Liam baada ya kusimama aliskilizia kwa sekunde kadhaa aliudii kitandani na kujisemea ndio kwanza hajamaliza hata siku moja lakini tayari kuna watu wamesha tumwa kushugulika nae
Mlango wa chumba 408 ukafunguliwa kimya kimya, kwa kutumia kifaa maalum. Wanaume watatu waliingia, wakiongozana na mmoja alie onekana kua kaitika umli wa miaka 40 adi 50 alionekana kua ndio kiongozi wao wengine walikua ni vijana tu ambao dam zao bado zinachemka na walikua na maumbo yaliyo jazia misuri wote walivalia suti uku shingoni wakininginiza vitambulisho walionekana
Liam baada ya kuwaona vizuri watu hao aliweza tutambua hisia zake hazikua sawa kwani kutoka na na uzoefu wake aliamini moja kwa moja watuao watakua ni wana usalama
Wewe ndio liam. Alisema mtu yule alie onekana kua kiongozi
Liam. Alinyanyua mkono wa kushoto, akawapungia hewani kama mtu anayewasalimia watoto wa nursery.
“hey mna shida gani mbona mnaingia bila ata hodi nikisema mmenivamia nitakua nakosea. Alisema liam
Bwana alie kua anaonekana ndio kiongozi aliwageuzia macho wenzake na kuludisha umakini kwa liam na kusogea mbele. Alikuwa mweusi wa asili, mwenye macho makali kama mchora ramani wa roho.
“Jina langu ni Inspector DCI Evans Mshindo. Tuko hapa kwa magizo ya kukuchukua kwa mahojiano hii ni kwasababu za kiusalama. Kila kitu kiko kisheria. Hivyo tuna kira haki za kukukamata hivyo usifanye mambo kua magumu vinginevyo tutalazimika kutumia nguvu
Liam kusikia hivyo aligeuka taratibu, akakaa pembeni mwa kitanda, akatikisa kichwa na kusema
“kishindo? Ndio jina lako? Duuh... linatisha. Ila si tishio. Sawa, nimeelewa. Naona nimeanza kuwashtua mapema.”
OK Inspector kishindo unaonaje unikiacha nikapumzika kwanza alaf kukikusha ndio uendelee na zoezi la kunikamata kwa maana ni usiku saiv ata maswali mnayo taka kuniuliza ntashidwa kuwapa majibu mazuli. Alisema liam uku akitabasamu
Sisi Tunafata maagizo hivyo unatakiwa kutii vinginevyo atutakua na jinsi zaidi ya kutumia nguvu. Alisema inpecta kishido
Capten unambembeleza sana alaf anaonekana kutudhalau kama vipi tumshkishe adabu. Alisema bwana mmoja miongoni mwa watu alio kuja nao inpecta Mshindo na kuanza kupiga atua kumsogolea liam.
Lakini kabla hajamsogolea zaidi liam alizuiwa na inpecta mshindo kujiamini kwa liam kulimfanya inpecta Mshindo kua na tahadhari kwani kwa uzoefu wake wa zaidi ya miaka 25 hakuwahi kwenda kumkamata mtuhumiwa na mtuhumiwa kuto onyesha hofu yoyote hali hiyo ilimfanya kua makini na Liam.
Lakini kwa muonekano wa liam aliamini hana kitu chochote cha ziada cha kumhofia aliona labda kujiamini kwa liam anaweza kua anatoka katika familia ya kitajir au yenye wazfa flan uko nje ya nch maana alikua na taalifa kua mtu kuyu ni leo hii ndio ameingia Tanzania hivyo alijiambia kama ni hivyo ilimladi amli ya kumkamata imetoka kwa mkubwa wake hatokua na kosa kama mambo yatakwenda ndivyo sivyo
Hey bwana mdogo usifanye mambo kua magubu tafadhali ongozana na sisi. Alisema inpecta Mshindo
Liam alijisemea kimoyo moyo nisiku yake ya kwanzatu alipanga kuitumia kwa kupumzika lakini watu hawa wamekuja kumuhalibia usingizi wake. Ata hivyo aliona acha tu akubali kuondoka nao ukizingatia ndio kwanza qmeingia nchini
Liam Akasimama, akavaa t-shirt aliyokuwa ameitelekeza kwenye sofa.
Watu wale walikaa kimya. Walimchunguza kwa macho. Kuona aanataka kufanya nini Hakukuwa na dalili ya uoga — si kwa sura, si kwa sauti, si kwa miili.
Liam Aliinama kuchukua simu, kisha akawatazama.
“Oke Twende basii.” alisema liam uku akitabasam na kuanza kuongoza njia na watu wale walimuweka katikati kama kumlinda
Wakiwa kwenye lifti, Evans Mshindo alimtazama kwa pembeni.
“Unajua kwanini tumekukamata ,?”
Liam akashtua bega lake kidogo kwa kebehi.
“afande sasa mimi ntajuaje. Alisema liam na kumfanya afande au inpecta Mshindo kukaa kimya
Walipofika chini, gari jeusi aina ya Prado lilikuwa tayari likisubiri. Mlango ukafunguliwa, Liam akaingia kwanza, kama anaalikwa kwenye cocktail ya Waziri wa Mambo ya Ndani. Askar wawili waliingia pia nyuma na kumuweka liam kati kati
Liam Akaangalia wale maofisa, kisha akawauliza:
“By the way... mnaonaje tukisha fika mniagizie budget ya kahawa? Alisema liam uku akitabasam
Askari wale kusikia hivyo Mmoja akacheka kimya kimya. Evans Mshindo hakusema kitu. Lakini alijua moja:
Mtu huyu si wa kawaida. Kutokana na uzoefu alio kua nao
Baada ya dakika kadhaa gari lilisimama mbele ya jengo la ghorofa lenye ulinzi mkali. Ilikuwa ni moja kati ya vituo vya siri vya usalama vilivyojificha katikati ya jiji ambapo ni ngumu kudhania kua jengo hilo ni la usalama,
Walipomshusha, Liam alishuka taratibu kana kwamba alikuwa anashuka kwenye zulia jekundu la Golden Globes. Akaangalia jengo, akakunja uso kisha akasema:
“Aise hii ni mala yangu ya kwanza kukamatwa na akari duu nakupa hongela sana bana kishindo. Alisema liam huku akitabasamu liam alikua akifanya makusuki kumuita afande huyo kishindo ili kumkela tu lakini bwana huyo alionekana kua mtulivu
Waliingia naye ndani kimya kimya. Baada ya kuingia walikutana ka kordo ndefu walitembea kidogo na kukunja kushoto wakatembea hatua kadhaa na kukutana na mlango waliingia na kutokea seemu iliyo onekana kua ni mapokezi
Na upande wakulia wa mapokezi kulukua na lift na walitembea kuisogelea na walimuamulu Liam kua wa kwanza kuingia na wao walifata lift ilianza kushuka chini na kitendo kile kilinfanya Liam kushanga kwake yeye alitalajia wangepanda juu lakini ilikua ndivyo sivyo
Baada ya lifti kufunguka walitoka n walikutana na korgo nyingina ilikua ndefu na pembeni kulikua na milango ya vyumba walitembea mpaka mlango wa mwisho na walimuingiza liam liam kulikua na meza ilio tenganisha viti viwili
Adande Mshindo alimuamulu liamu kukaa kwenye kiti moja wapo alikaa nai wakamfunga pingu kwa kuunganisha na meza kisha walitoka na kumuacha liam pekeake
Liam alijiwazia walishindiwa nini kumfunga ping tangu wakiwa hotelin na kuishia kusikitika aliangaza huku na kuku na kuona camera ilio kua ikimmurika
Muda mfupi baadaye, mlango ulifunguliwa na afisa aliyevaa suti ya kijivu aliyekuwa na uso mkali na macho yasiyo na wasiwasi wa aina yoyote
"Jina lako kamili tafadhali." Alisema kwa sauti ya amri.
"Liam Carter," Alisema Liam kwa utulivu huku akiegemea kwenye kiti. "Lakini wengine huniita 'Tatizo lisilopimika'."
Afisa hakutabasamu. Alichukua daftari lake na kuanza kuuliza maswali.
"Ulikuwa ukifanya nini Lush Bay Hotel usiku huu?" Alisema kwa ukali.
"Nilikuwa nikijaribu kupumzika baada ya safari ndefu ya maisha." Alisema Liam kwa kejeli.
"Unafanya kazi gani hasa?" Alisema afisa mwingine aliyekuwa nyuma ya kamera.
"Mimi ni mpelelezi wa ndoto zangu." Alijibu Liam huku akitikisa kichwa, "Na ninafanya kazi kwa niaba ya amani ya ndani."
Afisa wa kwanza aligonga meza kwa hasira. "Huu sio mchezo, Carter. Tuna taarifa zako. Tumeona hakuna rekodi zako zozote zaidi ya kua ulizaliwa Tanzania na uliondoka hujulikani ulikua wapi na unafanya nini alisema afisa kwa kufoka
"Liam aliamua kua siliazi Basi mtafute taarifa zangu vizuri zaidi. Huenda Kuna watu katika serikalini yenu watakua na access zaidi ya ninyi." Alisema Liam kwa saut ya mkazo.
Kwa muda wa zaidi ya saa moja walijitahidi kumvuta Liam azungumze kitu cha maana, lakini kila jibu lake lilikuwa limejaa mzaha, kejeli au utulivu uliowachanganya. Hawakutaka kutumia nguvu kutokana na kuto kua vizibitisho vya moja kwa moja amri
Nyinyi mnacho fanya apa ni kua na makisio tu wala hamna ushaidi mnacho fanya ni kama kutaka mimi nikili kua muhalifu wakanti mimi laia mwema na nilicho afanya ni kuludi kwenye nchi yangu kama hali itaendelea hivi mnaonaje nikishilikisha mwanashelia mwangu. Alisema liam
Lakini kabla hajajibu, afisa mmoja aliingia haraka akiwa na bahasha mkononi. Alimsogelea mwenzake na kunong'ona nae kwa haraka.
Wakamwangalia Liam kwa mashaka.
"Vipi tena?" Alisema Liam huku akiinama mbele kidogo,
Afisa wa pili aliufungua mdomo kwa shingo upande. "Bwana liam.. Inaonekana hakuna ushahidi wa kutosha wa kukushikilia. Lakini nikupe angalizo kila atua unayo piga tuko nyuma yako
"Asante sana ma afande" Alisema Liam kwa furaha ya dhihaka, "Ningetaka chai lakini sasa muda umeisha."
Alifunguliwa pingu na kuiinuka kutoka kwenye kiti, kisha walimuongozo kuelekea mlangoni.
"Tutakuwa tunakufuatilia nyendo zako hivyo kua makini." Aliongeza afisa wa yule
"Oka afande nawatakia kazi njema Fuatilieni kwa makini.
Ilikua ni majila ya saa7 usiku ndio muda ambao liam Alipotoka nje, aliangaza anga la jiji lililokuwa na mwanga hafifu ulio sababishwa na taa zilizo kua zikiwaka. Akavuta pumzi ndefu, macho yake yakitulia alitembea mdogo mdogo hakua akijua mtaa aliopo kutokana na kua sio mzoefu sana wa jiji baada ya ya kutembea kwa umbali kadhaa aliweza kuona taksi alisimanisha kuingia
Baada ya muda aliweza kufika hotelini alikua amechoka sa mizunguko na pulikushani zilizo tokea siku hiyo hakuitaji kufanya jambo lolote zaidi ya kujipumzisha
Ilikua ni Asabuh aliangalia saa ilikua ni mida ya saa5 asubuh Hakuwa na mawasiliano mapya. Simu yake ilikuwa kimya kama hakukua na mtu alie mtafuta. Lakini sasa, hakuhisi kukasirika wala kukosa subira.
Alibofya kitufe cha simu ya mezani, akapiga huduma ya chumba.
“Naomba kuletewa kifungua kinywa
Dakika kumi baadaye, mhudumu akaleta. Liam akatapa kifungua kinywa polepole huku akitazama bahari kupitia dirisha. Baada ya kula, alihema kidogo kwa furaha,
“Baada ya kumaliza aliona kuendelea kuka ndani ataboeka ivyo alifikilia angepata ata mtu wa kumpa kampani
Mara moja akamkumbuka yule msichana wa mapokezi – mwenye tabasamu la dhahabu, macho makubwa ya kuvutia na sauti tamu yenye vionjo vya pwani. Edina.
“Why not?” Alinong’ona kwa sauti ya kicheko, akajipiga kiganja begani na kutoka chumbani akiwa na shati la mikono mifupi na suruali ya khaki nyepesi.
Alifika mapokezi na alipo angaza aliweza kumuona Edina aliekua akimtafuta mwanamke huyo hakua akiudumia hivyo alitombea kumsogelea mrembo huyo
“Hey, Mrombo Edina... unanikumbuka?”
Edina alitabasamu kwa aibu kidogo, lakini akajibu kwa haraka.“Yaa siwezi kukusahau,.”
Liam alicheka.
“Ok mi nimngeni aapa nchini Nilihitaji tu... ah, ulafiki. Unaweza kua rafiki yangu?” alisema liam
“sawa hakuna shida ivi ulisema unaitwa nan vile?” Alisema Edina kwa ucheshi.
Jina langu ni liam. Alijibu uku akitabasam
Vip tunaweza kutembea tembea kidogo . Aliuliza Liam
kutokana na zamu yake ilikua imeisha na likua huru hivyo alikubali mara moja
Walitoka nje ya mapokezi, wakakaa kwenye bustani ya hoteli, pembeni ya mwanga mdogo wa taa. Edina akiwa na sare yake ya kazi, Liam akiwa kama vile anatoka kwenye onyesho la mitindo ya jioni.
“Wewe ni mzuri kupita kiasi kuwa mapokezi tu, Edina. Hakika mtu atakayekupoteza atakua kipofu wa moyo.” Alisema Liam huku akimtazama kwa jicho la dharau ya kupendeza.
“Wewe ndio mgeni pekee ambaye anaongea kama mwanasiasa wa mapenzi.” Alijibu Edina huku akicheka.
“Usinibebe vibaya, Edina... mimi ni mtu wa ukweli. Nimezunguka dunia, lakini tabasamu lako linaweza kufanya mtu asahau hata nywila ya benki.”
Edina alijigeuza kidogo, akajifunika uso kwa mikono yake.
“Usinifanye nicheke ka sauti kali, manager ataniona kama nimechanganyikiwa.”
Mazungumzo yao yaliendelea kwa dakika zaidi ya arobaini. Waliongea kuhusu Dar es Salaam, vyakula, vichekesho vya wateja, na hata tofauti ya chai ya Tanganyika na kahawa ya Colombia.
Ilionekana kama marafiki wa zamani waliokutana baada ya miaka mingi.
Mazungumzo yalichukua muda mrefu kidogo, Liam alisimama na kusema:
“Sikujua Dar ina watu wa dhahabu... mpaka nikakuona. Nashukuru sana kwa muda wako, Edina. Leo nimeinjoy sana compani yako... alisema liam”
“Nami nimefurahi kukujua zaidi.” Alisema Edina kwa tabasamu.
“Ni mwanzo tu... nina mengi ya kushangaza.” Alijibu Liam.
Waliagana kwa tabasamu. Edina akarudi kazini, Liam akarudi ghorofani.
Ni takribani wiki ilipita tangu Liam aweze kuingia nchini Tanzania na katika wiki yote mtu ambae alikua kama mwenyeji wake alikua ni edina dada wa mapokezi wiki hiyo liam aliitumia kujipa uzoefu na kutembelea baadhi ya maeneo ili kuuzoea mji
Ilikua ni usiku wa juma tano mwajila ya saa2 usiku
Liam aliamua kutoka hotelini, akahisi kuchoka na mpangilio wa kawaida. Hakutaka kwenda klabu wala baa; alitaka kutembea na kufikiri. Liam alikua mtaa wa Mwenge, karibu na sehemu za viwanda ambazo huwa tulivu usiku.
Alikuwa amevaa sweta nyepesi ya kijivu na kaptura ndefu. Aliingia katika mtaa mmoja wenye giza hafifu, taa chache zikipepesa pepesa mithili ya roho zinazokufa.
Wakati alipoanza kukata kona ya pili, hewa ilibadilika.
Haikuwa hewa ya kawaida.
Ilikuwa nzito—kama mvuke wa barafu unaopanda juu ya ngozi na kuchoma mishipa.
Akasimama. Hakuhitaji kuambiwa. Alihisi uwepo wao. Ilikua ni muda tangu alipo isi anafuatwa na watu walio kua wanamfata walikua si wa kawaida uwepo wao aliuhisi muda ndio maana akaamua kuchakua uelekeo ambao ni tulivu na hauna watu
Kutoka gizani, watu wanne walijitokeza, wote wakiwa wamevalia mavazi meusi, vinyago vya ajabu vinavyong’aa kwenye paji la uso, na macho yao yakimetameta mithili ya moto wa bluu. Haikueleweka walikua ni watu wa bala lipi kutokana na mavazi yayo yalikua yamewafunika mwili mzima ila watu wale waliongea kiswahili fasaha
“Liam Carter,” mmoja wao alisema kwa sauti ya kina na baridi. Tume pata taalifa kua wewe ndio mtu unae miliki Luminark hivyo kwa usalama wako tupatie nasi tunaadi kuacha hai vinginevyo usije kutulaumu
Liam alitabasamu kidogo, kisha akavuta pumzi ndefu.
“Luminark? Kwa hiyo nyie ndo mmefuata hicho kitu?”kwani hiyo Luminark ni nin maana ndio mala ya kwanza nasikia kutoka kwenu liam aliongea kwa utulivu wa ajabu.
Mmoja wao akasema kwa kejeli bwana mdogo kama hutotupatia tunacho hitaji usifikilie kama utatoka salama hapa
“Tutakichukua kwa lazima
“Ooh Basi sikilizeni ikiwa mnaamini kua mimi ndie ninahiyo Luminark basi msifikilie kua kuwa nitawakabidhi kilahisi. Ni lazima mniue kwanza ndio mchukue. Alisema liam
Bwana mdogo kwakua unajifanya mjeuli basi tutakuonyesha. Alisema mmoja wa wale watu
“Basi karibu... mjaribu bahati,” alijibu Liam uku akiwa na tabasamu.
Walijirusha kwa kasi ya ajabu. Mmoja akaenda juu, mwingine chini, wawili wakizunguka pande zake. Mikono yao ilianza kutoa nuru za ajabu, mithili ya nishati ya giza iliyochanganywa na moshi wa kung’aa.
Liam hakusogea hata kidogo lakini Alifunga macho sekunde moja, kisha akafungua tena — macho yake yakawaka kwa mwanga wa hudhurungi yalio kua yakin'gaa kwenye giza.
Alipoona wa kwanza akimfikia, aligeuka kwa kasi isiyo ya kawaida, akampiga ngumi iliyozalisha miale ya rangi nyekundu. Yule mtu akarushwa mita kadhaa na kuanguka kama gunia na papo hapo mwili wake ukaanza kuganda... Sekunde tatu baadaye, alibadilika kuwa jiwe jeupe linalong’aa kama almasi na kupasuka vipande viwili.
Mwingine akaruka kutoka juu, akizalisha miale ya moto uku mkononi akiwa na upanga mweusi ulio kua unatoa mwanga mweupe uliochanganyika na miale ile ya moto na kuufanya kua wenye kuvutia. Liam alikwepa na kuushika ule upanga mikononi mwake, kisha akauvunja vipande viwili kana kwamba ulikuwa ni fimbo na pale pale alikishika kile kipande chaupanga na kumchoma yule mtu kwenye shingo kisha akamsindikiza na teke lililo mmlusha mita kadhaa. Akaanguka chini kwa kishindo... na sekunde mbili baadaye — naye pia akabadilika kuwa jiwe la kung’aa.
Watu wale walipigwa na butwaa kwa mtu uyo kuwaua kwa shambulizi mojamoja na kingine kuvunjwa kwa upanga kwani upanga uo si kwamba ni wa kawaida bali ni mgumu sana na ngingumu kuvunjika ukichangana na nguvi ya ajabu ulio kua nayo walishangaa kwa liam kuweza kuuvuja na pale pale waliona mtu walie mfata si lahisi kama walivyo zani
“watu dhaifu kama nyinyi mnathubutu kujitokeza mbele yangu na kutaka Luminark. haha hakika mnaflaisha sana. Alisema liam kwa tabasamu
Waliobaki wawili wakaanza kushirikiana—walianza kuongea lugha isio eleweka, walikua wanamzunguka liam kwa kasi, na kufanya duara la moshi uliochanganyikana na miale inayo ng'aa wenye nguvu kumzunguka pia. Liam hakutaka kusubili wamalize kile wanacho kifanya hivyo pale pale, alinyanyua mkono wake wa kulia juu, na mkono wake ukang'aa — na kwa ghafla mwanga mkali ukapasuka kutoka mwilini mwake, ukafagia hewani, ukiyakata mawimbi ya giza kama upanga.
Ardhi ikapasuka kwa mlipuko wa mwanga huo na watu wale walikunbwa na wimbi la nguvu isiyo ya kawaida na kuwafanya kulushwa mita kadhaa
Wote wakaanguka chini, wakitetemeka. Liam akawaangalia akiwa amesimama juu ya kifusi cha vumbi lililotanda.
Hatimae pakawa Kimya Giza lilitulia tuli
Liam aliangalia kwa sekunde chache miili ya watu wale iliokua imegeuka mawe yanayong'aa mithili ya armas. akavuta pumzi ndefu. Na pale pale kwa sauti ya chini, alianza kunong’ona maneno yasio eleweka kugha yake.
Palepale miili ile ilio kua imegeuka mawe pamoja na Vipande vyote vilivyo zagaa vilianza kuyayuka kisha taratibu vikaondoka hewani — vikayeyuka kama moshi wa nuru, vikatoweka bila hata chembe ya ushahidi.
Kisha liam aliyafumba macho yake yalio kua bado yanatoa mng'ao na baada ya kuyafumbua yalikua yameludi katika hali ya kawaida
Will continue
Comments