Regina alienda mbali na kukumbuka aligombana na Hamza kwa kutotaka kutupa mavazi yake , alishindwa kuzuia hisia mbaya zilizoanza kumvaa na kujiambia kama kweli anachosema Fellini ni kweli basi mavazi hayo ya thamani si yatamfanya aonekane mjinga na mshamba.
“Mr Fellini macho yako yatakuwa yanakudanganya , haya mavazi aliovaa unaweza kuyakuta kila mkoa ndani ya Tanzania yanauzwa”Aliongea Regina kuepusha kuabika.
“Msiniambie hakuna ambae anaona uzuri wa mavazi aliovaa Mr Hamza pamoja na pensi yake?”Aliongea huku akiwaangalia mmoja mmoja kana kwamba anaomba kuungwa mkono.
Lakini wote walitingisha vichwa vyao kukataa , hakuna cha maana kwenye hayo mavazi zaidi ya uchakavu tu”
“Nyie watu hamjui kabisa , nadhani kwasababu sio mafundi, katika ulimwengu wa kifundi utaalamu wa juu zaidi ni kutengeneza vazi ambalo unao uwezo wa kulirudisha upya kwa mchakato mwepesi sana na ukauza sokoni kwa bei ileile”Aliongea mzungu huyo lakini hakuna hata mmoja ambae alielewa anachomaanisha, hata Salma aliesomea Person chuo namba moja cha mitindo kutoka Marekani hakuelewa.
SEHEMU YA 31.
Regina mara baada ya kuona haelewi alichomaanisha Fellini aliomba aeleze kwa lugha nyepesi, bado hakuwa amekubali nguo alizovaa Hamza ni za bei ya juu.
“Mr Fellini unaonaje ukituelezea kwa urahisi tupate kuelewa?”Aliongea na Fellini alimwangalia Hamza.
“Mr Hamza naomba ruhusa yako kushika nguo zako”
“Hakuna shida , ungeniambia vizuri ningekuelewa tokea mwanzo”Aliongea Hamza huku akicheka.
“Salma nadhani utakuwa unajua ni malighafi za nguo za namna gani zimetumika”Aliongea akimpa ishara Salma kusogea karibu na yeye pia alishika lakini dakika ileile muonekano wake ulibadiika.
“Noble family material!!?”Aliongea Salma huku akishangaa.
“Correct, hii ni aina ya kitambaa cha SCUBA ambacho kiliongezewa ubora kwa mara ya kwanza nchini Ubelgiji na baadae kikawa kitambaa namba mmoja kinachotumiwa ndani ya Savile , ni aina ya kitambaa ambacho mchakato wa kukitengeza kuwa mgumu na ndio maana sio swala la hela tu kununua kitambaa hiki, sasa unadhani nguo yoyote ambayo imetengenezwa na aina hii ya kitambaa inaweza kuwa ya kawaida?”
Regina mara baada ya kusikia kauli hio alishindwa kujizuia na kusogea na yeye ili kugusa kitambaa hicho kwa umakini , ijapokuwa alishawahi kugusa nguo za Hamza mwanzo lakini ile kejeli juu ya nguo hizo hakuweza kuona kitu special.
Lakini muda huo alivyogusa nguo hio ki uchunguzi ndio sasa anagundua ni kweli kitambaa chake hakikuwa cha kawaida kabisa.
“Mnajua nini kimeongezewa upande wa hio michirizi ya pensi kushoto na kulia?, angalia kwa pembeni utaona ni kama inabadilika rangi kutokana na mwanga?”Aliuliza Fellini na wanawake wote waliangalia kwa kutumia angle ya macho na kuona ni kweli rangi ya nguo inabadilika, lakini hakuna ambae alikuwa na majibu.
“Ngoja niwaambie , ni nyuzi nyuzi za madini ya
Platinum kutoka Afrika ya kusini, hii inafanya kitambaa chake kuwa cha thamani ya juu mno na adimu dunia nzima, gharama ya uzalishaji wa kutengeneza suruali ni Euro laki moja”Aliongea
Euro laki moja inamaana Hamza amevaa nguo ya thamani ya milioni mia tatu za kitanzania , Regina , Linda na Salma mara baada ya kusikia kauli hio walishindwa hata kupumua vizuri.
“Hey usiongee kwa nguvu , unataka watu wasikie na kuniwinda wanivue nguo nitembee uchi”Aliongea Hamza akimwambia Fellini.
Fellini alijikuta akigundua alikuwa na mzuka kiasi kwamba alikuwa akiongea kwa sauti na aliinamisha kichwa kuonyesha ishara ya kuomba radhi.
“Hilo ni la kwanza , kinachofuata na kutofautisha hizi nguo ni aina yake ya ushonaji”Aliongea na kisha alishika kola ya tisheti ya Hamza na kuinyanyua kwa juu.
“Nadhani mshawahi kusikia teknolojia ya Hermes ya ushonaji wa nguo za leather wanatuia SDD-
stilt method , hii njia ya ushonaji mara nyingi inatumia sindano mbili kwa wakati mmoja na kufanya bidhaa yoyote ya kampuni ya Hermes ya Leather kuwa imara sana na kupendeza kwa wakati mmoja
Ukweli ni kwamba kati ya washonaji wengi , kuna mbinu ya kale ambayyo ipo karibu kupotea , inaitwa Concealment Saddle needle techinique, hii ndio mbinu ambayo Master George anatumia , lakini mpaka leo hii hata yeye mwenyewe hajabobea kuitumia kwa asilimia mia moja , mbinu hii inakupa nafasi ya kutumia nyuzi tatu katika uzi mmoja, hivyo kufanya nguo kuwa imara na kudumu kwa muda mrefu”Aliongea na Regina na Salma walisogea karibu kuangalia namna ya ushonaji ulivyokaa na kwa kuangalia tu waligundua mashine ya cherehani ni ngumu sana kufanikisha ushonaji huo.
“Hakuna ushonaji wa aina yoyote duniani unaoifikia hii mbinu , cha kufurahisha zaidi ukitaka kuifumua nguo yote kwa urahisi unagusa sehemu moja na unatoa nyuzi zote na nguo inarudi katika kitambaa na baada ya hapo inaweza kufanyiwa maboresho na kisha kurudishwa katika muonekano wake mpya”
Regina aliishia kukosa hiari na kuamini kabisa maamuzi yake ya wakati ule hayakuwa sahihi , lakini aliona pia Hamza alikuwa ni mshenzi sana , yaani mtu anavaa nguo ya thamani kubwa namna hio lakini anajifanyisha ni masikini tena mbaya zaidi anajifanyisha mtu anaependa sana hela.
“Hamza kwahio ni kweli unafahamiana na huyo Master Alec , kwanini hukusema?”Aliuliza Regina.
“Umesahau nilikuambia nguo hizi nilipewa na rafiki yangu , halafu sio kama uliniuliza ni rafiki gani?”Aliongea na kumfanya Regina kumwemwesa midomo , ilikuwa ni kweli hakuuliza ni rafiki gani.
“Wewe ni dereva tu , kwanini nguo zako zitengenezwe na mafundi wanaoshonea nguo wafalme , au umeziiba ndio maana umeshindwa kujua thamani yake?”Aliongea Salma.
Fellini mara baada ya kusikia kauli hio ni kama hata yeye wazo hilo lilimwingia , kwani ni ngumu mtanzania kama Hamza kuwa na nguo ambayo imetengenezwa na Alec , hata kama Hamza alionekana kuchanganya damu ya kizungu lakini bado ilikuwa ni ngumu kuamini, isitoshe swala la kuchanganya damu halikuwa la kushangaza sana , Waafrika wengi walikuwa wanaanza kupoteza rangi yao halisi kutokana na kuzaa na watu weupe, hivyo kumuona mtu mwenye muonekano wa Hamza sio swaa la kushangaza.
Leo hii unaweza kukuta watoto wa mtaani wenye muonekano wa kizungu na kiafrika au waarabu na waafrika.
“Sidhani ni sahihi kusema hivyo , maana ninazo nguo nyingine nyingi tu ambazo ametengeneza Alec?”
“Nani anajua , pengine uliiba furushi la nguo , kama una urafiki na mtu mkubwa kama huyo inakuwaje leo hii upo hapa Tanzanina , tena Dereva , si ulitakiwa uwe Ulaya huko?”Aliuliza Salma , hakutaka kukubali kabisa.
“Kwahio vipi msaidizi wangu kuwa dereva , kwahio siku hizi tunabaguana kwasababu ya mavazi?”Aliongea Regina , hakutaka kuona Salma anapandisha mdomo mbele ya Hamza.
“Regina haijalishi unachoongea , tena nimezidi kuwa na mashaka , kuna namna mmepanga bada ya kuhisi hamuwezi kushidana na kampuni yetu , hivyo mnacheza kamchezo ka kumfanya Fellini kukubaliana na nyie”
“Unaumiza kichwa chako bure kwa kufikiria sana , kama nilivyosema , sina mpango wa kushirikiana tena na Zara, tuondokeni”Aliongea Regina lakini muda ambao Regina alianza kupiga hatua kuondoka hapo alizuiwa na Hamza.
“Hamza , unafanya nini?”
“Msaidizi wako nimeitwa mwizi , unadhani tunaweza kuondoka hivi hivi?”Aliongea. “Kwahio wewe sio mwizi?”Aliuliza Salma.
“Mr Hamza , je una ushahidi wowote wa kutuonyesha hizi nguo ni za kwako au unafahamiana na Master Goerge?”Aliuliza Fellini. “Sasa hivi ni saa saba kasoro hivyo itakuwa ni Asubuhi London , nadhani Mzee Roboti muda huu atakuwa macho , ninaweza kumpigia simu”Aliongea
“Nini , unasema una namba ya Master?, wakati hata mimi sina”Aliongea Fellini kwa mshituko.
“Unaongea ujinga , kama hakutengenezei nguo , kwanini uwe na namba yake”Aliongea na kumfanya Fellini kukakamaa mwili , alikuwa akijisikia vibaya kana kwamba ameona mende.
Regina na Linda wote walikuwa na hali ya shauku na matarajio kwa wakati mmoja , upande wa Salma alikuwa na wasiwasi mno.
Hamza alitaka kutumia simu yake kupiga lakini alisahau kwamba ni kimeo hivyo alimwangalia Regina.
“Mkurugenzi niazime simu yako , siwezi kupiga kimataifa kupitia simu yangu”Aliongea na Regina alitoa Iphone yake na kumkabidhi Hamza na palepale aliingiza namba alizokariri na kupiga na ndani ya dakika chache tu simu ilipokelewa baada ya kuita.
“Who is it …”Sauti ya kingereza ya kizee upande wa pili ilisikika , ilikuwa nzito mno na lafudhi ya London na Hamza alitoa tabasamu mara baada ya kutambua sauti hio ambayo hajaisikia muda mrefu.
“Elmo , its me..”Aliongea Hamza upande wa pili kulikuwa na kimya kama cha sekude arobaini hivi.
“Do you finally rembember this lowly person!?”Sauti upande wa pili ilijibu na ndio dakika ileile Hamza aliweka simu aweze kusikia yeye tu ili wasije kusikia jina ambalo Alec anaweza kumuita.
Hamza asingejua namna ya kujieleza kama wangesikia Alec anamwita kwa cheo chake cha heshima.
“Mzee Roboti sio kama nimekusahau , mpaka sasa kila nilipokuwa ikivaa mavazi ulionipa kama zawadi nakukumbuka , ni miaka mingi lakini nguo zako bado nazivaa”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.
“Niheshima kwangu kufanya kazi na wewe na nilikuwa nikitegemea tuendelee kufanya kazi pamoja ila umepotea , nakumbuka wakati nakutengenezea hizo nguo ilikuwa ni miaka mitatu iliopita”Aliongea mzee huyo akionekana kama vile analalamika.
“Okey , Okey mzee nilikupa likizo kwanza ili ujali afya yako , lakini kwasababu unaonekana kuwa tayari kunitengenezea tena nguo basi nakupa ruhusa , nitakutumia anuani ya ninapoishi kwasasa , nadhani unajua ninachopendelea”
“Kweli !, nipo tayari kufahamu sehemu unayoishi kwasasa , najua umeondoka bila kuaga hivyo itakuwa siri yetu kama tunawasiliana”
“Mzee japo umezeeka lakini akili yako inafanya kazi vizuri , ninakuamini ndio maana nimeamua kukupigia”Aliongea Hamza huku akicheka, alikuwa akiongea kingereza na lafudhi yake ni kama vile amekulia jijini London.
“Mimi kama kijakazi wako lazima niwe na akili japo kidogo , vinginevyo nitaweza vipi kutimiza wajibu wangu wa kukuhudumia?”Aliongea.
“Sawa sawa , tuachane na hayo kwanza , nimekupigia leo kwasababu kuna baadhi ya mambo nataka unisaidie kuyaweka sawa”Aliongea Hamza.
“Usisite kabisa kuniambia , nipo tayari kufanya chochote , hata kama nikuhatarisha maisha yangu”
“Sio swala kubwa sana , usiwe na wasiwasi , je kuna mwanaume anaefahaika kwa jina la Fellini kati ya wanafunzi wako ?"Aliuliza Hamza na wakati huo alikuwa akimwangalia Fellini.
Muda huo Fellini uso wake wa kizungu ulikuwa umepauka na kulikuwa na viashiria vya jasho katika paji la uso wake , alikuwa akijiuliza kama kweli
Hamza aliekuwa akiongea nae ni Master Alec , Hamza mwenyewe atakuwa ni nani
Salma na yeye alikuwa aking’ata lipsi zake huku akiwa amekunja ngumi , alionekana kuwa na wasiwasi mno.
“Mkurugenzi ni kweli anafahamiana na huyo mtu mzito , mbona naona kama anatufanyia magizo?”Aliuliza Linda.
Upande wa Regina yeye alikuwa katika kuwaza na aliishia kutingisha kichwa ,huku akishindwa kuongea neno, alijiambia atajua baada ya matokeo.
Lakini muda huo mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda kasi mno , alijiambia kama ni kweli basi koneksheni ya Hamza ni kubwa mno kama vile yupo ndotoni.
“Felini!?, Oh nimemkumbuka sasa , Fellini ni mwanafunzi aliekuja akiwa mdogo katika duka langu kwa ajili ya kujifunza kushona, lakini hakuweza kudumu sana maana moyo wake ulikuwa haujatulia sehemu moja , ijapokuwa alikuwa na kipaji lakini hakuwa na Ari ya kuja kuwa mshonaji mkubwa hivyo aliondoka , kwanini unamuulizia , Mshonaji kama Fellini ni wa daraja la pili na hana hadhi ya kuandaa nguo zako”Aliongea.
“Hamna mzee, sijakutana nae kwa ajili ya kunitegneenea nguo , nimekutana nae kwa bahati mbaya na ameweza kugundua maazi yangu wewe ndio umeyatengeneza, ila haamini amesema mimi mwizi”
“Nini!!, anakitafuta kifo , tafadhari bwana wangu naomba usiwe na hasira juu ya tabia ya Fellini , nitamwambia Eric amfukuze , mtu kama yeye hawezi kutuingiza kwenye mgogoro na wewe , kama bado hutoridhika unaweza kumfanya chochote nitaandaa maelezo”Aliongea na kumfanya Hamza kutamani kucheka kutokana na namna Alec alivyopaniki.
“Ndio maana nakuita Mzee Roboti unaishi kikanuni sana , haina haja ya kupaniki , sina mpango wa kumfanya chochote , nitampatia simu uongee nae , ninachotaka ni wewe kumthibitishia tunafahamiana , usiongee zaidi kuhusu mimi , nadhani umenielewa”Upande wa pili kimya kilitawala.
“Sawa sawa , najua nini chakufanya”Alijibu na Hamza alimpatia Fellini simu.
Upande wa Fellini mikono ilikuwa ikimtetemeka , ilimchukua sekunde kadhaa mpaka kupokea simu hio kutoka kwenye mikono ya Hamza.
Hakuwahi kuongea na mwalimu wake huyo kwa zaidi ya muongo mmoja,sasa wazo la kuona kwamba anakwenda kuongea na mwalimu wake huyo mtu mzito sana ndio maana alikuwa na hofu.
“Nice to talk to you , Master Alec”Aliongea Fellini kwa kitetemeshi lakini upande wa pili hakukuwa na jibu.
“I heard from Eric that you’re now quite famous outside ?”Sauti upande wa pili iliongea na palepale Fellini ni kama vigoti vinamlainika
“Hapana Master ,Mimi ni kivuli cha Sir Eric tu , nimekosea Master naomba radhi”Aliongea na upande wa pili ilionyesha ni kiasi gani Alec alikuwa amekasirika.
Muonekano aliokuwa nao Fellini ulimfanya Salma ambae alikuwa pembeni kushangaa mo , Mbobezi maarufu wa ulimwengu wa fasheni amebadilika
na kuwa kama piritoni hivyo kwa kuongea na mtu kwenye simu
Regina na Linda na wao walikuwa sasa washaamini mtu ambae anaongea na Fellini ni kweli ni huyo Alec mweye hadhi ya juu.
“Sikiliza wewe mtoto , mtu uliekutaa nae huwezi kumwita mwizi , ukimfaya akasirike basi hutonilaumu tukikutoa kwenye circle yetu na umaarufu wako kupotea , nadhani unajua ninachomaanisha”
Fellini alikuwa na hofu mno , alikuwa akijua maneno ya Alec sio ya kumuogopesha tu , ukweli ni kwamba kauli yake moja tu hawezi kuwa na umaarufu aliokuwa nao , alijua nguvu iliokuwa nyuma katika fasheni ya mavazi ilitawaliwa na watu kama Alec.
“Master usiwe na wasiwasi , najua nini napaswa kufanya”Aliongea.
“Mrudishie simu”
Fellini alimwangalia Hamza kama vile ni kiongozi wa heshima na jambo hilo liliwashangaza zaidi Regina , Linda na msaidizi wa Alec, upande wa Salma muonekano wake ulikuwa mbaya mno ,
maana kile kinachoendelea ni kama matusi kwake
.
Hamza aliongea na Alec kwa dakika kama mbili hivi na kisha alikata simu na kumrudishia Regina.
“Sasa nadhani kila mtu amethibitisha nguo hizi ni zangu , Mkurugenzi , tunaweza kuondoka sasa”Aliongea Hamza.
Regina alijihisi ni kama yupo ndotoni na aliishia kutingisha kichwa huku akimwangalia Hamza kwa wasiwasi.
Upande wa Fellini aliona haiwezi kuwa nzuri kama atamuacha Hamza aondoke akiwa na kinyongo.
“Mr Hamza nakiri ilikuwa ni ujinga wangu , hivyo naomba msamaha wako , kama ningejua na wewe ni mmoja ya watu wa kampuni ya Dosam nisingesita kufanya nao ushirikiano, naomba unipe nafasi ya kurekebisha makosa , nipo tayari kampuni ya Zara kushirikiana na Dosam Group” “Mr Fellini huwezi kufanya hivi , tushakubaliana kampiuni zetu zinaenda kushirikiana”Aliongea Salma kwa hasira.
“Miss Salma, hakuna mkataba wowote tuliosaini kati yetu , hivyo siwezi kusema kuna makubaliano ya kufanya kazi pamoja , baada ya kufikiria kwa kina nimeona kampuni ya Dosam inaweza kukuza hadhi yetu”
“Kwanini unaenda kinyume na maneno yako?” Aliongea Salma huku akiona swala hilo ni kama udhalilishaji, lakini Fellini alimpotezea kabisa.
“Kama nilivyokwisha kujitambulisha, mimi ni msaidizi tu , unapaswa kuongea na Mkurugenzi akikubali sina neno”Aliongea Hamza.
“Miss Regina naomba mazungumzo yetu yaanze upya , naomba kuona mipango yenu”Aliongea mara baada ya kupata ruhusa.
Upande wa Regina alikuwa asharudi katika hali ya kawaida akiuzima mshangao wake na alimwangalia
Salma kwa macho ya uchokozi na palepale alichukua mkataba ambao ulikuwa umeshikiliwa na Linda na kuuchana mbele yake.
“Cooperation is fine , but we need to redesign the cooperation proposal”Aliongea akimaanisha ushirikiano hakuna shida lakini wataenda kuandaa upya vipengele.
Fellini aliishia kuangalia chini , kwa wakati huo Regina alikuwa na Upperhand , hivyo ni kama yeye ndio anaomba ushirikiano na kampuni ya Dosam na sio Regina kumuomba yeye ushirikiano., Regina alishaliona hilo hivyo alitaka kubadilisha vipengele ili kuinufaisha kampuni yake.
“Hakuna shida, nipo tayari kusubiri kwa siku kadhaa”Aliongea Fellini , hakuwa yule mwenye ratiba iliobanana tena.
Hamza alimwangalia Regina kwa macho ya kuridhika , alimuona Regina kama mwanamke ambae akili yake inafanya kazi kuendana na hali kwa haraka , hali ya mazungumzo ya kibiashara imebadilika hivyo hakutaka kwenda na mkataba uleule.alitaka kubadilisha mbinu ili kujinufaisha.kitaalamu alimuona Regina kama mwanamke ambae sio mzembe kabisa likija swala la fursa.
Kwa vyovyote vile Kampuni ya Zara lazima ishirikiane na Dosam kama Fellini anataka kulinda hadhi yake katika ulimwengu wa fasheni.
Fellinni aliwasindikiza kabisa Hamza na Regina mpaka kwenye gari yao na kuwafungulia mlango huku akiwa na heshima kubwa .
Upande wa Salma alimwangalia Hamza kwa macho yenye ukali mno na kisha aliondoka bila hata ya kuaga.
“Mr Fellini huna haja ya kuwa hivi , ijapokuwa leo sijafurahishwa na namna tulivyoanza lakini nimeridhika na matokeo”Aliongea Regina.
“Ili Mradi Mkurugenzi umeridhika , hakuna tatizo kabisa , natarajia kufanya kazi na Dosam kwa miaka mingi”
“Kama hakuna lingine tunaondoka”Aliongea Hamza.
“Mr Hamza tafadhari subiri kidogo , najua nimekukosea leo , naomba uniwie radhi , kama kuna mahali ambapo hujaridhika tafadhari naomba uniambie nitarekebisha”
“Usiwe na wasiwasi , ili mradi kila kitu kitaenda sawa mimi sina shida , nitakusaidia pia kukupigia chepuo kwa Alec “
“Thank you so much, you are so magnanimous”Aliongea na muda huo Hamza alikumbuka aliachaga nguo kwenye hilo gari.
“Mkurugenzi , hivi zile nguo zangu bado zipo humu?”
Regina muonekano wake ulikuwa na hali ya kukosa utulivu na alinyoosha mkono nyuma na kutoa ule mfuko , mwanzoni alitumia nguo hizo kumdharau Hamza lakini dakika chache zilizopita zimegeuka kuwa hazina.
Hamza alichomoa shati kutoka kwenye mfuko huo na alivyolinusa lilinuka jasho kali mpaka akakunja sura, lakini katika macho ya Fellini alionekana kuwa katika mchangao.
“Unaweza kuchukua hizi nguo , chukulia kama zawadi kutoka kwangu kwa kuingia makubaliano ya kibiashara”Aliongea Hamza na kumkabidhi mfuko wote Fellini aliepokea kwa mikono miwili.
Hamza hakuwa na wasiwasi na nguo tena , alishaahidiana na Alec angeletewa nguo nyingine mpya
Mtu yoyote angeona shati ambalo Hamza amemkabidhi Mzungu Fellini wangesema huyo mzungu ni kichaa.
“Mr Hamza asante sana kwa ukarimu wako, nitaweka nguo hizi sehemu salama kabisa nikirudi” Aliongea Fellini, alipanga kuzifanya nguo hizo kama sehemu ya maonyesho ofisini kwake , ili kutukuza uwezo wa Master Alec katika swala zima la ushonaji.
Isitoshe Master Alec alikuwa ametengeneza kwenye maisha yake nguo nyingi sana lakini sio watu wengi ambao washawahi kuona nguo yenye muonekano wa kawaida kama hio lakini ya thamani , Rare things are priceless.Aliwaza Alec.
Kwa furaha mazungumzo yao yaliisha hivyo na Hamza aliendesha gari kurudi nyumbani.
Linda ambae alifika na gari yake aliweza kuangalia gari ya Regina ikitokomea huku akiwa na muonekano usioelezeka , katika macho yake kulikuwa na hali flani hivi ya kukata tamaa.
******
Upande mwingine ndani ya jiji la London ilikuwa ni asubuhi karibia maeneo yote , Uingereza haikuwa kama nchi ya Marekani ambayo ina Time Zone zaidi ya nne, pengine ni kutokana na udogo wa kijiografia wa nchi hii yenye maendeleo makubwa sana katika nyanja zote.
Katika mtaa wa Savile Row mwanaume mzungu mzee hivi mwenye nywele nyeupe pamoja na miwani alionekana akishuka katika ngazi katika moja ya jengo kwa kukimbia, alikuwa amevalia shati jeupe na Vest nyeusi.
“Erice, John”Mwanaume yule aliita kwa nguvu.
Dakika hio hio mwanaume bonge mzungu alijitokeza akiwa ameambatana na mwanaume mwingine kimbau mbau ,wote walionekana katika
umri wa iaka hamsini hivi na walikuwa wameshikilia vitambaa.
“Mwalimu , una maagizo yoyote”Yule bonge ndio aliitwa Erice na ndio alieuliza.
“Wote nyie acheni kazi zenu zote kwa sasa na mnifuate , nahitaji kutengeneza nguo nyingi suti na suruali”
“Mwalimu , bado hatujamaliza kutengeneza nguo za Mfalme wa Hispania na Prince wa Wales, sidhani kama tunaweza kukusaidia”Aliongea John.
“King or Prince let them all wait, For the past week, we have served one lord” Aliongea akimaanisha Mfalme au mwana mfalme wote wasubiri. kwani kwa wiki za nyuma walikuwa wakihudumia bwana mmoja tu.
“Mwalimu unamzungumzia bwana gani?”Erice aliuliza.
“Seraph”Aliongea Alec huku akigusa gusa kifua chake.
Erice na John mara baada ya kusikia jina hilo moja kwa moja walielewa ni mtu gani anaelengwa na wote kwa pamoja walikakamaa huku wakitamka kwa juu “Divine Wrath”
Comments