

JUMBA JEUSI
Ujasusi
82
Views
0
Rates
22
Chapters
Utangulizi
JUMBA JEUSI...... SIASA NI KAMARI....Je NANI HUIBUKA MSHINDI? JUMBA JEUSI ni andiko ambalo linaangazia siasa ⌠Zaidi
Pia unaweza kupenda

Masaa mawili ya kumbukumbu
Kijana Masumbuko ambae anaonekana kuwa na uwezo usiowa kawaida , uwezo wa kumfanya mtu kufanya kile anachokitaka yeye kwa kumkonyeza machoni huku akishidnwa kujua uwezo wake unatokana na nini , anaianza safari kutokea mkoani Tanga kuelekea mkoani Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta maisha kama ilivyo kwa vijana wengi ambao wanaamini kuishi ndani ya jiji la Dar es salaam ndio njia rahisi ya kutoboa kimaisha.
Kama ilivyokuwa jina lake hakuwa na maisha mazuri wala pesa yoyote mfukoni ya kumuwezesha kufika jijini Dar es salaam, kitu pekee ambacho alikuwa nacho na kujiamini anaweza kukamilisha safari yake hio ni uwezo wake wa kumpumbaza mtu kwa kumwangalia usoni kwa kile ambacho yeye anakiita kwamba ni masaa mawili ya kumbukumbu zake.
Hatimae kwa uwezo wake huo wa ajabu anafanikiwa kula na kushiba na kupanda basi ambalo linamfikisha jijini Dar es salaam burea kabisa.
Ndani ya jiji la Dar es salaam anakutana na Peter kijana msomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam , kutokana na namna ambavyo wamekutana wanajikuta wanakuwa marafiki wa kubwa na Peter anamxchkua Masumbuko na kwenda kuishi nae.
Peter ni mtoto wa Irene mwanadada ambae kazi yake ni uchangunduo kazi ya kuuza mwili wake kwa kufanya mapenzi na wanaume tofauti tofauti na kujipatia hela.
Irene miaka mingi nyuma akiwa katika harakati za kazi hio , anajikuta anapata mteja tajiri afahamikae kwa jina la Samir, katika hali ya kushangaza tofauti na siku zote ambazo amefanya kazi Samiri anampatia Mimba Irene.
Irene anagoma kutoa ujauzito kwa hofu ya kukosa kizazi baadae , hivyo anafanya maamuzi magumu na kulea ujauzito huo na licha ya kujua Samniri hawezi kukubali ujauzito wake anachukua maamuzi ya kijasiri na kwenda kumwambia kama amepata ujauzito wake na hawezi kuutoa kwasababu yta kuogopa kukosa mtoto baadae.
Samiri anamfukuza Irene nyumbani kwake na kumwambia hatambui ujauzito huo , lakini licha ya hivyo mke wake Samiri afahamikae kwa jina la Shani anagundua juu ya swala la Irene kubeba ujauzito wa Samiri na jambo hilo linamchukiza sana na kuogopa kwa kudhania kwamba licha ya Samiri kukataa ujauzito huo mbeleni anaweza akamtafuta mtoto wa Irene na kumrisha mali za familia.
Kutokana na hilo anaandaa mpango na kukodi mtu wa kumfatilia Irene kila siku na kumpa taarifa zake , miaka kadhaa mbele Peter anazaliwa na anafafikisha umri wa miaka saba na Shani anamtengenezea Irene ajali na anapoteza maisha.
Peter anampoteza mama yake bila ya kujua wazazi wake na maisha yanaanza upya anafauafuru vizuri kwenda kidatoi cha kwanza ana anapata ufadhili kwa kampuni ya misaada ya F and R foundation , kampuni ambayo inaongozwa na baba yake Samiri na Peter anafanikiwa kutetea ndoto zake kama ilivyo kwa watoto wengi wenye uwezo na anafdika chuo.
Siku moja akitoka kufana ununuzi wa simu katika mall za Mlimani City anajikuta kushangazwa na urembo wa binti mmoja ambae alikuwa akiingia katika maduka hayo kwa jili ya kufanya ununuzi, kitendo cha kushangaa anajikuta simu yake inakwapuiliwa na vibaka na kutokana na tukio hilo linamkiutanisha na Masumbuko ambae anamwahidi Peter anao uwezo wa kwenda kumrudishia simu yake kama tu atamslipa kiasi cha hela.
Peter anashangazwa na masumbuko lakini mwisho wa siku anakubaliana na Masumbuko kwseli anafaikiwa kumrudishia Peter simu yake

Shetani rudisha akili zetu
Saa saba mchana Frida alionekana akiingiza gari ndani ya hospitali na taasisi ya kitafiti ya Neuroscience inayopatikana Kibaha , kilomita kadhaa kutoka ilipo hospitali ya Tumbi.
Ilikuwa ni hospitali kubwa mno na ya kisasa yenye jengo moja lililoenda hewani kwa ghorofa kumi kumi na nane hivi na kufanya kuwa jengo refu zaidi ndani ya mkoa wote wa Pwani.
Hospitali hio ilijengwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia shirika la taasisi isiokuwa ya kiserikali ifahamikayo kama Haliz Neuroscience Foundation(HNF).
Taasisi ya Haliz ilisifika dunia nzima kwa kujikita zaidi katika kuutafiti ubongo na maswala ya neva kwa ujumla wake, sera ya taasisi hio ilikuwa ni kuwezesha mataifa mengi kujifunza namna mfumo wa ubongo na neva unavyofanya kazi na hii imechangia sana kufungua matawi yake mengi karibia nchi nyingi duniani.
Mashirika ya Afya ya umoja wa kimataifa yalikuwa yakiunga mkono kazi kubwa ambayo ilikuwa ikifanywa na taasisi hii kubwa ya kimarekanni isiokuwa ya faida(Non-profit organisation).
Katika miaka ya hivi karibuni maendeleo ya sayansi ya neva na ubongo yalikuwa yamepiga hatua kubwa sana , wale wagonjwa ambao walikuwa wamepoteza kumbukumbu ilikuwa rahisi kurejeshewa kumbukummbu zao ndani ya muda mfupi tu chini ya taasisi hii ya Haliz.
Haikuwa wagonjwa waliopoteza kumbukummbu tu , watu wengi ambao walionekana kusahau mambo muhimu katika maisha yao , iwe ni kubukumbu za utotini au za ukubwani taasisi ya Haliz ilikuwa na teknolojia ya tiba ya kurahisisha hayo yote.
Licha ya taasisi hio kufanikiwa lakini bado utafiti wa kuujua ubongo wa binadamu ulikuwa ukiendelea zaidi , kwani wanasayansi wanaamini ubongo uwezo wake ni mkubwa kuliko ile ambavyo inadhaniwa , hivyo wanaamini kuuwezesha ubongo kufikia uwezo wake kamili kimatumizi italeta maendeleo makubwa.
Frida alitembea kwa kujiamini kabisa ndani ya hospitali hio huku akipokelewa na harufu ya taasisi hio yenye kuzoeleka katika pua zake, kwa namna baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hio walivyokuwa wakimsalimia kwa kutingisha vichwa ilionekana alikuwa ni mfanyakazi mwenye cheo.
Aliishia kutoa tabasamu huku akitingisha kichwa kwa kuonyesha tabasamu kwa baadhi ya watu aliopishana nao ndani na ndani ya dakika kadhaa aliweza kuzifikia lift na kuingia ndani, lakini kabla hata ya mlango wa lift haujajifunga mwanaume mzungu wa makamo alievalia koti la kimaabara aliweza kuzuia lift hio na kuingia ndani.
Alikuwa ni mtanashati kweli aliependezeshwa na miwani ya macho , huku akiwa amepambwa na tabasamu.
âWell!. Fancy meeting you here, FridaâAliongea yule mzungu na kumfanya Frida kutoa tabasamu.
âUna ajenda gani kukimbilia lift Blake, huu si muda wako wa kufanya Demostrations na wanafunzi?âAliuliza Frida na kumfana Blake kutoa kicheko kama anakohoa.
âNdio nimemaliza, kulikuwa na mabadilishano na Dr John , Vipi wewe ndio umekuja kutubariki na utaalamu wako?,nilidhani upo likizo?â
âNipo likizo ndio , lakini haimaanishi sipaswi kufika hapa , nina biashara katika floor ya kumi na sabaâ
âWow!, Wow! , Floor ya wabobevu, sina neno la kuongezea, See you FridaâAliongea Dr Blake na ni muda uleule Lift ilisimama katika floor ya kumi na bwana huyo mzungu alitoka akimuacha Frida kuendelea na safari yake.
Frida aliishia kutoa tabasamu tu huku akiangalia namna ambavyo Blake anapotelea kwenye macho yake wakati lift ikijifunga.
Haikuwa kama ambavyo amesema Frida kwani mara baada ya lift kufika katika foor ya kumi na saba alitoka katika lift na kuingia katika floor hio ambayo ilikuwa na utulivu wa hali ya juu , ilikuwa ni ubaridi tu na harufu ya kuvutia , huku rangi ya taa zisizokuwa na mwanga mkali zikipendezesha eneo hilo.
Frida hakuingia ndani ya Foor hio bali alizunguka upande wa kushoto kwake na kuanza kupandisha ngazi kuelekea juu na ndani ya dakika chache tu aliweza kutokezea juu kabisa ya jengo hilo.
Licha ya kwamba alionekana kutembea kwa haraka, lakini kwa namna ambavyo alikuwa na spidi hakuonyesha hata kuchoka, alionekana kama aina ya wanawake ambao walikuwa na mazoezi makali.
Baada ya kutoka katika paa kabisa ya jengo hilo refu na kumfanya kuona mazingira ya mji wa Kibaha na baadhi ya maeneo ya Dar es salaam na Bagamoyo alivuta pumzi na kisha aliendelea kupiga hatua kusogea mbele.
Hali ya hewa haikuwa ya jua kali ,ilikuwa ni kama vile mvua ingenyesha muda wowote.
Mbele yake Frida alikuwa amesimama mwanaume alievalia suti ya rangi ya bluu akiangalia upande wa maeneo ya Dar es salaam kwa umakini mkubwa kana kwamba kuna kitu alichokuwa akitafuta.
Alikuwa ni mzungu kwa muonekao wa nywele tu na kadri Frida ambavyo alikuwa akitembea hatua zake zilionyesha hali ya kuwa dhaifu kiasi.
Kama ilivyo mwanaume yule alivyosimama ndio namna ambavyo Frida alienda kusimama katika ukingo wa jengo hilo na kuendela kuangalia upande wa mbele yake, ilikuwa ni kama vile anamwigizia yule mtu , na upande wa yule mtu hakugeuka kabisa ni kama alijua nani amefika hapo na kusimama pembeni yake.
âAny progress on KF-Target?âAliongea yule mzungu kwa sauti nzito.
âWe are almost there, Iâve initiated a plan to bring him closer to me, his curiosity will ensure our swift entry into the next phaseâAliongea akimaanisha kwamba anakaribia kumaliza , na ameanzisha mpango wa kumuweka karibu , anasema shauku yake itawafanya waingie hatua inayofuata kwa harakaâ
âElezeaâAliongea.
âNimemfanya anifanyie Delivery ya Viungo vya akili kutoka Binamu , uhakika ni kwamba atauliza maswali juu ya malipo makubwa yanayolipwa kwa ajili ya chungu kimoja kama njia ya usafirishaji, kwa kile nilichoona amevutiwaâ
âA risky moveâ
âCalculated Risky SirâAliongea Frida kwa kingereza na jibu lake lilimridhisha.
âVipi kuhusu wale wengine , namaanisha wanaoangalia kutoka mafichoni?â
âWe are keeping eye on them , once we have what we need, they âll be nothing more than loose endsâ
âEndelea na kazi kwa umakini , hatuwezi kuruhusu kosa loloteâ
âUmeelewekaâ
âSinagogi wanataka hii misheni kumalizika kwa haraka , siku zijazo utashughulikia na zaidi ya mtu mmoja katika tafiti yako , mategemeo makubwa yamewekwa juu ya hii sayansi mpya Frida ,natumaini kila kitu kitaenda sawa,Hatuwezi kuruhusu washindani wetu kupiga hatua kabla yetuâ
âIli mradi malengo yanakuwa wazi , kila kitu kitaenda sawa , natumaini utakuwa vizuri kwenye kuwatoa wasiwasiâ
âKama ni hivyo tutaonana tena katika hatua inayofuata kujua maendeleoâAliongea yule mwanaume na ilitokea kitu kama upepo tu kwani alipotea palepale na wala hali ile isimuogofye Frida ikionyesha ni jambo ambalo amezoea.

Damiani
Damiani mhitimu wa chuo kikuu cha uhasibu , anahitimu masomo yake na kurudi kijijini kwao kwa ajili ya kusubiria upepo wa ajira lakini katika hali ya kutokutegemea mama yake kipenzi anapigwa risasi mbili za kifuani na kufa hapo hapo na hio inatokana na kumpatia msaada mwanaume ambae hamfahamu mwenye asili ya ulaya (mzungu ) ambae na yeye alikuwa kwenye hatua ya mwisho ya kupoteza uhai wake kwani alikuwa na jeraha la risasi tumboni ,lakini mzungu huyo kabla ya kupoteza maisha anamkabidhi damiani nyaraka bila kumpa maelekezo ya aina yoyote ile .
Damiani anajikuta anajenga chuki na kisasi kwa watu waliohusika na mauaji ya mama yake , anajiapiza kuwatafuta mahali popote pale na kulipiza kisasi , katika harakati za kuwatafuta wabaya wake anajikuta akifahamu siri nzito iliokuwa nyuma ya kifo cha ghafla cha raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , anapata waraka ulioachwa na raisi huyo uliopewa jina la KAULI YA MWISHO YA RAIS KABLA YA KIFO CHAKE .
JE UNAFIKIRI ATAFANIKIWA KULIPIZA KISASI CHAKE ?
JE NI KAULI GANI YA MWISHO ALIO ACHA MHESHIMIWA RAISII KABLA YA KIFO CHAKE ?.
simulizi hii imekamilika , mwandishi ataiweka hapa hivi punde
.

Niliemdhania kahaba kumbe bikra
Roma mbeba mizigo ndani ya soko la Mbagala Rangi Tatu anamdhania Edna Kama mwanamke anaejiuza ,baada ya mwanadada huyu kuwekewa dawa ya usingizi kwenye kinywaji na maadui zake katika ulimwengu wa Biashara akiwa ndani ya hoteli na Roma anambeba Edna na kumpeleka Geto kwake na afanya nae mapenzi.
Edna kwa Mara ya kwanza analala na Roma pasipokujitambua na kupoteza usichana wake ,baada ya tukio Hilo anaamua kuolewa na Roma kwa mkataba wa Miezi sita ili kuepuka kuolewa na mwanaume asiempenda ,baada ya Roma kufunga ndoa na Edna anakuja kugundua kuwa mke wake anamiliki kampuni kubwa Nchini huku akiwa na utajiri wa kutisha.
Edna anamuona Roma kama mtu asiyekuwa seriasi na maisha kutokana na aina ya mfumo wa maisha yake ,maisha ya kuwa na wanawake wengi swala linalomkasirisha Edna.
Edna anajitahidi kuweka ukaribu na Roma ili kujua sababu ya mume wake macho yake kubadilika Rangi anapokuwa na hasira na kuwa ya kijani huku akiwa na roho ya ukatili mno
Idara na mamlaka za kiusalama Nchini zinashangazwa na uwezo wa Roma wa kuzungumza Lugha zaidi ya ishirini na mbili na wanaanza kutafuta taarifa zinazomuhusu Roma lakini licha ya kupata taarifa inayoonyesha Roma kusomea ndani ya chuo kikubwa Duniani Cha Harvard wanakosa taarifa zingine zinazomuhusu Roma na kuishia kujiuliza Roma ni Nani haswa