi ya kung'amua wahusika.

Kwa sababu ya mambo maovu kupindukia yanayofanyika ndani ya Dark Web, wewe kuingia na kuyatazama tu tayari huwa ni makosa ya kukupandisha kizimbani.

Ndio maana watu hawaingii kabisa kupitia simu, hata kama namna hiyo ipo. Ni hatari kabisa mtu kufanya hivyo. Hata watu wanapoingia kupitia kompyuta, kunahitajika umakini na uzingatiaji wa masharti magumu kabisa.

Kama nilivyosema, ndani ya Dark Web, kuna mambo ambayo kuyatazama tu ni makosa makubwa mno kutokana na 'content' yenyewe ilivyo.

Ninakupa mfano: ndani ya Dark Web kuna websites ambazo huonesha video za kutisha na kusikitisha, ambazo hupendwa na wale watu wanaoitwa 'sadists'. Hawa ni watu wanaopenda kufurahia kuona mateso.

Watu hawa huingia na kuanza kuchagua aangalie nini. Mfano, mhusika anaweza kuingia na kutaka aangalie video za mtu akiteswa kwa kuchomwa moto, au akikatwa kiungo kimoja baada ya kingine hadi anapokufa. Duniani kuna mambo ya ajabu mno! Sadists wanapenda wanapoona mtu huyo anavyoteseka na wanaburudika wanaposikia sauti za vilio vyake!

Kumbuka, hizi sio video za kutengeneza. Wako watu duniani wanaofanya kazi hiyo ya kurekodi video za mateso na wapo salama mradi ni ndani ya Dark Web.

Sadists wanapotazama kuna wanazolipia na kuna wanazotazama bure.

Kutazama video za namna hii ni makosa makubwa. Ni kuendelea 'ku-injinia' waandaaji wa mambo kama hayo. Ni kosa lenye adhabu kali kabisa. Kwa hiyo, usiwahi hata siku moja kutamani kutembelea Dark Web.

Katika kundi la websites za video za kutisha, kuna kundi la websites hizi ambazo huitwa 'Hurtcore.' Hili ndilo kundi baya kuliko makundi yote ya websites za video za kutisha na kuhuzunisha za Dark Web.

Hurtcore ni website za uovu uliopindukia kabisa. Hizi hurtcore, zinahusisha utengenezaji wa video za watoto wakifanyiwa ukatili uliokubuhu. Zinaitwa Child Sexual Abuse Material (CSAM).

Watoto wadogo wakiingiliwa kimwili, wakipigwa vipigo vya kikatili, wakiwa wamefungwa minyororo, na huku wakiwa wanapewa mateso yenye kuleta maumivu makali ya muda mrefu!

Sasa, Huyu bwana Peter akawaza afanye 'biashara' ya hurtcore. Ndio maana nilikuambia alifungua studio ya kisasa kabisa. Sasa, yeye aliamua ataifanya hii kama biashara ya daraja la kwanza kwa watazamaji 'Premium'. Nikisema Premium maana yake ataandaa video za mateso makali mno na kuziuza kwa bei ghali huko Dark Web. Pia, atakuwa akipokea 'oda' kutoka kwa watazamaji wake wakitaka video za mateso wanayotaka.

Fikiri video ukatili wa watoto zinavyoumiza! Wote hapa ni mashahidi pale video za namna hiyo zinapovujia mitandaoni.

Sasa, huyu Peter akaamua atakuwa akiandaa video za Hurtcore, zikionesha mateso kwa watoto wadogo! Sasa, kisheria hairuhusiwi kuandika maelezo ya mateso yanayohusu video fulani. Mfano useme, katika video fulani yenye jina fulani, mtoto anaingiziwa kisu sehemu zake za siri. Hilo ni kosa kisheria kwa kuwa unautweza utu wa huyu mtoto husika unayemzungumzia.

Peter aliamua kuwa atakuwa anafanya mateso ya kuwaingilia kimwili watoto wadogo kabisa, wa kike na wa kiume, huku akiwapa mateso mengine makali na kuwapiga vipigo vinavyoweza hata kusababisha kifo.

Kumbuka, hapa alikuwa akiishi kimaficho katika jamii ya watu masikini mno. Peter akajitafutia watu wa kushirikiana naye kwenye unyama wake. Kazi ya kwanza ikawa ni namna ya kupata watoto.

Hiyo haikuwa shida kwake. Kwa kuwa anaishi eneo masikini, kuwapata watoto ilikuwa kazi rahisi maana wazazi walikuwa wanakubali kuwatoa tu kwa ahadi za kwamba wanaenda kusomeshwa na kupewa mahitaji yote.

Watoto wengine walikuwa wakirubuniwa tu mtaani kwa kupewa pipi na biskuti. Peter sasa akawa ana studio safi kabisa, vifaa vya kisasa vya kurekodia, na mitambo yake ya kupost Dark Web.

Huko Dark Web akatumia akili zake kutengeneza website yake ambayo aliiwekea ulinzi "encryption" ipasavyo, kisha akaipa jina la No Limits Fun. Kutokea hapo akaanza 'kazi' zake rasmi.

Wale watoto aliowateka, akawa anawaficha huko ndani kwenye 'jela' yake. Akaanza rasmi kuwarekodi huku akiwapa mateso ya kuogofya!

Na kweli, akaanza kupata wafuasi. Kuanzia mwaka 2012, akaanza kujulikana huko Dark Web.

Fikiria, aliifanya hii 'biashara' kwa makali mpaka akaanza kupata oda! Sijui kama umeelewa. Mfano, mteja anamwambia: "Tengeneza video ya mtoto ukiwa unamnyonga kwa mikono kidogo-kidogo hadi afe! Hakikisha, wakati unamnyonga, awe amesimama juu ya makaa ya moto!"

Yaani, wateja wake wanamwambia aandae video za mateso ambayo wao ndio wanachagua! Ukisikia watu sadists ndio hawa sasa! Wana roho ya shetani kisawasawa! Yaani, wanafurahia kabisa wanachofanyiwa watoto hao, tena wanatoa oda ya video zingine za mateso sawasawa na matakwa ya oda zao.

Peter anawajibu yuko tayari, mradi wajiandae kulipia. Peter alivyokuwa ameweka mfumo wake wa malipo, utachoka! Ilikuwa mtu akitaka kulipa, alitakiwa kutumia sarafu mtandao (crypto currencies) kama Bitcoin. Utamkamataje Peter Scully kama analipwa kupitia sarafu mtandao?

Unaona sura yake wazi wazi kwenye video, lakini utampata wapi? Kama anatumia Dark Web, utampataje?

Peter akaanza kuingiza pesa nyingi kutoka nchi za bara la Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini. Peter akatamalaki. Anaonekana, anajulikana, lakini yuko wapi? Yupo Marekani? Yupo Afrika? Yupo Ulaya? Yupo wapi? Watu waanzie wapi kumtafuta? Ikawa ni kitendawili.

Akaendelea na kazi hiyo hadi ilipofika 2014 alipofanya jambo la kutisha kuliko yote. Alipost video ya dakika kama 50, dunia nzima ikatoa machozi. Kila kitu kilisimama.

Video hiyo ni maarufu kwa jina la "Daisy's Destruction" Kwenye video ile kuna hadi mtoto wa kike wa mwaka mmoja na nusu akisulibiwa vilivyo na baba Peter! Kwenye video hiyo, walikuwa watoto watatu: 'Daisy,' 'Liza' na 'Cindy.'

Kama nilivyosema, hairuhusiwi kusema ni mateso gani haswa ambayo watoto wale walikuwa wakifanyiwa. Ni makosa kabisa.