SEHEMU YA 29.
“Kuna ulazima wa kubadilisha na wikiend yote hii , nguo zangu nishazifua ni safi na hazina tatizo , kuna haja gani ya kuvaa nguo mpya?”Aliongea Hamza huku akiangalia Tshirt yake ya rangi ya bluu aliovaa na pensi yake.
“Kwahio zikiwa safi ndio nini, ni brand gani na umenunua shilingi ngapi?”Aliuliza Regina akiwa na muonekano wa kukereka.
“Kuhusu hilo ,.. sijui pia”Aliongea Hamza akigoma kujibu amenunua nguo zake shilingi ngapi.
“Mgeni tunae enda kukutana nae ni Mr Felini , mkurugenzi wa kitengo cha ubunifu kutoka Zara Group , sio mtu wa kawaida ni mbunifu namba moja duniani likija swala la mavazi, sasa akikuona na hayo mavazi yako unadhani atatuchukuliaje , anaweza asikubali kuongea biashara kabisa na sisi”Aliongea Regina.
Hamza alifikiri kidogo lakini aliona hakuna haja ya kujibishana na Regina hivyo alitingisha kichwa kukubali.
“Kama ni hivyo nitaenda kubadilisha”
Lakini sasa kabla hata hajasimama kutoka kwenda juu kubadili mavazi yake simu yake ilianza kuita na jina lilitokea Frida na palepale bila ya kujiuliza mara mbilimbili alipokea.
“Hello , Dr habari za asubuhi?”Alisalimia Hamza.
“Hamza haraka sana fika nyumbani kwangu , haraka sana ni dharula”Aliongea Frida na sauti yake ilikuwa na kitetemeshi na hilo Hamza alihisi.
“Kuna nini Dokta Frida?”Aliuliza Hamza huku akikunja sura na alihisi lazima kutakuwa na shida imempata lakini hakusikia sauti tena kwani simu ilishakatwa, Hamza alijifikiria kwa dakika kadhaa na aligeuka na kumwangalia Regina.
“Regina kuna dharula kuna sehemu naenda , hivyo nitatangulia”
“Dharula gani?” Aliuliza Regina lakini Hamza alikuwa ashatoka kwenye meza na alikuwa akitokomea nje
“Wewe , unaenda wapi , tuna kazi ya kufanya leo , rudiii”Aliongea Regina akimwangalia Hamza kwa mbali na Hamza alimuonesha ishara tu ya simu akimaanisha atapiga.
“Nimekufukuza kazi kwanzia leo, usije ukarudi hapa”Aliongea Regina kwa hasira lakini hakujua kama Hamza alikuwa amemsikia.
Shangazi mara baada ya kuona tukio hili aliishia kutingisha kichwa chake tu huku akuonyesha wasiwasi wa mahusiano ya Regina na Hamza.
Hamza alitumia dakika therathini hivi kutoka anapoishi mpaka Madale , alitumia taksi hivyo njia za mikato zilikuwa nyingi ili kuepuka foleni barabarani.
Kitendo cha taksi kusimama katika geti ya nyumba hio , Frida alikuwa tayari yupo nje na mara baada ya Hamza kufungua mlango kutoka, Frida alimpa ishara ya kurudi ndani ya gari na Frida na yeye aliingia.
“Tupeleke Asante Restaurant”Aliongea Regina.
“Malipo yataongezeka boss wangu”
“Just drive”Aliongea Regina na palepale dereva aligeuza gari na kurudi alikotoka.
Hamza alimwangalia Frida , alionekana kuwa na wasiwasi mno kana kwamba ni mwizi anaefukuzwa.
“Kuna nini Frida?”
“Tutaongea”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa , alijua Frida hakutaka kuongea mbele ya dereva.
Mgahawa wa Asante haukuwa mbali sana ni mita kadhaa kutoka anapoishi Frida mkabala na kanisa la wakatoliki na walishuka hapo huku Frida akitoa elfu therattini na kumkabidhi yule dereva n baada ya kupokea hela hio alionekana kuridhika.
Tuingie mgahawani sasa?”Aliongea Hamza mara baada ya kuona mwanamke huyo ana sita sita. “Hapana tunatembea taratibu taratibu nitakuelezea kadri tunavyotembea”Aliongea na Hamza alishukuru jua sio kali sana.
“Kuna nini?”Hamza alivunja ukimya.
“Wiccan wameanza kunifuatilia , leo nachukuliwa kwenda kuhojiwa”
“Kuhojiwa , unamaanisha nini?”
“Siwezi kusema sana , ila nimevunja kanuni za ki uanachama na baada ya mahojiano pengine nitaingia kwenye adhabu ya siku arobaini”Aliongea Frida akiwa na wasiwasi mno na swala hilo lilimshangaza Hamza.
Frida alikuwa akiangalia nyuma na mbele , ni kama alikuwa akiangalia kama kuna anaemchunguza.
“Kabla ya kuja kuchukuliwa nilihitaji tuonane, maana kuna uwezekano tusiweze kuonana tena kwa muda mrefu kidogo”Aliongea na kumfanya Hamza kumwagalia mrembo huyo machoni.
“Kosa ulilofanya linahusiana na mimi?”Aliuliza Hamza na Frida alitingisha kichwa kukataa. “Sijui nani ananiandama , lakini taarifa zimefikia umoja mimi ni shushu wa Sinagogi , napaswa kupinga vikali shutuma hizi katika mahojiano lakini sina uhakika”Aliongea Frida huku akishika mkoba wake vizuri.
“Mbinu zinazotumika kutuhoji sio za kawaida , kuna uwezekano nitaelezea kila kitu hata zile siri ambazo zipaswi kusema , sina muda mrefu wa kuongea na wewe , nataka kukuuliza swali moja tu?”
“Uliza?”Aliongea Hamza huku ndita zikijikunja kiasi.
“Baada ya kupata taarifa ya vifo vya kundi la wawindaji kutoka Samar , moja kwa moja nilijua kuna uwezekano umehusika na vifo vyao, kweli si kweli?”Aliuliza Frida na Hamza hakujua mwanamke huyo alijuaje lakini alitingisha kichwa kuashiria ndio na Regina alivuta pumzi nyingi na wote walikuwa wamesimama.
Kwa jjinsi walivyokuwa wakionekana ni kama Frida na Hamza ni wapenzi na hata baadhi ya watu waliokuwa wakiwaangalia walikuwa wakiwaonea wivu , isitoshe Frida alikuwa mwanamke mrembo na watu wengi katika mitaa hio walikuwa wakimjua kama mwanamke mgumu na wa hadhi ya juu.
“Naamini walichokifuata ni kitabu alichokuachia Dokta Genesha, huwa inanishangaza kuona watu wanawinda hiki kitabu ilihali hakuna katika dunia hii mtu anaeweza kutafsiri lugha yake”Aliongea Frida na kumfanya Hamza midomo kucheza.
“Unaonekana kujua mambo mengi mno , sishangai kwa jasusi kama wewe , ila niambie unadhani ni kweli hakuna mtu wa kuweza kutafsiri maandishi ya hiko kitabu?”
“Tofauti na wewe sidhani kama kuna mtu anaweza kukitafsiri , hata Dokta Genesha mwenyewe uwezo huo hana ndio maana alikupatia , haikuwa kwa bahati mbaya , wewe ndio mtu pekee ambae utaweza kutafsiri lugha yake, swala ambalo linaweza kuwa hatari zaidi”
“Kila mtu ananiambia ninaweza kutafsiri lakini bado nashindwa kuelewa natafsiri vipi lugha ambayo hakuna ambae anaijua?”Aliongea Hamza huku akikuna nywele zake.
“Hamza njia pekee ya kumjua Mzee ni kukitafsiri , hakuna namna nyingine , kwa maelezo ya dokta Genesha wewe pekee utaweza kukitafsiri baada ya kuujua uhalisia wako , namaanisha kumbukumbu za maisha yako ya nyumba ambazo umesahau?”
“Hey! Unaongea nini , kumbukumbu gani ambazo nimesahau , nina kumbukumbu zangu zote kasoro za wazazi wangu tu?”Aliongea Hamza na muda huo walikuwa washaanza kutembea , Frida alikuwa akiangalia saa yake.
“Kiihusu swala la kumbukumbu zako siwezi kusema sana , ila ni swala la ndoto ulioanza kuota, muda wangu umeisha , nilichokuitia ni kukukabidhi Mshumaa alioniachia Dokta Genesha”Aliongea Frida na palepale aliingiza mkono kwenye mkoba wake na kumpatia Hamza kiboksi.
“Mshumaa!!?”
“Ndio , Mshumaa huo ndio kitu ambacho Dokta Genesha ameniachia nikupatie , ni Mshumaa wa Nuru wa kuamsha ndoto , ukifika sehemu tulivu utaona vifaa vyake vyote vipo , hakikisha ikifika saa tano usiku unautumia ,ila ni hiari yako kuutumia katika huo muda , ndio njia ya wewe kutafsiri kitabu alichokuachia Dokta Genesha na ndio njia pekee ya kuujua uhalisia wako na kumfahamu Mzee, maelekezo yote namna ya kutumia yapo ndani”Aliongea na kumkabidhi Hamza ambae bado alikuwa na mshangao.
“Nilidhani ulisema mpaka tuingie kwenye chumba cha Nuru?”
“Maelezo ya Dokta Genesha wewe ndio mtu pekee unaejua chumba cha Nuru kilipo , lakini umesema hujui , njia pekee kwasasa nikutumia huo Mshumaa”Aliongea Frida.
“Umeongea sana Frida , lakini mpaka leo hii ni siku ya tatu tunaonana , sijui historia yako licha ya mambo ulionielezea , nakuamini vipi katika hili?”
“Huna haja ya kuniamini, Amini nafsi yako na kila unalopanga litafanikiwa , muda wangu ushaisha , endelea kutembea bila kuangalia nyuma”Aliongea na Hamza alikifiria kidogo na kisha aliendelea kutembea kama alivyosema na baada ya hatua kama isihirini na nane aliishia kukunja sura.
“Mateso mema Frida” Aliwaza Hamza peke yake.
Nyuma Frida hakuonekana tena , haikueleweka alipotelea wapi lakini watu walikuwa wakiendelea na shughuli zao na hawakuwa kabisa na habari na Hamza.
Kwa lugha nyepesi tukio ambalo sio la kawaida lilitokea nyuma ya Hamza lakini watu hawakuweza kuona kabisa wala kuhisi.
Hamza hakuona haja ya kupoteza muda , alijua ashamkasirisha Regina tayari kwa kuondoka bila ya kumpa maelekezo ya kutosha , hivyo aliona awahi kuelekea huko hata kama ni kwa kuchelewa.
Alipiga mahesabu kutoka Umoja Road mpaka Tegeta Kibaoni ingemchukua dakika nyingi kutembea wa mguu hivyo alihitaji usafiri , wakati akijishauri ni usafiri wa aina gani aliweza kusikia honi ya gari ambayo ilimpita na kwenda kusimama mbele yake.
Ilikuwa ni gari aina ya BMW X7 rangi nyekundu , kwa uelewa wa haraka wa Hamza aliona gari hio ni ya thamani na hakujua ni nani anapigiwa honi lakini mara baada ya kuchunguza aliona alikuwa peke yake.
Dakika ileile akijiuliza kama yeye ndio anaepigiwa honi , mlango wa gari ulifunguliwa na alitoka mwanamke mrembo katika ile gari alievalia suruali ya suti rangi ya ugoro hivi na viatu vya High Heels.
Alikuwa mrembo haswa na kumfanya hata Hamza mwili wake kumsisimka.
Mwanamke yule mrembo alionyesha ishara ya kuinua mkono akimwita Hamza na kitendo kile kilimfanya Hamza amkazie macho na palepale aliikumbuka sura hio ya kirembo , alikuwa ni Prisila Singano, Mrembo aliekutaa nae katika hoteli ya Dosam V wakati alivyofika kufanya usaili..
Hamza alitoa tabasamu , ukweli ni kwamba alikuwa akijiuliza mrembo huyo yupo wapi , kuna siku alitamani hata kumuuliza Regina lakini alihofia Regina anaweza kumfikiria vibaya.
Ila Hamza alijiuliza ilikuwaje mwanamke huyo alimuona maana walionana siku moja tu na pili yeye alikuwa amempa mgongo, inamaana hakuona sura yake kwani uelekeo aliokuwa akielekea na gari hio ndio ilipokuwa ikielekea.
Upande wa Prisila licha ya kusimamisha gari lakini alionekana kidogo kuwa na uso uliokuwa siriasi na aliingia ndani ya gari kabla hata Hamza hajamfikia.
Hamza alijiongeza na kuzuguka upande mwingine na kufungua mlango na kuingia ndani.
Gari ya mwanamke ni ya mwanamke tu , ilikuwa na harufu nzuri mno na ubaridi usiokera.
“Asante sana kwa Lift Prisila, habari za toka siku ile?”Aliongea Hamza huku akiweka muonekano wake wa kizembe.
“Unakumbuka jina langu?”Aliuliza Prisila huku akirudisha gari barabarani na muonekano wake uliimarika zaidi mara baada ya Hamza kutaja jina lake.
“Mwanaume yoyote ambae anaweza kusahau jina la mwanamke mrembo kama wewe atakuwa na matatizo”
“Kwa jinsi ulivyokuwa ukiniangalia nilijua umenisahau , ila nimeshangaa uko peke yako , yule mrembo yupo wapi?”Aliuliza Prisila huku akikaza macho barabarani.
“Mrembo gani?”
“Ulieshuka nae pale Asante Restaurant, nilikuwa ndani , nilitegemea mtaingia ila niliona mkiondoka , unadhani ningekufahamu kwa kuangalia mgongo wako tu?”Aliongea na kumfanya Hamza sasa kuelewa.
Prisila alikuwa na sauti nzuri mno na kila dakika ambayo mwanamke huyo alivyokuwa akiongea ndio mwili wake ulivyokuwa ukisisimka.
Hamza mara baada ya kusikia kauli hio sasa ndio alijua kumbe Prisila alimuona wakati akishuka na Frida pale mgahawani , ilileta maana kwani kulikuwa na watu wengi ndani ya mgahawa huo ndio maana Frida akasema watembee.
“Ni heshima kubwa kukumbukwa na mwanamke mrembo kama wewe?”
“Hakuna cha kushangaza kukumbuka , mimi ndio nilikukutanisha na Regina , si rahisi kusahau mpenzi feki wa bosi wangu , anyway hadhi yako imepanda pia , Dokta Frida sio mwanamke anaeweza kutangulizana na yoyote”
“Unamjua Dokta Frida?”Aliuliza Hamza na Prisila alitingisha kichwa.
“Baadhi ya watu wa kawaida wanaweza wasimfahamu
Frida , lakini katika ulimwengu wa wanataaluma wengi tunamfahamu , ndio maana nimeshangaa kukuona ukiwa na Frida ,Dokta namba moja wa taasisi ya Haliz, una siri gani ambayo hatuijui?”
“Siri gani tena?”Aliuliza Hamza na kuna kitu alishajua kuhusu Prisila ni mwanamke ambae yupo siriasi sana , ijapokuwa alionekana kama maneno yake yapo na viashiria vya urafiki lakini alionekana ni mwanamke anaehitaji majibu ya haraka.
“Kwa mtu yoyote aliewaona atasema mna ukaribu , kama sio wa kimapenzi, ni wa kindugu na kama sio wa kindugu basi pengine ni wa kikazi , lakini kwenye uhusiano wa kikazi ni asilimia chache sana uwezekano huo kuwepo , Frida ni mwanasayansi wewe ni mwanafunzi wa chuo taaluma mbili tofauti?”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa.
“Uliosema yote hayawezekani , mimi na Frida ni mtu na mfayakazi wake, ulivyotuaona nilikuwa nikipokea maagizo pale”Aliongea Hamza huku akicheka.
Prisila aliongeza umakini barabarani baada ya kufika makutano ya barabara ya Tegeta.
“Nimekupa lift ila hujanniambia unaelekea wapi?”Aliuliza na kumfanya Hamza kukuna kichwa. “Nilipaswa kwenda na bosi wangu kwenye kikao na mgeni wake ila nilipata dharula , sijui ni hoteli gani?”.
“Nini!, Dharula hio ni kukutana na Frida?, Regina akijua anakufukuza kazi?”
“Dharula ni dharula kwanini anifukuze kazi?”
“Sikulaumu , hujakaa muda mrefu na Regina , kama mpenzi feki kazi unayo?”Aliongea huku akicheka.
Prisila ndio mtu pekee ambae alikuwa akijua mahusiao yake na Regina ni feki , pengine ni kwasababu Prisila ndio aliweka tangazo mtandaoni na hata kumpokea Hamza katika usaili , kufikiria hilo Hamza shauku ilimjaa,haikuwa rahisi kwa Regina kumpatia kazi nyeti kama hio Prisila , ilimaanisha wawili hao lazima watakuwa na ukaribu.
Prisila kwa kutumia gari yake hio ya kisasa alipangusa katika kioo na kisha akapiga namba ya Linda na Hamza alitoa tabasamu na kuona huyu mwanamke ni jiniasi , amefanya kile ambacho alikuwa akiwazia amuombe afanye.
Hamza alikuwa ashapiga namba ya Regina kabla hata
hajaingia kwenye gari ya Priisila lakini haikupokelewa tena ilikatwa baada ya kuita kidogo,alijaribu na ya Linda hivyo hivyo lakini pia ilikatwa.
“Linda mpo hoteli gani?”
“Madam Prisila kwanini unauliza?”Sauti upande wa pili ilisikika . ilikuwa ya Linda na ilionyesha heshima.
“Nataka kujua kikao kinafanyikia wapi?” “Tupo Seaview hoteli”Aliongea.
“Okey!!”
Prisila palepale alikata simu na kumwangalia Hamza na Hamza alitabasamu.
“Uwezo wako wa kumsoma mtu ni wa juu , upo kama baba yako”
“Usifurahi sana , nimekusaidia hii inamaanisha una deni kwangu”
“Nipo tayari kulipa muda wowote Madam”Aliongea Hamza huku akitoa tabasamu la kizembe na Prisila alitoa kicheko hafifu.
“Nitakuacha Jogoo , nadhani itakuwa rahisi kupata usafiri wa kukufikisha Serena”
“Nitashukuru sana”
“Kama unanishukuru niambie ukweli mahusiano yako na Frida?”
“Ah..!” Hamza aliishia kushika pua yake na kujiambia inamaana bado swala la Frida linamsumbua huyu mwanamke , lakini hayo ni mambo yake binafsi kwanini anauliza sana.
“Ni kama nilivyosema”
“Okey!”Aliongea Prisila na muda huo walikuwa washafika tayari kituo cha Jogoo na Regina alisimamisha gari.
“Prisila asante sana kwa lift , nadhani tutaonana kazini?”Aliongea Hamza na Prisila alitingisha kichwa.
Hamza alitoka na kufunga kioo na Prisila aliondoa gari tataribu huku wengi wakiikodolea macho gari ile na ilipokumja kushoto waligeuza macho na kumwangalia Hamza.
Hamza kwa jinsi alivyoshushwa alijisikia vibaya kupanda daladala , lakini aliona pia daladala sio chaguo sahihi kama anataka awahi hivyo aliiita boda na kupanda , ili mbele kwa mbele achukue taksi itakayomfikisha Seaview.
Baada ya kupata pikipiki huku akihakikisha mzigo wake aliopewa na Frida upo salama aliondoka.
Nusu saa mbele wakati akiingia ndani ya hoteli ya Serena aliweza kuiona ile Lexus lx 600 ni alijua mara moja ni ya Regina maana ndio moja ya gari la kifahari ambalo lipo katika maegesho ya muda mfupi.
Hamza alijua kabisa Regina atakuwa aliendesha gari yake mwenyewe mpaka kuja hapo.
Hamza mara baada ya kufika alijipiga kichwani , hakujua Regina atakuwa katika floor ipi wala anakutana nae vipi na Hamza alisita huku akijiuliza au aende front desk kuuliza lakini kabla hata hajaamua cha kufanya aliweza kumuona Linda na hatimae Regina katika floor ya kwanza upande wa mhagawa na alijikuta akivuta pumzi ya ahueni na kisha alizipiga hatua kuwasogelea.
“Mkurugenzi , Linda , mbona mmekaa hapa , ndio manisubiri au?”Aliuliza Hamza.
Regina mara baada ya kumuona Hamza hakuweza kujizuia kukunja ndita na alimwangalia mara moja tu na kisha akashusha kichwa chake chini akijiweka bize na juisi yake huku akimpotezea, ilionekana alikuwa amekasirishwa na kitendo cha Hamza kuondoka bila kupata ruhusa yake kumuwahi mwanamke aliemsikia akiitwa Dokta Frida.
“Mkurugenzi alihitaji uwe mkalimani katika kikao chetu lakini ukaamua kuondoka kana kwamba jambo hili sio la muhimu , huhitajiki tena kwa kazi ya ukalimani hivyo unaweza kuondoka”Aliongea Linda.
“Kwanini niondoke, naamini hata bado hamjakutana na Mr Felini”Aliongea Hamza huku akiondoa wasiwasi wake na tabasamu.
“Tunaweza kuongea na Mr Felin kwa kingereza tu hata bila ya uwepo wako , na isitoshe kwa mavazi uliovaa ukikutana na mgeni wa heshima huyo ni kuleta matatizo tu”Aliongea Linda na kumfanya Hamza kuangalia mavazi yake.
“Kwanini unasema hivyo , sioni tatizo juu ya mavazi yangu”
“Mavazi gani hayo ambayo yashaanza kufubaa kwa kufuliwa mara nyingi, halafu staili yake ni ya kizamani kama vile upo karne ya ishirini”
“Hii ni Retro style, ina radha ya kifasheni ya upekee”Aliongea na Linda wakati alipokuwa akitaka kuendelea kujibishana nae aliacha mara baada ya kuona watu wakitokea upande wa lift.
“Mkurugenzi , Mr Felini na timu yake wale wanakuja”Aliongea Linda na mara baada ya Regina kusikia kauli hio aliweka glasi yake chini na kisha akasimama ili kwenda kuwapokea lakini kabla hata hajaanza kupiga hatua alimgeukia Hamza.
“Usinifuate unaweza kubakia hapa au ukiona hapakufai ondoka”
Hamza mara baada ya kusikia kauli ile alijihisi kama vile amekosewa na alijiambia inamaana mavazi yake yanaonekana sio ya thamani kiasi kwamba wanamnyanyapaa, Hamza aliangalia mavazi yake na aliona ya kawaida , isitoshe ni mavazi ambayo anahistoria nayo kubwa tu.
Lakini Hamza hakutaka kumuudhi Regina , ilionekana kabisa mwanamke huyo alikuwa akikipa kikao hicho thamani kubwa hivyo aliamua kukaa kusubiri.
Muda uleule Regina na Linda waliweza kuwafikia wazungu wale na kuwasalimia.
Felini alikuwa mrefu mwenye kifua kipana akiwa na nywele alizofunga kwa nyuma kama Halaand, alikuwa amevalia suti ya rangi ya bluu na nyekundu , shati jeupe ambalo lina kola ilionakshiwa kwa mua maua , jeans na sendo za ngozi.
Mtu wa aina hio na mavazi yake ilikuwa rahisi kumtofautisha na yule mzungu mwingine moja kwa moja hasa kwenye saa yake ya Patek Phillipe.
“Oh, you must be Miss Regina , I’ m really sorry , I took a break at the hotel and made you visit for a long time”Aliongea bwana huyu mzungu akiomba radhi kwa kumsubirisha Regina kwa muda mrefu wakati akiwa amepumzika, alionekana kuwa mkarimu.
Regina upande wake aliishia kutoa tabasamu hafifu , ijapokuwa lilioneksha hali ya ukaribisho lakini kwa ukauzu wake ni mara chache sana kumuona akitoa tabasamu la aina hio.
“Umekuwa kwenye ndege kwa masaa mengi hivyo ni haki yako kupata muda kidogo wa kupumzisha mwili
, nimekuwa na matarajjio makubwa juu ya kikao hiki , sasa hivi tayari ni saa sita muda wa chakula cha
mchana , mnaonaje tukipata chakula pamoja?”Aliongea Regina kwa kingereza
“Nimeshapata chakula tayari nilipokuwa kwenye ndege hivyo sitopata muda wa chakula cha mchana , napaswa kwenda Dubai baada ya hapa kutembelea matawi yetu na baada ya hapo nitaelekea Paris, ratiba yangu imebanana sana”Aliongea na jambo lile lilimshangaza Linda na Regina kwani
hawakutegemea kama Fellin angekaa Tanzania kwa muda mfupi sana.
Lakini ilikuwa sawa kwa mtu mbunifu maarufu kama huyo muda ulikuwa ni kitu cha thamani sana , maana ukiachana na kubuni mavazi ya kampuni lakini vilevile alikuwa akibuni mavazi yake mwenyewe kwa ajili ya maonyesho.
Kitendo cha mfanyabishara kama yeye kumualika mtu bize kama huyo kuja mpaka Tanzania ilikuwa ni heshima kubwa.
“Kama ni hivyo kwanini tusitafute sehemu na kukaa kwenda moja kwa moja kwenye maongezi?”Aliongea Linda.
“Yes”Aliongea na muda ule aligeuka nyuma kama kwamba kuna mtu mwingine alikuwa akimsubiria na kweli alinyanyua mkono mara baada ya kumuona mwanamke.
“Hey!, Salma , I am here..”
Mara baada ya kuona Fellin kuna mtu anamwita iliwafanya Linda na Regina kugeuka pia kuangalia mtu alieitwa Salma.
Alikuwa ni mwanamke mrembo haswa alievalia gauni lenye kola nyeusi la chui chui ambalo limebana sana , alikuwa amependeza mno kwa jinsi vazi hilo lilivyomkaa huku akivalia viatu vya skuna , alitembea kwa kujiamini mno.
Kwa jinsi alivyovalia unaweza kusema anaenda kwenye date lakini muonekano wake pamoja na
makeup ilimfanya kuwa na muonekano wa
kimaringo na kumfanya watu wengi wamwangalie.
“Salma Mohamed Salah!!”
Wasiwasi ulionekana katia macho ya Regina huku akimwemwesa midomo kwa kutaja jina hilo.
Hata kwa yule mwanamke mrembo mwenye kuchanganya rangi ya kiarabu na kiafrika alionekana kumfahamu Edna na alionyesha tabasamu lenye viashiria vya dharau.
“Regina na wewe upo hapa kwa ajili ya ushirikiano wa kibiashara na Fellini?, Nadhani nikuambie tu kwamba umechelewa na utaishia kukata tamaa”Aliongea.
“Salma unafahamiana na Miss Regina?”
“Ndio , tumesoma shule moja High school , baada ya kumaliza kila mtu alichukua uelekeo wake , hatujawahi kuonana kuanzia hapo mpaka wote tulipokuja kuwa wafanyabiashara na kuingia kwenye ushindani”Aliongea Salma.
“Basi vizuri , kama mnafahamina nadhani ni vizuri tukianza kuongea kuhusu ushirikiano , kuna mgahawa hapa hivyo haina haja ya kutafuta eneo lingine”Aliongea na palepale mzungu yule pamoja na msaidizi wake walisogea upande wa mgahawa.
Hamza mara baada ya kuona kundi hilo la watu limesogea karibu na yeye hakutaka kumkasirisha Regia hivyo hakuwasalimia kabisa na kula buyu.
Ukweli ni kwamba Linda na Regina hawakuwa na time nae kabisa na Regina muda huo mara baada ya kuona Salma alikuwa na mawasiliano na Fellini alijua kabisa mazungumzo yashaingia doa , mshindani wake mkubwa wa kibiashara kwa ukanda Afrika mashariki na kati ni kampuni ya Salah, lakini hata hivyo hakuwa na jinsi na kukubali kupitia changamoto hio, angejua kampuni ya Salah ilikuwa
ikitaka pia ushirikiano na Fellini pengine angejiandaa zaidi, kingine ambacho kilimshangaza Regina ni kwamba Salma alikuwa akisimamia kampuni ya mitindo upande wa China lakini ghafla anaonekana mbele yake, moja kwa moja alijua lazima kampuni imempa kazi ya kuhakikisha dili la ushirikano na Zara liafanikiwa kwa namna yoyote.
Wote kwa pamoja walitafuta siti zao na sasa kukawa na makundi matatu yanayowakilisha kampuni tatu tofauti , Regina akiwakilisha Dosam , Salma akiwakilisha Salah na Fellini akiwakilisha Zara. “Mr Fellini , we have an appointment to meet privately , joining of Salah family’s representative , I’ m afraid, is not appropriate”Aliongea Regina akimaanisha kwamba walikuwa na ahadi ya kukutana lakini kuunganisha na familia ya Salah , sio sawa.
Upande wa Felini alipewa Kiko ya kuvutia sigara na kuwasha na kisha akavuta moshi huku akiwa na tabasamu lenye utulivu.
“Usiwe na wasiwasi Miss Regina , nilikutana na
Salma kwenye maonyesho ya wiki ya Fasheni jijini New York na kugusia swala la kibiashara , najua familia yake ndio wamiliki wa kampuni kubwa ya mavazi ya Salah kutoka Uturuki , lakini sina mahusiano yoyote na yeye zaidi ya maswala ya kibiashara, yoyote kati yenu ambae atakuja na vipengele pamoja na ofa nzuri ya ushirikiano wa kibiashara sitokuwa na upendeleo wa kuchagua , kwa haki na uwazi nitachagua upande sahihi”
“Hehe.. Regina unaogopa nini, nakukumbusha tu familia yetu ndio wa kwanza kabisa kuwa wakala wa bidhaa za kifahari kutoka makampuni makubwa kabla yenu, Vigezo vyake ni vingi sana , sisi ni tofauti na kampuni yeu ambayo ipo kila sekta”Aliongea Salma.
“Kuwa na vigezo vingi haimaanishi chochote , nakubali nyie ndio mlianza kuleta mavazi ya kimitndo Tanzania lakini baada ya kampuni yetu kuingia katika biashara hio tuliwapita miaka mingi tu , Zara ni kampuni ambayo malengo yao ni
kuendeleza utawala wao wa kimavazi katika kila soko , unadhani ni rahisi kuingia mkataba na kampuni ambayo inalega lega sokoni”Aliongea Regina.
“Una mawazo ya kimasikini , hivi unadhani kujipanua kwenu kusiko na malengo ndio uwezo wa kampuni , sisi kama kampuni sio fasheni tu tunayoheshimu bali na utamaduni pia unaoendana na mavazi, kampuni yetu inaendeshwa kwa misingi ya kisera ilioweka tokea kuanzishwa kwake, hatuwezi kufanya kila biashara ambayo tunaona tunaweza kupata faida , kwetu sisi hela sio malengo bali ni kukuza utamaduni, tunataka ushirikiano na Fellini kwasababu malengo yetu ni kuhakikisha tunateka soko la fasheni inayoendana na utamaduni wetu wa kiafrika”aliongea Salma kwa kingereza akimjibu
Regina na Felini aliweza kusikia majibishano yao . “Salma yupo sahihi , kampuni ya Zara haingii katika ushirikano wa kibiashara na kampuni ambayo ina Asset nyingi wala thamani ya hisa sokoni, tunajua fika uchumi wa kampuni ni moja ya kigezo lakini kwa vyovyote vile tunazingatia kampuni ambayo ina sera zinazoendana na mazingira ya jamii husika”Aliongea Fellini.
“Mr Fellini nakiri kwamba katika biashara ya mavazi , kampuni ya Salah ina uzoefu mkubwa na taaluma , lakini tupo na nia ya dhati pamoja na ari ya kujiamini katika kuifanya kampuni ya Zara kuuza sana katika soko la Afrika”Aliongea lakini kauli ile ilimfanya Fellini kukunja ndita.
“Miss Regina , naomba uniwie radhi kama nitatoka nje ya mpaka , ukweli ni kwamba nimejaribu kufanya uchunguzi kiasi kuhusu wewe na nikiri nakuheshimu sana kwasabau upo katika kundi adimu la watu wenye akili nyingi duniani , lakini hata hivyo nimefuatilia malengo ya kampuni yenu sera yenu kubwa ni kujipanua na kuhakikisha mnaingiza faida kwa kiasi kikubwa , hivyo mbinu zenu za kibiashara
zipo kwa ajili ya kutengeneza hela..”
Regina alishangazwa na kauli za Felllini na alianza kujisikia wasiwasi katika moyo wake.
“Kama nilivyosema sera ya kampuni yetu ni kutamfuta mshirika ambae anatulewa ili kusambaza tamaduni zetu, tunachouza sokoni sio bidhaa tu bali ni wazo , huduma na ustaarabu ulioendelea katika jamii”
“Mr Fellin naelewa unachosema , sitoingilia mapendekzo ambayo mtakuwa mnatoa kama kampuni , ninachotaka kusema ni kwamba tunao uwezo wa kuwafikia wateja kwa haraka na kwa wingi zaidi kuliko kampuni yoyote ndani ya Afrika mashariki na kati”
“A nouveu riche is a nouveu riche , Regina huelewi tu , anachotafuta Mr Felleni ni mshirika wa kibiashara na sio muuzaji, maana yake ni kwamba lazima na wewe kama kampuni ushiriki katika mawazo ya ubunifu wa bidhaa, michoro , aina ya kitambaa na eneo la uzalishaji , ukishajua hatua zote hizo inamaana utaelewa na kilichokusudiwa katika bidhaa na itakuwa rahisi kumfikia mteja na kumfanya anunue .’listen up , its not the consumer its customer” Kulikuwa na kila ishara ya furaha katika uso wa Mr Fellini mara baada ya kusikia msemo aliomalizia nao Salma.
“Yes , Miss Salma is right , As expected of a talented girl who graduated from parsons school of Design , My analysis is very thorough , that is what I mean”Aliongea akimaanisha kama alivyotegemea kwa msichana mwenye kipaji aliemaliza chuo cha ubunifu cha Parson , uchambuzi wake ni yakinifu.
Salma mara baada ya kusifiwa alifurahi mno meno yote nje na alimwangalia Regina kwa tabasamu la uchokozi.
“Regina jikatie tu tamaa , wewe endelea na biashara ya kununua ardhi , kujenga viwanda na kununua hisa , mambo ya fasheni hayakufiti kabisa”
Kwa jinsi alivyoongea ni kama vile alikuwa akishindana na Regina au alikuwa na kinyongo cha muda mrefu.
Regina aliishia kubaki kimya na alimwemwesa lips zake , huku pembeni Linda akiwa na uso uliopauka kwa hasira.
Comments