Reader Settings

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Internation airport, Dar es Salam

Saa 9:30 mchana

Nguvu za injini ga Qatar Airways zilitulia polepole mlango wa ndege ukafunguli wa na kushaku ka talatibu Abılıa to kuanza

Miongo ni ma Abilia hao alioneka na mwanaume mmoja wa takribani miaka 24 ad 26 akishuka talatıbu alikua amevaa Shatı jeusı la mikono mirefu lililo fungwa shingoni Suluarı ya cargo ya kijivu na buti nene za ngozi begi dogo klikninginia upande wa kushoto wa bega

Sauti ya afsa wauhamiajı yenye upole lakını ya kazı lışıkıka

Kalibu Sana Tanzania ndugu Paspot tafadhali

kijanana (Alitoa kimya kimya mach bado kwenye dari la jengo)

"Hll hapa." Alimkabidhi afisa huyo paspot

Afisa alitazama pasipoti jina lililo andikwa lilimfanya agande kwa Sekunde kadhaa

: Liam..... Liam Carter umetoka wap?" Afisa alimuuliza mwanaume huyo ambae anafaamika kwa jina la Liam Carter kama paspot yake ilivyo andikwa

"Thailand. Alijibu mwanaumehuyo anaefahamika kwa jina la Liam. Afisa alimtazama kwa muda mfupi, akatabasamu kwa tahadhari. Kisha akampigia muhuri pasipoti na kumrudishia.

"Karibu Sana Tanzania, kaka liam

Asante (Liam alijibu kisha Akatembea mbele bila kuuliza lolote.)

Aliingia kwenye ukanda wa kuchukua mizigo, lakini hakusubiri -- hakuwa na mizigo mkubwa zaidi ya begi lake dogo. Alivuka sehemu ya ukaguzi, akaingia sehemu ya mapokezi. Uwanja ulikuwa na watu wengi, baadhi wakikimbia kuwakumbatia ndugu zao, wengine wakisubiri kwa macho yenye hamu. liam alisimama kwa sekunde chache. Hakukuwa na yeyote aliyemsubiri. Hakukuwa na hata bango la jina lake.

Alitembea kuelekea mlango mkuu wa kutoka. Gharika ya jua kali na joto ikampiga uso wake mara tu alipovuka mlango wa kioo. Akika ni kama nilivyo sikia nchi hii inajoto sana

Alitazama kulia na kushoto baada ya kuona taksi na kuanza kuzisogelea

Dereva mmoja wa Teksi baada ya kumuona akamsogelea haraka):

“Vipi bro! Tunaenda wapi leo? Masaki? Mikocheni? Sinza? Gari iko poa, AC iko full!”

Liam alitazama macho ya dereva kwa muda mfupi):

“Masaki. Kwenye. Hotel yoyote yenye utulivu.”

Dereva (akiwa amefurahi):

“Ah, sawa! Karibu kaka, twende basi! Bei ni rafiki -- elfu hamsini tu.”

Liam (akitikisa kichwa na kukubali

“Dah, fresh kabisa bwana. Karibu Dar es Salaam!”

Gari ilikuwa Toyota Crown ya rangi ya silver. Dereva alifungua mlango wa nyuma kwa haraka, liam akaingia kimya. Akatupia begi pembeni na kuangalia dirishani. Na safari ikaanza Jiji lilianza kufunguka mbele yake -- magari, foleni, bajaji zilizopambwa, milango ya maduka ya Mlimani City, matangazo ya kampuni kubwa, harufu ya jua juu ya lami.

Dereva (akajaribu kuanzisha mazungumzo):

“Unaonekana mpya kabisa. Mara ya kwanza kufika Bongo?”

Liam (bila kugeuka):

“Sio mara ya kwanza… lakini ni kama mara ya kwanza.”

Dereva (akiwa anacheka):

“Heh! Hiyo sasa ni deep. Ulikuwa nje miaka mingi nini?”

“Niliwahi kuishi hapa nikiwa mtoto. Kisha niliondoka…”

Gari likakaa kimya. Dereva hakuliza zaidi. Aliangalia kupitia kioo cha nyuma lakini macho ya liam yalikuwa mbali sana -- kana kwamba alikuwa anatazama mahali palipo nje ya dunia hii.

Toyota Crown ya rangi ya fedha ilipinda kona ya mwisho kuingia Masaki. Jua la mchana liling’ara juu ya mtaa wa Chole, na upepo wa baharini ulivuma taratibu. Gari ilipunguza mwendo mbele ya jengo lenye maandishi meusi yaliyong’aa: Lush Bay Hotel.

Dereva akatazama kupitia kioo cha nyuma):

“Bro, tumefika. Hii hapa Lush Bay, ni nzuri na ina utulivu wa maana kabisa. Internet ipo, AC kali, na chakula fresh.”

Liam akavuta pumzi kwa kina

“Nzuri. Ahsante.”

Alitoa noti ya dola 100 na kumpa bila kuongeza neno

Dereva akapokea kwa bashasha

“Karibu Dar kaka! Ukihitaji gari tena sema tu, naitwa Hashim hii ni business cad

Liam alipokea business cad kisha akashuka taratibu, akanyoosha viungo kama mtu aliyekaa muda mrefu. Alibeba begi begani na kutazama juu ya jengo kwa muda mfupi — macho yake hayakutoa maelezo, lakini ni kama alikuwa anajaribu kukumbuka kitu. Mlango wa hoteli ulifunguka kiotomatiki alivyokaribia.

Ndani ya mapokezi, msichana mrefu mwenye sare ya kijivu aliketi nyuma ya kaunta. Jina lake liliandikwa kifuani: Edna. Tabasamu lake lilikuwa la kawaida, lakini lilivutia.

Edna kwa sauti ya kitaalamu):

“Karibu Lush Bay Hotel. Umefanya reservation?”

Liam akamtazama dada huyo kwa sekunde kadha kama kam chunguza kisha akajibu kwa sauti ya utulivu

“Hapana. Nahitaji chumba — tulivu, chenye dirisha, na bila usumbufu.”

Edna (akitazama kwenye skrini ya kompyuta):

“Tuna Executive Single na Private Balcony Deluxe. Deluxe ina view nzuri ya bahari.”

Liam:

“Deluxe. Nachukua kwa siku saba.”

Edna akainua macho kwa mshangao kidogo

“Ooh, fresh. Utalipa kwa kadi au cash?”

Liam alitoa pochi ya ngozi, akamkabidhi kadi ya Visa:

“Kadi.”

Baada ya malipo kukamilika, Edna alimkabidhi kadi ya chumba, nambari 408.

“Chumba 408, ghorofa ya nne. Lifti iko upande wa kulia. Ukiwa na swali lolote, piga namba hii.”

Liam alitikisa kichwa taratibu

“Sawa.” kisha alienda kwenye lifti kwa hatua tulivu. Ukimya wake uligusika, kama hewa nzito. Mlango wa lifti ulifunguka, akaingia peke yake. Ndani ya lifti, Liam alitazama uso wake kwenye kioo. Alishika kifua chake na kuhisi mapigo ya moyo wake.

Liam akajinong’oneza

“Nimeanza. Sura ya mama... ndiyo pekee niliyonayo.”

Mlango ulifunguka kwenye ghorofa ya nne. Liam alitembea kwenye korido yenye mwanga wa manjano laini, akiangalia namba za milango. Alisimama mbele ya 408. Akaingiza kadi na mlango ukafunguka. Chumba kilipiga harufu ya sabuni safi na maua ya vanilla. Alifungua pazia — mbele yake, bahari ya Hindi iling’ara chini ya jua.

Alitupa begi juu ya kitanda, akaketi kwenye kochi karibu na dirisha. Mikono yake ilishikilia kichwa, macho yake yakiwa yamekwama kwenye upeo wa macho. Fikra zake hazikuwa baharini — zilikuwa mbali, gizani, ndani ya mahali pasipoelezeka.

Alisimama taratibu. Akachukua simu yake, akaishika mkononi bila kuifungua.

Liam kwa sauti ya chini, akajinong’oneza

“Tayari niko nchini nini kinafata

Liam alionokana ana vitu vingi sana kichwani vinavyo mtatiza alitafakali kwa sekunde kadhaa kisha akaamua kujipunzisha

*****

Flashback: Miaka 17 nyuma Jua la asubuhi lilikuwa na joto la upole. Ndege walikuwa wanapita anga la Buguruni, wakiimba nyimbo za kila siku. Ilikuwa ni siku ya Jumatano, shule ya msingi Mtoni Mchangani ilikuwa imejaa sauti za watoto, kicheko, na kelele za walimu waliokuwa wakijitahidi kuweka nidhamu.

Kulikua na mtoto, akiwa na miaka 8 tu, aliketi darasani kwenye dawati la tatu upande wa kushoto. Alikuwa mtoto mtulivu kupita kawaida, mwepesi kuelewa, na mwenye sura ya kuvutia iliyojaa utulivu wa kipekee. Wakati mwalimu wao, Bi Zena, alipokuwa anaandika kwenye ubao, macho ya mtoto huyo yalitazama dirishani — kama alikuwa anasikia kitu fulani, tofauti.

“Michael! Tazama ubao, si dirisha.” mwalimu zena alimwambia mtoto uyo ambae aliitwa Michael

Michael (kwa sauti ya upole):

“Samahani mwalimu... lakini... kuna mtu... ananiangalia kule nje.”

Wanafunzi wengine waligeuka. Dirishani kulikuwa wazi, ila hakuna mtu aliyemwona. Mwalimu alifika karibu, akatizama nje. Hakukuwa na mtu.

“Hakuna mtu. Rudi kwenye daftari lako na utazame ubaoni alisema mwalim zena

Dakika chache baadaye, kengele ya saa nne ililia — muda wa mapumziko. Wanafunzi walimiminika uwanjani. Michael naye alichukua kipande cha mkate wa siagi mama yake aliyomwekea, akaelekea kivulini chini ya mti wa mkungu karibu na uzio wa shule.

Hapo ndipo aliposimama.

Upande wa pili wa uzio, kulikuwa na mzee mmoja. Alivaa joho jeusi lenye maandishi ya dhahabu, na macho yake yalikuwa ya kijani kibichi. Alikuwa na tabasamu la ajabu, si la kirafiki, lakini pia si la tishio — bali la kuvuta mtu bila sababu.

Mzee huyo (kwa sauti ya ajabu, kama hewa):

“Michael... unakumbuka wimbo wa nyota tano?

Michael alitikisa kichwa. Ndiyo, ulikuwa wimbo mama yake alimfundisha akiwa mdogo.

“Ndiyo. Mama yangu hua ananiimbia nikitaka kulala.”

“Basi njoo, tukaendelee kuimba pamoja.” alisema mzee huyo

Ni hapo ndipo Liam alipoanza kutembea, taratibu, kana kwamba alikuwa kwenye usingizi wa macho. Aliingia kichakani kupitia uwazi uliokatwa kwenye uzio — njia ambayo haikuwa hapo siku zilizopita.

Walimu hawakumwona, walinzi wa shule hawakumwona, na hata wanafunzi wenzake walifikiri bado yupo chini ya ule mti.

Dakika ishirini baadaye, mtoto huyo anaye fahamika kwa jina la Michael hakuwepo. Uwanja wa shule ukazizima. hii ilifahamika kuwa mtoto mmoja hayupo mala bada wa kuludi daladani na kukosekana kwa mtoto huyo

Ilibidi walimu waanze wakishilikiana na mlinzi kumuuliza labda mtoto huyo alitoka lakini mlizi alijibu kua hakuna mtoto yoyote alietoka waliendelea kumtafuta nje ya madalasa kwa kuzani labda huenda alikua bado nje lakini mpaka yanatimia masaa 4 hakukua na dalili yoyote ilio onesha kupatkana kwa mtoto

Ilibidi waitwe police wakaja. Upelelezi ukaanza.

Askari wa Kituo cha Polisi Buguruni – CPL Mwita:

“Mliona mtu yeyote akichukua mtoto?” aliuliza afisa wa jeshi la polisi

“Hapana afande. Hii shule imezungukwa na ukuta. Na hakuna mlango mwingine zaidi ya wa mbele.” alijibu mlinzi wa shule

“Alikuwa na mkate wake. Alikaa tu kivulini kama kawaida. Halafu... alipotea. Kama upepo maana huna alie muona alisema mwalimu mkuu -Bi faidha

Ilibidi wawasiline na Wazazi wa Michael walipokuja, vilio vilitanda. Dada zake walilia kwa uchungu. Kakake mkubwa aliapa kutomcheka tena kama alivyozoea.

Tukio hilo liliingia kwenye vyombo vya habari. Magazeti kama Mwananchi, Majira, na Nipashe yaliandika vichwa kama:

"Mtoto Apotea Buguruni: Alimezwa na Hewa?"

"Tukio la Kimaajabu: " akika tukio hilo lilikua ni la kustaajabisha

Jeshi la Polisi liliunda kikosi maalum. Maafisa wa usalama wa Taifa wakaja. Lakini hakuna aliyepata ushahidi wa kamera, wala alama ya viatu, wala njia ya mtego.

Ilikuwa ni kana kwamba Michael alitoweka kutoka dunia hii

*****

Saa ilikuwa 6:00 jion. Hoteli ya Lush Bay, iliyoko Masaki karibu na bahari, ilikuwa tulivu, joto la jiji likianza kushuka polepole. Liam alikaa kwenye kiti cha ngozi chenye mvuto wa kifahari, miguu yake ikiwa imekunjwa kidogo, mikono yake ikiwa nyuma ya shingo.

Dirisha la chumba namba 408 lilifunguliwa nusu, likimuonesha barabara ya Chole Road na baadhi ya paa za majumba ya kifahari yaliyo jirani. Vioo vya dirisha viliakisi macho yake ya samawati yenye kina

Simu ya mezani ikaanza kuita

“Trriiiiii... Trriiiiii...”

Akastuka kidogo, kisha akaiinua taratibu.

kwa sauti ya taratibu): “Hallo...?” alisema liam

Sauti ya mapokezi: “Habari za jioni, bwana Liam. Tumepokea mzigo wako wa mkoba uliobaki airport. Je, tukuletee chumbani?”

: “Ndio, tafadhali. Ahsante.” alisema liam

Baada ya kutata simu, akasimama na kutembea taratibu kuelekea bafuni. Kioo cha bafuni kilimuonesha sura yake — sura ile ile, lakini ikiwa , na ukimya mzito. Akaushika uso wake kwa mikono miwili, macho yake yalionekana kama yanapambana na kivuli kisichoeleweka

Liam alijinong’oneza atimae leo niko Tanzania…”

Alihisi kama sauti ndani yake inamwambia kuna kitu kinamkaribia. Lakini bado hakijajulikana ni nini.

Mara mlango wa chumba ukagongwa.

“Pppppp!”

Liam akasogelea mlango na kuufungua. Kijana mhudumu wa hoteli, mwenye tabasamu dogo usoni, anasimama mlangoni.

Huu hapa mzigo wako. Alisema muhudumu na kumkabidhi mkoba ule liam

Ahsante sana. Alisema liam

Akapokea mzigo wake na kuufunga mlango. Akakaa kitandani, na kufungua zipu wa begi lake. Ndani kuna koti lake la ngozi jeusi, pochi ndogo ya pesa, na kijikaratasi kimoja cha zamani — kilichokunjwa mara nyingi sana.

Akakikunjua na kukitazama. ilikua Ni picha ya mwanamke mwenye sura laini, macho ya huruma, na tabasamu la mama. Ilionekana ni picha ya zamani sana na ilio chakaa lakini bado inasimulia hadithi.

(Liam kwa sauti ya upole sana): “Mama… bado nakukumbuka. Lakini... uko wapi? Alisema liam

Papo hapo, dirishani upepo ulianza avuma na matazia yalipepepelushwa na upepo kwa sekunde chache. Liam akanyanyuka taratibu, na kufunga dirisha. Lakini moyo wake haukutulia

Anahisi kuna mtu anamwangalia. Au kuna jambo linamvuta kutoka mbali — kitu cha zamani, kitu cha hatari.

Akaamua kupoteza mawazo na kuagiza chakula akipendacho kwa maana hakua amepata chchote kangu alipo ingia nchini alipiga mapokezi na baada ya muda aliletewa

Baada kumaliza kupata chakula muda ulikua umesha enda ilikua ni mida ya kwenye saa3 za usiku hivyo Akaamua kujilazaa juu ya kitanda, hakua na mpango wa kutoka ukizingatia ni mgeni macho yakitazama dari. lakini gafla tu aliamka na kushuka kwenye kitanda hii ni mala baada ya kuhisi atali iko kalibu nae

Mwili wake wote ulisisimka. Ilikuwa kama umeme mdogo ulivyopita mgongoni

WILL CONTINUE

Next