SEHEMU YA 13.
Upande mwingine katika mtaa wa kitajiri wa Masaki ndani ya moja ya kasri la kifahari walionekana wanaume watatu wakiwa wamefura kwa hasira.
Wawili kati ya wanaume hao walikuwa ni vijana na mmoja alikuwa ni mzee wa makamo hivi.
“Alex mpango wako umeendaje , vijana wamefanikiwa?”Aliuliza mara baada ya Alex kushusha simu chini akionekana kumaliza maongezi.
“Wamepigwa wote mpaka wakazimia”Aliongea Alex kinyonge huku akikaa chini kwenye sofa.
“Nini!!?”
“Chriss sijui mpaka sasa nadili na mtu wa namna gani , lakini huyu Hamza ni mtu wa ajabu kabisa, vijana walioenda kufanya kazi ni wa kuaminika , lakini wanasema eti Hamza alifika na mwanamke na ndie aliewashambulia”Aliongea.
“Alex huna haja ya kunyongea hivyo , si umesema huyu Hamza ni mzembe mzembe ambae hana mbele wala nyuma kwanini unamkuza , kufeli kwa plan A haimaanishi Plan B imefeli pia”
“Mjomba sio kwamba nanyongea wala kumkuza , ila kama sio wa kawaida kwanini mwanamke mrembo kama Frida anamuhitaji , anaonekana kabisa kutaka kumuweka karibu”
“Upo sahihi Alex , inaonekana huyo kijana sio wa kawaida na haupaswi kumdharau , lakini kutokuwa wa kawaida haimaanishi umeshindwa vilevile , changa karata zako vizuri”
“Mjomba kwanini usiniunganishe na Chatu , wale ni wabobezi katika kazi na hawana historia ya kushindwa”Chriss mara baada ya kusikia kauli ile alimwangalia baba yake kwa umakini.
“Hawa Chatu kwanzia sasa ni maadui zangu , wameniharibia mpango wangu na Eliza na Amosi amekataa kabisa kufanya kazi ile tena”
“Baba unamzungumzia Eliza yupi?”Aiongea Chriss
“Kuna mrembo mmoja wa kampuni ya Dosam , nilikuwa nikimfatilia kwa muda mrefu sana, Chriss nadhani unakummbuka skendo ya Dokta Bensoni wa Mayaya Clinic?”
“Unamaanisha ile ya kuomba rushwa ya ngono?”
“Naona unakumbuka vizuri , sasa mwanamke ambae amemfukuzisha kazi Dokta Bensoni ni huyu mrembo Eliza , alikuwa na mama yake pale hospitalini aliekuwa akihitaji matibabu , kutokana na Eliza kukosa pesa za kulipia ndipo Dokta Bensoni aliruhusu tabia yake kumvaa na kumuomba mrembo huyo ngono, siku ambayo anadhalilishwa pale Serena nilikuwepo na ndio mara yangu ya kwanza kumuona huyu mrembo Eliza , namna alivyomkataa Dokta Bensoni licha ya shida zake ilinifanya nimuone wa
kipekee na kuanzia hapo nilitaka kumfanya awe mama yako mdogo”
“Haha.. Mzee kwahio kitendo cha Dokta Bensoni kukataliwa ukaona huyo mwanamke anafaa kuwa mama yangu?”
“Bensoni yule alikuwa rafiki yangu wa kitambo namjua nje ndani , wanawake wote ambao amepita nawajua , hawa wanawake ni wa heshima zao na amepita nao kwa kutumia mbinu ya aina moja , lakini kwa msichana masikini asie na kitu kama Eliza alimkataa , unadhani huyo ni mwanamke wa kawaida?”
“Mjomba naunga hoja , huyo Eliza sio mwanamke wa kawaida , lakini vipi mpaka sasa ukashindwa kumpata?”
“Mara baada ya tukio lile nikaona nimsaidie kwa njia za siri na baada ya hapo ndio nimtokee, hivyo nikampa kazi hio Amosi na alifanya vizuri kwani alimkopesha kiasi cha pesa ambacho alitumia kumtibu mama yake, kama kawaida yangu baada ya hapo nikajitokeza sasa kunadi sera zangu lakini yule msichana hakutaka kunielewa kabisa , nadhani kitendo cha kuonekana na Dokta Bensoni ndio kilinitia nuksi , Chriss mama yako mtarajiwa alinikataa katakata na mbaya zaidi alilipa mkopo wote na nusu riba , tukio lile lilinipandisha hasira na nadhani unajua tabia yangu , sijawahi kukataliwa na mwanamke hivyo nilitaka kumnyanyasa kidogo kumshikisha adabu ili kuulegeza msimamo wake”
“Nadhani sasa naelewa kwanini Jasusi amesema sikufahamu vizuri , nilijua hakuna mwanamke wa kukutataa , kumbe umeshapigwa cha mbavu mzee , hahaha”Aliongea Chriss.
“Nyamaza mpuuzi wewe , unamcheka vipi mwanaume mwenzo kisa kakataliwa , hii ndio maana halisi ya kukua , umri umeenda ndio maana nimepata uzoefu mpya , tokea nipate hela hakuna mwanamke ambae ashawani kunikataa na niliamini hivyo lakini Eliza alibadilisha mtazamo wangu na hii imenifanya nimpende zaidi na zaidi”Aliongea lakini Chriss aliendelea kucheka.
“Kwahio Mjomba baada ya hapo nini kikaendelea?”
“Unajua wakati namwambia Amosi ampe mkopo , nilikuwa na uhakika asingeweza kulipa maana ni kiasi kikubwa mno na hakuwa na kazi lakini mipango yote ilivurugika mara baada ya Regina kuingilia kati”
“Regina! , Unamaanisha mkurugenzi wa makampuni ya Dosam?”Aliuliza Chriss. “Ndio huyo”
“Ilikuwaje akaingilia?”
“Sijajua , ila kwa taarifa nilizopata Regina ndio kalipa kiasi chote na kisha akamfanya kuwa msaidizi wake na sekretari”
“Duh!,Mjomba sijawahi kuwaza kwa pesa zako kuna mwanamke ambae atakukataa , imani yako ilikuwa kama imani yangu , mara baada ya kukumbana na kizingiti kwa Frida nadhani najua unachojisikia”
“Mjomba umekuwa ndio maana , achana na Chriss , anadhanau sana , huu muonekano aliokuwa nao ambao unatokana na juhudi zangu ndio unamfanya kupendwa na kila mwanamke”
“Baba kila siku unajigamba kwamba muonekano wangu umetokana na juhudi , utaacha lini?”Aliongea Chirss hakupenda sana hio kauli kutoka kwa baba yake.
“Haha.. sema kweli Chriss , unajua Mjomba amehangaika kwa kiasi gani kipindi hicho mpaka akampata shangazi mhindi”Aliongea Chriss na alitaka kuongea lakini alikatishwa na simu yake mara baada ya kuangalia anaepiga aligundua ni James.
“James huyu anapiga”Aliongea na kisha akapokea.
“Uko wapi Chriss?”
“Nyumbani , vipi mbona haraka hivyo hata salamu hakuna?”
“Kuna ms**nge kanitibulia kwa Regina, niambie uko wapi nije tuone unanisaidia vipi”
“Niko nyumbani kwa mzee”
“Poa”
Simu ilikatwa palepale na kumfanya Chriss kuanza kutoa kicheko cha nguvu, hakucheka kwasababu rafiki yake ana matatizo , ila alicheka kwasababu watu wake wote wa karibu walikuwa na matatizo sawa.
“Anasemaje , mbona unacheka Chriss?”Aliuliza Alex.
“Anasema mpango wake na Regina umebuma”
“Nilijua tokea siku nyingi hawezi kufanikiwa”Aliongea Mzee Gabusha.
“Unamaanisha nini baba?”
“Yule mwanamke sio wa kawaida , hivi unadhani Mzee Dosam kwanini kamrithisha mjukuu wake kampuni tofauti na baba yake , vipi kilichotokea mara baada ya kurithishwa? , IQ ya yule mwanamke inasemekana ni kubwa mno tokea akiwa mtoto na inasemekana akiwa na miaka mitano aliendwa kutengenezwa”Aliongea na kumfanya Alex na Chriss wote kushikwa na shauku.
“Mjomba unamaanisha nini kutengenezwa?”
“Hata mimi sijui kwasababu ni swala ambalo hata raisi wa nchi hii hawezi kujua, ila tetesi nilizosikia ni kwamba sio binadamu wa kawaida, hili ni swala nyeti sana msije kulisambaza , mimi mwenyewe siamini ila mtu alieongea kauli hio ni mtu anaejua siri nyingi”
“Dunia ina siri nyingi sana hii baba , hasa baada ya wazungu kuishi nchiin kwetu kwa muda , lakini kauli yako inaniogopesha na kuona mshikaji wangu James anajiingiza kwenye matatizo”
“Haha…James ukweli ni kwamba hana uwezo wa kumpata Regina sio yeye tu hata mimi na wewe , ijapokuwa yule mwanamke ni mrembo na ananivutia lakini najua ukomo wangu,, Mzee Wilsoni na Lamla wanafosi tu kumsapoti James kwasababu ya uhusiano wa familia zao , ila sidhai malengo yao kama yatatimia”
“Tena nimekumbuka , una dili gani na Jasusi?”Aliuliza Mzee Gabusha akimlenga Chriss alikuwa na dili gani na Amosi.
“Hakuna dili la siriasi kihivyo , kuna mipango yangu ya kibiashara niliomba anisaidie?”
“Chriss hakikisha hujiingizi katika maswala ya hatari , taarifa zimenifikia ni wiki ya pili sasa unajihusisha na wale wachawi kutoka Brazil”
“Baba umejuaje?”
“Nina njia nyingi za kujua kila kitu , Lile kanisa la
Wabrazil lipo chini ya Rada za jeshi kitengo cha MALIBU , Sijui nini kinachoendelea lakini kuwa makini , fanya ufanyavyo hakikisha hufi kabla ya kuniletea mrithi”
“Kama MALIBU kweli wanalifuatilia lile kanisa , Chriss zingatia ushauri wa mjomba , nimesikia licha ya mafundisho yao kuendana na ya kikristo lakini pia wanasisitiza mambo ya spiritism”Aliongea Alex.
“Kuna kitu kilichonipeleka pale na sio swala la ibada Alex , ni swala la kibiashara , ukiwa mfanya biashara hutakiwi kifungwa na imani za watu”Aliongea Chriss na muda uleule mlango wa sebuleni ulifunguliwa na James aliingia.
Alikuwa akijulikana hapo ndio maana hakuwa na haja hata ya kugonga mlango , James , Chriss , Alex walikuwa ni marafiki tena waliosoma shule moja , Alex na Chriss walikuwa ndugu huku James yeye akiwa rafiki yao , wote hao walikuwa wakisifika kama wazee wa makoloni, yaani mwanawake wao walikuwa wakimwita Koloni na wakimpata wanasemea wana’colonize’, wakimuacha aidha ni kwa uhuru wa bendera au kwa kumwaga damu , zilikuwa ndio lugha zao za ujana.
Mzee Gabusha hakuwa amepishana sana umri na mtoto wake Chriss na ndio maana muda mwingi walikuwa wakionekana kama marafiki , inasemekana Mzee Gabusha akiwa na miaka kumi na sita tu ndio Chriss alizaliwa mara baada ya kutoka kimapenzi na mwanamke wa kihindi ambae mara baada ya kujifungua alitoweka.
“Aisee kwa sura hio , kweli inaonekana sio kwema”Aliongea Alex.
“Mjomba habari za saa hizi?”Alisalimia James huku akijitahidi kujituliza.
“Kaa kwanza chini James”Aliongea Mzee Gabusha akiwa na shauku ya kutaka kujua nini kimetokea , ijapokuwa alijua Regina hakuwa mwanamke wa kawaida lakini alikuwa na shauku.
James mara baada ya kukaa chini alichukua glasi iliokuwa na kilevi , hakujali nani alikuwa akitumia hio glasi na alishusha pombe yote.
“Nini kimetokea James?”
“Leo Regina kamtambulisha boyfriend wake mbele yangu na mbele ya wazazi wake”Aliongea.
“Nini!!?”
“Ndio hivyo na huwezi kuamini huyo fala ni choko tu hana mbele wala nyuma , lakini namna alivyokuwa akijiamini mbele ya Regina ndio inanitia hasira zaidi na zaidi”Aliongea na kumfanya Alex na Chriss kuangaliana na kisha wakamgeukia Mzee Gabusha.
“Sasa hivi nimepokea taarifa huyo fala kahamia kabisa nyumbani kwa Regina”
“Unatania James , mwanaume gani wa kumfanya Regina alegee mpaka kwenda kuishi kwake, sidhani kama ni kweli?”Aliongea Chriss.
“Hata wewe umeona eh , kuna hisia zinaniambia yule choko yupo kwenye maigizo na Regina kwasababu ya mimi kulazimisha ndoa”
“James punguza jazba , ushasema huyo mtu ni choko halafu amekukasirisha hivyo ,basi anaonekana sio mtu wa kawaida”
“Mjomba sio kama namkuza . lakini kama hili likiendelea mipango yangu mingi inafeli , napaswa kumuoa Regina kwa haraka la sivyo dili na wale wachina litakuwa limekufa rasmi, baba nae kanikaa kooni”
“Bora wewe unamtaka Regina kukamilisha mipango yako , lakini James ni biashara gani hio ambayo inakutaka umuoe Regina kwanza ndio dili liendelee?”Aliuliza Alex.
“Alex magizo yako unayoyafanya pale FEMU ndio yanakupotezea muda na mambo mengi huyajui”Aliongea Chriss.
“Nina sababu za kuwa pale FEMU Chriss, mambo sio rahisi kama unavyodhani”
“Tuachane na hayo , Alex kuhusu wachina ni siku nyingine , nataka kujua namna ya kudili na hili swala haraka , mjomba naomba umsaidie kumpoza baba ni rafiki yako na anakusikiliza”Aliongea.
“James haina haja ya kuwa na wasiwasi, mimi na baba yako ni wafadhili wa wakuu wa Mheshimiwa Jongwe , kama ataingia madarakani kitu ambacho nina uhakika nacho asilimia mia fursa zitakuwa nyingi za kuirudisha ampuni yako katika mstari , kama unamtaka huyu Regina kwa ajili ya kampuni yako nadhani unapaswa kuachana nae , nitaongea a baba yako na atanielewa”
“Mjomba ukweli nampenda sana Regina , ijapokuwa ni kweli kwa namna nyingine nataka kukamilisha mipango yangu kupitia yeye , lakini moyo wangu unampenda sana na sipo tayari kuona mtu yoyote anamchukua”Aliongea na kumfana Chriss na Alex kuangaliana.
“Kwahio unataka tukusaidie nini James ?”Aliuliza Alex.
“Hisia zangu zinaniambia kabisa yule mpuuzi anatumiwa na Regina ili kuzuia mchakato wa ndoa usiendelee , ninachotaka ni vijana waingie kazini , atekwe na baada ya hapo apewe kibano nijue ukweli kwanza na kisha tumpe onyo la kukaa mbali na Regina”Aliongea James huku akionekena alikuwa akimaanisha kwa namna ya kauli aliokuwa akiongea.
“Hio kazi ni ngumu kukusaidia James , hiki kipindi ni cha uchaguzi na mimii ni mdhamini namba moja wa mgombea wa uraisi, kosa kidogo tu wapinzani watatumia kama siraha ya kujinadi, James mimi kama mjomba wako na rafiki wa baba yako swala la Regina achana nalo kwasasa , najua kampuni yako ipo karibu kufirisika lakini uchaguzi ukipita tenda zote za kiserikali zitakuja kwetu , hii ndio maana ya
mimi na baba yako kuwa kidedea kuhakikishaJongwe anaingia ikulu, wewe ni mwanaume zipo njia nyingi za kumpata Regina
kama kweli una nia basi sio lazima kutumia fujo, labda kama wewe mwenyewe huamini uwezo wako wa kutongoza mwanamke”
“Mzee unaongea sana ki utu uzima , katika hali hii ya James wote tupo katika ‘ground’ moja , wewe mwenyewe njia zako za kawaida zimekushinda zidi ya…”
“Chirss usivuke mpaka…”Alionya Mzee Gabusha na palepale alisimama na kuondoka.
“James mimi pia nipo kwenye tatizo kama lako , hapa Chriss ndio anajiona mshindi tu lakini hana ushindi wowote, ni mwezi wa ngapi huu tokea aanze kumfatilia Prisila lakini anatolewa nje”
“Alex unataka kusema nini…”Aliongea Chriss huku macho yake yakibadilika na kuwa ya usiriasi.
“Ninachomaanisha ni kwamba sisi kama marafiki hili ni swala la kusaidiana, njia zipo nyingi sana”
“Njia hazipo nyingi sana , njia ambayo mnataka kufanya ni kama ambayo umeifanya muda uliopita na haijakupa majibu”
“Njia gani ulifanya Alex?”Aliuliza James,.
“Kuna choko mmoja ametengeneza ukuta kati yangu na Frida , leo niliwapa kazi vijana kwenda kupekuwa anapoishi kutafuta ni kitu gani anaficha mpaka Frida kumuhitaji , lakini wapuuzi wale wameambulia kipigo mpaka kuzimia”
“Haha.. Alex wewe umafia huujui , kama umetuma vibaka ulitegemea nini , tena wanaenda mchana kweupe”Aliongea James.
“Huna unachokijua James nyie wote wawili hamjui ni hustle ngapi nimepitia mpaka leo hii ni meneja wa usambazaji wa viungo vya akili na sasa pesa ninayo na tunazungumza lugha moja , mimi sio kama nyie utajiri mmeukuta , mimi nimeanzia chini na huko chini mambo mengi yametokea, umafia naujua sana tu”
“Huu sio muda wa kujisifia , nina miadi na Prisila leo hivyo kwasasa nashauri James usikilize ushauri wa mshua na wewe Alex … tafuta sababu kwanza kwanini hilo koloni linamtaka mwanaume mwingine na sio wewe , pengine unachokiwaza sicho kabisa” “Unamaannisha nini ninachokiwaza sicho?”
“Wewe unamjua Frida vizuri nje ndani , yule mwanamke umesema kakulia nje ya nchi na ni juzi tu hapa karudi , unadhani unamjua vizuri nje ndani, Vipi kuhusu viungo vya akili , kwanini anatumia? , wewe unawatafuta wateja ?, si Binamu ndio wanatafuta wateja na wewe ndio unafanya usambazaji tu?”
“Upo sahihi Chriss , kitendo cha Frida kuwa mteja wangu ni ishara namba moja sio wa kawaida , lakini sheria ya kazi yangu inanizuia kumfuatilia”
“Ndio ujiulize unaitaka kazi au unamtaka Frida”Aliongea na kisha aliondoka.
“Chriss unaenda wapi sasa , hatujamaliza swala langu” “Nimemuacha Anitha tayari kwasababu ya Prisila , lazima nimkomalie la sivyo nitaishia kuita ya Delivery”Aliongea na kutokomea nje.
“Unapanga kufanya nini James?”
“Kwasasa nitatafuta namna yoyote ile ya kumlazimisha Regina akubali ombi langu la ndoa , kwa hizi dharau ambazo amenionyeshea leo lazima nimfanye alie kilio cha mtoto akiwa kitandani , tuone kama ataendeleza maringo yake”Aliongea James kwa hasira na kisha alisimama na kuondoka.
Alex mara baada ya kuona ameachwa peke yake alijiambia na yeye lazima Frida awe wake kwa namna yoyote ile,. Hata kama itakuwa ni kumuua Hamza ikitokea wana mahusiano.
*****
“Shangazi , nimerudi”
Ilikuwa ni saa kumi na mbili kamili wakati Regina akisukuma mlango wa kuingilia nyumbani kwake na mara baada ya kufika katika sofa alijirusha kwa kujiachia kiasi kwamba nguo aliovaa iliyaacha mapaja yake wazi huko koti la suti akitupa kule.
Baada ya kujinyoosha kidogo hatimae aligeuka akiitafuta rimoti ilipo ili awashe TV lakini hapo ndipo alipokumbana na sura chafuchafu iliokuwa ikimwangalia kwa tabasamu kutoka nyuma ya sofa.
“Regi naona ndio unarudi”
Hamza alikuwa ameshikilia Screwdriver kwenye mikono yake , alikuwa hajavaa hata shati zaidi ya libukta kubwa kubwa hivyo kuacha wazi mwili wake uliojengeka kimazoezi.
Ni muda huo huo Regina alikumbuka kuna mtu ambae ameongezeka nyumbani kwake na kwa namna ambavyo amejiachia alijikuta akiwa mwekundu kama nyanya na haraka sana alisimama na kujiweka sawa
“Muhuni sana wewe , unaangalia nini!!?”Alibweka huku akimsukuma Hamza ambae alikuwa nyuma ya sofa akimchungulia.
“Regina unafanya nini , kwahio siruhusiwi kukaribisha nyumbani”Hamza alijitetea mara baada ya kupigwa.
“Kwanini unaangalia kifua changu ..”Aliongea huku akiziba kifua na mikono yake miwili.
“Halafu kwanini huna nguo?”
“Naongea na wewe ndio maana nakuangalia na siangalii kifua , ni kama ishara ya heshima tu , kuhusu nguo zangu ni kama tabia ambayo na wewe unayo ukifika nyumbanni na kuvua nguo zako na kujiachia”
“Hii ni nyumba yangu na sio yako , huruhusiwi kutembea kifua wazi “Regina alikuwa na tabia ya ukimya sana na hio ni mara yake ya kwanza kuongea kwa sauti hivyo hasa kwa maeneo ya nyumbani,alikuwa na hasira kweli.
Aliishia kujilaumu yeye mwenyewe kwa kuona kwamba hakuchagua mtu sahihi kwa kuamini mwanzo ni mtu mzuri kumbe sivyo.
Hamza mara baada ya kuona mrembo huyo alivyokasirika aliamua kuvaa shati lake haraka haraka.
Regina aligeuza shingo yake mbali asimwangalie Hamza lakini alikuwa ashaona kifua chake na mgongo wake na mapigo ya moyo yalisimama.
Ilikuwa mara yake ya kwanza kuona mwanaume kuwa na mwili mzuri hivyo , ijapokuwa Hamza mwili wake haukuwa umetuna sana kimisuli lakini ulikuwa umebalansi vyema.
“So this chap actually do Gyms?”Ndio yalikuwa mawazo yake muda huo na haraka sana alitingisha kichwa chake na kujiambia anafikiria ujinga gani.
Mara baada ya kuona tayari Hamza ashabadili mavazi alisimama na kwenda kuchukua rimoti kwa ajili ya kuwasha TV, mara baada ya kuipata na akiwa anataka sasa kuwasha aliweza kugundua kuna kitu hakipo sawa na mdomo wake mzuri ulipanuka kwa mshangao
“Wewe.. wewe ,, umeifanyia nini TV yangu ?”
Regina hakuamini TV yake ya kisasa na ya bei ghali hivyo ilikuwa imetolewa ukutani na kufunguliwa funguliwa.
Comments