
Masaa mawili ya kumbukumbu
Kijana Masumbuko ambae anaonekana kuwa na uwezo usiowa kawaida , uwezo wa kumfanya mtu kufanya kile anachokitaka yeye kwa kumkonyeza machoni huku akishidnwa kujua uwezo wake unatokana na nini , anaianza safari kutokea mkoani Tanga kuelekea mkoani Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta maisha kama ilivyo kwa vijana wengi ambao wanaamini kuishi ndani ya jiji la Dar es salaam ndio njia rahisi ya kutoboa kimaisha.
Kama ilivyokuwa jina lake hakuwa na maisha mazuri wala pesa yoyote mfukoni ya kumuwezesha kufika jijini Dar es salaam, kitu pekee ambacho alikuwa nacho na kujiamini anaweza kukamilisha safari yake hio ni uwezo wake wa kumpumbaza mtu kwa kumwangalia usoni kwa kile ambacho yeye anakiita kwamba ni masaa mawili ya kumbukumbu zake.
Hatimae kwa uwezo wake huo wa ajabu anafanikiwa kula na kushiba na kupanda basi ambalo linamfikisha jijini Dar es salaam burea kabisa.
Ndani ya jiji la Dar es salaam anakutana na Peter kijana msomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam , kutokana na namna ambavyo wamekutana wanajikuta wanakuwa marafiki wa kubwa na Peter anamxchkua Masumbuko na kwenda kuishi nae.
Peter ni mtoto wa Irene mwanadada ambae kazi yake ni uchangunduo kazi ya kuuza mwili wake kwa kufanya mapenzi na wanaume tofauti tofauti na kujipatia hela.
Irene miaka mingi nyuma akiwa katika harakati za kazi hio , anajikuta anapata mteja tajiri afahamikae kwa jina la Samir, katika hali ya kushangaza tofauti na siku zote ambazo amefanya kazi Samiri anampatia Mimba Irene.
Irene anagoma kutoa ujauzito kwa hofu ya kukosa kizazi baadae , hivyo anafanya maamuzi magumu na kulea ujauzito huo na licha ya kujua Samniri hawezi kukubali ujauzito wake anachukua maamuzi ya kijasiri na kwenda kumwambia kama amepata ujauzito wake na hawezi kuutoa kwasababu yta kuogopa kukosa mtoto baadae.
Samiri anamfukuza Irene nyumbani kwake na kumwambia hatambui ujauzito huo , lakini licha ya hivyo mke wake Samiri afahamikae kwa jina la Shani anagundua juu ya swala la Irene kubeba ujauzito wa Samiri na jambo hilo linamchukiza sana na kuogopa kwa kudhania kwamba licha ya Samiri kukataa ujauzito huo mbeleni anaweza akamtafuta mtoto wa Irene na kumrisha mali za familia.
Kutokana na hilo anaandaa mpango na kukodi mtu wa kumfatilia Irene kila siku na kumpa taarifa zake , miaka kadhaa mbele Peter anazaliwa na anafafikisha umri wa miaka saba na Shani anamtengenezea Irene ajali na anapoteza maisha.
Peter anampoteza mama yake bila ya kujua wazazi wake na maisha yanaanza upya anafauafuru vizuri kwenda kidatoi cha kwanza ana anapata ufadhili kwa kampuni ya misaada ya F and R foundation , kampuni ambayo inaongozwa na baba yake Samiri na Peter anafanikiwa kutetea ndoto zake kama ilivyo kwa watoto wengi wenye uwezo na anafdika chuo.
Siku moja akitoka kufana ununuzi wa simu katika mall za Mlimani City anajikuta kushangazwa na urembo wa binti mmoja ambae alikuwa akiingia katika maduka hayo kwa jili ya kufanya ununuzi, kitendo cha kushangaa anajikuta simu yake inakwapuiliwa na vibaka na kutokana na tukio hilo linamkiutanisha na Masumbuko ambae anamwahidi Peter anao uwezo wa kwenda kumrudishia simu yake kama tu atamslipa kiasi cha hela.
Peter anashangazwa na masumbuko lakini mwisho wa siku anakubaliana na Masumbuko kwseli anafaikiwa kumrudishia Peter simu yake