“Acha makusudi ya kujikweza , sheria namba moja katika ulimwengu wa mapigano ni kujitambulisha wewe na shirka lako , mimi ni mwanafunzi kutoka Shirka ya Tai Mweusi, jitambulishe Shirka lako na wewe kama ujasiri huo unao , udhalilishaji wa leo utalipwa mara mia zaidi”
“Nimefundishwa na Master Kato Hawk ushawahi kumsikia?”Aliuliza Hamza
“Kato Hawk , mbona sijawahi kumsikia ni raia wa wapi?”Aliuliza Mzee Konki akionyesha kutomjua.
James mara baada ya kuona Mzee Konki anaanza kuuliza maswali ya kipuuzi alitamani kwenda na kumpiga , ila uwezo huo hakuwa nao.
James alikuwa akimjua Kato Hawk, mtu yote mpenda filamu za angemfahamu Kato Hawk.
“Ushawahi kumsikia mtu anaeitwa Kato Hawk huko jeshini?.”Aliuliza Regina ki udadisi swali hilo likienda kwa Yonesi.
Yonesi na wenzake walikuwa wakimjua ndio lakini hawakutaka kumwelezea Regina na walishangaa kwanini hamjui.
“Taja jina la Shirka ulilojifunzia, sijawahi kusikia jina la mtu uliemtaja?”
“Kama hujawahi kumsikia mtu maarufu kama huyo , basi sioni haja ya kukuambia nenda kaulize”Aliongea Hamza akiwa na muonekano wa kejeli.
Mzee Konki alikuwa na hasira mno , kama sio kuumia mkono wake angejaribu kuzipiga tena na Hamza , alijua kuvunjika kwa vidole vyake hawezi kupona ndani ya siku kadhaa.
“James , turudi kwa leo ila naahidi , nisipokuja kulipiza hili labda sio mimi Konki Master”Aliongea Konki kwa hasira , hakuamini miaka yake yote ya kujifunza mapigano na kutia mguu Tanzania anakuja kukutana na udhalilishaji.
James mara baada ya kusikia hivyo alifurahi , alijua lazima mzee huyo atakuja tu kulipiza kisasi.
James ashaona kabisa Hamza sio saizi yake hivyo aliondoka kimya kimya
Regina alimwangalia Hamza kwa macho ya kiulizo na alijiambia ndio maana aliweza kumuokoa kiwepesi tu, hali hio ilimfanya kukosa hiari ya moyo wake na kujisikia hali isioelezeka.
Wakati wa kurudi nyumbani kulikuwa na foleni kubwa mno hivyo gari ilisogea taratibu taratibu. “Kwahio Master wako ndio anafahamika kwa jina la Kato Hawk , umefahamiana nae nje ya nchi nini?”Aliuliza Regina.
Swali lile lilimfanya Roma kushituka na kidogo tu akanyage kwenye pedeli tofauti na breki kugonga magari ya mbele yake.
“Regina inamaana hujawahi kusikia hilo jina?”
“Ningekuuliza kama najua , hata Yonesi nimemuuliza ameonekana hajui”
Hamza alijifikiria na kujiambia inakuwaje hawamjui , lakini hata hivyo aliona kwa mwanamke kama Regina ni haki kutokumjua.
“Nilikuwa nikiongea ujinga tu pale , usichukulie siriasi”Aliongea Hamza.
“Kwanini unakuwa hivyo ,unaona aibu kuwa na Master eh?”
“Haha.. nimeongea kumugopesha tu yule usichukulie siriasi”
“Usiponiambia nitatafuta mtandaoni na lazima nitajua tu”Baada ya kuongea hivyo alichukua simu yake na kuingia kwenye mtandao wa google na kuandika jina la Kato Hawk.
Hamza aliishia kutingisha kichwa tu na kujiuliza kwanini huyu mwanamke ana shauku ya kujua siri zake namna hio.
Ndani ya nusu dakika tu , Regina mashavu yake yalikuwa mekundu na aliishia kung’ata lips zake na kuweka simu chini bila kuongea chochote.
Hamza mara baada ya kuona muonekano wa Regina alijua tayari ashaujua ukweli kuhusu Katona alitamani kucheka kicheko kikubwa.
“Hehe, nilikuambia mimi usitafute haya ona sasa?”Aliongea Hamza huku akicheka.
“Muhuni sana wewe..”Aliongea Regina akiwa na hasira , hakuaminni alikuwa ameuliza swali hilo kwa Yonesi na wenzake , alijihisi kuona aibu
“Nilishakuambia nilikuwa nikiongea ujinga, halafu kingine Kato Hawk hawezi kuwa na vigezo vya kuwa master wangu , uwezo wangu wa mapigano kwa kutumia vidole ni wa juu mno”
“Kimya , endesha gari” Regina hakutaka kumsikiliza tena , alitamani kumsogelea na kumpiga kibao.
“Basi ngoja nikuambie ukweli , kama usiponiamini unaweza kujaribu kutafuta tena”
“Ukiongea ujinga tena nitakata mshahara wako”
“Sawa Madam , kama hutaki kusikia basi nitakaa kimya”Aliongea Hamza huku akitamani kucheka.
****
Upande mwingine wa jiji kulikuwa na kikao kilichojumuisha kundi la watu wenye mafunzo ya kimapigano lifahamikalo kwa jina la Tanzania Martial Art Association.
Kundi hili halikuwa la kihalifu lakini kwa namna moja lilitafsirika kama la kihalifu kutokana na usiri mkubwa wa ajenda zao , unaweza kusikia kuna kundi hili lakini huwezi kujua ni kitu gani wanachokifanhya wakikutana.
Kuna wanaosema kundi hilo hufadhiliwa na Binamu , hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa madai hayo., lakini taarifa ya kuaminika hata baadhi ya wanajeshi wenye vyeo vya ukomandoo jeshini walikuwa ni wanachama na hawakujiunga kwasababu walitaka bali walipambanishwa na wenzao na kukidhi vigezo na kuingia katika umoja huo na kulikuwa na faida kubwa sana ya kimaslahi kwa kila mwanachama wa kundi hilo.
Sasa katika moja ya jumba la kifahari lililopo Tegeta
kulikuwa na kundi la watu ambao walikuwa wamevalia mavazi ya suti na walikuwa wamekaa eneo la sebule yenye masofa mengi ya thamani ya juu.
Kwa muonekano wao ilionyesha kabisa hawakuwa watu wadogo katika jamii , mmoja ambae alikuwa katikati ndio kiongozi alifahamika kwa jina la
Fanueli Yowe au unaweza muita Kanali Yowe.
Ndio alikuwa ni Komandoo wa jeshi la taifa lakini pia mwanachama wa umoja huo wa sanaa ya mapigano.
Ukiziangalia sura zote zilizokuwa ndani ya eneo hilo usingeamini kama walikuwa na uwezo wa kupigana wa hali ya juu na baadhi yao ni makomandoo wa jeshi.
“Nadhani kila mmoja wenu amesikia , mwanachama wetu mpya Mzee Konki amekutana na mtaalamu wa hali ya juu wakati alipokodiwa na Mzee Benjamini wa kampuni ya Zena?”
“Hii maana yake ni kwamba mpaka sasa hakuna mmoja wetu hapa anaemuweza mtu huyu , maana tunajua fika Mzee Konki ndio mwanachama wetu mpya ambae ametushinda wote kimapigano, hii ni taswira mbaya kwa umoja wetu na maslahi yetu kwa ujumla katika nchi hii, kwa kusema hayo nimeitisha kikao hiki ili kuwauliza mnaonaje hili swala?”
“Kwa mtazamo wangu lazima mtu huyo atakuwa si wa hapa Tanzania na hata kama ni wa Tanzania basi
amerudi hivi karibuni na pengine ameajiriwa kulinda kampuni ya Dosam”
“Mimi pia nadhani huyu ndio mtu alieripotiwa kwetu na Amosi , unajua Amosi licha ya kutokuwa na uwezo wa hali ya juu lakini ana macho ya kuona mtu ambae ana uwezo mkubwa , nasikia baada ya hapo Amosi alipokea vitisho kutoka kundi la Chatu aache kabisa kumchokoza yule mwanamke mfadhili wetu anaemtaka”
“Unamaanisha Dina ndio aliingilia , nadhani kadri siku zinavyoenda ndio anasababisha matatizo zaidi”Aliongea mwanaume mwingine aliefahamika kwa jina la Gosu au Mzee Gosu ni mstaafu kutoka polisi.
“Kwanini mnampa bichwa yule msichana ,tunajua wote hapa hatumuwezi lakini hatuwezi kumsujudia pia”
“Mimi nadhani tuachane na swala la Dina , na Mzee Konki mwenyewe atuelezee ni kwa namna gani tutarudisha heshima yetu , wenzetu kutoka nje ya nchi wakisikia kuhusu hili watadharau na hawatukubali kufanya biashara na sisi”
“Nadhani kwanza tumfahamu ki undani ni nani , alitaja Master jina la Master aliemfundisha lakini sikuweza kumfahamu , nadhani kati yetu hapa kwenye huu umoja lazima atakuwa amesikia jina hilo , amesema anaitwa Kato Hawk na ni maarufu sana” “Eeh!!
“Watu wote walikaa kimya na kufanya hali itulie na kitendo kile kilimfanya Mzee Konki kushangaa.
“Mbona kila mtu amekaa kimya?, au inamaana mnamjua tayari?”
“Mzee Konki nadhani ni kweli umechoka mno , unaonaje ukiingia chumbani kupumzika kwanza”
“Mkuu kwanini nipumzike , hiki kikao si kinanihusu mimi na yule mpuuzi?”
“Mzee Konki acha kututania , yaani unatuambia mcheza filamu za ngono anaejitamba mtandaoni kuwa ni Bruce lee ndio mtaalamu wa mbinu ya kucha za tai.”
“Nini !!, Mcheza filamu za ngono , mnamaanisha nini?”
“Mzee Konki hatukulaumu , wewe ndio mzee hapa hivyo hutumii sana mtandao wa internet hivyo ni rahisi kutomfahamu Kato Hawk, huyo mtoto inaonekana alikudanganya makusudi , haina haja ya kuwa siriasi hivyo”Aliongea Mzee Fanueli Yowe.
Mzee Konki mara baada ya kuagalia sura ya kila mmoja alijikuta akishindwa kuzuia kicheko na muda huo huo watu wote walimuunga mkono na kuanza kucheka na ghafla tu akaacha na wote wakaacha.
“Mpuuzi sana yule mtoto , nitamchuna ngozi”Aliongea kwa hasira , hakuamini haikuwa swala la kupigwa tu lakini vilevile ametajiwa mcheza filamu za utupu kama Master.
Kato Hawk kabla ya kuwa muigizaji wa filamu za kimapigano alifahamika kama Gerald Lupe alikuwa ni mcheza filamu za ngono maarufu sana , kitendo cha kubadilika kutoka ugiizaji wa filamu hizo na kuingia katika sanaa ya mapigano huku akijifananisha na Bruce lee ndio alijibatiza jina la Kato, uhusika wa Bruce lee katika filamu ya Green Hornet(1966)
,hakuna mtu ambae alikuwa akiamini kama Gerarld Lupe au Kato alikuwa akijua mapigano , kilichomfanya kuwa maarufu sana hadi Tanzania ni wakati alipofika nchini katika uigizaji wa filamu huko Ngorongoro na kupewa mapokezi makubwa kwa kigezo cha kutangaza utalii, kilichomfanya pia kuwa maarufu dunia nzima ni namna ambavyo alikuwa akijibrand kwa kutengeneza vidio fupi fupi katika mtandao wa Tiktok na Reel Instagram akionyesha staili mbalimbali za mapigano kama Bruce Lee lakini ikaja kujulikana anafanya Editing huku kile watu walichokuwa wakiona sio uhalisia.
Skendo hio ya kufanya editing ilimfanya kuzomewa na watu wengi mtandaoni huku wakimuonya
asitumie utambulisho wa kusema yeye ni Bruce lee aliezaliwa(Recarnated) katika mwili wa Gerald Lupe kwani ni kuchafua hadhi ya kumbukumbu za kishujaa za Bruce lee.
Hivyo ukiingia mtandaoni ukiandika jina la Kato Hawk ni Gerald Lupe mcheza filamu za ngono maarufu anaedai ni Bruce lee aliezaliwa katika mwili wa Gerald Lupe.
“Mzee Konki haina haja ya kuwa na hasira , tunachopaswa kuamini kwasasa ni kwamba huyu mtoto sio wa kawaida , kama ni hivyo unadhani kwanini hajatoa jina la Shirka analotokea.
“Kesho mapema narudi Thailland kwenye Shirka langu , nipo tayari kualika hata wataalamu wa hali ya juu wa kimapigano kwa ajili ya kumshikisha yule mtoto adabu”Aliongea kwa hasira.
Kauli ile iliwafnaya wote waliokuwa hapo ndani kufurahi , walijua fika Mzee Konki kama ninja wa daraja la juu lazima atakuwa anafahamiana na maninja wengine wa uwezo wa juu.
“Mzee Konki tutasubiria kurudi kwako kama ndio hivyo , ruhusa unayo kutoka kwetu”Aliongea Mzee Yowe.
******
Siku iliofuata ilikuwa ni jumamosi , Kwasababu ilikuwa wikiend haikuwa lazima kwenda kazini mapema , hivyo Hamza alitoka nje kwenye uwanja wa bustani ya nyumba na kuanza kuchukua mazoezi.
Mazoezi yake Hamza hayakuwa ya kawaida hata kidogo , hayakuwa ya kukimbia wala ya kuruka ruka.
Ilikuwa ni kama vile anakata mauno kwa jinsi alivyokuwa akifanya , lakini utofauti ulikuwa kwenye viungio vya miguu yake vilikuwa vikipinda katika mjongeo wa aina yake.
Kwa lugha nyepesi ni kama vile anajaribu kucheza cheza tu kupoteza muda , hakukuwa na kitu cha kushangaza sana kwa kile anachokifanya na mtu asiejua anachokifanya angeishia kucheka , kilichokosekana ni mziki wa saida Karoli wa Maria Salome tu.
Lakini Hamza alikuwa siriasi mno , alikuwa tena amefumba macho kabisa huku akiendelea kukata mauno.
“Wewe, wewe umekuwa chizi , kwanini unakata mauno asubuhi asubuhi yote hii ?”Ilikuwa ni sauti tamu ya Regina na ilimfanya Hamza afumbue macho yake.
Regina alikuwa amevalia tisheti ya rangi ya pink iliomfanya chuchu zake kuchomoza kama miiba , kikaptura cha rangi nyeupe na raba aina ya Converse , alionekana kama vile ni mwanafunzi wa chuo anaejiaandaa kwenda Jogging.
“Mbona unanikodolea na macho yako?”Aliuliza Regina huku akiona aibu za kike.
“Regina kumbe na wewe una ratiba za kuchukua mazoezi”
“Wiki nzima kazini , siku mbili za mazoezi , unadhani ukiwa na shida ya mwili unaweza kufanya vizuri kazini , halafu acha kubadilisha topiki , kwanini unacheza kibwebwe asubuhi asubuhi?”
“Kibwebwe ndio nini , hii sio mchezo ni mbinu yangu ya mazoezi , ina nguvu ya ajabu mno”
“Mh ,mbingu gani hio ya mazoezi ya kukata viuno , jina lake inaitwaje?”
“Jina lake .. dah hata sijawahi kulifkiria.. kwa mtu wa kawaida anaweza kuona nacheza au kufanya maigizo lakini usichokijua ni kwamba nisingeweza kuwa na uwezo niliokuwa nao leo hii kama sio hii mbinu”
“Unajaribu kumdanganya nani , mimi nadhani ni kwasababu tayari wewe ni kichaa hivyo hata sikulaumu ukikata viuno asubuhi asubuhi”Aliongea Regina na alijua kabisa Hamza anaendelea na mchezo wake wa kumdanganya.
“Unadhani nadanganya , ijapokuwa kuna maelezo mengi ambayo naweza kukuelezea mpaka uelewe ila hii ni mbinu inayokuwezesha kuwa na muunganiko wa kimapigano”
“Acha uongo wako , kama ukiona kichaa kishaamka tafuta sehemu ya mbali ucheze midundiko yako , usije kumuua Shangazi kwa presha”Aliongea Regina na hakutaka kuongea nae zaidi bali alitoka nje ya geti na kuanza kukimbia katika barabara ya ufukwe wa bahari kuchukua mazoezi.
Mara baada ya Regina kutoka Hamza hakujali kejeli za Regina kabisa aliendelea kucheza kama vile ni mchawi , alikuwa akicheza anapanda juu anaenda mpaka chini halafu anarudi tena na kutingisha kiuno , kwa namna alivyokuwa akifanya ungeishia kucheka tu na kujisemea bangi ya asubuhi asubuhi sio nzuri.
Baada ya lisa kupita hatimae Regina alirudi akiwa anakimbia na kwa kuangalia mwili wake tu alijua Regina hakuwa mzembe kabisa na ilimshangaza na kujiuliza kwanini hakuona hilo mapema, au ni kwasababu ya urembo wake ndio maana hakumchunguza, Hamza aliishia kuguna tu na kujiuliza Regina ana siri gani na kuwa na mwili wa kijeshi.
Hamza mara baada ya mazoezi aliamua kuingia ndani na kujisafisha na kisha alikaa mezani kwa ajili ya Breakfast ambayo ilikuwa imeandaliwa na shangazi.
Regina na yeye alikuwa ndio wa mwisho kukaa mezani , kama kawaida ya tabia ya wanawake kujiremba ndio maana alichukua muda mrefu na mara baada ya kukaa mezani alikula kidogo tu tena nusu kikombe cha maziwa.
Wakati Hamza akiwa bize aliweza kuona simu ya Regina inaita kupitia kio chake , ilikuwa ni ya Linda sekretari wa Regina.
“Linda Mr Frei amefika tayari?”Aliuliza Regina mara baada ya kupokea.
“Ndio Mkurugenzi , Mr Ferney ndege yake imekwisha kutua, anajiandaa kuelekea Hotelini , nasikiliza maelekezo yako?”
“Haina haja ya kumsumbua kwasasa , atakuwa amechoka sana , tukiongea nae sasa hivi anaweza asitoe ushirikiano mzuri,tuma barua pepe kwa msaidizi wake na muulize ni saa ngapi tunaweza kukutana”
“Sawa madam”
Mara baada ya kukata simu Regina alimgeukia Hamza aliekuwa bize kumalizia vitafunwa vyote.
“Nimekuandalia nguo kadhaa na zimewekwa kabatini chumbani kwako , kazivae kama zilivyo muda si mrefu tunaondoka”Aliongea Regina.
Comments