Reader Settings

Lengley,Virginia CIA HQ, 2021 FEBRUARY 0800Am

Ilianza kama siku tulivu ndani ya makao makuu haya , ambayo yalikuwa na pilika pilika za kiusalama, kwani kila mfanyakazi alionekana kuwa bize kuhakikisha kila mtu anatimiza majukumu yake ,  kama ilivyokuwa moja ya falsafa kwa wazungu “muda ni mali” basi kwa pilika pilika hizo waliendana na falsafa yao hio .

Basi asubuhi hio ndani ya ofisi ya DCI`s(Director of the Intelligence Agency) alionekana bwana George crispian mkuu wa kitengo cha Directorate of science and Technology  akiwa ameambatana na Jane Smith mkuu wa kiitengo cha Directorate of Intelligence , wote asubuhi hio walionekana kuwa na jambo la muhimu la kuripoti  kwa mkuu huyo wa CIA bwana Luis Tenet .

Jambo walilokuwa wanazungumzia asubuhi hio ilikuwa ni juu ya misheni iliopewa jina la Dragon X Trail  , misheni  ambayo ilikuwa ikienda kufanyika  nchini Tanzania.

Mbele ya meza hio kubwa iliokuwa imezungukwa na watu wa tatu  juu yake kulikuwa na fomu ama bahasha tatu  ambapo kila bahasha ilikuwa na taarifa  iliokuwa jumuishi juu ya  misheni  Dragon X ,bahasha namba moja ilikuwa na taarifa  kutoka NSA , fomu hii au bahasha ilikuwa  imebeba taarifa ya picha , hapa nazungumzia picha kama picha , na picha hizo zilikuwa zikizionyesha ubongo wa binadamu  , lakini pia  zilikuwa zikionyesha pia Screenshot ya  jumbe za meseji kupitia mtandao wa Watsapp , jumbe  hizo zilikuwa zikitoka  kwa  Profesa au daktari ndani ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kwenda  kwa mkuu (CEO) wa kampuni ya kitehama ifahamikayo kwa jina la EARTH TECH INC , kampuni iliokuwa na makazi yake ndani ya Taifa la Tanzania mkoani Arusha ..

Fomju ya pili ambayo   hii sasa haikutoka NSA  bali ilikuwa imetoka  ndani ya CIA  na ilikuwa imewasilishwa kwa DCI na mkuu wa kitengo cha Directorate of intelligence  yaani Bi Jane Smith  , Fomu hii ilikuwa  imejaa nyaraka zenye taarifa kutoka kwa Undercover  Agent(wakala) kutoka Tanzania(jina halikutajwa).

Fomu ya tatu hii ilikuwa ipo kwenye meza ya mkuu wa CIA ndani ya fomu hii juu kabisa ya  ukurasa wa kwanza  kulikuwa na maandishi ya DRAGON X TRAIL MISSION APPROVAL  ikiambatana na neno Confidential ,  fomu hii ilikuwa imetoka kwa Raisi wa USA  kupitia ofisi ya  DNI kwenda  kwa CIA.

Sasa basi ndani ya ofisi watu hao walionekana  kujadili jambo , lakini baada ya kama nusu saa hivi ,  waliongezeka watu wawili  watu hawa  walikuwa ni wakuu wa vitengo viwili  yaanni Directorate of support pamoja na ile  ndogo kabisa  ya Directorate of clandestine  .

Walikuwa  wote ni wanaume na baada ya kuungana  , walionekana kuwa katika kikao na mwisho wa kikao  walionekana walikuwa wakijadili mtu ambae anakwenda kuiongoza  misheni  hio ya DRAGON X TRAIL.

Lakini kati ya wale watu wawili walioingia ndani ya ofisi hio kwa kuchelewa mmoja alionekana kutoa faili  na juu ya hilo faili  likuwa na nembo kubwa ya alama ya UMOJA NAMBA TISINI NA SABA yaani U-97 na faili hilo lenyewe likiambatana na neno CONFIDENTIAL 

Hii misheni ni nini  haswa  , kwanini ifanyiwe ndani ya Taifa laTanzania , jibu  la jambo hilo linakuja kupitia tukio  ambalo ndani ya Taifa lilionekana ni tukio la kawaida kabisa kutokea katika jamiii , lakini kumbe ni  jambo ambalo lilikuwa limebeba  athari kubwa kwa jamii  ..

Tukio hilo linakwenda kwa jina la  MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU  ni tukio la kusisimua  lililotengeneza  sababu  ya kuundwa kwa misheni iliofahamika kwa jina la DRAGON X TRAIL. 

Lakini ni tukio ambalo lilipelekea  kufichuka kwa siri kuu ya UMOJA NAMBA

TISINI NA SABA  siri ya kitabu cha BOOK OF ALL NAMES

Huo ni utangulizi wa kitabu changu  kinacho enda kwa jina la MASAA

MAWILI YA KUMBUKUMBU 

Sasa kwa wewe ambae ushakwisha kusoma  UMOJA NAMBA TISINI NA SABA (waraka wa raisi kabla ya kifo ) basi nakuomba usome na tukio 

lililotokea katika kitabu cha MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU  ili 

upate maana halisi ya ya code name U-97  je ni nini maana halisi ya hilo neno  , je kuna umoja huo kwenye jamii au duniani kwa ujumla wake basi usisite kusoma.

Mambo makuu mawili utakayo yapata kuyajua katika kitabu hiki ni pamoja na jinsi gani mashirika makubwa  ya kimitandao yanavyokagua mawasiliano ya wateja wao wote dunia nzima . 

Utapata kujua nini  nini kiligunduliwa katika BLUE BOOK project, pia utakuja kugudnua namna projekti hio ilivyo changia  uundwaji  wa project ya TOP ON FILE project iliokuwa ipo chini ya STAR LABS  pamoja na IBM .

Je unataka kujua ni nini kilichonyuma ya DRAGON X TRAIL MISSION  hakikisha haukosi kusoma  .

Hii simulizi imerudi rasmi na itakuwa inaendelea hapa kila siku kipande kimoja mpaka mwisho

Next