SEHEMU YA 24.
Swali lile ilikuwa ni kama Trigger ya bunduki , Hamza alibadilika palepale , zile nywele zake za kizungu zilisimama na kuanza kuchemka kama singa singa huku sura yake ikitisha.
Ilikuwa ni kufumba na kufumbua Miwani ya Frida ilishadondoka chini huku yeye mwenyewe akielea hewani akiwa amezingirwa na kitu kama kizimba cha Dimension’tatu chenye kufika mwanga flani mweupe na kufifia kwa wakati mmoja.
Hamza hakuwa na huruma hata kidogo , muda huo alionekana sio Hamza tena , ni kama shetani.
“Wewe ni nani?”Sauti hio ndio iliomtoka Hamza huku Frida akiendelea kufurukuta.
“Naitwa… naitwa Frida Franklin Genesha , Agent Two F”Aliongea na mara baada ya kuongea vile usinga wa nywele za Hamza ulirudi katika hali yake ya kawaida na Frida alidondokea katika sofa.
Hamza alisogea mpaka katika Sofa la mbele na kukaa chini huku akikunja nne na tabasamu la uovu usoni .
“Haina haja ya kuendelea kuwa katika muonekano feki , unaonaje ukiondoa hio Mask ya kichawi tuone sura yako halisi”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu na kauli ile ilimfanya Frida aliekuwa akihema kama mbwa aliekimbia maili nyingi kutoa mshangao.
“Ulinifahamu tokea siku ya kwanza!!?”Aliuliza akiwa katika hali ya mshangao na Hamza aliishia kutoa tabasamu.
“Nilipokuja hapa siku ya kwanza sikukufahamu moja kwa moja , lakini kuna kitu kilinifanya nikushuku mara moja”Aliongea Hamza na kumfanya Frida kuongeza umakini.
“Inawezekana ikawa kawaida katika jamii , lakini ni mara chache sana kushuhudia mwanamke anaogelea akiwa na pete ya thamani kubwa kidoleni’Aliongea na palepale alinyooshea mkono wa Frida aliovaa pete.
Frida mara baada ya kusikia kauli ile sasa alielewa , ni kweli tokea avae hio pete hakujua ni lini aliivua na anasababu za kufanya hivyo.
“In the Knows kati ya mwanachama na mwanachama wa Wiccan katika kutambuana mara nyingi huhusisha alama ya vito , japo zipo njia nyingi,mimi nilikufahamu na nilijua kuna uwezekano na wewe umenifahamu , nimekuja leo hii nikitarajia swali lako”Aliongea Hamza.
“Haiwezekani , ni kweli pete yangu ipo katika orodha ya In the Knows lakini hii pete aina ya Pentacle iliotumika ni siri ya dunia, alama yake inaingia katika orodha ya The lost symbols , mpaka
kuifahamu inamaanisha na wewe ni mwanachama, tena katika digrii ya juu”
“Mimi sio mwanachama wa Wiccan”Aliongea Hamza kivivu huku akitoa tabasamu la kizembe.
“Kama wewe sio mwanachama wa Wiccan ni nani , wewe ni Muislamu , Mkristo au Mbuddha?”
“Unaniuliza swali la namna hio inanifanya nishangae , umejitambulisha kwangu kama Agent Two F , hii ni neno la kodi ambalo Dokta Genesha alinitajia , ulivyotaja jina hilo nikakuacha mara moja , nadhani unalifahamu hivyo , kama ndio haina haja ya kuniuliza mimi nipo upande upi wa kiimani katika ulimwengu huu , hayo ni maswali ambayo wewe unatakiwa kunijibu , Vinginevyo nitaamini hujatoka katika kivuli cha Dokta Genesha , ushajua siri yangu napaswa kukuua kama huna majibu”Aliongea na Frida alionekana kufikiria kidogo.
“Nimechukua tahadhari tokea unakaribia kufika hapa , lakini tahadhari haitoshi , umenifahamu kama mfuasi wa Wiccan na siwezi kukupa majibu nikiwa katika vifungo vya kiroho vya Wiccan”.
“Njia gani unaweza kujifungua katika vifungo na kujibu maswali yangu yote , nakupa heshima hii kwasababu ya Dokta Genesha hivyo unapaswa kuwa mkweli”Aliongea Hamza.
“Njia pekee ni kuuvua muonekano wangu katika chumba cha nuru , ndio jia pekee ambayo watu wa madhabahu hawatogundua , nikiwa katika uhalisia wangu nitaweza kujibu maswali yako yote”Aliongea na kumfanya Hamza kushangaa.
“Kwahio wewe ni Double Agent , unafanya kazi chini ya Sinagogi na Wiccan kwa wakati mmoja?”
“Wote tuliopo chini ya kivuli cha Genesha kiasili ni wanasinagogi , sidhani hili ni swala la kukushangaza , kabla sijaingia katika chumba cha nuru unapaswa kujibu swali langu kwa maelekezo ya Dokta Genesha?”
“Uliza swali lako?, maana ikija wakati wa maswali yangu unapaswa kujibu yote”
“Ushawahi kuota ndoto kama uhalisia , upo katika mazingira ambayo ni tofauti na ulimwengu wa kawaida?”Aliuliza Frida huku wakiwa na muonekano wa siriasi.
“Umejuaje nimeota ndoto ya namna hio?”Aliuliza Hamza akiwa ameshangaa , ilikuwa ni kweli kabisa aliota ndoto yupo katika mazingira ambayo sio ya kawaida.
Hamza ni kama sasa anaanza kuamini uwezo wa Frida , ukweli ni kwamba wakati anarudi Tanzania alikuwa akisubiria mtu ambae anaweza kumwambia yeye ni nani , sio kama hakuwa akijua yeye ni nani la hasa , alikuwa akijua yeye ni Hamza na historia yake kwa ufupi , lakini kuna swali kubwa ambalo linahusiana na nguvu iliopo ndani ya mwili wake.
Kwa maelekezo ya Dokta Genesha ambae alikuwa mwalimu wake , alimwambia amtafute Agent Two F na ndio maana mara baada yya Frida kutaja jina lake kamili alimuacha mara moja.
Frida alimwangalia Hamza , licha ya kuonekana kuridhika lakini alionekana akifikiria pia.
“Ulichoota sio ndoto , uhalisia wako ndio unakuita, ndio njia pekee ya kumfahamu mtu aliekuwa nyuma yako mpaka kufikia leo hii”
“Unamaanisha Mzee?”
“Hio si ndio misheni yako kwa sasa ya kumfahamu Mzee , huwezi kumfahamu kabla ya kuujua uhalisia wako , mimi sio mtu wa kujibu maswali yako, ni wa kukuongoza tu kisayansi kupitia taaluma yangu, kufupisha tu majibu yapo ndani ya nafsi ambayo imelala ndani yako”
“Nafsi unataka kumaanisha kuna nafsi zaidi ya niliokuwa nayo?”Aliongea Hamza akiwa katika mshangao na Frida tofauti na kujibu alishika ile tarakishi na kuchezesha vidole kwa dakika kadhaa na kumpatia Hamza.
“Hizi ni takwimu za wagonjwa wa akili kwa upande wa Afrika tu katika kipindi cha mwaka 2020 mpaka mwaka huu , ni idadi mara kumi zaidi ya miaka yote ya nyuma”Aliongea na Hamza alisoma takwimu ile , ilikuwa ni kweli kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa akili.
“Umegundua nini?”
“Wengi ya hawa wagonjwa naona wanafanana dalili na Diagnosis, Ugonjwa wa akili wa DID ndio umeshika kasi , Zamani ugonjwa huu wa akili ulikuwa adimu sana”
“Ndio ulikuwa adimu , hivyo inamaanisha kuongezeka kwa wagonjwa wa aina hii kuna sababu, hii ni takwimu za wale tu ambao wameripoti hospitalini , lakini wapo wengi hawajui wanaugua huu ugonjwa, japo wanaonekana kuwa wa kawaida kwa nje lakini kwa ndani kuna kitu kikubwa kinachoendelea”Hamza mara baada ya kusikia maelezo hayo alijikua akimfikiria Mellisa mpenzi wake na Amiri , alijiuliza au Mellisa alikuwa pia mhanga wa ugonjwa huo , alifikiria lakini aliona haiwezekani iwe hivyo.
“Umeongea sana , nataka kujua kinachofuata ni nini , umesea majibu ninayo mwenyewe lakini sina ninachoelewa, halafu kwanini hutaki kuwa katika uhalisia wako , hio mask unavua saa ngapi?”
“Kitendo cha kuvua hii Mask moja kwa moja najitoa katika mtandao wa Wiccan ,siwezi kufanya hivyo hapa na pia siwezi kukuingiza katika uhalisia wako nikiwa katika mtandao wa Wiccan , lazima niingie katika Chumba cha nuru kwanza”
“Chumba cha Nuru, ndio kwamba huwezi kushitukiwa unachofanya?”
“Ukishaingia katika chumba cha nuru ni kama unapotea katika mazingira ya kawaida , kwa maana mtandao wa kimadhabahu wa Wiccan hauwezi kujua eneo ulipo na unachofanya ni nini?”Hamza alionekana kumwelewa hata hivyo alikuwa na uzoefu wa aina hio.
“Tanzania kuna chumba cha Nuru?”
Hamza alikuwa akijua kuhusu chumba cha Nuru ,
Dokta Genesha alikuwa ndio mgunduzi mkuu wa
Nuru ndio ilikuwa uthibitisho wa kisayansi aliokuwa nao wakati akitangazia ulimwengu kwamba ulimwengu wa kiroho ni uhalisia na anaweza kuthibitisha hilo, lakini ukweli ni kwamba alichogundua Dokta Genesha kilikuwepo na kikafanywa siri kama ililivyokuwa siri kwa dunia na kwanzia hapo Dokta Genesha hakuwahi kuweka wazi ni ushahidi gani aliokuwa nao mpaka kuaminisha watu kwamba ulimwengu wa kiroho ni uhalisia.
“Swali hilo napaswa nikuulize wewe , kwa maelezo niliokuwa nayo wewe ndio mtu pekee unaejua wapi kilipo chumba cha Nuru”Aliongea na kauli ile ilimsahngaza Hamza.
“Unamaanisha nini mimi ndio ninajua , kama ninajua ningeuliza?”Aliongea Hamza akiona kabisa ni kama Frida anamchezea akili.
“Mpaka sasa Wiccan udhaifu wao mkubwa ni elementi zilizounda nguvu ya Nuru , licha ya ukweli kwamba Nuru ndio ugunduzi uliokuwepo tokea zama za kale lakini hakuna mwanachama yoyote ambae alishawahi kushuhudia kwa macho ushahidi huo , imebakia kuwa katika makisio ndani ya Wiccan , lakini haibadilishi ukweli kwamba kitu hicho hakipo na wanaamini ni nguvu ambayo ni mali yao?” “Wiccan ni wachawi kama wachawi wengine tu , kwanini wanahangaika na Nuru , kitu ambacho kina madhara kwao?”
“Hawahaingiki na Nuru , Wanaamini nguvu hio imetokana na alementi zote nne za dunia yaani , Roho , hewa , maji , moto na Ardhi,mfano mwepesi alitoa mwanachama wa juu kabisa wa Wiccan Ann Marie Galagher , ili mmea ustawi unahitaji ardhi , maji au unyevunyevu , moto au jua na hewa ambayo ni oksijeni kutoka Carbondioxide sasa katika hivi vitatu vinawezekana kufanya kazi pamoja kwa kuunganishwa na roho , sasa unaona hapo hawahangaiki na Nuru kwani tayari Nuru ipo katika elementi hizo tano”
“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Nuru inayozungumziwa hapa sio nuru kama nuru inayoonekana bali ni kitu tofauti kabisa?”
“Ndio lakini wanaamini msingi wake ni ndani ya elementi zote za dunia na hakuna sababu ya nje ya nuru , siri hii wamekuwa wakiiwinda kwa muda mrefu sana na wote wenye majibu walishakufa , ambae alikuwa na siri hii ni Dokta Genesha na ndie ambae ametengeneza chumba cha Nuru ambapo mpaka
sasa haieleweki kipo sehemu gani lakini ndio udhaifu mkubwa wa nguvu ya Wiccan”
“Sasa kwanini mimi niwe ndio ambae najua chumba hiko , hapa mnanichanganya sijui chochote”
“Kitendo cha kuota tayari ndoto hio inamaana unaukaribia ukweli , kazi ambayo inatakiwa kukufanya kwasasa ni kuendelea pale ulipoishia?”
“Unamaanisha nilipoishia kuota ama , inawezekana vipi kumfanya mtu kuendelea kuota kama unaangalia filamu”
“Ni kitu ambacho hakikuwa kikiwezekana lakini teknolojia imekuwa, katika ulimwengu wa kiroho
you’re more than yourself, wewe ni zaidi ya wewe mwenyewe”Aliongea na kumfanya Hamza asimame.
“Kabla sijaondoka nataka kwanza kujua vyungu hivyo kazi yake ni nini , kwanini gharama yake ni kubwa , tuanzie kwanza hapo na ndio tuendelee”
“Tunachonunua sio chungu , chnngu ni njia ya usafirishaji tu , kinachonunuliwa ni viungo vya akili iliolala, unaweza kusema ni kama dawa inayomsaidia mtu kuota nje ya uzoefu wa kumbukumbu za maisha yake”
“Unamaanisha kuna vitu vipo katika chungu hiko?”
“Hilo ndio jibu , kinachofanyika unapewa kifaa maalumu ambacho kinapasha joto chungu hicho na hapo hutoa marashi ya aina flani yanayokufanya mwili wako kuwa kama umekufa huku akili yako
ikifanya kazi katika mazingira ya nje ya kumbukumbu zako, sijui ni siri gani ilopo juu ya marashi hayo lakini nilikuwa nikifanya utafiti mwaka wa tatu huu sijaweza kuona chochote tofauti kisayansi nje ya udongo wa kawaida uliotengenezea”
“Kwahio wewe unachukua hivi vyungu sio kwasababu unataka kutumia kama viungo vya akili , bali ni kwasababu ya kufanyia utafiti?”
“Upo sahihi , kuna siri kubwa ndani yake ,ambao ndio na itafuta , wenye kujua siri hii ni Binamu pekee na ndio wenye mtandao wa usambazaji dunia nzima , kwasasa imekuwa mbadala wa madawa ya kulevya, inaweza kuwa chanzo pia cha ongezeko kubwa la ugonjwa wa akili”.
Hamza alijikuta akiangalia saa na muda ulikuwa umeenda kweli , ilikuwa ni saa moja kamili tayari za usiku.
Alitamani kujua vitu vingi kutoka kwa Frida lakini simu yake ndio iliomshitua , alipoangalia aliekuwa akipiga ni Shangazi na alipokea haraka na baada ya kumsalimia swali lilofuatia ndio lilimshangaza Hamza.
“Hamza kuna sehemu mmepitia , mtakula huko huko au niwahesabu kwenye chakua cha usiku?”Swali lile lilimshangaza Hamza.
“Shangazi kwanini unauliza hivyo?”
“Nimeona hamjarudi wote ndio maana nauliza”
“Shangazi unamaanisha Regina hajarudi bado?”
“Ndio , kwani hampo pamoja , nimeshindwa kumpata hewani ndio maana nimekupigia wewe , nini kinaendelea?”Shangazi alionekana kuwa na wasiwasi na Hamza alisimama palepale.
“Basi sawa shangazi , usiwe na wasiwasi ngoja nimtafute nitakupa jibu muda si mrefu”Hamza kengele ya hatari ilishagonga katika akili yake na kwa haraka sana alipiga simu ya Regina na iliita ndani ya sekunde chache tu na kupokelewa.
“Regina upo wapi , Shangazi anasema hakupati hewani”Sauti iliomjibu Hamza ilimfanya uso wake kujikunja palepale.
“Mr Hamza it seems like this beautiful lady real does have a special relationship with you…”
Hamza mara moja alishaijua sauti hio kutokana na lafudhi yake , alikuwa ni Mendoza jamaa mwenye Marasta aliekutana nae siku kadhaa nyuma.
“Hivi unajua unachokifanya kwanza?”Aliuliza Hamza huku akihisi miguu yake kuwa na ubaridi
Upande mwingine licha ya kwamba walikuwa mbali na Hamza lakini walikuwa na hofu kubwa mno , kama sio kwa matamanio yao juu ya kitabu walichokuwa wakifatilia wasingeenda mbali kumshika simba masharubu
“Mr Hamza tunajua kabisa tunachokifanya kitakukasirisha , lakini kuna ule msemo wa ni kheri kufa ukiwa unajaribu kuliko kutojaribu kabisa.
“Ongea unachotaka kutoka kwangu ni nini?”Aliongea Hamza.
Comments