Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA MBILI 

★★★★★★★★★★★★★★★★


SAA MOJA NA NUSU KABLA YA XANDER KUFIKA KWENYE NYUMBA HIYO PAMOJA NA LUTENI WEISIKO


Ni wakati wako kwenye sherehe ya Alice ya siku ya kuzaliwa kwake, mapacha walikuwa wamesimama pamoja na marafiki wakiongea huku wanapata vinywaji. Huu ulikuwa ni muda mfupi tu baada ya kuwa wamemaliza kula chakula pamoja na wazazi wao na mdogo wao. Baada ya Alice kwenda na Casmir ndani ya nyumba ili waongee, Xander, akiwa ndani ya mwili wa Sandra, akamfata pacha wake na kumvuta pembeni ili waongee kidogo. Akamwambia kuwa alitaka kuondoka mara moja.

"Nini? Unataka kwenda wapi?" Sandra, akiwa ndani ya mwili wa Xander, akashangaa.

"Naenda tu kuonana na rafiki yangu hapo kona..." Xander akamwambia.

"Rafiki gani wakati una mwili wangu?"

"Nisikie. Mama na baba wameenda ndani. Nafikiri wanaenda kupeana 'baby me I like that,' kwo' hawatoki sasa hivi..."

"Kwa hiyo?"

"Sichukui muda mrefu, ila ikitokea wameniulizia sijarudi..."

"Xander huo ni mwili wangu. Sa'hivi ni usiku unaenda wapi, akitokea kibaka huko akaku..."

"Umesahau aliye ndani ni Xander bwana, hakuna kibaka anagusa hapa. Na... nina hizi..."

Akanyanyua kiganja chake juu kumwonyesha Sandra funguo za gari la mama yao.

"Unataka kuiba gari la mama?" 

"Ni guarantee kwamba nitawahi..."

"Unaenda wapi? Kwa madam V? Unajua huko ni mbali..."

"Siendi kwa madam V, hivi wewe! Just trust me... nakuja sasa hivi... nafata tu ishu yangu hapo kona chap..."

"Haki ya Mungu Xander kama unaenda kuitembeza kitu yangu..."

"Utaniua. Siwezi kufanya hivyo. Nakuheshimu sana Sandra... iijapokuwa huyu ni mimi ninaiambia sura yangu hivyo hahahah..." Xander akatania.

"Dakika 10 uwe hapa," Sandra akamwambia.

"Yes ma'am..." Xander akasema na kumpigia saluti.

Akaondoka haraka akiwa amevaa gauni na viatu vya kike virefu vilivyompa shida sana kutembea, mpaka Sandra akawa anamcheka. Akaingia upesi kwenye gari la Alice na kuanza kuliondoa hapo, akiwaambia walinzi getini kuwa anafata kitu fulani muhimu na anarudi upesi. Wakamfungulia, kisha akaondoka na kuanza safari ya kuelekea kwa madam Valentina. Kihalisi alikuwa amemdanganya Sandra kwa sababu alijua kama angesema anaenda huko basi dada yake asingekubali hilo. Ilikuwa muhimu kwake kumwambia Sandra kwamba anaondoka kwa sababu alijua pacha wake angemtetea tu hata kama angechelewa kurudi. 

Kwa king'ang'anizi chake Xander alikuwa amechochewa kufanya lolote lile ili tu amwone mpenzi wake mpya, madam Valentina. Ni kama alikuwa mraibu kwa mwanamke huyo, hasa kwa sababu hakuwahi kuwa na uhusiano na mtu aliyemwacha mbali kiumri namna hiyo. Alitaka tu kuwa naye kila mara na ndiyo sababu akaikimbia na sherehe ya mama yake kwa kuwa aliona inaboa. 


★★


Baada ya mwendo wa dakika kadhaa, simu yake ikaanza kuita, na mpigaji alikuwa ni Sandra. Akakwazika kwa sababu alijua bila shaka ilihusiana na yeye kutakiwa kurudi nyumbani. Akajifikiria ikiwa angerudi, safari yake isingekuwa na maana yoyote kwa kuwa hakutimiza alichotaka. Akaamua kuipuuza tu mpaka ilipokata, kisha ikaanza kuita tena. Aliona ni bora tu aitolee sauti, ili isimsumbue kichwa, yaani iwe ni kama hatafutwi, kisha akairusha kwenye siti za nyuma ya gari. 

Simu iliendelea kuita, lakini wakati huu mpigaji akawa ni mama yake. Yeye bila kujua umuhimu wa simu hizo, akawa amelifikisha gari mpaka nje ya nyumba ya madam Valentina. Akashuka na kuiacha simu yake ndani ya gari akielekea kwenye geti la nyumba hiyo. Alifikiria tu hata akimwona kwa ufupi angeridhika kisha ndiyo angerudi nyumbani. Akagonga geti, kisha akasubiri kwa hamu. Aliwaza labda hata Valentina alikuwa ameshalala, lakini hangekubali kuondoka mpaka amwone, hata kama ingehitajika kumwamsha. 

Baada ya sekunde kadhaa, akasikia sauti ya madam Valentina ikiuliza "nani?" naye akamwambia ni Xander. Mlango mdogo wa geti ukafunguliwa, na hapo mbele yake akawa amesimama Valentina huku amevaa nguo laini ya kulalia iliyoacha mapaja yake wazi. Xander akiwa ndani ya mwili wa Sandra akawa anamwangalia kwa furaha sana, huku Valentina akimtazama kimaswali.

"Alexandra... una... oh ni Xander. Xander mbona uko hapa now?" Valentina akamuuliza.

"Nilikuwa nataka niku-surprise," Xander akasema.

"Lakini..."

"Tafadhali nikaribishe ndani. Mwili wa Sandra unahisi baridi... na hivi viatu ni majanga..." Xander akamwambia.

Valentina akampisha mlangoni ili aingie ndani. Baada ya kuwa amepita, Valentina akafunga mlango huo wa geti kisha naye akamfata. Xander akaingia mpaka ndani ya nyumba mpaka sehemu ile ya sebule, na sasa akawa amesimama usawa wa masofa baada ya Valentina kuingia pia.

"Unaonaje hili gauni? Nimetokelezea eh?" Xander akamwambia.

"Ndiyo, lakini huo ni mwili wa dada yako kwa hiyo... ni yeye ndiyo ametokelezea," akasema Valentina.

"Ni sawa lakini, mimi ndo' naumiliki. Huwezi kuamini washkaji wanavyoniangalia sana chuoni na maeneo mengine utadhani mie chakula!" 

Valentina akatabasamu kidogo huku anamwangalia. 

Xander akamsogelea. "Najua hukutegemea mimi kuja," akamwambia.

"Ndiyo sikutegemea, unajua sa'hivi saa ngapi? Si ungeniambia kama unakuja... je kama ndugu yangu angekuwa amefika hapa?" 

"Kwani huwa anatafuna watu?"

"Angekupika."

"Ahahahah... siyo mbaya, maana mchuzi wangu mtamu..."

"Ni wa dada yako..."

"Eee si ndiyo nasema, angalau mwili wangu ungekuwa sehemu nyingine salama."

Valentina akacheka kwa kuguna.

"Samahani kukuvamia. Nilitaka sana kukuona," Xander akasema huku anamsogelea.

"Lakini Xander..."

Kabla hajamaliza kuongea, Xander akamshika kiunoni na kuanza kuibusu midomo yake taratibu, na kimahaba sana. Kila mara alipoiachia, Valentina angesema "Xander," kisha yeye angeendelea tu kumpa denda hiyo. Kwa Valentina bado ilikuwa ni ajabu kwa sababu ni kama alikuwa anapiga busu na mwanamke mwenzie, hata kama aliyekuwa ndani ni mwanaume. Xander akajitoa mdomoni mwa Valentina na kumwangalia machoni kwa hisia sana.

"Bado unahisi ni kama vile unambusu Sandra eti? I mean come on, tunafanana... just imagine ni mimi na..."

"Lakini haiwezi kuwa WEWE Xander. Najua uko humo ndani, lakini... nimekuzoea tu wewe ukiwa kama wewe. Siyo rahisi kwangu ukiwa namna hii... ni tofauti..." Valentina akafunguka.

Xander akahuzunika sana. Alimwelewa vizuri mno Valentina, na roho yake ilimuuma kwa kuwa hakuweza kujua angewezaje kuiondoa hali hii. 

Kutokea chumbani kwake, Valentina aliweza kusikia simu yake ikiita. Xander akamwachia na kwenda kwenye sofa kukaa, akiwa amevunjika moyo sana. Valentina alimwonea huruma, lakini ni kama tena hakujua la kumwambia ili kumsaidia. Simu yake ilikata na kuanza kuita tena, hivyo akamwambia Xander kwamba anaifata na atarejea ili waongee. Akafika chumbani na kukuta mpigaji ni Xander, yaani Sandra, naye akapokea.

"Hallo... Madam V..." ikasikika sauti ya "Xander."

"Ndiyo... Alexandra mwenye besi..." akasema Valentina.

"Samahani... Xander yuko kwako?" 

"Ndiyo..." 

"Tafadhali naomba kuongea naye... ni muhimu sana..."

Valentina aliweza kuhisi kutokana na jinsi maneno hayo yalivyosemwa kwamba kuna jambo halikuwa sawa. Bila kujibu lolote akatoka haraka chumbani kwake na kumpelekea Xander aliyevaa gauni simu yake. Akamwambia kwamba pacha wake alikuwa akimtafuta.

"Aaigh... umemwambia niko hapa?" Xander akalalamika.

"Chukua Xander, inaonekana ni muhimu sana," Valentina akasema.

Xander akaichukua simu akiwa anajua bila shaka dada yake angeanza kulalamika kuhusu ni wapi alikuwa.

"Sandra vipi?" Xander akasema baada ya kuweka simu sikioni.

"Xander toka huko haraka njoo nyumbani!" Sandra akamwambia kwa sauti ya chini upande wa pili.

"Mzee ameshaanza kumtafuta mdoli wake eeh?"

"Acha masihara. Kuna shida imetokea. Wahi nyumbani sasa hivi..." 

"Yeah... actually... sidhani kama n'tarudi leo maana huku mambo ni fire!" Xander akatania.

"Xander... maisha yako yapo hatarini! Unapaswa kuni..."

Kabla Xander hajasikia kile ambacho "dada" yake alitaka kumwambia, simu ikakatwa. Akashangaa kiasi na kubaki ameitazama tu simu ya Valentina kiganjani mwake. Valentina akaketi karibu yake.

"Vipi, kuna tatizo gani?" akamuuliza.

"Sijui. Huyu mdoli ananiambia niondoke huku haraka, sijui maisha yangu yako hatarini, hata simwelewi..." 

"Nini?" Valentina akashangaa.

"Inawezekana ananitisha tu. Nilimwambia nitawahi kwa sababu huu ni mwili wake kwa hiyo anafikiri nitaogopa ili niwahi kurudi..."

"Hapana Xander. Subiri. Amekwambiaje kabisa?"

"Kasema hivyo nilivyokwambia, halafu akakata simu gha...."

Kabla hajamaliza kuongea akakumbuka kwamba Sandra alikuwa ameshaanza kumtafuta tokea yuko kwenye gari. Ikaanza kuonekana kwake sasa kwamba hii haikuwa utani, na labda kuna jambo fulani lilikuwa limetokea. Akanyanyuka haraka na kutoka nje ya nyumba, akimwacha Valentina anamshangaa. Akaenda mpaka kwenye gari lake upesi na kutoa simu yake, kukuta missed call 32; kutoka kwa mama yake na pacha wake. Akapiga mluzi wa mshangao, na hapo hapo Valentina akawa amefika nyuma yake.

"Xander nini kinaendelea?" Valentina akauliza.

"Sijui tu. Naombea isije ikawa nasubiriwa na mijeledi ya mzee huko hahah..." Xander akajaribu kutania.

"Mpigie Sandra. Muulize nini kinaendelea..."

Xander akatii. Akamwambia Valentina waingie ndani kwanza, na baada ya kufika sebuleni akampigia tena Sandra; zamu hii kwa simu yake mwenyewe. Ikapokelewa.

"Halloo..." Xander akasema.

"Sandra... uko wapi?" ikasikika sauti ya mama yake upande wa pili, akiwa anafikiri huyu ni Sandra.

"Mama... niko huku kwa..."

"Unawezaje kuondoka bila kusema unakoenda? Una matatizo gani wewe siku hizi? Unajua kwamba lolote baya linaweza kukupata? UKO WAPI?!" akauliza Alice kwa ukali.

"Mama punguza jazba... niko kwa rafiki yangu. Kwani shida gani mpaka unafoka hivyo wakati hii siyo mara yangu ya kwanza?" Sandra (Xander) akajitetea.

"Uliaga? Uliaga?" mama yake akauliza kwa ukali.

Xander akasikia sauti ya baba yake ikisema, "Basi Alice, inatosha. Sandra, uko wapi?" 

"Niko huku... mitaa siyo mbali sana na chuo..." akajibu.

"Kote huko umeenda kufanya nini? Oh God... Sandra... nisikilize kwa makini. Kuna watu wanataka kutudhuru, na wanaweza kuwa popote pale muda wowote ule. Nahitaji kuwapeleka kwenye usalama. Sandra unanielewa? Maisha yako yapo kwenye hatari! Nataka ufanye kile ambacho nitakwambia haraka sana..." baba yake akasema.

Xander akatulia kidogo, akiyatafakari maneno ya baba yake, kisha akajibu, "Ndiyo baba... nakusikiliza..."

"Unakumbuka nyumba ya babu yako Daudi ilipo? Kule tulipokuwaga tunawapeleka mkiwa wadogo kumtembelea?" Casmir akamwambia.

"Mjomba wako yule?"

"Ndiyo..."

"Yeah... napakumbuka. Lakini baba..."

"Nisikie. Nataka uje huko haraka sana. Ndiyo tunakoenda sasa hivi. Usiende nyumbani, na uhakikishe huongei na yeyote kuhusu hili. Sandra unanielewa dear? Harakisha mpenzi..." baba yake akaongea kwa hisia.

"Sawa baba. Nakuja..." 

Xander akamwambia akiwa amechukulia jambo hilo kwa uzito. Valentina akawa akimwangalia kwa umakini sana.

"Sawa," akasikika Casmir.

"Kuwa mwangalifu Sandra. Nakupenda," akaisikia sauti ya mama yake ikisema hivyo.

"Nakupenda pia mama..." akajibu.

Kisha simu ikakatwa. Xander akabaki ameachama mdomo wake tu akiwa anatafakari jambo hilo. Valentina aliona jinsi uso wake ulivyoonyesha amezama kwenye mawazo mengi.

"Xander, what's going on?" akamuuliza.

"Valentina... nahitaji unisaidie nguo. Aam... suruali nyepesi tu na T-shirt tafadhali, na sweta la ziada nahitaji... nahitaji... na viatu vyepesi..."

"Xander calm down. Niambie nini kinaendelea? Wazazi wako wamekwambia nini?" 

Valentina sasa alikuwa ameushika uso wa Sandra, yaani Xander akiwa kwa ndani, naye Xander akamshika shingoni kwa viganja vyake.

"Wameniambia nahitaji kuwahi. Kuna tatizo fulani... nahitaji kwenda sasa hivi..." Xander akamwambia.

"Tatizo gani? Niambie..."

"Please... just... nipatie nguo hizo. Nahitaji sana kuwahi..."

Valentina alishindwa kuelewa ni nini kilikuwa kinaendelea. Xander akamwachia na kuanza kuvua gauni alilovaa, hereni, viatu, na kuviweka pembeni. Valentina akaona tu aelekee chumbani kumfatia nguo zake ambazo zingemfaa, huku bado akiwa haelewi yanayoendelea. Akachukua na viatu vyake vyeupe vya raba na kumpelekea. Baada ya kumpa, Xander akiwa kwenye mwili wa Sandra akavaa haraka haraka sana, na uzuri ni kwamba viatu na nguo hizo zilimtoshea. 

Sasa akajihisi mwepesi, naye akamwambia Valentina kwamba alihitaji sana kuondoka ila wangeonana tena. 

"Unamaanisha nini? Unaenda wapi Xander?" 

Kijana akamsogelea tu madam wake karibu na kumpiga busu ya upendo, kisha akasema, "Nakupenda Valentina. Always remember that."

Maneno yake yalimshangaza sana mwanamke huyu. Xander akamwachia upesi na kuondoka hapo huku Valentina akimsindikiza kwa utizami uliojaa maswali mengi. 

Xander akawahi mpaka kwenye gari na kuliwasha, akiwa ameingiwa na msisimko mkubwa uliofanya atetemeke kutokana na hofu aliyohisi. Alikuwa anataka sana kumwambia Valentina kilichoendelea, lakini alijua kwamba baba yake alikuwa na maana fulani kusema asimwambie YEYOTE kuhusu hili. Hivyo aliwaza huenda ilikuwa ni kwa faida ya mpenzi wake kama asingejua, hata kama alimwacha njia panda. Aliitazama tena nyumba hiyo na kumwona Valentina akiwa amesimama getini pale, kisha akaligeuza gari na kuanza safari ya kuelekea kule alikoambiwa aende na baba yake.


★★


Xander aliendesha gari akijaribu kukumbuka kwa usahihi njia aliyopaswa kupitia ili kuweza kufika huko. Kichwani kwake alijiuliza vitu vingi sana; wangeenda wapi, wangefanya nini baada ya hapo, na hali hii ingekoma lini. Baada ya dakika kadhaa akiwa mwendoni, alifika kwenye barabara ya moja kwa moja isiyokuwa na njia nyingine ya mkato. Yaani ilinyooka moja kwa moja mbele bila kuwa na barabara yoyote iliyojitokeza kuelekea sehemu nyingine. 

Akafika sehemu fulani na kuona gari mbili kwa mbele zikionekana kuwa zimegongana, na hivyo barabara ikawa imezibwa. Akakaribia hapo zaidi na kuwaona watu watatu; mmoja akiwa amelala chini barabarani na mwingine akiwa ndani ya gari huku kichwa chake kikining'inia nje ya mlango wa gari. Wa tatu alikuwa akijivuta chini kuja upande wa Xander akionekana kuhitaji msaada. 

Ilionekana kuwa ajali mbaya sana, naye Xander akasimamisha gari akiwa amekosa njia ya kupita. Ni wakati huu ndipo simu yake ikaita, naye akaona ni baba yake ndiye anapiga. Akapokea na kumwambia kuwa alikuwa njiani, na baada ya hapo akakata. Akajiuliza afanye nini. Akiangalia na hali iliyokuwa inamwandama, isingekuwa rahisi kusema atoke akatoe msaada wakati na yeye maisha yake yalikuwa hatarini. Lakini hangeweza kumwangalia tu mtu huyo akiteseka, hivyo akafungua mlango na kutoka ndani ya gari. Aliwaza kwenda kumsaidia mtu huyo, labda kumweka kwenye gari ili ampeleke hospitali fulani huko mbele, kisha ndiyo angeelekea kwa wazazi wake. 

Akamfikia chini hapo na sasa akamwona vizuri zaidi. Alikuwa mwanaume mwenye umri na mwili mkubwa, aliyejaa damu tumboni na kichwani. Akamsikitikia sana.

"Kaka... pole... ni ajali... umeumia wapi?" akamuuliza.

"Aahh... nisaidie... tumegongana hapo... nipeleke hospital binti yangu..." mwanaume huyo akasema.

Xander akaanza kujaribu kumwinua.

"Na hao wengine?" akamuuliza.

"Hao wamekufa..." akajibu.

Akamnyanyua juu na kuanza kumsaidia kulielekea gari, lakini walipolifikia, mwanaume huyo akamzungukia nyuma na kumsukuma kwa nguvu sana, kitu kilichofanya aangukie kwenye gari. Kabla Xander hajageuka, akakazwa mikono yake kwa nyuma na kukandamizwa hapo, hivyo akashindwa kunyanyuka. Wasiwasi ulimwingia sana. Mwanaume huyo alikuwa na nguvu mno, na yeye Xander kuwa ndani ya mwili wa Sandra ilikuwa ni shida kwa sababu hangeweza kujinasua.

"Unafanya nini? Si umeumia wewe?" Xander akauliza kwa hofu.

"Tulia... Alexandra Casmir," mwanaume huyo akasema.

Xander akatulia akiwa ametambua kwamba mtu huyo alimfahamu, hivyo huo wote ulikuwa ni mtego! Akatambua sasa kwamba inaonekana hawa ndiyo watu wanaojaribu kuwaua, na yeye akawa ameingia kwenye mtego wao kiulaini. Akahisi mikono yake ikianza kufungwa kwa kamba nyuma yake, na hatua zingine zikasikika zikiwa zinakuja.

"Dah... yaani haya marangi yananuka!"

"Hahahah... nani asingeamini kwamba hiyo ni ajali?"

"Luteni, P bado anafikiri hatukupaswa kuweka show yote hiyo..."

"Why not? Napenda roleplaying," akasema mwanaume aliyemfunga Xander.

Kisha akamgeuza na kumbeba, halafu akamkalisha hapo juu ya gari. Xander akawa anamtazama kwa wasiwasi huku mwanaume huyo akiwa anajifuta rangi zilizoonekana kama damu usoni.

"Hujambo? Naitwa Weisiko. Kuanzia sasa mimi ndiyo babysitter wako. Samahani kuhusu hiyo show fake, ila... natumaini ume-enjoy. Nilitamani kuwa mwigizaji zamani wakati niko shule. Bado hiyo kitu haijanitoka ndo' maana nikaona tukuburudishe kidogo mtoto mzuri," Luteni Weisiko akamwambia.

"Weisiko? Luteni Weisiko? Wewe si unafanya kazi pamoja na baba?" Xander akauliza.

"Ouh... sauti nzuri sana. Kama tu sura yako... nilitaka kukwambia mara tu uliposema 'poulee,'" Weisiko akasema huku akiushika uso wa Sandra kwa wororo.

Wenzake wakacheka kidogo, huku Xander akihisi hasira sana kwa sababu hakupenda na hangetaka dada yake atendewe kwa njia ya dharau.

"Casmir ana vitu vingi vizuri. Yaani... hayuko kule juu sana ila alivyonavyo ni treasure sssafi kabisa. Namwonaga mke wake... mama yako... ule weupe... nami huwa natamani sana nimtie rungu siku moja. Lazima awe na maji matamu sana, eti?" Weisiko akasema kwa dharau.

"Fala wewe! Kanywe ya mama'ako," Xander akamwambia akiwa amekasirika.

Luteni Weisiko akamwasha kofi la nguvu usoni lililofanya Xander ahisi maumivu sana. Huu ulikuwa ni mwili wa dada yake ukipigwa. Weisiko akamkamata nywele zake kwa nyuma na kumsogeza karibu na uso wake akimwangalia kiukatili.

"Chunga mdomo wako msichana!" akamwambia.

"Na wewe chunga maisha yako bro. Ni bora uniue... cause I swear to God, nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe nikitoka hapa!" Xander akasema kwa ujasiri.

Luteni Weisiko akacheka na kumwachia. 

"Uko kama baba yako. Always kidevu juu. Lakini leo utajifunza kwamba maisha ni mafupi sana, kwa hiyo kama hukuwa umejitahidi kula ujana... basi tutakusaidia kula wako," Weisiko akasema, na wanajeshi wake wakacheka sana kwa dharau.

"Kama unafikiri nitakwambia wazazi wangu walipo, umeula wa chuya," Xander akasema kwa ujasiri.

"Oh sihitaji uniambie walipo, ninajua walipo. Nataka tu... kuhakikisha mnakuwa pamoja wakati wenu wa mwisho... hiyo si itakuwa vizuri?" akasema Weisiko.

"Umejuaje walipo?"

"Me mwenyewe nashangaa. Yaani Meja wa kikosi cha wanajeshi wa nchi anashindwa kutumia akili yake na mafunzo ya miaka mingi kukumbuka kwamba tunaweza ku-tap simu? Akili yake itakuwa mbali sana leo. But, hiyo kwetu ni jambo lenye faida kwa hiyo... asifiwe Meja..." Weisiko akamwambia kwa kejeli.

Xander akahuzunika sana.

"Usihuzunike mrembo. Angalau nakupeleka kuwa pamoja na familia yako kwa mara ya mwisho. Ningeamua kukuua hapa hapa ningefanya hivyo, maana hata huko familia yako walipo, watu wangu wameshawazingira. Kwa hiyo... bucker up... tuna safari ya kuanza," Weisiko akasema.

Kisha akamvuta kutoka hapo kwenye gari na kumwongoza kuelekea ndani yake. Akamwingiza siti za nyuma, na wale wanaume wengine wawili wakaingia na kukaa naye; yeye akiwa katikati. Mmoja wao alikuwa ameshika bastola mkononi ili "binti" asilete ujanja wowote, naye Luteni Weisiko akaingia sehemu ya kuendeshea na kuliondoa gari hapo haraka sana.

Njia nzima Xander aliwawaza sana watu wa familia yake. Hata akaanza kulia, huku wengine waliomo wakipiga story za mambo ambayo hayakueleweka kabisa kwake. Xander akahisi hii ilikuwa ni makosa yake kwa kuwa kama asingeondoka muda ule, basi labda mpaka sasa angekuwa pamoja na familia yake wakielekea sehemu nyingine salama zaidi. Weisiko alimsemesha mara kwa mara kumwambia kwamba asiogope mno kwa kuwa kifo cha kupigwa risasi ni rahisi kuliko kuchomwa moto. Xander alimchukia sana mwanaume huyo. Lakini hapa hakuwa na ujanja wowote ule wa kujitoa mikononi mwao.


★★


Walifika mpaka maeneo ya nyumba ile, lakini gari waliliegeshea mbali kidogo ili lisionwe na familia ya Casmir. Weisiko akamgeukia "Sandra" na kumwambia kwamba wangeenda pamoja mpaka pale, na hakupaswa kusema wala kufanya lolote ambalo lingemletea shida. Akamkumbusha kuwa kulikuwa na wenzake wameizingira nyumba hiyo kisiri, hivyo kama angeleta ujanja basi watu wa familia yake wangeuawa kabla hajawaona kwa mara ya mwisho. 

Kihalisi Weisiko alikuwa anamdanganya tu, kwa kuwa hapo ilikuwa ni yeye pamoja na wenzake wawili tu. Lakini Xander hakulijua hili, naye alifikiri ni kweli. Hivyo, wakatoka kwa pamoja, na wale wanaume wengine wawili wakatangulia ili kwenda kuizunguka nyumba, wakiwaacha Weisiko na "Sandra" wanatembea taratibu kuielekea pia. Walipokuwa wakiikaribia, Weisiko akamwambia kwamba alipaswa kufika pale na kuomba afunguliwe mlango, kisha mambo mengine yangefuata. 

Xander aliwaza sana afanye nini ili kuweza kuwaonya wapendwa wake kuhusu hatari hii bila kuwahatarisha. Ni wakati wakiwa wameikaribia nyumba zaidi pale alipokumbuka jambo fulani. Alikumbuka kwamba anaweza kuongea kwa kutumia akili, na dada yake angeweza kumsikia. Ijapokuwa hawakuwa karibu, akaona ajaribu tu ili kama kungekuwa na faida yoyote basi isaidie, maadamu ametafuta njia ya kutoa msaada. Akaanza kuita kwa kutumia akili, 'Sandra... Sandra... Sandra unanisikia?' Hakupata jibu lolote kichwani kwake, lakini akaendelea kujaribu tu. 

Walipoukaribia zaidi mlango, akasikia sauti ya dada yake kichwani kwake ikisema 'Xander... uko wapi?' Akataka ajibu, lakini ni hapa ndipo wakawa wamefika, naye Weisiko akamwekea bastola kichwani huku akijibanza ukutani, na kumwonyesha kwa ishara kuwa augonge mlango na kuwaambia wafungue. 

Xander akagonga mlango, kisha akaita, "Baba..." Akasema kichwani kwake hapo hapo 'Sandra, kuna hatari huku nje! Kuna hatari huku nje...' Akasikia sauti ya baba yake ikisema mlangoni hapo "Sandra!" huku nyingine ya dada yake kichwani ikisema 'Kuna hatari? Hauko mwenyewe? Xander...' 

Papo hapo mlango ukafunguliwa, naye Xander akasikia sauti "yake" ya juu kutokea ndani ikisema "Baba subiri!" Lakini akatambua kwamba onyo hilo lilitolewa kwa kuchelewa sana, kwa maana sasa akamwona baba yake, mama yake, na dada yake (akiwa kwenye mwili wake) ndani hapo, na wote walikuwa wanashangaa kwa hofu baada ya kumwona akiwa amewekewa bastola kichwani. Luteni Weisiko akatoka alipokuwa amejibanza na kuja nyuma yake Xander huku akiwa bado ameiweka bastola kichwani pake.

"Habari za wakati huu Meja..." Weisiko akamsalimu Casmir.

Wale wanaume wawili pia wakaja kutokea pembeni wakiwa wameelekeza bunduki zao kwa familia hiyo, kisha Weisiko akamkaba Sandra (Xander) kwa nyuma. 

"Luteni... usimuumize... naomba mwachie binti yangu!" akasema Casmir kwa hofu.

Alice akawa analia sana, naye Azra pamoja na Salome wakawa wameendelea kujificha kule ndani.

"Tokeni nje... wote," Luteni Weisiko akamwambia Casmir huku anarudi nyuma.

"Weisiko... mwachie binti yangu," Casmir akamwomba.

"Nje! Now!" Weisiko akafoka.

Casmir akaanza kutoka huku Alice na Xander (Sandra) wakiwa nyuma yake. 

"Tupa bastola hiyo Meja," Weisiko akamwambia.

Casmir akaitupa pembeni. Mmoja wa hao wanaume aliyekuwa upande huo akaiokota na kuitolea risasi zote, kisha akairusha mbali.

'I'm sorry Sandra... I'm sorry...' Xander akatumia akili kumwambia dada yake hivyo.

Sandra, akiwa ndani ya mwili wa kaka yake alikuwa analia sana na kutetemeka, kitu kilichofanya Weisiko aone ni kama kituko.

"Yaani we' libaba lizima unalia kama demu? Dada yako afanye nini sasa?" Luteni Weisiko akasema kwa kejeli.

Kutoka kichwani kwake Xander, akamsemesha dada yake, 'Sandra naomba unisikilize. Ninaweza kumzunguka huyu mjinga haraka na kumnyang'anya bastola kwa kumshtukiza. Nitakaposema 'now'... msukume huyo mwanaume mwingine kwa nguvu zako zote ndani ya mwili wangu... mwili wangu una nguvu sana. Umenielewa?'

'Me siwezi. Naogopa,' Sandra akajibu kwa akili pia.

"Mwache mtoto wangu tafadhali..." Alice akamwambia Weisiko huku akilia.

"Usijali mpenzi. Kila kitu kitakuwa sawa. Wengine wako wapi?" Weisiko akauliza.

Wote wakabaki kimya.

"Najua una warembo wengine humo ndani. Goko, tafadhali wafate wajiunge nasi..." Weisiko akasema.

Alice akaanza kulia zaidi akisema hapana. Goko huyo akawapita akiwa ameelekeza bunduki yake mbele na kuingia mpaka ndani.

'Sandra nisikilize. Siwezi kuvumilia kuona wanawaumiza. Nilifikiri wako wengi lakini ni wachache tu. Fanya navyokwambia... kwa ajili ya mama, na baba, na Azra... and for you...' Xander akaendelea kumsisitiza dada yake kichwani.

"Msiogope Meja. Kila jambo litakuwa rahisi ikiwa mtatupa ushirikiano mzuri kama Captain Kendrick alivyofanya... basi," Weisiko akasema.

"Umemuua Kendrick!" Casmir akasema kwa kuvunjika sana moyo.

Weisiko akamtazama kwa kiburi tu. Casmir akaangalia chini na kuanza kutikisa kichwa kwa njia ya kuonyesha ameelewa.

"Sasa ninaelewa. Ni nyie. Wewe na Kanali. Nyie ndiyo mliokuwa mnawapatia Demba Group silaha ili wafanye yale maovu. Na tena hata siyo group... ni baadhi ya wanajeshi mnaowatumia. Ahah... yote hayo kwa faida gani Luteni? Power? Nyie ni wakandamizaji. Kwa hiyo unataka kuniua kwa sababu niliyaona yale masanduku? Mnaogopa ningemwambia General si ndiyo?" Casmir akasema kwa hisia.

"Ni wajibu wangu Meja. Niko hapa kuutimiza. Nothing personal..." Luteni Weisiko akamwambia.

"Tumekukosea nini? Hata kama una ugomvi na mume wangu ndiyo uwaue na watoto wangu pia?" Alice akasema kwa huzuni.

"Oh no mrembo... sina ugomvi na yeyote. Lakini..."

Kabla Weisiko hajamaliza kuongea, wote wakasikia sauti ya Goko huko ndani akipiga kelele za maumivu. Wote walishtuka na kutazama huko isipokuwa Xander (akiwa ndani ya mwili wa Sandra), ambaye kwa kutumia akili akasema 'NOW!' kisha akatumia mguu wake kupiga sehemu za siri za Weisiko kwa nyuma. Ilikuwa ni baada tu ya Sandra (akiwa ndani ya mwili wa Xander) kusikia maneno hayo kichwani kwake naye pia akatenda kwa uharaka na kumrukia mwanaume yule mwingine pale pembeni, na wote wakaanguka chini.

Weisiko alihisi maumivu sana na kufanya mikono yake ilegee, hivyo Sandra (Xander) akawahi kujitoa mikononi mwake ili amnyang'anye bastola, lakini Weisiko alikuwa na nguvu sana hivyo akaweka kipingamizi kikali. Casmir pia akatenda kwa uharaka sana na kuwahi pale chini walipodondokea yule mwanaume na Xander (Sandra), kisha akaanza kupambana naye ili kumnyang'anya bunduki yake haraka. 

Kule ndani, wakati Goko ameingia muda ule kuwatafuta waliobaki ili awatoe nje, Salome na Azra walikuwa wamejiandaa kwa kushika mbao nene na kujibanza sehemu zenye giza. Kwa hiyo kelele ya Goko ya maumivu wote waliyoisikia ilikuwa ni baada ya Salome kumtandika Goko na ubao huo mnene shingoni kwa nyuma na kumfanya adondoke chini, kisha wasichana wote wakaendelea kumtandika kwa pamoja na mbao zao. Salome akamwambia Azra wawahi kutoka ili kunusuru maisha yao baada ya kumshushia kipondo hicho kizito na kumwacha akiwa hoi.

Hapo nje purukushani iliendelea, na sasa Casmir akawa anashindana nguvu na mwanaume yule aliyeangushwa na Xander (Sandra) kuchukua bunduki. Sandra akiwa ndani ya mwili wa kaka yake bado aliogopa sana, hivyo akawa anashangaa tu mambo yakiendelea namna hiyo. Alice aliweza kuona Luteni Weisiko akimkata Sandra (Xander) kwa kisu kidogo alichokuwa nacho kiunoni, kilichomchana sehemu ya tumboni na kufanya aangukie pembeni akiugulia maumivu, kisha Weisiko akaanza kuifata bastola yake akitambaa chini. Alice akavaa ujasiri na kuwahi pale kwa Weisiko ili kumzuia asiichukue bastola.

Ni wakati huu ndiyo Salome pamoja na Azra walitoka ndani mule na kukuta vurugu hilo hapo nje. Casmir alipowaona, akamwambia Xander (Sandra) amtoe dada yake na mdogo wake hapo na wakimbie haraka sana. Wakati Alice alipoanza kugombania ile bastola na Luteni Weisiko, mwanaume huyo aliweza kumshinda nguvu na kuielekezea tumboni kwake, kisha risasi ikafyatuka huku miili yao ikiwa imebanana. 

Risasi hii ilimtoboa Alice mpaka mgongoni, na wote waliosikia mlio wake wakatazama upande huo kuona damu zikimtoka mgongoni!

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Previoua Next