SEHEMU YA 16.
Ilikuwa ni kama kila kitu kilikuwa chekundu mbele yake kama moto, mbingu na ardhi vyote vilikuwa ni rangi ya moto , lakini ilikuwa ni ghafla tu mwanga ule mwekundu ulififia na sasa alichoweza kuona ni giza totoro, ilikuwa ni kama vile anazama baharini na hakuwa tena na msaada.
Lakini akiwa katika hali ya kukata tamaa , ghafla tu ni kama vile ni kuchomoza kwa jua hatimae mwanga ulijitokeza mbele yake , kupitia mwanga ule alijihisi ni kama vile nguvu zake sasa zimemrudia kiasi na alihangaika kwa kusogea mbele ili aufikie ule mwanga.
Mara baada ya kupiga hatua aliweza kuona ule mwanga ukizidi kuwa mweupe huku giza ambalo lilikuwa nyuma yake likizidi kumezwa na mwanga ule na ndani ya sekunde kadhaa giza lote lilipotea. “Ah…!!!”
Ghafla tu alikaa kitako na sasa alikuwa akihema kwa nguvu kama mtu alietoka ndotoni , na katika ndoto alioota alijihisi ni kama vile alikuwa akiunguzwa na
moto wa jehanamu ambayo ulimfanya kutokufurukuta hata kidogo na kujihisi kuwa katika mateso makali.
Ndoto ilikuwa ni ya uhalisia mkubwa mno kiasi kwamba ilimfanya kutaharuki na mapigo yake ya moyo kwenda mbio.
Mara baada ya kuhema kwa dakika kadhaa , alijikuta akitulia na sasa aliruhusu macho yake na akili yake kufanya kazi katika uhalisia , hivyo kuanza kuangalia mazingira.
Lakini sasa mara baada ya kuangalia mazingira aliokuwepo , alizidi kutaharuki , alikuwa kwenye mazingira ambayo hakuelewa yupo wapi , kitanda alichokuwa amelalia hakikuwa cha kawaida,kwanza kilikuwa chembamba sana.
“Nipo wapi?”
Aliuliza swali hilo , katika hali kama hio alijua kabisa hakuwa katika mazingira ya kawaida , hata kama pengine alipata ajali na sasa yupo hospitalini , hilo eneo halikuwa hospitalini kabisa.
Mapigo yake ya moyo ambayo yalikuwa yametulia yalianza kwenda kasi tena , aliangaza kulia na kushoto , mbele na nyuma lakini hakukuwa na mabadiliko ,
alijitahidi kusimama lakini alihisi hali ya kizunguzungu ikimvaa na kidogo tu aanguke chini.
Alijitahidi kushikilia ukingo wa kitanda ili kujiegamiza asidondoke chini , alikusanya nguvu zake zote ili aweze kutoka nje , akili yake ilikuwa ikimwambia kabisa hakuwa katika mazingira ya kawaida , alitaka kujua alikuwa wapi na shauku yake ilimpa nguvu ya kujikongoja ili kutoka nje.
Mlango ndani ya chumba alichokuwemo ulikuwa umechoka sana , ulionekana ni ule wa zamani mno , pembeni ya kona hio kulikuwa na chungu kikubwa mno kilichowekwa kwenye kijisturi., haikuwa hivyo tu kulikuwa na jiko lililochakaa na kuni ambazo zilionekana kuchomwa zilikuwa zimekwisha zima na kufanya eneo hilo kuwa la baridi mno.
Kila kitu kilikuwa kigeni kwake ,hakuwa na uelewa alikuwa wapi , udhaifu na hali ya kizunguzungu aliokuwa akisikia ilimletea shida sana.
“Hii sehemu ni wapi?!, najihisi ni kama vile nimeamka kutoka kwenye ugonjwa wa ajabu…”
Mawazo mbalimbali yalipita lakini hakuwahi katika maisha yake kuwa katika hali ya ajabu kama hio, hali ya kupaniki ilimvaa pia na kitu pekee ambacho aliona pengine ni bahati hakukuwa na kitu cha kutisha wala kuhatarisha usalama wak.
Mara baada ya kuvuta pumzi nyingi hatimae alijikakamua na kisha alijongea kutoka nje kwa kusukuma mlango.
“Burn the witch !Aderon is going to burn a witch”
“Choma mchawi huyo , Aderon anaenda kuchoma mchawi”
“Kila mtu”
“Burn that damn witch to ashes!!”(Choma huyo mchawi mpuuzi mpaka awe majivu)…..
“Puuuh!!!”
Hamza alijikuta akiamka huku akihema mno , hakuamini kile alichokuwa akiona sio uhalisia bali ni ndoto.
Kilichomfanya kuamkaa ni kumwagiwa maji ya baridi kabisa na hapo ndipo aliposhituka akihema.
Alijikuta akiangaza macho yake kulia na kushoto , kama mtu ambae ana hakiki mazingira, mara baada ya kuona mwanamke aliekuwa mbele yake , alijikuta akipata ahueni na kuvuta pumzi.
Eliza ndio mwanamke ambae alimuamsha Hamza , alijitahidi sana kumuasha kwa kumtingisha , lakini alishindwa kabisa na hapo ndipo alipochukua jukumu la kumuamsha kwa maji ya baridi , na hatimae aliweza kuamka , mwanzoni alihofia mara baada ya kuona haamki, sasa kitendo cha kushituka kwa Hamza kilimfanya kupatwa na ahueni na sasa anaona alikuwa katika eneo la sebuleni ndani ya nyumba ya mrembo huyo na alianza kuvuta kumbukumbu za jana yake.
******
Hamza mara baada ya kuingia katika Bar ya muembeni mwanamke ambae alimwita alikuwa ni Eliza , mwanadada mrembo ambae alimsaidia kutoka katika mikono ya Amisi na genge lake.
“Hamza ni wewe”
“Eliza ?”
Hamza mara baada ya kugeuka ndio aliweza kumuona Eliza akiwa katika meza na kundi la wanawake wengine warembo na wote walikuwa wamevaa mavazi ya kufanana.
“Kwa muonekano wako nilidhani hufikagi kwenye mazingira kama haya”Aliongea Eliza na muda huo alionekana pia alikuwa ameanza kulewa.
Kitendo cha Hamza kumuona mwanamke huyo mrembo ambae alikuwa akimfahamu mudi yake kidogo ilirudi na alisogea katika meza yao.
“Hii ni mara yangu ya kwanza hapa”Aliongea Hamza.
“Eliza mbona hututambulishi , huyu ni boyfriend wako?”Mmoja ya mrembo aliekuwa katika meza moja na Eliza aliongea , alikuwa amevalia suti.
“Una mwanaume mtanashati kweli na mwenye kuchukua mazoezi , kumbe hii ndio aina ya wanaume unaopendelea Eliza …”Mwanamke yule hakuacha kumsifia Hamza.
“Asha , unaongea nini , huyu ni kaka yangu”Aliongea Eliza akimtambulisha Hamza kama kaka yake.
“Acha aibu Eliza , wewe tuambie huyu ni nani , nadhani wale wanaume wanaokufukuzia watakufa kwa wivu wakijua una bwana”Mwingine aliongea akitania.
Ilionekana wanawake hao wote walikuwa wakifanya kazi pamoja kutokana na mazoea yao.
“Endeleeni tu kunitania na mtaona namna nitakavyokazia tukiwa kazini..”Aliongea na muda huo huo alimwangalia Hamza.
“Hamza unaweza kuungana na sisi kama upo mwenyewe”Aliongea Eliza , hakuwa na aibu kama mara ya kwanza alivyokutana na Hamza.
Hamza mpango wake ni kutafuta mtoto wa kike yoyote yule kupitisha nae usiku lakini baada ya kukutana na wanawake warembo kama hao aliona akubali na kukaa nao.
Muda huo alikuwa tayari ashaagiza bia yake na aliendelea kunywa huku stori mbalimbali zikiendelea na aliweza kugundua wanawake wote waliokuwa hapo walikuwa chini ya idara ya Eliza kazini na ilionekana Eliza ndio aliewatoa out mara baada ya kupandishwa cheo kazini kwake.
“Eliza vipi wale watu , hawajakusumbua tena?”Aliuliza Hamza kimitego.
“Huwezi kuamini kilichotokea , hivi unajua kiongozi wao alikuja kwenye kampuni ninayofanyia kazi kwa ajili ya kuomba msamaha , mimi mwenyewe sijui nni ni kilichotokea , lakini vyovyote vile yaliopita yashapita.. sitaki hata kukumbuka namna nilivyodhalilika mtandaoni”Aliongea “Ni vizuri kama hatokusumbua tena”
“Eliza lazima kuna mtu amekusaidia kwa siri , kwa taarifa tulizopata nasikia Amosi amekuja akiwa na nundu usoni ikionekana kama vile kuna mtu kampiga”Aliongea.
Hakuna kilichojificha ndani ya kampuni, mrembo aliekuwa pale mapokezi ndio aliesambaza umbea juu ya Amosi kuonekana kuumia usoni.
“Acha kuota , unadhani mambo ni kama kwenye filamu..”Eliza aliongea huku akikataa ile kauli.
Ukweli nin kwamba mrembo huyo alikuwa na wasiwasi pia juu ya kile kilichotokea , lakini kadri ambavyo alifikiria siku hio hakuweza kupata jibu , isitoshe kwenye maisha yake hakuwa na marafiki ambao wanaweza kumsaidia.
“Vyovyote vile , Naomba leo nilipie kila utakachonunua hapa kama asante ya kile ulichonifanyia juzi na kuniokoa kutoka kwa wale mabaradhuli”Aliongea na aliinua glasi yake akigongesehana cheers na Hamza.
Hamza alifurahi kuona mrembo huyo alivyokuwa amechangamka,ukweli hakujua kama mrembo huyo alikuwa akitumia kilevi.
“Kwahio Eliza usiniambie huyu ndio babe aliekuokoa jana”Aliongea.
“Mimi siamini kama huyu kaka yako kweli, Eliza acha kuficha bwana”Waliongea kumtania na ilimfanya Eliza kuwa mwekundu mno lakini muda uleule Eliza aliweza kuona kundi la watu wakisogelea na palepale uso wake ulibadilika.
Mabadiliko yake yalionekana kwa kila mtu aliekuwa hapo ndani na kufanya wote wageuke.
Mwanaume wa maji ya kunde ambae alikuwa mrefu na amevalia t-shrt ya Ginvenchi na saa ya Rolex alionekana , alikuwa na wajihi wa uchangamfu, akiwa ametangulizana na wanaume wanne pia ambao walikuwa wamevaa mavazi ya bei ghali.
“Aiyaa… nikadhani nilikuwa nikikufananisha , kumbe ni wewe mrembo wetu Eliza”Aliongea yule mwanaume.
Eliza alionekana kujizuia na alijifanya kama vile hajasikia na aliendelea kudili na kinywaji chake.
Asha na wale wanawake wengine walikuwa katika hali ya chuki mara baada ya kuona ni kama wanataka kuvurugiwa.
Upande wa Hamza wakati akiwa hajui kinachoendelea , tayari yule mwanaume alionekana kumwangalia kwa kejeli.
“Hey! Mzee potea na umwachie bosi nafasi yako”:Aliongea moja ya vijana waliokuwa wametangulizana nae.
Hamza hakutaka kuonewa na wale watu kizembe na alikaa vilevile bila kuonyesha wasiwasi.
“Kama una uwezo jaribu kuniondoa na akae bosi wako”
“Wewe boya , unajua mimi ni nani , uliza uambiwe , mtu yoyote ambae anajifanya kutaka kupandishiana na mimi lazima avunjike mkono au mguu”
“Kumbe ndio ulivyo, nimekuelewa?”Aliongea Hamza huku akiendelea kupiga kinywaji chake.
Mara baada ya kuona Hamza hakutaka kuondoka , bwana yule alipiga meza kwa mkono wake.
“Hili ni onyo la mwisho , ondoka kwa hiari yako”
“Zefa naomba uondoke , acha kutuharibia mudi , ondoka na genge lako tuna mambo yetu”Eliza alikosa uvumilivu.
“Haha.. Eliza naona sasa kwa hiari yako umelitaja jina langu , acha kuwa mkali hivyo , nilikuwa na wasiwasi tu na rafiki yangu wa kitambo ndio maana nimekuja kukujulia hali”
“Haina haja na hatujawahi kuwa marafiki”
“Roho mbaya hio , nilitaka nikutoe angalau hela kidogo ufanyie matumizi, nimesikia gharama za hospitali ni kubwa mnno kwa matibabu ya mama yako asiejiweza kitandani”
Mara baada ya Eliza kusikia habari za mama yake zikiingizwa hasira zilimpanda mno na hakuweza kuvumilia tena na palepale alichukua glasi iliokuwa na mvinyo na kumwagia Zefa.
“Mnyama mkubwa wewe , unatoa wapi ukijogoo wa kumuingiza mama yangu hapa”
“Wewe malaya , nadhani umekuwa kichaa”Aliongea Zefa kwa hasira na palepale alitaka kumchapa Eliza kibao lakini mkono wake uliishia hewani mara baada ya kudakwa.
Eliza alijua angepigwa na kile kibao na alifumba macho kukisikilizia lakini hakikumpata .
Hamza alitumia mkono wa kushoto kuudaka mkono wa Zefa wa kulia.
“Ni udada huu kutaka kumpiga mtoto wa kike”Aliongea Hamza akiwa katika sura ya upole. “Niachie wewe boya , unakitafuta kifo sio”Aliongea na palepale alijaribu kutumia mkono wake mwingine wa kushoto kujaribu kumpiga Hamza usoni, lakini kabla hata ngumi ile hajamfikia Hamza kwa mkono wake wa kulia alikuwa tayari ashamsukuma Zefa na kudondoka chini.
Hata Zefa mwenyewe hakuelewa kilichotokea , kwani nguvu kubwa isiokuwa ya kawaida ilimsukuma ghafla tu na alidondoka kama vile alikuwa hajasukumwa bali amedondoka kutoka umbali wa juu , alisikia maumivu makali mno kutokana na kuteguka mkono.
“Boss, uko ssawa”
Lile genge lake la watu lilimsogelea bosi wao na kumsaidia kusimama.
Eliza na wenzake walishangaa hata baadhi ya wateja waliokuwa ndani ya bar hio waliosikia mzozo huo walishangazwa na kitendo cha Zefa kudondoka chini baada ya kusukumwa.
“Hamza , unapaswa kuondoka haraka , sidhani kama utawaweza kwa ulichomfanyia mwenzao”Aliongea Eliza akimsihi Hamza kukimbia lakini Hamza hakuwa hata na ishara ya kutaka kuondoka , alikuwa katika hali ya utulivu kabisa.
“Niondoke , halafu wewe nakuacha na nani?”Aliongea na kauli ile ilimfanya Eliza kujishangaa lakini kwa wakati mmoja alijisikia vizuri mara baada ya kuona Hamza anajaribu kumlinda.
“Umemuumiza bosi halafu unataka kuondoka , hakuna kuondoka mpaka tukushikishe adabu boya wewe”Waliongea wale vijana , wote walionekana kulewa pia akiwemo bosi wao na palepale walimsogea Hamza kutaka kumshambulia lakini kilichowatokea ilikuwa ni maumivu.
Hamza hakutaka tena kuvumilia yale makelele na alisimama na kilichoendelea ilikuwa ni vijana wale na bosi wao kuchezea kichapo cha kufa mtu.
Ki ufupi ni kwamba hali ya hewa ilibadilika kabisa na hata wale wateja waliokuwa ndani ya eneo hilo walishangazwa na uwezo wa Hamza wa kupigana , wahudumu walijitahidi kutuliza hali lakini ilishindikana.
“Wewe boya , nitakuonyesha , nitakutafuta kwa nama yoyote ile , lazima nilipe kwa leo hii”Aliongea Zefa kwa hasira na kisha alijikongoja na watu wake na kuondoka ndani ya eneo hilo mara baada ya watu kuingilia ugomvi huo.,
Wale wanawake ambao Eliza alikuwa ameambatana nao na wenyewe waliondoka na kumuacha Eliza akiwa na Hamza
Eliza alikuwa kwenye mshangao , ukweli ni kwamba licha ya siku hio ni kama mara ya pili ya Hamza kupambana na watu lakini wale wa siku ile na wa wakati huo walikuwa na utofauti , hao walikuwa na uwezo mkubwa wa kupambana , lakini Hamza kiwepesi kabisa aliwadhibiti.
Kwasababu bili haikuwa imelipwa , Eliza alilipa bili na kisha Hamza aliondoka na mrembo huyo mpaka nje.
“Hamza huna woga kabisa
“Kwanini?”
“Zefa baba yake ni mkuu wa polisi kanda ya Dar es salaam , watu wengi walipelekwa polisi kwasababu ya kugombana na Zefa , anatumia hadi magenge ya wahuni kuadhibu watu ambao ana kisasi nao na hakuna wa kumfanya lolote”
“Hata kama , kwanza simjui na nilichofanya ni kutotaka wewe kuchokozwa”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Eliza kuonyesha hali kidogo ya kuchanyikiwa na kusita na alimwangalia Hamza machoni na kushindwa kuongea neno.
“Mbona unaniangalia hivyo?”Aliuliza Hamza mara baada ya kuona mwanamke huyu kasimama.
“Tunaweza kwenda kutembea tembea kule beach, japo ni usiku lakini watu wapo”Aliongea Eliza kwa kusita sita.
Hamza japo alishangaa ombi hilo ila hakukataa, walitoka katika Bar hio ya Mwembeni na kisha walisogea upande wa Beach , kulikuwa na Bar nyingine katika beach hio na mziki ulikuwa ukisikika , baada ya kufika wote walinunua vinywaji va baridi na kisha walishikilia mkononi na kutembea katika fukwe hio , Eliza alikuwa na kibegi chake huku Hamza akiwa mikono mitupu.
“Zefa alikuwa akinifuatilia kwa muda mrefu , kwa zaidi ya miaka miwili , lakini nilimjua sio mtu mzuri hivyo nilikuwa nikimkataa kila alipokuwa akinitongoza , siku moja akiwa amelewa alifika nyumbani kwetu na alianza kunilazimisha tufanye mapenzi , wakati nikiendelea kufurukuta mama aliweza kufika na mara baada ya kuona kitendo kile alipatwa na mshituko uliompelekea kupooza kiwiliwili cha chin…”Aliongea Eliza huku machozi yakianza kujilenga lenga katika mboni za macho yake.
“Lakini kwasababu ya baba yake kuwa mkuu wa kituo cha polisi na vilevile kuwa na konekshini alikamatwa kwa siku chache tu na kisha akaachiwa huru , ilikuwa ni siku kadhaa tu mara baada ya mama kupona kutoka hospitalini lakini alipatwa na kiharusi na sasa amekuwa ni wa kulala tu hospitalini kwa zaidi ya miaka miwil, kutokana na tukio hili ndugu zangu walianza kunisema vibaya na kunifanya nisipate msaada wowote wa kumuuguza mama..”
Hamza mara baada ya kusikia mrembo huyo akiongea kwa huzuni aliweza kuona ni hali gani alikuwa akipitia kwenye maisha yake.
Juzi alimkuta kwenye matatizo na leo pia alikuwa kwenye matatizo , ilioekana kulikuwa na watu wengi sana waliokuwa wakiyafanya maisha yake kuwa magumu.
“Baada ya tukio hilo ndio nilitoka nyumbani na kuhamia kwenye Apartment na kitu kinachochukua muda wangu mwingi ni kazi na kwenda hospitalini tu”
Eliza alikuwa amejikunyata kwenye miguu yake kutokana na upepo mwingi uliokuwa ukivuma alihisi baridi na baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu aliinua macho yake na kumwangalia Hamza.
“Hamza najua hatufahamini na leo ni mara ya pili umenisaidia , kwanini umekuwa mtu mzuri kwangu ghafla tu?”Aliuliza.
“Nilifanya nilichopaswa kufanya , isitoshe mimi ni mwanaume na huwa napenda kujichukulia pointi mbele ya mrembo kama wewe”Aliongea Hamza huku akigida pombe iliokuwa mkononi mpaka ikaisha na kutupa kopo ,kauli yake ilimfanya Eliza kucheka.
“Unaonekana kuwa mtu muwazi sana , lakini napaswa kukushukuru kwa wema wako licha ya kwamba hunifahamu”
Hamza hakuongea chochote na alichukua bia nyingine ya kopo na kuifungua.
“Vipi nikupe..”
“Hapana .. nitashikwa na haja ndogo muda si mrefu , nimekunywa sana leo”Aliongea na Hamza hakutaka kumpa tena kilevi.
Baada ya kukaa kama nusu saa katika fukwe hio Hamza aliona muda umeenda.
“Eliza nitakusindikiza mpaka unapoishi , muda umeenda, sawa”Aliongea na kumfanya Eliza aliekuwa amezika kichwa chake katika mapaja kunyanyua kichwa chake na kumwangalia Hamza usoni.
“Utaweza kweli kunifikisha mpaka ninapoishi..?”Aliuliza na swali lile lilikaa kimtego.
Upande wa Hamza alijiambia kwanini ashindwe kufika , isitoshe hana pa kwenda kama ni chumba alisharudisha na mpenzi wake feki kamfukuza.
Hamza alimchukua Eliza na palepale walitoka hapo na kurudi barabarani na kisha walipanda bajajaji mpaka anapoishi Eliza.
Hamza hakuwa na mpango wa kusimama getini , aliingia kabisa hadi ndani kwenye lift na Eliza alikuwa kimya tu , baada ya kufika katika floor husika wote walitoka mpaka kwenye mlango.
Eliza alionekana kuwa na wasiwasi mno na alikuwa akijiuliza na kujiambia imekuwaje leo kuja na mwanaume mpaka anapoishi tena usiku huo, ijapokuwa alikuwa amelewa kiasu lakini fahamu zake zilifanya kazi vizuri kabisa.
Lakini hata hivyo ashamruhusu mpaka kufika hapo asingemwambia aondoke , kitendo cha kumfanya Hamza kuja mpaka hapo ni kama nia yake ilikuwa wazi kabisa
Alijiambia yeye ni mtu mzima na kama atamwambia Hamza aondoke ingeonekana kama anamchezea akili bila sababu ya msingi.
Alikumbuka tukio la juzi kusaidiwa na Hamza na leo pia kusaidiwa na Hamza mbele ya mwanaume anaemchukua, palepale alifanya maamuzi ya liwalo na liwe , hata kama simjui vizuri ngoja nimkaribishe.
“Eliza vipi , umekosea ufunguo?”Aliuliza Hamza mara baada ya kuona namna ambavyo mrembo huyo alikuwa na wasiwasi akichangua kibegi chake Muda uleule hatimae aliweza kupata kadi ya mlango na kuweka sehemu husika na hatimae mlango kufunguka.
“Karibu ndani…”
Mara baada ya Eliza kuingia ndani alitupia mkoba wake kwenye sofa na kupunguza nguo na kubakia na shati pekee na kufanya chuchu zake zilizosimama kuonekana vizuri , ilikuwa ni jambo la kuvutia kwa Hamza kweli.
Eliza aligeuka nyuma na kupepesa macho yake mazuri huku akimwangalia Hamza aliesimama mbele yake.
“Hamza .. umeoa au una mpenzi?”Aliuliza huku akisita sita, hakuwa akimjua Hamza vizuri na kitu pekee ambacho aliona anapaswa kujua angalau ni kama mwanaume huyo ana mke au ameoa , hakutaka kujihusisha na waume za watu na kujiingiza katika matatizo, aliokuwa nayo yalimtosha.
“Nina girlfriend lakini ni feki , vipi unaweza kusema nipo kwenye mahusianno?”
“Ndio inamanisha ndio , unamaana gani kusema ni feki?”
“Ukweli ni kwamba sina mpenzi , bado nipo single”Aliongea maana hakutaka kuongea sana maswala ya Regina.
Eliza mara baada ya kusikia kauli ile alijikuta akipatwa na ahueni na alimsogelea Hamza na kisha aliinua uso wake na kumwangalia , alioekana kuwa na wasiwasi na kusitasita kwa wakati mmoja.
Hamza mara baada ya kuona mrembo huyo anajilengesha kwake hakujua acheke au aune.
“Eliza unafanya nini?”Hamza alijifanya mzembe na swali lile lilimfanya Eliza kushikwa na aibu.
“Wewe , kwani hujui ninachofanya au unanichokoza”
“Sijui”
“Kama hujui basi”Aliongea na kisha akageuka lakini dakika ambayo alitaka kuondoka Hamza alimshika mkono na kumvuta kwake na palepale alimpiga denda
“Uh..”
Eliza hata hakujua alivyofika kifuani kwaHamza lakini alishitukia tu akiwa tayari ashabusiwa, kiini cha macho yake kilicheza cheza mno na kabla hajaendelea alijitoa kwa Hamza.
“Subiri kidog”Aliongea.
“Nini shida?”Aliuliza Hamza kwa sauti nzito huku akipumua kwa nguvu maana hisia zishamvaa tayari.
“Naomba niende kwanza kujisaidia”Aliongea na hakusubiri hata jibu alikimbilia chooni.
Eliza mara baada ya kukaa chooni na kushusha mkojo hatimae alipumua kwa nguvu huku akiwa na wasiwasi , hakuwa mzoefu sana na wakati huo alijiuliza akishatoka hapo nini kinaendelea, alikuwa akivutiwa na Hamza lakini hakutaka kufika hatua ya kufanya mapenzi kwa haraka sana.
Lakini baada ya kukaa kwa muda wa dakika kumi na tano alitoka na hapo ndipo aliposhangaa mara baada ya kumkuta Hamza ashajirusha kwenye sofa na anakoHamza , akiwa usingizini, alijikuta akipatwa na ahueni na alirekebisha AC na kisha akachukua blanketi na kumfunika na kuingia chumbani kwake.
Lakini wakati huo sio kwamba Hamza alikuwa amelala , alijifanyisha alikuwa amelala tu ili kutokumfanya mrembo huyo kuwa na wasiwasi.
Baada ya nusu saa kupita ndio alipotelea usingizini na anajikuta anaota ndoto ya ajabu mno.
Comments