Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

Hamza  kadri alivyokuwa akisikiliza  ndio uso wake ulionyesha mabadiliko , hayakuwa mabadiliko ya mshangao bali ya kuchanyikiwa pia.

“Mbona  nasikia lugha  ambayo sijawahi  kuisikia popote  ni  lugha gani hii?”Aliongea Hamza na kumfanya Amiri na yeye kuonyesha ishara ya kutokujua.

“Hapo ndio  pamenichanganya sana ,  hio sauti ni ya Mellisa wangu , siwezi kosea Bro , lakini anaongea lugha ambayo siijui”Aliongea Amiri  na  Hamza aliongeza umakini katika kusikiliza ili ajaribu  kutafsiri  nini kinaongelewa , alikuwa akisikia sauti ndio lakini lugha  hajawahi kuisikia.

“Hii lugha sijawahi kuisikia popote , au ni lugha sizizo rasmi za kimakabila, wanaongea nini”Hamza alionekana kujiuliza.

“Baada ya hapo  watabadili  lugha , sikiliza kwa umakini  bro”Aliongea Amiri  na Hamza alitingisha kichwa na kusikiliza.

“Silvia  kadri  tunavyochelewa ndio  uwezekano  wa kurudi kuwa mdogo , tunatakiwa kumpata  Princess Natasha  mapema kabla ya Profesa”

“Rosaron   hatujui  mpaka sasa  roho ya Natasha inaishi katika mwili wa nani ,  sio rahisi  kumpata”

“Atatutafuta  yeye mwenyewe baada ya teknolojia ya

Somnus  kufanikiwa , tunatakiwa kusubiri lakini kuwa tayari vilevile, kosa kidogo tu  litamuamsha  na Profesa , wakiungana itakuwa ngumu kwetu”

“Rosaron  unadhani  tupo sahihi ,  namaanisha Pincess Natasha kuwepo hapa  Tanzania!!?”

“Tumefika hatua hii kutokana na imani  tulioaminishwa , njia pekee  ya sisi kuonekana  ni kurudi, Silvia wewe ndio uliekuwa mpenzi  wake , mapenzi yana nguvu  akiamka  atakutafuta wewe, ndio maana upo hapa”

Hio ndio  namna ambavyo sauti zilisikika , lakini katika maongezi hayo  Hamza na Amiri wote hakuna ambae alisikia neno  Mellisa , kwa maana kwamba maongezi hayo  hayakumhusu Mellisa.

“Sijasikia  jina la Mellisa”Aliongea Hamza

“Sijasikia jina   lake pia , lakini sauti ni yake”

“Una uhakika  hio ni sauti ya Mellisa?”

“Ndio , siwezi kusahau sauti ya Mellisa hata niwe nimelewa pombe”Aliongea na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.

“Vipi sauti ya  pili  unaitambua , namaanisha hio ya mwanaume?”

“Sijawahi kuisikia , lakini kwa rafudhi yake

anaonekana sio mbongo”Aliongea na Hamza pia alikubaliana na  Amiri sauti ya  pili ilikuwa sio  mtu mwenye rafudhi  ya kiswahili.

“Hebu  subiri”Aliongea Hamza na kisha alichukua Earpord zote mbili na kuzitumbukiza kwenye masikio na kupelekea mbele  ile rekodi ya sauti, Amiri  alibakia kimya asijue nini ambayo Hamza anajaribu kufanya.

Hamza alikuwa akisikiliza ka kurudisha nyuma sauti na kwenda mbele  na ndani ya dakika tano alitoa Eapord  zile masikioni.

“Umegundua nini?”

“Najiuliza kwanini hawakuendelea kuongea kwa  ile lugha na kubadilisha katika lugha ya kiswahili , pia  sauti ya mwanaume tuliokuwa tukisikia ni ya Mzungu rafudhi  yake , tena mzungu wa Ulaya  kila kitu kinaonyesha  alikuwa akiongea na  Mellisa kutumia kifaa maalumu au simu”

“Unamaanisha  hakuwa ndani  kwa Mellisa?” Aliuliza Amiri na Hamza alitingisha kichwa.

“Kama hakuwepo unazungumzia  nini kuhusu jina la

Silvia , kwanini huyo mzungu kamtambua  kama Silvia mpenzi wangu?”

“Hapa siwezi kukupa jibu la moja kwa moja , kuna mawili  ambayo yote yanawezekana , kuna uwezekano  ni kweli Mellisa  ni Silvia  au   huenda ana multiple Personality,  kuhusu  kuwa Silvia  hilo  halina maelezo mengi  lakini  kama kweli  ana ugonjwa wa nafsi mbili  ni ngumu kufanya mawasiliano  na mtu au mtu kupigia akitarajia Mellisa kuwa Silvia au Silvia kuwa Mellisa”

“Kaka sijakuelewa kabisa ,

umenichanganya?”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza amwangalie machoni , ni kweli bwana huyu alionekana kuchanganyikiwa.

“Ushawahi kuagalia filamu  ya Split?”

“Bro mimi sio mpenzi wa Filamu  kabisa”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.

“Okey , ipo hivi  ninachomaanisha mpenzi   wako Mellisa  kuna uwezekano akawa mgonjwa wa akili   wa  kuwa na  nafsi mbili , yaanni nafsi ya Mellisa na muda mwingine anakuwa Silvia kama ulivyosikia,  ila kwa hapa nashindwa kuamini moja kwa moja , kwasababu kama kweli ni Silvia  kwanini akaongea lugha ambayo haieleweki  na baadae akahamia katika lugha ya kiswahili kama kawaida, vipi kuhusu alichokuwa akiongea ni kitu cha uhalisia?”

“Kwahio unamaanisha anaweza asiwe mgonjwa wa akili au vipi , mpaka kuweka hayo maswali?” “Ndio anaweza asiwe na shida hio?”

“Kama sio hivyo  atakuwa na shida gani?”

“Kuna kitu nakiwaza lakini sina uhakika nacho , hata kama nikikuambia nitazidi kukuchanganya , kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho Mellisa  hakusaliti kama ulivyomdhannia, sauti  ya mwanaume  ukisikiliza kwa umakini  sio  katika ile nyumba”

“Bro unaonekana kujua vitu  vingi na ndio sababu ya mimi kukushughulish, awali nilitaka kuona kama kweli Mellisa ananisaliti lakini  hisia zako na zangu  sasa hivi zimefanana , lakini hilo sina shida nalo , Mellisa ana tatizo  na  mimi kama mpenzi  wake napaswa kumsaidia , Bro yule mwanamke nampenda na napanga kumuoa  kabisa , hili swala lazima nilipatie ufumbuzi”Aiongea  Amiri  akiwa siriasi. “Hili swala nitakusaidia  lakini utahitaji kuwa mvumilivu , kitu ninachotaka kujua  kutoka kwako je  kuna chochote  kitu ambacho sio cha kawaida ushawahi kuona   pale anapoishi  na kwanini ulidhania anakusaliti?”

“Alianza kubadilika , nilikuwa na tabia ya kwenda kwake usiku , lakini siku moja  nakumbuka ilikuwa Jumaane miezi minne iliopita , nilikuwa nimelewa siku ile nilipofika kwa Mellisa alikataa kabisa nikiingia ndani  na alipogundua ni  mimi  hakufungua  kabisa, kutokana na pombe  sikujua kilichotokea , lakini asubuhi nilikuwa  ndani  kwake , mwanzoni nilidhani baada ya kulewa nilikuja kwake akanifungulia kawaida nikaingia , lakini mara baada ya tukio  la pili ndio kumbukumbu za siku  hio zikajirudia  na  kukumbuka alikataa kunifungulia”

“Tukio  la pili likoje”

“Hii siku hakunikatalia  kuingia ndani , ila alinisubirisha  kwenye mlango , jambo hili halikuwa la kawaida , baada ya dakika kama tano niliingia ndani lakini  kuna harufu   kama marashi hivi ambayo  Mellisa hatumii , nilitafuta haya marashi wakati akiwa amelala  lakini sikuyaona , haikuwa hivyo tu usiku  alikataa  kunipa kabisa, haikuwa mara ya kwanza au mbili tu Bro , imekuwa kama   ratiba , kila nikienda  kwa Mellisa siku ya Jumanne lazima anifanyie janja janja nisile mzigo”Aliongea na kumfanya  Hamza kumwangalia Amiri.

“Umesema kila Jumanne , inamaana  hata  siku ulioenda kwake amelewa na  mara  ya pili kunusa harufu  ambayo sio ya kawaida , ilikuwa Jumanne?”

“Ndio nakumbuka siku niliolewa ilikuwa jumanne , ki ufupi  Mellisa kila ikifika Jumanne  hataki tuonane kabisa , hii ndio sababu ya  kumuwekea kinasa sauti  , zile kamera zilikuwa zikileta picha tu ila sauti hakuna , nikaenda kuweka  kinasa sauti na jana ndio nimesikia hiki ulichosikia”

Muda uleule simu ya Amiri ilianza kuita  na mara baada ya kuangalia jina alimpa ishara  Hamza kwamba ni Mellisa ndio anapiga.

“Muda mzee , nilioahidiana nae”Aliongea Amiri   na Hamza alimpa ishara apokee simu kwanza.

“Babe  uko wapi , mbona hutokei?”

“Nakuja dakika chache , nipo  maeneo haya haya” “Sawa , wahi njaa inaniuma”

“Sawa love , nakuja”

“Kwahio  unasemaje Mzee?”Aliuliza  Amiri mara baada ya  kumaliza kuongea na simu.

“Kuwa nae karibu kwanza , angalia kama kuna kitu  kisicho kawaida , au matumizi ya dawa yoyote, kwasasa  nina shauku na hii lugha  waliokuwa wakiongea mwanzo, naweza kuchukua  sauti zao nikaitafutie ufumbuzi?”

“Nakuachia kila kitu mtaalamu , mwenyewe nina shauku ya kutaka   kujua Mellisa anaongea  lugha gani , mwanzoni nilijua labda  ni roho mtakatifu , yule ni mkristo na wakristo kuna muda wanaongea lugha zisizoeleweka”

“Kunena kwa lugha  wanaita , inawezekana  mpenzi wako alikuwa akinena kwa  Lugha   wakati akiongea na Rosaroni”Aliongea Hamza na kumfanya  Amiri kutabasamu.

“Unazingua kaka”

“Sijazingua , naamaanisha ni kitu ambacho hakiwezekani  kunena kwa ligha huku unaongea na mtu  , tena mzungu”

Amiri  alichomoa flash na kuunganisha na OTG kisha akakopi faili  lile la sauti na kumpa  Hamza.

“Ukipata chochote  nishitue  nakuaminia sana mtaalamu”

“Nikifanikiwa nitakuambia , ila kuhusu hii lugha…anyway nitakushitua”Aliongea Hamza  na kisha alishuka kwenye gari.

“Sema mzee hatujaonana  kama wiki na nusu hivi ila muonekano wako  umebadilika sana, umekuwa bomba”Aliongea Amiri akiwa ameshusha kioo , ni kama sasa anamuona  Hamza akia na mavazi ya bei  ghali.

“Nimeangukiwa na bahati , pengine  ninaweza kubadilika zaidi ya hivi”Aliongea  Hamza huku akitabasamu.

“Haha.. hapo kidogo  mrembo Anitha anaweza kukusikiliza , halafu umekuja na usafiri gani , ulipokuwa ukiongea ni kama ulikuwa ukiendesha?” “Nilikuwa nikiendesha ndio ,   kuna mtu niliomba niendeshe gari yake”Aliongea Hamza hakutaka kumuonyesha  Amiri kama alikuja na ile Lexus , maswali yangekuwa mengi .

Hamza mara baada ya kuachana na  Amiri  alifikiria kidogo ,  aliwaza kurudi  nyumbani  lakini wazo hilo  ni kama halikuwa  kipaumbele kwenye halmashauri yake ya kichwa, lakini mara baada ya kukumbuka  alimwahidi Shangazi angekula  akirudi aliona arudi nyumbani tu  moja kwa moja.

****

Upande wa Regina  hakupata hata hamu ya kula mara baada ya   kuongea na simu, baba yake alimpigia akimlaumu kwanini anataka kuunua kampuni ya Omega  inayojihusha na uhandisi wa Programu endeshi za tarakishi.

Baba yake alimwambia sio vizuri   lakini  pia ingemgharimu  hela nyingi kununua kampuni hio kwani hisa zake zimepanda.

“Regina kwanini unafanya maamuzi bila  ya kushirikisha wajomba  zako  na wakurugenzi wa   bodi?”

“Huu ni mpango ambao ulishapitishwa tayari katika kikao  kilichofanyika mwezi uliopita”Aliongea Regina.

“Unadhani  walichopitisha ndio wanachotaka , wamefanya yote kukusikiliza kwasababu wanakuamini  sana  lakini vilevile hawana  uelewa na  maswala ya  komputa ,  Tanzania kwa mara ya kwanza tunaingia katika  biashara ya uhandishi wa Programu endeshi , kwanini unataka kujiingiza katika vitu ambavyo  huna uzoefu navyo , isitoshe  ni mpaka  wakurugenzi wote wa bodi wakubali”Aliongea  Mzee Wilsoni.

“Kwanini hawakujitokeza kwenye kikao na kunipinga waziwazi?”

“Wewe mtoto ,  hawakujitokeza mbele  yako kwasababu wanaheshimu mawazo ya  babu yako , ndio watu waliokuwa wakifanya kazi na babu yako kwa  miaka na miaka , wanachokifanya ni kutotaka kuona unafanya maamuzi ambayo  yapo nje ya sera ya kampuni”

“Baba , ijapokuwa  wewe ni moja ya  mmiliki  mkubwa wa hisa lakini huna nafasi yoyote ya uongozi , hivyo siwezi kuzungumza hili swala na wewe , kama wao ndio  wanataka kuongea basi waache waongee na mimi mwenyewe , sio wewe  kuwa msemaji wao”

“Hakuna shida , bodi ya  wakurugenzi kesho  itakaa kikao  na  unapaswa kutushawishi  kwa  fact , ukishindwa kutushawishi  usije kutulaumu tukipiga  kura ya kutokuwa  na imani na wewe kuendelea kuwa   katika nafasi ya ukurugenzi wa kampuni, na ikitokea hivyo  utapoteza kila kitu”

Wajomba  ambao walikuwa wakizungumziwa  hapo   mmoja wapo alikuwa ni Mzee Willium , huyu alikuwa  makamu  raisi wa kampuni  na mwingine alikuwa ni  Mzee Sebastian  ambae pia alikuwa Mkurugenzi msaidizi., wote hao walishikiria nafasi hizo kutokana na hisa walizokuwa wakimiliki ndani ya kampuni ya Dosam.

Regina hakutaka kuendelea kujibishana na baba yake  na alimwambia kesho ahudhurie kikao cha bodi kama   kweli anataka kupinga mpango wa kununua kampuni  mpya ambayo imeanza kustawi inayojihusiaha na uhandisi wa programu endeshi, pamoja na  akili mnemba.

Ijapokuwa Regina alikuwa ashaweka mizizi yake kama kiongozi wa kampuni  lakini  bado kuna waliokuwa na nguvu ya ushawishi  na haikuwa rahisi ya kuwaondoa.

Wafanyakazi kama Eliza , Prisila na  wengineo ambao wananafasi za  juu na  wanamuamini  Regina katika maamuzi  ukweli ni kwamba ushaiwhi wao unahesabika kama mdogo mno , kwao walikuwa kama wafanyakazi tu.

Hivyo  hata kama  viongozi hao wakae  kikao na kutaka kufanya maamuzi makubwa  yasingepita moja kwa moja , lazima yangepita katika bodi  ya wakurugenzi na kisha  wao ndio wanapiga kura ya kupitisha maamuzi hayo , huo ndio utaratibu  kwasababu kampuni   ya Dosam haikuwa ya Regina peke yake.

Kilichokuwa kikimuuzi  Regina  zaidi ni  pale ambapo baba yake alikuwa akitumiwa na watu wa nje kujaribu kumbadilisha mawazo , haikuwahi kutokea  Mzee Wilsoni kukubaliana na mawazo ya binti yake , siku zote  ni mwenye kumpinga,sio kwamba hakuwa akikubaliana nae bali ni kwasababu alikuwa  akijaribu kumlinda kwa  staili yake , alijua  akimfanya  Regina kupunguza kujiamini  ndio anamlinda.

Sasa wakati  Hamza akiwa SamakiSamaki kama angeingia katika  mgahawa huo  angeweza kumuona James na baba yake wakiwa  pamoja na wazee wawili ambao  wana miaka  makadirio  kama ya miaka hamsini hivi wakiwa wamezungukwa na wahudumu  ambao walikuwa wamevalia kimitego.

“Mzee Willium  kwahio  ni kweli Regina anataka kuinunua Omega?”Aliuliza  baba yake James.

Mzee Willium alikuwa  na nywele  rangi nyeupe  tupu, wakati huo walikuwa ameshikilia  mrembo mmoja mkono huku akijaribu  kuthaminisha  maumbile yake.

“Ni kweli kikao  cha wahisani kilishapita mbona”Aliongea huku akicheka.

“Mzee Willium  nina marafiki zangu kadhaa  na tumefanikiwa kumshawishi Wilsoni , tunapanga kupinga kila ambacho  Regina ataongea kesho”Aliongea Mzee Sebastiani na kauli ile ilimshangaza kidogo  baba James.

“Mzee Wilsoni amekubali?”Aliuliza.

“Wilsoni bado ni mtoto  na hajui mambo mengi , tulichofanya ni kusema maneno machache ya hapa na pale na akatuamini , nadhani mpaka sasa amempigia simu binti yake na kumlalamikia  lakini ninavyojua mimi Regina hawezi kumchukulia siriasi”

“Kesho  katika kikao  lazima Regina atakuja na mbinu za kutaka kuwashawishi  ili kuinunua Omega , muda huo nitahitaji  mnitumie taarifa  hio”Aliongea Baba James.

“Usiwe na wasiwasi  huna hata haja ya kuomba , tumekuwa tukifanya kazi pamoja kwa muda mrefu , hatuwezi kumruhusu Regina kufanikiwa kuinunua”Aliongea Mzee Willium.

“Ni kweli kabisa alichoongea  Willium , tunachosubiri hapa ni James kufunga ndoa na Regina na mpango wetu kuanza , pumbavu kabisa  tunaruhusu vipi  undugu wa  kitajiri tuliojenga kwa miaka kuishia katika mikono ya msichana mdogo kama Regina”

James mara baada ya kusikia kauli ile alitoa cheko  na kisha aliinua chupa  ya wine  akiwa amesimama. “Asanteni sana wazee wangu ,  ili kuonyesha ni namna gani ninashukuru nitawamiminia kinywaji,

Baadae kama  nikifanikiwa katika mpango wangu  Dosam tutaiunganisha na kampuni yetu , nawahakikishia  sitowaangusha , mtapata hisa za kutosha  katika kampuni yetu”Aliongea James na mabwana wale  matabasamu yalikuwa nje nje.

“Usiongee sana unamaliza mate tu bwana mdogo , tunajua  ukubwa wa familia yenu  , hatuwezi kuishi kwa kujibana bana chini ya utawala wa  yule  msichana mkatili”Waliongea huku wakicheka na  kwa pamoja waliinua  glasi zao na kugongesheana.

Baba yake na James alimwangalia mrembo  aliekuwa nyuma yake na kisha alimpa ishara, mwanamke yule   alielewa somo na  kimapozi kabisa alizungusha mkono katika shingo ya mzee Willium huku akilegeza jicho.

“Pedeshee Willium muda umeenda  na naogopa mwenzio  , unaonaje ukinipa lift kwenda nyumbani”Aliongea huku akiwa  amerembua , alikuwa mweupe  na mapaja  yake makubwa yalivutia   kwa mwanaume yoyote rijali.

“Hakuna tatizo mrembo , wewe niambie unaishi wapi , halafu kama ni mbali kwanini hukuongea  mapema ,  pengine tungeanza safari mapema”Aliongea huku akimkonyeza.

“Aiyaa, Mzee Willium unajua  hadi unaboa … mimi sitaki bwana….”Aliongea yule  mwanamke lakini wakati huo akihakikisha manyonyo yake kumsugua  vilivyo  Mzee Willium.

Upande wa Mzee Sebastian hakutaka kulembesha  na alikuwa  akichimba mgodi  hapohapo mezani  kwa   mrembo mwenye  umbo matata  rangi ya kunde, wote walionekana vilevi vimewakolea.

James na baba yake  waliangaliana na wote kwa pamoja   walitoa tabasamu lenye uovu ndani yake.

****

Siku iliofuata Hamza alienda  kazini  kama kawaida  na alihakiksiha tarakishi yake haifuatiliwi ili afanye  mambo yake.

Hamza alijua alikuwa na kazi kubwa hivyo  alihakikisha kwanza kiporo cha jana anakimaliza  ili  awe na muda wa kutosha wa kufanya mambo yake bila wasiwasi ikiwemo swala la kufatilia  ile lugha aliokuwa akiongea Mellisa.

Mpaka inafika mchana alikuwa ashamaliza kazi yote  na alijisifia  kwa kuwa na uwezo mkubwa wa akili wa kufanya vitu haraka haraka.

Baada ya kuona njaa inauma  moja kwa moja alitoka na kuelekea mpaka chini  kwenye mgahawa.

Kitendo cha kuingia katika mgahawa huo wa kampuni macho yalikuwa yakimwangalia , ukweli ni kwamba tukio la jana ni kama limempa umaarufu  na kufanya watu wengi wamfatilie na walifahamu alikuwa msaidizi wa bosi.

Ukiachana na alichokifanya  jana  siku hio wafanyakazi wa kike ikiwemo Asha na Mirium hamu yao ilikuwa ni kuona   namna   Yonesi na  Hamza wataendeleza pale walipoishia jana, hawakuwa na uelewa kilichotokea  jana  kwa Yonesi kupigana na Hamza.

Wafanyakazi wengi walikuwa wakiamini lazima  Yonesi na  Hamza wataishia kuwa wapenzi na hicho ndio ambacho walikuwa wakitamani kuona, waliamini  Yonesi hakuwa akinyanduliwa na  ikitokea pengine  ukauzu wake utapungua  na kufanya maisha yawe marahisi  hivyo kete zao ilikuwa ni Hamza.

Hamza marra baada ya kuchukua chakula chake hakuhaingika kutafuta sehemu ya kukaa kama jana , aliangalia tu kushoto  na alimuona Yonesi akiwa peke yake na alipiga hatua na kwenda kukaa pembeni yake.

“Habari za mchana Kapteni?”Aliongea Hamza

Previoua Next