Reader Settings

SEHEMU  YA 27. 

Hamza ilibidi amuelezee Regina kwanini anataka aachane nae ,  alimwambia  kwamba  kama wataendeea kuwa pamoja kuna watu lazima wataendelea kufika  kumtafuta na kusababisha matatizo , hivyo watu wa karibu yake watakuwa hatarini , hivyo  hakutaka  kumuingiza  yeye katika matatizo yake.

“Usiwe na wasiwasi  kabisa, nitalipa  malipo ya kuvunja mkataba , pia  haina haja ya kunilipa  kupitia kampuni , nitaondoka bila kuchukua hela”Aliongea Hamza.

Regina macho yake yalichanua , hakujua kwanini lakini licha ya uhusiano wao kuwa wa kimkataba  ila baada ya Hamza kusema  anataka waachane kila mtu ajue mambo yake , alijihisi kukosewa , kutokubali na  kujisikia vibaya.

“Kama ukiondoka sasa hivi , nitadili vipi na familia ya Mzee Benjamini , nitaenda kuwaambia nini wazazi wangu , unataka kuondoka halafu uniachie matatizo, huo ni ubinafsi usingekubali tokea  mwanzo kama ungeondoka  unapojisikia”Aliongea Regina  huku akiwa amebadilika  kabisa.

“Regina  nilijua tu utakasirika , lakini jua  ukiwa na mimi utajiingiza  kwenye matatizo , hivyo ni  kheri  mimi kuondoka kuliko kuhatarisha usalama wako”

“Nimekasirika  ndio lakini siogopi  hatari  yoyote itakayonijia kwanini unanisemea?”

“Lakini   hizi  ni hatari za kujitakia hazikuhusu kabisa , wewe ni wa nje tu , hivyo haina haja ya  kujiingiza kwenye matatizo yangu”

“Wa nje? , wewe si ndio wa nje?”

“Unamaanisha nini?”

“Sikukuambia chochote  kuhusu James wakati ule unasaini mkataba  lakini pia  wazazi wangu , sasa kwasababu yangu  unachukiwa na James na familia yake na wazazi wangu hawakupendi pia, katika hili hata wewe ni  wa nje  tu  na halikuhusu lakini mimi ndio nimekuingiza , kwanini hukuondoka  wakati ule  na kuamua kuondoka sasa baada ya matatizo  yako?”Aliuliza Regina na kumfanya Hamza kushangaa , ni kweli hakuwahi fikiria juu ya hilo.

“Ngoja  nikuambie sababu ,  hukuondoka kwasababu  huwaogopi, wewe ni muongo, wasifu wako ni feki , kila kitu ni feki , pengine hata jina lako sio Hamza  lakini   kitu kimoja ambacho  nina uhakika nacho , hukuwahi kuwahofia  James na familia yake kama wangeamua kukushambulia , si ndio”Aliongea Regina  na Hamza alishindwa kujibu chochote.

“Sasa  hivi ndio umeniingiza kwenye matatizo  ndio unataka tuvunje mkataba , unanichukuliaje? , unaniona dhaifu sio??, unadhani mimi sio mvumilivu?”

Hamza  na Regina waliishia kuangaliana tu  kama  mambwa wanaobwekeana, lakini kwa upande wake  baada ya kuona namna mwanamke huyo alivyokasirika  na muonekano wa kukosewa  Hamza alishindwa kujizuia na kutabasamu.

“Sio kwamba nakuona dhaifu , niwe tu mkweli mimi sio mtu wa kufikiria  mbali kama wewe ,  ninachotaka  ni kutokukuingiza kwenye matatizo tu”

“Kwahio unadhani ukiondoka  na matatizo yangu ndio yataisha?,unadhani tokea niwe CEO nishawahi kuwa salama , hivi unadhani kwanini nimeweka bajeti kubwa kwa ajili ya kitengo cha ulinzi wa kampuni  na

hata kumuajili  Yonesi kutoka jeshini kwa ajili  ya kuwafundisha wenzake?,wewe ni mwanaume lakini

matatizo  yakitokea unataka kukimbia, Uoga tu ndio unakusumbua?”

Hamza hakudhania  Regina angelichukulia hilo swala kwa  namna hio , alichokuwa akijaribu kufanya ni kuhakiksiha anabakia kuwa salama.

“Regina nimesema muda gani nakimbia matatizo , umenielewa vibaya , kama kweli  unaniona mimi muoga  unadhani ningekuja kukuokoa?”

“Kama wewe sio muoga na mimi kama  mwanamke  siogopi kitu , kinachokugopesha nini mpaka unataka kunikimbia?”Aliuliza Regina huku akimwangalia  Hamza machoni.

“Ungejua  ninachojaribu kukuepushia ni kheri usingejibishana na mimi na kukubali mara moja”Aliwaza Hamza katika kichwa chake lakini hakutaka kuongea waziwazi  na aliishia kutoa tabasamu kwa namna  Regina alivyoonyesha ujasiri mbele yake.

“Kwasababu wewe ndio umesema hivyo basi  sitofanya kama nilivyosema”Mara baada ya mrembo huyo kusikia hivyo alivuta pumzi.

“Unadhani unaweza kuja kwenye maisha yangu na kuondoka , unadhani unaweza kuwa msaidizi wangu na Boyfriend feki unavyojisikia ,  hata kama unataka kuvunja mkataba mimi ndio mhusika mkuu  lazima nikubali  maana nimekuajiri”

“Ni kweli wewe ndio mwenye kauli ya mwisho , lakini tuishie hapa , sitotaka kukuelezea zaidi kuhusu mimi , isitoshe  uhusiano wetu ni wa kikazi zaidi hivyo sio wajibu wangu”Aliongea Hamza.

“Okey , nitakuacha kwa leo , lakini nitajua tu iwe ni  mapema au kwa kuchelewa”

Mpaka hatua hio  Regina ashaona kabisa Hamza alikuwa akificha vitu vingi sana kuhusu  yeye  , kitu ambacho  kilimfanya  yeye mwenyewe kuvutiwa kujua zaidi.

Asichokijua Regina ni kwamba  baada ya hapo hatokuwa  wa kawaida tena, hisia zake mbele ya Hamza ndio zilianza kubadilika mara moja kuanzia siku hio.

Hamza  na yeye aliishia kumwangalia mwanamke huyo  , alikuwa mzuri  mnno wa kuvutia  kwa macho ,  licha ya madhaifu machache  lakini upande wake mzuri ulikuwa umeyafunika.

Ghafla tu Hamza alijiktua akiangua kicheko , jambo ambalo lilimshangaza  Regina.

“Unacheka  nini?”

“Nimekumbuka ulivyosema hata jina langu linaweza kuwa feki , Mimi naitwa Hamza Mzee ndio jina langu halisi”Mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akiona aibu za kike.

“Wewe ni mjinga ,  nani kasema anataka kujua jina lako halisi , hata kama umedanganya tutaenda na hili hili la Hamza”

“Vizuri , kwasababu mimi ni mfanyakazi tu huna haja ya kuwa na wasiwasi na mimi sana haha…”

“Hebu harakisha uko , chakula kinapoa  kwa kuongea  muda wote pumba”

“Sawa sawa , nitamaliza , ni bahati tu  nimebakisha miezi mitatu  pekee , vinginevyo nani anaweza kukuvumilia..”

“Unasemaje?”

“Ah ..  sijasema kitu”

“Wewe, tutaona , mshahara wako lazima ni ukate”

“Haiwezekani Boss , nimefanya kosa gani”

******

Swala la Regina kutekwa liliisha kimya kimya , huku likijulikana kati ya  Hamza na Regina mwenyewe , upande wa  Regina  hakuwa mdhaifu dhaifu hivyo  halikumuathiri , ilikuwa ni kama kitu cha kawaida tu kumtokea.

Kils siku  kama kawaida Regina alikuwa na utaratibu wa kutumia Makeup kwa mbaali na kufanya uso wake ambao tayari  ni wa kirembo kuzidi kuvutia .

Kila nguo  Regina aliovaa ilikuwa ikimpendeza , iwe ni rangi nyeusi , ya kijani au nyekundu, nguo nyingi za kike  ambazo zilimfiti ni kama ametengenezewa yeye tu.

Hamza alijiuliza inakuwaje mwanamke akawa mrembo hivi , siku za nyuma wanawake aliowaona kama kipozeo tu  kwa mwanaume , hakuwahi kupenda hapo kabla wala kumhusudu mwanamke , alijua kila mwanamke mzuri  ni mali ya  wenye nazo kwa ajili ya kutuliza akili zao.

Hamza alitamani  Regina awe anakaa siti ya mbele lakini alipendelea kukaa nyuma na kushindwa kuuthaminisha  vizuri urembo wake , kitu ambacho kilimshangaza zaidi jana walikuwa wakiongea na kucheka wakati wakurudi , lakini asubuhi  hio Regina alikuwa kauzu  isivyokuwa kawaida.

Hali hio ilimfanya Hamza kuona labda  kuna kosa amefanya asubuhi na kumsababishia mwanamke huyo kukasirika..

“Hakikisha  kesho hukai mbali na mimi?”Aliongea Regina aliekuwa siti ya nyuma ya gari.

“Kesho si  jumamosi  wikiendi , unakuja kazini pia?” “Kuna mgeni wa muhimu  tutakutana nae kesho  muda wowote ,  ni Mfaransa na wewe unakijua vizuri kifaransa  , hivyo itakuwa vizuri ukiwa  na mimi kama msaidizi”

“Okey Boss”

Tokea asubuhi itimie ndio mara ya kwanza Regina ananyanyua mdomo na kumuongelesha.

“Hivi Regina , kuna kitu chochote ambacho  nimefanya kimekukasirisha?”Aliuliza  Hamza.

“Kwanini?”

“Kwasababu umekuwa kauzu  sana”

“Wasiwasi wako tu , au   unataka nikuchekee chekee muda wote”

“Sio hivyo , nakosa tu amani ulivyo mkimya”Aliongea na  Regina  aliishia kuonyesha muonekano wa kimapozi bila kubadili muonekano.

“Otea..”Aliongea  

“Naoteaje sasa?”

“Basi tafuta majibu”Mara baada ya kuongea hivyo hakuonekana  kujisumbua tena na Hamza.

Hamza aliona bora hata asingeuliza maana amejitia  mawazo tu , hajafannya chochote lakini anaambiwa atafute majibu.

Mara baada ya kufika kazini  Hamza  alifanya kazi kama kawaida , hakuwa akizembea , ijapokuwa kila  akifanya kazi alitafuta muda wakupumzisha akili yake kwa kufanya vitu anavyopenda mtandoani  lakini kazi alizopatiwa alizifanya vizuri tu.

Muda wa mchana kama kawaida alishuka mpaka  mgahawani na kuchukua chakula chake na kisha  mara baada ya kumuona Yonesi akiwa peke yake  kwenye meza alienda kukaa.

Hamza  hakuwa muongeaji mara baada ya kukaa katika maeza ya  Yonesi aliendelea kujiweka bize  na chakula hata kwa Yonesi  ni kama vile alikuwa ashazoea  tu  na hakumfukuza  Hamza , lakini  alikuwa na wasiwasi kutokana na utulivu wa Hamza , alimzoea kuwa roporopo.

“Unafikiria nini?”.

“Unaniuliza mimi?”

“Kuna mtu mwingine hapa?”

“Umeanza lini kunijali?”

“Nani kasema anakujali , nimekuuliza swali tu kama hutaki kujibu acha, wasiwasi wangu muhuni kama wewe kuna kitu  lazima unakipnga kichwani”

“Kapteni wewe na Regina mmefahamiana kwa muda gani?”

“Muda mrefu tu  , kwanini unauliza?”

“Regina ni mtu wa kubadilika badilika kuna muda unaweza kuongea nae vizuri lakini dakika chache zijazo anakuwa mtu mwingine kabisa , nimejairbu kuwaza labda nimemkosea mahali lakini nimeshindwa kukumbuka kabisa”Yonesi baada ya kusikia kauli ya Hamza alijikuta akishangaa  lakini  muonekano wake ulibadilika na kuwa ule wa kejeli.

“Unafikiria sana vitu visivyo na maana , Mkurugenzi akuongeleshe wewe ni nani , hayo ni mawazo yako tu ndio yanakusumbua”

“Kama ni hivyo basi nyie wanawake hamueleweki”

Hamza licha ya kwamba amepitia maisha flani ambayo mtu wa kawaida hawezi kupitia  na hata kuwa na uzoefu wa hali ya juu lakini  likija swala la  kumuelewa mwanamke ilikuwa ngumu mmno kwake.

Baada ya lunch, Hamza alichukua matunda kama kawaida na kwenda nayo juu,  wakati  anatoka kwenye lift  aliweza kukutana  na Eliza ambae alionekana alikuwa akitoka ofisini kwa  Regina.

“Eliza umerudi!?”Aliuliza Hamza huku wakionyesha furaha ya kumuona mrembo huyo.

“Huruhusiwi kuonyesha unanijua sana  tukiwa kazini”Aliongea  Eliza kikauzu.

“Oh , hakuna shida , halafu vipi mbona upo hivyo , hujafurahi kuniona?”Aliuliza Hamza mara baada ya  Eliza kuonekana   hataki kuongea nae.

“Nina kazi kibao, tutaonana”Aliongea Eliza na kisha aliingia kwenye lift akimuacha Hamza  akimwangalia mpaka mlango ulipojifunga.

Hamza alijikuta akihema kwa nguvu na kujiuliza kwanini leo ni kama vile kila mwanamke hakuwa akitaka kumuongelesha.

Aliamua kuingia zake kwa Mkurugenzi ili kukabidhi  yale matunda , Regina alikuwa bize kama kawaida yake akiwa na furushi la makatarasi juu ya  meza yake.

“Mkurugenzi , kula matunda kidogo usifanye kazi na njaa”

“Sawa ,  unaweza kuyaweka hapo”Aliongea Regina  bila hata ya kuinua macho. 

Kwa namna Regina alivyokuwa makini Hamza alikuwa na shauku ya kutaka kujua mwanamke huyo ni kitu gani anafanyia  kazi , hivyo alisogea karibu na upande wa meza yake kuchungulia.

“Hey , usichungulie, toka ofisini kwangu”Aliongea kikauzu na kumfanya  Hamza kulazimisha tabasamu  na kimya kimya  akatoka  huku akimwemwesa midomo na kujiambia wanawake wa aina hii ni ngumu sana kuendana nao vizuri hata kama una nia nzuri kwao.

Hamza mara baada ya kuingia ofisini kwake  alianza kumfikiria Eliza na muonnekano wake wa dakika kadhaa zilizopita , baada ya kufikiria alihisi  pengine  Eliza na  Regina waliongea  kuhusu yeye ndio maana alionekana kana kwamba alikuwa akimkwepa.

Hamza mara baada ya kushikwa na wazo hilo palepale , hakutaka kusubiri  alinyanyuka na kuelekea katika ofisi ya Eliza ili kujua kwanini mrembo huyo ni kama hana furaha  kumuona.

Dakika chche tu  alikuwa ameshafika katika idara ya  mauzo(Sales department) , Eliza  alikuwa  akiongoza idara hio kama meneja  mara baada ya kupandishwa cheo kutoka  kuwa msaidizi wa Regina.

Baada ya kufika katika idara hio alikaribishwa , alijulikana tayari kama msadizi wa Regina hivyo  mara baada  ya kutaja shida   yake ni kuonana na Eliza  alielekezwa  katika ofisi yake.

“Come in” Sauti kutoka ndani iiliitikia   baada ya  Hamza kugonga mlango na kumfanya aingie.

Eliza ambae alikuwa akiangalia tarakishi  alishangaa mara baada ya kuona ni Hamza.

“Kwanini upo hapa?”Aliuliza  na Hamza alitembea na kwenda kuweka mikono yake yote  juu ya meza huku akimwangalia  mrembo huyo  kwenye macho. “Eliza  je kuna kitu chochote unahisi kunishuku?” “Kukushuku , unamaanisha nini?”Aliuliza Eliza huku akiwa na muonekano wa kushangaa  na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja.

“Unaonekana kutokuwa furaha  hata pale uliponiona , au kuna mtu alisema chochote kunihusu mimi?”

Eliza mara baada ya kujua kile kilichomleta Hamza hapo aliishia  kuweka mikono yake  juu ya meza na kupitisha vidole vyake  na kuishia kutoa tabasamu.

“Hakuna”

“Kama ni hivyo kwanini  unaonyesha kutokuwa furaha baada ya kuniona?”

“Otea”

Hamza mara baada ya kusikia kauli hio  hakujua alie au acheke , maana  hata Regina alimwambia hivyo hivyo.

“Eliza hebu acha  kunitesa na kujitesa , naoteaje  sasa kitu nisichokijua , hatujaongea zaidi ya wiki sasa , mimi nitajua  ni wapi nimekukosea?”

“Kwahio unakiri kabisa hatujaongea wiki nzima , tuseme hukuwa na salio  kunipigia , vipi hata meseji umeshindwa kunitumia?”Hamza  sasa alijua wapi kosa lake lilipo.

“Eliza  nisamahe , mimi sio mzoefu sana likija swala la  mahusiano ndio maana  sikupiga simu”

“Nani aamini maneno yako ,  sipo kichwani  mwako ndio maana, usingenikiss kabisa kama unashindwa kujua namna ya  kuwajibika”Eliza alitaka kusema  umenikisi kitaalamu vile halafu  unasema  huna uzoefu ila hakutaka kuongea hivyo na kubadilisha maneno.

“Eliza kukukiss na kukupigia simu ni vitu viwili tofauti , nilikosa tu sababu ya kukupigia  ndio maana , ila nilikuwa nikikuwazia”

“Kwahio unapiga  ukiwa na sababu ya kunipigia , hebu toka ofisini kwangu acha kunipotezea muda nina vitu vya kufanya”Aliongea huku akionyesha kukasirika akiwa amesimama.

Hamza aliona kuendelea kuongea nae akiwa amekasirika hivyo haina maana tena , alimsogelea Eliza kwa haraka  na kushika kiuno chake na kisha akamkiss na  kumfanya  Eliza kutoa macho maana hakutegemea kile kitendo , Eliza aliishia kushika  mbavu za Hamza na kuziminya , alikuwa hataki lakini kujiondoa alishindwa.

Baada ya dakika  moja  Hamza alimuachia , alijua akiendelea wanaweza kuingia katika hatua  isiofaa katika mazingira hayo ya  kazini.

“Nakuahidi kuanzia sasa nitakuwa nakupigia bila hata ya sababu”Aliongea Hamza huku akimwangalia Eliza ambae ameshikwa na aibu lakini kwa namna moja alijisikia  vizuri mno na furaha.

“Nimekusikia ,ushamaliza kazi zako , niache nimaliza na zangu”

“Jumapili  utakuwa na  muda , unaonaje  tukitoka  out hata kwenda kupunga upepo baharini   na kula mihogo?”

Eliza alifikiria kwa muda na kweli aliona  hana  ratiba yoyote  Wikiend  hivyo aliishia kutingisha kichwa kukubali.

Muda huo huo  mlango wa  ofisi ya Eliza uligongwa  na  sauti ya Mirium ilisikika.

“Meneja , hali sio nzuri huku , kuna tukio kubwa limetokea”.Eliza alijiweka sawa huku akiondoa hali ya aibu  usoni na kurudia ile ya kazini na kisha alisogelea mlango na kuufungua.

“Nini tatizo?”

Mirium mara baada ya kuona na  Hamza yupo ndani ya ofisi aliishia kutingisha kichwa  kumpa ishara ya  salamu.

“Dakika chache zilizopita kupitia taarifa ya habari  Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Omega  ametangaza kukubali  kutia saini kwa niaba ya  kampuni yake kuuzwa kwenda  Zena Corporation”

Eliza macho  yake yalisinyaa na alitoka  moja kwa moja na kwenda katika  ofisi kubwa pana iliokuwa na Tarakishi  nyingi za wafanyakazi wa idara ya mauzo.

Muda huo  wafanyakazi wa kampiuni nzima walikuwa wakiangalia taarifa hio ya bahari.

Zena Corporation ilikuwa chini ya  familia ya mzee Benjamini  baba yake na James.

Kila mtu alionekana  kuwalaani Zena  kwa kukosa aibu na kuingilia dili lao  la kuiunua  kampuni ya  Omega.

Eliza aliongoza  wafanyakazi wenzake katika idara ya mauzo kujadili kile kilichokuwa kimetokea.

Upande wa Hamza  alikuwa akijua dili hilo la kampuni ya  Dosam kutaka kuinunua  Omega hivo kuona taarifa hio alijua na Regina atakuwa katika hali  mbaya, ukweli hakujua kama Regina atakuwa katika hali gani.

“Kama sio pingamizi kutoka kwa  wakurugenzi  wasaidizi , Zena wasingeweza kufanikiwa”

“Ndio , Mkurugenzi alikuwa sahihi pia , kama sio

hivyo mnadhani  Zena wangefikiria kuinunua Omega?”

“Mimi nashindwa kuelewa , hawa wakurugenzi ni wazee  lakini bado wanashindwa kuelewa soko linakoelekea , kwanini wanapinga ustawi wa kampuni”

Wafanyakazi walikuwa wakiongea wao kwa wao  huku wakimuonea huruma bosi wao  kwa namna ambavyo wakurugenzi  wenzake wamemsaliti mpaka kufanikisha Zena kuinunua Omega.

Mipango ya  Regina  katika kupanua  kampuni ilikuwa wazi kwa kila mmoja , alitaka kununua kampuni ya maswala ya Tehama ya Omega kwa ajili ya kuingia katika biashara ya Akili Mnemba(Artificial intelligence), alijua  ili kampuni yake iweze kupanuka zaidi alihitaji kitu ambacho kinaendana na wakati  uliopo na ujao , kwa Regina aliona  mfumo wa akili  bandia utakuwa ndio kesho ijayo.

“Meneja ni nini tunapaswa kufanya , Omega ndio hio tushaikosa , unadhani  mauzo yetu yataendelea kupanda”’Aliuliza Asha na wengine  wote.

“Tupo kwenye idara ya mauzo, tunachotakiwa kufanya ni kutimiza wajibu wetu , hili swala lipo chini ya idara  ya Trustees , Mikakati  na masoko , tunamuamini Mkurugenzi wetu Regina, najua atapata  ufumbuzi ,nimeongea  vya kutosha  sasa , tungieni kazini”Aliongea  huku akipiga  makofi  akitawanya wafanyakazi wote kurudi katika nafasi zao za kazi.

Hamza mara baada ya kuona hilo alijua lazima Regina atakuwa anajisikia vibaya , ilionekana dhahiri  kuna mtu ndani ya kampuni alivujisha taarifa.

Muda wote wa mchana wafanyaazi wa juu wa kampuni waliingia ndani ya ofisi  ya  Afisa mtendaji mkuu wa kampuni mmoja baada ya mwingine , ilikuwa  ni kama  kampuni yote ilikuwa   katika hatari , Hamza aliweza kuona namna ambavyo  Regina amechoka wakati wa kuondoka.

Mara baada ya kuingia kwenye lift aliishia kuegamia lift  na hakuongea neno , Hamza na yeye hakutaka kumsumbua , ilikuwa ni mara ya kwanza kuona mwanamke huyo akionyesha hali ya kukosa utulivu  na kwa namna flani  Hamza alimuonea huruma.

Kwa  mfanyabiashara  kama Regina kwake hela inakuwa sio kipaumbele tena , bali kipaumbele ni malengo ya kampuni  kutimia.

Kitendo cha kufika katika  maegesho  ili kuingia kwenye gari waliweza kuona gali nyeusi aina ya Caddilac ikiwa imeegeshwa.

Mabodigadi  wawili  wenye miili ya kibaunsa walikuwa wamesimama pande zote za gari wakiwa na miwani za jua  huku mlango wa kuingilia katika gari hio ukiwa umefunguliwa na alionekana  James ambae alikuwa amevalia shati  la mikono mirefu na suruali ya kitambaa  pamoja na saa ya dhahabu.

Ukiachana na mabodigadi hao pamoja na  James kulikuwa na mtu mwingine  mzee  hivi , alikuwa amevalia shati refu mfano wa kaunda  rangi ya bluu bahari , kitu kimoja ambacho hakikuwa cha kawaida  kutoka kwa mzee huyo ni macho  yake , yalikuwa yamejaa uovu  sio wa kawaida.

Dakika ile le Kaptenni  Yonesi pamoja na walinzi  walitokea  mbio mbio 

“Mkurugenzi , samahani tumeshindwa kuwazuia ndani ya muda”Aliongea Yonesi.

Regina macho yake yalikuwa yamejaa ukauzu na alionyesha kila ishara ya kuwa  na hasira , mara baada ya kumwangalia  James kwa sekunde alitembea kulisogelea gari lake.

Lakini James alitabasamu  kikejeli  na alimkinga Regina kwa mbele  na kisha akamwangalia na Hamza aliekuwa nyuma.

“Wewe kumbe bado upo tu , nimesikia umekuwa msaidizi  , hio nafasi inakufaa sana  kwenye maisha ya Regina”Aliongea.

Hamza alimwelewa alichokuwa akimaanisha , hakutaka kukubali   yeye na Regina ni wapenzi Regina upande wake hakutaka  uhusiano wake kutambulika kwa walinzi hivyo  alimwambia  James ampishe apite.

“Regina achana na ukauzu wako ,  najua  haupo kwenye mudi leo  lakini hayo ni maswala ya kibiashara, maswala yetu binafsi  hayawezi kuathirika” “Hakuna   maswala binafsi  kati yangu na wewe”

“Kinachokukasirisha ni kuikosa Omega, wasiwasi wa nini , mimi na wewe tukishaoana  familia yenu na yetu itaungana , nimeandaa mahali  tayari  ambayo  familia yako itaipenda”

“James  acha kwenda mbali , upo ndani ya maegesho ya kampuni yetu ,  Mkurugenzi anataka umpishe, sijui unanisikia?”

“Nisipompisha  utanifanya nini wewe Mal**ya”

“Unanitukana  wewe mwanaharamu”

Yonesi hakutaka kujizuia tena , hakupenda matusi na aliona amshikishe adabu  lakini  Regina alimzuia.

“Yonesi punguza hasira”

“Mkurugenzi .. amenitukana umemsikia..”Aliongea lakini aling’ata meno yake kwa hasira na kutulia. “James unachotaka kutoka kwangu ni nini mpaka unatoa matusi hapa?”Aliuliza Regina.

“Sitaki chochote , kwanini nitake kitu kutoka kwa mwanamke  ninaempenda  kama wewe, nataka ukubali kutoka na mimi usiku  kwa ajili ya chakula”

“Sijisikii vizuri”

“Kama hujisikii vizuri nitakupeleka hospitalini”Regina aliishia kumwangalia kwa macho ya hasira , hakupenda uking’ag’anizi wa James hata kidogo.

“Regina unatakiwa kujua tayari  umeshindwa, kama ukiendelea kuhangaika kama hivi , hali itakuwa mbaya zaidi kwako na kwa watu wanaokuzunguka , kama una akili kubali  kuolewa na mimi  na tuishi maisha ya furaha , nakuhakikisha hototeseka”

Mara baada ya kuongea hivyo alinyoosha mkono akitaka  kumshika  Regina kidevu.

Yonesi mara baada ya kuona tukio hilo alimkinga Regina na mwili wake.

“Acha ukichaa wako , huruhusiwi kumsogelea Mkurugenzi”

“Fu**ck , wanaumee,  hebu muondoen huyu ch*ko”’ “Yes sir”

Mabodigadi wawili waliovalia suti nyeusi  walisogea  mbele kwa ajili ya kumtoa  Yonesi.

Walinzi waliofika na  Yonesi , mara baada ya kuona kapteni wao anasogelewa na wao walisogea na kuwakinga  wale mabodigadi.

Mabodigadi  wa upande wa kampuni ya Dosam walikuwa wanne na walishindana na mabodigadi wawili aliofika nao James, walikuwa wengi na walikuwa maveterani wa jeshi hivyo ilikuwa faida kwao.

Yonesi mara baada ya kuona maadui zake wanazidiwa aliruka na teke na kumpiga moja ya bodigadi  na akaenda mzima mzima chini na palepale wale wengine walimdhibiti yule mmoja.

Regina mara baada ya kuona walinzi wake wameweza kufanikiwa  kushinda alivuta pumzi ya ahueni.

Lakini James hakuwa  na wasiwasi wowote  na aligeuza shingo yake na kumwangalia yule mzee.

“Master Konki huyu mwanamke sio wa kawaida , hata kama ukimshambulia haiwezi kuonekana  unamnyanyasa maana ni mwanajeshi”Aliongea  James.

Yule Mzee alieitwa Master Konki  alimwangalia  Yonesi kwa macho ya kumchunguza na aliishia  kwenye kifua chake akithaminisha urembo wa  mwanamke huyo.

“Mwanamke mrembo kama huyu lakini anataka kushindana nguvu na wanaume , hebu ngoja nimfundishe adabu kidogo aanze kufikiria namna ya kumhudumia mwanaume”Aliongea hukuwa akiwa na tabasamu la kifedhuli.

 Yonesi mara  baada ya kuona mzee huyo anamsogelea uso wake ulizidi kuwa siriasi , alijua kitendo cha  James kuja hapo akiwa  anajiamini akiongozana na mwanaume huyo basi  lazima atakuwa na uwezo  wa juu.

Hamza  palepale alipitisha macho yake   ya ki uchunguzi kwenye mwiali wa mzee huyo  na aliweza kuona kitu kilichomfanya kukunja sura na kumuonea huruma Yonesi matatizo anayojitafutia 

“Nina wasiwasi  naweza nimshindwe huyu mzee”Aliwaza Yonesi kwa hofu.

“Kapteni  huyu  mwanaume amezeeka lakini bado anaonekana kuwa na tamaa , nipe nafasi nimfundishe  adabu mimi”Aliongea  moja  ya mlinzi wa kampuni.

“Sogea  mbali , mimi ndio kiongozi wewe ni  msaidizi tu nitamshikisha adabu mimi”Aliongea  Yonesi kwa kujigamba.

“Kapteni kuwa tu makini , mimi nitakushangilia  ukishinda”Aliongea Hamza  huku akicheka.

“Huna haja ya kuongea”Alijibu.

“James   nadhani ushanipa  ruhusa ya kumkamata huyu mwanamke na kuondoka nae”

“Usiwe na wasiwasi Master  Konki , mimi shida yangu ni mchumba wangu Regina , huyo mwanamke unaweza kumfanya chochote ukishamshikisha adabu, nakuhakikishia hivi  , hakuna  kitengo cha usalama cha aina yoyote ndani ya taifa hili kitakuuliza”

“Vizuri sana kijana , nimekaa  mafunzoni kwa muda mrefu bila  kuonja  nyama tatu , kwa urembo wa huyu binti  atakidhi kabisa  matamanio yangu”Aliongea   Konki.

“Na uzee wote huo  lakini  unaongea   bila busara ,  usamehewe bure , isitoshe  mpaka kuja na James hapa  inaonyesha ni kwa namna  gani huna akili”Aliongea Yonesi kwa hasira.

Dakika hio hio  Yonesi aliamua kukaa mkao wa kijeshi , huku akimwangalia Mzee Konki na macho ya  tahadhari.

“Sogea mrembo nione  ni kipi  una cha kunishangaza”

“Umeomba mwenyewe usije kunilaumu”Aliongea Yonesi na palepale aliinua mguu wake na kudhamiria kumpiga yule mzee lakini kabla hata hajamfikia  Konki alikuwa ashainua   mkono wake na kuzuia lile teke huku vidole vyake vitatu vikitengerneza  umbo  kama  kucha za  Tai  na kwa ustadi wa  hali ya juu alimchoma  na vidole vile eneo  la mguuni.

“Arghhhhh..”

Yonesi alijikuta akipiga ukulele wa maumivu na bila ya kupenda alirudi nyuma huku akisikiliza maumivu , hakuamini vidole vitatu  tu vinaweza kumletea maumivu makali ya namna hio.

“Mbinu ya  kimapigano ya kucha za Tai”Aliongea huku akiwa na mshituko,  Yonesi hakutarajia mzee kuwa na uwezo huo , kwa kawaida Yonesi alikuwa mzoefu likija swala la  mbinu za kimapigano , wakati alipokuwa jeshini alishahudhuria kozi ya kimapigano katika  taifa la Thailland  na  China.

Unachopaswa kujua likija swala la  mapigano  kama vile Kung fu , unachoona mtaani au kwenye filamu mara nyingi ni  kwa ajili ya maoneysho tu lakini likija  yale mapigano halisi , mbinu zake  ni ngumu sana kuona zikitumika  mfano  wake ni kama mbinu ya hio ya vidole vya Tai, ni  mbinu ambayo  anaejifunza anafundishwa kuua siku zote na mara nyingi unamlenga mtu katika maeneo dhaifu ya mwili.

Licha ya Mzee Konki kuonekana mzee lakini  spidi yake haikuwa ndogo na nguvu ya vidole pia haikuwa haba mpaka kufanikiwa kumsabishia Yonesi maumivu makali.

Mzee Konki hakuacha kushambulia , alizidi kumsogelea  Yonesi huku akiwa na macho ya uchu, kama sio uwezo wake wa kukwepa  pengine vidole vingeweza kumtoboa  eneo la kifuani.

Regina ambae alikuwa akiangalia  mpambano huo aliishia kukunja sura , hakuamini  James ameenda mbali mpaka kukodi mtu wa aina hio.

“Mzee Konki usiwe sana siriasi , nataka umshikishe tu adabu  nisije onekana mtu mbaya mbele ya mchumba wangu”Aliongea James.

“Msichana  nimependa sana hio miba hapo  kifuani kwako , kubali tuondoke pamoja kuliko kuendelea kuwa mlinzi”Aliongea Mzee Konki.

“Kwenye ndoto zako”Aliongea Yoinesi na kuzunguka na teke akimlenga kumpiga  Konki kwenye shingo  lakini mguu wake ulishikwa.

“Haipendezi kwa mrembo kama wewe  , ila  ngoja tu nikuvunje mguu mmoja  , tuone kama  utaendelea kuleta  ukinzani hehe..”

Aliongea  Master  Konki huku akicheka na palepale aliweka vidole vyake katika mkao wa kucha za Tai ili kumponda nazo  Yonesi kwenye mguu.

Dakika ambayo Yonesi anawaza  anakwenda kuvunjwa mguu wake na kuishia kufumba macho  alikuja  kugundua hakuna kilichomtokea. “Hamza?!”

Yonesi alimkodolea macho  Hamza , bila hata ya kujua Hamza alikuwa ashatokea pembeni yake na kushika  mkono wa  Mzee Konki.

Mzee Konki alikunja sura  na kujaribu kusogeza mkono wake  lakini aligundua hakuweza hata kujitoa na aliishia kuachia mguu wa Yonesi  na mkono mwingine aligeuza kuwa  vidole vya Tai  na kujaribu kumshambulia  Hamza kwenye macho.

Lakini ile  mkono unamkaribia Hamza  na yeye alikuwa ashatengeneza staili ileile ya vidole vya Tai na 

Mzee Konki mara baada ya kwenda kugusana na vya Hamza alijikuta akitamani kutoa ukulele kwa  maumivu yaliozidi mpaka vidole vikashikwa na ganzi, kidogo  tu vidole vyake vivunjike.

Hamza mara baada ya pale  alimsukuma  nyuma yule mzee  na kumfanya ajikokote asidondoke.

“Wewe Mzee , Kapteni Yonesi ni kama  mjukuu wako  lakini  huoni aibu unataka kumvunja mguu”Aliongea  

Mzee Konki alibakia katika mshituko wa  ajabu huku akimwangalia Hamza , hata kwa  Regina na  Yonesi  walikuwa wamepatwa na mshituko , James muonekano wake ulikuwa ni ule wa  kukakamaa.

“Unaijua sanaa ya  ndole za Tai pia!!?”Aliuliza Mzee Konki huku akiwa na mshituko  kwani  Hamza alitumia mbinu yake.

“Kwani hii mbinu  ina ugumu gani kutumia?”

“Unaongea ujinga , hii ni  mbinu ya sanaa ya kucha za Tai , ngoja nikuonjeshe utamu wake”

Mzee Konki aliona ni kama udhalilishaji  hivyo kwa hasira aliruka hewani  kama mshale huku akitanguliza mkono wake wenye staili ya kucha za Tai kumlenga  Hamza  katika shingo yake.

Hamza  alivyosimama kizembe ni kama vile amekosa cha kufanya na anasubiria shambulio  hilo , lakini  ile Mzee huyo anamkaribia na yeye alinyoosha mkono wake  katika staili ya kucha za Tai na kumzuia kwa kubananisha vidole vyake na vya yule Mzee.

Baada ya kuvibananisha katika vidole vyake alizungusha kwa nguvu  na kwa hasira kali.

“Arghhhhhhhhh..”

Mzee Konki alitoa ukulele wa aina yake , mifupa ya vidole vyake ilisikika ikitoa mlio  wa kuvunjika kutokana na nguvu aliotumia Hamza  na  mara baada ya kutua chini aliangalia mkono wake  akiwa katika maumivu makali huku akimwangalia Hamza katika mshangao.

“Wewe mtoto .. umejifunzia wapi hii mbinu!!?”

Mzee Konki  alikuwa akiamini kwenye taifa la Tanzania  hakuna mtu ambae anaweza  kumshinda likija swala la mapigano bila ya siraha , hasa  katika kutumia mbinu yake hio ya  Kucha za Tai.

Alikuwa amefika bongo na mpango wake ni kwenda kushindana na wanajeshi  wote ambao wanajita makomandoo , alikuwa akitaka kujihakikishia yupo mwenyewe mwenye mafunzo makali ya  kimapigano, lakini kwa bahati mbaya   anakutana na Hamza kabla hata  ndoto yake haijatimia na anashikishwa adabu , kitu cha kumshangaza zaidi aliemshikisha adabu alikuwa  ni kijana mdogo sana kuliko yeye ambae amejifunza kwa miaka mingi kuimaster hio  mbinu.

Regina ,Yonesi na wengine  pia walikuwa wanamwangalia Hamza  kwa maswali , walishaona Yonesi hakuwa na uwezo wa kumzidi  huyo  mzee licha ya kupitia  kitengo cha special forces jeshini.

James mara baada ya kuona tukio lile aliishia kupiga hatua moja kurudi nyuma  , alikumbuka baba yake alichomwambia kuna uwezekano huyo Hamza asiwe  mwepesi na sasa ndio anaamini.

“Mtu  alienifundisha ni maarufu sana  dunia nzima , anajulikana kila kona ya dunia kutumia hii mbinu, nikikuambia jina lake unaweza kupatwa na mshituko”Aliongea Hamza.

Previoua Next