Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA ISHIRINI

★★★★★★★★★★★★★


Joshua alikuwa amefika hapo pamoja na mwanamke mwenye mwonekano wa umri usio mbali sana na wa Ankia, mweusi wa maji ya kunde, mrefu kiasi cha kumfikia Joshua, naye alikuwa amevaa gauni la kijani lililoubana mwili wake na kuishia magotini. 

Alikuwa na mwili ule wa umenawiri-haujanawiri hivi, kawaida tu yaani, lakini alikuwa na hips nene zilizoonyesha alikuwa na ujazo wa kutosha huko nyuma. Miguu yake ilionekana kung'aa kwa mafuta lainishi, alikuwa amevalia wigi la nywele fupi kichwani kama za wakorea, na midomo yake ilikuwa minene. Joshua yeye alikuwa amevaa T-shirt la njano pamoja na suruali ya jeans, na wakati huu alikuwa amenyoa ndevu zake zote kidevuni. 

Tesha akasimama kutoka sofani, naye Mariam akasimama kutoka chini. Mama zao wakubwa na hata Shadya wakasimama pia wakiwa wanawatazama wageni kama vile ni wageni sana kwao, nami nikaendelea kuwaangalia kwa umakini. Sasa nikawa nimeelewa kilichofanya Miryam aonekane kutekwa kiakili muda mfupi nyuma. Alikuwa anasubiria ujio wa hawa watu.

"Karibuni jamani," Miryam akawaambia hivyo wawili hao.

"Asante sana. Shikamooni," mwanamke huyo mgeni akaongea hivyo na kuwasalimu mama wakubwa huku akionyesha ishara ya kupiga magoti kiasi.

Bi Jamila na Bi Zawadi wakaitikia salamu yake kwa kusema 'marahaba.'

Joshua pia akasema, "Shikamooni," lakini wanawake hao hawakumjibu na kubaki wamemwangalia tu kwa umakini.

"Mimi, huyu anafanya nini hapa? Ameleta tena fujo zake? Aisee... ngoja nimpigie mzee Hamadi," Tesha akasema hivyo huku akitoa simu yake.

Shadya akatoka upande huo waliokuwa wamesimama wageni pamoja na Miryam, naye akaenda kusimama pembeni yake Mariam.

"Tesha hapana... hebu tulia. Mimi ndiyo nimewakaribisha... weka simu chini," Miryam akamwambia hivyo.

Tesha akamwangalia na kuuliza kwa sauti ya chini, "Nini? We' ndiyo umewaita?"

Hali hapo ilikuwa imeanza kujenga uzito, nami nikamwona Mariam akianza kubabaika kwa ule mtetemo wake wa kichwa. Agh, hiyo haikupaswa kutokea! Presha yoyote ambayo ingemwingia msichana huyu ingesababisha tuanze kurudi nyuma tena wakati alikuwa anaonyesha maendeleo, na ni wazi kilichosababisha hilo ilikuwa ni woga wake kumwelekea Joshua.

Nikasimama na kumgusa Shadya mkononi, naye aliponiangalia nikamwambia kwa sauti ya chini, "Naomba umpeleke Mamu chumbani."

Kwa kunielewa vizuri, Shadya akamshika binti mkono na kuanza kwenda pamoja naye chumbani kweli.

"Mimi, wewe ndiyo umewaleta hapa? Ili iweje?" Tesha akamuuliza hivyo dada yake tena.

"Tesha nakuomba ushushe hiyo sauti. Hawa ni wakubwa... wamekuja tuongee. Naomba ukae tuzungumze," Miryam akaongea kwa utulivu.

Mwanamke huyu akawaonyesha wageni masofa ili wakae, kistaarabu sana. Kiukweli hata mimi pia nilikuwa nashangaa, iweje iweje mpaka huyo jamaa akaja tena sehemu hiyo na kukaribishwa vizuri. Na huyo mwanamke alikuwa nani?

"Tuzungumze? Tuzungumze nini na huyu mbwa, Miryam?" Tesha akasema hivyo kwa hasira.

"Tesha!" Miryam akasema hivyo kama kumzuia.

"Jamani Tesha... tumekuja tu kuongea vizuri. Haina haja ya magomvi..." huyo mwanamke akasema hivyo.

"Magomvi? Unayajua magomvi aliyokuwa ameyaleta hapa huyo mume wako?" Tesha akamwambia hivyo.

"Tesha niangalie..." Miryam akasema hivyo.

Tesha akamwangalia kweli, na ni muda huo ndiyo Shadya akawa amerejea peke yake. 

Nikawa nimetulia tu usawa aliosimama Tesha sasa, huku nikiona namna ambavyo huyo mke wa Joshua alinitazama sana.

"Ninakuomba ukae chini. Nisikilize... kuwa na adabu... kwa ajili yangu," Miryam akamwambia hivyo mdogo wake.

"Miryam nakuheshimu sana. Sana. Lakini hii kitu... siwezi kukubali. Amekuja kuongea nini? Hivi kweli... ma' mkubwa... hii ina-make sense? Miryam amekuwaje?" Tesha akaongea kwa hisia.

"Ndiyo utulie mwanangu tusikilize kilicholetwa hapa..." akasema hivyo Bi Zawadi.

"A-ah... hapana. Siwezi me kukaa na mtu aliyewashushia nyie heshima mbele ya watu kwa kusema hamna faida yoyote hapa! Anawajua? Kamtukana mpaka na dada halafu anamleta hapa? Ili iweje? Nisikilize nini labda atakachosema huyu mjinga?" Tesha akamwambia hivyo Bi Zawadi kwa hasira.

Mama wakubwa wakawa wametulia tu.

"Tesha mdogo wangu... usiwe hivyo. Mimi nimekuja tukae chini tuongee ili..." Joshua akawa anaongea kwa upole.

"Toka hapa mjinga wewe!" Tesha akamfokea.

"Tesha!" Miryam akamwita kiukali.

"Nini Miryam? Nini? Mbona unakuwa kama umerogwa?" Tesha akasema hivyo kwa hasira.

"Tesha hebu acha!" Bi Zawadi akasema hivyo.

Miryam akawa anamtazama mdogo wake kwa mkazo.

Nikamshika Tesha mkononi na kumwambia, "Oy, hebu jitulize. Siyo fresh, uko mbele ya mama zako."

"Ah... JC mwanangu, labda unisaidie kuelezea hii kitu. Hivi hata inaeleweka kweli? Huyu mbwa mpaka anamwita mdogo wangu taahira, anamwita Mimi dada nusu, halafu nimkaribishe eti nini... kisa kashusha sauti leo?" Tesha akaendelea tu kulalamika.

Alikuwa na haki kabisa ya kutenda namna hiyo, kwa sababu hata kama ingekuwa ni mimi nisingeweza kujihisi amani kukaa sehemu moja pamoja na mtu kama Joshua aliyefanya mambo mengi mabaya sana kwa hii familia. Sijui Miryam alikuwa na moyo wa aina gani! 

Tesha alikuwa amekasirika mpaka jasho likaonekana kumtoka, naye Miryam akamwambia, "Nimekuomba ukae kimya kwa kuniheshimu mimi, lakini umekataa, si ndiyo?"

"Mimi, usitumie kiwango cha heshima nilichonacho kwako kunifanya nionekane jackass. Hata ufanye nini, hata useme nini... siwezi kupoteza muda wangu kumsikiliza wala kuongea na huyu mjinga..."

"Tesha! Mimi ni kaka yako..." Joshua akamkatisha.

"Wewe ni mpumbavu sana! Yaani kama unajiweza, niko tayari kuvuruga hii sebule nikipigana na wewe mpaka kukuua, lakini never siwezi kukuita wewe kaka yangu! Umeshakufa kwangu," Tesha akamwambia hivyo.

Dah! Hii kitu ilitia sana huruma. 

Niliwaangalia mama wakubwa na kuona namna ambavyo hata wao walihisi maumivu aliyohisi Tesha japo walijikaza na kutosema lolote, na Miryam alikuwa amekosa la kusema na kubaki akimtazama mdogo wake kwa kuvunjika moyo. 

"Tesha... tutoke kidogo," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

"Ee mwanangu, twende tuondoke. Hapa siyo," Tesha akasema hivyo na kuanza kuuelekea mlango kwa kasi.

Ilikuwa kasi iliyofanya mke wa jamaa asogee pembeni kwa woga kiasi mpaka kumpamia Miryam, naye Tesha akampita Joshua na kuufungua mlango kwa nguvu, kisha akatokomea nje. Aisee! 

Nikawaangalia mama wakubwa na kusema, "Warembo wangu... mimi naenda. Mamu akishtua kwa lolote niiteni."

"Sawa mwanangu. Mwangalie basi na huyo, eti?" Bi Zawadi akasema hivyo, akiwa amemaanisha Tesha.

"Hamna shida. Tutaonana baadaye," nikamjibu.

Wakakubali kwa kutikisa vichwa vyao, nami nikaanza kuelekea mlangoni. 

Sikuwasemesha wala kuwatazama wageni hata kidogo, na ile nilipoufikia mlango nikamwangalia Miryam na kuona amejishika tu kiunoni huku akitazama upande mwingine kwa kuvunjika sana moyo, nami nikatoka tu ndani hapo. 

Hali ya hewa ilikuwa imebadilika ghafla, na Tesha alionyesha ni jinsi gani alivyokuwa na hasira kali sana kumwelekea ndugu yake. Yaani alikuwa anatamani hadi kumuua, na nilijua hilo kuwa kweli maana aliwahi kusema kwamba kwa ajili ya dada yake angeweza kuua mtu yeyote. Ila hilo lisingekuwa jambo la busara kufanya, nami ningepaswa kuhakikisha namwangalia kwa ukaribu ili asije kwenda kuua mtu huko kweli! 

Hakuwepo hapo ndani ya geti, nami nikatoka nje na kumkosa pia. Mh? Ankia hakuwepo kwa hiyo Tesha asingekuwa ameenda kule ndani kwetu hasa kwa sababu nilimuuliza Fatuma hapo nje ikiwa amemwona jamaa anapita upande huu, lakini akakataa. Huyu angekuwa ameondoka, nami nikaona nimtafute kwa simu. Piga karibia mara tano, wapi. Zote hakupokea. 

Nikaamua niende kumtafuta Masai, lakini nako nikamkosa. Ikawa wazi kwamba alikwenda sehemu nyingine isiyofahamika kwangu, kwa hiyo kama nisingempata kwa simu basi ndiyo nisingeweza kufanikisha zoezi la kuangalia usalama wake. 

Nikaamua kurudi pale kwa Ankia na kwenda kukaa tu sebuleni, nikingoja kupata taarifa yoyote kuhusu alipokuwa huyo kijana kutoka kwa watu niliowaulizia pale Masai; yaani kama angefika hapo biashara ikianza kazi. Sijui kwa nini tu lakini nilikuwa nahisi kuishiwa pozi kabisa kwa sababu ya kujua mambo yaliyokuwa yakiendelea kwenye hiyo familia. 

Bila shaka, Miryam alikuwa anajaribu kutafuta amani, lakini ilionekana kuwa ngumu mno kwa yeyote kukubaliana na njia yake ya kuona mambo; hata mimi sikumwelewa kwa kweli. Ni kitu gani kilichokuwa kinamfanya afumbie macho mambo mengi mabaya ambayo Joshua alikuwa amefanya na kujaribu kumweka karibu yao tena? 

Ni lazima kulikuwa na kitu kilichomsukuma atende hivyo, lakini najua haingekuwa rahisi kwa ndugu zake kukubaliana naye. Hata Mariam tu alisumbuliwa mno na uwepo wa mwanaume huyo karibu nao, na hilo lilikuwa tatizo ambalo ningepaswa kuzungumza na Miryam kulihusu.

★★

Nikaendelea kukaa sebuleni nikiwa nasubiri lolote lile, na kiukweli niliweza kuhisi hali ya msongo kichwani iliyonifanya nijihisi mzito kiasi. Feni ilikuwa inanipuliza lakini bado nilihisi joto. Akili yangu ilikuwa katikati ya mambo mengi ya kufikiria kiasi kwamba mpaka nikawa nahisi kukosa amani. 

Sikujua ni yapi yaliyokuwa yanaendelea kwenye hiyo nyumba baada ya kumwacha Joshua pamoja na wapendwa wangu, sikujua Tesha alikuwa wapi, na huyu Ankia na yeye aliona aondoke tu wakati ambao nilihitaji company kidogo. Nikaona uhitaji wa kufanya jambo lenye kuchangamsha kiasi, lakini sikuwa na wazo zuri lisilo lenye kuboa. 

Ikiwa imekwishafika mida ya saa saba mchana sasa, nikawa nimempigia Ankia kumuuliza kama angerudi mapema, naye akaniambia alikuwa amekwenda mtaa wa eneo wanaloliita Emirate sijui, nadhani kwa mashoga zake, na akasema akitoka huko ilikuwa ni kupitilizia saluni kwanza ili atengeneze nywele zake. 

Akaniuliza ikiwa kulikuwa na shida, nami nikamwambia nilikuwa nimemkosa tu kwa sababu ya kuboeka kukaa mwenyewe ndani. Akiwa hajui kuhusiana na mambo yaliyokuwa yametokea kwa majirani zetu, akaniambia nimwite Tesha tu ili anipe ushirika wake, nami nikaona nisianze kumsumbua kwa kumwambia hali ya huku kwa wakati huu, kwa hiyo nikamkubalia na kukata simu. 

Kukosa lolote jipya kutoka kwa Tesha baada ya kumpigia na kumkosa kwa mara nyingine tena kukanifanya niamue kwenda kulala tu ili muda upite. Nikaingia jikoni kwanza na kuuangalia mkate aliokuwa ametengeneza Ankia. Ulikuwa mkubwa, umbo la duara kufatisha sufuria, na sehemu fulani ilikuwa imekatwa kwa pembetatu pana kuonyesha kwamba Ankia na marafiki zake walikuwa wamekula kabla hawajaondoka. Nikakata kiasi na kuanza kumega, nami nikarudia sofa tena sebuleni ili nikimaliza kuula ndiyo nielekee chumbani kulala. 

Niliposhika simu, nikakuta ujumbe mfupi kutoka kwa Soraya.  

'JC mim naumia san. Sielew kwnn umenitup namn hii. Au kun sehm nmekosea? Nambie nijirekebishe'

Ukasomeka hivyo. Dah! Huyu Soraya huyu! Alinifanya nihisi sauti yake kabisa ikiwa imesema maneno hayo, na sasa akawa mpaka ananifanya nijihisi kuwa mwenye hatia. Kwamba namwonea. 

Unajua huyu alikuwa mwanamke aliyeolewa na hata kama hangekuwa ameolewa, sikuwa na lengo la kudumisha uhusiano wa kimwili niliokuwa nimeanzisha pamoja naye; hasa baada ya haya mambo mengine huku kuongezeka. Ni kama tu nilivyokuwa nimemweleza Ankia kuhusu namna navyoendesha maisha yangu kwa upande wa mapenzi, na hiki ni kitu ambacho nilitaka Soraya pia akielewe ili asije kunizoea mno mpaka akaanza kushindwa kupumua akiwa na familia yake. 

Nikamjibu hivi kwa sms, 'haujakosea, nina mamb mengi tu dear'

Akajibu, 'mamb mengi JC? mamb gn? Si uliniambia uko likizo? ama umepat mwnmk mwngn?'

'Nikisema ndyo?'

'lkn JC'

'Kwan we unatak iweje Soray? Unatak nn hasa?'

'natak kuw na ww'

'Soma hii uelewe vyema Soraah. Wewe na mimi siyo wapenz pekee, ni wapenz marafiki. Una mume, na mimi nina mtu wangu. Usitarajie labd niwajibike kwako % zote, unaelewa?'

'kwan me nimekuomb uwajibike JC? me natak tukutan2.. nimekumiss'

Nikaisoma sms hiyo kwa ufikirio, nami nikamjibu, 'Saw. Tukutane wap?'

'nakusikiliza2 ww,' akajibu hivyo.

'Uko free saiz?'

'ndy'

'Saw. Naingia hapo Mbagala muda so mref. Ukuje pale pale pa sikuile, si unapakumbuk'

'ndy'

'Ee uje. Kwanz uko wapi?'

'nyumban'

'Watoto je?'

'nawaacha na mtu'

'Poa. Jiandae tukutane fasta,' nikamwandikia hivyo, kibabe yaani.

'aya'

Mpango wangu wa kwenda kulala ukawa umevurugwa, lakini si ningeenda kujinoma bwana? Hata hivyo mwanzoni nilikuwa nikitaka kufanya jambo lenye kuchangamsha ili niondoe msongo uliokuwa umeanza kuniingia, kwa hiyo ni kama Soraya alikuwa amekuja kuwa ukombozi. 

Nikaona uhitaji wa kujimwagia maji tena, kisha nikatia pamba nyepesi na kuvaa kwa mara ya kwanza zile ndala nzito na mpya nilizonunua siku ile Kariakoo. Nikawa nimekaa fiti kimwonekano na kunukia fresh, kisha nikamjulisha Ankia kwa ujumbe kwamba hata mimi ninatoka pia hivyo ninafunga mlango kwa funguo, halafu ningeziacha zake kwa majirani zetu pale kwa kuwa hakuondoka na funguo zake za ziada. 

Nikiwa nimeshatoka na kufunga kabisa ndiyo akawa amenijibu kwa kusema ameelewa, nami nikaelekea pale kwao Tesha. Nikagonga geti, na baada ya sekunde kadhaa Shadya akawa amefungua. Akanisifia kwa kupendeza na kuuliza nilikokuwa naenda, nami nikamwambia nafika hapo Mbagala mara moja kuonana na rafiki. 

Akamuulizia na Tesha, ndiyo nikamwambia tu kwamba tuliachana baada ya kuwa ameondoka kwao ila sikujua alipokuwa amekwenda kwa sasa, lakini nikamhakikishia kwamba angekuwa sawa. Nikamkabidhi funguo za nyumba yake Ankia na kumwambia ikiwa ningechelewa kurudi kabla yake basi angezikuta hapo, naye akawa amekubali. 

Nikaona niulize tu hali ilikuwa vipi hapo ndani, naye Shadya akasema yaani kulikuwa na bonge moja la maigizo kutoka kwa Joshua na mke wake. Akaniambia jamaa hadi alipiga magoti kabisa na kuishika miguu ya Bi Jamila na Bi Zawadi akiwa anaomba msamaha, na sasa walikuwa wakiendelea kuzungumza kuhusu mengi waliyohitaji kufanya ili kurudisha amani kwa familia nzima, hususani kumshawishi Tesha awe mpole. 

Ila hata Shadya akaonyesha bado hamwamini huyo mwanaume, na mimi nikamwambia tu aendelee kusikilizia hali. Nikamwambia aende ndani na kuwapa warembo wangu salamu yangu ya kuaga, na ikiwezekana tungeonana baadaye, kisha ndiyo nikaondoka. 

★★

Dakika chache baadaye nikawa nimefika Mbagala, nami nikakunja mguu mpaka kufikia Zakhem na kuingia kwenye hoteli ile niliyomtandikia Soraya penzi la maana siku ile mpaka sasa akawa analililia tena. Nikalipia chumba cha elfu thelathini, nami nikawa nimeomba kuingia kwenye kile kile nilichotumia siku ile baada ya kukuta kiko bila mteja. 

Nikakaa kitandani na kumsubiria mja wangu. Nikajaribu kumpigia Tesha simu tena bila mafanikio, nami mpaka nikaingiwa na hasira na kuamua kuachana naye. Kama hakutaka kunijibu, basi, na hata hamu ya kwenda kutazama mechi tayari ilikuwa imeshakata hasa kwa kuwa hapa nilikuja kucheza yakwangu mwenyewe. 

Nikaweka simu pembeni na kuwasha TV ndogo iliyokuwa humo. Zilikuwepo chaneli kadhaa za king'amuzi cha Azam, nami nikaitafuta chaneli ambayo ingeonyesha mechi ile niliyokuwa nimeisusia, nami nikaipata. 

Nikaendelea tu kutulia hapo kama nusu saa hivi, ndipo simu yangu ikaita. Soraya huyo. Nikapokea kumsikiliza, naye akasema ameshafika Zakhem kabisa, hivyo nikamwambia aanze kuingia kwenye hoteli hiyo na mimi ningekutana naye ngazini. Alikuwa hana aibu wakati huu inaonekana maana alikubali haraka, kisha akakata simu. 

Nikanyanyuka na kutoka ndani hapo, nami nikaenda kusimama kwenye kingo ya ngazi na kumsubiri. Mtoto huyo akafika. Alikuwa anapanda ngazi taratibu, nami nikatumia sekunde chache kumchora kwa macho. 

Alikuwa amevaa yale magauni wapendayo kuvaa wanawake waislamu ambayo huvaliwa na suruali ya skinny kwa ndani, yaani miguuni, na kufikia mikononi nguo hiyo inakuwa ya mtindo huo huo wa skinny kama hako kasuruali. Lilikuwa jeupe, lililoubana kiasi mwili wake na kuuchoresha vizuri sana, na kichwani alivalia ushungi uliopendezesha sana uso wake mweupe. Oh, na chini miguuni alivaa kiatu kirefu chenye rangi ya samawati. 

Wanaume aliokuwa anapishana nao walimwangalia kwa macho yenye uchu kwelikweli, naye akawa amemaliza kupanda ngazi na kuja upande wangu. Nilikuwa namwangalia kwa macho makini tu, lakini yeye akashindwa kujizuia kutabasamu na kuangalia chini kwa haya huku akitembea kwa mdundo wake wa kianamke. 

Akanifikia karibu, akiwa ameshika pochi ngumu ya njano mkononi, naye akasema, "Mambo?"

"Mambo yamefanyaje?" nikamuuliza hivyo nikiigiza kuwa makini kweli. 

Akacheka kwa pumzi na kuubana mdomo wake huku akiniangalia kwa uvutio.

"Em' njoo hapa..." nikamwambia hivyo na kumshika mkono.

Nikaanza kukielekea chumba nikiwa namvuta taratibu mpaka tukaingia pamoja. Ni baada tu ya kuingia na kuufunga mlango ndiyo nikakishika kiuno chake kutokea mgongoni na kumvuta kwangu kwa nguvu. Nikambana na kuanza kubusu upande wake mmoja wa shingo, naye akaangusha pochi yake chini.

"Hhh... JC..." akanena kwa kunong'oneza.

Sikutaka kelele. Yaani hapa nilichokuwa nataka ilikuwa kufuata ushauri wa wimbo wake Darassa; acha maneno, weka muziki! 

Ndani ya sekunde chache Soraya akajikuta hana nguo, hana viatu, mpaka ushungi nikamtolea na kumwacha na nywele zake laini alizoziwekea kibanio kisogoni. Na chenyewe kikatupwa! Nikamrusha kitandani, kisha nikaanza kumpa tomasa na kumnyonya viamsha hisia mpaka akaanza kuchemka. 

Nikatoa nguo zangu pia, nami nikampa pipi anyonye, naye hakupinga. Hisia zangu zilikuwa karibu mno kwa wakati huu yaani ilikuwa kidogo tu nimwagilie mdomo wake, lakini nikajizuia na kumweka aruke kichura; yaani mimi nilale, yeye aendeshe. Na kalijitahidi kweli siku hii. 

Alipochoka ndiyo nikaanza kazi. Piga, piga, piga, mitindo miwili tu, akaanza kutetemeka miguu. 

"Nakojoa... nakojoa...."

Akawa anaongea kwa presha kweli, nami nikaendelea kumshindilia mpaka akamwaga shukani! Leo alikuwa amepagawa kweli yaani alitoa malalamiko ya raha kwa sauti yake yote. Nilipenda sana jinsi alivyojiachia, kale kaupole kake aliamua kukapotezea.

Alionekana kushangaa namna ambavyo niliendelea kumtandika tu bila kutua mzigo wangu hata mara moja, nami nikamwambia nilikuwa sitaki kujiachia mapema kwanza kwa hiyo nilikuwa najikaza. Lakini baada ya dakika chache mwili ukashindwa kujizuia tena, nami nikajiachia ndani ya mwanamke huyo kwa raha zote! 

Soraya alikuwa anaonyesha kupenda sana jinsi nilivyomwogesha ndani kwa ndani, kwa kuwa aliendelea kunibana kwake mpaka nilipomaliza. Na nilijisikia vizuri kweli baada ya kumaliza kazi kiaina hiyo. Tukaendelea kulala pamoja tu kitandani hapo, na nilipoona mechi imeanza, nikatambua ilikuwa ni saa kumi jioni sasa. 

Nikiwa nimeegamia mto huku Soraya akiwa amelalia kifua changu, nikamuuliza, "Vipi mommy, unahisi njaa?"

Akasema, "Njaa yangu ilikuwa kwako JC, ninachohisi sasa hivi ni furaha kwa sababu umenishibisha."

Nikatabasamu na kusema, "Haya bwana. Ni fresh kama umefurahi."

"Sana. Yaani na ulivyo na mapigo matamu, halafu kama hauchoki!"

"Ahahah... afya kwa mazoezi tu."

"Kumbe? Mpaka nikafikiri labda unatumia dawa."

"Kwa nini? Kwani mzee wako huwa anatumia?"

"Hapana. Yaani JC... mume wangu ni mchovu tu... akienda mara mbili amechoka..."

Nikacheka kidogo.

"Ana mahaba ya kuku jamani! Halafu siyo fundi kama wewe ulivyo," akaniambia hivyo.

"Kwa nini usiongee naye? Labda akabadilika. Ama hampendani?"

"Hamna, ananipenda. Tunashirikiana kuwahudumia wanetu, sema tu ndo' hivyo... ameacha kuchangamka. Nilikuwa naogopa kutoka nje ya ndoa ingawa nimeshawishiwa sana na wanaume wengi, lakini wewe... nikashindwa kujizuia."

"Sasa mimi nina nini kwani? Hiki kibamia ndo' useme kinakuzuzua hivyo?"

"We! Hiyo yote unaiita kibamia? Acha kufuru. Sumaku yako imenivuta kwa nguvu sana JC, unayajua kweli yaani. Natamani hata nikumiliki," akaniambia hivyo.

Umeona? Kule kule kwa Ankia.

Nikasema, "Najua, lakini..."

"Usijali JC... naelewa. Umeshanielewesha. Hata wewe una mtu wako kwa hiyo hapa tuko kusaidiana tu. Please... tuyaweke hayo pembeni. Tufurahie tu wakati huu, sawa?"

Aliongea kistaarabu sana mpaka nikawa namwonea huruma kiasi. Lakini kukaza ilikuwa lazima. Sababu nilizijua mimi mwenyewe.

Kwa hiyo tukaendelea tu kulala hapo pamoja huku nikiangalia mechi na kumpigisha mwanamke huyu story, naye akaniomba tucheze mechi fupi tena. Sikumnyima. Na alikuwa ameniomba fupi tu ili ndiyo tuondoke hapo lakini nikampa ndefu ili aende kwake akiwa ametosheka kwa leo. Nilimvuruga mno huyu mwanamke mpaka akasema imetosha, ningemuua! 

Kwa hiyo angalau mechi zangu na Soraya zikawa zimemalizika kwa ushindi, na Simba nayo ikawa imeshinda kwa magoli mawili kwa moja dhidi ya Singida; na walikuwa ugenini kama vile tu ambavyo na mimi nilikuwa nashinda mechi za ugenini huku Mbagala! 

Ikawa imefika saa kumi na mbili na nusu hivi jioni, giza likianza kulivaa anga huko nje, nasi tukaoga pamoja na mimi kumtandika kidogo tena mwanamke huyo cha bafuni, kisha ndiyo tukavaa na kuondoka hapo. 

Soraya alikuwa amenipa ahadi kwamba hangesahau kamwe penzi nililokuwa nampatia kuambatana na furaha aliyokuwa akihisi ingawa alikwenda kinyume na sheria za dini yake, naye akasema ikiwa 'majaaliwa' yangekuwa upande wake, basi tungekuja kukutana kwa mara nyingine tena. Sikuwa na neno, nasi tukaachana na kuelekea sehemu za makazi yetu.

★★

Nilifika pale nyumbani mida ya saa moja na kukuta Ankia akiwa bado hajarudi. Nikaamua kufungua tu milango hapo na kwenda ndani ili nipumzike kidogo. Funguo niliyokuwa nimeiacha kwa kina Tesha ilikuwa ile ya Ankia, niliyofungulia wakati huu ikiwa ni ile ya ziada aliyokuwa amenipatia, kwa hiyo nikafikiria labda hiyo yake ingefatwa baadaye. 

Nikakaa zangu tu sebuleni na kuanza kuchat na Soraya, ambaye hakutaka kuacha kunisifia kwa mapenzi motomoto niliyotoka kumpatia masaa machache nyuma, nami nikawa nimemwambia ajitahidi sana kuwa mwangalifu ili asije kukamatwa na mumewe; nisije kuwekwa katikati ya chanzo cha ndoa yake kugeuka kuwa matatizo. Sawa alikuwa mtamu, lakini mimi hiyo kitu nilifanya kujichangamsha tu, ohoo!

Muda ukaendelea kutembea, mpaka inafika saa tatu usiku bado nilikuwa ndani tu nikisubiri kusikia chochote kuhusu Tesha, lakini simu yake haikupatikana wala hakukuwa na mtu mwingine aliyenipa taarifa za jamaa kuonekana Masai. Hata Bobo mwenyewe hakujua.

Nikawaza labda sijui alikuwa amesharudi hapo kwao, na huenda kutoka kwenda kumwangalia lingekuwa jambo la muhimu kufanya. Ilikuwa ni hali tu ya kujali iliyonifanya nihisi kuwajibika kwa huyo kijana, kana kwamba alikuwa mdogo wangu kabisa. 

Ankia hakuwa amerudi bado kutoka saluni, na mara kwa mara nilikuwa nikizungumza na marafiki kwenye simu na kuchat na Soraya pia, na ilipogonga tu saa nne kamili nikaamua kutoka ndani hapo ili niende kwa jirani yetu kumwangalia rafiki yangu. 

Nikavaa masai zangu miguuni kwa kuwa zile ndala mpya nilikuwa nimeshazirudisha chumbani, nami nikaanza kuelekea upande wa nje, lakini kabla sijalifikia geti letu dogo, nikawa nimekanyaga kitu fulani kigumu kilichosababisha masai yangu moja mguuni ivutwe, na hivyo nikawa nimejikwaa na kusukumwa mbele kwa mshtuko huo. 

Ilikuwa kwa nguvu, na hilo likasababisha hicho kiatu changu kikatike sehemu ya kuingizia kidole gumba cha mguu, lakini sikuumia. Ah nikaisogelea masai yangu nikiwa peku mguu mmoja, na sikupenda kweli kukanyaga chini, nami nikachuchumaa ili kuangalia kilichonikwaa. 

Ilikuwa ni msumari, ukiwa umepigiliwa chini na kubaki umechungulia juu kiasi, nami nikaelewa hilo kuwa utundu wa watoto ambao wangeingia mpaka sehemu hiyo ya mwanzo getini na kufurahia michezo yao, na sasa wakawa wamenisababishia hasara. Ingebidi kumwambia mwenye nyumba wangu ili awaonye la sivyo tungekuja kukatika vidole. 

Nikauchomoa msumari huo na kusimama, lakini kwa ule mpigo wa haraka wa macho baada ya kugeukia ukuta, nikawa nimemwona Joshua kupitia matundu ya ukuta akitoka kule ndani, simu ikiwa sikioni, na akiwa kama anakuja upande wangu. Nikachuchumaa tena na kuusogelea ukuta, nami nikauegamia na kutulia. 

Sikufikiri kwamba bado huyu jamaa na mke wake walikuwa hapo, lakini kumwona ametoka ndani ili aje huku kote kuzungumza na simu kuliamsha mashaka. Nilikuwa tu nimeingiwa na ile hisia ya kipelelezi, nikitaka kujua aliongea na nani na kuhusu nini; fikira za kwanza ikiwa masuala ya wanawake wengine. 

Nikasikia vizuri hatua zake zikikaribia ukuta kwa upande wa pili, na maongezi yake yalikuwa kwa sauti ya chini lakini yenye msisitizo mkali.

"...unapiga, unapiga, unapiga, nimekwambia niko kwenye kikao... mbona huelewi?" akawa anasema hivyo.

Nikaweka umakini wangu zaidi.

"Sa... saawa... naelewa. Kwani we' hofu yako iko wapi? Hunijui?.... Muda, muda kitu gani... si ilikuwa juzi tu? A-ah... usilete masuala yako bwana... unanielewa? Nisikilize. Acha kulalamika, hau... hauna haki ya kulalamika nimekucheleweshea kwa sababu zoezi lenyewe hukulikamilisha.... lakini hata hivyo si bado nilikuahidi ningekulipa?... Ndiyo... wiki zimepita sawa.... ah... unazingua. Oya, me nitakutafuta, nimekwambia... nimekwambia niko kwenye kikao, mbona huelewi?... Mambo magumu kwangu pia... ndiyo bado.... bado niko kwenye harakati za kutafuta.... Ah... usilalamike Yohana... kwanza yote haya ni makosa yako!... Makosa yako ndiyo, kama ungekuwa umemgonga hiyo siku sasa hivi si tungekuwa tushapata hizo hela?"

Macho yangu yakakaza zaidi baada ya kusikia maneno hayo, moja kwa moja nikiwa nimeelewa maana yake.

"... ndo' utulie Yohana... hilo dili limeshafeli... Eee... we' tulia, niko nao huku nimeanza kubembeleza, taratibu nitapata njia ya kuzoa hela hapa, kwani we' hunijui? Ndo' usikilizie muziki sasa... nimerudi...."

Ah! Haki ya Mungu! Yaani alinifanya nihisi kuchoka. 

"Tatizo unakuwa na presha mno... we' nipe tu wiki wala usijali, kwanza hilo gari si lilikwanguka tu, ina maana mwenye nalo ndo' anakusumbua akili namna hiyo? Aa wapi wewe... tulia. Nitakupa, halafu ndiyo tukamilishe hiyo ishu ya shamba... taratibu tu... aina hiyo. Usipige tena mpaka nikutafute, kichwa wewe! Hahahah... kafie huko Bunju!"

Nadhani hapo ndiyo akawa amemaliza maongezi yake hayo ya siri, isipokuwa tu hiyo siri na mimi nikawa nimeinakili. 

Hatua zake za kuondoka hapo zikanifanya nisimame, nami nikamtazama kupitia matundu ya ukuta kumwona akirudi kule ndani; bila shaka kuendeleza unafiki wake. Ah Mungu mkubwa jamani! Yaani hata ufanye mabaya na kuyaficha jinsi gani, akiamua kuyafunua utapatikana tu!

Nikabaki hapo nikiwa natikisa kichwa kwa kuhuzunika. Huyu mwanaume hakuwa mtu kabisa. Yaani alikuwa hafai. Kusikiliza maneno hayo yote kulikuwa kumenifanya nitambue namna gani alivyokuwa mbinafsi, tena kupindukia. Mara ya kwanza nimekutana naye alinifanya nikamkasirikia, lakini wakati huu, nikawa nimemchukia. 

Kumbe ni yeye ndiye aliyetengeneza ajali ile ya gari iliyokusudiwa kumwondoa binti Mariam, tena mdogo wake wa damu kabisa, ili tu afanikishe mipango yake ya kuchukua mali iliyoachwa kwa ajili ya huyo binti. Hilo zoezi liliposhindikana ndiyo akaunda kale kampango ka wizi kupitia hati bandia za kimahakama, na tena na hapo akafeli. 

Kwa hiyo sasa alikuwa anatengeneza mbinu nyingine tena ili aje kuivuruga hii familia, tena ni familia yake kabisa! Alikuwa anautumia upendo wa Miryam kwa familia yao ili kuingia ndani, awadanganye-danganye halafu puuf... awamalize. Hakufaa kabisa! 

Unajua kwa jinsi ambavyo mambo yalikuwa yamekwenda tokea ile siku nimemwokoa Mariam asigongwe kwa gari, nilikuwa nimeshaanza hadi kusahau kwamba kweli tukio lile lilikuwa la kupangwa, na sasa ndiyo Joshua akawa amethibitisha kuwa yeye ndiyo mfumaji wa hiyo mipango. Sijui kama na huyo mke wake alimuunga mkono kwa haya mambo lakini kiukweli ilikuwa imepita kiasi. 

Nisingeweza kuwaacha waiharibu amani ya familia hiyo ambayo niliona wazi ilikuwa imeanza kuwa imara zaidi kutokea kwa binti Mariam aliyekuwa ameanza kuonyesha dalili za kupona, na kama ingehitajika nijiunge na Tesha ili kumwondoa huyo mtu aliyejiita kaka yao, ningefanya hivyo. Alikuwa mtu mchafu sana, nami ningehakikisha anakomeshwa kwa kutupwa kwenye kiroba cha uchafu alipostahili kuwa!

 

★★★★★★★★★

  ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Previoua Next