

Masaa mawili ya kumbukumbu
Kifantasia
Ujasusi
Komedi
Uchawi
Kisasa
Biashara
Kutisha
Kijeshi
484
Views
2
Rates
3
Chapters
Utangulizi
Kijana Masumbuko ambae anaonekana kuwa na uwezo usiowa kawaida , uwezo wa kumfanya mtu kufanya … Zaidi
Pia unaweza kupenda

Shetani rudisha akili zetu
Saa saba mchana Frida alionekana akiingiza gari ndani ya hospitali na taasisi ya kitafiti ya Neuroscience inayopatikana Kibaha , kilomita kadhaa kutoka ilipo hospitali ya Tumbi.
Ilikuwa ni hospitali kubwa mno na ya kisasa yenye jengo moja lililoenda hewani kwa ghorofa kumi kumi na nane hivi na kufanya kuwa jengo refu zaidi ndani ya mkoa wote wa Pwani.
Hospitali hio ilijengwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia shirika la taasisi isiokuwa ya kiserikali ifahamikayo kama Haliz Neuroscience Foundation(HNF).
Taasisi ya Haliz ilisifika dunia nzima kwa kujikita zaidi katika kuutafiti ubongo na maswala ya neva kwa ujumla wake, sera ya taasisi hio ilikuwa ni kuwezesha mataifa mengi kujifunza namna mfumo wa ubongo na neva unavyofanya kazi na hii imechangia sana kufungua matawi yake mengi karibia nchi nyingi duniani.
Mashirika ya Afya ya umoja wa kimataifa yalikuwa yakiunga mkono kazi kubwa ambayo ilikuwa ikifanywa na taasisi hii kubwa ya kimarekanni isiokuwa ya faida(Non-profit organisation).
Katika miaka ya hivi karibuni maendeleo ya sayansi ya neva na ubongo yalikuwa yamepiga hatua kubwa sana , wale wagonjwa ambao walikuwa wamepoteza kumbukumbu ilikuwa rahisi kurejeshewa kumbukummbu zao ndani ya muda mfupi tu chini ya taasisi hii ya Haliz.
Haikuwa wagonjwa waliopoteza kumbukummbu tu , watu wengi ambao walionekana kusahau mambo muhimu katika maisha yao , iwe ni kubukumbu za utotini au za ukubwani taasisi ya Haliz ilikuwa na teknolojia ya tiba ya kurahisisha hayo yote.
Licha ya taasisi hio kufanikiwa lakini bado utafiti wa kuujua ubongo wa binadamu ulikuwa ukiendelea zaidi , kwani wanasayansi wanaamini ubongo uwezo wake ni mkubwa kuliko ile ambavyo inadhaniwa , hivyo wanaamini kuuwezesha ubongo kufikia uwezo wake kamili kimatumizi italeta maendeleo makubwa.
Frida alitembea kwa kujiamini kabisa ndani ya hospitali hio huku akipokelewa na harufu ya taasisi hio yenye kuzoeleka katika pua zake, kwa namna baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hio walivyokuwa wakimsalimia kwa kutingisha vichwa ilionekana alikuwa ni mfanyakazi mwenye cheo.
Aliishia kutoa tabasamu huku akitingisha kichwa kwa kuonyesha tabasamu kwa baadhi ya watu aliopishana nao ndani na ndani ya dakika kadhaa aliweza kuzifikia lift na kuingia ndani, lakini kabla hata ya mlango wa lift haujajifunga mwanaume mzungu wa makamo alievalia koti la kimaabara aliweza kuzuia lift hio na kuingia ndani.
Alikuwa ni mtanashati kweli aliependezeshwa na miwani ya macho , huku akiwa amepambwa na tabasamu.
“Well!. Fancy meeting you here, Frida”Aliongea yule mzungu na kumfanya Frida kutoa tabasamu.
“Una ajenda gani kukimbilia lift Blake, huu si muda wako wa kufanya Demostrations na wanafunzi?”Aliuliza Frida na kumfana Blake kutoa kicheko kama anakohoa.
“Ndio nimemaliza, kulikuwa na mabadilishano na Dr John , Vipi wewe ndio umekuja kutubariki na utaalamu wako?,nilidhani upo likizo?”
“Nipo likizo ndio , lakini haimaanishi sipaswi kufika hapa , nina biashara katika floor ya kumi na saba”
“Wow!, Wow! , Floor ya wabobevu, sina neno la kuongezea, See you Frida”Aliongea Dr Blake na ni muda uleule Lift ilisimama katika floor ya kumi na bwana huyo mzungu alitoka akimuacha Frida kuendelea na safari yake.
Frida aliishia kutoa tabasamu tu huku akiangalia namna ambavyo Blake anapotelea kwenye macho yake wakati lift ikijifunga.
Haikuwa kama ambavyo amesema Frida kwani mara baada ya lift kufika katika foor ya kumi na saba alitoka katika lift na kuingia katika floor hio ambayo ilikuwa na utulivu wa hali ya juu , ilikuwa ni ubaridi tu na harufu ya kuvutia , huku rangi ya taa zisizokuwa na mwanga mkali zikipendezesha eneo hilo.
Frida hakuingia ndani ya Foor hio bali alizunguka upande wa kushoto kwake na kuanza kupandisha ngazi kuelekea juu na ndani ya dakika chache tu aliweza kutokezea juu kabisa ya jengo hilo.
Licha ya kwamba alionekana kutembea kwa haraka, lakini kwa namna ambavyo alikuwa na spidi hakuonyesha hata kuchoka, alionekana kama aina ya wanawake ambao walikuwa na mazoezi makali.
Baada ya kutoka katika paa kabisa ya jengo hilo refu na kumfanya kuona mazingira ya mji wa Kibaha na baadhi ya maeneo ya Dar es salaam na Bagamoyo alivuta pumzi na kisha aliendelea kupiga hatua kusogea mbele.
Hali ya hewa haikuwa ya jua kali ,ilikuwa ni kama vile mvua ingenyesha muda wowote.
Mbele yake Frida alikuwa amesimama mwanaume alievalia suti ya rangi ya bluu akiangalia upande wa maeneo ya Dar es salaam kwa umakini mkubwa kana kwamba kuna kitu alichokuwa akitafuta.
Alikuwa ni mzungu kwa muonekao wa nywele tu na kadri Frida ambavyo alikuwa akitembea hatua zake zilionyesha hali ya kuwa dhaifu kiasi.
Kama ilivyo mwanaume yule alivyosimama ndio namna ambavyo Frida alienda kusimama katika ukingo wa jengo hilo na kuendela kuangalia upande wa mbele yake, ilikuwa ni kama vile anamwigizia yule mtu , na upande wa yule mtu hakugeuka kabisa ni kama alijua nani amefika hapo na kusimama pembeni yake.
“Any progress on KF-Target?”Aliongea yule mzungu kwa sauti nzito.
“We are almost there, I’ve initiated a plan to bring him closer to me, his curiosity will ensure our swift entry into the next phase”Aliongea akimaanisha kwamba anakaribia kumaliza , na ameanzisha mpango wa kumuweka karibu , anasema shauku yake itawafanya waingie hatua inayofuata kwa haraka”
“Elezea”Aliongea.
“Nimemfanya anifanyie Delivery ya Viungo vya akili kutoka Binamu , uhakika ni kwamba atauliza maswali juu ya malipo makubwa yanayolipwa kwa ajili ya chungu kimoja kama njia ya usafirishaji, kwa kile nilichoona amevutiwa”
“A risky move”
“Calculated Risky Sir”Aliongea Frida kwa kingereza na jibu lake lilimridhisha.
“Vipi kuhusu wale wengine , namaanisha wanaoangalia kutoka mafichoni?”
“We are keeping eye on them , once we have what we need, they ‘ll be nothing more than loose ends”
“Endelea na kazi kwa umakini , hatuwezi kuruhusu kosa lolote”
“Umeeleweka”
“Sinagogi wanataka hii misheni kumalizika kwa haraka , siku zijazo utashughulikia na zaidi ya mtu mmoja katika tafiti yako , mategemeo makubwa yamewekwa juu ya hii sayansi mpya Frida ,natumaini kila kitu kitaenda sawa,Hatuwezi kuruhusu washindani wetu kupiga hatua kabla yetu”
“Ili mradi malengo yanakuwa wazi , kila kitu kitaenda sawa , natumaini utakuwa vizuri kwenye kuwatoa wasiwasi”
“Kama ni hivyo tutaonana tena katika hatua inayofuata kujua maendeleo”Aliongea yule mwanaume na ilitokea kitu kama upepo tu kwani alipotea palepale na wala hali ile isimuogofye Frida ikionyesha ni jambo ambalo amezoea.

Damiani
Damiani mhitimu wa chuo kikuu cha uhasibu , anahitimu masomo yake na kurudi kijijini kwao kwa ajili ya kusubiria upepo wa ajira lakini katika hali ya kutokutegemea mama yake kipenzi anapigwa risasi mbili za kifuani na kufa hapo hapo na hio inatokana na kumpatia msaada mwanaume ambae hamfahamu mwenye asili ya ulaya (mzungu ) ambae na yeye alikuwa kwenye hatua ya mwisho ya kupoteza uhai wake kwani alikuwa na jeraha la risasi tumboni ,lakini mzungu huyo kabla ya kupoteza maisha anamkabidhi damiani nyaraka bila kumpa maelekezo ya aina yoyote ile .
Damiani anajikuta anajenga chuki na kisasi kwa watu waliohusika na mauaji ya mama yake , anajiapiza kuwatafuta mahali popote pale na kulipiza kisasi , katika harakati za kuwatafuta wabaya wake anajikuta akifahamu siri nzito iliokuwa nyuma ya kifo cha ghafla cha raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , anapata waraka ulioachwa na raisi huyo uliopewa jina la KAULI YA MWISHO YA RAIS KABLA YA KIFO CHAKE .
JE UNAFIKIRI ATAFANIKIWA KULIPIZA KISASI CHAKE ?
JE NI KAULI GANI YA MWISHO ALIO ACHA MHESHIMIWA RAISII KABLA YA KIFO CHAKE ?.
simulizi hii imekamilika , mwandishi ataiweka hapa hivi punde
.

Niliemdhania kahaba kumbe bikra
Roma mbeba mizigo ndani ya soko la Mbagala Rangi Tatu anamdhania Edna Kama mwanamke anaejiuza ,baada ya mwanadada huyu kuwekewa dawa ya usingizi kwenye kinywaji na maadui zake katika ulimwengu wa Biashara akiwa ndani ya hoteli na Roma anambeba Edna na kumpeleka Geto kwake na afanya nae mapenzi.
Edna kwa Mara ya kwanza analala na Roma pasipokujitambua na kupoteza usichana wake ,baada ya tukio Hilo anaamua kuolewa na Roma kwa mkataba wa Miezi sita ili kuepuka kuolewa na mwanaume asiempenda ,baada ya Roma kufunga ndoa na Edna anakuja kugundua kuwa mke wake anamiliki kampuni kubwa Nchini huku akiwa na utajiri wa kutisha.
Edna anamuona Roma kama mtu asiyekuwa seriasi na maisha kutokana na aina ya mfumo wa maisha yake ,maisha ya kuwa na wanawake wengi swala linalomkasirisha Edna.
Edna anajitahidi kuweka ukaribu na Roma ili kujua sababu ya mume wake macho yake kubadilika Rangi anapokuwa na hasira na kuwa ya kijani huku akiwa na roho ya ukatili mno
Idara na mamlaka za kiusalama Nchini zinashangazwa na uwezo wa Roma wa kuzungumza Lugha zaidi ya ishirini na mbili na wanaanza kutafuta taarifa zinazomuhusu Roma lakini licha ya kupata taarifa inayoonyesha Roma kusomea ndani ya chuo kikubwa Duniani Cha Harvard wanakosa taarifa zingine zinazomuhusu Roma na kuishia kujiuliza Roma ni Nani haswa

Gereza la Hazwa
Mvua ilimwagika kwa nguvu, upepo mkali ukiparaganya miti na radi zikilipuka mithili ya mapigo ya ngoma ya kuzimu. Huu si msitu wa kawaida—ni Elnino, kichaka kinachomeza roho za wasiotarajia, hata mchana ukiwa na giza lisilo na mwisho.
Lakini usiku huu, kivuli kilikuwa kinakimbia kwa kasi ya kutisha, miguu yake ikizama kwenye tope zito. Uso wake ulikuwa umefunikwa na nywele chafu na ndevu ndefu, macho yake yakiangaza hofu isiyoelezeka. Alikuwa akitoroka—lakini kutoka kwa nani?
Nyuma yake, wanaume sita walimsakama. Wanne wamevaa mavazi ya kininja, wakipotea na kurejea kwenye giza kama manyoya yanayorushwa na upepo, huku wawili wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi. Hakukuwa na huruma katika macho yao, ni mauti tu.
Kisu kikubwa kiliruka kwa kasi kuelekea shingo yake, kikapita kwa milimita chache tu. Punde hakuonekana tena. Mmoja wa wawinda wake alisimama, akisikiliza kwa makini—lakini upepo ulisambaza sauti kila upande, ukivuruga hisia zake. Waliashiriana kimyakimya: “Muaue.”
Lakini ghafla… tone la jasho likamdondokea mmoja wao. Akakoki bastola, akaiinua juu, akifyatua bila kusita. Hakuna kilichompata mtu huyo wa kutisha, aliyejirusha kutoka juu ya mti kwa kasi isiyoelezeka. Mikono yao ilikutana kwa sekunde chache, mapambano ya mwili kwa mwili yakaanza juu ya mti. Risasi sita zilifyatuka—hakuna hata moja iliyompata.
Mlio wa mifupa ukasikika. Shingo ya askari mmoja ilikatika kwa sekunde chache tu. Mwili wake ukaanguka huku damu ikimwagika kwa kasi. Mwanaume huyo mchafu hakuwa na muda wa kusherehekea ushindi. Kisu kikubwa kilikuwa kimetua mgongoni mwake, kikamdhoofisha—lakini hakuwa tayari kufa.
Mbele yake kulikuwa na maporomoko makubwa yasiyo na mwisho. Nyuma yake, waninja wanne na askari mmoja wamesimama, wakitazama kwa macho baridi. Hakuhangaika kugeuka… alijirusha kwenye giza la maporomoko.
"He is not human, he’s completely a devil."
"But no survive, he is no more there."
"Let's go and take Donald’s body."
wakiamini kuwa msako wao umeisha. Lakini walikosea…
Mwanaume huyu alikuwa mfungwa wa miaka 10 katika gereza ambalo hakuna aliyewahi kutoroka kwa miaka 200. Gereza ambalo hakuna mfungwa anayejua lilipo. Lakini leo, mtu mmoja yuko nje.
Nani huyu? Ni kwa nini wanamtaka afe? Na je, kweli ameangamia kwenye maporomoko hayo...?