Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA KUMI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★


Kwa kuona sijatoa jibu lolote kwa salamu aliyonipa, Joshua akatabasamu kidogo na kuinamisha uso, kitakatifu eti, kisha akanipita na kuingia ndani humo. Alitoa 'vibe' za 'bad guy' kama kwenye filamu za wazungu, nami sikuweza kujizuia kutaka kujua ni jambo gani alilokuwa amelileta mezani kwa bibie Miryam. Ama labda ni Miryam ndiyo alikuwa amemwita? Nisingeweza kujua, na mtu yeyote angeweza kuniambia sikupaswa kujua maana haikunihusu. Au uwongo? Lakini nisingeweza kupuuzia uwezekano wa mwanaume huyo kufanya jambo lingine la kipuuzi kwa sehemu hii, kwa hiyo nikataka kuhakikisha. Nikatoka sehemu hiyo ya mlango wa ofisini na kuifikia meza ya msaidizi, nami nikapokewa kwa tabasamu mwanana na mwanamke mrembo Soraya.

"Vipi?" nikamuuliza hivyo nikiwa nimesimama karibu na meza hiyo.

"Safi. Naona mmemaliza maongezi yenu," akasema hivyo.

"Ndiyo. Bosi wako mtata kweli."

"Ahahah... labda ukimchokonoa, ila ni mstaarabu sana..."

"Eti eh? Na huyu jamaa aliyeingia sa'hivi? Unamjua?" nikamuuliza hivyo.

"Eee, ni ndugu yake. Kaka yake sijui... sina uhakika sana, ila najua ni ndugu yake," akanijibu.

"Aaa, kwa hiyo hatamchokonoa boss eh?"

"Ahahah... sidhani. Amekuja kiupole, sioni kama kutakuwa na baya."

"Alipanga mapema kuja leo?"

"Yeah, da' Miryam aliniambia angekuja. Ndiyo alipofika nikamwambia asubiri kwanza maana mgeni bado ulikuwa ndani," akaniambia hivyo.

"Au siyo? Ukanipa heshima yangu mtoto.." nikamwambia hivyo, naye akacheka kidogo.

Kwa kujua sasa kwamba ni Miryam ndiye aliyemwita huyo jamaa hapo, nikaona labda mambo yasingeenda vibaya. Alikuwa na maana yake.

Nikamwambia Soraya, "Haya bana.  Me ndo' natoka. Ushagakataa kuja kututembelea."

"Aam... nitakuja tu. Mambo mengi, si unajua? Kama hivi..."

"Wala hamna presha, usijali. Sema naona unapendezea sana kubadili mazingira, maana unakaa sana hapa. Huwa hata unatembea?" nikamuuliza hivyo.

Akatikisa kichwa kidogo kukataa.

"Kweli? We' ni wa kitako tu na hicho kiti?" nikauliza tena.

Akacheka na kusema, "Kawaida tu. Majukumu. Nikitoka hapa... ni kuwahi nyumbani. Nitatembea saa ngapi?"

"Wikiendi je?"

"Hata Jumapili nakuwa zangu ndani. Sizururagi mimi. Ijumaa hapa naenda zangu msikitini saa sita, da' Miryam ananiachia niende nyumbani. Sinaga mipango mingi ya kutoka wala labda iwe na ulazima kwa hiyo... ndiyo hivyo," akaniambia hayo.

Nikawa namwangalia tu usoni huku nikitabasamu kimchezo, naye akacheka kidogo kwa pumzi na kuung'ata mdomo wake wa chini.

"Mbona unaniangalia hivyo?" akaniuliza.

"Kwani we' umenionea nini?" nikamuuliza.

"Unaniangalia kama unanijaji. Unafikiri nakudanganya au?"

"Macho yangu hayajasema hivyo, we' ndo' umeyajaji vibaya..."

"Kumbe? Yanasemaje kwani?"

"Yanasema kama vipi baadaye nikutoe out... ila we' usiyependa kuzurura najua hautaweza," nikamwambia hivyo.

"Mhm... unaongea wewe..."

"Ahahah... bado hujanisikia nikiongea. Utachoka..."

Akaniangalia kwa macho mazuri, naye akasema, "Kwa hiyo unataka kunitoa out?"

"Ee fresh tu, kama ukitaka," nikamwambia.

"Me muda sina JC."

"Kwani unatoka saa ngapi?"

"Saa kumi na moja."

"Na uliniambia unakaa Sabasaba?"

Akatikisa kichwa kukubali.

"Asa' si hapo tu? We' ukitoka, nambie, tukutane, tule hata mishkaki, uende home. Ndo' urafiki huo, siyo kwenye simu tu," nikamwambia.

"Mmm?"

"Eeeh."

"Na nikichelewa?"

"Kwani... ahah... we' ni mtoto? Au mume mkali?" 

"Hapana... me..." akababaisha jibu.

"Usijing'ate Soraah. We' ukimaliza tu nicheki..." nikapigilia msumari ndani zaidi kwenye ushawishi.

Nadhani alielewa vizuri kabisa kwamba nilikuwa namwonyesha kuvutiwa naye ingawa sikwenda huko moja kwa moja, na yeye pia akafanya ionekane kwamba hakufikiria huko.

Akasema, "Sawa. Nikiwahi, n'takwambia. Mishkaki si unaninunulia?"

"Usiwaze. Hayo ndiyo mambo sasa. Unamaliza kazi, unabembea kidogo na rafiki, ndiyo unaingia makwenu, au siyo?"

"Mh... kubembea tena?" 

"Ahahahah... uko innocent sana, hadi raha. Me ngoja niwahi, naingia Kariakoo sa'hivi. Ukinijali utani-text. Usiponi-text, basi ndo' ntaila mishikaki mwenyewe," nikamwambia hivyo kiutani.

Akacheka kidogo na kusema, "Haya bwana. Unaenda Kariakoo kufanya nini?"

"Naenda kuchukua nguo fulani, afu' nageuka."

"Sawa."

"Haya, baadaye beauty Soraah," nikamuaga kiaina hiyo.

Akatabasamu na kutikisa kichwa kidogo, nami nikampita na kwenda nje. Huyu mwanamke nilitaka kuhakikisha napita naye, maana alionekana kuficha utamu fulani hivi ndani ya huo upole wake mwingi aliokuwa nao. Haikujalisha suala la yeye kuwa ameolewa, maana mpaka kufikia wakati huu bado nilikuwa kwenye zile nyendo za kuharibu mitambo niliyoielewa hata kama ilikuwa imeshaunganishwa kwenye nyumba za wengine. Na Soraya alikuwa mtambo material. Sikujua sana ikiwa angeridhia kufika na mimi kule ambako ningetaka tufike, lakini kama angekataa wala nisingemlazimisha. Ila nilimtamani sana. 

Kwa hiyo nikajiondokea pande za Kijichi baada ya hayo, nami nikachukua daladala zilizoelekea Kariakoo. Nilikuwa nikifikiria mambo mengi kuhusiana na vitu nilivyotakiwa kufanya ili kuanza kumpatia Mariam msaada wa kisaikolojia ambao ungefaana na hali aliyokuwa nayo. Sikubobea sana kwenye masuala ya saikolojia wala magonjwa ya akili, lakini nilijua mengi kuhusu hali iliyomwandama, na utundu wangu ungesaidia niweze kucheza na akili yake vyema mpaka ikae sawa tena. Nilipofika Karikoo, nilizunguka pande tofauti, nikaingia kwenye duka moja lenye kuuza bidhaa kama nguo, suruali, viatu, na kununua T-shirt zuri sana la mikono mirefu, pamoja na ndala nzuri zenye rangi mchanganyiko. Nilipenda mionekano mizuri sana kimavazi, na kutumia hela niliyokuwa nayo kwenye mavazi lilikuwa jambo la kawaida sana kwangu. 

Baada ya kutoka hapo, nikaelekea kwenye mgahawa mzuri wa kisasa ili kupata chakula. Nikawa nimemjulisha Ankia kuwa asinitinzie chakula cha mchana maana ningechelewa kurudi na hivyo kula huku huku nilikokuwa. Nilikaa kivyangu tu huku nikiendelea kula na kuchat na marafiki kwenye simu, kisha nikaondoka hapo baada ya kushiba. Nikaenda sehemu zingine pande hizo za Kariakoo na kununua kinanda kidogo kwenye duka la vifaa vya ala za muziki, chenye vibonyezeo vilivyowekewa sauti ambazo zimesharekodiwa. Yaani, ukibonyeza kimoja kinatoa mlio (instrumental) wa twinkle twinkle star, ama mlio wa happy birthday, kwa midundo ya kinanda. Kilikuwa kizuri sana, na lengo la kukinunua lilikuwa kwa ajili ya Mariam. 


★★


Nikatoka huko Kariakoo ikiwa inaingia mida ya saa kumi jioni sasa, kwa mwendo wa taratibu wa daladala, na aisee! Nilikoma kupanda hizi daladala za kutokea Gerezani mpaka Kisemvule. Yaani watu wanabanana mpaka unakosa pozi na pumzi, hasa ukiwa umesimama kama mie ilivyokuwa wakati huu. Pigia picha ingekuwaje wakati wa usiku ikiwa tu gari liliweza kushonana namna hiyo kukiwa jioni ya mapema, na niliombea asitokee mtu wa kujamba la sivyo ningezimia! Lengo lilikuwa kuwahi nyumbani, niweke mizigo, kisha niangalie utaratibu unaofaa ili nikamjali mamacita Soraya. Hakuwa amenipotea akilini hata kidogo. Yule alikuwa wa ukweli. Lakini msongamano wa magari ukafanya dakika za kukawizwa barabarani ziwe nyingi hasa kuanzia maeneo ya Uhasibu, mpaka inaingia saa kumi na moja bado tukawa tunaisaka Sabasaba. Sijui shida ilikuwa nini. Hivyo hivyo mdogo mdogo tukaendelea kusogea, nami nikapata ujumbe kutoka kwa Soraya. 

'Ndo natoka.'

Agh! Siyo lazima mpaka mtu awe amesoma sana ili kuelewa kwamba mtoto alikuwa anataka kuelekezewa fikira, na zangu kwa wakati huu zilikuwa kwake kweli, kwa hiyo ningejitahidi nisimvunje moyo. Nikamjulisha nilikuwa maeneo ya karibu na Rangi Tatu, naye akasema tayari yuko kwenye bajaji kuelekea huko pia. Duh! Hapa isingewezekana kwenda kwanza kule nilikokaa na kurudi tena, kwa hiyo ingebidi nikutane naye nikiwa na mifuko ya bidhaa nilizonunua. Kwa kuwa ilionekana yeye ndiye ambaye angewahi kabla yangu, nikamwambia akishuka eneo la Zakhem basi aende kwenye mgahawa wowote wa karibu hata pale pale Zakhem Hotel, ndiyo sehemu ambayo tungekutana maana bado nami nilikuwa kwenye gari. Akanikumbusha kuhusu kupaswa kuwahi, nami nikamwambia asiwaze.

Dakika chache kupita nasi tukawa tumefika Rangi Tatu. Ile nimeanza kutembea tu kuelekea Zakhem Soraya akanipigia, 'wewe uko waapi' na kasauti kake ka upole, nami nikamwambia niko karibu. Nikajitahidi kutembea haraka kiasi mpaka nilipofika eneo la mgahawa wa Zakhem na kumpigia kumuuliza yuko upande gani. Akaniambia ameniona na ananifata, nami kweli nikamwona akija kutokea kwenye duka dogo la bidhaa upande wa nyuma niliouvuka kabla ya kuufikia mgahawa huu maridadi. Nikakata simu. Alikuwa anakuja kwa mwendo wa taratibu tu, gauni lake laini na refu mpaka chini likipeperuka kiasi kwa upepo uliopuliza kwa nguvu, na uso wake uliochorwa duara la ushungi aliovaa ukimpa mwonekano mzuri sana. Hii ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kumtazama vizuri akiwa amesimama, kwa hiyo nilipendezwa hata zaidi na mwonekano wake. Akanifikia karibu zaidi, naye akatabasamu kiasi huku mimi nikimwangalia kwa umakini. 

"Nimechelewa sana?" nikamuuliza.

Akatikisa kichwa kidogo kukanusha.

"Twende sa' hata ukanywe soda na mishikaki kidogo," nikamwambia hivyo.

"Hapana... JC... nitachelewa," akasema.

"Utachelewa wapi? Saa kumi na mbili hii kweli?"

"Saa moja tu natakiwa niwe nimeshafika nyumbani. Nahitaji kuwapikia wanangu."

"Sawa. Basi... angalau nipe tu hata kimoja Soraah," nikamwambia hivyo.

Akakunja uso wake kimaswali na kuuliza, "Kimoja?"

"Ee, fasta tu," nikamwambia.

"Sijakuelewa JC..."

"Nataka nisafishe chumba na wewe," nikasema hivyo.

"Ku... kusafishaje? Kusafisha chumba?"

"Acha kujitoa akili, najua unanielewa bwana."

"Eh... ahah... eheh... makubwa jamani..."

"Nini sasa?"

"Wewe... sasa... si nilikwambia nimeolewa?"

"Ndiyo, najua. Ila me nakuelewa, na we' najua unanielewa."

"Mm... me hapana... siwezi... dini yangu hairuhusu..."

"Hairuhusu nini? Mbona mwenzako anaruhusiwa kuwa na wanawake mpaka wanne? Huoni siyo fair?"

"Ye' ni mwanaume... ndiyo imeshaandikwa hivyo..."

"Hakuna kitu, huo ni uonevu bwana. Ona... najua unataka kuwahi, kwa hiyo... nipe tu kidogo maana... nakuhamu sana Soraah..." nikamwambia hivyo huku namwangalia kwa macho yenye ushawishi.

"Eh... hamna... natakiwa kuwahi, kwanza me siwezi... maana..." 

Akawa anajizungusha kimaneno sana, akiongea kwa namna yake ya upole lakini nikiona wazi kwamba alitaka nimbembeleze zaidi, ila kama nilivyokuwa nimesema mwanzo, ikiwa asingeridhia, nisingemlazimisha.

Nikamwambia, "Basi poa. Haina shida. Twende hivi ukapande gari uende nyumbani."

Akabaki kunitazama kama vile hakuwa amenisikia.

"Vipi?" nikamuuliza.

"Umekasirika?" akaniuliza pia.

"Sijakasirika. Si umesema unataka kuwahi? Twende ukapande gari uende."

Akaangalia chini kiasi kwa huzuni.

"Nini, mbona unakuwa hivyo?" nikamuuliza.

"Usichukulie vibaya JC, me..."

"Sijachukulia vibaya, Soraya. Si una haraka, majukumu? Ndiyo nakwambia haina shida. Nenda uwahi," nikasema hivyo.

"Sa' mbona kama umechukia?"

"Sijach.... okay. Nimehisi vibaya, lakini nitafanyaje? Una mambo muhimu ya kufanya pia. Kayafanye."

"Siyo hivyo tu, najua umechukia kwa sababu nimekukatalia. Usichukie JC," akaongea kwa kubembeleza.

Nikamwambia, "Hapana, we' usiwaze. Twende ukachukue tu usafiri na me niende home. Nitapambana na hali yangu."

Akawa ananiangalia kama anataka kulia eti, kisha anaangalia pembeni, mara huku, mara kule, nami nikawa nimeshachoshwa na presha ya kutazamwa sana na watu kwenye eneo hilo.

"Soraah twende. Au vipi?" nikamuuliza hivyo kwa sauti makini.

Akaniangalia na kuuliza, "Kwani ulikuwa unataka twende wapi?"

Ohohoo! Pasi ndefu kuelekea goli la ushindi!

Sikutoa jibu. Nikaushika mkono wake na kuelekea naye kwenye jengo refu la hoteli iliyokuwa karibu na hapo, nisijali hata kuangalia jina wala nini. Nilikuwa namvuta Soraya kama vile natembea na mtoto, nami nikaiona sehemu ya mapokezi na kwenda kuzungumza na mhudumu. Huku Soraya akiwa amesimama nyuma yangu, nikauliza gharama ya vyumba vya kulala wageni sehemu hiyo, nami nikajulishwa kuwa kuna vyumba vya shilingi elfu thelathini mpaka elfu themanini kwa siku. Nikatoa elfu thelathini chap kulipia kimoja, na huyo mhudumu akaniongoza mimi na Soraya kuelekea kwenye vyumba. Eh, huyu mwanamke alikuwa na aibu! Kwa wengi mambo ya hivi ni kawaida lakini kwake yeye haikuwa hivyo, maana alitembea kwa kuficha uso wake utadhani dunia nzima ilikuwa inamwangalia yeye. 

Huyo mhudumu akatufikisha kwenye chumba kimoja kwenye ghorofa ya pili, nasi tukaingia ndani. Kilikuwa na mwonekano mzuri, safi sana. Kitanda kilikuwa kipana na kirefu, kilichotandikwa shuka jeupe na kuwekewa mito, huku juu kukiwa na neti. TV ya flat screen ukutani, meza yenye droo kadhaa na viti vya kukalia, kabati la ukutani la nguo, mlango ulioelekea kwenye bafu na choo safi, pamoja na taulo mbili zilizokunjwa na kuwekwa kitandani pia, mapazia marefu yaliyofunika madirisha makubwa, vyote vilikuwemo. Huyo mhudumu akatuacha mimi na mali safi humo ndani, nami nikafunga mlango kwa funguo baada ya kuiweka mifuko yangu mezani. Soraya alikuwa amesimama usawa wa kitanda akionekana kutafakari vitu, nami nikaona nisimcheleweshe. Nikaja nyuma yake na kukibana kiuno chake kwa mikono yangu, huku nikibusu shavu lake usoni kutokea nyuma, lakini akashtuka na kujitoa kwangu, naye akakaa kitandani. Alionekana kuogopa.

"Vipi Soraah?"

"Me... bado naona kama tumepeleka mambo haraka sana," akaniambia.

"Bado hata hatujaanza!" nikamwambia. 

"Simaanishi hivyo..."

"Nakuelewa. Ndiyo maana hii ya mwanzo nimetaka tuifanye chap tu, maana una haraka. Ama?"

"Me bado naogopa jC..."

"Unaogopa nini? We' si mkubwa kwangu? Unaogopa nini sasa?"

"Sijawahi ku-cheat."

"Ndo' ujifunze," nikamwambia hivyo.

Akaniangalia kimkazo na kucheka kwa kuguna.

"Usiwe hivi bwana... muda unaenda..."

Nikamwambia hivyo na kumsogelea, nami nikapiga magoti chini katikati ya miguu yake iliyofichwa kwa gauni na kuushika uso wake, nikitaka kumbusu, lakini akawa ameinamisha tu uso wake.

"Soraah, ni nini?" nikamuuliza.

Akabaki kimya.

"Unaumwa? Uko P?" nikauliza tena.

Akatikisa kichwa kukataa.

"Nini sasa? Tutumie muda vizuri basi, saa moja itakukuta bado unajing'ata... eleweka..."

Akaniangalia kwa macho yaliyojaa hisia nzito sana, na hivi yalikuwa lege, nami nikaifata midomo yake na kuanza kumbusu. Busu nzito sana na taratibu ili nimhemshe vilivyo, nami nikashika upande mmoja wa kifua chake uliofichwa kwa nguo. Akaushika mkono wangu na kuutoa kifuani kwake, lakini nikalazimisha kuminya-minya hapo, naye akautoa tena na kukatisha busu yetu. Nikamwangalia na kuona namna alivyokuwa anajishauri bado, na kiukweli hii sitaki-nataka ilikuwa inaniboa sana, basi tu. Nikakishika kidevu chake ili nimtazamishe kwangu, naye akaniangalia machoni kwa hisia za woga-woga tu, kitu ambacho kilifanya nihisi stimu inanitoka. 

Agh, nikamwachia na kusimama, kisha nikakaa kitandani pia na kutazama pembeni nikiwa nimeudhika. Niliweza kuona uso wake ukiniangalia mara kwa mara japo sikumtazama kabisa, nami nikaangalia saa mkononi na kukuta ni saa kumi na mbili na dakika arobaini na kitu. Hapo nikaona ni kazi bure tu kulipia elfu thelathini yote halafu mwanamke mwenyewe akawa analeta swaga za kishamba, wakati nilikuwa namkubali mno.

"JC..." akaniiita kwa sauti ya chini.

Nikamwangalia, nikiwa na uso makini.

"Umekasirika?" akaniuliza hivyo.

Nikamkazia macho tu, kisha nikatazama pembeni tena.

"Hautaki kunijibu?"

"Nikujibu nini? Unataka nifanye nini sasa? Maana sikuelewi..."

"Mmh... JC... mimi... siyo kwamba nafanya makusudi, ila... nina aibu..."

"Agh..." nikafanya hivyo na kupiga ulimi mdomoni.

"Mbona unafanya hivyo?"

"Unazingua, Soraah. Unasema una haraka, me nimekujali nikakwambia tupige mambo fasta, bado unajivuta. Asa' muda si umeshakata?" nikamwambia hivyo kwa kuudhika.

"Siyo hivyo... sijazoea tu..."

"Haya nenda," nikamkatisha.

"Bee?"

"NE-NDA! Wahi nyumbani," nikamwambia hivyo kwa mkazo.

Akabaki kunitazama kwa huzuni.

Nikasimama na kwenda kuufungua mlango kwa funguo, naye akasimama pia. Nikarudi sehemu ile yenye meza ili niichukue mifuko, naye akaja nyuma yangu.

"JC... usikasirike..." akawa ananiomba hivyo.

"Ishaisha hii. We' chukua mkoba wako, tuondoke," nikamwambia hivyo.

Nikaichukua mifuko yangu nikiwa nimeudhika kweli, lakini akaikwapua kutoka mikononi mwangu na kuiweka mezani tena, akiniangalia kama vile anataka kulia.

"Soraah mbona sikuelewi? Unataka nini sasa?" nikamuuliza.

"Mm... nakutaka weewe..." akasema hivyo kwa sauti yenye upole.

Nikabaki kumtazama usoni kwa umakini.

"Ila... ninaogopa tu JC. Sijawahi kufanya kitu kama hiki... sija... nakuogopa yaani... unanifanya nasisimka sana mpaka... mpaka naogopa... sijawahi kuwa na mwanaume mzuri kama wewe... yaani...."

Nilimwangalia kwa njia ya uelewa sasa, nikianza kumwona kama Ankia tu. Ila yeye hakuwa mzoefu, kwa hiyo sasa nisingejali tena masuala ya muda; hapa ningetakiwa nimnyooshe ili na yeye ajue kwamba tupo kwenye karne ya 21, baby!

Nikamshika usoni kwa viganja vyangu, nikiyakandamiza mashavu yake na kumsogelea karibu zaidi, nami nikamuuliza, "Haujafanya vitu vingi eh?"

Akatikisa kichwa kukubali.

"Sawa. Nilifikiri ni mashauzi tu. Nisamehe kwa kuudhika," nikamwambia hivyo kwa upole.

Nikahisi mikono yake ikikishika kiuno changu na makucha yake yakinichoma kiasi.

"We' ni mwanamke mstaarabu, naona hilo sasa. Ila kama unanitaka kweli... jiachie. Mimi ndo' najaza nafasi zilizoachwa wazi... we' ziache tu ziwe wazi. Sijui umenisoma?" nikamuuliza hivyo.

Akatikisa kichwa kukubali.

Aloo! Midomo yake ilikuwa imelainika kwa mate, uso wake mweupe ukionyesha hamu nzito kunielekea, nami nikaanza tena kumbusu na kumwongezea pigo za wazungu zile. Huyu alikuwa wa aina ya kutulia na kulala tu huku amefunika uso kwa mkono, kwa sababu alikuwa mpole mno na mwenye aibu. Hakuwa na mambo mengi ya ajabu, bali akajiachia tu kwangu na kufurahia kitulizo alichoonekana kukihitaji kutoka kwangu. Nikamwacha na kwenda kuwasha taa, ikiwa imeshaingia saa moja usiku, kisha nikamrudia tena. Alikuwa ameshakolezwa utamu asiambilike chochote yaani, na kiukweli nilimfurahia mno. Nilijihisi vizuri sana. Joto lililokuwa limepanda ndani yangu lilisisimua mno nilipolishusha namna hiyo kwa huyu mwanamke. Nilikuwa nimeamua kuwahisha mambo ili kweli dada wa watu awahi nyumbani, lakini si utamu ukawa umemkolea? 

Nikamwambia, "Soraah... saa moja ishaingia. Jisafishe uende."

"Mmm... bado..."

"Bado nini?"

"Mmm..."

"Unataka tuendelee?"

Akatikisa kichwa kukubali bila kuniangalia.

"Asa' si utachelewa?"

"Ah... bwanaa..." akaongea hivyo kwa deko.

Nikatabasamu kidogo na kutikisa kichwa, kisha nikamvuta tena. Zamu hii nikaanza shambulizi lenyewe yaani, nikamfumua bila kumpumzisha. Alikuwa analia huyo! 

Nikaendelea tu kumtandika huku nikimsemesha. "Utamu umekukolea, si utafika nyumbani vibaya?"

Akawa akiguna tu.

"Wewe... si ulikuwa unakataa-kataa, unaogopa muda... unaogopa kuchelewa?"

"Mmm... sikujuaa..." hatimaye akaongea.

"Hukujua nini?"

"Sikujuaa... sikujua kama we' ni mtamu hivi..."

"Ahahah... wanao si watalala njaa sasa?"

"Mmm...."

Mwanamke bwana akawa anaonyesha raha tu na malalamiko yake, na hatimaye hiyo sikujua yake ikashika hatamu. Akapasua bomba kwa mara ya tatu huku akishtuka kwa nguvu kama vile mwili mzima umepatwa na kwikwi, nami ndiyo nikamtulizia hapo. Akalala hoi kitandani, huku akijing'ata mdomo na kupumua kilegevu, nami nikamgeuza alale chali ili nichezee mwili wake. Alikuwa anarembua hatari, nami nikampiga kofi laini shavuni.

"Wewe... amka... amka tuondoke. Saa mbili sa'hivi," nikamwambia. 

Akawa ananiangalia kilegevu tu.

"Soraah... sitaki kuja kusikia umepigwa huko, maana mna ratiba zenu. Nyanyuka twende," nikamwambia hivyo.

Nikataka kunyanyuka, lakini akanishika mkononi na kunivuta kwake tena, asitake kuniachia. 

"Nini?" nikamuuliza.

"Tukae kidogo..." akasema hivyo.

Nikatabasamu na kuuliza, "Na nyumbani?"

"Mmh... nitaenda baadaye... nimechoka..."

"Aa wee... unataka wanao walale njaa? Saa mbili sa'hivi, kwanza ulikuwa unaenda kupika nini?"

"Ubwabwa."

"Ndo' unyanyuke sasa, washaanza kulia njaa..."

"Ah... me nitasema kulikuwa na foleni... baba yao atawanunulia chakula..." akaongea kwa deko.

Unaona? Hawa viumbe wakishagalishwa vitu vitamu ndiyo wanakumbuka kwamba kuna kitu kinaitwa kudanganya. Si muda ule alikuwa anapiga kelele eti ooh nitachelewa, sasa hivi kiko wapi? Nikacheka tu kidogo na kuushika uso wake taratibu.

"Siyo vizuri hivyo unajua?" nikamwambia.

"Me nataka tukae kidogo..."

"Kwa nini?"

Akanishika shingoni na kusema, "Bado nawashwa."

"Ahahahah... sa'hivi aibu imekutoka eh?"

Akatikisa kichwa kukubali.

"Usijali. Nitakukuna tu. Ila sa'hivi muda unatupinga. We' vaa na me nivae twende. Tutapanga siku nyingine tukutane. Si umeshanizoea sasa hivi?" nikamwambia hayo.

Akatikisa kichwa kukubali.

"Fresh. Fanya hivyo," nikamwambia.

Nikapeana naye busu tamu, kisha nikajitoa kitandani hapo. Nikavaa, nikamsaidia mwanamke avae pia, na ingawa alionekana kutaka tuendelee kweli lakini nikasisitiza kumwambia muda kwa leo haungeruhusu, na tungepanga wakati mwingine tukipata nafasi nije kumoa mapenzi zaidi hata ya leo, naye akaonekana kufurahi. Nikafungua droo moja kwenye ile meza na kutoa chanuo, nikachana nywele na kujiweka vizuri, na yeye pia akajiweka vizuri mwilini kwa kujipulizia manukato yake ili asifike nyumbani ananukia mimi. Uzuri hakuwa ameutoa ushungi wake pindi nzima ya mechi yetu, kwa hiyo tukabeba vilago vyetu na kuondoka. 

Tukaingia tena barabara ya Zakhem kuelekea Rangi Tatu pale, tukitembea taratibu tu huku nikiwa nimemtangulia mamaa. Tulipoufikia mgahawa wa Zakhem, nikamwambia twende hapo, nami nikaenda kununua nyama za kuku pamoja na mishikaki, kisha ikafungwa nasi tukaanza kurudi barabarani. Mpaka kufikia muda huu, Soraya hakuwa ametafutwa na mume wake, kwa hiyo yeye akawa amemtafuta na kusema alikuwa amepatwa na dharura lakini ndiyo alikuwa njiani kurudi nyumbani. Dhambi hizi! Hivyo vyakula nikawa nimempatia mwanamke ili avipeleke kwa watoto huko kwake kama zawadi ya upendo, na niliona wazi kwamba Soraya alifurahia sana. Tukaachana kwenye mazingira mazuri baada ya kuhakikisha amepanda gari la kwenda huko kwake, nami pia nikapanda la kuelekea Mzinga. Mission ikawa accomplished!


★★


Nikafika nyumbani kwake Ankia hatimaye na kumkuta mwanamke huyo akiwa amekaa sebuleni pamoja na mama Chande, na kulikuwa na mvulana mdogo hapo pia wa miaka kama 10 hivi. Kwa haraka nilitambua kwamba mvulana huyo alikuwa mtoto wa mama Chande, labda ndiyo Chande mwenyewe, na nilipowapa wanawake hao salamu za wakati huu wa usiku, waliziitikia huku wakiniangalia kwa njia iliyoniambia kwamba kulikuwa na tatizo. Nikaona nipite tu kwanza na kuelekea chumbani kuiweka mizigo, nikiwa nadhani labda walikuwa tu na ishu zao zisizonihusu hata kidogo, na baada ya kutoa mavazi yangu, nikavaa nguo nyepesi ili niende kuoga. Si unajua joto la mwili lingekuwa juu baada ya mechi niliyocheza na Soraya? 

Kwa hiyo nikatoka chumbani ili nielekee bafuni, lakini nilipofika hapo sebuleni tena, nikakuta Ankia akiwa ameinamisha uso wake, viganja akiviunganishia usoni, huku machozi yakionekana kumtoka. Hali hiyo ikanitatiza sana. Mama Chande alikuwa ananiangalia kwa macho yenye subira, bila shaka akitaka nijue nini kilichokuwa kinaendelea hapo, nami nikasimama karibu na sofa alilokalia yule mvulana mdogo huku nikimwangalia mama Chande pia.

"Vipi? Mbona huyu analia?" nikamuuliza hivyo mama Chande.

"Eh... kaka... ni makubwa yametokea. Kuna msiba," akasema hivyo.

Kauli hiyo ikanifanya nimwangalie Ankia, nikiwa nimehisi labda msiba huo ulikuwa wa mtu wa karibu zaidi na mwenye nyumba wangu. Lakini kabla hata sijauliza nani kafa, mama Chande akanipa jibu, na ni jibu ambalo sikuwa nimetegemea kabisa!

"Haujasikia kumbe?" akaniuliza hivyo.

Nikatikisa kichwa kukanusha. 

"Joy amefariki," akaniambia.

Nilihisi kama vile pozi lilinitoka kabisa baada ya kusikia maneno hayo, lakini nikaendelea tu kumwangalia mwanamke huyo kwa utulivu.

"Unamfahamu Joy, si ndiyo? Amefariki. Tena... ameuawa," mama Chande akasema hivyo.

Eh! 

Nikabaki nimesimama hapo hapo bila kusema lolote, nami nikatazama pembeni nikiwa najaribu kuisawazisha vyema taarifa hiyo kichwani kwangu. Ingepaswa kuwa kitu chenye kushtua mno, na kilinishtua, lakini mshtuko nilioupata ulitokana haswa na fikira za ni nini ambacho kilikuwa kimesababisha mwanamke huyo afe ghafla. Tena kujua kwamba alikuwa ameuawa ndiyo kuliongezea fikira hizo ukali wa moto wake, kwa sababu tayari ningeweza kukisia ni nani aliyekuwa msababishi. Aisee! Kumbe mambo yalikuwa tata namna hii? Aliyefanya hivyo alikuwa anataka kuonyesha hatanii, na nilimjua vizuri sana. Sasa kutokea hapa huu mchezo ungeelekea wapi? 

 

★★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Previoua Next