ENDELEA.......................
“Unahisi ni kwanini alitoroka na kupotea wakati alikuwa hana kesi wala kosa lolote lile?” ni sauti nyingine nzito ambayo aliiskia kutoka kwa mwanaume huyo baada ya kukamilisha maelezo yake ya kwanza.
“Sina majibu kamili kwa sababu ilikuwa ni ghafla sana ila nakumbuka kwa baadae walihusisha lile jambo na upoteaji wa madini walihisi huenda mtu yule alitoroka na madini hivyo kwa niaba yake nilifungwa mimi jela kwa miaka mitatu ulifanyika uchunguzi mkubwa sana mpaka pale walipo jiridhisha kwamba hakukuwa na kitu chochote kile ndipo walipoweza kuniachia na kazi nikafukuzwa” alijibu bila kumumunya maneno alihitaji sana kuiponya nafsi yake, maelezo yake yalimfanya mtu huyo aweze kuivuta pumzi kwa nguvu kisha akaweza kutamka.
“Naitwa Liverton, ni komando kutoka upande wa kaskazini mwa Afrika ndani ya nchi ya Libya mimi na wenzangu tupo ha….”
“Ebu samahani kidogo naomba urudie hapo kidogo umeniacha sijakuelewa” neno komando alikuwa akilijua sana ni neno ambalo lilikuwa na uzito wake mkubwa unapokuwa unalitaja kwa sababu hutumika na vitengo nyeti sana vya usalama wa taifa wa nchi husika na watu hao huwa sio rahisi kukutana nao na kama utakutana nao basi utawajua kama raia wa kawaida na sio kuwatambua kwa nafasi zao kirahisi wanaishi kwa usiri mkubwa mno.
“Mimi hapa na wenzangu kumi na moja ni makomando kutokea katika nchi ya Libya kwenye kitengo cha LIBYAN ARMED FORCES (LAF) huko kaskazini mwa Afrika ndiyo sababu upo hapa nasisi tunahitaji maelezo yako pamoja na msaada wako kwa pamoja” alikuwa kwenye taharuki kubwa sana Kani alishindwa kuelewa Alen na hawa makomando wana uhusiano gani mpaka wamfuatilie na kuzihitaji taarifa zake kwa nguvu kiasi hicho.
“Mnahitaji nini kwake?” alijikuta anazidi kuwa mtu mwenye wasiwasi mkubwa kupita maelezo alikuwa amebanwa na watu ambao kwenye maisha yake alikuwa akiwasikia wakisimuliwa tu, alikuwa akiwajua namna watu hao walivyo na roho ngumu hata tamthiliya mbali mbali ambazo kwenye maisha yake alifanikiwa kuzitazama zilitosha kumpa tafsiri kamili ya nini maana ya neno komando.
“Huyo mtu ambaye wewe umesema unamjua kama Alen na ni rafiki yako wa muda mrefu hakuna kitu chochote ambacho unakijua kwake yeye zaidi ya sura yake tu labda ni…….”
“Hapana hapana huo ni uongo mkubwa unasema vipi simjua rafiki yangu ambaye muda wowote nikimhitaji tu nampata hahahhahh mtakuwa mmechanganyikiwa nyie sio bure” watu waliokuwa mbele yake alikuwa akiwaogopa sana lakini alijikuta akipandwa na hasira aliona ni kama wanamdhihaki kuambiwa hamjui mtu ambaye ni rafiki yake kwa muda mrefu sana kwenye maisha yake na hicho kitu yeye binafsi hakuweza kabisa kukubaliana nacho ila alimeza mate kwa shida baada ya kurushiwa baadhi ya picha ambazo zilionyesha mtu mwenye sura kama huyo ambaye alitoka kumtetea kwamba ni rafiki yake na alikuwa akimjua kwa usahihi, utofauti wa huyo mtu kwenye picha na Alen yalikuwa ni mavazi tu, huyo mwanaume wa kwenye picha alikuwa amevaa gwanda ambalo kwa haraka haraka alihisi ni la jeshi japo hakuwa na uhakika sana maana lenyewe lilikuwa na rangi iliyo changanyika na rangi ya kawaida ila lilijaa nyota kwenye mabega yake yote mawili na mwanaume huyo alikuwa ndani ya tabasamu zito la kuvutia.
“Umemtambua huyo mtu kwenye hiyo picha hapo?” aliulizwa Kani akiwa ameishika hiyo picha akijaribu kubishana na nafsi yake yeye mwenyewe kuna nafsi ilimpatia jibu kwamba mtu huyo alikuwa ni Alen ila kuna nafsi ilipinga kabisa kwamba hakuwa yeye, Alen alimjua sana hakuwa mtu wa haya mambo na alikuwa ni legelege kupita maelezo.
“Nooooo, wanafanana sana ila huyu sio Alen yule ni mtu ambaye ninamjua sana nimeishi naye kwa muda mrefu Alen hawezi kuwa hivi na hata haya mavazi siyo ya nchi yetu kabisa bendera ya nchi yetu haipo hivi siwezi kukukubalia hata kama ungehitaji kuniua kwa hili ni uongo huyu sio Alen” ilikuwa ni haki yake kukataa hilo jambo binadamu ambaye ameishi na kukaa naye kwa muda mrefu leo hii alikuwa anaonyeshwa picha za mtu mwenye nyota hizo za kutisha alipingana kabisa na hilo wazo kwa asilimia zake zote.
“Nilipokuwa kijana mdogo wakati bado nipo shule moja kati ya sababu iliyo nifanya nikafanikiwa kuyajua mambo mengi sana nikiwa nina umri mdogo ni kupenda kuuliza, sikuwa mtu ambaye nilikuwa napenda sana kupinga pinga hususani yale mambo ambayo ni wazi mimi sikuwa nikiyajua kabisa kwenye maisha yangu. siku hizi mambo yamekuwa tofauti sana shule zinaonekana kuzalisha kizazi cha kijinga kwa sababu watoto wa siku hizi wanaonekana kuwa wajuaji kupita maelezo hawawezi kuuliza namna mambo yanavyo fanyika na kwenda wao huwa wanakazana tu kusema haiwezekani, sasa wewe hapo ambaye hata nikikuuliza tu unitajie majina matatu ya huyo mtu huyajui, nikikwambia unitajie sehemu aliyo zaliwa hata huijui na umeishi naye kwa muda mrefu kwa kusingizia unamjua kwa vile umefanya naye kazi na kakusaidia unapata wapi hicho kiburi cha kuikataa hiyo picha bwana mdogo?” ni sauti ambayo ilitoka kwenye koo la mwanaume haswa ikiwa inamuasa Kani, aliinama chini baada ya kuambiwa ukweli wa mambo ambao ulimgusa moja kwa moja na kujiona yeye ni mpumbavu alitakiwa kuuliza huyo mtu ni nani hasa na sio kuanza kupinga kitu ambacho ni wazi aliambiwa hajui lolote lile.
“u uuuna…taka kuniambia kwamba Alen ni…….” Hakupewa hata nafasi ya kumalizia sentensi yake
“Ni wanadamu wachache sana huwa wanapata bahati ya kumfahamu huyu kiumbe pamoja na hizi siri zake, ukizijua hizi siri basi ni wazi umekuwa mtu wetu na utatakiwa kufanya kazi nasisi mpaka pale maisha yako yatakapofikia ukingoni na leo unakuwa mmojawapo hili sio ombi wala kwamba tunakubembeleza ni lazima iwe hivi vinginevyo tunaondoka na viungo vyote vya mwili wako na tunakuacha ukiwa hai uone namna dunia inavyo wanyanyapaa watu wenye ulemevu bila kuwa na macho, ulimi, miguu wala mikono na sehemu zako za siri ( alitetemeka sana mpaka mkojo ulimtoka baada ya kuambiwa hayo maneno)” mwanaume huyo alisimama na kuendelea.
Ni miaka nane sasa imepita tangu huyo mtu alipo anza kutafutwa na idara za kijasusi za nchi ya kaskazini na magharibi mwa Afrika, huyo mtu anatafutwa kuliko hata jinsi watu wanavyo itafuta pesa ili wapunguze ukali wa maisha ambayo kila siku yanazidi kuwakaba watu shingoni na kuwadhalilisha baadhi ya wanaume mjini kwa kuonekana nao ni wanawake ni vile tu wanavaa suruali kwa sababu hawana jipya mfukoni hayo ndiyo maisha ya mjini, huyo ni mwanadamu ambaye ukifanikisha upatikanaji wake basi unakuwa umeagana na umasikini kwenye maisha yako utapewa aina ya mali unazo zihitaji wewe mwenyewe na utazitumia mpaka siku unakufa hautakuja kufanikiwa kuzimaliza. Huyo kiumbe sio Alen kama unavyo mjua wewe wala sio mtanzania kama unavyo mjua wewe japo ana uraia pacha ambao kwa nchi hii tunahesabia kwamba haupo ndiyo maana nimesema kwamba sio mtanzania lakini pia huyo binadamu sio dhaifu kama wewe unavyo litamka hilo neno ambalo hautakiwi kuja kulirudia tena kwenye maisha yako na mdomo wako unatakiwa ukome sana kutamka hilo neno, huyo mtu unavyo mtaja unatakiwa uwe na uwoga sana sio kama kichwa chako kinavyo kudanganya kwamba yupo hivyo.
Jina lake halisi anaitwa Zakaria Mansour ana miaka 35 kwa sasa, ni msomi mwenye PHD (Doctor of Philosophy) kwenye masuala ya ARCHITECTURE DRAFTING OF BUILDINGS (msanifu na muandishi wa majengo) hakuna jengo anaweza akalitazama kwa dakika tano akashindwa kuichora ramani yake yote kuanzia chini kwenye msingi mpaka mwisho wa urefu wake. Ni mzaliwa na ni raia wa nchi ya Libya ambako ndiko sisi tunako toka katika mji mkuu wa Tripoli, baba yake ni raia wa kuzaliwa kabisa wa nchi ya Libya aitwaye Mansour Omran ila mama yake ni mtanzania aitwaye Sekelaga Philebert ni mtu kutoka kwenye ardhi ya wajivuni huko kama inavyo julikana ndani ya nchi hii ni Mhaya na inasemekana watu hawa wawili walikutana kwenye chuo kikuu cha OXFORD UNIVERSITY huko nchini Uingereza na walidumu kwenye ndoa yao kwa mwaka mmoja tu pekee wakafanikiwa kupata mtoto mmoja tu ambaye ndiye huyo ambaye wewe unamuita Alen. Kwa nafasi uliyo nayo ni ndogo sana kuna mambo ambayo hutakiwi kabisa kuyajua kwa gharama yoyote ile ila kwa kifupi ni kwamba huyo mwanaume ni komando na pia amewahi kuwa jasusi hatari zaidi kuwahi kuishi kwenye hili bara la Afrika na sio mtu wa kuvutia kama sura yake inavyo sadiki kwenye hiyo picha unayo iona ni binadamu wa kutisha na anaogopwa sana.
Sababu inayo fanya mpaka anatafutwa sana ni kosa la kuhusika na mauaji ya watu 50 wa familia mbili ambazo zilikuwa marafiki pamoja na kuua wanajeshi 67 na makomando 33 huko Afrika ya kaskazini pamoja na magharibi lakini hakuweza kukamatwa alifanikiwa kutoroka kabla hajatiwa nguvuni, hakuwahi kujulikana kwamba alipotelea wapi kwenye uso wa dunia hii ila mashaka makubwa yalikuwa ni nchi ya Tanzania ambako ni asili ya mama yake ndiyo sababu tupo kwenye nchi hii kwa muda mrefu sana na sio sisi tu wapo watu wengi sana ambao wanamtafuta kwa nguvu zote lakini pia kila nchi Afrika nzima kuna picha zake zimesambazwa kwenye idara za usalama tunasaidiana kumtafuta. Leo kwa mara ya kwanza tumefanikiwa kuiona picha yake mtandaoni ndiyo maana tuliamua kuharibu mifumo ya simu yako na kuzifuta zile picha tukakutafuta ulipo kwa sababu picha inaonekana imepigwa hivi karibuni maana yake tulijua unafahamu alipo, zile picha kama zingeonekana au watu wengine wangewahi kukupata mpaka muda huu hivi tunavyo ongea hapa ungekuwa marehemu anatafutwa sana huyo binadamu na siyo mtu wa kucheka naye akibadilika anaweza kuumaliza huu mji ndani ya msaa sita ukapishana na maiti kila unapo pita” Kani alikuwa ameyatoa macho kama vile alibanwa na mlango maelezo yote hayo ilikuwa ni ndoto ya kuvutia ila haikuwa kweli kwamba kulikuwa na mwanadamu katili namna hiyo ubaya kila alicho ambiwa alisisitiziwa ni ukweli hakukuwa na cha kusimuliwa ndoto wala tamthiliya ya kuvutia huo ulikuwa ni uhalisia wa maisha halisi ya rafiki yake ambaye alimuita kwamba anaitwa Alen na alijihalalishia kwamba anamjua sana.
“Naomba maji, naomba maji tafadhali” joto kali lililokuwa linampanda kwenye nguo zake lililikausha koo lake na kulifanya kuwa kavu kupita kiasi alihitaji kulilainisha kwanza ili apate nafasi ya kuweza kuuliza maswali kwa usahihi hakuwa anaelewa elewa namna wakati ulivyokuwa unamhukumu kwa kile ambacho alihisi anakijua yeye wakati hajui lolote, alirushiwa kikopo cha maji ya baridi aliyamaliza yote akahema kwa nguvu akajiinamia na kuinuka tena.
“Kama hayo maneno ambayo umeniambia ni ya kweli basi hii dunia hakuna sehemu salama kabisa kwa ajili ya maisha ya binadamu kuendelea kuivuta pumzi ya bure ambayo huwa tunapewa baadae tunajisahau na kuanza kujisifia kwamba sisi ndio wenye nguvu tunasahau mtoaji wa hiyo pumzi anatushuhudia namna tulivyo wachoyo wa fadhila, unaweza ukaniambia huo uwezo ambao unausema wewe anao aliweza kuupata wapi na hao watu aliweza kuwaua kwa sababu ipi hasa mpaka ifikie hatua mtu ambaye wewe mwenyewe umesema ni jasusi na komando aweze kutafutwa kwa nguvu na gharama kubwa namna hiyo?” aliambiwa mambo ya kutisha ambayo yalimfanya kuona ni vyema tu awe kawaida aliona kuendelea kuweweseka anajiongezea uoga, Kani sasa alikuwa anauliza huku akiwa amesimama.
“hakuna swali hata moja ambalo utaweza kujibiwa hapo pengine utabahatika kuja kuyajua siku za mbeleni ila kazi yako kwa sasa ni ndogo tu unatakiwa kumlegeza huyo mtu ili sisi tuje tumchukue na kuondoka naye baada ya hapo utapewa kila unacho kitaka”
“Hey namlegeza vipi mtu ambaye umesema sio binadamu wa kawaida sasa si ni shetani huyo” alianza kutetemeka sana alikuwa ametoka kusimuliwa kuhusu dubwana hilo lilivyo hapo tena anaambiwa kwamba alitakiwa kumalizia kazi ambayo ndiyo iliwafanya wamuahidi kumpatia chochote kile.
“Kuna dawa ambayo tutakupatia utampulizia nayo itammaliza nguvu na kummlegeza kabisa hatakuwa na uwezo wa kufanya chochote”
“Umesema huyo ni komando mwenzenu kwanini msiende wenyewe mkamchukue mimi niwaonyeshe tu sehemu ambayo anapatikana?”
“Hapa kati yetu wote kumi na mbili ambao nimekutajia kama huyo mtu akiwa kwenye utimamu wake na mzima wa afya basi hakuna yeyote ambaye anaweza hata kuugusa unywele wake japo mmoja tu akiwa bado mzima wa afya”
“Whaaaaaaat?”
Alen kwenye hesabu za wanaume, hadithi aliyopewa Kani kuhusu huyo rafiki yake wa machimbo ya madini ilibaki inamchanganya na kuendelea kumtisha hakuelewa sasa amuamini nani kwenye maisha yake yote ……… je ni kweli anayo ambiwa kuhusu Alen au anaingizwa cha kike? Na kama ni kweli je atafanikiwa kumkamatisha mwanadamu ambaye wamesema ni dubwana la ajabu namna hiyo?..........ukurasa wa tano natia nukta tukutane wakati ujao.
Bux the story teller
Comments