MIMI NA MIMI
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI
★★★★★★★★★★★★
Baada ya mazungumzo hayo yenye kuchochea hisia pamoja na mama wakubwa, Bi Zawadi akasema angekwenda kuniwekea makande aliyopika ili nile hatimaye, nami nikakubali hilo na kisha kurudi kukaa sofani. Wote kwa pamoja walitaka kujua mengi kuhusu udaktari wangu, nami nikawaelezea kwa njia nyepesi tu kuhusiana na masuala ya vitengo vya utabibu nilivyohusika navyo, muda ambao nilifanya kazi kwenye hospitali ile, mpaka kufikia wakati huu nilioamua kuchukua likizo fupi na kuja kukaa huku Mbagala. Nikaweka wazi kwao lengo langu la kuja kuishi huku kuwa kujaribu aina tofauti ya maisha niliyozoea kwa maeneo tofauti niliyopitia na kuishi, kama vile kujisahaulisha kwamba mimi nilikuwa daktari. Nimekaa kwenye vyumba vingi vya hospitali na kuzungukwa na watu wengi wenye kuhitaji msaada kwa muda mrefu kiasi, kwa hiyo nilihitaji kupumzika kidogo ndiyo nije kuendelea na wajibu wangu kama tabibu baadaye.
Kande lilikuwa tamu sana. Nikamaliza na kumshukuru Bi Zawadi, na ni hapo ndiyo sisi wote tukasikia honi ya gari nje ya geti la nyumba hii. Bi Zawadi akasema kwamba bila shaka huyo angekuwa ni Miryam, naye akataka kwenda kufungua geti lakini nikamwomba nimsaidie kufanya hivyo ili atulie tu ndani hapo. Akakubaliana na hilo. Nikaangalia muda kwenye simu yangu na kuona ilikuwa ni saa tisa alasiri sasa; ikionyesha Miryam na Tesha walitumia muda mrefu sana huko ofisini kwa mwenyekiti, ama labda walikwenda na sehemu nyingine pia ukitegemea walitoka na gari. Nikaenda hapo getini na kulifungua geti kuruhusu gari liingie. Vuuu likapita ndani, nami nikafunga tena geti. Nilipokuwa ndiyo nimemaliza tu kulifunga, nikaangalia gari hilo na kuwaona Miryam, Tesha, pamoja na Shadya wakiwa wameshashuka, wanawake hao wakiwa wananitazama usoni kwa umakini, huku Tesha akija niliposimama.
Akanifikia karibu, nasi tukagonga tano huku akisema, "Vipi mwamba?"
"Poa tu. Za huko?" nikamuuliza.
Hakutoa jibu, bali akaangalia chini na kushusha pumzi, kisha akapigisha ulimi wake kidogo mdomoni kama vile kuonyesha amevunjwa moyo na jambo fulani, naye akageukia upande aliosimama Miryam. Mimi pia nikamwangalia mwanamke huyo, ambaye alikuwa ananiangalia kwa njia tulivu tu, nami nikampungia mkono kidogo kama kumpa salamu.
"We' JC? Vipi? Akina shangazi wameshakugeuza gateman?" Shadya akaniuliza hivyo kiutani.
Nikatabasamu na kumwambia, "Na mshahara wameshanipa."
Akacheka kidogo na kumwangalia Miryam, lakini mwanamke huyo alikuwa serious kama vile amemeza chura au nini, naye akaelekea tu ndani. Shadya akatoa mifuko fulani yenye kujaa vitu vingi ndani ya gari hilo na kumfata Miryam ndani huko pia, nikibaki mimi na kijana Tesha hapo nje.
"Mambo yameendaje?" nikamuuliza.
"Ah... sister anazingua JC," Tesha akaniambia.
"Kafanyaje? Hamjamshtaki ka... a... huyo... huyo jamaa?" nikauliza tena.
"Umeona mwanangu? Hata wewe umetegemea tungemshtaki huyo fala, afungwe. Sasa Mimi si mama huruma sana? Kawaambia wamwachie," Tesha akaongea kwa sauti iliyoonyesha kuudhika kwake.
"Kawaambia wamwachie? Yaani kama vile amemwombea msamaha au?"
"Agh, mizinguo tu kaka! Hilo fala limemtukana hapa, lingeiba ishu ya Mamu, afu' tu eti anaenda kumwambia mzee Hamadi wamwachie jamaa! Imenidis sana..."
"Labda anaona kumfunga ndugu yenu haitafaa. Ameongea naye kwani?"
"Eee... Joshua ametoa makamasi hapo ndo' Mimi akamwonea huruma eti. Wamemwambia lakini wasije kusikia amezusha fujo wala chochote kile tena la sivyo watamfunga bila kujali huruma za dada. Ah... me nilikuwa natamani aende akanyee debe leo! Basi tu..." Tesha akasema hivyo.
Nikatabasamu kidogo na kusema, "Dada yako siyo mtu wa visasi inaonekana. Halafu... anaijali familia yenu, nyie wote yaani, hata kama huyo Joshua kapotea. Mwelewe tu... na umuunge mkono. Sawa?"
"Agh... bado inakera bana. Nilitaka nimwone huyo bwege amevaa karoti leo nije kula kuku mimi. Sasa sa'hivi nakuja kula tu kande huku nimevimba, ndo' nini? Ah..." akaongea kwa kuudhika.
"Ahahah... nenda kale kande, litapunguza hasira. Ni tamu," nikasema.
"Umeshakula?"
"Yah, Bi Zawadi kanionjesha."
"Au siyo? Sawa, ngoja na me nikale, nipige maji afu'... ah... mishe gani unafanya baadaye?"
"Nipo tu."
"Sijui twende tukazurure tu Mbagala? Ningekuwa na mshiko tungeshindia Masai..."
"Ahahaha... Gonga amenipigia mara kadhaa, sijui anataka nini..." nikamwambia.
"Ih, kweli? Hujapokea?"
"Hamna, sioni haja. Nahisi kama atan'sumbua tu..."
"A-ah... usizingue. Mtafute, najua anataka kukuita. Fanya mambo basi, uniunganishe na mimi angalau tukazimue za ofa, ama nini?"
"Ahahah... Tesha unapenda kunywa wewe!"
"Hahaha... aaa siyo sana. Ila hizi ofa kabambe siyo za kupitwa. Fanya mambo tuilambe hiyo," akasema hivyo na kuniwekea ngumi usawa wa kifua changu.
Nikaigonga kwa ngumi yangu pia na kusema, "Haya bana. We' nenda kale, tutashtuana baadaye. Waambie mama wakubwa nimeondoka eh? Tutaonana tu hata kesho."
"Haya poa kaka," akasema hivyo.
Tukaachana kiaina hiyo, nami nikarudi moja kwa moja mpaka ndani kwake Ankia.
Nilikuwa nimeijaza akili yangu mambo mengi kutokea asubuhi hii, lakini sasa angalau ilikuwa imepewa wepesi kiasi baada ya kuzungumza na Bi Zawadi na Bi Jamila kuhusiana na familia yao. Kilichokuwepo sasa ilikuwa kutafuta muda mzuri wa kuongea na dada mkubwa, Miryam, kuhusu suala la tatizo lililomwathiri mdogo wake, na ndiyo ningeanza kweli kumsaidia Mariam. Nilipofika sebuleni hapo sikumkuta Ankia, nami nikasogea mpaka upande wa kuelekea jikoni nikidhani angekuwa huko lakini nikamkosa. Bila shaka angekuwa chumbani kwake, labda kalala, na nilipokuwa nimeamua tu kuelekea chumbani kwangu ili nikapumzike, mwanamke huyo akaniita kutokea chumbani kwake.
"JC..."
Nikaitika, "Naam..."
Sauti yake ikasema, "Ndo' umerudi?"
"Ndiyo. Ndo' naingia..."
"Funga basi huo mlango halafu uje..."
"Mlango wa sebule?"
"Eeee..."
"Kuna nini tena huko weye?" nikauliza kiutani.
Nikasikia akicheka, naye akasema, "Njoo bwana."
Tayari nilikuwa najua mambo ya kutarajia nikienda chumbani kwa mwanamke huyo, na kiukweli kwa muda huu nilikuwa na mhemko ufaao kukutana nayo hayo mambo. Si ni ile kuvutiana-vutiana sana na mwanamke huyo aliyekuwa amenielewa kupitiliza? Kwa hiyo kama alitaka nimpe alichokitaka sasa hivi, nilikuwa nimeamua kumtolea uvivu. Nikaenda kuufunga mlango, yaani kuufunga kwa funguo, hiyo ikiwa ndiyo maana yake nilijua hivyo. Nikaenda mpaka kwenye mlango wa chumba cha mama mwenye nyumba wangu, nami nikaufungua na kuingia ndani humo.
Kilikuwa chumba chenye upana kiasi, kukiwa na kitanda kikubwa cha tano ya sita, kabati la nguo na stendi ya chuma ya kuning'iniza vitu kama nguo na mikoba, shehena ya kuwekea viatu, na dirisha kubwa ukutani lililofunikwa kwa pazia refu na kuacha upande mmoja tu ndiyo uwe wazi kupitisha hewa bila shaka. Harufu ile nzuri ya Ankia ilikijaza vyema chumba hicho, nami nikaachia tabasamu hafifu baada ya kuona jinsi kitanda chake kilivyopambwa vizuri. Siyo mashuka wala mito, ila Ankia ndiye aliyekuwa pambo lenyewe. Mwanamke alikuwa amejilaza kwenye kitanda hicho kwa kulalia tumbo, huku miguu yake akiitandaza kiasi na mikono yake akiikunja na kuikutanisha usawa wa kichwa chake; akiulaza uso wake kwenye viganja vyake alivyoviunganisha pamoja. Alivaa khanga moja pekee mwilini, ikifanya mlima wake hapo nyuma uonekane vyema kwa jinsi ulivyotuna, na mapaja yake yenye nyamanyama yakiwa wazi kwa nyuma. Uhlalaah! Ilikuwa kama vile ni chakula kimewekwa mezani, na mimi nikitakiwa kuwa mlaji ningeamua tu nianze kukitafunia wapi.
Ankia kweli alikuwa ameamua kunionyesha, na mimi nisingemvunja moyo. Alikuwa ananiangalia huku akitabasamu kwa njia ya shau, lile tabasamu la kuonyesha tunaelewana sana, nami nikaingia humo na kusimama usawa wa kitanda huku nikimwangalia.
"Keki hiyo..." nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.
Akaelekeza fikira zake katikati ya suruali niliyovaa, naye akaniangalia tena machoni.
"Naona umeuandaa msosi vyema. Ama ulikuwa unataka kulala?" nikamuuliza.
Akafumba macho yake na kutikisa kichwa kukataa. Nikakaa kitandani usawa wa miguu yake, nami nikaanza kutembeza vidole viwili kwenye mguu wake wa kushoto kwa kuvipandisha kuelekea pajani.
"Siyo siri Ankia... umenona," nikamwambia hivyo.
"Asante," akanena hivyo kwa sauti ya chini.
"Nina njaa ujue... njaa ya kula hiki chakula chako. Ila nahitaji kujua kama itakuwa salama kula mpaka mwisho," nikamwambia hivyo.
"Ni salama. We' kula tu," akaniambia.
Huku nikitekenya mguu wake, nikamuuliza, "Kweli? Chombo ni safi?"
"Imetakata kabisa."
"Kwa hiyo nijilie tu?"
"Kula. Yote yako..."
Eh bwana eh!
Akaendelea kutulia tu, nikimwona namna alivyoibana na kuiachia midomo yake mara kwa mara, nami nikaamua kukatisha maneno ili nianze kushughulika kweli na hiyo keki. Na nilimtendea haki huyu mwanamke mpaka akawa anaomba po kila mara. Alikuwa anaongea maneno ya kiingereza na kikabila cha wazaramo, raha ikiwa imemkolea haswa, na kuna haka kamsukumo kalikonishawishi niendelee tu na mimi mpaka kufikia sehemu ya mridhiko, nayo ikaja na kuachiwa. Si alisema ilikuwa salama kabisa? Mimi nikaishushia ndani-ndani ukweli. Ikafata sasa ile sehemu ambayo tukishagamaliza hiyo kitu tunaanza kuwaona wenzetu kuwa kama nguruwe! Ila hapana, sikumwona Ankia kuwa nguruwe. Ni uchovu tu wa raha niliopata maana ni muda mrefu kiasi sikuwa nimejiachia namna hiyo. Nimefanya uhuni mwingi sana kiasi kwamba hata tu kumwambia mtu mimi ni daktari haikuonekana kuwa kweli, maana madaktari hupendaga kujionyesha wana aina fulani ya utakatifu lakini ndiyo watu wakatili na wachafu zaidi hapa duniani! Natania tu.
Riadha yangu na Ankia ikawa imeishia hapo, angalau kwa wakati huu. Nikaanza kupitisha kiganja changu usoni kwake, naye akaingiza kidole changu kimoja mdomoni mwake na kuanza kukinyonya. Jasho lake na langu lilifanya ngozi ziteleze kwa namna tulivyoibana miili yetu.
"Hapo vipi? Umekaa sawa?" nikamuuliza hivyo baada ya kukitoa kidole mdomoni mwake.
"Mhm... una mapigo matamu JC..." akaniambia hivyo.
"Hata wewe uko vizuri. Utanifanya nioge kwa mara ya pili," nikamwambia.
Alionekana kuchoka, kwa kuwa aliendelea kulala namna hiyo hiyo huku akinitazama kilegevu.
"Makeke yamepungua sasa, au siyo? Ngoja me nikaoge," nikamwambia hivyo.
"Tangulia nije..." akasema hivyo.
"A-ah... we' tulia, me naenda kuoga kwanza halafu ndiyo utafata..."
"Kwa nini tusioge wote?"
"Macho mengi."
"Asa' hapo nani atatuona? Halafu we' si huwa haujali watu? Unamwogopa nani sasa?"
"Simwogopi mtu. Ila mimi siyo wa hivyo. Napenda ya ndani yawe ya ndani, siyo mpaka kila mtu ajue. Na huu mtaa wenu umekaa kama wa Kazamoyo," nikamwambia.
"Mh? Haya baba. Chochote kile kwa ajili yako, mi' nitafanya. Umenipa raha kweli... we' siyo mchezo..." akasema hivyo.
Nikatabasamu kidogo kuanza kuivaa boksa, nami nikamwambia, "We' ni mtamu sana."
Akatabasamu kidogo kwa haya, naye akasema, "Wewe pia."
"Me naenda sa' kujimwagia, af' naingia kulala. Sawa?" nikamwambia hivyo na kusimama.
"Hauli?" akaniuliza.
"Nimeshiba. Zawadi mweupe kanipa kande."
"Aaa... umeongea nao?"
"Ndiyo."
"Wamesemaje?"
"Wamenikubalia. Nataka nimsaidie Mariam na shida aliyonayo, ikiwa mambo yataenda vizuri, basi atakaa sawa."
"Unataka kumsaidiaje sasa?"
"Utaona. Ila ndo' napaswa niongee na dada yake kwanza."
"Walikuwa hawajarudi bado? Nimesikia kama gari limeingia..."
"Ndo' wamerudi me ninatoka, nitatafuta tu wakati mwingine niongee naye. Nataka sana nimsaidie huyu msichana. Niombee nifanikiwe," nikamwambia hivyo.
Akatabasamu.
"Nini?" nikamuuliza.
Akatikisa kichwa na kusema, "Una roho nzuri. Natamani ningekumiliki kimoja."
Nikatabasamu na kuokota nguo zangu huku nikimwambia, "Siyo roho nzuri, sema ni hicho kimoja nilichokupiga hapo ndiyo kimekumaliza akili kabisaa. Usijali. Utakipata tu tena. Endelea tu kuwa mtoto mzuri."
Akatabasamu na kuniangalia kwa madaha. Nikamsogelea na kumpiga busu kavu mdomoni, hii ndiyo naiita busu ya kishkaji, nami nikatoka chumbani kwake hatimaye.
★★
Nilikuja kuamka mida ya saa kumi na mbili kasoro, jioni, nami nikanyanyuka kutoka kitandani na kuvaa nguo nyepesi. Tokea nilipomaliza tu ile ishu yangu na Ankia muda mfupi nyuma, nilienda kuoga na kisha kuja kulala kidogo. Nikachukua simu na kukuta jumbe chache pamoja na 'missed call' kutoka kwa Chalii Gonga, nami nikaamua nimtolee jamaa uvivu hatimaye na kumpigia. Alipopokea, akaanza kuniuliza kwa nini sikuwa nikijibu miito yake, nami nikamwambia sikuwa karibu na simu leo kutokana na kuiacha ndani ipigwe chaji wakati nilipokuwa nimetoka. Nilibuni hadithi hiyo upesi kwa kusema yaani ndiyo nilikuwa nimerudi tu sasa hivi, nami nikamuuliza ikiwa kulikuwa na jambo muhimu alitaka kunieleza. Akaniuliza kama ningeenda Masai baadaye, nami nikasema haikuwa jambo la uhakika, lakini akasema tu nije kwenda huko na nikifika niagize chochote naye angekuja kulipia. Dah! Jamaa alikuwa ameanza kuleta mambo nisiyofagilia hata kidogo; shobo nyingi. Alisema na yeye hakuwa mtu wa shobo sana ila kwangu alikuwa ameanza kushoboka mno, na ili kumridhisha tu nikasema poa, ningefanya hivyo.
Tukaachiana hapo, nami nikaingia upande wa jumbe fupi na kumjibu Tesha, aliyekuwa anauliza kama tutaingia Masai ama tukatembee Mbagala. Nikamwambia tutaenda Masai mida ya saa moja, kwa hiyo apite hapa kwa Ankia ili twende. Baada ya hapo, nikatoka chumbani hatimaye na kwenda sebuleni. Ankia hakuwepo sehemu yoyote kati ya sebule na jikoni, nami nikakisia kuwa huenda alikuwa amelala bado. Yeye pia aliniambia angelala, kwa hiyo nikaenda tu kwenye sofa na kukaa. Nikapitia-pitia mitandao ya kijamii kidogo na kusoma vipengele fulani vifupi vya masuala ya kitabibu, kisha nikaachana na simu ili umakini wangu niuweke kwenye ile feni ya Ankia. Nikaifata na kuanza kuichunguza hapa na pale, nikijaribu kuiwasha na kubashiri tatizo lingekuwa wapi mpaka giza lilipoanza kuvizia kuingia, hali hiyo ikifanya ndani pawe na ugiza.
Ni taa ya sebule iliyowashwa ndiyo ikanifanya niachane na feni hiyo baada ya kumwona Ankia, nami nikampa tabasamu la mapokezi huku yeye akiniangalia na kufikicha jicho lake moja. Akiwa ametoka kuamka, kasura kake kalivimba kiasi, na mwilini alivaa ile ile khanga moja niliyomkuta nayo muda ule chumbani, kitu ambacho kikanikumbusha mchezo wetu mzuri uliomwacha akinimwagia sifa za mimi kuwa fundi.
"Good morning," nikamwambia hivyo kiutani.
"Unaniona kama sijasoma? Morning sa'hivi?" akaniuliza.
"Angalia saa uone. Ndo' inaingia saa moja. Ubishi wa nini?"
"Kichwa chako! Iko saa moja moja kwani?"
"Ziko ngapi, ishirini?"
"Hebu acha mambo yako. Umeamka zamani?"
"Hamna, sina muda mrefu. We' ndo' unalala kama gogo."
"Nilikuwa nimechoka..."
Akasema hivyo na kuja kukaa kwenye sofa karibu na sehemu niliyochuchumaa kwa kupiga goti moja chini, huku feni ikiwa mkononi mwangu. Nikaendelea kuichokonoa.
"Umeweza kuitengeneza?" akaniuliza.
"Hamna... ila we' ngoja. Hii inazunguka sasa hivi tu, mapemaa..."
"Mhm... haya bwana. We' ndo' fundi, nakuaminia..."
"Haupingwi kwa hilo mama..."
Akatabasamu kidogo na kuendelea kunitazama nilipoendelea kutia juhudi kuirekebisha feni hiyo, kisha nikaifunga na kujaribu kuiwasha. Si ikaanza kuzunguka! Ankia akaachama kimshangao, huku na mimi nikitabasamu kwa furaha, halafu nikamwangalia kwa macho yenye kiburi. Akacheka kwa furaha na kunikumbatia, akisema amekubali sana maajabu yangu.
Nikaiweka feni pembeni na kukaa karibu yake, ikiwa inatupuliza sasa angalau kupunguza joto, nami nikasema, "Mishe gani sa'hivi?"
Akashusha pumzi na kusema, "Labda kupika. Nilikutunzia ugali mchana... ila najua sa'hivi hautaliwa. Inabidi tu nikafate mboga sokoni halafu nije kupika na ubwabwa... tule."
"Mboga gani?"
"Sijui samaki... au nyama?"
"Ahirisha tu..."
"Kwa nini? Yaani tusile?"
"A-ah... tutakula. Nataka twende Masai. Tutakula huko," nikamwambia.
Akaachia tabasamu na kuuliza, "Unanitoa dinner eh?"
"Ahahah... hapana, usikijaze kichwa chako hayo mambo. Tunaenda na Tesha," nikamwambia.
"Aaaa.... nikafikiri mimi na wewe tu. Afadhali lakini, sitasumbuka. Mwanaume wangu anaenda kuninunulia msosi, nitake kipi kingine?"
"Ahaa... Basi nitakuwa nakupeleka tu kula msosi, sawa? Ila suala la kukupelekea moto sahau..." nikamtania.
"Ila wewe..."
"Nini sasa? Si hautaki kingine ila msosi?"
"Mm... me sitaki..."
"Unataka nini? Kula lazima, kuliwa hiari..."
Akacheka kidogo na kunilalia begani.
Simu yangu ikaanza kuita, nami nikaitoa na kukuta namba ngeni. Agh! Sikupenda kabisa kupokea namba nisizozifahamu maana usumbufu ulikuwa mwingi sana, naye Ankia alipoona sipokei, akaiangalia namba hiyo kwenye kioo cha simu yangu.
"Nani?" akaniuliza.
"Ah... sijui... me sipokei," nikamjibu.
"Kwa nini sasa? Je kama ni muhimu?"
"Atume ujumbe. Mimi simu nisizozifahamu huwa sipokei..."
"Sasa ndo' nini?"
"Ndiyo hivyo."
"Je kama ni Tesha? Au mtu mwingine mnayefahamiana naye?"
"Hakuna. Mimi watu naofahamiana nao huwa nawa-save. Sipendagi usumbufu wa namna hii..."
Simu ikakata, kisha ikaanza kuita tena; namba ikiwa hiyo hiyo.
"Agh..."
"Pokea tu JC. Hataacha kupiga usipopokea. Tuchukulie ni ndugu yako. Nisikilize tu. Pokea..."
"Na nikikuta siyo? Nikufanyeje?"
"Nifanye chochote unachotaka..." akanijibu kwa nyodo.
"Mmm... haya..."
Nikapokea simu hiyo hatimaye, nami nikaiweka sikioni. Sikuzungumza, lakini aliyekuwa upande wa pili alipoanza kuongea, nikaweka uso makini.
"JC... hhh... JC..."
Sauti hii niliifahamu, ikiwa ni ya mwanamke. Uzito wa namna ambayo ililiita jina langu uliniambia kwamba mwanamke huyu alikuwa akilia.
"JC... naomba unisaidie... njoo.... p... njoo tafadhali..."
Ilikuwa ni Joy.
Nilishangaa kiasi. Sikuwa na kumbukumbu ya kumpa namba yangu lakini hilo halikuwa lenye umuhimu sana kwa wakati huu. Nilijiuliza alikuwa amepatwa na nini kilichohitaji mimi ndiyo nimpe msaada. Sikutaka kujiingiza kwenye shida zingine zaidi za watu wa aina yake lakini jambo hili lilivuta hisia zangu za kujali kumwelekea. Alikuwa amekumbwa na nini huyu mwanamke?
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★
Comments