SEHEMU YA 14.
Roma alikuwa ameshikilia Screwdriver na ni kweli alikuwa ameifungua Tv na alikuwa bize kuitengeneza ndio maana hata wakati ambapo Regina anaingia hakuweza kumuona kwasababu alikuwa ameinama akiwa bize.
“Oh … nilikuwa nikiangalia Tv muda si mrefu lakini niligundua ilikuwa na ukungu hivyo picha kutoonekana vizuri ndio maana nimeifungua kuitengennea , subiri kidogo na maliza muda si mrefu”
Regina pumzi ni kama zilitaka kumkata na alijitahidi kujituliza kwa kuvuta hewa nyingi na kuishusha.
“Hivi unajua imenigharimu kiasi gani kununu hio Tv?”
“Milioni moja nahisi”
“Ongeza nane”
“Milioni moja na nane”
“Wewe mjinga , ni milioni nane”
“Duuh kumbe ghali hivi , ndio maana inaonekana kuwa ya teknolojia ya juu”
“Sasa wewe kuona ukungu kidogo tu ndio ukaifungua , unajua kuirudisha kama ilivyokuwa , unajua Tv zinavyofanya kazi?”
“Ngoja tuone kama nitaweza kuitengeneza”
“Uone kama unaweza , seriously?”
“Regina kwanini unagombana na Hamza , yaani ndio umerudi unachoanza ni kufoka?”Aliongea Shangazi Mariposa ambae alitoka jikoni mara baada ya kusikia makelele ya Regina kufoka.
“Shangazi kwanini umemruhusu afanye hivi ,ameharibu Tv”
“Kumbe ndio kilichokukasirisha , hebu muache aitengeneze akishindwa tunaweza kununua nyingine tu au kumwita fundi”Aliongea akiwa na tabasamu na kisha alimgeukia Hamza.
“Hamza harakisha , muda wa chakula unakaribia” “Sawa , ndani ya dakika tano nitakuwa nishamaliza”
Regina aliishia kumwangalia shangazi yake na Hamza wanavyoongeleshana na aliona kuna kitu hakipo sawa , imekuwaje wamekutana leo lakini wanaonekana kuzoeana kama wameishi pamoja muda mrefu.
Regina wakati akimwangalia Hamza akizungusha nati na kukunja kunja alitamani kumtupia rimoti.
“Acha kuzidi kuiharibu , utailipia ikiharibika kabisa”
“Haiharibiki , you must trust your man”Aliongea Hamza akiwa anajiamini
“Huna aibu kabisa”Aliongea.
Regina hakuwa na uwezo wa kufanya chochote kwa wakati huo na wakati alipogeuka aliweza kumuona Shangazi Mariposa akimwangalia huku akitabasamu , alionekana kufurahi namna ambavyo Regina alikuwa amekasirika na kufoka , ilikuwa ni mara ya kwanza.
“Shangazi , ongea chochote , huyu mtu kaja kusababisha matatizo tu hapa”
“Mimi ni mzee , unaniambia vipi niingilie mahusiano yenu changa, ngoja nijipikie zangu , mnaweza kufanya mnachotaka”Aliongea
“Nini , mahusiano changa..”Regina ni kama hakuwa amesikia kauli ile vizuri lakini Shangazi alikuwa tayari ashakimbilia jikoni, hata hivyo alikuwa akijua Hamza na Regina ni wapenzi kweli maana hakumwambia kama ni feki.
Aliishia kuondoa kibanio cha nywele zake kama kwamba kufanya hivyo kichwa chake kitakuwa chepesi kutokana na hisia hasi alizokuwa nazo.
Muda ambao chakula kishaiva Hamza na yeye alikuwa ashamaliza na kuirudisha sehemu yake.
Regina kwa haraka haraka alichukua Rimoti na kuwasha lakini mara baada ya kubonyea mara kadhaa Tv haikuwezekana kuwaka.
“Angalia ulichofanya sasa”
Alilalamika kwa hasira , sio kwasababu alikuwa akijali sana kuhusu Tv kuharibika maana hela za kununulia mpya anazo lakini alikuwa na hasira kwa kitendo cha Hamza kujimilikisha nyumba yake na kuanza kuharibu vitu.
“Regina , umeshikwa na homa?”Aliongea Hamza na kutaka kumuwekea Regina kiganja cha mkono wake kwenye paji la uso lakini mkono wake ulibetuliwa.
“Homa gani ,acha kubadilisha topiki , si ulikuwa ukionekana kama vile fundi mjuzi tu , sasa umeharibu Tv na unatakiwa kunilipa”
“Hey mrembo , hivi Tv inawaka bila ya waya wake wa umeme kuchomekwa kwenye kebo?”Aliongea Hamza huku akiwa ameshika kiuno
Shangazi wakati akitoka jikoni na kusikia kauli ya Hamza aliishia kugugumia kwa kuzuia kicheko.
Regina alishangaa kidogo lakini alificha mshangao wake kama kwamba anapotezea.
“Kutokuchomekwa haimaanishi imefaa”Aliongea na kisha akachomeka kebo kwenye umeme na baada ya hapo alibonyeza na chombo kiliwaka na kuanza kuonyesha picha katika ubora wa hali ya juu.
“Aiyaa ,, naona kweli kale kajiukungu kamepotea , Hamza unaonekana kuwa fundi mzuri”
“Fundi wapi shangazi , kabahatisha tu haina haja ya kumsifia , isitoshe kutengeneza sio jambo kuubwa ki hivyo”Aliongea huku akimwangalia Hamza kwa kutompa sifa zake.
“Mbona kama unajaribu kunitengenezea cha kuongea , sijasema kutengeneza Tv ni jambo kubwa , mimi nimesema nitaitengeneza na imefaa”Aliongea lakini Regina alijifanya hajasikia na alizipiga hatua mpaka kwenye meza kwa ajili ya chakula na macho yake mazuri yalichanua mara baada ya kuona chakula kingi kikiwa mezani.
“Shangazi , mbona chakula ni kingi hivi?”
“Umemleta Boyfriend wako nyumban ndio maana nimepika kingi kumkaribisha”
“Kuna haja gani ya kumkaribisha , kama ningejua ni mtu wa aina hii nisingechukua hata uamuzi wa kumfanya kuja kuishi hapa”
“Hakuna tiba ya majuto kwenye ulimwengu huu , mimi namuona Hamza mtu mzuri tu, naona unajua kuchagua”Aliongea
“Shangazi , wewe hujui tu alivyo , halafu chakula ni kingi na hatuwezi kumaliza , naona upike kama kawaida tu na usiongeze sana kwa ajili yake” Hamza hakujali Regina alichokuwa akiongea na alichukua sahani na kisha akapakua wali kiasi na kisha akampatia Shangazi.
“Shangazi asante kwa juhudi zako”Aliongea.
Shangazi hakujua hata aseme nini , tokea aanze kushi na Regina haikuwahi kutokea mtu akampakulia chakula , siku zote aliwapakulia wengine chakula. “Jipakulie tu Hamza , nitapakua mwenyewe”
“Sio sawa , wewe ndio mkubwa hapa , ni sahihi kwa sisi wadogo kukupakulia , usiniambie Regina hajawahi kukupakulia chakula?”
Mara baada ya kuuliza swali hilo lilimgusa Regina na sasa ndio alikuwa akifikiria na kuona Shangazi yake alikuwa akimhudumia kwa zaidi ya miaka kumi sasa lakini hakuwa hata akikumbuka kama kuna siku ambayo ashawahi hata kumpakulia chakula.
Sio kwamba yalikuwa maringo bali ni kwasababu siku zote anakuta tayari kila kitu kishaandaliwa na yeye ni kukaa tu na kula , hivyo hakuwahi hata kufikiria kufanya kama alichofanya Hamza.
“Regina , ijapokuwa Shangazi ni kama mlezi tu kwako , lakini utatakiwa kuonyesha unamjali pia , Shangazi anatumia daladala kwenda sokoni lakini una magari zaidi ya kumi hapa ndani , weka ratiba rudi nyumbani na mchukue muende wote kwa pamoja sokoni”Aliongea Hamza.
Upande wa Regina kadri alivyokuwa akisikia kauli hio ndio ambavyo alijisikia ni mwenye hatia , lakini kitendo cha Hamza kumfundisha cha kufanya hakutaka kukubaliana nacho.
“Jali mambo yako , nimeishi na shangazi kwa miaka ningi , sitaki unifundishe , kumpakulia tu shangazi chakula ndio sasa unajiona umemfanyia jambo la maana sana”
“Regina haina haja ya kuwa na hasira , Hamza alikuwa akijaribu kuonngea kile anachoona ni sahihi , nimekuona ukikuwa hivyo nakujua ni kwa namna gani unavyonijali”
“Shangazi kama ukitaka kwenda sokoni niambie twende pamoja , nilishindwa kung’amua hili”
“Hakutakuwa na muda wa kukusbiria mpaka urudi kazini ndio twende sokoni na kisha tuandae chakula , huna haja ya kuwa na wasiwasi , isitoshe sijazeeka sana”
“Wasiwasi wangu huyu mtu ataendelea kukufanyia maigizo ya kukujali .. anajua kujifanyisha mtu mwema kweli usimuone hivyo lakini ni mtu mbaya mwenye ajenda nyingi”
“Regina acha kuongea upuuzi, ni saa ngapi nilijifanyisha?”
“Kila unachofanya ni maigizo”Aliongea Regina.
Kuona namna nyumba ilivyokuwa imejaa makelele ya Regina na Hamza , Shangazi alijikuta akijisikia furaha , zamani nyumba ilikuwa kimya sana , lakini ujio wa Hamza ni kama uliifanya ichangamke na ionekane kweli ni nyumbani.
“Hamza ujio wako umeichangamsha sana nyumba sio kama zamani”
Regina alitaka kuongea lakini alikosa kujiamini , hakuwa akijua ni kwanini alikuwa akipandwa na hasira kwa kumuona Hamza tu.
“Yameisha sasa , na tule maana chakula kinapoa”Aliongea Shangazi na wote walianza kula.
Regina bado hatia ilikuwa ikimtafuna kutokana na maneno ya Hamza , lakini hata hivyo alikula bila ya kuongea chochote.
Regina alikuwa akila kistaarabu mno , alitafuna bila ya kuonesha meno yake nje
Upande wa Hamza ni kama mbwa anaetafuna mfupa , meno yote yalikuwa nje kutokana na spidi yake ya kutafuna na alimaliza akaongeza , akamaliza na akaongeza tena.
Kwa mshangao wa Regina chakula chote kilikuwa kimeisha .
“Unakula kama Mzimu uliofufuka”Aliongea Regina maana kwenye maisha yake hakuwahi kuona mtu anakula namna hio , lakini Hamza hakujali kejeli zake , aliondoa vyombo na kisha alimshukuru Shangazi kwa chakula kitamu.
“Ngoja kwanza nikapigwe na upepo”Aliongea Hamza na kisha alitembea kutoka nje.
Dakika kadhaa za kujivuta ili chakula kimkae vizuri tumboni Maybach nyeusi ilisimama nje ya uzio.
Mwanaume na mwanamke walishuka kutoka kwenye ile gari na mara baada ya kuwaangalia aliweza kuwajua ni Mzee Wilsoni na mke wake Lamla.
Kulikuwa na dereva ambae alifuatishana nao , alikuwa mrefu wa mita kama 1.7 akiwa na mwili uliojazia kimazoezi ,uso uliokomaa na wenye kovu karibu na na eneo la nyusi, alionekana kuwa mwenye ari kubwa na ilionekana kabisa hakuwa dereva wa kawaida.
Mara baada ya kumuona Hamza Lamla na Mzee Wilsoni nyuso zao zilijikunja.
“Karibuni nyumbani wakwe, ila mmechelewa kidogo ndio tumemaliza kula”Aliongea Hamza.
“Unafanya nini hapa?”Aliuliza mzee Wilsoni akiwa na sura kauzu.
“Regina ameniambia nihamie , nadhani hataki kukaa mbali na mim”
“Oneni jamani , huyu mtoto amerukwa na akili kabisa , ni mwanamke gani wa kuruhusu mwanaume kuishi nae kabla ya ndoa , hili swala likifahamika ataiweka wapi sura yake”Aliongea Lamla lakini muda uleule mlango wa kutokea ulifunguliwa. “Nimemkaribisha mpenzi wangu nyumbani kuishi na mimi na sio mtu wa kufanywa siri na kwanini nione aibu kwa walimwengu”
“Wewe mtukutu , kwanini unajibishana na wazazi wako?”Alifoka Lamla mama wa kambo wa Regina.
Regina alikuwa kauzu mno na hakusogea hata nchi wakati akimkodolea macho mwanamke huyo , ilionyesha ni dhahiri kiasi gani hawakuwa wakipatana.
Kitendo cha Regina kusimama mlangoni kilimfanya Shangazi aliekuwa akisafisha meza kutoka haraka na
kutaka kumuondoa Regina mlangoni na kuwakaribisha ndani.
“Ingieni ndani jamani , karibuni”
“Tuingie ndani , na tukaongee vizuri na Regina juu ya hili”Aliongea Wilsoni na Lamla alimwangalia kwa jicho la dharau Hamza.
“Sawa tunaingia lakini hili ni swala la kifamilia , mtu wa nje kama huyu hapaswi kuwepo”
“Huyu ni mpenzi wangu sio mtu wa nje , mwanaume ambae nitaolewa nae”
“Wewe.. unaruhusu vipi mdomo wako kuongea hayo maneno”
“Nimeongea ukweli”
Lamla mama wa kambo wa Regina alikuwa na hasira mno kiasi kwamba macho yake yalikuwa yakianza kuwa mekundu
“Mnaona wenyewe , ananidharau sana kwasababu mimi ni mama yake wa kambo tu”
“Hebu acheni malumbano nyie wawili , Regina tunakujali sana ndio maana tumekuja usiku usiku hapa kwa ajili yako , kuna mambo hatukukuelezea vizuri wakati wa mchana , sio vizuri kuzuia wazazi wako kuingia ndani”
“Regina , waache wazee waingie ndani”Aliongea
Shangazi na Regina kwasababu alikuwa akimheshimu Shangazi aliondoka mlangoni na kuingia ndani.
Upande wa Hamza hakutaka hata kuingia ndani , alipendelea kukaa hapo kuendelea kupigwa na upepo.
“Zaka baki mlangoni na muangalie huyo mtu kwa umakini mkubwa , usimruhusu alete fujo wakati wa mazungumzo ya kifamilia ndani”
“Sawa Madam”Zaka aliitingia kwa heshima.
Mara baada ya kila mmoja kuingia ndani , Zaka na Hamza ndio watu pekee waliobakia nje na Hamza
“Kiti hicho hapo bosi , unaweza kukaa”
“Asante mkuu , lakini bosi haruhusu sisi walinzi kukaa chini wakati wa kazi”
“Iko hivyo kumbe , mbona inasikitisha”
“Mr Hamza , naona inaboa kuendelea kusimama tu hivi , kwanini tusifanye kitu cha kutuchangamsha kidogo?”
“Oh , unadhani tunaweza kufanya nini?”
“Unaonekana ni mtu wa mazoezi makali , itakuwa unapiga tizi mara kwa mara , sina hobi nyingi sana tofauti na kushindana nguvu kwa mikono”Aliongea.
“Unamaanisha Arm Wrestling , mbona wazo baya sana hili , mimi mdogo kwako”
“Usiwe na wasiwasi , kuwa mkubwa haimaanishi kuwa na nguvu nyingi , kinachoangaliwa ni kama wewe ni mwanaume halisi , nina uhakika kwa mtu kama wewe mpenda mazoezi huwezi kuogopeshwa na kitu kidogo kama hiki , kwanza unamiliki mtoto mkali kama Regina halafu muoga?”
“Ah , kwasababu unaongea kwa staili hio basi sina jinsi ya kukubaliana na wazo kao , tutashindana mara moja tu , wasiwasi wangu nitakuumiza”
“Haha… nasubiri kwa hamu uniumize”
Baada ya kukubaliana wote kwa pamoja walisogea mpaka kwenye meza ya mawe ya kupumzikia na kisha wakachuchumaa na kushikana mikono yao “Utaniambia ukitaka tuanze?”Aliongea Hamza.
“Hivi unajua kazi yangu ya mwanzo ilikuwa ni ipi?”Aliuliza Zaka.
“Si udeteva , au una kazi nyingine”
“Upo sahihi , kwasasa mimi ni dereva lakini zamani nilikuwa katika kikosi cha makomandoo mikoa ya kaskazini huko , usije kunilaumu kama nitakuumiza ,, jilaumu wewe mwenyewe kwa kumchokoza Madam”Baada ya kuongea kauli hio palepale aliongea kwa sauti waanze.
Dakika ileile misuli ya mkono wa Zaka ilituna kwa nguvu ikilazimisha mkono wa Hamza kushuka chini.
Mkono wa Hamza ulianza kushuka chini na kidogo tu uguse sakafu na kwa nguvu alizotumia Zaka ilionekana angeumia kama angegusana na pembe ya ile meza kama sio kuvunjika kabisa.
Lakini sasa wakati Zaka akijua ashamaliza kazi ya kumshikisha Adabu Hamza kwa kumchokoza bosi wake , alikuja kugundua Hamza hakuwa na mabadiliko yoyote , ijapokuwa mkono wa Hamza ulikuwa umeelemea chini lakini alishindwa kuendelea kuusukuma uguse sakafu ya meza ile ya jiwe.
Haikujalisha ni nguvu kiasi gani alitumia, Zaka alishindwa kusukuma mkono wa Hamza na mbaya zaidi haukutikisika hata kidogo.
“Unaonekana kuwa vizuri kwenye nguvu za mikono kwa mtu kama wewe ambae kazi yako ni udereva”Aliongea Hamza huku akiwa na tabasamu la kichokozi. Na ghafla tu mkono wa Zaka ulinyanyuliwa kwa nguvu kubwa kwenda upande mwingine na ile unafika kwenye kingo ya meza ile ya jiwe kilichosikikika ni sauti ya mvunjiko wa mfupa.
“Arghhh , mkono wangu..”
Hamza muda uleule alimuachia Zaka ambae mkono wake ulikuwa ukimtetemeka kwa maumivu makali
“Nilikuambia wasiwasi wangu ni kukuumiza tokea mwanzo , kama maumivu yamezidi tuite gari la wagonjwa”
Zaka jasho lilimtoka , kwa mtu kama yeye aliepitia jeshi alipatwa na wasiwasi palepale.
“Wewe ni mtu wa aina gani , kwanini mikono yako ina nguvu namna hio?”
“Sina nguvu , wewe ndio ambae ni dhaifu , unaonekana kuwa na utapia mlo wa madini ya Kalsiamu”Aliongea Hamza na kutoa tabasamu la kifedhuli na kisha alipiga raba kurudi ndani.
Upande wa ndani majadiliano yalikuwa yamepamba moto , Mzee Wilsoni na mke wake walikuwa wakimsihi sana Regina kubadili maamuzi yake na kukubali kuolewa na James
“Regina , mimi baba yako na shindwa kukuelewa kabisa , kuna kitu gani Hamza anacho ambacho mtoto wa Mzee Benjamini anakosa , hebu fikiria kuhusu James , kuanzia taswira ya familia ake , monekano , elimu , uchumi na mengineyo mengi James anayo na huyu Hamza hana , ukiachana na hayo ni mtu ambae anakupenda na hajaanza leo kukufuatilia , kwanini unaendelea kumuona kama mtu mbaya?”
“Kuna haja hata ya kuuliza , anachofanya ni kwenda kinyume na mtazamo wetu kwa makusudi kabisa , anataka kupigana na kila kitu tunachoongea ili aonekane ni mwenye uwezo wa juu kiakili kwasababu ni CEO”Aliongea Lamla.
“Nyie mnaigopa familia ya mzee Benjamini na sio
mimi , kabla ya kifo cha babu alinisihi sana niwe msimamizi wa kampuni zote za Dosam na nihakikishe hakuna mtu wa nje wa kuikwapua, mkiendelea na maswala ya kuongea kuhusu James , basi sina chochote cha kuongea na nyiwe , Shangazi wageni wanaondoka”Aliongea Regina na kusimama kutoka kwenye sofa.
Dakika ambayo Hamza aliingia ndani ndio alikuwa akimsikia Regina akisema wgeni wanaondoka na aliona maongezi hayo yamedumu kwa muda mfupi sana.
Lamla mara baada ya kumuona Hamza akiingia sura yake ilijikunja palepale.
“Zaka yuko wapi , kwanini upo mwenyewe?”
“Ah , yule dereva wenu , alikuwa ameboreka na aliomba tucheze kamchezo kakushindana nguvu ya mikono , lakini kwa bahati mbaya amevunjika mkono”Aliongea Hamza huku akiwa na sura ya kizembe.
“Nini!, inawezekana vipi ?”Aliuliza Lamla akiwa katika mkanganyiko.
Regina hata yeye sura yake ilibadilika pia , kwa kile alichokuwa akijua Zaka alikuwa ni moja ya madereva waliokuwa wakiaminiwa mno na Lamla lakini wakati huo huo akiwa bodigadi , hakuwa mtu wa kawaida wa kuvunjika mkono kirahisi.
“Zaka ni kichwa maji , kwanini kushidana nguvu kimikono kwa ghalfa tu , alisema kabisa ni veterani wa jeshi kitengo cha komandoo , nilishakuambia usitafute mlinzi mwenye mdomo sana, turudi tutapata mlinzi mwingine”Aliongea Mzee Wilson akiwa na hasira.
Lamla alikuwa ameshikwa na aibu mno na aliishia kumtukana Zaka kimoyo moyo na kupigisha miguu chini na kisha akatoka nje kuondoka.
Mzee Wilsoni mara baada ya kuona mke wake akikimbia kutoka njce alionekana kama vile hakutaka kumuona binti yake kuendelea na msimamo wake.
“Tena nimekumbuka Regina , ulisema familia ya Benjamini wananyanyasa wafanyakazi , nini hasa kilichotokea?”
“Mdhibiti mkeo na mtoto wako kwanza , huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu maswala ya kampuni”
“Wewe.. yaani mimi baba yako naonyesha wasiwasi kwa ajili yako unaniongelesha hivyo , wewe pia ni binti yangu ukumbuke”
“Sitaki uwe na wasiwasi , nachukia kuona namna unavyoruhusu watu kukutumia kwa manufaa yao” “Kwahio kwenye macho yako naonekana kama baba nisiejielewa si ndio?”
“Wilsoni inatosha sasa , Regina anaongea kwasababu ya hasira , usiwe hivyo”Aliingilia Shangazi.
Mzee Wilsoni alikuwa na hasira mno na aliishia kuvuta pumzi nyingi huku akimwangalia Regina na kisha alipiga hatua kutoka ndani ya nyumba hio.
Kutokana na kuvunjika mkoo kwa Zaka yeye mwenyewe ndio alishika usukani lakini alikuwa amefura mno , ni kama vile hakutaka kuendesha.
Baada ya wazazi hao kuondoka , hatimae amani ya nyumba ilirudi , Regina hakubakia sebuleni na alipandisha juu na waliobakia ni Hamza ni Shangazi.
“Shangazi Regina ana mdogo wake?”
“Ndio, ana mdogo wake wa kiume , wamepishana miaka mitatu , anaitwa Frank , bado yupo chuo , mama zao ni tofauti na hawana ukaribu sana tokea wakiwa watoto, Baada ya babu yake Regina kufariki aligawa hisa zake zote za kampuni kwa Regina na kumfanya awe mkurugenzi , ndio maana unaona mdogo wake hampendi kabisa”
Hamza aliishia kutingisha kichwa na aliona kuna kitu sio cha kawaida , katika familia nyingi za kitajiri watoto wa kiume ndio hurithishwa mali na sio wanawake.
“Shangazi vipi Regina ana ndugu yake anaefanana nae?”Aliuliza Hamza na kauli ile ilimshitua kidogo Shangazi.
“Hana , mama yake Regina alikuwa ni mfanyakazi wa ndani na alipopata ujauzito alifanya siri na akaacha kazi akarudi kwao , baada ya hapo akaja kujifungua na akapoteza maisha punde tu baada ya kujifungua, Regina aliishi kituo cha kulelea Yatima mpaka alipofikisha miaka kumi na ndio hapo babu yake alivyomchukua na kumleta nyumbani, ilikuwa ni swala la kushangaza kabisa kwani hata Wilsoni hakuwa akijua hilo”.Aliongea na kumfanya Hamza kumuonea huruma kidogo Regina.
“Vipi kuhusu baba yake na wewe ni ndugu kabisa?”
“Mimi na Wilsoni sio ndugu kabisa , alienileta katika familia ya Regina ni babu yake , historia yangu kidogo inaweza kufanana na yako”Aliongea na kumfanya Hamza kushindwa kuuliza sana maana alijua angekumbusha kumbukumbu za nyuma.
Upande wa Hamza kuna kitu kilichokuwa kikimsumbua akili tokea siku ya kwanza aliokutana na Regina , haelewi ni nini lakini kuna hisia zinamwambia ashawahi kukutana na Regina,kwa jinsi alivyokuwa akikumbuka ni kama vile mtu aliekuwa amepoteza kumbukumbu.
“Hamza , nini hiki kinachotoa harufu kwenye chumba chako?”Sauti ilisikika kutoka juu , alikuwa ni Regina , Hamza palepale alipandisha haraka haraka kwenda juu na alimkuta Regina akiwa amesimama kwenye mlango wa chumba chake , ambacho mlango ulikuwa wazi.
“Regina unamaanisha nguo zangu ?”Aliuliza kama vile haelewi huku akinyooshea mkono nguo ambazo zilikuwa zimesambaa chumba kizima.
“Niliona ni usumbufu kuzifungia kwenye kabati hivyo nikazicha nje , naonaga ndio njia nyepesi ya kuzivaa”
“Husikii harufu yoyote?”
“Nasikia , hio ni harufu yangu ya uanaume , huwa inakuwa nzito”
Kauli hio ilimfanya Regina kuwa kauzu zaidi na alitamani kumpiga Hamza teke na kudondokea chini huko sebuleni.
“Kuna baadhi ya nguo nimesahau kuzifua ndio maana zinatoa harufu , sorry kwa hilo”Aliongea Hamza mara baada ya kuona dalili za mrembo huyo kukasirika.
“Zitupe zote , nitakupa hela ukanunue mpya”
“Kwanini nifanye hivyo , hizo nguo zikifuliwa vizuri tu zinakuwa sawa , ni hasara kutupa nguo , kama unaona zinakusumbua sana na harufu nitaenda kuziosha sasa hivi”
“Nimesema nitakupa hela , hutolipia hata senti moja”
“Sio swala la pesa , hizi ni nguo ambazo nimezizoea na nina mazoea nazo kabisa na baadhi nimepewa kama zawadi na marafiki zangu siwezi tupa kirahisi”
Baada ya kuongea hivyo , haraka haraka aliingia katika chumba chake na kukusanya zote na kuziweka katika begi na kushuka nazo chini.
“Shangazi , naweza kwenda kufulia wapi , au mna mashine ?”Aliuliza na alielekezwa.
Regina alijikuta akikosa cha kusema , ashawahi kukutana na masikini pia pengine ikiwa hata yeye wakati akiwa kituo cha watoto Yatima lakini hajawahi kukutana na mtu kama Hamza wa kung’ang’ania nguo chakavu.
“Regina , hapa umepata bwana , yaani anajali mpaka nguo zake chakavu , naamini huyu hawezi kubadilika haraka ukiolewa nae”
Upande wa Regina haikueleweka alikuwa akifikiria nini na alionekana kuwa na hisia mchanganyiko.
“Shangazi , mwambie anifuate kwenye chumba changu akishamaliza kuosha nguo zake”Aliongea na kisha aliondoka.
Comments