SEHEMU YA 25.
“Ni rahisi sana kitabu au tuambie wapi alipo Tembo wa Trishaza na ndio tutamuachia huyu mwanamke haraka iwezekanavyo”Aliongea Mendoza
“Mabadilishano yatafanyikia wapi?”Aliuliza Hamza , hakutaka kupoteza muda.
“Kama tulivyotarajia , kumbe kitabu unacho?”Aliongea na muda ulule alimtajia eneo ambalo anapaswa kwenda.
“Mr Hamza tunakupatia masaa matatu kamili , ukipitisha hayo masaa usije kutulaumu huyu mwanamke akipotea na sisi”Aliongea na Hamza hakutaka kuendelea kusikiliza porojo zao kwani alikata simu.
“Kuna nini?”Aliuliza Frida.
“Nadhani nitakutafuta siku nyingine”Aliongea Hamza na mara moja alimuacha Frida akimwagalia kwa wasiwasi.
Hamza mara baada ya kutoka nje kabisa alimpigia Shangazi simu na kumwambia ashampata Regina na watarudi muda si mrefu ila asiwahesabu kwenye chakula cha usiku , alifanya hivyo kwa ajili ya kumtoa wasiwasi.
Sehemu ambayo Mendoza aliokuwa amemtajia
ilikuwa ni Zinga ya Bagamoyo kijiji cha wavuvi.
Eneo hilo lilikuwa tulivu mno, pengine ni kwasababu wavuvi walikuwa washaondoka kuelekea baharini kuvua.
Nje kabisa ya moja ya Ghala la kampuni ya uvuvi Gari ya Regina ile Lexus ilikuwa imeegeshwa karibu kabisa na sehemu nyavu za kuvulia zinapohifadhiwa.
Ndani ya Ghala hilo kulikuwa na harufu nzito mno ya samaki , Regina alikuwa amefungwa kwenye kiti na hakuwa na uwezo wa kusogea hata kidogo, nywele zake zilikuwa zimechanguka pia kutokana na kibanio kumtoka na vile alivyokuwa akitingisha kichwa ndio alivyozidi kuchanguka.
Hakuwa akipiga kelele hata kidogo zaidi ya kuangalia wanaume wawili waliokuwa mbele yake na muonekano uliojaa sumu.
Regina alikuwa akikumbuka wakati alipokuwa akikaribia nyumbani ni mwanamke wa kizungu ambae alionekana kama mgeni ndio aliesimamisha gari yake akionekana kutaka kuuliza swali.
Matokeo yake kitendo cha kushusha kioo tu alijikuta akinusa marashi ambayo yalimpelekea kupoteza fahamu na mara baada ya kushituka alikuwa tayari ndani ya eneo lenye harufu kali katika ghala hilo akiwa amefungwa , mwanzoni alidhani yupo feri lakini mara baada ya kuangalia taa hafifu ndani ya ghala hilo na maboksi ya kutunza baridi alijikuta akiaini hakuwa karibu na jiji la Dar.
Akili yake ilimwambia kabisa watu wale hawakuwa watanzania hata kidogo na hio ni kutokana na namna walivyokuwa wakiongea.
“What is your goal , if you want money , then you should ask me to call home”Aliongea Regina kwa kingereza akimaanisha nini lengo lao, kama ni hela basi wamuache apige simu nyumbani.
“Madam , My Companion Huda is only joking , she has no ill intentions , we just want to know what kind of relationship you have with that Mr Hamza , who is he and where he’s from”Aliongea akimaanisha yeye na mwenzake Huda wanatania tu , na hawana nia mbaya , wanachotaka kujua ni uhusiano wake na Hamza , ni nani na anatokea wapi.
“Mr Hamza.. Mnamaanisha Hamza!!”Aliongea
Regina akionekana kushangaa na palepale alijiuliza au hili kundi la watu lililomteka hawakuwa wakimlenga yeye bali ni Hamza.
Kitu kingine ni kwamba walikuwa wakiuliza kuhusu uhusiano wake na Hamza , sasa alijiuliza kwanini waulize swali hilo.
Regina alishindwa kujizuia kimawazo na kuamini pengine ni James ndio ametuma watekaji kwa ajili ya kuupata ukweli juu ya uhusiano wake na Hamza , lakini alijiuliza kwanini raia wa kigeni.?.
“Ni Boyfriend wangu , pia ni mwanachuo na fundi wa vifaa vya kieletroniksi”Aliongea Regina kwa kingereza.
“Boyfriend!!, Ndio maana anakujali mno mpaka kuwa tayari kutupatia Ankh, inaonekana anakupenda sana”
“Anka!! Unamaanisha nini?”Aliuliza Regina mara baada ya kusikia sauti hio lakini hakuelewa maneno hayo yalikuwa yakimaanisha nini.
Upande mwingine kati ya wanawake wawili waliokuwa katika kundi hilo , yule aliefahamika kwa jina la Corrella uso wake ulionyesha kutoridhika.
“Umesema ni fundi na mwanafunzi , mtu ambae ameweza kujua uwepo wetu hawezi kuwa mwanafunzi na fundi , acha kututania wewe mwanamke”Aliongea na dakika ileile alitoa kisu cha kung’aa sana na kumsogelea Regina na kukiweka karibu na uso wake , ilikuwa ni kama vile anataka kukata pua ya Regina.
Regina macho yake yalianza kuonyesha kupaniki , ijapokuwa siku zote hakujali sana kuupamba uso wake lakini yeye ni mwanamke na siku zote alikuwa akijivunia kuwa mzuri , ni mwanamke hata hivyo , aliona kama akipotezewa urembo wake itakuwa ni kheri ya kifo.
“Nilichosema ni kweli , kama huamini muulizeni mwenyewe”Aliongea na Mendoza alimsogelea Huda na kumzuia kwa kumshika mkono.
“Huda muache , pengine Hamza siku hizi kaamua kuwa mwanafunzi na fundi , ni jambo la kawaida kwa ninja kama yeye kuwa na utambulisho feki”
Regina mara baada ya kusikia utambulisho feki ,Ninja Regina mara baada ya kusikia maneno hayo ni sasa ni kama akili yake inafanya kazi na kuona ni kweli Hamza alionekana sio wa kawaida.
“Madam , ushawahi kusikia kitabu chochote chenye alama ya Ankh kutoka kwa Mr Hamza , au Kitabu cha Riwaya ya ndege juu ya mti wa uzima?”
“Mnasema sijui anka gani , ni kitabu cha namna gani hicho?”
“Inaonekana kweli huelewi tunachozungumzia , ni kitu muhimu hivyo uwezekano ni mkubwa hawezi kukiweka holelaholela mtu yoyote kuona , Sio rahisi kumuonyesha mpenzi wake”
Yule mwanamke aliefahamika kwa jina la Huda alichora chini alama flani hivi ,haikuwa kama msalaba bali ilikaa kama rungu yenye mkato katikati. “Hujawahi kuona kitabu chenye alama ya namna hii?”Aliuliza yule mwanamke na Regina aliishia kutingisha kichwa kwamba hajawahi kuona , ukweli ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuona alama hio.
“Hajui chochote , inaonekana Mr Hamza alikuwa makini kuficha”Aliongea Correla.
Regina aliishia kusikiliza mazungumzo yao na yalionekana sio kati yake na Hamza kabisa na alianza kuwa na wasiwasi zaidi.
“Sio James aliewatuma?”Aliuliza Regina , ijapokuwa aliona kabisa swali hilo ni la kijinga lakini aliona aulize.
“James , ni nani huyo na anakaa wapi?, sisi ni wawindaji wa binadamu kutoka Samar , unaweza
kutuita Tumbili Wenye mbawa za Mwewe”Aliongea kwa majisifu.
Regina japo hakuelewa walichokuwa wakimaanisha lakini alishaamini sio watu waliotumwa na James , maana ndio adui yake ambae alidhani anaweza kumteka.
“Nadhani tukamfunge ndani ya boti yetu moja kwa moja , tusipopata kitabu tunaondoka nae , ndio namna pekee ambayo hatutaweza kupambana nae ana kwa ana”Aliongea bwana mwingine , huyu hakuwepo katika kundi ambalo lilimsimamisha Hamza kule Kongowe.
“Noni, ulichoongea kinaleta maana , nitaliacha hili mikononi mwako”Aliongea Mendoza
Regina mara baada ya kuona kile kinachoenda kutokea alizidi kuwa na wasiwasi na alijiuliza au alikuwa akishikiliwa kwa kudhaniwa ni mpenzi kweli wa Hamza.
Aliona woga kwani mmoja wapo alikuwa kabisa na bastora kiunoni na moja kwa moja akili yake ilijua watu waliokuwa mbele yake wanazidi kuwa hatari kila alivyokuwa akiwafikiria na kuwachunguzana, hisia zake zilimwambia kama ni hivyo basi na Hamza atakuwa hatarini.
Alikumbuka namna ambavyo Hamza alivyokuwa akimkwepa Yonesi wakati wakipigana na kutofanya mashambulizi , aliona kabisa kitendo kile ilikuwa ni Hamza kuwa muoga.
“Subirini kwanza,mmekosea jambo moja , kunikamata kwenu hakutowapatia hicho kitabu”Aliongea Regina.
“Oh , kwanini unasema hivyo?”Aliuliza aliekuwa mlangoni.
“Mimi nimefahamiana na Hamza juzi tu hapa ni mtu muoga mno , nina uhakika anawaogopa mno na hawezi kuhatarisha maisha yake kuja kuniokoa , huu mpango wenu ushafeli tayari”
Mara baada ya kumsikia akiongea hivyo watekaji wote waliangua kicheko kana kwamba alichoongea ni ujinga wa karne.
“Unadhani tunaweza kukuamini?, Yaani Hamza atuogope sisi haha…hiki ni kichekesho cha mwaka”
“Kwanini asiwaogope? , nyie hamumjui yule vizuri , ni muoga kweli”Aliongea Regina huku akiona yeye mwenyewe maneno yake ni ya ajabu.
“Wewe mwanamke unadhani sisi ni wajinga , tulishampigia tayari wakati ukiwa hujitambui na ametuambia anakuja , nadhani muda si mrefu atafika hapa , anaonekana kujali kweli usalama wako” “Nini!?Anakuja? , kwa uoga ule inawezekana vipi?”
Regina alionyesha kushangaa na kudhani alikuwa amemdhania Hamza vibaya lakini mara baada ya kufikiria anakuja kukutana na hawa wahalifu alianza kushikwa na wasiwasi na aliona kama Hamza ana akili ni bora asije kabisa , Hamza anaemjua yeye ni mtu ambae anaogopa mshahara wake kukatwa na amekaa kizembe zembe.
Hamza hakuwa hata mwanaume kwa kitendo chake cha kushindwa kujizuia na kumchungulia kupitia kioo , alijiambia hio sio tabia ambayo mwanaume jasiri anaweza kufanya, sasa mtu yule aliempiga chabo ndio aje kumuokoa , aliona haiwezekani lakini hata hivyo aliona atulie aone mwisho wake.
Alijikuta akifikiria na upande wa pili wa Hamza na aliona kuna muda mwingine anaonekana kuwa siriasi hivi na kuwa na akili nyingi lakini pia ni mkarimu mpaka kumletea matunda kwa ajili ya kupoza njaa , Regina hakukataa na kuona inawezekana roho yake nzuri ikamtuma kuja kumuokoa.
Wakati Regina akijiuliza maswali mengi Hamza ni nani mpaka kuwa na ujaisri wa kuja kumuokoa dio muda mlango wa ghala hilo uligongwa.
“Noni mlete huyo mwanamke kuelekea kwenye boti , nitadili nae mimi”Aliongea Mendoza mara baada ya kuona Hamza amefika.
“Hey , usiniguse”Aliongea Regina mara baada ya kuona yule mwanaume bonge wa kifilipino aliefahamika kwa jina la Noni akitaka kumgusa.
“Stupid Woman , try this”
Aliongea Corrella aliekuwa amesimama mbele ya Regina na alitoa kichupa kama cha spray na kumpulizia usoni na palepale mara baada ya kuvuta yale marashi alipoteza fahamu palepale.
Dakika hio hio kabla hata hawajamfungua kutoka kwenye kiti mlango wa mbele wa ghala ulipigwa teke na kufunguka mara moja licha ya loki zake kuwa za chuma, pengine ni kutokana na kutu ndio maana imekuwa rahisi.
Baada ya mlango kufunguka , mtu alieonekana mlangoni alikuwa ni Hamza akitafuna bublish huku mguu mmoja ukiwa hewani , akionyesha kwamba mlango huo aliupiga na teke moja tu mpaka kufunguka.
Mendoza , Huda na Noni wote walikuwa kwenye mshituko kutokana na nguvu za Hamza, kwani teke moja tu mlango ulikuwa umefunguka.
Hamza hakuwa na wasiwasi kabisa ni kama amekuja kutalii , alikuwa akitafuna bablish huku akipiga hatua za taratibu kuingia ndani kama bosi wa watekaji hao.
Lakini kadri ambavyo alikuwa akipiga hatua walijihisi miili yao kuwasisimka , ilikuwa ni kama vile ghala lote limefunikwa na nguvu isio kuwa ya kawaida, dakika ileile Vivuli vitano viliweza kuonekana katika kila upande wa ghala hilo na ilikuwa ni kama vile vivuli viilikuwa vikiwaangalia wale watekaji jambo ambalo liliwashangaza.
Walianza kushikwa na hofu na waliweza kuona ni namna gani Hamza alikuwa akitisha kama vile ni jini.
“Nadhani niliiwaambia hampaswi kuwepo Tanzania na kunifuatilia , ila naona hamkunielewa”Aliongea na palepale alimsogelea Correla ambae alikuwa karibu na Regina akiwa ameshikilia kisu.
“Usisogee kama hutaki huyu mwanamke kufa mbele yako”Aliongea kwa kuamrisha.
Hamza alionekana ni kama vile hajamsikia na aliendelea kusogea mbele,muonekano wake haukubadilika hata kidogo, alikuwa akitembea kana kwamba anapita kwenye kiambaza cha nyumba.
Lakini sasa kadri dakika zilivyokuwa zikiongezeka hali ilizidi kuwa ya baridi ndani ya eneo hilo huku Hamza akizidi kutisha na nywele zake zilianza kucheza cheza
Nori kuona vile palepale alichomoa bastora kutoka kiunoni na kumnyooshea.
“Simama hapo hapo, ukisogea tu nitakulipua”Aliongea
“Lipua tu, ila unatakiwa kwanza kuitoa katika safety deposit”Aliongea na palepale ndio aligundua hakuwa amepandisha risasi kwenye chemba kutokana na kuwa na woga., kosa la namna hilo kwa uzeofu wake halijawahi kumtokea.
Ijapokuwa kwa haraka sana aliitoa katika hali ya usalama lakini mikono yake ilianza kutetemeka. “Mr Hamza tunachotaka ni kitabu cha Ankh, ukitupatia tunakuhakikisha huyu mwanamke atakuwa salama”Aliongea Marasta.
“Si nilishawaambia sina kitabu cha Ankh tokea muda mrefu tu”
“Nini?”
Wote waliangaliana kwa mshangao kana kwamba walikuwa hawajamsikia vizuri.
“Kama ni hivyo , tuambie alipo Dokta Genesha”
Hamza wala hakujali , ki ufupi hakuongea lolotte tena na sasa alikuwa mita kama kumi kutoka kwa watekaji watatu , mara baada ya kusikia lile swali aliishia kutingisha kichwa chake.
“Mr Hamza usitukuchukulie wepesi , au unadhani hatuwezi kumdhuru huyu mwanamke?”Mara baada ya kuongea Huda kisu chake kilikuwa kishafikia shingo ya Regina huku Nori akiwa amemlenga Hamza na bunduki.
Hamza alisimama akiwa katika umbali wa mita kama sita hivi na kuwaangalia wote wanne bila ya kupepesa macho
“Kwasababu mmeweza kuteka basi naamini mnaweza kuua pia”
“Kama unalijua hivyo unapaswa kutoa
ushirikiano”Aliongea Huda na kufanya midomo ya Hamza kucheza.
“Mmethuburu kufanya utekaji lakini haimaanishi mnaweza kuua mbele yangu”
Mara baada ya kusikia kauli hio walijikuta wakiwa katika hali ya kuchanganyikiwa lakini ndani ya sekunde iliofuata nguvu kubwa ya ajabu ilitokea na kuwababishia wahisi kama vile pumzi zinawaishia huku wakati mmoja ni kama vile wameshikwa na jinamizi na washindwe hataakupiga hatua , Hamza muda huo alikuwa ashawasogelea tayari.
Wakati sasa wakijua Hamza hakuja kutii maagizo yao bali kupigana , waliishia kujitahidi kurudi nyuma , na ghafla tu Nori alivuta Triga na kumlenga Hamza na bunduki.
“Bang , Bang, Bang!!”
Risasi zilifyatuka huku zikibeba joto kali lakini ajabu risasi zile ni kama vile zimetoboa karatasi na kupita,
Hamza alikuwa ni kama vile amefifia katika ile
sehemu aiokuwa amesimama na ni mwanga flani wa sura yake tu ndio uliokuwa ukicheza cheza, ilikuwa ajabu kweli.
Huda mara baada ya kuona hakukuwa na madhara juu ya risasi zile kwenda kwa Hamza aliamua kudili na Regina lakini alikuwa amechelewa kwani mkono wake ulioshikilia kisu ulikuwa umeshikwa na kivuli na ushindwe kuusogeza kabisa, hakujua hata ni kitu gani kimemshika na wakati akijaribu kufurukuta Hamza alikuwa ashamsogelea tayari.
Wawindaji wale wote walijikuta wakishangazwa na tukio hilo na walimwangalia Hamza kwa woga mno.
Walijiuliza nini kimetokea , mbona alikuwa mbali mno na alipo Huda lakini ameshindwa hata kumchinja yule mwanamke , ni nguvu gani iliokuwa ikimsaidia.
“Crack , Crack!!!”
Huda hakuwa hata na muda wa kujibu shambulizi , mikono yake yote ilikuwa imevunjwa vunjwa.
“Arghhhhhh…”
Hamza hakujali hata ukulele wake alimuondoa Huda mbele ya Regina kwa teke na kwenda kudondokea kwenye kingo ya kimbweta cha kuhifadhia maboksi ya kuhifadhia samaki,kutokana na nguvu iliotumika kumrusha kuwa kubwa alijikuta akivunjika uti wa mgongo na maisha yake yalikoma palepale huku damu nyingi zikimtoka.
“Huda!!”
Walijikuta wakiita wakiwa hawaamini mwenzao alikuwa ameshapoteza maisha , kila mmoja alishikilia siraha yake , wengie wakiwa na visu na wengine wakiwa na vifaa kama misumari mirefu na kutaka kumlenga Hamza lakini Hamza alikuwa mwepesi mno kwani sarakasi alizoruka hazikuwa za kawaida na kisha kuwapiga na Roundhouse kick.
“Arghhh!!”
Mara baada ya kuwapiga na mateke kifuani watekaji wale walijikuta wakipiga ukulele mkali na kwenda kudondokea kwenye ukuta huku wakitema damu nyingi chini, ilionekana eneo walilopigwa kifuani nguvu yake ilibomoa mpaka mapafu kwani walionekana wakishidwa kuvuta hewa na waliishia kutapatapa na kupoteza uhai kwa teke moja tu la kifua.
Ndani ya sekunde kumi tu Huda , Nori na Dodo walikuwa wameshapoteza maisha
Aliebakia alikuwa ni Mendoza na Mhindi na ilionekana ndio waliokuwa na nguvu kuliko wenzao wote.Walikuwa ni maninja daraja B,ni kosa kuwafananisha na wanajeshi au makomandoo, walikuwa zaidi ya makomandoo.
Katika mapigano ogopa yule mwanafunzi ambae anafundishwa kuua na si vinginevyo , uwezo wake unakuwa sio wa kawaida kabisa na ndio kilichokuwa kwa Mendoza.
Lakini mbele ya Hamza ni kama walikuwa watoto wa darasa la tatu ambao hawakuwa na mahali pakukimbilia.
Ijapokuwa alikuwa na hofu lakini utashi wa kutaka kuishi ulimfanya kutoa kisu kutoka katika kiuno chake na kutaka kumkata nacho shingoni Hamza, alikuwa ametumia uwezo wake wote wa kininja ili kuhakikisha shambulizi lake linafanikiwa.
Hamza mara baada ya kuona kisu kinakaribia kuikata shingo yake,alikuwa ashanyoosha mkono wake kwa chini na kuwekza kukikamata kwa vidole viwili tu tena kule kwenye makali.
Mtekaji alijaribu kusukuma mbele lakini alishindwa kabisa , ilikuwa ni vidole viwili tu vilivyoshikilia kile kisu lakini ni kama vile ni chuma ndio kimeshikilia.
Hamza aligeuza macho yake na kumwangalia , alikuwa na macho sio ya kawaida , ijapokuwa hayakutoka katika ubinadamu wake lakini ilidhihirisha hakuwa mtu mwenye huruma hata kidogo kwa namna ambavyo kiini cheusi kilivyokuwa kikipotea , Mhindi mara baada ya ya kuona namna ambavyo Hamza amebadilika kwa woga aliichia kile kisu na kukaa chini.
Hamza alikuwa na macho ya kichawi , macho yake ni kama yamepoteza kiini na hicho ndio kilimuogopesha Mhindi mtekaji na kuishia kukaa chini kwa hofu huku akijuliza ni macho ya namna gani.
“Wewe ni nani?”
Mendoza aliishia kuuliza kwa hofu akimwangalia Hamza kwa mshangao lakini Hamza hakujibu zaidi ya kutoa tabasamu la kikatili.
“Haiwezekani .. au wewe ni..?”
Mendoza aliekuwa na ujasiri wote alikuwa akimwemwesa midomo kwa woga kana kwamba ukichaa umemvaa , kutokana na msukumo wa nguvu kubwa isiokuwa ya kawaida alihisi mkojo ukimtoka palepale , wazo baya lilimwingia na kujiuliza inamaana kundi lao litakwenda kufutwa kama anachohisi ni cha kweli.
Mara baada ya kuona Hamza anaweza kuwa yule anaemdhania palepale alishuka chini na kupiga magoti.
“Sikujua wala kutegemea anuani ilioachwa katika maabara ya Dokta Genesha ni kuja kukutana na wewe , kama ningejua wewe ndio rafiki yake aliemzungumzia , sisi pamoja na kundi letu tusingekubali kuibeba kazi hii , naomba kwa gharama ambayo tumekwisha kulipa kwa vifo vyetu usije kuadhibu na umoja wetu wote”Aliongea Mendoza.
Hakujali tena kama atapoteza maisha hapo hapo , alichojali ni kuokoa umoja wao tu kwa muda huo maana kitendo cha kuja kumchokoza mtu aliekuwa mbele yake inamaanisha moja kwa moja umoja wao umeingia katika vita nae.
Muda uleule Hamza alikuwa ashatoka kwenye ule muonekano wake wa kishetani na kurudi kawaida
“Mimi sijali , mnaweza kuja kunitafuta lakini nitaendelea kuwapoteza mmoja baada ya mwingine, sina mudi ya kwenda kupambana na genge lenu lote la wachawi mimi”Aliongea Hamza.
“Ni kweli kabisa , sisi kwako ni kama kunguni tu , naomba kifo changu kiondoe kinyongo baina yako na kundi letu”Aliongea na palepale aliinnua kisu kilichokuwa chini na kujichoma eneo la moyo mwenyewe na kudondoka chini.
Kilikuwa ni kitendo cha kushangaza , alijichoma yeye mwenyewe kwa ajili ya kumzuia Hamza asiweke kinyongo na kundi lao.
Mhindi mara baada ya kuona mkuu wake kashajiua hakutaka kujiua kama ilivyokuwa kwake na mara baada ya kuona Hamza ameangalia pembeni palepale alisimama na kutimua mbio lakini jambo lile lilimfanya Hamza kutoa tabasamu na kurusha kile kisu kilichokuwa mkononi mwake na ile Mhindi anaukaribia mlango kisu kiliingia kutoka kwenye kisogo na kutokezea kwa mbele kwenye koromeo na akadondoka chini akitapatapa.
Hamza hakujali kabisa hata kitendo kile na aligeuza macho yake na kumwangalia Regina aliekuwa kwenye usingizi mzito na kuishia kutabasamu.
Comments