SEHEMU YA 20.
Yonesi kama bodigadi alikuwa na taarifa zote za
Regina kuajili msaidizi wake mwingine na mara baada ya kufahamu ni Hamza aliishia kushangaa na kujiuliza nini kinachoendelea , hakuwa na taarifa zote, alihisi kuna kitu kinaendelea kati yao lakini aliona ni kheri ajirushe baharini aliwe na mamba kuliko kuamini Regina anaweza kutoka kimapenzi na mwanaume kama Hamza.
Kingine ambacho kilimfanya Yonesi kumdharau Hamza ni tabia yake ya kukosa aibu na uwoga woga usio na maana , yeye alipenda wanaume ngangari lakini kitendo cha siku ile kumuachia msaala kule gongo la mboto alimuondolea nyota ya heshima kama mwanaume.
“Kapteni, unapaswa kuwa na sababu ya msingi kunifukuza kwenye hii meza, hakuna sheria inayonizuia kukaa kwenye hii meza si ndio?”
“Nenda kakae meza inayofuatia haina mtu , kwani lazima ukae hapa”
“Siendi popote”Aliongea Hamza.
“Kwanini?”Aliuliza huku akiwa amekunja ndita.
“Kwasababu nataka kuona namna mwanamke mrembo kama wewe unavyokula”
Yonesi alikuwa ni mweupe kabisa , kauli ile japo haijamshangaza sana lakini kulikuwa na viashiria vyote, sura yake ilianza kubadilika rangi na kuwa nyekundu.
Ni kweli anatongozwa sana , lakini haijawahi kutokea mwanaume kuongea kuhusu muonekano wake bila wasiwasi kama Hamza, lakini ilikuwa ni dakika ile aling’ata meno yake kwa hasira
“Wewe mpuuzi , rudia kauli yako tena uone”
“Kapteni nimesema wewe ndio mrembo kuliko wote hapa , lakini ajabu umekaa mwenyewe”
“Ukiendelea kuongea ujinga wako , nitakushushia kipigo hapa hapa bila kujali watu”
“Ah!, basi yaishe Kapteni , nimeacha usije kunipig”Aliongea Hamza akijifanyisha kuwa mzembe huku akinywa juisi yake kwenye glasi.
Yonesi alikosa hata nguvu ya kumfukuza Hamza tena na aliamua kujiweka bize na chakula chake , lakini kadri alivyokuwa akila ndio alivyokosa ule uhuru aliokuwa nao na aliinua macho yae na kumwangalia Hamza , lakini ndio anaona Hamza alikuwa akimkodolea macho eneo la kifuani.
Hamza alikuwa akifurahia chakua chake , kilichomfanya kumkodolea Yonesi macho ni aneo la kifuani tu , alikuwa akiona namna manyonyo yake yalivyokuwa yakivutia.
“Mh , juzi nadhani sijamwangalia vizuri , anaita sio poa”Aliwaza Hamza ndani kwa ndani
“Unaangalia nini?”Aliuliza Yonesi kibabe.
“Unataka kujua kweli wa ninachoangalia?”
“Jibu swali?”
“Naangalia hayo mayai kwenye sahani yako”
“Kuna mayai gani kwenye sahani yangu!!?”Yonesi aliongea kwa hasira mno huku akipiga kofi meza na kufanya watu kugeuka na kuangalia kinachoendelea, lakini Hamza alijifanyisha kuwa bize kula chakula chake.
“Kapteni ni kweli nimekuona na mayai kabisa , tena mawili ..”Hamza aliendelea kumchokoza Yonesi.
“Mbwa wewe ,nani ana mayai , sema ulichokuwa ukiangalia lasivyo nitakufanya kipofu”Aliongea huku akimnyooshea Hamza na uma.
“Kama unabisha , wewe unadhani nilikuwa nikiangalia nini?”
“Kwahio unabishana na mimi , unadhani maneno yangu ni ya bure siwezi kukufanya chochote”
Yonesi kwenye maisha yake hakutaka kuonewa kizembe na kwasababu hasira zishamvaa aliona amshikishe adabu Hamza hapo hapo , hivyo alichukua uma na kumlenga nayo uelekeo wa macho.
Watu waligeuka mara baada ya kuona tukio hilo wakitaka kujua mwisho wake
Lakini Hamza hakukwepa wala kufanya chochote , alikuwa akiendelea kutafuna huku Uma ile ikimkaribia machonni .
Yonesi asingeweza kumchoma nayo kweli machoni na baada ya kufika nchi kadhaa karibu na jicho la Hamza aliishia njiani , upande wa Hamza hakupepesa macho hata kidogo.
Kitendo kile kiliwashangaza watu , maana mtu yoyote angeogopa kwa kulengwa na ncha machoni , lakini Hamza hakuonyesha hofu.
“Kapteni unajua kila mtu anatuangalia , huoni sio vizuri kunichokoza mchana yote hii”Aliongea Hamza akitabasamu , alijiambia Yonesi hata amshikilie bunduki hawezi kuogopa.
Yonesi aliishia kushusha uma chini huku akijiuliza imekuwaje huyo mpuuzi leo kujiaminni hivyo.
“Leo nitakusamehe , ukinichungulia siku nyingine hutoamini nitakachokufanyia” Aliongea na kumfanya Hamza kutabasamu tu.
“Kapteni , naomba kuuliza?”
“Nini?”
“Wewe ni D au F?”
“”…”
Yonesi alishindwa hata kuongea kutokana na namna alivyokuwa amekasirika kwa mara nyingine na Swali lile.
“Mpuuzi wewe , ulikuwa kweli ukinichungul..”
Kabla hata hajamaliza sentensi yake alijizuia mara baada ya kuona ameongea kwa sauti kubwa na kufanya watu kumwangalia , uso wake ulikuwa umebadilika mno kutokana na hasira , hakuwahi kudhalilishwa kiasi hicho ndani ya kampuni.
“Hamza nifuate”Aliongea kwa kuamrisha , hakutaka kuleta fujo ndani ya mgahawa , aliona ni bora amtoe hapo akampe kibano pembeni.
“Sijamaliza kula”Hamza alikataa.
“Wew..”
Kitendo kile kilifanya Yonesi agundue watu walikuwa wakicheka kwa siri na aliishia kusugua meno yake kwa hasira na alifyatua mkono wake wa kulia kijeshi kwa ajili ya kumshika Hamza tai , lakini Hamza alirudi nyuma na kufanya mkono wake kupita.
Yonesi aliona Hamza aliotea hivyo alizunguka upande wa pili kwa ajili ya kumshika , Hamza hakuwa na haraka mara baada ya kuona Yonesi anamkaribia alipiga kiti teke ambacho kilienda kumvaa afande Yonesi na kumfanya akose mhilimili na kuelekea chini akitanguliza uso.
“Ahh..”
Yonesi alijua alikuwa akidondoka vibaya , kitendo cha
Hamza kupiga kiti teke hakukiotea kabisa ,sekunde hio akiona anakwenda kudondoka vibaya Hamza alikuwa ashamzuia kwa mkono mmoja na kumshikilia kifuani sehemu ileile ambayo ilimfanya kukasirika kwa kuchunguliwa.
Yonesi ni kama alikuwa amepigwa na shoti , alijikuta akitetemeka mara baada ya kuona namna mkono wa Hamza ulivyoyashikilia manyonyo yake
“Wewe muhuni umenigusa..”
“Kapteni , unamaanisha nini kugusa wakati nakuzuia usidondoke”Aliongea Hamza na muda uleule Yonesi alisimama vizuri, mara baada ya kuona macho ya wafanyakazi yamezidi kuongezeka , alimwangalia Hamza kwa macho makali.
“Subiri uone , inaweza isiwe sasa hivi ila nitakufanya ujutie kwa ulichonifanyia leo”Aliongea Yonesi kwa hasira na kisha aligeuka zake na kuondoka huku kichwa kikiwa chini , kwa mara ya kwanza mbabe wake ndani ya kampuni alipatikana.
Kila mtu alimwangalia Hamza kwa mshangao na kumkubali , hio ilikuwa mara yao ya kwanza kuona Yonesi akitawaliwa na mwanaume na ashindwe kufanya chochote, wanaume wengi walionekana dhaifu mbele ya Yonesi.
Hamza wala hakujali vile vitisho na baada ya kumaliza kula alichukua matunda ya apple kwenye friji na kisha akaweka kwenye mfuko na kuondoka
nayo , alijua Regina hajala hivyo alijihisi sio vizuri kutopeleka chochote hata kama ataonekana anajipendekeza.
Mara baada ya kutoka kwenye lift moja kwa moja alienda mpaka kwenye mlango wa mkurugenzi na kugonga.
“Come in”
Hamza alisukuma mlango na kisha akaingia , aliweza kumuona Regina akiwa bize amekodolea tarakishi yake huku akionekana kuandika vitu kwa karamu kwenye notebook.
Mbele yake kulikuwa na nyaraka nyingi ambazo ilionekana alikuwa akizifanyia kazi pia , ki ufupi alikuwa bize.
“Weka ripoti hio juu ya meza na unaweza kuondoka”Aliongea Regina bila ya kuangalia aliengia , alijua ni Linda sekretari wake.
Mara baada ya Hamza kuweka matunda yale juu ya meza ndio sasa Regina aliinua macho na kumwangalia.
“Kwanini ni wewe?”
“Sekretari wako kasema hupendelei kula chakula cha mchana na nimeona sio vizuri , kula hata matunda nimekuletea”
“Nishakula na haikuhusu kama nimekula au sijala”Aliongea bila ya ishara ya furaha yoyote.
“Kwahio umekula?”Aliongea Hamza huku akizungusha macho yake na ndio alipoweza kuona mfuko uliojaa makopo , yalikua kama kumi na mbili hivi.
“Gum- syrup!!”Hamza alionekana kushangaa ,
“Hiki kinywaji ndio unachotumia kama chakula cha mchana ?”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumwangalia.
“Kumbe unajua hata jina lake kwa kingereza ni Gum syrup?, kweli wewe ni mwanachuo una exposure ya kujua vitu vingi”Aliongea Regina lakini Hamza hakujali.
“Hata kama unataka kuzuia njaa hutakiwi kutumia aina hii ya kinywaji cha virutubisho , unatakiwa kula chakula?”
“Chakula kinaathiri mzunguko wa damu na oxygen kwenye ubongo na muda wangu wa kufanya kazi ni muhimu sana, sitaki kusinzia, kitu kingine huna kigezo hata kimoja cha kunijali”Aliongea kikauzu.
“Kula angalau hata hayo matunda , kuliko kushinda na tumbo ambalo halina kitu”
Licha ya kwamba Hamza alikuwa akionyesha kumjali , lakini kwake alimuona kama mtu asiemfahamu tu.
“Ondoka nayo , sitokula”Aliongea lakini Hamza alitoa kicheko na kisha akashika simu yake.
“Ngoja nimpigie shangazi na kumwambia unashindia vinywaji vya virutubisho mchana na huna ratiba ya chakula cha mchana”
Regina mara baada ya kuona anachotaka kufanya
Hamza alijua maana yake ni nini , kama kweli Shangazi angelifahamu hilo angekuwa na wasiwasi mno maana kwake ni kama mama. “Weka simu chini , acha kupiga”
“Nitafanya hivyo kama utakula matunda yote
nilioleta la sivyo hili swala nitalifikisha kama lilivyo kwa Shangazi”
“Mbona unapenda kunisumbua na mitunda yako mibaya mibaya”Aliongea huku akionyesha hasira za wazi.
“Nakusumbua sio,ngoja tuone kama nakusumbua , mimi nampigia”
“Wewe inakuhusu ni nini kwanza kula kwangu , unanijali kama nani?”
“Nimeshiba tayari ila kuona hujala chochote nimejikuta na shikwa na huzuni”
“”..”
Regina aliishia kuegamia kiti chake huku akimwangalia Hamza , ni kama hakuwa ametegemea angetoa jibu la aina hio.
“Huzuni utoe wapi , umekaa kiuongo uongo tu”
“Acha maswali mengi , unakula au huli”
“Nitakula , acha kuendelea kunichukiza”
“Hilo ndio jibu sasa , nitakaa hapa hapa mpaka nione umemaliza ndio naondoka”Aliongea lakini Hamza alimwangalia mara baada ya kuona Regina amekunja sura huku ameshikilia mkononi apple.
“Sipendi kula na maganda yake na mimi mvivu wa kumenya”
“Ukila na maganda yake ndio vizuri , yamebeba
Asidi ya kutosha inayosaidia kuondoa uchomvu”
“Ndio hivyo sipendi sasa , unalazimisha”
“Uvivu tu ndio unasumbua “
Aliongea Hamza na kwasababu hakuwa na chaguo lingine ilibidi atafute kisu na kuanza kuyamenya moja moja na kuyaweka kwenye sahanni.
Spidi yake ya kumenya ilikuwa kubwa mno na ndani ya dakika chache tu alikuwa ashamaliza yote.
Regina alianza kuyatafuna haraka haraka , alitaka kumaliza ili aendeee na kazi yake.
“Halafu una malengo gani , kwanini unalazimisha nile haya matunda?”
“Sina malengo yoyote , ninachotaka ni ujaze hilo tumbo lako , kwanini una mawazo mabaya kila ninachofanya”
“Umekaa kimashaka mashaka ndio maana”Aliongea huku akiendelea kula kama abiria anaetaka kumaliza haraka apande basi.
Baada ya Regina kumaliza kula alionekana kukumbuka kitu na kumwangalia Hamza.
“Zile nyaraka ulizotafsiri nimeziona , umetafsiri vizuri sana kuliko hata Freelancer tuliemwajiri kututafsiria mara ya mwisho, nadhani uwezo wako wa kuongea kifaransa na kingereza ni C2?”
“C2 maana yake ndio nini?”
“Hujui?, Inamaana hujawahi kufanya DEF test?, C2 maana yake ni kiwango cha juu cha kuongea lugha ambayo sio uliozaliwa nayo”
“Sijajifunza kifaransa na kingereza kwa njia rasmi, wakati nilipokuwa nje ya nchi nilikuwa nikiongea na watu mara kwa mara ndio maana nilizidi kuzoea”
“Ushawahi kuwa nje ya nchi, masomoni au?”Aliuliza Regina kwa mshangao , alihisi ni vizuri kumjua Hamza angalau kidogo.
“Ndio nilipofikisha miaka kumi nilidhamia nje ya nchi, kutokana na maisha kuwa magumu nilijikuta nikifanya kila aina ya kazi, bahati nzuri kutokana na muonekano wangu wa kuchanganya rangi nikapata familia”
“Sasa ilikuwaje ukarudi?!!”
“Kuna mambo yalitokea ,nilishindwa kuendelea kuishi katika familia yangu mpya mara baada ya kugundulika kama mtanzania”Aliongea Hamza , Regina japo alikuwa na maswali mengi aliona aishie hapo kuuliza , alitamani kujua ilikuwaje mpaka akafika chuo.
Mara baada ya kumaliza kutafuta yale matunda alihisi ukakasi kwenye midomo na alihitaji maji ya moto kwa ajili ya kusukutua.
“Nitakusaidia kumimina maji?”Aliongea Hamza mara baada ya kumuona Regina akisogelea Dispenser ya maji ya moto.
“Nishafika tayari , haina haja”Aliongea na kumfanya Hamza arudi kukaa kwenye sofa.
Lakini sasa kitendo cha Regina kuinama ili achukue Glasi ilifanya gauni lake kupanda juu kutokana na kuwa na shepu kubwa , alikuwa amechukua tahadhari ya kugeukia upande wa nyuma lakini akasahau kuna kioo ambacho kina akisi mwanga.
Hamza alikaza macho , alikuwa na shauku ya kutaka kuona mwanamke kauzu kama Regina huko ndani atakuwa anavaaje.
Regina mara baada ya kugeuza uso wake na kumuona Hamza anapoangalia alishituka na kugeuka nyuma na hapo ndipo alipojua alikuwa akionekana kwenye kioo kwa nyuma.
“Wewe…!!!”
Regina alijikuta akisimama wima huku akijiweka vizuri na kisha akageuka huku akimkazia macho
Hamza , wazo la kumuua Hamza lilimvaa palepale.
Hamza alikuwa ashageuza macho yake na alijifanyisha kushangaa kwa mabadiliko ya Regina.
“Mkurugenzi nini shida , kwanini unafoka?”
“Hujawahi kuona mwanamke , umekuwa chizi?”Aliongea akiwa amekasirika.
“Boss kama unataka kunifokea ni bora ukaniambia sababu , sijafanya kosa lolote”
“Sijawahi ona mwanaume mshenzi kama wewe ambae huna aibu na kuchungulia watu”
“Nini!, unamaanisha nini kukuchungulia , mimi muda wote nilikuwa nikifurahia mandhari mazuri ya jiji letu, Mkurugenzi utakuwa unanifikiria vibaya”
“Bado unabisha tu”Aliongea na wakati huo alimimina maji ya moto kwenye kikombe na kumsogelea Hamza.
“Boss unataka kufanya nini?”
“Kwanini?, unadhani nataka kukumwagia maji kama huna kosa?”
“Mkurugenzi , ni kweli umenifikiria vibaya . ila kama dhamira yako ni kunimwagia maji ya moto basi ni kheri nikimbie tu”Aliongea Hamza lakini muda ule mikono ya Regina ilicheza na kufanya maji ya moto kutoka katika kile kikombe na kuelekea katika miguu yake .
Lakini Hamza alikuwa na spidi kwani aliyakinga yale maji kwa kupitia viganja vyake ili yasimfikie na kitendo kile kilimshitua Regina na mara baada ya akili yake kufanya kazi aliwahi kuweka kile kikombe chini
“Hujaungua?”
“Mikono yangu inasugu na ngozi yake ni ngumu , maji kidogo hivi hayawezi niunguza”Aliongea na Regina mara baada ya kuangalia mikono ya Hamza haijaungua kidogo alijisikia amani.
“Sorry , sijamwaga makusudi”Aliongea Regina bila ya kumwangalia Hamza machoni, hakutegemea kama Hamza angechukua hatua ya kukinga maji na mikono yake yasimuunguze.
“Hakuna shida, ili mradi tu Mkurugenzi hutoendelea kunifikiria vibaya, nitaacha hili lipite”
Mara baada ya kuona namna Hamza alivyoongea kipole aliona pengine ni kweli alimfikiria vibaya na hakuwa akimchungulia.
“Ni kweli hujanichungulia?”Aliuliza kwa kusitasita.
“Kama huniamini basi siwezi kuendelea kujielezea , narudi ofisini kwangu”Mara baada ya kuongea hivyo Hamza alisimama na kupiga hatua kuondoka ndani ya ofisi hio akimuacha Regina kwenye mawazo. “Mkurugenzi , kabla sijaondoka naomba nikuulize swali?”Aliongea Hamza mara baada ya kufika mlangoni.
“Uliza?”
“Huwa unapendelea rangi ya pink plain au pink yenye maua maua?”Aliuliza na kabla hata hajajibiwa alishatoka na kufnga mlango.
Upande wa ndani Regina alinyanyua kikombe kile cha glasi na kurusha mlangoni , lakini ashachelewa na kilichosikika ni sauti ya kuvunjika tu.
“Hamzaaa..!!!”
Regina alitoa ukulele wa hasira huku sura yake yote ikiwa nyekundu.
Aliona mpango wake wa mwanzo wa kumfundisha kazi kulingana na kozi yake anayosomea ulikua ni wa
kijinga , dakika hio hio alishaona alikuwa amemsingizia kumbe yote hayo alikuwa akichezewa akili.
Upande mwingine mara baada ya Hamza kuingia tu katika ofisi yake simu yake ilianza kuita na alipoangalia jina la anaepiga alikuwa ni Amiri rafiki yake.
Alishangaa kidogo kwani tokea siku ambayo alimsaidia kutega kamera hawajaonana.
“Hello!!”
“Bro vipi?”Sauti ya Amiri ilisikika na ilikosa utulivu jambo ambalo Hamza alilijua haraka sana.
“Poa kabisa , mambo vipi?”
“Mambo sio shwari kaka?” “Kwanini unasema hivyo?”
“Hata sijui nikuelezee vipi , ila nimechanganyikiwa tokea jana”Aliongea na Hamza aliamini lazima ni swala linalohusiana na Mellisa.
“Ni swala la Mellisa nini?”
“Ndio kaka, sijui ni mauza uza gani yanaendelea kwa huyu mwanamke , ila naomba tuonane leo hii , ikiwezekana hata sasa hivi , pengine unaweza kuwa na majibu ya nilichokiona”
“Kwasasa kuna mishe imenishika hapa , unaonaje baadae saa kumi na moja”
“Sina jinsi kaka nitasubiri , wewe ndio mtu wangu wa karibu ninaeweza kukushirikisha hili , pengine unaweza kuwa na majibu , mimi nimekwama”
“Sawa nitakushitua”
Hamza baada ya simu ile alikaa kwenye kiti , alikuwa na shauku pia ya kujua ni kitu gani ambacho kimetokea , maana kwa alichokuwa akiongea Amiri alijua kuna jambo kubwa ameona kupitia zile Kamera za siri.
******
Upande mwingine Amosi alionekana akiegesha gari yake katika kituo cha kujazia mafuta cha Puma kandokando ya barabara ya Haile Selasie na mara baada ya kutoka katika gari hio nyeusi aina ya Mercedenz alipiga hatua na kuingia uelekeo wa hoteli ya Peninsula.
Alikuwa makini mno katika tembea yake , ni kama vile mtu ambae anaogopa kufatiliwa, wakati huo simu ilikuwa sikioni na mara baada ya kuignia ndani kabisa ya hoteli hio eneo la mapokezi aliongea maneno machache tu na kisha alisonga mbele na kuzisogelea ngazi.
Jengo la hoteli hio halikuwa refu sana na mara baada ya kufika floor ya tatu alisimama katika mlango wa chumba na akagonga mlango na hazikuchukua hata dakika chache mlango wa chumba ulifunguliwa na ksiha akaingia ndani.
Chumba hakikuwa cha ghali sana , kilikuwa cha kawaida tu kitanda kikubwa cha sita kwa sita pamoja na Tv.
Mtu aliemfungulia mlango alikuwa ni mwanaume wa makamo hivi mrefu mweusi ambae ana nywele ndefu na masharubu.
“Mzigo vipi?”Aliongea Amosi mara baada ya kusalimiana kwa kugongesheana tano.
“Huu hapa boss”Aliongea yule kijana na kuchukua bahasha iliokuwa juu ya kitanda na kumpatia.
Amosi alifungua bahasha ile kwa kuihakiki na kisha alitingisha kichwa kuonyesha kuridhika.
“Kuna maagizo mengine?”
“Hamna , nimepatiwa hizo tu”Aliongea yule bwana na kumfanya Amosi kukagua chumba hicho kwa dakika kadhaa na kisha alitingisha kichwa na kugeuka kuondoka.
“Simama hapo hapo?”Sauti kutoka nyuma ilisikika ikimwamrisha na kumfanya ageuke huku akiinua mikono yake juu mara baada ya kuona amenyooshewa Bastora, huku yule mtu akiwa hana utani hata kidogo kwenye macho yake.
Ni dakika ileile mlango wa bafuni ulifunguliwa na akatoka mwanamke ambae ni kama alikuwa akitoka kuoga kutokana na kwamba hakuwa na nguo zaidi ya Bathrobe ya rangi nyeupe, alikuwa mrembo haswa.
“Tresha!!”Aliongea Amosi kwa mshangao.
“Amosi!!”
Comments