SEHEMU YA 17.
“Mwenzetu , unalalaje usingizi mzito hivyo?”Aliongea Eliza mara baada ya Hamza kuamka.
Hamza bado akili yake ni kama ilikuwa imetawaliwa na ndoto aliokuwa ameota na aliishia kumwangalia tu Eliza.
Akili yake ilianza kukusanya matukio na alikumbuka jana alilala kwenye sofa na sio kitandani na hio ni mara baada ya kukisi na mrembo huyo na akakimbilia chooni.
“Mbona huongei chochote Hamza , umeniogopesha ujue kwa namna nilivopata shida ya kukuamsha”
“Babe , unajua wewe ni mrembo mno”Aliongea Hamza akijitahidi kurudi katika hali ya kawaida na kupotezea kile alichoota, kauli ile ilimfanya Eliza kusahau hata namna alivyopata shida ya kumuamsha Hamza na alishikwa na viabu vya kike.
“Umeniitaje?”Aliuliza na kumfanya Hamza kutoa tabasamu.
“Tumeshakiss tayari na kugusana , sidhani kama ni kosa kukuita mpenzi”
Eliza hakujua hata namna ya kujibu kwani hakuwa akichukia pia kuitwa mpenzi , ukweli alijisikia vizuri.
“Muda umeenda , nenda kaoge na kusafisha kinywa upate kifungua , kinywa”Aliongea kupotezea ile hali.
Hamza mara baada ya kufika chooni hatimae alivuta pumzi nyingi na kuzishusha , alikuwa akijitahidi kuwa sawa mbele ya Eliza lakini bado ni kama akili yake imetawaliwa na kile alichoota.
“Bwana eh , ni ndoto tu kama ndoto
nyingine”Aliongea na kisha aliangalia mazingira ya choo hicho na aliweza kuona taulo pamoja na mswaki na dawa ya meno vikiwa vimewekwa , ilionekana Eliza alishaandaa kwa ajili yake.
Alijisikia viuri kwa kuona E.liza ni mwanamke anaejua kujali mwanaume, kwa muda mrefu hajahudumiwa na mwanamke mrembo.
Mara baada ya kuoga na kujifuta alirudi na kuungana na Eliza kwenye meza kwa ajili ya kifungua kinywa , kulikuwa na mayai ya kukaanga , chapati na supu ya kuku.
“Hizi chapati umepika?”Aliuliza.
“Hapana nimenunua kwa jirani hapo anatembeza , huwa mimi sio mtu wa kukaa sana nyumbani , sio
kwamba sijui kupika chapati ila mahitaji sina”Aliongea akionekana kama vile anajitetea.
“Sijamaanisha hivyo?”
“Kwanini sasa na muonekano huo?”
“Ni kwamba sijapata kifungua kinywa nje na ninapoishi kwa muda mrefu sana”
“Oh , kama ni hivyo unaweza kuja mara kwa mara nitakupikia”
“Kwahio unamaanisha unataka tuishi pamoja”Aliuliza Hamza huku akicheka. “Wewe , sijamaanisha hivyo”Aliongea huku akiona aibu na kujiambia ni mjinga kwanini kuongea kauli ya aina hio yenye utata.
Hamza alipiga supu hio nzito na kupotezea kabisa swala la ndoto , hakutaka kujihangaisha nalo kwanza alikuwa na mambo mengi kichwani ikiwemo swala la kumtafuta Mzee.
Baada ya kumaliza kifungua kinywa Eliza alipaswa kuelekea kazini na Hamza mara baada ya kuangalia ratiba chuo aligundua alikuwa na kipindi saa nne, hivyo aliona huo ni muda wa kuondoka kwenda chuo akapoteze poteze muda.
Eliza alitumia gari la kampuni na alimpa Lift Hamza mpaka Tazara na kisha alichukua dalalada kuelekea chuo.
Licha ya kwamba hakuwa na mudi alienda kwasababu kipindi cha saa nne ni cha Profesa Singano mzee wa bonus point.
Hakukuwa na foleni kubwa sana na alitumia kama dakika ishirini hivi mpaka kufika chuo na mara baada ya kushuka alianza kutembea taratibu taratibu kusogelea geti la chuo.
Lakini kabla hata hajalifikia Toyota Corola ilifika na kusimaa pembeni yake na kioo cha mbele kikashushwa na dakika ile wanaume watatu walitoka katika gari ile.
“Hamza Mzee , ndio wewe”Aliongea mmoja ya wale watu mwenye mwili mkubwa kidogo na Hamza aliitikia kwa kutingisha kichwa.
“Sisi ni polisi kituo cha mjini kati , upo chini ya ulinzi kwa kosa la uhalifu”Aliongea mmoja ya wale polisi na kisha alimsogelea Hamza kwa nia ya kumshikilia.
Jambo lile lilimshangaza Hamza maana hakujua hata ni uhalifu upi ambao amefanya mpaka kuja kukamatwa na polisi asubuhi yote hio.
Hamza hakutaka kuvuta attention ya watu na alikubali kistaarabbu na kisha aliingizwa kwenye ile gari na ikaondoshwa kwa haraka.
Dakika chache mbele gari ile ilipita Gerezani na kusonga mbele , jambo ambalo lilimshangaza Hamza.
“Afande si mmesema mmetokea kituo cha mjini kati?”Aliuliza Hamza.
“Acha uboya dogo , kituo cha mjini kati umekisikia wapi, tunakupeleka chimbo kukushikisha adabu”Aliongea moja ya bwana mwenye sura ngumu na kumfanya Hamza sasa kuelewa kinachoendelea.
Hakutaka hata hivyo kuleta vurugu kwenye gari hio na aliacha kuona mwisho wake.
Foleni ilikuwa hakuna kabisa hivyo gari hio ilitembea kwa spidi kubwa na ndani ya dakika kadhaa waliipita Mbagala na kufuata njia ya kwenda Kongowe na kisha gari ile ikakunja kushoto na kuingia katika barabara ya Vumbi na kusonga mbele na ilikuja kupita Bar moja ambayo Hamza hata hakusoma jina lake ila ilienda kusimama nje ya moja ya jengo ambalo lilikuwa limezungushiwa ukuta na kisha ikaingia ndani.
Kitendo cha gari ile kusimama tu na mlango kufunguliwa hatimae Hamza alijua nani amekuja kumkamata,ilionekana bwana aliemshikisha adabu jana yake ndio ametafuta tena ugomvi.
Zefa ndio aliekuwa mbele yake , akiwa amezungukwa na vijana wengine , haikueleweka eneo hilo lilikuwa ni kwa ajili ya nini lakini Hamza alijua tu hio ni ngome ya kihalifu.
“Wewe boya , nadhani jana maneno yangu uliyasikia vizuri , nilisema lazima nikushikishe adabu , sasa leo utapata kipigo mara mia ya kile ulichonifanyia jana”Aliongea Zefa kwa hasira.
“Unajifanya kidume sana , mwanamke niliemhangaikia kumpata kwa muda mrefu wewe hujafanya juhudi yoyote unalala nae kizembe , leo utanitambua, Vijana mpigisheni magoti”Aliongea kwa hasira mno na sasa Hamza aliona hasira yake bwana huyo ilionekana imechanganika na wivu.
Lakini kaba hata ya vijana wale hajaanza kumshugulikia Hamza honi ya gari ilisikika nje na ndani ya sekunde kadhaa tu geti lilifunguliwa na gari aina ya Mercedenz iliingia ndani.
Vijana waliokuwa wapo tayari kwa ajili ya kumshughulikia Hamza walikakamaa na nyuso zao kuwa na wasiwasi.
“Madam!!”
Moja ya bwana ambae ndio alifika na kumkamata Hamza akijifanyisha polisi aliongea na kusogelea ile gari.
Muda uleule mlango wa gari ile ulifunguliwa na viatu vyenye visigino virefu vilianza kuonekana kabla ya mwili wote.
Mrembo Dina ndio ambae alitoka kwenye gari hio na kufanya vijana wote wamwangalie kwa heshima , hakuna kijana ambae alikuwa jasiri wa kwenda kinyume na Dina , walikuwa wakimjua vizuri ukatili wake licha ya kwamba alionekana mpole na mrembo kupindukia.
“Madam kwanini umekuja mpaka huku, hakuna taarifa kwamba leo utatutembelea”Aliongea yule bwana kwa heshima huku akifosi tabasamu , lakini alionekana kuwa na wasiwasi .
Zefa hata yeye alikuwa akimjua Dina na siku zote licha ya ubabe wake na kupenda kwake wanawake kwa Dina hakuwahi hata kuwaza kumtongoza.
Dina alionekana alikuwa na haraka sana na aliangalia mazingira kwa sekunde kadhaa na kisha alipotezea swali lile na alimsogelea Hamza na kusimama mbele yake na kuinamisha kichwa.
“Samahani , sijatarajia swala kama hili litatokea”Aliongea Dina kwa heshima mbele ya Hamza.
Genge lile ikiwemo Zefa mwenyewe walishikwa na butwaa kwani hawakuelewa ni kipi kinatokea mbele ya macho yao.
Dina malkia na mmiliki wa kundi la Chatu alikuwa akionyesha heshima mbele ya Hamza?, mwanamke mrembo ambae viongozi wa kisiasa na wa jeshi walikuwa nyuma yake, lakini leo hii anaomba msamaha mbele ya mtu kama Hamza.
Wanaume hao watukutu walikuwa wakitamani hata kumwangalia mrembo Dina kwa ukaribu , walikuwa wakimhusudu mno lakini licha ya kuwa na utofauti mkubwa kati yao na Hamza lakini aliekuwa akipewa heshima ndio yeye.
Sasa tukio lililofuatia ndio liliwashangaza zaidi kwani Hamza alimshika Dina kidevu na kukiinua juu , kama vile ni mfalme mbele ya masuria wake.
“Dina kwanini unaomba msamaha , mimi ndio nilifanya fujo na kumpiga mtu na hata sasa hawajanifanya chochote”Aliongea Hamza.
“Kwahio huna hasira yoyote na mimi?”
“Haha.. kwanini niwe na hasira , kama ningekuwa na hasira nisingekutumia ujumbe wa maandishi”Alionngea na Dina alionekana kuvuta pumzi ya ahueni.
******
Regina hakuwa na kikao asubuhi hivyo hakuharakisha kwenda kazini na saa nne ndio muda alioshuka chini kwa ajili ya kupata kifungua kinywa , hakuwa na wasiwasi wowote na baada ya kifungua kinywa alikaa kwenye sofa na kuangalia habari za kimataifa huku akila tunda la shufaa kimapozi.
Shangazi alionekana kuwa bize na alionekana akitoka nje akiwa ameshikilia nguo ambazo zimekwisha kukauka , zilikuwa ni nguo za Hamza alizofua jana na kuziacha.
“Regina, jana umemfukuza Hamza na hakurudi kabisa na nguo zake pia hajachukua , ukute amelala mtaani huko”Aliongea na sasa ni kama vile Regina anamkumbuka Hamza kwani alishikwa na mshangao. “Hivi kumbe jana aliondoka kabisa na hakurudi?”
“Ndio , chumba chake kipo wazi usiku mzima , sijui hakuna kilichomtokea , kwanini usijaribu kumpigia simu na kumuuliza yupo wapi?”Aliongea.
“Mtu mzima kabisa yule , hakuna chochote cha kumtokea , pengine ukute amelala alikokuwa akiishi”Aliongea Regina akiwa sio mwenye ishara ya kujali kabisa lakini ilikuwa tofauti kwa Shangazi.
“Nadhani hutonichukia kwa kuongea kwangu sana , lakini jana Hamza aliongea vile mpaka ukakasirika kwasababu ya maisha aliopitia”Aliongea na kumfanya Regina kumwangalia Shangazi kwa shauku kidogo.
“Unamaanisha nini Shangazi?”
“Hebu fikiria hata wewe , hana wazazi na tokea akiwa mdogo amekuwa peke yake, pengine ana hamu kubwa kutaka kuwa hata na wazazi kama ilivyokuwa kwako , pengine kwa kukosa wazazi ameshikwa na uchungu kwa namna wewe na baba yako mlivyokuwa mkijibishana jana , sidhani hata kama akitaka baba wa kubishana nae anaweza kupata”
“Shangazi kwahio unamaanisha ni Yatima?”Aliuliza Regina huku akishangaa na kumfanya kuwa mzuri zaidi lakini kauli yake ilimshangaza Shangazi.
“Inamaana wewe hukuwa ukijua?”
Regina aliishia kumumusa lipsi zake na alikumbuka namna alivyomfukuza jana Hamza, alionekana kuelewa kwanini Hamza alitaka kuzungumzia swala la baba yake.
“Ngoja nijaribu kumpigia”Aliongea na kisha akachukua simu yake.
“Shangazi wewe ndio unataka nifanye hivyo , ila sio mimi ninaetaka kumpigia”Aliongea Regina kama vile ni mtu ambae anajihami lakini kauli yake ilimfanya Shangazi kutabasamu na kutingisha kichwa.
Baada ya kuipiga namba ya Hamza hatimae iliita na kumfanya akohoe kidogo kusaficha koo na kweli muda uleule simu ilipokelewa.
“Uko wapi?”Aliuliza Regina kistaarabu.
“Nipo kitaa” Sauti ya kikauzu ilisikika.
“Najua upo kitaa , nauliza upo kitaa gani?”
“Kuna shida?”
Kauli ile ilimfanya Regina kukunja sura , alitaka kujali kuuliza amelala wapi usiku lakini sauti ya Hamza ilimfanya kupotezea wazo hilo.
“Hakuna shida.. nauliza tu”
“Kama huna cha kuongea nakata simu”
Bila hata ya kuongea simu pale ilikatwa
Mrembo huyo sura yake ilibadilika na kwa hasira aliweka simu chini kwa nguvu na kisha aling’ata pande la Apple kwa hasira kama kwamba tunda hilo limemkosea.
“Shangazi , haina haja ya kumjali , muache na maisha yake”Aliongea
Shangazi Mariposa alijikuta akitingisha kichwa , aliona ni bora asingependekeza wazo la Regina kumpigia simu.
Comments