SEHEMU YA 21
Mwanamke ambae alikuwa amepambwa na tabasamu mbele ya Amosi alikuwa ni Tresha , pengine Hamza angekuwepo ndani ya hilo eneo angemfahamu mara moja , ndio mrembo ambae alimpagawisha katika Apartment za Dosam Homes , mwanamke ambae kwa maelezo ya Amiri uzuri wake ni wa kutengeneza na inasemekana ni mfanyakazi wa Binamu Island.
Amosi alimwangalia Tresha kwa dakika kadhaa na kisha akayainua macho yake na kumwangalia mwanaume aliemnyooshea Bastora.
Upande wa Tresha hakuonyesha ishara yoyote ya furaha , ilionekana alikuwa akifahamiana na Amosi lakini muda huo alikuwa siriasi.
“Tresha nini hiki, kwanini upo hapa na nini kinaendelea?”Aliuliza Amosi.
“Nikuulize wewe Amosi unafanya nini hapa?”Aliongea Tresha na alimsogelea Amosi na kisha alichukua ile bahasha.
Amosi alikuwa na wasiwasi mno na kwa haraka haraka alijua kabisa yupo ndani ya mtego.
“Tresha najua unachomaanisha , lakini swala hili linahusiana vipi na wewe?”.
“Swali hilo ulitakiwa kumuuliza aliekupa kazi , nilishakuonya siku nyingi ikitokea umeingilia njia zangu tutakuwa maadui wakubwa na leo tupo hapa”Aliongea na hapo sasa hisia mbaya zilianza kumvaa Amosi na kitu kilichomjia akilini kwake mara moja ni kujiokoa.
Alimjua mwanamke huyo fika , licha ya kuonekana mwanamke mrembo lakini ni kibaraka wa watu wa Binamu Island ambae hana huruma hata kidogo.
“Usije kufikiria kufanya chochote cha kijinga , sekunde ambayo utasogea hata nchi moja ndio utakuwa mwisho wa uhai wako Amosi”
“Unataka nini kutoka kwangu Tresha , kama Binamu wameagiza kifo changu haikuwa na haja ya kuniwekea mtego kama huu”
“Haha.. hubadiliki hata kidogo , siku zote akili yako inafanya kazi kwa haraka ukiwa katika hatari , ungekuwa sawasawa kiakili ungejiuliza maswali mengi kabla ya kuwa mtumwa wa pesa, niambie Amosi umeahidiwa kiasi gani cha malipo kwa ajili ya kufanya kazi ya hatari namna hii , unaniuliza nini nataka kutoka kwako? , hakuna chochote ninachotaka kutoka kwako , Curiosity killed the cat “
Mara baada ya kumalizia msemo ule wa shauku ilimuua paka alimpa ishara yule bwana kumpiga Amosi risasi.
“Wait!!”Amosi alizuia kifo chake na kumfanya Tresha kumpa ishara yule bwana asiruhusu risasi.
“Unataka kusema nini Amosi , kitakachokufanya uendelee kuishi”
“Naomba niulize swali?”
“Kwasababu ya historia yako unaweza kuuliza kabla ya kupoteza uhai”
“Kanali Dastani ndio aliekupatia taarifa juu ya ninachofuatilia?”Aliuliza Amosi akiwa na macho yaliojaa uchungu.
“Ukishajua ni Dastani utafanya nini , unadhani kuna uwezekano wa kulipiza kisasi hata baada ya kufa”
“Kwasababu jibu lako linaweza kunifanya nikupatie kitu cha thamani zaidi kuliko kifo changu”
“Amosi nipo hapa kwa maamgizo ya Binamu , unadhani ni kipi unaweza kuniambia nikaenda kinyume, una kitu gani cha thamani zaidi ya kifo
chako?”Aliongea Tresha huku muonekano wake
ukiwa siriasi lakini swali lile lilimfanya Amosi aone bado hawezi kufa kizembe.
“Nawajua nje ndani Night Shadows na namna ya kuwasiliana nao!!!”Aliongea Amosi na kauli ile ilimfanya yule bwana ambae alikuwa ameshikilia bastora kupepesa macho kwa kumwangalia Tresha na hio ndio nafasi adhimu ambayo Amosi alikuwa akiitafuta.
“Clang!!!”
Ilikuwa ni wepesi wa hali ya juu mno , kitendo cha yule mtu alieshikilia siraha kupepesa macho pembeni baada ya kutaja Night Shadows Amosi alikuwa ashahama aliposimama na kumtupia Bedlamp iliopasuka kwenye mikono yake na bastora kwenda pembeni.
Tresha ambae alikuwa mita kadhaa kutoka alipo Amosi hakuweza kufanya chochote kwani hakuwa na siraha.
Amosi hakuzubaa , mpango wake ilikuwa ni kukimbia na sio kushindana na Tresha , alijua mwanamke huyo likija swala la map[igano hamuwezi maana ni Ninja aliepitia mafunzo na mafunzo yakamzoea.
“Bang!!!”
Bahati mbaya spidi yake haikutosha na bastora iliofungwa kiwambo cha kuzuia sauti ilikohoa , kama sio kupinda kidogo tu pengine ingekuwa mwisho wake palepale.
Amosi licha ya kupigwa risasi hakutaka kusikilizia maumivu , bahati nzuri alikuwa hajauloki mlango , hivyo spidi yake ya kutoka ndani ya chumba hicho ilimfanya kukoswa koswa na risasi nyingine.
“Fuckk!!!”
Tresha alitoa tusi huku yule bwana alieshikilia bastora kutaka kukimbilia nje lakini alizuia.
“Carlos Stop!!!”Aliongea Tresha kwa nguvu na mwanaume mweusi ambae sasa tunafahamu jina lake ni Carlos aliishia mlangoni.
“Tresha tunapaswa kumuua kama oda yetu ilivyo”Aliongea Carlos.
“Umefeli kumuua akiwa mbele yako unadhani unaweza kumuua akiwa kwenye korido , unataka kuibua taharuki , unataka kuonekana katika Kamera”Aliongea Tresha huku akionyesha hali ya kukasirika.
“Wewe ndio umesababisha misheni imefeli , nilikuambia tokea mwanzo hili nitalimaliza mwenyewe , kulikuwa na haja gani ya kutaka kushiriki?”Aliongea Carlos na kauli ile ilimfanya Tresha kutoa tabasamu.
“Ndio tulipaswa kumuua , lakini ni mpaka atupe taarifa tuliohitaji , likija swala la kuua Carlos unatoka nje ya malengo ya misheni”Aliongea na kumfanya Carlos kuvuta pumzi na kuzishusha.
“Ninachojua mimi ni kuua, nimefundishwa hivyo?” “Ndio maana ya uwepo wangu hapa Carlos, tunapaswa kupata taarifa tunayotaka kutoka kwake , ndio tumuue sio vinginevyo?”
“Ameshakimbia , unadhani itakuwa rahisi?”
“Hilo niachie mimi , namjua Amosi nje ndani , nimefanya nae kazi kwa muda mrefu”Aliongea na kisha mwanamke huyo aliangalia mazingira ya chumba na kisha alichukua bahasha ambayo Amosi alionekana kuifuata na kutoa makaratasi na kuyakagua kwa muda.
“Unapaswa kuondoka”Aliongea Tresha ambae alipanda juu ya kitanda na kujiachia na kumfanya Carlos kumwangalia mrembo huyo kwa macho ya kimatamanio lakini Tresha hakujali macho yake na palepale aliweka bastora yake kwenye kiuno na kutoka nje huku akidhibiti hasira zake.
Upande mwingine Amosi alikuwa amesambaza matone ya damu kila mahali ndani ya hoteli hio lakini hakujali , hata watu aliopishana nao wakati akiwa ameshikilia ubavu wake wa kushoto hakutaka kuwapa hata nafasi ya kuona sura yake , ki ufupi akili yake ilikuwa katika tahadhari ya kujiokoa na alikimbia kweli.
Hoteli hio ilisifika kwa ulinzi mkali na usalama lakini kilichotokea kiliwashangaza watu.
Dakika chache alikuwa ashatokezea barabarani na kuanza kujikongoja kusogelea gari lake.
“Amosi!!”
Sauti ilimwita, ilitokea katika gari nyeupe RAV4 iliosimama kando ya barabara , Amosi aliangalia gari hio na kuonekana kuitambua na bila ya kujiuliza mara mbilimbili aliisogelea, mlango wa gari hio ulifunguliwa na aliingia ndani na hapo hapo ikaondoshwa.
*****
Hamza mara baada ya kumaliza kuongea na simu iliotoka kwa Amiri alikaa kwenye tarakishi na kisha alianza kufanya utundu wake , alishajua tarakishi za wafanyakazi zinafuatiliwa hivyo alitaka kuifunga tarakishi yake ki ujanja aendelee na mambo yake bila kushitukiwa.
Dakika ambayo ndio anamaliza kuseti mitambo , Linda aliingia akiwa na rundo la makaratasi mkononi , zilikuwa nyingi kiasi kwamba hata kubeba alionekana kupata shida.
“Hizi nyaraka unatakiwa kuzitafsiri kutoka kingereza kwenda lugha ya kiswahili , ziishe zote leo hii”Aliongea kikauzu na kauli ile ilimshangaza Hamza.
“Linda haiwezekanni ni nyingi mno kumalizika kwa siku moja “
“Bosi ndio kasema , eti kwasababu uwezo huo unao hataki kuona ukipotea bure”Linda aliweka nyaraka zile mezani na kisha kwa maringo alitoka.
Alikuwa akijua kabisa Hamza amemchokoza bosi , kwani alisikia akipiga makelele kutoka ndani ya ofisi yake ndio maana akapewa adhabu hio.
Ki ufupi kwa Regina ilikuwa ni kisasi mwanzo mwisho ili kumkomesha.
Hamza aliishia kujisikia uchungu lakini hata hivyo alikuwa akiupenda mshara wake hivyo aliishia kukubali kufanya kazi.
“Bora ningejifanyisha tu sijaona kitu , angalia sasa msala niliojitengenezea”Aliwaza Hamza.
Mpaka inafika jioni Hamza aliweza kutafsiri nusu tu ya kazi yote aliopewa na aliona hakuna uwezekano wa kumaliza yote na aliona atafute namna yoyote ya kuongezewa siku.
Lakini kabla hata hajajua cha kufanya mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na Linda.
“Ni muda wa kuondoka kazini sasa , nenda maegeshoni na washa gari , washa AC na kisha msubiri bosi”Aliongea na Hamza alivuta pumzi ya ahueni , alikuwa amechoshwa kweli kuendelea kukaa hio sehemu.
Aliingia zake kwenye lift ambayo ilimpeleka moja kwa moja mpaka maegesho ya chini kabisa ya jengo hilo na kutoka , lakini wakati akitaka kusogelea gari ya Regina aliweza kumuona Kapteni Yonesi akiwa amesimama pembeni huku akimwangalia kwa macho yaliojaa sumu.
Ilionyesha ni dhahiri alikuwa amejitega hapo ili kumpata Hamza amshikishe adabu.
“Wewe mhuni hatimae umejitokeza”Aliongea kikauzu.
“Kapteni ndio unajiandaa kutoka kazini na wewe , hehe kwaheri tutaonana kesho”Aliongea Hamza akijifanyisha mjinga.
“Nani kakuambia naondoka?, unadhani naweza kusahau kirahisi kilichotokea mchana”
“Mchana kumetokea kitu gani?, mbona hata sina kumbukumbu”
“Wewe mpuuzi usie na aibu , kwahio unakataa kosa lako sio , umenidhalilisha mbele ya watu na sijakufanya chochote , huu ndio muda , nisipokushikisha adabu siwezi kuendelea kuitwa Kapteni”Aliongea na sekunde ileile alifyatuka kama mshale akitanguliza mguu akilenga maeneo nyeti ya Hamza.
Hamza aliishia kukwepa pigo lile na kumfanya Yonesi kupita.
“Kapteni ukiendelea hivi utanikasirisha ujue , mimi ni mwanaume na sio vizuri kupigana na mwanamke” “Unajiita mwanaume , kwangu wewe ni mwanaume ulievaa suruali tu, kama unajiamini pigana na mimi tuone”Baada ya kuongea hivyo alijiandaa kumshambulia tena Hamza lakini aliishia njiani mara baada ya mlango wa lift kufunguka na Regina kutoka.
Regina mara baada ya kuona tukio lile alijikuta akishangaa huku akikunja sura.
“Yonesi , nini kimetokea?”
“Boss nina mashaka na tabia ya huyu mtu …”Aliongea Yonesi na kuanza kuelezea kilichotokea mchana juu ya Hamza kumchungulia manyonyo yake na kisha kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi.
“Boss tusipomshikisha adabu mapema , hii tabia itafanya wafanyakazi kunidharau”Aiongea Yonesi akipigilia msumari.
“Mkurugenzi , usimsikilize Yonesi na porojo zake , mimi hio tabia ya kuchungulia watu sina kabisa , mimi nilikuwa nimekaa zangu kwenye meza tukiwa tunaangalia na nilimsifia kidogo tu kama ni mrembo na ndio akakasirika”Hamza alijitetea , lakini kwa bahati nzuri au mbaya Regina na Yonesi wote ni wahanga wa tabia ya Hamza na kwa muda huo alikuwa akimchukia mno Hamza kiasi kwamba mpaka meno yake yalikuwa yakimuwasha., Alidhani swala lile lilimtokea yeye tu kumbe alikuwa amemfanyia uhuni na Mlinzi wa kampuni .
Dakika hio hio Regina aliona aungane na Yonesi kumshikisha Hamza adabu l akini hakutaka kuonyesha kama alikuwa na yeye ni mhanga wa kupigwa chabo.
“Kama ni hivyo basi unaruhusa yangu ya kumshikisha adabu , angalia tu usije kumuua au akalazwa, anapaswa kuja kazini”Aliongea Regina na kumfanya Hamza amwangalie na kuona namna ambavyo Regina alikuwa amejaa sumu juu yake.
“Usijali mkurugenzi , najua ninachokifanya”Aliongea Yonesi na palepale muonekano wa kishujaa ulimjaa, alikuwa kama komandoo anaejiandaa kwa misheni ‘shikisha adabu’.
Subiri kwanza , twendeni mpaka floor ya pili katika chumba cha mazoezi”Aliongea Regina , alijua ikitokea mfanyakazi wa kampuni kushuhudia tukio la
Yonesi kumpigwa Hamza inaweza kuleta shida
“Kuna haja ya hili , mkurugenzi au unakinyongo na mimi?”Aliuliza Hamza.
“Eliza alisema wewe ndio uliemsaidia kumuokoa katika udhalilishaji , naamini unao uwezo wa kushindana na Yonesi japo kidogo, chukulia kama mazoezi ya kukuweka fiti kidogo uonekane mwanaume”Aliongea Regina.
Hamza hakuwa na jinsi zaidi ya kutii maagizo ya Mkurugenzi na kwenda katika floor ya pili kwa ajili ya kushikishwa adabu.
Dosam ilikuwa ni kampuni yenye wafanyakazi wengi na biashara zao zilihusisha bidhaa za thamani , hivyo walikuwa na kitengo cha ulinzi ambacho ikitokea mzigo unasafirishwa basi ndio huhusika kuimarisha ulinzi , hivyo kwa ajili ya idara ya ulinzi ilitengwa floor nzima ya pili kwa ajili ya mazoezi , kulikuwa na kila aina ya vifaa ikiwemo Gym na hata eneo la kupimana nguvu.
Ilikuwa ni muda wa kuondoka kazini , hivyo hakukuwa na watu ndani ya eneo hilo.
Yonesi alimchukua Hamza na kumpeleka katika
Arena , alifanya hivyo ili isitokee Hamza akakimbia wakati wa kumpiga.
“Ni kweli unataka kupigana na mimi?”Aliuliza Hamza.
“Usiwe na wasiwasi , ngoja nikunyooshe nyooshe viungo , lakini sitokuua”
“Basi hakuna shida , ila kumbuka miguu na mikono haina macho hivyo kuwa makini”
“Acha woga , jali usalama wako kwanza”
Mara baada ya kumaliza sentesi hio Yonesi alimsogelea Hamza kwa spidi huku akinuia kumchapa ngumi ya bega.
Lakini alichokifanya Hamza ni kuwa na spidi kidogo tu kwani mara baada ya ngumi ile kumfikia aliinama ikapita lakini muda huo huo bila ya Regina kuona
Hamza alishainua mkono na kugusa msambwanda.
“Ahhhhhh…”
Yonesi alijikuta akipiga makelele mara baada ya kuhisi mkono ukimgusa upande wa kushoto.
“Mshenzi wewe” Ishara ya mauaji ilimvaa Yonesi. “Kapteni vipi tena , mbona unafoka wakati tunapigana?”Aliongea Hamza ambae alikuwa amejificha kwenye kona ya steji.
“Umenigusa tena”,
“Unamaanisha nini nimekugusa , kwahio wewe unaweza kunipiga lakini mimi siruhusiwi kukugusa, kama ni hivyo unaweza kuniua hapa hapa”.
“Mhenzi wewe , hujui kupigana kazi yako ni kugusa tu”
“Nimegusa wapi?”Hamza alikuwa akijua fika ni wapi amegusa lakini alijifanyisha hajui , alijisikai vizuri, alitaka kumshikisha adabu mjeda huyu bila hata ya kumpiga.
Regina alikuwa akiangalia pambano na hakuwa akielewa kinachotokea , kutokana na spidi ya Hamza.
Yonesi hakujua namna ya kuongea tena hivyo alijiamulia kupambana tu , awamu hio alikuwa amedhamiiria kumpiga Hamza kwa kutumia mguu na sio ngumi tena
Hamza aliishia kuvuta pumzi na dakika ambayo shambulizi linamfikia alishafanikiwa kusogea kushoto.
Yonesi alijikuta akipandwa na hasira mara mbili mara baada ya kuona amepiga hewa , lakini hakutaka kujiuliza Hamza kaweza vipi kukwepa shambulizi lake hivyo aligeuka na kumsogelea tena na kuanza kurusha ngumi mfululizo.
Hamza alikuwa akijifanyisha kuwa muoga wa ngumi zile na kurudi nyuma kila mara Yonesi alipokuwa akishambulia , alionekana kama amezidiwa lakini ukweli ni kwamba yeye ndio aliekuwa na maamuzi ya kumaliza pambano hilo au kulirefusha
Yonesi aliishia kumkimbiza Hamza kila mahali alipohama lakini mwisho wa siku yeye ndio aliekuwa wa kwanza kuchoka.
“Kwanini unakuwa muoga na kukimbia kimbia kama panya , kama kweli wewe ni mwanaume usikimbie na tupigane ana kwa ana”
“Kapteni unachofanya ni kulazimisha nifanye kitu ambacho sitaki na kwasababu sitaki nitaendelea kukimbhia”
“Kuwa mwanaume basi”Aliongea kwa kufoka.
Hata Regina ambae alikuwa akiangalia alishindwa kuvumilia mara baada ya kuona Hamza anachofanya ni kukwepa tu na hashambulii.
“Hamza jikaze basi hata kidogo?”Aliongea.
“Nijikaze niumie , naogopa nisije kupoteza taifa la kesho hapa hapa”
“Huna lolote , pigana na mimi acha
kukimbia”Aliongea Yonesi na palepale alimsogelea Hamza kwa mara nyingine , uwezo wa Yonesi kuanzisha mashambulizi haukuwa wa kawaida , alikuwa akijua kujipima wakati wa kushambulia mno alichokosa ni spidi tu basi na ndio maana kila shambulizi alilorusha Hamza alikuwa na uwezo wa kulikwepa bila shida yoyote
Mwishowe Yonesi aliona kabisa Hamza pengine kuna kitu anaficha , inawezekana vipi mtu wa kawaida kuweza kuwa na stamina ya aina hio , maana yeye alikuwa amechoka lakini Hamza ni kama bado ndio anaanza na anahema kawaida tu.
Kilichomkasirisha zaidi ni kwamba mpuuzi huyo alikuwa akimwigizia na hakuwa akionyesha uwezo wake kabisa , kitendo hicho kilimfanya Yonesi aone ni udhalilishaji.
Mara baada ya kufeli zaidi ya mara tano , hatimae alipata wazo ambalo lilimfanya adondoke chini kwa kupiga magoti na kufunika uso wake na viganja na kuanza kulia kwa kwikwi.
Kwa namna ambavyo Yonesi alikuwa akilia ilikuwa ni kama mke aliefiwa na mume wake , mtu yoyote angemuona mjeda huyo mrembo angemuonea huruma.
Hamza alijikuta akiingiwa na aibu baada ya kuona Yonesi analia hata kwa Regina hivyo hivyo alishangaa kuona Yonesi analia, maana ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona afande akilia baada ya kupigwa.
Ukweli ni kwamba Regina hakuona Hamza akimpiga Yonesi na upande mwingine alimjua Yonesi kama mwanamke jasiri na mkali.
“Hamza muombe msamaha Yonesi , kama mwanaume unatakiwa kujua wakati wa kuacha”Aliongea Regina lakini Hamza alijihisi ni kama anaonewa , maana hakumpiga hata kidogo Yonesi.
Hamza hakutaka kuona Yonesi akiendelea kulia na alimsogelea kwa ajili ya kumbembeleza
“Kapteni usiendelee kulia , nimekosa mimi nisamehe sa…”
Kabla hata Hamza hajamaliza kuongea Yonesi aliibuka na kibao na kumchapa nacho Hamza upande wa kushoto, baada ya kibao aliunganisha na ngumi kwenye tumbo na kumfanya Hamza kutoa mguno.
“Naomba unisamehe Kapteni , vinauma , vinauma”Hamza alibembeleza asemehewe huku akifanya kuugulia maumivu chini sakafuni.
“Wewe mpuuzi nitahakikisha kila siku utakayoniona unanikimbia”Aliongea Yonesi huku akisimama na kupumua kwa ahueni.
Regina aliekuwa chini ya steji alishia kushangaa mara baada ya kugundua kumbe Yonesi alikuwa akijifanyisha mdhaifu kutafuta nafasi ya kumshitukiza Hamza.
Mashambulizi yale yalionekana kumuumiza Hamza na Regina alijiuliza atakuwa katika hali gani.
Mara baada ya kilichotokea Regina aliishia kumlaani Hamza ndani kwa ndani kwa kujifanyisha kijeba na kuchungulia chungulia wanawake na kujiambia anastahili kweli kipigo.
Mara baada ya kumshinda Hamza , Kapteni Yonesi hakuhisi hata kidogo furaha wala mafanikio , alikuwa akijua kabisa yeye ndio ambae ameshindwa.
Aliishia kujiwazia huyu Hamza kila dakika anazidi kuonekana sio wa kawaida na pengine hata kufanywa kuwa msaidizi ni kutokana na Regina kufahamu hilo.
“Mkurugenzi , nitaondoka sasa , kwaheri”Aliongea Yonesi.
“Ni kweli unapaswa kwenda kupumzika , siku imekuwa kubwa kwako”Aliongea.
Hamza alikuwa bado amelala kwenye steji licha ya Yonesi kuondoka na Regina alimwangalia kikauzu.
“Uko sawa wewe? , kama bado hujafa amka tuondoke”
“Regi nimeumia kwa ndani”Aliongea Hamza.
“Acha maigizo , kama huamki naondoka zangu”
“Nataka busu ili niamke”Aliong ea na kauli ile ilimshangaza Regina na kumfanya kuona aibu za kike , lakini tofauti na kuwa na hasira alimuuliza.
“Wapi unataka upigwe busu?”
Hamza mara baada ya kusikia swali lile alijikuta akifurahi na kujiambia kumbe kupigwa nako kuna faida na kwa haraka haraka alitumia kidole chake kuonyesha eneo la mdomoni.
Regina alivuta pumzi nyingi huku ukauzu ukizidi kumvaa , aliangalia pembeni na kuona kifaa cha kuchukulia mazoezi ya mkono na mara baada ya kukiokota alimlenga nacho Hamza mdomoni.
“Kiss your ass!!”
Hamza aliweza kukwepa haraka kifaa kile kabla hakijampata na kusimama na kumwangalia mwanamke huyo alivyokuwa amefura kwa hasira. “Hey! Nilikuwa nakutaia tu usikasirike hivyo”
“Ukiendelea kuongea ujjinga nitahakikisha unapata mshahara nusu”
“Ah , boss basi yaishe, nimekosa mimi naomba usinikate mshahara , nitaenda kuwasha gari tuondoke sasa”
Hamza hakutaka kukosa pesa kwa tukio dogo kama hilo , isitoshe kutafsiri makatarasi yote yale haikuwa kazi ndogo ambayo anaweza kukubali kukatwa mshahara kizembe.
Lisaa limoja baadae wote waliweza kufika nyumbani na Shangazi alikuwa bize kuandaa chakula cha usiku.
“Hamza vipi siku yako ya kwanza kazini?”Aliuliza na Hamza alitaka kusema amenyanyaswa siku nzima lakini Regina alimpiga jicho asije kuongea ujinga na akaacha na kuanza kucheka.
“Haha.. Shangazi siku yangu ilikuwa nzuri sana , sitaki tu kuongelea ilivyokuwa lakini ,itoshe kusema nimepata Vitamini ya macho”
Kauli yake ilikuwa na zaidi ya maana na kumfanya Regina aliekuwa pembeni yake kupandwa na hasira na kutaka kumpiga na rimoti palepale.
Hamza alikuwa na miadi yake hivyo hakutaka kukaa sana nyumbani , ijapokuwa chakula ndani ya nyumba hio kinawahishwa hakutaka kula kwanza mpaka amalizane na Amiri., hivyo alipandisha juu kujiandaa kuondoka lakini wakati anashuka aliweza kumsikia Regina akiongea na simu na moja kwa moja aliweza kujua ni baba yake aliekuwa akiongea nae lakini aliishia kukaa kimya , ilionekana kuna jambo ambalo liliwafanya kujibishana tena.
“Shangazi natoka kidogo , kuna rafiki yangu nataka kuonana nae”Aliongea Hamza.
“Lakini chakula cha usiku kinakaribia kuiva utawahi kurudi?”
“Sijajua Shangazi , kama nitachelewa naomba uniwekee tu nitakula nikirudi , anaonekana kuwa na matatizo”Aliongea Hamza na Shangazi alionekana kumuelewa , ukweli alifurahi kuona Hamza alikuwa angalau na rafiki.
“Sawa, wahi ukamuone rafiki yako”
Hamza mara baada ya kuaga alitaka amuage Regina lakini mwanamke huyo alionekana bado alikuwa akiongea na simu , huku muonekano wake ukiwa umebadilika hivyo alijua maongezi hayo ni siriasi.
Alitoka nje na kuchukua ile Lexus ya Regina na kuondoka , akiwa njiani alimpigia Amiri lakini hakupokea , lakini hata hivyo hakutaka kughairi , aliendelea kuendesha na wakati anakaribia daraja la kigamboni simu iliita.
“Uko wapi bro , nilikuwa nimetingwa kidogo”
“Okey , ndio nimetoka niambie tuonane wapi?”
“Samaki Samaki bro , ukikaribia nishitue”
“Poa”
Licha ya kwamba anakoenda ni mbali , lakini kutokana na kuwa na gari kali hakuona shida , pili hakuwa ametoka usiku muda mrefu.
Ilikuwa ni saa moja kwenda na nusu na foleni hazikuwa kubwa sana upande wa magari yanayorudi mjini , hivyo hakupata shida kubwa, dakika arobaini tu aliweza kufika Samaki Samaki na alimpigia simu Amiri.
“Bro umewahi mno , nikajua kwa foleni utachukua muda kidogo kufika”
“Nipo na usafiri binafsi , tuonanae wapi”
“Ah kumbe , nisubiri hapo mgahawani nakuja muda si mrefu”
Hamza aliangalia mazingira ya eneo hilo na palionekana kuchangamka, kulikuwa na magari mengi.
Kutokana na gari yake kuwa ya bei ghali hakupata shida ya kuegesha , watu waliomuona akitoka kwenye gari hio ya Lexus walimwangalia kwa macho ya maswali mengi.
“Bro!!!”
Hamza kabla hata hajapiga hatua kuingia ndani ya mgahawa aliweza kuitwa kwa nyuma na aligundua aliekuwa akimwita ni Amiri.
“Nilijua utachukua muda”Aliongea.
“Nilikuwa maeneo haya haya , njoo tuongee kwenye gari”Aliongea Amiri huku akizungusha macho.
Amiri alikuwa ameegesha Aud yake katika maegesho ya muda mfupi na waliingia ndani wote , jamaa huyo alionekana kuwa na haraka mno na hilo Hamza aliliona.
“Unaonekana akili haijatulia lakini kwa muonekano wako nadhani hali sio mbaya kama nilivyofikiria”Aliongea Hamza.
“Nimechanganyikiwa kutokana na kuwa na maswali mengi , lakini bado nina hofu , pengine unaweza kunipa jibu ambalo linaweza kuifanya hali yangu kuwa mbaya zaidi”Aliongea.
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , wewe ndio ambae ulichukua hatua , inabidi kuyakabili matokeo”
“Nadhani tuongelee hapa hapa kwenye gari , nina miadi na Melisa , nimepata ahueni tumeonana kabla ya kukutana nae”
“Unakutana nae sasa hivi?”
“Ndio , nilimuahidi nitamtoa Out leo , japo nina wasiwasi na kinachoendelea lakini angalau nataka
kuondoa huu mkanganyiko kabla hatujaonana”Aliongea na palepale alitoa simu pamoja na Earpod na kumpa Hamza.
“Sikiliza hio na unipe majibu”
“Nisikilize tena , nikajua ni Vidio”
“Bro , tuliweka kamera za vidio ndio lakini sikuweza kuona cha maana, mpaka siku moja nilipoona tukio ambalo sio la kawaida , ndio ambalo lilinipelekea kuweka kinasa sauti”
“Tukio gani?”Hamza aliuliza kwa shauku.
“Sikiliza kwanza hio sauti niliosikia kutoka ndani kwake”Aiongea na Hamza alitingisha kichwa kukubali.
Comments