Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA TANO

★★★★★★★★★★★★★★


Gari nililokuwa nimepanda lilifanya safari ya kuelekea Kigamboni huko, nami niliamua kutoshuka kabisa mpaka mwisho ambapo lingesimama. Ilikuwa kama tu siku ile ambayo nilitoka na Tesha kuja kutembelea huku, yaani likaelekea mpaka pale ambapo mimi na jamaa tulipanda daladala iliyotupeleka mpaka Kariakoo, kwa hiyo na hili la sasa hivi lilikuwa la utaratibu huo. 

Hivyo niliposhuka, wazo likawa kwenda kukata tiketi ya kupanda meli ndogo ya abiria kwenye kivuko cha bahari, kisha nikifika upande wa pili ndiyo nipande daladala ya kunirudisha mpaka Mzinga. Sikujali nani wala nini yaani; nikapanga foleni hadi ilipofika zamu yangu kupata kadi, nikaipata na kupanda meli, tukavushwa salama mpaka upande wa pili, na moja kwa moja nikaelekea stendi ya magari ambapo ningechukua daladala. Nikapanda tu moja ambayo nilikuwa na uhakika ingenifikisha Kongowe huko, na kwa utulivu tu nikaendelea kusubiri hadi pale lilipoondoka hatimaye.

Bado nilikuwa nikiwaza kuhusiana na haya mambo yote, lakini zaidi ni uamuzi wangu wa kumpigia Festo na kumwomba tuonane. Kuna vitu nilikuwa nataka kuhakikisha navipata zaidi, na jamaa alikuwa na hiyo nguvu ya kunihakikishia. Alikuwa amekubali kukutana na mimi, lakini hakusema ni wakati gani zaidi tu ya kwamba angenitafuta na kunipangia pa kukutana hivi karibuni, kwa kuwa mambo yake yalikuwa mengi mno, ratiba ilimbana. Sikuwa na namna ila kumkubalia tu, kwa hiyo kuusubiri mkutano huo na jamaa lingekuwa jambo la lazima.

Lakini hiyo haikumaanisha kwamba kwa kila jambo ambalo lilikuwa limetokea kuanzia hiyo jana nilikuwa nikitegemea Festo ndiyo awe kama suluhisho langu, hapana. Huyu alikuwa kama njia tu ya kunifikisha mahala fulani, katika sehemu fulani ya haya yote, na baada ya hapo ndiyo mengine yangefuata. Ila hata kama ingetokea kwamba jaribio langu kwake lingeshindikana, basi ningetafuta njia nyingine tu ya kutatua vikwazo nilivyokuwa naona vikija; mimi kama mimi. Kama nilivyokuwa nimeshasema, huu ulikuwa ndiyo wakati wa kuwa tayari kuchukua maamuzi mazito, na nilikuwa tayari.

Nimekuja kufika Kongowe ikiwa imeshaingia saa moja, na kutokea hapo mpaka Mzinga nikaamua kutembea tu taratibu. Kumbukumbu kadhaa zilirejea kichwani kwangu baada ya kuipita ile hospitali ambayo tulimpeleka Mariam usiku ule wa matukio mabaya kumpata yeye pamoja na Tesha, nami nikatumia muda huo kuwapigia simu akina Bi Zawadi ili kuwasalimu. Waliendelea vizuri, na Mariam akapewa simu anisalimie pia, huku nikiwaambia ningechelewa kurudi leo hivyo kuja kuonana ingekuwa mpaka kesho, nao wakaonekana kuridhia.

Sikuwa hata nimechelewa kivile, ila ni basi tu kwa muda huu sikuwa na ile amani iliyotosha kuniruhusu hata kwenda kuwatembelea wapendwa wangu hao nikishafika huko. Amani iliyokuwa imevurugwa hasa na kujikuta nafatiliwa na mtu aliyeonekana kuwa na nia mbaya kunielekea. Nilihitaji zaidi kukaa tu kivyangu, pale kwa Ankia, nipige-pige mahesabu kifikira na nini, kisha nipumzishe mwili na akili kwa ajili ya mambo mengine ambayo yangefuata. 

Sijui kwa nini tu yaani ila nilikuwa nimeshaanza kuhisi kama vile kuna kitu kikubwa sana kilikuwa kinakaribia kutokea kwenye maisha yangu. Tena kibaya. Na haya yote niliyokuwa nimejiingiza kufanya ndiyo yangekuwa sababu ya kitu hicho kutokea. Kwa hiyo hisia hii ilinivuta chini mno kwa sababu kwa wakati huu ndiyo ilikuwa na nguvu zaidi, hivyo kweli ningehitaji kutuliza hisia na akili kwanza, na kwa muda uliotosha.

★★

Nimekuja kufika kwa Ankia ikiwa imeshaingia saa mbili usiku, nami nikamkuta mwanamke huyo akiwa ndani tayari pamoja na marafiki zake wale wavaa pini puani na mama Chande pia, wakitengenezeana urembo wa Yna kwa kuzichorea mikononi. Ankia pia alikuwa amechorwa, na baada tu ya kusalimiana nao nikaelekea zangu chumbani kubadili mavazi, kisha nikatoka na kwenda kujimwagia kwanza. Nikarudi ndani tena na kutulia tu chumbani baada ya kuvaa nguo nyepesi.

Aliyekuwa ananipa company zaidi kwa muda huu ilikuwa ni Dina, ambaye alinitafuta ili tuendelee na maongezi yetu yaliyokatishwa ile jioni baada ya Kevin kunipigia. Nilikuwa sijisikii hata kuchat naye lakini nikawa mpole tu kwake na kuendelea kutumiana naye jumbe fupi za kirafiki, na hatimaye akawa amefunguka kuvutiwa sana na mimi.

Dina alikuwa mwanadada mwenye akili iliyofunguka, kama tu Ankia, yaani ingawa alijua ningeweza kuwa natoka na mtu mwingine kimapenzi, alikuwa tayari kujiweka karibu nami bila kujali hilo kabisa. Ili kutofikishana mbali sana, nikamwambia ndiyo, nilikuwa na mpenzi, na isingekuwa vizuri nikimsaliti kwa kufanya uhusiano na mtu mwingine, lakini Dina akaendelea kuonyesha msisitizo wa hisia zake kwangu, japo hakuwa wa ile aina ya kulazimisha mahusiano. Alitaka tu mambo huyo!

Nikiwa nimejilaza tu kitandani kwa kuegamia mto huku nachat naye, Ankia akawa amekuja chumbani hapo, naye akasogea mpaka kitandani na kukaa usawa wa ubavu wangu huku akinionyeshea jinsi viganja vyake vilivyopendezeshwa ya michoro ya Yna.

"Imeshakauka?" nikamuuliza.

Akatikisa kichwa kukubali huku akitabasamu.

"Umechora tattoo za waislam Ankia, hata Eid bado?" nikamsemesha kizembe.

Akaigiza kuudhika na kusema, "Si uniambie tu kama nimependeza na we' naye..."

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Ni nzuri. Inaonekana unapenda sana uislamu."

"Kwa nini?"

"Kuanzia harufu, mashosti zako, mpaka haya mambo... mbona iko wazi?"

"Wala, me mroma mroma. Siwezi kujifungia huko mie mpenda pombe," akasema hivyo.

Nikatabasamu kivivu na kutazama simu tu.

"JC, vipi? Unaumwa?" Ankia akaniuliza hivyo.

Nikamwangalia na kusema, "Hamna, niko kawaida. Mbona uulize hivyo?"

"Nimeona umeingia kama vile huna raha..."

"Nimechoka tu," nikamwambia hivyo kiupole.

"Unachoshwa na nini?" akauliza.

Nikabaki kimya wakati nikijibu jumbe ya Dina kwenye simu.

"Ndo' unachat na demu wako mpya?" Ankia akaniuliza.

"Hamna. Huyu ni rafiki yangu," nikamwambia.

"Ndiyo anayefanya kila ukiondoka unachelewa kurudi, na ukirudi unakuwa umechoka sana, si ndiyo? Huyo rafiki yako huyo?" akaongea kwa njia ya utani.

"Unaniuliza hivyo we' kama nani?" nikamsemesha kiujeuri, lakini kwa utani.

"Mimi kama mama watoto wako," akajibu.

"Unataka kipigo sasa hivi, eti? Em' nenda kawatawaze kwanza hao watoto huko..." 

Ankia akacheka kidogo na kunipiga mkononi kidogo, naye akasema, "Chakula kimeiva baba. Njoo ule."

"Nitakula baadaye. Napumzika kidogo," nikamwambia.

"Mmm..."

"Nini sasa?"

"Sema tu kama umetoka umeshiba huko..."

"Yeah, nimekula saa kumi, so... bado sina njaa kivile," nikamwambia.

"Haya. Leo kweli unaonekana kuchoka, sijui hata ulikuwa unamfanya nani..."

"Halafu we' Ankia wewe, inaonekana umenimiss tu wewe. Unawashwa-washwa sana siku hizi. Unataka nikutandike, eti?"

"Thubutu! We' mwenyewe ndiyo ulikuja na swaga za 'ooh... sasa hivi tuwe marafiki tu, hakuna kunyanduana...' hiyo ya kunitandika itoke wapi? Ndiyo imeisha hiyo mpangaji wangu. Hugusi hili sambwanda tena," akaniambia hivyo.

"Ahahahah... naona mama Chande anakulisha bangi zake," nikamwambia.

"Kwa nini?" akauliza huku akitabasamu.

"Umeanza kuongea kama yeye, kwa hiyo naona akili zenu zitafanana tu. Hilo 'sambwanda' kama halijabantalala ndani ya wiki moja tu, basi ndo' nitajua haujatembezwa naye kwenda kulipigisha makofi," nikamwambia hivyo kiutani.

Ankia akacheka kwa sauti kubwa na kugonga kiganja chake kwenye changu, naye akasema, "Eti 'bantalala!' Me siyo wa hivyo, utasubiri sana."

"Mhm... sawa."

"Haya, sisi tunaenda kula. Halafu... Adelina ameniambia mliongea," akasema hivyo.

"Alikupigia?"

"Eeeh, tumeongea leo, akasema atakuja Jumapili... ulimwalika tuje kuangalia mechi?"

"Yeah. Ni sawa akija na kulala hapa?"

"Eeh! Kwa nini isiwe sawa? Acha mambo yako bwana. Ila ndo' utunze ya kutosha. Yanga itashinda, na utaninunulia bia zote nazotaka," akaniambia hivyo.

"Ahahah... endelea kuota..." nikamwambia hivyo huku nikiendelea kuchat.

"Hahahah... haya baba, tutaona. Yaani Aziz Ki lazima afanye yake," akaniambia.

"Na limdomo lake..." nikasema hivyo kiutani.

Akanyanyuka huku akiendelea kuongea kuhusiana na mechi ya watani wa jadi ili aamshe maneno na kwa kina mama Chande huko, na mimi nikaendelea tu kuchat na Dina mpaka kufikia saa nne usiku kabisa. Ndiyo nikaamua kwenda kupakua chakula kwa muda huo, rafiki zake na Ankia bado wakiwepo, nasi tukajumuika pamoja kimaongezi japo sikuzungumza nao kwa wingi; sanasana Ankia tu na mama Chande.

Haikuchukua muda mrefu nikawa nimerejea chumbani tena, na aisee Dina hakutaka kuniacha. Mtoto alinielewa, alikuwa amenimiss japo aliniona kwa siku moja tu, na akaelezea hamu yake kubwa ya kuniona siku ya kesho wakati ambao angekuja pamoja na dada yake, Doris, kuwatembelea wakina Miryam. Tumekuja kuagana usiku wa saa saba kabisa nikiwa nimetosha kuchat na mwanadada huyo, nami ndiyo nikaanza kuutafuta usingizi wangu. 

Ijumaa ikawa imepita.


★★★


Nimekuja kuamka asubuhi kwenye mida ya saa tatu hivi, ikiwa ni Jumamosi sasa, na kama kawaida, ratiba yangu ingeanza kwa usafi wa mwili kwanza. Nilikuwa najihisi ahueni kiasi baada ya kupumzika, na nilitaka kwa leo nimezwe na mambo mengine tofauti kabisa na yale yaliyowahusu wabaya wangu, kwa hiyo ningetumia muda mwingi pamoja na Ankia na familia yake Miryam. Na nilitaka kumwona huyo Doris pamoja na Dina leo.

Kwa hiyo ikawa ni kunywa chai pamoja na Ankia hapo kwake, tukakaa kupiga story za hapa na pale  huku tukiangalia TV hadi mida ya saa sita mchana, kwa kuwa leo Ankia asingekwenda dukani kwake kwa sababu alizojua mwenyewe. Hata kwa asubuhi hii, Dina alikuwa ameamka na mimi kwa kutuma jumbe za salamu, nami nikawa nikichat naye mara kwa mara mpaka aliposema kuwa yeye na dada yake tayari walikuwa njiani kuja huku Mzinga.

Nilikuwa nimejaribu kumpigia madam Bertha na kumtumia ujumbe pia, lakini hakurudisha majibu. Inaonekana bado nilikuwa nimemkwaza sana, na sijui hiyo ingeniacha wapi lakini kwa kweli ilipokuja kwenye suala la kuwa na "mtoto," tena pamoja na Bertha, kilikuwa siyo kitu cha kuchukulia juu juu. Angeendelea tu kuvimba na mimi ningeendelea kujifanya najaribu kumbembeleza, lakini nisingekubaliana naye kwa suala hilo kabisa kwa kujua mambo yaliyokuwa yakija.

Nikaamua tu kuendelea kutulia, na ilipotimia mida ya saa nane bado nilikuwa ndani tu na Ankia, wakati huu akiwa anapika ugali na samaki huko, ndiyo nikatumiwa ujumbe na Tesha. Tesha bana akaniambia kwamba Dina alikuwa ndiyo amefika, kwa hiyo niende, lakini nikamwambia 'tulia wewe.' Kujipeleka kisa wageni wamefika ingekuwa ni michoro ya hali ya juu, kwa hiyo nikamwambia ningeenda baadaye kabisa na si sasa.

Misisitizo zaidi ikaja baada ya Dina na yeye kuanza kunitumia sms kuwa niende anione, lakini nikaendelea kukaza tu. Mpaka Ankia amepakua, tukala, tukamaliza, Dina na Tesha bado walikuwa wananisumbua tu niende, niende, niende, na ilipofika mida ya saa kumi hivi jioni, ndiyo nikawa nimepigiwa simu na Bi Zawadi. Cheupe wangu. Hii ndiyo ingekuwa 'sina jinsi' yangu niliyohitaji zaidi, maana kwa mwito wa mama huyo kwenda hapo kuwatembelea, jibu la moja kwa moja lilikuwa 'yes!' 

Bi Zawadi alinitaka niende hasa ili anitambulishe kwa huyo Doris, ile tu kujuana mimi ni nani kwenye hiyo familia na nini, kwa hiyo mwana nikaingia chumbani kuvaa suruali na T-shirt, nikatengeneza nywele vizuri, kisha ndiyo nikatoka na kwenda mpaka hapo kwao. Nilikuwa nimemwacha Ankia akiwa ameingia chumbani kwake kulala kidogo, na nilipoingia hapo getini nikakuta gari la bibie Miryam likiwepo. Inawezekana bibie alikuwa amewahi kurudi kwa ajili ya wageni ama leo hakwenda kazini kwake, hivyo nikasogea mpaka mlangoni na kuomba kuingia kwa kusema 'hodi.'

Aliyesema 'karibu' alikuwa ni binti Mariam, na ile nimeingia tu, nikapokelewa kwa shangwe sana na binti huyu, akinikumbatia kwa nguvu kama kawaida yake. Mariam alivaa moja ya madera yake ya kawaida, na bado kunikumbatia kwake mbele ya ndugu zake namna hiyo kulinifanya nijihisi uajabu kiasi, lakini nikajitahidi kuonyesha utulivu. Ilikuwa kama vile sebule ilijaa, maana walikuwepo mama wakubwa, Mariam mwenyewe, Shadya, Tesha, Miryam, Dina, pamoja na mwanamke mwingine rika la bibie Miryam, ambaye bila shaka ndiye aliyekuwa Doris. 

Nikasalimiana na wa hapo vizuri sana, nikawasalimia na wageni vizuri pia, kisha nikaenda kuketi sofani pamoja na Mariam baada ya Tesha kutuachia nafasi. Hapo sasa ndiyo Bi Zawadi na Shadya wakaanza kunitambulisha kwa wageni kwa mapambo ya hali ya juu, na mimi nikajitahidi sana kumsemesha Doris kirafiki na kumpa hongera yake ya kuelekea kuwa jiko rasmi. Alikuwa mwanamke mzuri, mweusi wa maji ya kunde kama Dina tu, akiwa si mnene sana wala mwembamba, na alikuwa na shepu ya ukweli hata kwa kumwangalia tu alipokuwa ameketi.

Wakati huu alikuwa amevalia T-shirt la mikono mifupi la kijivu lililoficha kifua chake kilichobeba maboga haswa, pamoja na suruali nyeusi iliyombana kiasi cha kuonekana kama skinny. Nywele zake alikuwa amesukia rasta nyembamba na fupi, zilizomwagika kuzungukia kichwa kama vile tambi, akiwa na macho makubwa na midomo minene iliyopakwa lipstick yenye kung'arisha.  Saa yake mkononi na pete, hereni, bangili, mkufu, vilionyesha alikuwa mwanamke aliyependa vitu vizuri vyenye gharama na kupendezesha, lakini alitaka kuonekana 'simple' tu kwa watu wengine. 

Baada ya kuongea kidogo mambo ya hapa na pale nikatambua alikuwa msomi, na alifanya kazi kwenye kitengo fulani maalumu huko TRA. Alikuwa na ka aina fulani ka uzungu, na niliona akikakoleza zaidi ili ile hali ya yeye kuwa 'msomi' ionekane wazi. Lakini hapa akili yangu ilikuwa imekengeushwa zaidi na Dina, kwa sababu mwanadada huyo alikuwa ananitazama utadhani nilikuwa chakula cha jioni. 

Yeye alivalia shati pana kweli kupita umbo lake dogo-dogo, jeupe lenye mistari-mistari, ambalo kwa njia ya mtindo alikuwa amelifungia mbele ya tumbo lake kama fundo. Uwazi mdogo wa tumbo lake ulionekana, na yeye alikuwa amevalia suruali ya jeans ya blue iliyokoza na kurembwa na rangi nyeupe hapa na pale. Alikuwa amesuka rasta ndefu za kahawia alizoziachia mpaka huko mgongoni kwake, akisindikiza maongezi yenye kufurahisha hasa kutoka kwa Tesha na kuendelea kunitazama mara nyingi sana; nafikiri akiwa anasubiri ishara.

Bibie Miryam alikuwa akishughulika zaidi na suala la msosi, kwa kuwa alikwenda jikoni na kurudi kujumuika nasi, na yeye alikuwa amevaa kinyumbani kwa kutia T-shirt nyeusi ya mikono mifupi pamoja na khanga ngumu iliyomfunika kutokea kiunoni. Nilipenda sana jinsi ambavyo alikuwa amepaka rangi nyeusi kwenye kucha za vidole vyake vya kiganja cha kushoto, na kila mara ambayo tungeangaliana usoni, angenipa tabasamu la kirafiki, nami ningejihisi amani sana na kumrudishia pia. 

Ikawa ni muda ulioneemeka sana wa kufurahia ushirika wa maongezi pamoja na familia hii ulionifanya nijihisi vizuri zaidi ya ilivyokuwa kwa siku ya jana, nami nikaendelea kuwa hapo pamoja nao hadi giza lilipoingia kuuelekea usiku.

★★

Ikiwa imekwishaingia mida ya saa moja kuelekea saa mbili, bado nilikuwa ndani hapo nikipiga story mbili tatu pamoja na Bi Jamila, Bi Zawadi, Shadya, na Doris. Hawa ndiyo waliokuwa wamenikamata zaidi kwa wakati huu, na Doris alikuwa ameshanizoea haraka. Alikuwa mcheshi pia, kwa hiyo tuliwaburudisha sana hawa wenyeji utadhani sisi ndiyo tulikuwa wazawa wa hapo. Bibie Miryam alikuwa huko nje akifanya nini sijui, halafu Tesha, Mariam, na Dina walikuwa chumbani kwa jamaa wakifanya mambo ya vijana na nini, si unajua? Ile kupatana zaidi. 

Tesha alikuwa ameshanitumia jumbe kadhaa kuniambia niende huko chumbani pia nikajaribu hata kumtekenya Dina, angefanya hata kumwondoa Mariam kabisa, lakini najua alijua hiyo haingekuwa kitu yangu kukubaliana naye kabisa. Hata Dina alikuwa akinitumia sms pia kusema amefurahi mno kuniona, anatamani tuongee, lakini mimi nikaendelea kukazia fikira zangu zaidi kwa warembo hawa wengine sebuleni.

Katikati ya maongezi yangu na wanawake hawa, simu yangu ikaanza kuita, nami nikaona mpigaji kuwa mama. Nikawaomba waniekskyuzi kidogo ili nikapokee simu, kisha nikaenda mpaka pale nje varandani na kupokea. Hapo nje nikawa nimemkuta bibie Miryam, akiwa mbele zaidi kuukaribia ukuta wa uzio, na akionekana kutumia simu yake kwa ishu zake, hivyo nikaendelea kuongea na mama yangu huku nikimwangalia bibie. 

Mama alikuwa ananisalimu tu, na mimi pia nikamwambia ningekuja kwenda nyumbani kabisa ili kumwona ndani ya hizi siku chache mbeleni, nasi ndiyo tukaagana baada ya hayo na umakini wangu ukarudi kwa bibie pale. Alionekana kuwa makini sana kuchat na nani sijui, nami nikaamua kumfata ili nimsemeshe kidogo. Tayari alikuwa ameniona, kwa hiyo nadhani alipoona navaa ndala zangu akafikiri ninataka kuondoka.

Akasema, "Unaenda, Jayden?"

"Hamna, nipo. Sisepi mpaka nile msosi wako," nikamwambia hivyo kiutani.

"Ahaa, sawa. Nilikuwa nafikiri unataka kuondoka, maana una katabia tukishaivisha tu ndiyo unanyanyuka kukimbia..."

"Ahahahah... Shadya atakuwa ameshanisema sana."

"Na ni kweli..." akasema hivyo huku umakini wake ukirudia simu.

Nikasogea mpaka pembeni yake na kuuegamia ukuta, nami nikasema, "Hiyo taa ya... imeungua eh..."

Nilikuwa nikimwonyesha taa ya upande ule uliolekea kwenye bomba la maji kuzungukia mpaka huko nyuma ya nyumba yao, ambayo haikuwa ikiwaka kama ya hapa mbele, naye akaangalia huko mara moja na kusema, "Eeeh, itakuwa imeungua. Tesha atakuja kubadilisha."

"Okay. Ndugu zako ni watu wazuri sana," nikamwambia hivyo, nikijitahidi kutengeneza mazungumzo zaidi.

"Nani, Doris? Eeh. Yuko vizuri," akasema hivyo.

"Ni mabinamu, si ndiyo? Na ni upande wa baba au mama?" nikamuuliza hivyo.

"Aaa... ni... ukoo wa baba sanasana..." akajibu hivyo huku akiwa bize na simu.

"Ahah... sorry, inaonekana uko bize, nakuvuruga tu hapa. Ngoja ni...."

"Oh no, haunivurugi wala. Nilikuwa tu na... natuma email hapa... nimemaliza," akasema hivyo na kuniangalia.

Nikatoa tabasamu hafifu.

"Na wewe? Ulikuwa unaongea na nani kwenye simu? Baby?" akaniuliza hivyo kiutani.

"Aa wee... ahahahah..." akanifanya nicheke kidogo.

Yeye pia akacheka kidogo.

"Sinaga habari hizo mimi..." nikamwambia.

"Mmm, sawa," akafanya hivyo kikejeli.

"Ilikuwa ni mama bwana. Alikuwa ananisalimia," nikasema hivyo.

"Aaa, kumbe ndiyo maana. Nimesikia unaongea kwa sauti ya kudeka, nikafikiri ni baby," akanitania.

"Ahahah... hapana. Me niko single," nikaongea kwa kujitutumua.

"Mmmm..." akafanya hivyo.

"Nini sasa, hutaki?" nikamuuliza hivyo nikiwa najihisi raha sana kuongea naye namna hii.

"Mhm... haya bwana. Mama hajambo?" akabadili mada.

"Eeh, yuko poa. Wako tu sa'hivi wanasubiria dada yangu ajifungue."

"Ooh, kumbe dada yako mjamzito?"

"Ndiyo. Sikuwahi kukwambia?"

"Hapana, ulishasema tu kwamba una dada, sikujua kama anakaribia kujifungua," akasema hivyo.

"Well, yupo karibu sana kujifungua. Kama siyo mwezi huu, basi ujao mwanzoni," nikamjulisha.

"Okay. Hongera kwake. Na yupo na mama na baba yenu?"

"Yeah."

"Sawa. Uliwahi kusema nyie mme... tokea Mwanza eh? Familia nzima yaani?"

"Aaa... ni mimi, dada yangu Jasmine, na mama sanasana. Dar es Salaam tumekuja hasa baada ya mama kufunga ndoa na huyu mzee wetu miaka kadhaa iliyopita..." nikamweka wazi.

"Ahaa..."

"Eeeh. Mume wake na mama yangu ndiyo... aliyefanya mama na dada wakaja Dar, ila me tayari nilikuwa nimeshakuja huku na wao walipofika pia," nikamwambia hivyo.

"Sawa. Ni vizuri. Na huyo mzee wako yuko poa eh?" akauliza hivyo.

"Sana. Yuko peace mno. Amenisaidia kwa vitu vingi, mpaka hapa nilipo amechangia kwa mengi sana," nikamwambia hivyo.

"Je... baba yako mzazi kabisa?"

Nikaangalia pembeni kwanza na kusema, "Simfahamu."

"Kwa nini?" akauliza hivyo.

"Sikuwahi kumwona. Alinitelekeza mimi na Jasmine tukiwa wadogo mno, yaani... alimwacha tu mama... akaenda wapi sijui... ndiyo hivyo, mpaka leo," nikamwambia.

"Pole kwa hilo," akasema hivyo.

"Hamna tabu wala," nikamwambia.

"Kwa hiyo mlilelewa na mama yenu peke yake? Hujawahi kumtafuta baba yako?" akaniuliza. 

"Wa kazi gani sasa?" nikamuuliza pia kwa sauti tulivu.

Akabaki kimya na kuendelea kunitazama kwa utulivu.

"Jasmine alikuwa na miaka miwili sijui, na mimi bado hata nilikuwa sijaanza kusimama, jamaa akakimbia. Maisha hayakuwa rahisi kwa mama kutulea akiwa peke yake, na hakuwahi kumtafuta, sijui... msaada? Hapana. Alipambana, na Mola akamsaidia, tukakua, tukafika sehemu... na yeye sasa hivi yupo sehemu yake ametulia. Ya nini tena kuanza kusumbuka kutafuta watu wasiojali kutuhusu?" nikamwambia hivyo.

Akaonekana kutafakari maneno yangu kwa ufupi, naye akasema, "Kwenye maisha hata mie nimeshajifunza kupokea na kuthamini zaidi kile nachopata kwa kuwa nakihitaji, siyo kukitaka. Hata me sikumpata baba niliyemtaka, ila nikapewa baba niliyemhitaji, na kwa hilo nikaridhika. La muhimu tu ni kuridhika, na naona ndivyo ilivyo kwako. Kama inakupa amani zaidi usipohangaika kumtafuta, basi hiyo ni sawa," Miryam akasema hivyo.

Kauli yake ilieleweka, lakini sikuelewa vizuri sana alimaanisha nini aliposema hivyo kumhusu baba yake yeye, nami nikataka kuulizia upana wa maana ya maneno hayo.

Nikasema, "Ndiyo, ni kweli unavyosema. La muhimu ndo' hilo, sionagi faida kuangalia hayo mambo, nimeridhika na jinsi maisha yanaenda kwa uweza na baraka za Mola..."

Akatikisa kichwa chake taratibu kukubaliana na hilo.

Nikaanza kumuuliza, "Ila, Miryam... umemaanisha nini uliposema kwamb..."

"Mimiii..." 

Sauti ya Bi Zawadi kutokea ndani ikasikika ikimwita bibie namna hiyo, naye akaitika.

"Bee... ngoja nione ikiwa wageni wanahitaji kitu fulani, na... ninapakua muda si mrefu, usikimbie," Miryam akasema hivyo na kuanza kuondoka.

Nikamtikisia kichwa kukubali hilo huku nikitabasamu, naye akaelekea ndani kwao.

Nikaendelea kusimama hapo nikiwa nimeegamia ukuta, tafakari za mambo mengi yaliyohusiana na maongezi yangu na bibie Miryam zikiwa zinazunguka kichwani, kisha nikatoa simu kuangalia muda na kukuta ni saa mbili kasoro robo hivi. Nikawaza labda tu nielekee hapo ndani pia, sijui walikuwa wamemwita Miryam kwa masuala ya kuivisha, lakini jambo fulani likavuta umakini wangu.

Kutokea upande ambao ulielekea kwenye bomba la maji nje ya nyumba hii, jicho langu likaanza kuona kama mwanga fulani uliokuwa ukishtua-shtua, nami nikatazama huko na kutambua kwamba ilikuwa ni mwanga wa tochi ya simu uliozimwa na kuwashwa kwa makusudio ya kuvuta uangalifu wangu. Kwa sababu taa ya upande huo ilikuwa imeungua na kutobadilishwa bado, isingekuwa rahisi kumwona usoni aliyekuwa akinifanyia hivyo, lakini nikamtambua. Ilikuwa ni Dina.

Alikuwa ameegamia ukuta wa nyumba uliokaribiana na ukuta wa uzio kuelekea nyuma kabisa ya nyumba hii, na kwa kuwa yeye angeweza kuniona mimi hapo nilipokuwa nimesimama, nikamtolea ishara kwa mkono kuwa aje, lakini yeye ndiyo akatoa ishara kuwa nimfate. Yale mambo ya 'kumchum kumchum,' yaani nyatia nyatia. 

Nikaona isiwe shida, nikaenda mpaka hapo, naye akasogea mpaka usawa wa sehemu ambayo kulikuwa na chumba cha nje ambacho ndiyo kilitumiwa kutunzia vifaa vingi vya nyumbani, stoo yaani, na kijengo chake kidogo kiilifanya njia ya kuzungukia mpaka huko nyuma ya ukuta wa uzio iwe nyembamba, na yeye ndiyo akasimama hapo. Inaonekana alikuwa ameniita kwa yale madhumuni ya 'sisi wawili tu,' na kulielewa hilo kukanifanya nimkaribie zaidi na kumsemesha kwa sauti ya kunong'oneza.

"Vipi Dina?"

Alikuwa ameukunjia mguu wake mmoja mbele huku mikono akiiegamiza ukutani, naye akajibu kwa kunong'oneza, "Ndiyo nimepata nafasi kuja nje... nikakuona."

"Umepitia mlango wa huku nyuma?" nikamuuliza.

"Eeh..."

"Nani kakufungulia? Tesha?"

Akatikisa kichwa kukubali.

"Dah! Mbona unataka kunitia majaribuni afu' tuko kwa watu?"

Akatabasamu na kuuliza, "Majaribu yapi tena?"

"Kwani we' umeniita gizani ili iweje?"

"Si ili nikuone?"

"Kwenye mwanga ulikuwa hunioni?"

Akacheka kidogo na kuuziba mdomo wake eti kwa madoido. 

"Wanafanya nini ndani sa'hivi?" nikamuuliza.

"Wamemwita aunty Miryam ili waongee kidogo, halafu wapakue sijui... me ndiyo nikachomoka," akasema.

"We' chautundu kumbe? Halafu unajifanya malaika..." nikamtania kidogo.

Niliweza kuona Dina akitabasamu kiasi na kung'ata mdomo wake wa chini, kisha akashika T-shirt langu kwa kidole kimoja sehemu yenye uwazi shingoni na kuanza kulivuta kumwelekea. Ilikuwa wazi kwamba alitaka nimfate mdomoni ili tupige denda, nami nikaona isingekuwa mbaya kuionja midomo yake kwa mara ya kwanza. 

Nikaifata na kuanza kunyonyana naye midomo, ulimi, meno yakigongana, huku nikiwa nimekishika kiuno chake, naye akajisogeza karibu yangu zaidi na kuizungushia mikono yake mgongoni kwangu. Kwa sababu alikuwa mfupi ilinihitaji kuinama kiasi ili asinyanyue miguu yake, na tayari hamu ilikuwa imenipanda mno kufanya msuli wangu ukaze ile mbaya, na ukikandamiza tumbo lake kwa nguvu.

Hatimaye nikaivunja busu hiyo na kugeuka nyuma kuangalia usalama, kisha nikamtazama na kusema, "Aisee... Dina! Umeniwashia balaa."

"Mhm... unataka nilipoze?" akasema hivyo na kuishika mashine yangu ikiwa ndani ya suruali, kisha akawa anasugua-sugua hapo.

Nikamwambia, "Hapa jau. Tutapanga siku nyingine."

"Me naitaka hiyo jau sasa hivi..." akasema hivyo.

"Dina!" nikashangaa.

"Kidogo tu..."

"Dina, mazingira. Tutakutana siku nyingine..."

"Kidogo tu JC..." akawa ananibembeleza kama vile anataka kulia.

"Tuko kwa watu Dina, umekuja kama mgeni... kwanza ndo' wanapakua. Wakikutafuta wakatukuta? Halafu kwanza me nimebanwa kukojoa..."

"Nikojolee tu mimi..." 

"Wewe!" nikamshangaa.

Akaendelea tu kupasugua pale pagum-gum.

Nikamuuliza, "Kwa hiyo utarudi ndani unanuka mikojo? Mbona umekuwa hivi?"

Akasema, "Nina hamu sana na wewe, JC. Na ni muda mrefu..." 

Masikini! Mpaka nikamwonea huruma. Mwanadada alionyesha kuwa na hamu kali kwelikweli, na mimi ningekuwa nani kumnyima msaada? Eti? 

Pamoja na kuwazia usalama wetu kutokana na mazingira, nikaamua nimpe utamu angalau kidogo. Nyakati kama hizi ndiyo mwanaume unatakiwa uchukue maamuzi ya haraka kwa kutumia akili, na ujanja unahusika pia. Hapo nilikuwa sijambo. 

Nikaona nimsogeze Dina nyuma zaidi ili tujibananize kwenye kile kinjia cha kuelekea nyuma, na nikamfikisha kwenye sehemu ambayo ukuta ndiyo ulikunja kona. Kwa hiyo, mimi nikawa nimesimama upande huu ambao tulikuwa, huku mwili wake ukiwa kwa upande ule wa nyuma, kwa hivyo ingekuwa rahisi kuona kama mtu angekuwa anakuja upande wangu au upande wake. 

Dina alikuwa ameshaanza kuhangaika na zipu ya suruali yangu, lakini mimi nikaishika mikonp yake na kuugeuza mwili wake ili anipe mgongo, halafu yeye akajiongeza na kuanza kuishusha suruali yake na chupi nyekundu aliyovalia kwa ndani. Alikuwa na mwili mweusi, na upande huu wa nyuma taa ilikuwa ikiangaza, lakini ukuta ulituficha vizuri. Nilikuwa nahisi msuli wangu umekaza ile mbaya, si unajua mara ya kwanza na mtu mwingine inavyokuwa? Maua! 

Mtoto akauegamia ukuta huku akinibinulia kalio lake lisilo kubwa sana, nami nikafungua suruali yangu pia na kuishusha, nikiiachia mashine itambe. Hapa shida kubwa ingekuwa mbu, walipiga kelele yaani utafikiri kulikuwa na sherehe, lakini siye hatukuwajali hata kama wangeng'ata vipi. 

Dina akapandisha mshati wake juu vizuri huku akijaribu kunigeukia ili aniangalie, nami nikaanza kukichokonoa kitoweo chake kutokea nyuma kwa vidole vyangu, na kilikuwa kimelowana haswa. Nikapakaa kidogo ute huo kwenye mashine yangu, kisha nikakiingiza kichwa kidogo ndani yake na kumshika mgongoni kwa mkono mmoja kama namkandamiza ainame chini zaidi. Hakuwa mbishi. Nikaanza kuingiza mtambo ndani zaidi na kumkuna taratibu tu, kisha nikakishika kiuno chake kwa mikono yote na kuanza kukoleza utamu. 

Aisee! Dina alikuwa na kitu cha moto, halafu muda mwingine nilihisi kama kinanikwangua kabisa. Nilielewa kuwa sikumlainisha vya kutosha huko chini, kwa hiyo nikajitahidi nisimtandike kwa nguvu mno. Yeye mwenyewe alionekana kufurahia za taratibu, na mimi nilikuwa makini kuangalia huko mbele na huku nyuma kuhakikisha usalama, na show ikaendelea kwa dakika kama mbili hivi, kisha nikaichomoa mashine. 

Bado ilikuwa imewamba, lakini nilitaka kumwambia Dina tuishie hapo. Sasa sijui shauri ya mazoea? Kabla hata sijamsemesha, mwanadada akanigeukia na kuchuchumaa, naye akaishika mashine yangu na kuitumbukiza mdomoni mwake. Ai kubabake! Maneno yakapotea. 

Nikawa naisikilizia midomo yake ilivyokuwa inaukuna mtambo wangu taratibu, na alipenda sana kuzungusha ulimi kwenye kichwa, kisha akasimama tena na kugeuka kwa mtindo ule ule. Inaonekana aliihitaji ikiwa na ulaini zaidi wa mate yake, nami nikaona nisimvunje moyo. Nikaingia tena. 

Piga za kistaarabu tu kwa mtindo mmoja, na zile 'ahh sss' zake ndiyo zikawa zinasikika zaidi wakati huu lakini kwa sauti aliyoibana. Pamoja na umbo lake lisilo kubwa lakini mtambo wangu mrefu ulikuwa unazama wote, na inaonekana aliufurahia zaidi ulipofika kwenye mabandama huko. Akalishika T-shirt langu na kuling'ang'ania kwa nguvu huku akijitahidi kunigeukia na kuniangalia, na macho yake yalikuwa yamelegea haswa. 

Niliridhika tu kwamba hakutoa sauti ya juu sana maana kule ndani walitulia, na utamu kolea, utamu kolea, changu cha kwanza chenye kiherehere kikaja upesi ndani ya dakika saba tu. Nilikuwa natamani nijiachie ndani yake yaani, ila... hapana. Sikuwa na uhakika kuhusu faida na hasara za jambo hilo kwa huyu dada. Nikamwonya tu kuwa mi' nakaribia, naye akafanya kitu ambacho sikuwa nimetarajia. 

Akajichomoa kutoka kwenye mashine yangu na kunigeukia tena, kisha akachuchumaa na kuishika, halafu akaanza kuinyonya na kuichua haraka-haraka sana. Dah! Alitaka nimwage, na alitaka yammwagikie mdomoni. Alikuwa ameshaangalia ujinga mwingi wa wazungu huyu mtoto kama siyo kuufanya! 

Nikaona nimpe, maana kweli nilikahitaji hako kahisia na mimi, ndipo vitu vikaja na kunifanya nimwagilie mdomo wake huku nikijikaza nisitoe sauti ya juu ya mridhiko. Kumwangalia Dina, nikakuta akiwa analamba mashine yangu huku ikionekana kila kitu alikuwa amekunywa. Kila kilichotoka! Dah, kweli hiyo ndiyo ilikuwa hamu. Na siyo mbaya, mtoto akawa ameongeza glucose mwilini. 

Baada ya hiyo pindi yenye kusisimua, nikavuta suruali yangu, naye pia akasimama na kujiweka sawa zaidi. Nikamtazama usoni na kuona jinsi ambavyo aliniangalia kwa njia iliyoonyesha furaha, ile ya kimahaba, nami nikamfuta mate kidogo pande za mdomo wake.

"Nenda ndani sa'. Umeridhika?" nikamuuliza.

Akatikisa kichwa mara moja kukubali.

"Au unataka tuendelee?" nikamuuliza tena.

Akatikisa nyusi kukubali.

"Oh no... imetosha kwa leo. Tukikutana siku nyingine haitakuwa quickie, sawa? Utafurahia zaidi, kwa hiyo andaa namna ya kumkimbia bwana'ako," nikamwambia hivyo.

Akacheka kwa pumzi fulani ndefu, huku akikileta kichwa chake mpaka kifuani na kukilaza hapo kwa njia ya aibu na kudeka eti. Ih!

Nikamshika na kusema, "We', usisinzie hapa, nenda ndani. Pita hapo, me napitia huku... uende unawe huo mdomo, afu' utulie kama vile hatujuani. Usilegeze hayo macho mbele ya ndugu zako..."

Akacheka kidogo kwa furaha, naye akasema, "Sawa daddy. Nimeelewa."

Alikuwa ananiangalia kwa kurembua, naughty, nami nikamwambia, "Em' nenda huko... eti daddy..."

Yanakuwaga kama mazezeta yakishapagawa!

Akageuka na kuuelekea mlango wa nyuma ya nyumba hii hapo mbele yetu, nami nikataka kurudi kupitia huku gizani mpaka pale pale nilipokuwa nimesimama muda ule na Miryam, na ile nimeanza tu kupiga hatua na kutazama mbele, nikashtuka kiasi moyoni na kusimama ghafla baada ya kukutana na mtu mwingine ambaye alikuwa amesimama hapo. Nilihisi mtetemo uliopita mwilini shauri ya kutotarajia kabisa kumwona, na ilikuwa ni binti Mariam! 

 

 

★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Previoua Next