Reader Settings

SEHEMU YA 39.

Iliishia Hamza anapokea simu  ya mwanamke ambae anaanza  kwa kumuita  Prince Rich.

Endelea sasa:

Hamza  mara baada ya  kusikia  lafudhi hio ya  uingereza alijua nani  aikuwa akiongea kwenye simu.

“Don’t be coquettish Flora , you are already  old enough to be my grandmother , how can I stand  such coquetish words?”Aliongea Hamza kwa kingereza akiwa na tabasamu.

“Sio tabia nzuri kuongelea  umri wa  mwanamke  kwa staili hio , wewe ni mkubwa  kwangu  lakini  kwanini unanishambulia?”

“Kama unajua mimi ni mkubwa kwako basi unapaswa kuwa siriasi kidogo, halafu kumbuka  kuniita Hamza Mzee  ndio jina langu jipya ,usiniite  majina ya zamani”Aliongea Hamza.

“Nimekuelewa , sasa uniambie  Mr Hamza wapi tunakutana , nimekumisi mno”

“Kwasasa kuna mambo nataka kuyaweka sawa , tukutane jioni , tutapata chakula cha usiku pamoja , usije na walinzi wako sitaki  attention”

“Nimekuelewa ,  hapa  karibu na hoteli  niliofikia kuna McDonalds , itakuwa vizuri tukikutana hapo”

“Naona umesafiri na uzungu wako  mpaka Tanzania , hutaki kujaribu  radha ya vyakula vya kitanzania?”

“Sio kama unavyofikiria ,nyumbani  chakula changu ni cha kupimiwa sana na siruhusiwi kula vyakula vya  madukani, nipo Tanzania nitakula kila ninachoona  kinanifaa”

Hamza hakutaka kubishana nae, hivyo aliamua  kumuacha afanye anavyotaka , aliuliziaa tu hoteli aliofikia  na wakakubaliana muda wa kukutana  na kisha akakata simu.

Baada ya  hapo  moja kwa moja Hamza  alienda moja kwa moja mpaka kwenye idara ya mauzo , alihitaji kumpatia taarifa Eliza   juu ya dokta ambae  anapaswa kumwangalia mama  yake amefika Tanzania.

“Kwanini upo hapa  mapema yote haya?”Aliuliza Eliza mara baada ya Hamza kuingia katika ofisi yake.

Hamza  hakutaka kupoteza muda alimsogela mrembo huyo na kisha alimshika kiuno na kumbusu  mdomoni.

“Nimekumisi  sana  siku nzima ya jana na leo ,  nimekuja kukukiss?”

“Unimisi wapi , najua kabisa mpango wako ni kwenda kula chakula cha mchana  na  Yonesi, Asha ameniambia  imekuwa ratiba yenu , lazima

mkae meza moja kila siku kwa ajili ya chakula”Aliongea  Eliza huku akionyesha dalili ya wivu.

“Sio hivyo Eliza,  nimemuona Kapteni  akila peke yake  ki’upweke ndio maana ninampa kampanni , unaonaje tukifanya nae urafiki na kumchangamsha mara kwa mara”

“Huwezi kunipata mchana , muda mwingi  natoka  hivyo  ni mara chache sana kuniona katika mgahawa wa kampuni”

Hamza mara baada ya kusikia jibu hilo alijikuta akivuta  pumzi ya ahueni , alijiambia kama akikaa meza  ambayo  kuna Yonesi na Eliza  kuna tukio baya lazima lingetokea.

“Niambie , najua  una sababu ya kuja  ofisini kwangu?”Aliongea Eliza

“Daktari niliekuambia  nitamwita kuja kumwangalia mama yako tayari yupo hapa Dar , jioni  nitaenda   kuonana nae wakati wa chakula cha usiku , tunapaswa kwenda pamoja”

“Dokta amefika! , mbona hukuniambia  nikafanya maandalizi ya  atakapofikia, napaswa kumpa heshima yake kama mgeni wangu”

“Usiwe na wasiwasi maandalizi yashafanyika , unachopaswa ni kutangulizana na mimi tu , nitaenda chuo  nikitoka huko

nitakutaarifu”Aliongea Hamza na Eliza alitingisha kichwa kumuelewa.

Kwasababu muda umeenda Hamza alielekea chuo moja kwa moja  kwa kutumia  mwendokasi.

Asilimia kubwa ya wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu walikuwa wanaelekea Field , kwa  wanafunzi wa mwaka wa tatu  walikuwa wakimalizia field yao ya mwisho.

Ijapokuwa Regina alikuwa akijua kuchagua nguo  lakini nguo ambazo  Dina alimvalisha Hamza zilikaa ki ujana zaidi na kumfanya Hamza  kuvutia mno na swala hili lilimfanya kuangaliwa  na  wanafunzi wengi ambao alipishana nao.

Macho yao ilikuwa ni kama  pale  ambapo unadharau kitu  ambacho mwanzoni hukujua ni cha thamani na mara baada ya kuokotwa na mwingine unaanza kuona thamani yake , hayo ndio macho ya wanawake warembo  aliopishana nao Hamza.

Siku kadhaa zilizopita Hamza alionekana  kuwa wa kawaida sana , kitu pekee ambacho  kilikuwa kikimfanya  kuonekana  ni muonekano wake pekee wa kuchanganya rangi  lakini hakukuwa na dalili yoyote ya  Hamza kuwa mtu mwenye hela.

Sio kama Hamza hakuwa na hizo dalili ni kwasababu alikuwa katika jamii ambayo ilikuwa   ni ya daraja la chini   kuliko yeye hivyo  hawakuweza kuona  dalili ambazo zimejificha kama ilivyokuwa kwa   yule mzungu alivyoitambua hadhi ya Hamza  kupitia mavazi.

Hivyo  Hamza karibia siku zote aliweza kufika chuoni hapo  akiwa na mavazi ya  bei ghali mno lakini hakuna mwanafunzi hata mmoja aliewahi kutambua,  yale mavazi ambayo yalikuwa  na chapa za makampuni makubwa ndio yalionekana  ya thamani.

Hamza sasa siku hio alikuwa amevaa mavazi ambayo yalikuwa na  chapa   ya kampuni  kubwa  zenye jina duniani ndio maana aliteka macho ya watu wengi , saa tu pekee ambayo alivalia  ilimfanya asionekane  kinyonge.

Hata yeye mwenyewe alijua kwanini watu  walikuwa wakimwangalia hivyo ilimfanya kutokujali lakini kwa wakati mmoja  kujisikia vizuri kwa kuonekana , ni tabia ya   kila binadamu kupenda  kuonekana  zaidi katika kundi la watu.

Hamza aliingia chuoni lakini tofauti na siku zote ni kwamba hakuweza kuonana na watu ambao alikuwa amezoeana nao , alikuwa maarufu lakini hakuwa na mazoea ya watu wengi.

Wakati akitaka kuelekea upande wa maktaba simu yake ilianza kuita  na alipoangalia  jina aljikuta  akishangaa kidodo , alikuwa ni  CR(Class representative)  wake ndio  aliekuwa akipiga , alishangaa kwasababu ndio amefika chuo na CR anampigia simu.

“Madam!Kwema?”Alipokea Hamza.

“Kwema Genious, nimekuona ukiingia  geti la chuo  nikakumbuka   kuna mtu alikuwa akikutafuta”Sauti ya kike iliongea.

“Nani alikuwa akinitafuta  Winnie?”

“Profesa Singano, aliniambia nikutaarifu jana lakini  mambo yalikuwa mengi nikasahau, nenda ofisini  kwake nadhani atakuwepo”Aliongea  na upande wa pili ulionekana kuwa na haraka maana simu ilikatwa mara  moja.

Hamza aliishia kujikuna kichwa  na kujiuliza Mr Bonus point anamtafutia nini , lakini hata hivyo hakutaka kufikiria sana , alitii wito na kuanza kutembea kuelekea upande  jengo la utawala.

 Baada ya kupanda lift  sekunde chache tu alikuwa  nje ya ofisi ya  Mzee wa Bonus pointi , kilichomchosha  Hamza ni uwepo wa watu wengi ndani ya eneo hilo, ambao  ilionekana walikuwa kwenye foleni ya kwenda kuonana na Profesa Singano.

Ilileta maana hata hivyo maana  Profesa alikuwa  ni 

Cordinator  wa  wanafunzi hivyo   huwa inakuwa kawaida kukuta watu wengi wakitaka kuingia  katika ofisi yake.

Hamza alikagua sura zilizokuwa katika eneo hilo  na karibia zote  zilikuwa  ni za wanafunzi wa mwaka wa pili   na mwaka wa tatu kozi tofauti.

Kwasababu alikuwa akiujua utaratibu hakuaka   kuuvunja  hivyo alikaa kwenye  viti mwisho  kabisa akisubiria zamu  yake , hata hivyo kwa haraka haraka aliona angekaa hapo  muda mrefu  mno.

Zilipita dakika  chache tu  mwanafunzi alitoka  , Hamza hata hakuwa bize kuangalia nani anaingia au anatoka , alikuwa amekza macho kwenye simu yake akiperuza  peruza kwenye mtandao wa Jamiiforum , ni tabia yake hio hivyo haikumpotea kirahisi.

“Hi!”

Kabla ya kusikia sauti tamu ikimsalimia alichoanza   kuhisi ni marashi mazuri ya kuvutia  na Hamza aliinua macho yake  na kumwangalia  aliempa  salamu , alikuwa ni Anitha, mwanamke ambae  Hamza alishawahi kumtokea na  akampiga chini  kwa kuambiwa hana hadhi , ilishangaza siku hio  mrembo huyo kuanza  salamu  kwenda kwa Hamza  maana alikuwa akimdharau mno.

“Nimekusalimia Hamza”

Aliongea Anitha mara baada ya kuona Hamza ana mwangalia tu bila kumjibu , alionekana kuwa na muonekano wa kirafiki .

“Oh! Mambo  mrembo?, nimeshangaa kidogo  maana sio kawaida  hii?”

“Sio kawaida  nini?”Aliongea Anitha.

Ki ufupi Anitha alikuwa mwanamke  mrembo  haswa , dosari yake pekee ni miguu tu , alikuwa  na miguu miembamba, ilikuwa ikivutia lakini haikuendana na umbo lake.

“Sio kawaida kupokea salamu kutoka  kwako?”Aliongea Hamza huku akitabasamu.

“Itakuwa kawaida kwanzia sasa  na kuendelea?”Aliongea huku akitoa  tabasamu  , lakini  pia hakuacha kumwangalia Hamza kuanzia juu  mpaka chini na macho yake yalikuwa yakionyesha  wazi kile ambacho anafikiria.

“Salamu yangu  kwako ilikuwa kama tusi , ulinipiga tofali kila kona , nini kimekupata ndani ya siku hizi chache , unaumwa?”Aliongea Hamza.

Ukweli Hamza kama angekuwa muigizaji angekuwa na kipaji kikubwa sana , kwa jinsi ambavyo alikuwa akionekana  mbele ya Anitha  alikuwa ni kijana wa kawaida  sana mpole.

Kauli ile  ya Hamza kiasi flani ilimfanya  Anitha kujisikia vibaya  kwa kuona aibu.

“Uliyasababisha wewe, unaongea kama vile  hujui?”Aliongea huku akikaa chini  kwenye  benchi.

“Nimeyasababisha  nini?”

“Kipi kilikufanya  kunitongoza mbele ya mpenzi wangu , tena kwa  kupiga magoti mbele za watu na kila mtu anaona?”Aliongea Anitha  na kauli ile ilimuacha Hamza  na mshangao.

Na alijiambia inamaana siku ile alivyoziweka wazi hisia zake  kwa  Anitha  mpenzi wake alikuwa kwenye kundi la wanafunzi ,  lakini mbona hakuwa na habari.

“Ile siku  hukuwa ukinitongoza  , ulikuwa ukinidhalilisha , ni  jaribio ambalo umefanya  nionekane sio mwaminifu”

“Kwahio unachomaanisha , siku ile   mpenzi wako  alikuwepo , mbona sikuwa na habari  kama una mpenzi  ndani ya chuo?”Aliongea Hamza na kumfanya  Anitha kumwangalia  Hamza kwa usiriasi.

“Mpenzi lazima  awe wa chuo  tu?”Aliuliza na Hamza aliishia kushika pua.

“Kama  lilikuwa jaribio  la kukudhalilisha , niliishia kujidhalilisha mwenyewe ,  lakini  kwanini unaongea kama vile  unanilaumu , yale yashapita  na nilipotezea”Aliongea Hamza huku akianza kuonyesha dalili ya kukosa uvumilivu  wa  kuendelea kuongea  na Anitha, siku zote wanawake hawakosi  sababu , alihisi pengine  anadanganywa na Anitha  ili apata gia ya kurudisha muda nyuma ,  lakini Hamza alikuwa na Eliza tayari hivyo  hakumhitaji  Anitha.s

“Ulipotezea au umenipotezea?”

“Vyote”Aliijibu Hamza  na kumfanya  Anitha kuvuta mdomo.

“Kwasababu  tayari ushafanikiwa  kupata mpenzi  na anakupendezesha?”Aliongea  huku akiangalia mavazi ya  Hamza.

“Unamaanisha nini?, umejuaje nimepata mpenzi mzuri zaidi yako?” Hamza aliona huyu mwanamke ashaanza kuleta dharau.

“Huna  haja ya kumsifia mbele yangu , ninachojua  tu hamuendani”Aliongea  na kisha alisimama  lakini Hamza alimzuia.

“Nani siendani nae?”Aliuliza  Hamza  akiwa siriasi kidogo .

“Eliza!”Aliongea  na kisha bila hata ya Hamza kuuliza  zaidi amemjuaje Eliza mwanamke huyo aliondoka mbele yake, akionekana kabisa  hajafurahishwa na Hamza kuwa katika mahusiano.

Hamza hakujua acheke wala alie,lakini hata hivyo hakutaka kujali sana , hakuwa na mpango tena na  Anitha ,  kwanza  hata kumtongoza kwake   kupitia njia ya  ile mpaka kukataliwa alikuwa kwenye majaribio ya uanaume bwege, kwenye maisha yake hajawahi kutongoza, yeye ndio aliekuwa  akishobokewa na warembo.

Anitha   haikueleweka  alikuwa  amemuona  wapi Hamza na  Eliza , lakini ilionekana  wazi aliamini mabadiliko ya Hamza yalitokana na gharama  za mwanamke , ni kama hakuwa akiamini kama Hamza anao uwezo wa kujinunulia mavazi ya bei ghali.

Hamza aliendelea kusubiri zamu yake ifike lakini muda ulikuwa ukienda na taarifa zilitolewa ambao  wamebakia  kuonana na Profesa  wafike siku inayofuata.

Hamza alichoka kwenye mambo ambayo yalikuwa yakimchoka kwenye maisha yake ni kupanga foleni, lakini hata hivyo alishukuru  maana  ilikuwa ni muda wa chakula cha mchana na mpango wake ilikuwa  ni kwenda kula  kazini.

Lakini sasa  wakati  akijiandaa kutoka  Profesa Singano alitoka nje  na alikuwa ametangulizana na  mama mmoja ambae Hamza alimtambua ni

Sekretari.

“Mr Hamza!”

Profesa Singano aliita , Hamza alikuwa akifahamika na  karibia  walimu wake wote , hio yote ni kutokana na uwezo wake  darasani , alikuwa ndio kichwa   tokea akiwa mwaka wa  kwanza.

“Yes!, Good afternoon Professor!”Alisalimia  Hamza, huwa ilikuwa ngumu sana kwake kusema shikamoo hivyo mara nyingi alikuwa akitumia salamu ya kingereza.

“Good afternoon ,I’ve been expecting you”Aliongea Profesa akimaanisha alikuwa akitarajia  ujio wake baada ya kumuita.

“Niwie radhi profesa , nilichelewa kupata taarifa za wito  wako”

“Hakuna shida , wanafunzi  wengi  hampo maeneo ya karibu  ni  kawaida kuchelewa kupokea taarifa,  huu ni muda wa mchana , unaonaje  ukiungana   na mimi kwenda kupata chakula cha mchana ili nikuambie na  dhumuni la kukuita?”Aliongea Profesa  na Hamza alisita kidogo.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi  bwana mdogo,  gharama zitakuwa juu yangu”Aliongea Profesa na kumfanya Hamza kutoa tabasamu huku akitingisha kichwa  kukubali.

Ukweli ni kwamba sio kama hakuwa na hela ya kulipa  , ila kwasababu mpango wake ilikuwa ni kurudi  kazini kula  chakula cha bure  aliona lazima ajihakikishie  Profesa atalipia chakula chake.

Dakika kadhaa tu wote  kwa pamoja walikuwa  ndani ya mgahawa  katika hoteli ya Peacock, ni sehemu ambayo maprofesa wengi walitumia kupata chakula   maana ilikuwa  mkabala na chuo  , hata baadhi ya wanafunzi   wa chuo  waliingia ndani ya hoteli hio lakini  ni wale ambao walikuwa na uwezo wa  juu wa kifedha.

Hamza  licha ya  kujiuliza nini ambacho Profesa Singano anamtafutia , lakini   alichowaza kwa dakika hio ni kuagiza chakula  cha maana, sekretari ambae walitangulizana nae alionekana kwenda kuungana na wenzake.

“So, I’m sure  you’re wondering  why I called  you?”Alianza maongezi mara baada ya   oda zao kuchukuliwa. “Ndio Profesa”

“Kwenye wiki hizi  tatu nimepokea watu  watatu  tofauti tofauti waliofika chuo  na kuulizia taarifa zako , ndio maana  nimechukua   uamuzi kukuita”

“Kweli!!, Ni wakina nani?”Aliuliza Hamza huku akionyesha mshangao.

“Sina uhakika sana , hawakuacha majina yao , ila   kati yao kuna  waliojitambulisha kutokea  kampuni ya Zena”

“Zena!?”Aliuliza  Hamza kwa mshangao kidogo na akili yake ilifanya kazi,hio ni kampuni ambayo  ipo chini  ya  James.

“Ndio , unaifahamu?”

“Naisikia  lakini sina mawasiliano na mfanyakazi yoyote wa Zena Profesa”Alijibu Hamza na kumfanya Profesa kumwangalia usoni kwa umakini.

“Haishangazi  sana kufuatiliwa na watu wa kampuni ya Zena , wewe ni mwanafunzi   namba  moja  katika  kozi yako, walionyesha  kuvutiwa  pia na wewe  na wamesema wanataka  kukuingiza kwenye  timu yao ya  idara ya fedha”Aliongea Profesa na Hamza aliishia kujiwazia ndani kwa ndani, hakuna  kitu  kama hicho kampuni ya Zena kumtafuta kwa

ajili ya kazi ni  James huyo  akihangaika kumchimba.

Ukweli ni kwamba haikuwa mara ya kwanza Hamza kufuatiliwa  na  watu wa makampuni , lakini   yeye hakuwa  na mpango wa kuajiriwa , kitendo cha kujiunga na chuo   yalikuwa ni maagizo ya Mzee tu pekee, chuoni kwenyewe aliingia kimagumashi kwa kufoji vyeti  vya  elimu ya  high school.

“Ni fursa  kwangu  hio Profesa , lakini kwasasa malengo yangu  ni kufanya kazi ndani ya  kampuni  ya  Dosam ,  napanga  internship kuanzia huko moja  kwa moja”

“Dosam ni kampuni nzuri , sio wazo baya”Aliongea na  muda uleule wahudumu walichafua meza yao kwa vyakula  na kumfanya Hamza kumeza mate   kama vile chakula sio chake.

“Profesa kuhusu  wengine waliokuja kunitafuta , hujawatambua wametokea wapi?”

“Wote walijitambulisha  kwa namna inavyofanana , lakini  kwa uzoefu wangu  maswali waliouliza yalinifanya  nione  kuna  la ziada”

“Kitu gani cha ziada?”

“Wameuliza  sana taarifa zako za maisha ya chuo, na mambo mengi binafsi , kama ni waajiri haikuwa na haja ya kuuliza”Aliongea Profesa huku akionekana kumwangalia Hamza , ni kama kuna  kitu  ambacho alikuwa akitafuta. “Unaonekana kutokuwa na wasiwasi?”

“Mimi kama raia  mwema , nisiekuwa na ugomvi  na mtu  sidhani kama  napaswa kuwa na wasiwasi”Aliongea Hamza huku akijiweka  bize na chakula lakini upande wa Profesa aliona kabisa  kuna kitu  sio cha kawaida kutoka kwa Hamza.

Ukweli ni kwamba sio   kwasababu ya Hamza  kutafutwa  na watu  siku kadhaa  bali ni tokea Hamza alivyojiunga  chuo  na  matendo yake ya  kila siku.

“Umejiandaaje na mtihani wako wa mwisho?”Aliuliza Profesa

“Ah , Nimejiandaa vizuri  tu  Profesa”Aliongea Hamza huku  kidogo akijifanyisha kuona aibu za kizembe.

“Wakati unaanza chuo  uliomba uongozi  kutokukujumuisha na baadhi ya kazi za vikundi kwasababu ulikuwa ukijitafutia kipato ,  unaweza vipi  kusoma  na kufanya kazi kwa wakati mmoja na ukaendelea kushikilia namba moja ndani ya darasa?”.

“Profesa niseme tu sijawahi kusoma  kabisa , uwezo

wangu wa kutunza kumbukumbu ni mkubwa”Aliongea na  kauli ile ilimfanya  Profesa kushangaa kidogo lakini hata hivyo aliacha kuuliza maswali mara baada ya simu yake kuita.

Wakati wa kuongea na simu Hamza alijua nani alikuwa akiongea nae , ilionekana ni  Prisila ndio anaongea na baba yake kwani mzee huyo alibadilika mara moja kutoka kuwa profesa na kuwa baba, ilionyesha ni dhahiri kiasi gani  Prisila  alikuwa na ukaribu  na baba yake , Hamza hata hivyo hakujali sana maana hakuwa na ukaribu  na  Prisila ila alikumbuka  alikuwa na deni na mrembo huyo.

Baada ya kumaliza kupata chakula aliachana na Profesa na aliamua kurudi  maktaba ambako kama kawaida yake alipoteza muda kwa kufurahia AC  na kuperuzi mitandaoni mpaka  jioni ikamfikia ndani ya chuo.

Hamza mara  baada ya kutoka   alimpigia simu  Eliza , miadi ya kukutana na Dokta Ronica   ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu  za jioni.

Kwasababu Hamza alikuwa  mjini na Eliza  nyumbani ilibidi amsubiri  aje yeye wakutane njiani ndio waende.

Nusu saa mbele  Hamza aliweza kukutana na Eliza  na kuingia kwenye gari lake na walienda moja kwa moja kusimama  mbele ya mgahawa wa McDonald’s kilomita chache kutoka ilipo Serena hotel.

“Sehemu ambayo tunakutana na huyo dokta ni  ndani ya huu mgahawa?”Aliuliza Eliza kwa mshangao kidogo.

“Ndio , ni mpenzi wa  mavyakula aina ya Hamburger  na chipsi na kadri chakula kinavyokuwa cha bei rahisi  ndio  anaona ndio kitamu”

“Mh , chakula cha hapa ni  cha bei rahisi?”

“Haha..Eliza  uzunguni KFC na McDonalds ndio wanaunza chakula  bei  rahisi lakini chenye ubora , vyakula vya bei rahisi hapa  Tanzania  havina ubora wa kuzidi hii migawaha ya fastfood”

“Kwanini anafurahi kikiwa cha rahisi , ninachojua  madaktari kutoka Ulaya na Amerika wengi  wana kipato  cha juu, kwanini rafiki yako anaonekana kama masikini?”Aliongea Eliza na kumfanya Hamza kucheka.

“Hey!, sio masikini  kuna utofauti mkubwa wa  kuzaliwa  ukiwa  tajiri na  kuzaliwa masikini  na kisha ukawa tajiri , yeye  alizaliwa akiwa masikini lakini akaja kuwa tajiri , hivyo kuna  radha ya vyakula vya bei rahisi  havisahauliki na mara kwa mara lazima uvikumbuke , wengine sio kukumbuka tu  ni kwasababu  pia vinawakumbusha walikotoka”

“Nimelewa sasa yupo hapa sio kwa ajili ya kula

chakula bali kwa ajili ya kujikumbushia mapambano yake?”

“Safi , hapo umepatia , wataalamu wa mauzo wengi  mnajua kuelezea kitu  kwa  lugha rahisi na kueleweka ,  unakidhi kuwa meneja”Aliongea Hamza huku akishika  shavu  la Eliza.

“Wewe acha kunifanyia hivyo , tunangaliwa ujue”Aliongea Eliza huku akiona aibu za kike na Hamza alimuacha akiongoza njia.

Hamza mara baada ya kuingia ndani ya mgahawa huo aliweza kumuona mwanamke  ambae ni mzungu  mwenye nywele  nyeupe(Blonde)  na kavaa kofia  ya chepelu , tisheti nyeupe  na jeans.

Kwenye meza yake kulikuwa tayari na

Baga(Burger) nne , soda ya Cocacola , glasi ya juisi  na boksi mbili za chipsi.

Ukimwangalia ungesema  ni mtu ambae alikuwa na njaa kwa muda mrefu maana  mkononi tayari alikuwa ameshikilia  Burger lakini  kuna zingine ambazo hakuwa amegusa.

“Flora !!”Aliita Hamza huku akimshika mkono  Eliza na  kusogea  nae upande wa  alipo mwanamke huyo.

“Ugh!!”

Mwanamke huyo wa kizungu  alishituka mara baada ya kuitwa jina hilo  na kutokana na kubugia kiasi kikubwa cha baga aliishia kutoa chembechembe za mkate.

“Hamza why did you only just arrive?,I’ve been waiting for you guys  for half an  hour , I really can’t help  but eat first.”Aliongea akimwambia Hamza kwanini ndio  wanafika  maana  amesubiri kwa zaidi ya nusu saa  na alikosa uvumilivu na kuanza kula.

“This burger  with blu-thin mushroom is so delicious”Aliendelea kuongea.

“Unaongea nini wewe , mbona sijawahi kusikia  Buga  ya aina hio?”Ukweli ni kwamba Hamza hakuwa mpenzi wa  mibaga hivyo hakuelewa  alichokuwa akimaanisha   Dr Flora Ronicas.

Hamza alimvuta mbele  Eliza ambae alionekana  kukaa kizembezembe na kumuweka mbele yake.

“Ngoja nikutambulishe , huyu  ni  Eliza  niliekutajia , mama yake ndio mgonjwa unaekwenda kumtibia”Aliongea Hamza.

Upande wa Eliza alikuwa akimkagua mzungu huyo 

, kwa maelezo ya  Hamza ni  dokta kutoka Marekani  lakini  alivyokuwa akiongea ni tofauti kabisa na  watu wa Marekani alionekana kuwa muingereza  mwenye pua iliochongoka , kidevu chenye  ncha  na macho  yenye kiini kilichopauka , alikuwa  mwanamke mrembo wa kizungu ambae  ungetamani kumwangalia mara mbilimbili na kwa  uwezo wake wa kukadiria umri alijiambia pengine ana miaka ishirini hivi  kwenda therathini.

“Hello , my name is Eliza Mlowe , Nice to meet you  Dr Ronica”Aijitambulisha Eliza kwa kingereza , alikuwa  ashamuuliza  Hamza jina lake kabla ya kuingia.

Lakini mara baada ya kumuona daktari mwenyewe  ambae alikuwa  mrembo lakini vilevile  anaekula sana , wasiwasi alikuwa nao  kuamini kama huyo ndio daktari anaekwenda kumponyesha mama yake.

“Niite Flora tu , wewe ni mpenzi wa   Hamza haina haja ya kuwa  mpole kiasi hicho”Aliongea  huku akiendelea kuwa bize  na  mkate wake.

Eliza masikio yalipata moto na kumwangalia Hamza , hakujua  Hamza alikuwa  ameenda mbali  kumtambulisha kama mpenzi wake.

“Flora  nimekuambia  usijionyeshe sana  lakini   sio kujigeuza chokoraa , unadhani  kula  namna hio ndio kujificha?”

“Mimi mwenyewe  nilikuwa sijui , ndio mara yangu ya kwanza kuja Tanzania  na sikujua  kama  nina umaarufu ,  kufika tu  simu zimeanza kuingia watu wanataka  kuonana na mimi , sijui wamejuaje nipo  Tanzania, lakini muda wa kuwajali sina , kama

usingeniita ningekuwa zangu Rochester naendelea na utafiti”

Eliza mara baada ya kusikia  hivyo alijiuta akishangaa na alimwangalia  Hamza kwa maswali.

“Kwanini hukuniambia Dokta Flora ni maarufu 

hivyo , mimi nilijua ni daktari wa kawaida wa binadamu”

“Awe maarufu asiwe maarufu  , wewe mchukulie kama rafiki yako , wewe ni wa kwetu kwanzia sasa  haina haja ya kujiweka  nae mbali”Aliongea Hamza na Eliza alifurahi kusikia hivyo.

“Dr Flora , umekwisha kupitia  taarifa ya matibabu ya mama yangu , umeonaje?”

“Hali yake sio nzuri ,  lakini haimaanishi kwamba hana nafasi ya kupona , mpaka nitakapomfanyia uchunguzi   ndio nitajua zaidi,  taarifa ambayo  mmenipatia  haijazingatia vitu vingi  hivyo ni ngumu kuwa na  suluhisho, teknolojia ya tiba imeendelea ila kwa hapa   Tanzania naona  bado sana”

“Kwahio Dokta unamaanisha unaondoka na  mama yangu kwenda Marekani  moja kwa moja?”

“Ndio , mimi naondoka kesho kutwa , kuhusu  mama yako  utaratibu wa kusafirishwa utakamilika ndani ya wiki moja”Aliongea na  Eliza baada ya kusikia hivyo alisita.

“Vipi kuhusu  malipo ya gharama za matibabu na mahitaji mengine?”

“Kwasababu ya Hamza nitakutajia bei ya chini tu, unaonaje tukianza na Dollar milio…”

“Utalipia dollar elfu kumi ambazo ni sawa na  milioni ishirini na tano za kitanzania”Aliongea Hamza akiingilia  lakini kauli yake ilimfanya  Dokta Flora mikono yake kutetemeka huku akimkazia macho  Hamza.

“Milioni ishirini , kumbe rahisi hivyo?”Aliongea Eliza kwa mshangao , wakati  anakuja hapo alikuwa akiwaza matibabu yatakuwa ni zaidi ya  milioni mia moja kama mgonjwa wake atasafirishwa na alikuwa akiwaza kwenda kumpigia magoti bosi wake Regina ampatie mkopo.

Upande wa  Hamza alimwangalia  Dokta  Ronica na tabasamu na kisha alibadilisha lugha na kuanza kuongea kiitaliano.

“Unathubutu vipi  kupokea  gharama za matibabu  kumtibu mama mkwe wangu, Unataka niipige bomu Mayo clinic”

“Gharama ya  chini  ya matibabu ni bilioni ishirini  na hapo sijajumlisha  ya makato kwenda kwa Mwanafalme wa Saudi Arabia ,  utajiri wote huo uliokuwa nao  unanilipa hela ya maji , huu ni uonevu  , nimekuja  Tanzania kwasababu  ninaamini kuna mapato”

“Sikia  Flora  hela unazo za kutosha , huna haja ya hela wewe , isitoshe mimi saivi  sina hela , pesa zangu zote zimepotelea nje ya nchi , hivyo usifikire  kuona kama nitakulipa  hela nyingi, bado  najitafuta”Aliongea Hamza huku akiwa na usiriasi wa hali ya juu.

“Wewe  na mshikaji wako wa Saudi Arabia mnaninyanyasa sana mkihitaji kitu kutoka kwangu ,  ila haina shida chukulia  ninachofanya  leo hii ni zawadi  yangu  kwako kama mdogo wako  wakati wa ndoa yako na Eliza”

“Haha..  hayo ndio maneno sasa ..”Aliongea Hamza huku akicheka  , huku akijiwazia huyu chizi kaja  Tanzania akiwa na mawazo ya  kumchuna hela zake  lakini mpango wake umegeuka ndoto.

“Nyie mnaongea nini jamani ,  ni Milioni ishirini  au kuna makosa?”Aliuliza Eliza ambae hakuwa akielewa  Hamza na Dokta Flora wanaongea nini. “Gharama ni hio hio,  taasisi yetu imekuwa ikitibia  watu wengi kwa  bei rahisi  ili kujua mbinu  za kupunguza gharama za matibabu, hivyo usiwe na wasiwasi”Aliongea Flora.

“Kama ni hivyo mlikuwa mkitumia lugha gani   , Hamza ulikuwa ukijadiliana nae kunipunguzia bei , nitajisikia vibaya ukifanya hivyo?”

“Ni lugha   ya kirumi , nilikuwa  nikiongea maongezi binafsi kuhusiana na  mwalimu wake , hivyo tunaweza sasa kuongea kuhusu gharama , halafu  udaktari ni swala  la wito   kutoka kwa Mungu   haina haja ya kutanguliza malipo”Aliongea Hamza huku akicheka.

“Ndio Miss Eliza usiwe na wasiwasi sana kuhusu gharama”Aliongea  Frola aliekuwa akilazimisha tabasamu lakini moyo wake ulikuwa ukiuma hatari kwa uonevu wa Hamza..

Eliza alikuwa msomi , kuna kitu alihisi lakini kwasababu dokta mwenyewe ndio amesema aliishia kukubali tu.

“Sikutarajia kama utakuwa unajua zaidi ya kuongea kifaransa , kingeereza na kitaliano , unaweza kuzungumza lugha  ngapi?”Aliuliza Eliza  , kila kitu kilikuwa kikimwambia Hamza  ubini wake sio wa kawaida kabisa  lakini  pia  kuwa na uwezo wa kufahamina na dokta   kama huyo halikuwa swala la kawaida.

“Sijajua kuhesabu, halafu lugha ni kama zana  tu , sawa kabisa na kanuni ya kushikilia  spana au

Screwdrivers kufungua  nati tofauti tofauti , hakuna  kitu cha ajabu kuongea lugha nyingi”

Eliza  aliona kabisa  Hamza anaongea pumba ili tu kukwepa kumwambia ukweli  hivyo hakuuliza zaidi.

Lakini   mara baada ya kuona  Dokta huyo  ndio anaekwenda kumtibia mama yake nje ya nchi , aliona kuna kila haja ya  kumfahamu  ki undani.

“Dokta Flora  uaonekana kuwa mdogo mno ,  hakuna mtu ambae  anaweza kuamini wewe ni daktari mkubwa, utakuwa ni moja ya madaktari  vijana  katika fani ya  tiba”Aliongea  Eliza na kauli ile ilimfanya Hamza kukohoa kwa kupaliwa, upande wa  Flora  alijisikia vizuri .

“Kama ni hivyo otea nitakuwa na umri gani?”Aliongea akiwa na tabasamu na kana kwamba anamrahisishia  Eliza kujua umri wake alianza kuchezea nywele zake, isitoshe  nywele ni kiashiria kikubwa cha umri .

“Umri wako utakuwa kati ya miaka  ishirini na nane kwenda therathini”Aliongea  na kumfanya  Flora kucheka.

“Hamza, your girlfriend said that  I am  between 28

to 30 years old , she is really a cute little  girl”Aliongea  Flora na kumfanya Eliza kumwangalia  Hamza.

“Hamza nimekosea wapi?” aliongea Eliza na kumfanya Hamza kukuna kichwa, ila hakumlaumu  kabisa Eliza.

“Ana miaka sitini na sita  huyo?”

“Nini!!?”

Eliza alijikuta akimaka  kwa sauti kiasi kwamba kushitua watu waliokuwa ndani ya mgahawa huo. 

Eliza  aliona anachezewa akili kabisa  na aliishia kuziba mdomo  wake na kujiambia  yaani hawa watu wanamuonaje kwa mfano ,  hakukuwa na uwezekano  msichana mrembo  namna hio kuwa na miaka sitini na sita.

“Usishangae sana  Eliza nilichokuambia ni ukweli , hata wewe kama utakuwa mtaalamu   wa maswala ya tiba  na kuwa na mbinu za kuuboresha mwili   unaweza kuwa  kama yeye miaka arobaini ijayo , lakini unapaswa kuwa na pesa nyingi pia”Aliongea Hamza.

“My research is  mainly focused  on extending  the life  of humans  , so it  is not difficult  for me to make myself look younger”Aliongea  Dokta Flora akimaanisha kwamba   tafiti zake anazo fanya ni  kujua namna ya kurefusha maisha ya binadamu na yeye kama mtafiti sio ngumu kujitengeneza na kuwa kijana zaidi.

Ijapokuwa Flora alielezea kwa  namna hio lakini ilikuwa ngumu bado kwa  Eliza kuamini  , lakini   kwa namna moja ama nyingine  alikuwa akionea wivu   muonekano wa  Flora.

Alikuwa akimwangalia  Flora kwa macho ya uchunguzi , hakuwa akiamini kabisa  kama mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa ni  bibi yake , lakini kwasababu sayansi ilikuwa ni njia ya  uwezekano  mwingi  aliona   pengine yote ni kweli , isitoshe dunia imejaa siri nyingi. 

Baada ya  kumaliza kula  waliagana ,  Dokta Ronicas alirudi hotelini kwake huku Eliza akiendesha gari.

Njjia nzima Eliza alikuwa akimwangalia Hamza kwa kuibia ibia , alionekana kama mwanamke mwenye maswali mengi.

“Ijapokuwa   mimi mpenzi wako ni  handsome sana , haina haja ya kuniangalia muda wote”Aliongea Hamza.

“Halafu lini nimekubali kuwa mpenzi wako?”

“Hata kama hujakubali , ni bure tu , kwa vyvoyote vile moyo  wako  umeshakubali”Aliongea Hamza kwa  tabasamu la uchokozi.

Eliza aliishia kuinamisha kichwa chake chini   kwa aibu za kike , na mara baada ya kufikiria kwa muda alimwangalia Hamza. “Hamza  .,,, Asante sana”

“Huna haja ya kunishukuru , wewe niambie ni lini utanipikia”Aliongea Hamza huku akimkonyeza.

“Unaonaje Wikiend ukija  nyumbani , nitakupikia chakula kitamu sana”

“Dili, usije  kubadilika”Aliongea Hamza kwa furaha ,  huku akijiwazia kwenda kwa Eliza kuna mambo mengi yanaweza kutokea , pengine  ukaribu wao unaweza   kuongezeka zaidi na zaidi.

Lakini  Hamza alishangaa kidogo mara baada ya Eliza  kupoteza tabasamu  usoni mwake  , alionekana kana kwamba alikuwa na wasiwasi.

“Eliza  unafikiria nini , au  bado hujakubaliana na mama yako kwenda kutibiwa nje ya nchi?” “Hapana , Dokta Flora anaonekana sio  daktari wa kawaida  na  ninaamini atamtibia mama vizuri … lakini. , wakati nilivyoona namna unavyoongea nae kiitaliano leo hii , ghafla tu nilihisi , siwezi kufiti kwenye ulimwengu wako”Aliongea Eliza.

Hamza alishangazwa na kauli hio , hakutegemea Eliza  angekuwa na mawazo ya namna hio  , lakini hata hivyo alielewa hisia zake.

“Kwamba huamini maisha yangu ya nyuma?”

“Sio kama siamini , ila  najihisi  kuna umbali mkubwa kati yetu”Aliongea   na Hamza alitaka  kumbembeleza  kwa maneno  lakini ghafla tu mwili wake ulimsisimka mara baada ya kunusa hatari ya   kupata ajali.

Previoua Next