SEHEMU YA 36.
Wakati wa mchana wote taarifa ya Regina Afisa mtendaji mkuu kumpata msaliti wa kampuni zilisambaa kwa kila mmoja , lakini haikuwa hivyo tu pia kwa kitendo cha Regina kuwatumia wasaliti kuidanganya kampuni ya Zena ni moja ya habari hizo.
Kulikuwa hata na baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa wakitaka kuzijua habari hizo na kuzichapisha katika mitandao yao.
Wiki iliopita , wafanyakazi wengi walikuwa katika hali ya mawazo mara baada ya kampuni yao kushindwa kuipata Omega , lakini kumbe haikuwa mpango wa Regina kuipata Omega.
Regina alikuwa amedanganya kampuni nzima kwa kuwaaminisha kwamba alikuwa akitaka kuinunua Omega na kuikosa , hata kuigiza kabisa kuonekana kama vile alikuwa katika msongo wa mawazo.
Ijapokuwa wengi walimpongeza Regina kwa kumuua adui yake bila ya kumwaga damu lakini upande mwingine walimuona Regina kama mwanamke mkatili sana, haikuwa swala la kudanganya watu wa kampuni ya Zena tu lakini vievile amefannikiwa kuidanganya kampuni nzima kuamini alikuwa akitaka kuinunua Omega.
Baada ya kazi kama kawaida Hamza na Regina walishuka chini pamoja katika lift.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni walikuwa pia ndani ya lift hio na walimsalimia Regina kwa heshima , lakini kulikuwa na hali ya kumuogopa katika macho yao , kitu ambacho kilionekana wazi tofauti na mwanzo.
Tukio la siku hio licha ya kwamba lilikuwa na faida kwa kampuni , lakini lilifanya wafanyakazi kuzidi kumhofia.
Yaani ni kama mwanzoni walikuwa wakiamini Regina sio kama wanavyomfikiria , lakini mara baada ya tukio hilo waliamini Regina ni kama wanavyomfikiria.
Regina alikuwa akiiona hofu yao lakini aliishia kukaa kimya kama kawaida yae , hakujali watu walivyokuwa wakimfikiria.
Barabara kuelekea wanakoishi ilikuwa na msongamano sio wa kawaida hivyo gari ilikuwa ikisogea kidogo kidogo , Hamza hata yeye alionekana kuboreka kuendesha gari kwenye msongamano kama huo na aliishia kuangalia kioo cha nyuma kuona Regina anafanya nini.
Lakini Regina muda huo alikuwa akiangalia upande wa nje ya barabara huku akiwa na hali flani ya wasiwasi.
“Usiwe na mawazo hivyo , kwenye hii dunia usitegemee kupendwa na watu wote”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kushangaa.
“Nani ana mawazo , hebu endesha gari huko”
“Regina huoni tupo kwenye foleni , ila kwa tukio la leo kama ungekuwa mwigizaji ungekuwa maarufu
mno , wiki iliopita nilidhani ulikuwa katika mawazo kwa kuikosa Omega” “Vipi … umekasirika kukuigizia?” “Nikasirike , kwanini nikasirike?”Aliulia Hamza.
“Si ninekundanganya na wewe?”
“Kwannini swala hili linikasirishe , hili sio swala la kisheria kwamba lazima uniambie kila kitu , kucheza rafu sokoni ni swala la kawaida kwa wafanyabiashara, ijapokuwa watu wanaweza kufikiria una roho ya kikatili , lakini yote umefanya kwa ajili ya kampuni , kama ningekuwa wewe pengine ningefanya hivyo hivyo, kama nilivyosema , huwezi kupendwa na watu wote kumbuka pia siku zote unapopata kitu jua unapoteza kitu”
“Na wewe unaamini hivyo?”Aliuliza na Hamza alitingisha kichwa.
“Ijapokuwa nimekudanganya mara kadhaa lakini hili namaanisha , ila siku nyingine Regina tukio kama hili likitokea ni kheri uniambie hata kwa siri sitowaambia watu, yaani nakuona una mawazo najaribu kukubembeleza kumbe napoteza nguvu zangu bure tu,itakuwa ni kujitia aibu tu”
“Sitaki unibembeleze , wewe ni nani kwangu mpaka unibembeleze , halafu kwanini nikuamini huwezi kutoa siri?”Aliongea Regina huku akikunja nne , lakini Hamza aliishia kucheka.
“Kwasababu mimi ni mpenzi wako , hivyo lazima unizingatie”
“Wewe sio mpenzi wangu , wewe ni mpenzi wangu wa maigizo tu , mpenzi wako ni huyo ulietoka nae out jana”Aliongea Regina kwa hasira.
“Kwahio vipi , nisipokuwa na mpenzi wewe utakubali kuwa mpenzi wangu , sidhani kama utakubali kutoka na mimi kimapenzi?”
“Nani kasema sitokubali”Aliongea lakini dakika hio hio alijua maneno yake hayakukaa sawa na kuulaumu mdomo wake kwa uropokaji , lakini jibu lile lilimshangaza Hamza.
“Regina kwahio unamaanisha unataka ku’date’ na mimi?”Aliuliza na kumfanya Regina kuona aibu kidogo.
“Kwannini unajiaminisha sana , ushawahi kuniuliza hilo swali?”
“Basi ngoja nikuulize sasa hivi , Regina je unataka tuwe wapenzi ki ukweli ukweli?”
“Mjinga wewe , Sitaki na sitotaka”Aliongea huku akimkodolea macho bila ya hisia.
Hamza alijikuta akikosa neno ,alijiambia ni kheri asingeuliza tu , maana jibu lilikuwa wazi.
“Hata mimi sitaki pia , kwanza nina mpenzi tayari na ni mpole na mchangafu kuliko wewe”Aliongea Hamza huku akionyesha furaha kabisa mara baada ya wazo la Eliza kumjia akilini .
Upande wa Regina ukauzu ulizidi kuonekana katika macho yake na aliishia kushika sketi yake kwa mikono yote miwili.
“Naona unamsifia sana huyo mpenzi wako , inaonyesha kabisa nimemzidi vitu vingi ndio maana unanilinganisha nae”
“Regina usiniambie unaona wivu , kwanini tokea jana nilipoanza kumzungumzia mpenzi wangu naona kuna kitu hakipo sawa kwako?”
“Nini, yaani mimi niwe na wivu na wewe , nimekuwa chizi , halafu ukiendelea kuongea ujinga wako sitokupa hata shilingi ya mshahara wako” “Bosi usifanye hivyo , najua hunipendi lakini usinikate mshahara”Aliongea Hamza akijitetea.
Regina alikuwa na hasira sio ya kawaida kiasi kwamba kifua kilikuwa kikimpanda na kushuka , aliishia kuvuta mdomo na kisha akageuza kichwa chake na kuangalia nje.
Haikueleweka foleni ilisababishwa na nini , lakini muda ambao walifika nyumbani giza lishaingia tayari.
“Umeongea pumba zako kwenye gari mpaka umesababisha nimechelewa kufika nyumbani”Alilalamika Regina.
“Nunua gari lenye mabawa siku nyingine nitalipaisha , yaani unanilaumu kwa msongamano wa magari ambao sijausababisha”
“Ni makosa yako , ungetafuta njia nyingine, halafu usibishane bishane na mimi”
“Okey , samahani bosi kwa kukuchelewesha nyumbani na kukukwaza”Aliongea Hamza , hakuaka kuendelea kubishana na Regina juu ya swala hilo maana hata kosa lake hakuwa akilijua. “Shangazi ni bora uwe unapika moja kwa moja na
kuendelea kula tu , usitusubiri ukiona tumechelewa”Aliongea Hamza.
“Nilijua mtachelewa sana , chakula cha kupasha sio kizuri ndio maana nachelewesha kupika , hii AC inapoozesha chakula kwa haraka, subirini kidogo nimalizie”Aliongea Shangazi huku akielekea jikoni.
Hamza hakutaka kusubiria chakula sebuleni na alienda jikoni pia .
“Shangazi unaonaje tukigawana upishi ili tumalize haraka, mimi nitatumia jiko la umeme”Aliongea Hamza na Regina aliekuwa amekaa kivivu sebuleni alishangaa baada ya kusikia kauli hio.
“Wewe unajua kupika?”
“Najua ndio , kwani kuna ugumu gani kupika?”
“Kwahio kumbe kila binadamu siku hizi ni mpishi?”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kutingisha kichwa kwa masikitiko.
“Ni hivyo tu sina mpango wa kuonyesha uwezo wangu leo hii , nina nyota tano za Michellin , likija swala la upishi”
“Michellin wanatoa nyota tatu tu za upishi , wewe hizo tano umezitolea wapi , unadhani wote sisi ni washamba?”Aliongea Regina akimkosoa.
“Natania tu , nilikuwa namaanisha ninao uwezo wa kuharakisha mapishi na yakawa ya kiwango”:Aliongea Hamza .
Shangazi alifurahi kuona amepata mtu wa kumsaidia hivyo alimwachia Hamza samaki aziunge.
Hamza mara baada ya kuanza kukatakata vitunguu na nyanya kwa spidi kali pamoja na mpangilio wake wa ki upishi jambo hilo lilimsahngaza Shangazi.
Ndani ya muda mfupi tu mboga saba zote zilikuwa zimeiva na kila kitu kilikuwa kipo kwenye meza.
Regina alijikuta akimeza mate kutokana na harufu nzuri ya chakula , mara baada ya kusogea mezani na kuangalia namna samaki alivyokatwa katwa katika vipande vya nyama , pamoja na namna ilivyopambwa na kachumbali kwa juu ilipendeza kwa macho.
“Regina , Hamza ni fundi mno kwenye upishi , mimi nashindwa kutumia jiko la umeme kukadiria moto lakini yeye ameweza na hakuna kilichoungua na chakula chake kinapendeza”Aliongea Shangazi kwa kusifia. “Shangazi chakuka kuonekana vizuri haimaanishi ni kitamu”Aliongea Regina na alichukua uma na kisha kuchukua kipande cha samaki na kupeleka mdomoni na kitendo cha kutafuta mara kadhaa muonekano wake ulibadilika mara moja.
“Haha ,, unaonaje , nishakuambia nina nyota tano”Aliongea Hamza kwa majisifu.
Regina aliishia kukosa neno la kuongea kwasababu radha ya hio samaki ilikuwa ni zaidi ya radha ambayo alikuwa akiipata kutoka kwenye chakula kinachopikwa na Shangazi.
Regina aliishia kujiambia kwanini huyu mwanaume kila kitu anajua , alijikuta akiishia kuchukia kwa kitendo cha Hamza kujua kila kitu.
“Regina kwa Hamza hapa nadhani sina wasiwasi hata nisipokuwepo baadae, hata kama usipojifunza kupika Hamza atakuwa yupo tayari kukusaidia”Aliongea Shangazi na mara baada ya kusikia kauli ile Regina alijikuta akiwa mwekundu.
“Shangazi kwanini unaongea hivyo”
“Nini , inamaana Regina hajui kupika , Shangazi huyu ukimuacha mwenyewe ataisha kula mayai ya kuchemsha au hotelini”
“Regina hata mayai ya kuchemsha hajui kabisa , anachojua ni kufanya biashara tu, nakumbuka alishawahi kuchemsha mayai mpaka maji yakakauka huku mayai yakipasuka na kubakia makasha tu”Aliongea shangazi na kuanza kucheka.
“Ili mradi hakuungua tu , inatosha”Aliongea Hamza.
“Nyamaza wewe , kwani kujua kupika ndio nini , nikiamua kujifunza nitaweza pia’”Aliongea Regina huku akiona aibu , ni kama anaona Hamza anamdharau kwa kutokujua kupika na kuonekana amekuzwa kimayai mayai.
“Regina usikasirike ni utani tu , hebu kaeni tule kwanza”Aliongea Shangazi lakini Regina alikuwa na hasira mno na kadri alivyokuwa akimwangalia Hamza ndio alivyokuwa akizidi kuchukia.
Muda huo huo simu ya Hamza iliita na alipangalia jina la mtu anaepiga ni Lau mfanyakazi wa Mgahawa wa Dina.
Hamza hakutaka Regina kusikia anachoongea hivyo alitoka nje na kupokea simu
“Lau vipi kuna tatizo?”
“Madam ameniambie nisikueleze , ila yupo kwenye matatizo makubwa”Aliongea Lau upande wapili akioyesha kuwa na wasiwasi.
Comments