MASAA KADHAA NYUMA.
Jaususi Mstaafu Amosi hakutaka kuchelewa hata dakika moja mbele ya Kanali Dastani , alijua akifanya kosa tu atawahiwa ndio maana usiku huo huo mara baada ya kumuwekea kirusi Kanali katika chumba cha Pub ile moja kwa moja alianza kufanya uchunguzi juu ya wapi ataweza kumpata Mchuku, mkuu wa Gereza.
Katika ujasusi wake kuna mambo makuu mawili ambayo alipata , kwanza alijua kuna mfungwa ambae amehusika na kesi ya Sedekia ambae yupo gerezani , jambo hili hakuwahi kulisikia hapo kabla licha ya kwamba ni swala ambalo lilitokea wakati yeye akiwa kitengoni , hakujua kwanini swala hili lilifichwa sana.
Swala la pili nin mahusiano ya Tresha Noah na Kanali , alikuwa akijua fika Mheshimiwa Raisi ambae anakwenda kumaliza muda wake alikuwa ni raisi ambae anapenda warembo , hili lilikuwa swala la wazi mpaka kwa watanzania , licha ya kwamba Raisi Elias alifanya makubwa katika uongozi wake lakini udhaifu wake ilikuwa ni wanawake , tokea siku ambayo alifiwa na mke wake akiwa madarakani ndio aliongeza moto.
Ukweli ni kwamba wakati wa kifo cha First Lady kinatokea sekeseke liibuka huku ikiaminika ni raisi huyo kumuua mke wake baada ya kumsaliti na moja ya tajiri Mkubwa aliekimbia nchi na kuishi uhamishoni kwa muda mrefu.
Wengi wanaamini kutokea kwa kifo cha First lady kulimfanya azidi kubadilika tabia na kuendekeza ngono, lakini kwanzia hapo Raisi Mbilu alikuwa makini sana na wanawake ambao anatembea nao , hata kama hakuwa akiwapenda lakini hakutaka wamsaliti , pengine ilikuwa ni Trauma aliopata kutoka kwa mke wake ambae inasemekana alimpenda sana.
Sasa Amosi kujua swala la mwanamitandao ya kijamii maarufu Tresha Noah kuwa na mapenzi ya siri na Kanali ilikuwa ni kete ambayo kwake aliona itafikia muda atatakiwa kuicheza vizuri na sio kwa kurupuka.
Kutokana na swala la mfungwa huyo kuwa siri , hakujua moja kwa moja atakuwa yupo gereza gani na njia pekee ambayo aliona inaweza kumpa majawabu ya haraka haraka ni kupitia kitengo cha TISA(Tanzania inteligence service Agency).
Lakini hata hivyo asingeweza kupata taarifa hio ya siri kwa uharaka bila ya kutumia mtu mwenye madaraka na pia katika mazungumzo ya Kanali Dastani alisikia Waziri akihusishwa hivyo moja kwa moja aliona sio jambo jepesi.
“Shit.. nimesahau kitu muhimu Mchuku ni mkuu wa Gereza hivyo ni rahisi kufuatilia anahudumu katika gereza lipi kupitia Mkuu wa Magereza”Aliwaza Amosi huku akijiona mjinga,kwanini hakufikiria njia nyepesi hio.
Dakika ileile baada ya wazo hilo kumwingia alisimamisha IST yake pembeni na kulitafuta jina la moja ya Askari polisi ambae aliamini lazima atakuwa na taarifa ya wakuu wa Magereza kwa upande wa jiji la Dar es salaam, alienda kwenye majina mpaka akalifikia jina la Afande Chika na kupiga simu lakini jibu ambalo alipata lilimkatisha tamaa , simu yake haikuwa hewani , lakini hata hivyo aliona haina haja ya kukata tamaa , alitafuta namba nyingine , jina lilikuwa ni Sajenti Ulimboka na alipiga na simu iliita dakika chache na kupokelewa na kuanza kusikia makelele.
“Amosi nipigie baadae , nipo eneo la tukio’Sauti upande wa pili ilisikika na kumfanya Amosi kukunja ndita.
“Ulimboka namuulizia Afande Chika, hapatikani hewani kupitia namba yake ya kawaida”Aliongea Amosi kwa haraka haraka.
“Amosi unaemtafuta jeshi la polisi pia linamtafuta , sijui kwanini unamtafuta ila kwasasa nipo kwenye majukumu ya kazi, nipigie
asubuhi”Aliongea Ulimboka na kabla hata hajampa maelezo Amosi ya kueleweka simu ilikatwa palepale na kumfanya Amosi kutamani kutoa tusi.
Mpaka hapo koneksheni yake polisi ilikuwa ishafika mwisho , Amosi licha ya maisha yake mtaani kuonekana kama vile ni ya kihalifu hakuhitaji kujuana na askari wengi polisi , alihitaji afande mmoja tu mwenye nguvu na ambae anaishi kifisadi na huyu alikuwa ni Afande Chika.
Asichokijua Amosi ni kwamba Afande Chika aliingia katika mikono ya Chatu na haieleweki alifichwa wapi mpaka kutokuonekana kwake au amekufa au lah.
Baada ya kukosa jibu la haraka haraka aliona amuhusishe bosi wake wa kazi ,yaani Brigedia Doswe , ilikuwa ndio njia yake ya mwisho kutaka kupata kile anachohitaji tena mapema mno.
Hakujali muda ni saa ngapi na ingeonekana ni ukorofi wa namna gani kumpigia Brigeida muda huo lakini kwasababu jeshi ni kazi ya wito pia, hakujifikiria mara mbilimbili na kupiga simu na iliita kwa muda mrefu bila ya kupokelewa , alipiga mara nyingine na haikupokelewa na aliamini moja kwa moja Brigedia huenda amelala hivyo aliona labda afanye asubuhi asubuhi , jambo la uhakika tu ni kwamba Brigedia angeona missed call zake angempigia.
Amosi kinyonge alirudi garini na kuliwasha kisha taratibu aliliingiza barabarani huku mpango wake ni kurudi nyumbani kwa ajili ya kupumzika, akiwa njiani alikuwa akifikiria kauli ya Ulimboka juu ya DCP Chika kutafutwa na polisi, ilikuwa kichekesho kwake , yaani polisi anatafutwa na polisi wenzake, alijua lazima kuna kitu kinachoendelea.
Wakati akiwa katika mataa ya Mwenge ili aelekee Mikocheni kwenye apartment yake simu yake ilianza kuita na alipoangalia anaepiga ni Brigedia , palepale alipunguza mwendo wa gari na kupokea simu. “Jambo Afande “
“Jambo ,Amosi habari za usiku , kuna taarifa yoyote?”Aliongea Brigedia na sauti yake iliashiria haraka na Amosi alilitambua hilo.
“Nimepata uelekeo wa ile kazi ya Wabrazili , nilimfuatilia Kanali na nimemsikia akiwa katika mazungumzo na moja ya wakuu wa Magereza wakizungumzia juu ya Mfungwa aliehusika na kifo cha Sedekia…”
“Amosi hebu acha kuendelea kuongea kwanza , Umesikia wapi hio taarifa nyeti hivyo ya daraja la kwanza kitengoni?”
“Mkuu ni kama nilivyosema nilisikia mazungumzo kutoka kwa Kanali Dastani..”Aliongea Amosi huku akijiuliza mbona amekasirika baada ya kusikia hilo swala , inamaana hata yeye alikuwa akijua na ameupiga kimya.
“Amosi kuhusu swala hilo ni sehemu ya siri za taifa kwa kushirikiana na washirika wetu wa nje , ni swala linalogusa diplomasia ya nchi , niambie unachotaka nikusaidie ni nini kwenye uchunguzi wako , ila achana na swala kabisa la mfungwa , sitoweza kukuepusha tena na kifo uking’ata zaidi ya usichoweza kumeza”
“Nataka kujua Afande Mchuku ni Mkuu wa gereza lipi Afande , nimejaribu kuwasiliana na Afande Chika lakini hapatikani hewani…”Aliongea na upande wa pili ulikuwa kimya na kumfanya Amosi kusimamisha gari mkabala na hoteli ya Krebyss.
“Amosi nipo na Afande Mafulu hapa CP wa mkoa , kama unaemzungumzia ni Afande Kigo
Mchuku taarifa za kifo chake zimeripotiwa sasa hivi kwa wakati mmoja na za DCP Chika , kuna uwezekano unachotaka kufuatilia kwa Mchuku ndio kimemuua akiwa chooni huko Fulu Dozi
Bar Segerea , alikuwa kaimu mkuu wa gereza la
Segerea baada ya Afande Simba kupalalaizi , Amosi kesho fika ofisini kwangu nadhani tuna la kuongea, kwasasa nakata simu nipo kwenye kikao”Aliongea na simu ilikatwa palepale
Amosi alijikuta akitoa macho , yaani ndani ya dakika kumi tu mtu ashapoteza maisha , akili ilijaribu kumwambia pengine ni Dastani lakini iligoma kabisa, Japo Kanali Dastani aliaminiwa kwa uwezo wake wa akili na ushapu lakini sio kwa namna hio ,kuna kitu tayari alikihisi pengine kuna muhusika mwingine , lakini swali liliibuka palepale , kwanini Mchuku afariki ndani ya dakika chache baada ya kuwasiliana na Dastani , akili yake ilimjibu lazima alichorekodi kina taarifa ya kutosha , swali lingine kama ameuwawa je alichorekodi kimechukuliwa na muuaji jibu hakupata na kwa haraka haraka aling’ata meno kwa hasira na kujiambia anapaswa kuwahi Fuludozi Bar eneo la tukio kabla ya taarifa hazijamfikia Kanali Dastani , aliamini lazima angepata kitu.
*******
Upande mwingine nusu saa mbele lango la nyumba ya mapumziko ya Mheshimiwa raisi
lilifunguliwa na gari aina ya V8 iliingia na palepale alitoka mwanaume mwenye muonekano mgumu kidogo mwenye masharubu.
Kama Amosi angekuwepo angemfahamu mara moja , ndio mwanaume ambae alimpiga risasi ya ubavuni mpaka kumpelekea kulazwa siku kadhaa katika hospitali ya jeshi.
“Nipo kwa ajili ya kuonana na
mheshimiwa”Aliongea bwana huyo mara baada ya kuzuiwa na bodigadi namba moja wa raisi.
“Mheshimiwa ametoa taarifa hataki usumbufu”Aliongea bodigadi yule akiwa na sura isiokuwa na utani , hakuwa na dalili yoyote ya kumpisha, sio kama hamjui alikuwa akimjua lakini alizingatia itifaki za ki usalama kwa mheshimiwa, hususani muda huo wa usiku.
“Ni swala muhimu Afande , napaswa kuripoti mara moja kwa mheshimiwa na kupotea” “Kama nilivyosema Mheshimiwa kapumzika, hakuna namna ya kuonana nae sasa hivi, kama una maagizo yoyote yaache hapa
nitayafikisha”Aliongea na kumfanya bwana yule kumwangalia kwa macho makali kidogo na alionekana kutulia kidogo na aliingiza mkono mfukoni lakini kitendo chake kilifanya walinzi wote kukoki bastora na kumnyooshea wakidhani anatoa siraha licha ya kumkagua getini, lakini bwana yule alinyoosha mkono juu kwa ishara ya kujisalimisha huku mkononi akionekana ameshika kitu.
Afisa huyu mkuu wa kitengo cha Itifaki mara baada ya kuona kitu kilichokuwa kwenye mikono ya yule bwana alinyoosha mkono na kuchukua.
“Ni taarifa ambayo nilipaswa kumpatia mheshimiwa moja kwa moja , kazi alioniagiza nimemaliza”Aliongea na Kanali Ashrak alimwangalia bwana huyo kwa macho ya umakini na kisha aliwapa ishara wenzake kushusha siraha chini.
Unajua nyumbani kwa raisi unaweza ukaruhusiwa kuingia getini lakini ukashindwa kupita mbele ya kitengo cha itifaki ya kumuona Raisi ambacho huongozwa na ADC mwenyewe , hiki ndio kilichomkuta.
“Bundi najua ukaribu wako na mheshimiwa na naheshimu hilo lakini kwasasa hali ya usalama kwa mheshimiwa imeimarishwa ni vizuri ukipotea mpaka pale mheshimiwa atakapokuhitaji yeye mwenyewe. This isn’t personal” Aliongea ADC na Bundi alitingisha kichwa kuelewa na kisha alisindikizwa na kutoka nje kabisa.
Kanai Ashrak aliishia kuangalia ile flashdrive na kisha alitoa tabasamu na kuiweka mfukoni na baada ya pale alitoa ishara kadhaa kwa wenzake na kuingia ndani, pengine alikuwa akipeleka ujumbe ule kwa mheshimiwa lakini mara baada ya kuingia ndani haikuwa hivyo , mmoja kwa moja alielekea katika chumba kingine ambacho ndani yake kilikuwa na tarakishi.
****
Kilichowaacha midomo wazi zaidi ni kwamba Yulia hakuleta ukinzani na zaidi sana alionyesha kufurahi kushikwa mkono na kutolewa nje, lakini kitendo cha Hamza kumtoa Yulia mpaka kwenye Korido mabodigadi waliingilia kati na kumzuia.
“Mkuu muachie bosi wetu , vinginevyo usitulaumu tukichukua hatua”Aliongea mmoja wapo lakini kauli yao ilimfanya Yulia uso wake kujikunja na kuwafokea.
“Ondokeni njiani , yoyote atakaemchokoza huyu mwanaume awe makini maana nitamtimua , kingine msinifuate”Aliongea na kufanya wafuasi wake kuangaliana kwa mshangao , hawakuwahi kumuona bosi wao kuwa legelege mbele ya mwanaume kama hivyo.
Hamza alimpeleka Yulia mpaka floor inayofuata upande wa balkoni sehemu ambayo aliona ni tulivu.
Mara baada ya kusimama alijikuta akivuta pumzi nyingi na kumwangalia mwanamke huyo , upepo wa bahari ndio uliowapuliza na kufanya nywele za kizungu za Hamza kupepesuka.
Hamza alikuwa akimchunguza mrembo huyo na kitu pekee alichoona ni kwamba hakuwa amebadilika kabisa , alikuwa mrembo vilevile kama alivyomuacha.
“Unaniumiza bwana mkono wangu”Aliongea na palepale alimfanya Hamza kukumbuka kumbe amemshikilia mkono huyo mrembo. “Sorry”Aliongea Hamza na kumuachia.
“Usiwaze unaweza kuendelea kunishika mpaka uchoke , kwasababu miaka saba iliopita ulikuwa muhuni zaidi ya hivi , kunishika mkono tu kuna tatizo gani?”
Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akimeza mate mengi na kutoa tabasamu.
“Hehe ,, mpaka leo unakumbuka”Aliongea Hamza lakini mrembo huyo ambae macho yake ni kama yamejaa maji aliendelea kumwangalia Hamza huku akionekana kuwa mbali kihisia.
“Imekuwaje upo hapa Tanzania, sehemu ambayo sijawahi kuiwazia utakuwepo hata mara moja?”
“Kuna mambo yalitokea na kunifanya kuchoka maisha niliokuwa nayo, nikaona nibadilishe mazingira na kwasababu ya kuijua lugha ya kiswahili vizuri Tanzania ndio niliona mahala sahihi”
“Unajua kiswahili?”Aliongea , ukumbuke hapa muda wote walikuwa wakitumia kingereza.
“Najua ndio”Aliongea Hamza kwa kiswahili na kumfanya Yulia kushangaa.
“Sikutegemea kama ungejifunza kiswahili na kuongea kama mzawa”Aliongea.
“Mimi ni Mzawa hivyo najua kiswahili vizuri tu siwezi kukuambia chochote lakini jua hivyo”Aliongea Hamza.
“Mwisho wa siku licha ya kuwa hapa nchini hujajua kilichotokea na kukutana kwetu ni kwa bahati mbaya tena, wakati ule hukutaka kunipatia hata mawasiliano yako na sasa unaanza kunificha pia” “Ni kwasababu mambo yangu hayahusiani kabisa na wewe , Madam unapaswa kujua sasa hivi mimi ni mfanyakazi na mwanachuo tu , hivyo yaliopita tuyaache yapite”
“Mwanachuo?, Mfanyakazi?”Aliuliza kwa mshangao , ilikuwa ni kama vile amegundua uwepo wa sayari nyingine katika mfumo wa jua kwa mshangao wake.
“Nipo Dosam pale msaidizi wa karibu kabisa na CEO?”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu la kejeli ni kama vile nafasi hio haikuwa ikimtosha, Regina na hasira zake za karibu angekuwepo pengine angemtukana. “Nini..isijekuwa umempenda bosi wa kampuni ya Dosam , Regina Wilsoni namfahamu vizuri alivyo mrembo”
“Hehe… najua CEO wetu ni mrembo lakini
haimaanishi kwamba nimempenda nipo kikazi zaidi”
“Siwezi kuamini , kwa uwezo wako si ni rahisi sana kupata pesa , isitoshe sidhani kama Regina anakufaa inasemekana ni mgonjwa wa aki…”Alitaka kuongea lakini alisita.
“Ni mgonjwa wa nini..??”Aliuliza Hamza akiwa siriasi na kumfanya Yulia kuonyesha kujutia palepale mdomo wake , lakini alijua ni kwasababu ya furaha kubwa aliokuwa nayo.
“Sina maelezo ya kutosha , taarifa hizi ni za siri pia , nimesikia ni mgonjwa wa akili wa nafsi mbili , itakuwa vizuri zaidi ukifuatilia kwa upande wako”Aliongea Yulia na kumfanya Hamza kushangazwa na jambo lile mno. “Kuna mwingine anaejua kuhusu hili?”
“Sidhani kama kuna anaefahamu , lakini niamini mimi taarifa hii ni ya siri mno hata familia yake hakuna anaejua kasoro bibi yake pekee, ninachomaanisha ugonjwa wake ukimpata hata kama anaweza kukupenda akiwa na nafsi ya Regina akibadilika anaweza akakupotezea moja kwa moja”Aliongea na kumfanya Hamza kuwaza lakini muda huo Yulia alitumia kumsoma Hamza kimawazo na kuna kitu alichogundua lakini hakutaka kukiweka wazi.
“Kuhusu hili nitafuatilia , kama umesema ni la siri naomba liendelee kuwa siri , mimi kama msaidizi wake wa karibu chochote kikimpata nitawajibika”Aliongea Hamza na kauli yake ilimfanya Yulia kuwa na wivu wa wazi.
“Yulia ninachomaanisha usije ukaruhusu mawazo yako yakaenda mbali , nipo ndani ya kampuni ya Dosam kwa ajili ya kutengeneza pesa kama watu wa kawaida , mimi sio mtu ambae umekutana nae miaka saba iliopita”
“Kama huo ndio mpango wako , kwanini usijiunge na kampuni yetu ya PRIMA? Nitakupa nafasi ya kuwa bodigadi wangu, haijalishi Regina anakulipa kiasi gani nipo tayari kulipa zaidi yake”
“Hapana haiwezekani , nimeshasaini nae mkataba , isitoshe kwa ulichosema nadhani anahitaji ulinzi zaidi kuliko wewe”
“Unanionaje , nipo tayari kukuliipa milioni ishirini kwa mwezi , kama haitoshi nitajie kwa ajili yako nipo tayari kulipa kiasi chochote”Aliongea na kumfanya Hamza kuona Yulia anachagua cha kujibu maneno yake na kumfanya acheke.
“Yulia tulikutana kwa muda mchache sana Zurich , hivi unadhani kuniona vile ndio kunijua , ukweli ni kwamba hujui chochote kuhusu mimi halafu unataka niwe bodigadi wako?, mbona kama unaniamini sana kupitiliza”
“Mimi ninachojua wewe sio mtu mbaya , kama kweli ungekuwa ni mtu mbaya usingeniokoa katika dakika zangu za mwisho za uhai”Aliognea huku awamu hio akilegeza sauti na mikono yake kuiweka katika mabega ya Hamza.
“Au upande wako mwingine unakufanya kuwa mbaya , kama ni hivyo nakufaa zaidi ya Regina”Aliongea huku aking’ata lipsi zake kwa namna ya kukonyeza na pumzi yake kuizuia na kufanya jicho kulegea.
Matendo yote ya Yulia yalimfanya Hamza mwili wake kuwaka moto, Yulia alikuwa akijua anachokifanya katika kumpagawisha.
Hamza mara baada ya kuona yanakwenda kumshinda alimshika kwenye shingo kwa spidi ya hali ya juu na kwenda kumbana kwenye ukuta na kusogeza mdomo wake karibu zaidi huku Yulia akiendelea kumwangalia kwa macho ya kumruhusu lakini yaliojaa waswasi kwa wakati mmoja.
Comments