SEHEMU YA 49.
“Namaanisha tumeanza pamoja hivyo tutamaliza pamoja”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu la kawaida lakini macho yake yalionyesha namna gani alikuwa siariasi.
Refa hakufikiria sana na aliishia kumuuliza Regina kama anakubaliana na wazo la Hamza na Regina upande wake aliishia kukubali na mechi ikaanza lakini kwa sura tofauti.
Wachezaji wanne upande wa Dosam huku Aroni akiwa amekaa pembeni kana kwamba anasubiria kuangalia kinachokwenda kutokea.
“Sikia nipasieni mpira mimi , hakikiisheni mnaeupka kufanyiwa rafu”Aliongea Hamza na wachezaji watatu wote walitingisha kichwa kukubaliana nae.
Upande wa wachezaji wa Zena waliamua kutumia uwezo wao wote wakiwa wengi uwanjani , isitoshe waliona ingekuwa ni aibu kama watapoteza shindano kwa timu iliopo na wachezaji pungufu.
Lakini mwishowe mara baada ya mpira kumfikia Hamza walijikuta wakitamani kuzimia , Hamza alikuwa katikati kabisa ya court na bila kusema chochote alirusha mpira mpaka kwenye kikapu na ukaingia na kuwapatia pointi tatu.
Kitendo hicho cha ushindi wa Hamza kutokea mbali uliamsha hata mashabiki wa kampuni ambazo zimekwisha kutolewa na kuanza kuishangilia kampuni ya Dosam.
“Mungu wangu , Jamani Hamza weweee..!!”
“Wewe kaka jamani..!!”
“Kama angekuwa na urefu hata sentimita kadhaa nadhani anavigezo vya kushiriki NBA”
“Haha.. umeenda mbali sana lakini ni kweli yupo vizuri”
Watu walianza kuongea wao kwa wao huku kelele
zikiwa zimejaa , katika kipindi chote cha mashindano pengine siku hio ndio mchezo huo umekuwa na hisia kubwa kwa wanaoangalia.
Wachezaji wa Zena waliona ni ngumu kumzuia Hamza kutoshinda hivyo walitumia mbinu ya kumzunguka kuhakikisha hapati mpira.
Lakini sasa Hamza ni kama anawapotea kimazingara na wanapotaka kumzunguka ashapotea na kuwa sehemu nyingine na kukamata mpira na hakujali eneo alilosimama akiupata hakufanya mbwembwe na kuutupia golini huku akijikosesha mara kadhaa huku mara nyingi akipatia.
Hamza hakutaka kuonyesha vitendo ambavo sio vya kawaida , alihakikisha mbinu zake zote zinaonekana katika macho ya wanaomwangalia kwa kuhakikisha namna ambavyo anakwepa wapinzani wake.
Ndani ya muda chache ubao ulisoma hamsini na moja kwa ishirini na tatu na Hamza pekee alishinda pointi arobani, hivyo matokeo ya mchezo yalionekana wazi.
Mpira wa mwisho mara baada ya kumfikia Hamza aliamua kuonyesha ujuzi sasa alikimbia na mpira kwa kuudunda dunda mpaka pembeni ya uwanja na kisha kwa umakini mkubwa sana alirudi kati na kugonganisha katika ubao wa gori na kisha kwa uwezo wa juu ali’dunk’ na kwenda kuujanza mpira kwenye kikapu na mkono mmoj. “Damn! anajua hata Ku’slum dunk?”
“Nilijua anachojua ni kulenga kikapu tu”
“Hii inakwenda kuwa aibu kwa upande wa itmu ya Zena kushindwa na wachezaji wanne”
Watu walikuwa wakiongea kila walichowaza huku wengine wakishangalia kwa ujuzi wa ku’dunk’ alioonyesha Hamza.
Upande wa timu ya Zena sura zilikuwa nyeusi tii , moja ya mfanyakazi wa kampuni hio alikuwa ni mchezaji mkubwa sana wa mpira huo ndani ya jiji la Dar na alishangazwa na uwezo wa Hamza.
Aroni aliishia hata kusahau maumivu yake na alijikuta akiungana na wengine kushangailia
Baada ya kuona hamasa hio ya mashabiki wapya kila mfanyakazi wa kampiuni ya Dosam alijawa na furaha.
Eliza aliishia kuruka ruka kwa furaha , alitamani kutoka alipo na kwenda kumbusu Hamza lakini kariba yake haikumuwezesha kufanya hivyo.
Regina aliishia kumwangalia Hamza na macho yaliojaa hisia , kwa jinsi Hamza alivyokuwa akijiamini na mwili wake wa mazoezi ulivyo mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi mno.
Linda ambae hajawahi kumkubali Hamza alijikuta akionyesha ishara ya kumheshimu.
Viongozi waliohudhuria walijikuta wakisimama na kuanza kupiga makofi , walikuwa pia na furaha japo wengi wao walijilazimisha kuja kutokana na mashindano hayo kukosa msisimko lakini kwa kilichotokea kiliwafurahisha.
Chriss alikuwa na wasiwasi kwenye macho yake , ukweli ni kwamba licha ya kampuni yake kushindana hakuwahi kuitilia mkazo kushinda , kilichompa wasiwasi ni kwamba licha ya Prisila kujitetea asubuhi lakini bado alikuwa na wasiwasi , aliona kuna kila dalili ya Prisila kumpenda mwanaume kama Hamza ambae ana uwezo mkubwa.
Katika macho yake hakumuona Hamza kama mwanaume mwenye pesa bali mwenye uwezo na kunasababu iliomwambia ndio maana Prisila alimchagua ku’fake’ nae kuwa boyfriend wake , isitoshe habari za Hamza kufahamiana na Yulia alizisikia pia.
James yeye alijikuta akibadilika sura kutokana na hasira , aliishia kuinamisha kichwa chake chini na taratibu alitoka kwenye jukwaa na kuelekea upande wa parking na kisha kuondoka.
Hakuaka kuendelea kukaa hapo , alikuwa amemsahau hata rafiki yake Chriss aliekuja nae.
Kutokana na uwezo wa Hamza timu nyingine ilikataa kuingia uwanjani hivyo timu ya Dosam ilipewa ushindi moja kwa moja na kuwa mabingwa.
Hakuna timu ambayo ilipenda kudharirishwa na Hamza maana ni kama alikuwa akicheza peke yake uwanjani.
Hamza alikabidhiwa cheki ya pesa kiasi cha shilingi milioni mia na mara baada ya kuona tarakimu hizo alijikuta akijawa na majuto na kujiambia kwanini hakufikiria hili kabla , pengine mara baada ya kuja bongo angejiingiza kwenye mchezo wa basketball na ingekuwa rahisi mno kwake kujipatia pesa za haraka.
Mara baada ya kupokea kitita hicho kama mchezaji bora hakuwaza kuzitumia yeye , alijua fika ni wapi anapaswa kuzipeleka . sehemu ambayo anakumbukumbu nayo wakati wa utoto wake.
Jioni mara baada ya mashindano kuisha Regina aliandaa tafrija ndogo katika hoteli ya Dosam V kwa ajili ya kuwazawadia timu yote ilioshiriki katika mashindano hayo.
Tokea aanze kufanya kazi kama kiongozi wa kampiuni hajawahi kuona morali ya wafanyakazi wake kuwa juu namna hio na aliona ni swala la kusherehekea.
Lakini hata hivyo jina la Hamza halikusahauliwa maana ndio liliipatia heshima kampuni.
*****
Upande mwingaine wakati wafanyakazi wa kampuni ya Dosam wakisherehekea ushindi kwa furaha kubwa , nyumbani kwa mzee Benjamini wingu zito lilikuwa limetanda kuzunguka nyumba yao tu.
Ndani ya jumba la kifahari la Mzee Benjamini katika eneo la sebuleni Mzee Benjamini na James walikuwa wamekaa kwenye masofa huku chupa kadhaa za whiskey zikiwa zimeenea.
Walionekana walikuwa wamekunywa mno , macho yao yalikuwa mekundu na yamevimba kama ya nguruwe.
“Kulingana na uchambuzi .. taarifa ya habari ikitoka hisa za kampuni ya Dosam zitapanda kwa asilimia tatu na hisa zetu zitazidi kuporomoka kwa asilimia mbili”Aliongea Mzee Benjamini.
“Kushuka tena , nimeweka juhudi kubwa kuzipandisha na zinakwenda kushuka tena?, F*ck him, haya yote ni kwasababu ya huyu mpuuzi Hamza , huu ndio ulikuwa mpango pekee wa kuirudisha taswira ya kampuni yetu lakini tumeshindwa tena”Aliongea James kwa hasira huku akipasua glasi ukutani.
“James usiwe na wasiwasi tulikuwa kwenye kikao kizito na mstaafu Mgweno na ajenda kubwa ilikuwa ni namna ya kumuondoa Hamza hapa Tanzania , mheshimiwa kupitia umoja wa Makomandoo ametoa agizo Master Konki kufika mara moja nchini na watalaamu wa mapigano, mawasiliano yashafanyika na muda si mrefu atafika na kumshikisha adabu”
“Baba hata kama hao watu kutoka kundi la Mwewe mweusi wakifika sidhani kama wanaweza kumjeruhi Hamza na hata kama wafanye hivyo hawawezi kubadilisha chochote ndani ya kampuni
yetu ni raia wa kigeni sidhani watakuwa na ujasiri wa kumuua Hamza”Aliongea James na kumfanya Mzee Benjamini kuwa kimya , hata yeye pia alikuwa akifikiria juu ya swala hilo.
“Baba si ulisema mara ya mwisho kama hatuwezi kumpata Regina kwa njjia za kawaida tutatumia njia nyingine , huoni huu ni muda sahihi wa kutafuta maninja hatari ili kumuua Hamza na Regina”
“Kuwaua wote kutarahisisha changamoto zetu nyingi , lakini kwa maelekezo ya mstaafu huu ni mpango wa mwisho kabisa kama mbinu zote zikishindikana, isitoshe pia tuna watu wetu ndani ya familia ya Regina”Aliongea na dakika hio hio anamaliza aliweza kusikia kelele za mwanamke kutoka nje.
“Waueni , kama msipo waua sasa hivi tunaweza kuchelewa kabisa”
Baada ya kauli hio kusikika iliwafanya James na baba yake kugeuza vichwa.
Alikuwa ni Lamla mke wa mzee Wilsoni na Regina mama yake wa kambo.
“Rebe nini tatizo , kwanini umekuja ghafla ghafla?”Aliuliza mzee Benjamini.
“Madam , nini kimetokea?”Aliuliza James
Lamla ambae aliitwa Rebeka na Mzee Benjamini kama vile yupo kwake alitupa mkoba wake kwenye sofa na kisha alijimiminia kilevi kwenye glasi na kupiga mkupuo mmoja.
“Kama nisingekuja kukuelezea kinachoendelea pengine ningechelewa”
“Nini kimetokea?”
“Si yule Ajuza amekuja Dar jana kwa ajili ya matibabu na inaonekana hana muda wa kutosha kuendelea kuishi na mpango wake ni kumrithisha Regina hisa zake zote”Aliongea kwa hasira
“Nini!!?, Amekuwa kichaa , kwahio anaacha kumpaitia mtoto wake Wilsoni na kumpatia mjukuu wake?”
“Kinachokasirisha zaidi , Benjamini yule kizee hana mpango kabisa wa kumpatia mtoto wetu Frank hata hisa moja na ameenda mbali kumwambia aende eti akafanye kazi katika nafasi ya chini, yaani nimeitumikia ile familia kwa muda mrefu na bado wananidharau”Aliongea Lamla huku aking’ata meno kwa hasira lakini upande wa James alikuwa na mshituko.
“Baba.. madam , mnaongea nini, Frank ni mtoto wenu?”Aliuliza kwa hamaki na kumfanya Mzee Benjamini kunywea.
“Benjamini inamaana hujamwambia James bado?”Aliuliza na kumfanya Mzee Benjamini kumwangalia mtoto wake.
“Sikia James ukweli ni kwamba Frank ni damu yangu .. hivyo ni mdogo wako”Aliongea
MzeeBenjamini na kauli ile ilimwamsha James
“Nini!!, nyie watu mekuwa vichaa ?”
“Wewe mtoto hebu kaa chini , cha kushangaza nini hapo , unadhani ningejisumbua vyote hivyo kupambania ndoa yako na Regina na kushirikiana na baba yako ili tuichukue kampuni ya Dosam, unadhani nimefanya bure, ni kwasababu mimi na baba yako tunahistoria”
James alikuwa ameshikwa na bumbuwazi bado hakuwa ameamini kinachoendelea.
“James sisi ni familia”Aliongea Lamla.
“Wilsoni ni mwanaume mpuuzi puuzi , kwa miaka yote hio ameshindwa hata kujua Frank sio mtoto wake , ni hivyo tu Mzee Dosam aliwahi kumleta Regina kipindi kile na kumfanya kuwa sehemu ya familia na mpango kuvurugika … kama sio Regina tungeweza kuichukua kampuni ya Dosam muda mrefu sana”
“Mzee Dosamu yule hakuwajhi kuwa mtu mwepesi na hata kwa mke wake ni hivyo hivyo , sina uhakika kama yule kikongwe hajui Frank sio damu ya mtoto wake , mimi nadhani anajua ndio maana yupo tayari kumpatia Regina hisa zake zote”
“Tunapaswa kuhakiksiha Frank anaendelea na mafunzo ya kivitendo ndani ya kampuni ili kuonyesha uwezo wake , ninaamini yule kikongwe anaweza kuishi kwa muda mrefu kidogo kabla ya kutoa hisa zake na Frank atakuwa na uwezo wa kuthibitisha uwezo wake”
“Unadhani atabadilika , ana hisa asilimia 32 yule na yupo tayari kumpatia Regina zote?”
“Nimeulizia idara ya sheria na nilichoambiwa wosia wa Mzee Dosam utafuatwa kama kawaida , Kama Regina ataoana na Hamza ndio atawapaitia hisa zake”Aliongea Lamla.
“Huu ni upuuzi yaani kumpa mtu hisa kwasababu
kaolewa , yaani sijawahi kuona sababu kichaa kama hii”
“Hata mimi nimewaza hivyo hivyo , ninachoona yule kikongwe anachotaka kuona ni Regina kuolewa kabla ya kufa , lakini maamuzi ya kumpatia hisa Regina yashafanyika muda mrefu na anafanya maigizo tu”Aliongea Lamla kwa chuki.
“Vipi kuhusu Mzee Wilsoni, hana pingamizi lolote katika hilo?”
“Pingamizi alitoe wapi , mwenyewe bado anamuogopa mama yake na hataki kumpinga kwa kuogopa atapokonywa asilimia saba anayomiliki, yaani hana analojua kichwa maji kabisa , nachukia kipindi kile kukubali kuolewa nae”
“Lamla ni makosa yangu kipindi kile , kama sio wazazi wangu usingekuwa katika hali hii”Aliongea
MzeeBenjamini huku akimpeti peti na kumfanya Lamla kulegea
“Baba unamaanisha nini , usiniambie ulilazimishwa kuoana na mama yangu?”Aliuliza James.
“Ah, sijamanaisha hivyo ni kwamba baba alichanganya mambo , ni makosa ya baba”Aliongea Benjamini huku akijitetea.
“Sitaku kuhusika kwenye maswala yako mzee , nimezdhalilishwa vya kutosha na Regina na yule
mwanaharamu Hamza , ninachotaka ni wao kufa sio kingine”
“James yupo sahihi , hatuna muda wa kupoteza , ikitokea Bi Mirium kumpatia Regina hisa zake moja kwa moja hatuna cha kufanya tena , tunapaswa kuchukua hatua sasa hivi”
“Huna haja ya kuongea sana , ninajua mtu ambae anaweza kuniunganisha na muuaji mbobevu hapa Dar , awamu hii nitatumia pesa yoyote kuhakiksiha namuua Regina na Hamza”Aliongea James na kwa hasira aliondoka.
Kitendo cha James kuondoka ni kama wamepewa uhuru kwani Lamla alimbusu mdomoni Mzee Benjamini na kisha kuegamia kifua chake.
“Benja .. unadhani James hatonichukia?”
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , umekuwa msaada mkubwa kwake kwa muda mrefu , nina uhakika mambo yakienda sawa ataelewa tunachokifanya sio kwa ajili ya Frank pekee”
“Upo sahihi kwa ajili ya Frank na James tumeshirikiana kwa muda mrefu kwa siri sana kukamilisha mipango yetu , hatuwezi kuruhusu tulichopanga miaka kumi na tano nyuma kupotea hivi hivi na kampuni kuchukuliwa na
Regina”Aliongea Lamla na kumfanya Mzee Benjamini kugida kilevi chote kilichobakia na kisha alisimama na kumshika Lamla kiuno.
“Leo hakuna kurudi , nimekumisi kwa muda mrefu , hebu twende chumbani kwanza”Aliongea na kumfanya Lamla uso wake aliojichubua kuwa mwekundu.
“Yaani wewe , kila ukiniona unachowaza ni ngono
tu , miaka yote hio ni kazi ya kukupa tu huchoki wewe mwanaume “
“Hehe , kama umechoka wewe sema , mimi naiweza shoo kuliko yule goigoi wako, au nasema uongo?”
“Tena hata usimtaje huyo mjinga , hebu twende zetu tukaliamshe”
******
Siku iliofuata katika bahari za michezo ni juu ya ushindi waliopata kampuni ya Dosam na namna ambavyo Hamza alionyesha uwezo wake.
Ilikuwa ni habari ambayo ina taswira chanya kwa kampuni hivyo hisa zake zilipanda kama ilivyotabiriwa
Wakati wa chai ya asubuhi Regina aliona habari hio na alijikuta akifurahi mno.
Baada ya kumaliza kula walipokea Delivery kutoka kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya kimataifa na mzigo huo ulikuwa ni wa Hamza.
Hamza alisaini na kisha akapoktea mzigo wake , ulikuwa ukitokea London Uingereza na ilionekana Master Alex alikuwa ashamaliza kazi yake ya kuandaa mavazi ya Hamza ya kuvaa.
“Aiii.. huyu mzee inaonekana ametumia juhudi kubwa sana kukamilisha kazi sio kwa uzito huu”Aliongea Hamza na kisha alilitupia boksi lile kwenye ngazi akiwa hana haraka ya kulipeleka juu kwake.
Regina aliishia kuangalia lile boksi na macho yake yalionekana alikuwa na shauku ya kutaka kuona nguo alizoletewa Hamza.
“Vipi Regina unataka na wewe kuona nguo zangu za ndani?”Aliuliza Hamza na kumfanya Regina uso kuanza kupata joto kutokana na kauli ya Hamza , maana ni kama anamwambia baada ya kuona nguo yake ya ndani siku ile basi ni zamu yake na yeye kuona zake.
“Sina shida , hebu fanya haraka
tuondoke”Aliongea Regina huku akinywa juisi yote kwa mkupuo mmoja.
“Nimeheshimisha kampuni kwa kushinda , hujaniambia ni zawadi gani unanipatia?”
“Nitakupa muda wowote , haraka ya nini , kwani huna kitu kingine cha kuongea kisichohusisha hela?”
“Kama ni hivyo basi nitaongea kitu kingine kisichohusisha hela , eti Regi ni lini tunafunga ndoa kama bibi alivyosema?”Aliuliza Hamza na kumfanya Regina kuzidi kubadilika na uso wake wa kirembo kuwa mwekundu.
“Sifungi ndoa halafu nani anataka kufunga ndoa na wewe?”Aliuliza na kumfanya Hamza kucheka , hata hivyo alikuwa akitania tu.
Tokea bibi yake Regina ataje swala la ndoa , Regina alikuwa sensitive sana na neno ndoa , ukimtajia ni kama Simba aliekanyagwa mkia.
“Nimeuliza tu , hasira za nini sasa?”
“Ukiniuliza hilo swali la kipuuzi tena nitahakikisha sio zawadi tu ambayo utakosa bali ni mpaka mshahara wako”Aliongea kwa hasira na alitamani kumwagia Hamza maji ya uso.
Shangazi ambae alikuwa bize jikoni aliishia kusikiliza mtafaruku huo na kujikuta akitingisha kichwa chake kwa masikitiko.
Ilikuwa ni bahati tu bibi yake Regina alikuwa hospitalini bado la sivyo angecharuka kusikia makelele hayo.
Muda huo huo simu ya Regina ilianza kuita na Regina alimwangalia Hamza kwa sekunde na kisha kuipokea. “Linda kuna nini?”
“Bosi mambo sio mazuri huku , yule mtu aliekuja mara ya mwisho anaejiita Konki amerudi tena akiwa na kundi la wathailland na wameingia mpaka floor ya pili idara ya walinzi na Gym, inaonekana wamekuja kulipa kisasi”Aliongea Linda.
“Nini!!?”
“Kapteni Yonesi anajaribu kuwazuia lakini sina uhakika kama ataweza , vipi nipigie simu polisi?”Aliuliza na kumfanya Regina kufikiria kwa muda , alijua fika mpaka wakafika katika kampuni yake kuna mkono kutoka kwenye jeshi la polisi hivyo haiwezi kuwa na maana.
“Mwambie Yonesi asifanye kitu chochote , tunakuja muda si mrefu”
“Sawa bosi”
Regina mara baada ya kukata simu hakuweza kumuona Hamza mbele yake tofauti na ngurumo ya gari na hakutarajia Hamza angekuwa mshapu kiasi hicho , alitoka haraka haraka na kuingia kwenye gari
“Tunaelekea…”
Regina kabla hata ya kuongea gari ilinguruma kama simba na kupiga msele huku ikiacha moshi kana kwamba inataka kupaa.
“Ahhhhhh.., wewe wewe unafanya nini?”
“Funga mkanda vizuri , leo barabara inaweza isiwe nzuri”Aliongea Hamza huku akikunja sura.
Regina alitaka Hamza kuendesha gari kwa haraka lakini hakutaka Hamza kuchafua hali ya hewa kwa kuendesha gari kama kichaa , lakini mara baada ya kukumbuka kinachoendelea kwenye kampuni hakutaka kumzuia.
Aliishia kufumba macho na mara baada ya Hamza kuliingiza gari barabarani kama mshale alilitoa nduki na walichukua dakika ishirini na tano mpaka kufika makao makuu , ilikuwa bahati kwao hakukuwa na msongano.
Mpaka gari linakuja kusimama ndani ya maegesho ya kampuni Regina alijihisi tumbo la kuhara lakini aliamua kujikaza na kuvuta pumzi na kisha kushuka na kuingia ndani.
“Linda hali ipoje?”Aliuliza Regina mara baada ya kupokelewa na Linda.
“Mkurugenzi wapo katika floor ya mazoezi , Yonesi anabishana nao , anang’angania kushindana nao”Aliongea Linda na mara baada ya Regina kusikia hivyo kwa haraka sana aliingia kwenye lift pamoja na Hamza na kwenda juu.
Mara baada ya kuingia katika floor hio waliweza kumuona Master Konk na kundi la wanaume nane, watano wakiwa ni weusi huku watatu wakiwa sio raia wa Tanzania na kulikuwa na wafanyakazi wengine wa kampuni ambao wamefika pia kuangalia.
“Hakikisha wafanyakazi wote waliofika hapa kuangalia wanaondoka na kuendelea na majukumu yao”Aliongea Regina akimpatia Linda maagizo na ndio muda ambao Linda anagundua wafanyakazi wengi walikuwa wamefika kuangalia kinachoendelea na kwa haraka aliwaambia waondoke wakaendelee na kazi.
“Yonesi hebu shuka kwanza hapo?”Aliongea Regina akimtaka Yonesi kutoka kwenye ulingo, hakutaka kukurupuka maana alikumbuka mara ya mwisho alimshindwa Master Konki na kama sio Hamza angeumizwa.
“Mkurugenzi wamekuja kutafuta tu matatizo hapa , kama tusipowapa sababu ya kuondoka watarudi tena”
“Wewe msichana hivi unadhani unaweza kuwazidi hawa , yaani unishindwe mimi uweze kushindana na hawa wataalamu wa sanaa ya mapigano”Aliongea Master Konki alikuwa bado na Bandeji kwenye mkono wake na alichukua nafasi ile kumtambulisha Mthalland mmoja aliekuwa mrefu wa mita kama moja na nusu hivi , ambae amevalia mvazi ya kitamaduni ya Thailland ,ni kama amevaa shuka halafu akalitengeneza suruali
“Mimi ni makamu kiongozi mkuu wa dhehebu la Black Eagle nafahamika kwa jina la Chekani , mwanafunzi wetu mzee Konk alitoa taarifa ya kukutana na mtu anaemzidi kwa kutumia msingi wa sanaa ya kimapigano wa mbinu yetu ya vidole vya Tai , hivyo kwa shauku nimesafiri na kaka zangu hawa wawili kujionea wenyewe, ni maagizo pia kutoka kwa baba yangu”
“Mzee mara ya mwisho sikuwa makini na sikutarajia kama una mafunzo yale lakini awamu hii hata tukutane sina uhakika kama utaniweza”Aliongea Yonesi huku akimsogelea yule bwana aliejitambulisha lakini bwana yule aliefahamika kwa jina la Chakeni alimwangalia Yonesi kwa dharau.
“Sina mpango wa kupigana na mwanamke , usiniambie wanaume mliopo hapa hakuna mwenye uwezo wa kupigana na mimi”Aliongea
Chekani huku macho yake yakitua kwa Hamza.
“Hili sio swala la nani kuwa mwanamke au mwanaume bali ni swala la uvunjifu wa sheria , kampuni ya Dosam ni kubwa na kuingia ndani kuleta taharuki ni kuvunja sheria , serikali inatulinda pia, sijui uhusiano wa kundi lenu la mapigano na serikali ukoje lakini usije kuona hatuwezi kufanya chochote”Aliongea Regina kwa hasira na Mzee Konki macho yake aliyageuzia kwa Hamza.
“Haina haja ya kutumia sheria kutuogopesha na hatujaja hapa kuvunja sheria , sababu ya kuja ni kwa ajili ya kupambana na huyo mtoto . hili swala halina uhusiano wowote na kampuni yako”Aliongea Mzee Konki.
“Yaani mmekuja ndani ya kampuni halafu mnasema hili swala halina uhusiano wowote na kampuni?”Aliuliza Yonesi.
“Hakuna shida , kama hamtaki tukitumia eneo hili basi tunaweza kutafuta sehemu nzuri ya kupigana ,sidhani tukiondoka na Hamza hili litakuwa na uhusiano na kampuni”Aliongea Master Konki na kumfanya Regina kumwangalia Hamza.
“Una maamuzi gani?”Aliuliza , Regina hakuwa na uelewa mkubwa sana kuhusu sanaa ya mapigano hivyo alikuwa na wasiwasi Hamza anaweza kumshindwa Kachani.
Upande wa Hamza wasiwasi wake ni kuogopa walinzi wa kampuni akiwemo Yonesi watapigwa lakini mara baada ya kukuta hakuna kilichotokea alijikuta akipumua.
“Sijachukua mazoezi ndani ya muda mrefu kidogo
, nadhani sio mbaya kama nikienda nao”Aliongea Hamza
“Subiri kwanza , unamaanisha nini , unadhani wanaweza kunishinda?”Aliuliza Yonesi akizuia na hakuwa na furaha baada ya Hamza kutokumuuliza chochote.
“Kapteni Yonesi hawa wapo hapa kwa ajili yangu , sidhani kuna haja ya wewe kujihusisha”
“Mimi ndio kapteni wa timu ya ulinzi , nina kila sababu ya kulinda usalama wa wafanyakazi wote , sitaki kuonekana kama sina thamani na kazi yangu siiijui”Aliongea Yonesi na kisha akamwangalia Regina.
“Mkurugenzi tafadhari naomba uniamini mimi , awamu hii siwezi kushindwa”Aliongea Yonesi kwa namna ya kubembeleza na ilimfanya Regina na Hamza kushangaa kwani hawakuamini Yonesi atakuwa siriasi mno kuhusu swala hilo, ilionekana ni dhaihiri kabisa Yonesi hakukubali kushindwa kirahisi.
“Basi haina haja ya kuondoka mtapigana hapa hapa , Hamza muachie Yonesi pambano”Aliongea Regina.
“Asante sana Mkurugenzi kwa kuniamini nakuahidi sitokuangusha”Aliongea huku akionyesha shukrani za dhati kabisa kwa Regina.
Muda huo Chekani hakuwa na jinsi zaidi ya kuingia kwenye ulingo kwa ajili ya kupigana na Yonesi licha ya kuona msichana huyo hana chochote cha kumtishia”
Unadhani Yonesi atashinda au atadundwa mpaka maji ayaite mma.
Comments