SEHEMU YA 51.
Sister Maya mara baada ya kuulizwa swali lile alionekana kuwaza kidogo na kisha akamwangalia Frida.
“Hakuna sababu yoyote , wote tunaamini katika siri ambazo hatujaambiwa”Aliongea Sister.
“Siri ambazo hamjaambiwa!, unamaanisha nini kusema hivyo?”
“Ndio, licha ya kwamba umekuwa chini ya Sinagogu kwa muda mrefu lakini je imani yako inakuambia nini kuhusu siri , je unaamini kuna uwezekano wa uwepo wa siri kubwa sana ambayo hujaambiwa katika maisha yako kuhusu ulimwengu ulivyo?”Aliuliza na kumfanya Frida kutingisha kichwa.
“Naamini zipo siri nyingi ambazo sijaambiwa mpaka sasa”
“Hio ndio sababu yetu binafsi , kila mwanasinagogi anaamini katika siri ambazo hajaambiwa na sio ukweli ambao tunaaminishwa, wala sababu ambazo tunapewa ili kuamini”Aliongea na kumfanya Frida kufikiria sentensi yake.
“Kama ni hivyo basi kila mtu anaweza kuwa Mwanasinagogi , siamini katika ulimwengu huu hakuna asieamini uwepo wa siri juu ya vitu mbalimbali”
“Huo sio msingi pekee wa imani yetu , tunachoamini zaidi ni ile siri ambayo tuna malengo nayo, unaweza kuamini kuwepo kwa siri lakini huna juhudi yoyote ya kuzitambua hizo siri basi wewe sio Mwanasigiogi, kwa lugha nyepesi Sinagogi ni jamii ya watu wanaoamini katika kweli ambayo haijasemwa lakini inaonyesha dalili”
“Dalili!, naweza kufahamu zaidi?”Aliuliza Frida kwake ndio mara ya kwanza kufahau kuhusu kauli hio , isitoshe katika jamii ya wanasinagogu kuna madaraja ya uanachama ndio unaweza kujua baadhi ya vitu.
“Kuhusu hili nadhani una majibu tayari , kama sio hivyo usingerudi katika taasisi ya Feliz na usingefanikiwa kumshawishi Askofu Alfonso kukurudisha licha ya kwamba kwake unaonekana mtu hatari”Aliongea Sister na kumfanya Frida kutulia na kuanza kutafakari maneno ya Sister.
“Unamaanisha kuhusu wimbi la watu wenye zaidi ya nafsi moja!!?”Aliongea na kumfanya Sister Maya kutingisha kichwa.
****
Huna haja ya kuwa na wasiwasi , ni nesi ndio kakubadilisha”Aliongea Hamza mara baada ya kuona Yonesi alikuwa na wasiwasi kama yeye ndio amembadilisha.
“Nimeuliza nguo zangu ziko wapi na sio nani kanibadilisha”Aliongea Yonesi huku kidogo akihisi ahueni.
Hamza hakutaka kubishana nae hivyo alimpatia bakuli lile la uji lakini sasa kitendo cha Yonesi kuchota kwenye kijiko na kupeleka mdomoni alijikuta akishindwa baada ya kuhisi maumivu makali ya viungo vya ndani.
“Ngoja nikusaidie acha ubishi unakuwa mjinga sasa kuzidi kujiumiza kwa ujeuri wako”Aliongea Hamza na kumfanya Yonesi kukosa sababu ya kukataa.
Hamza alianza kumlisha Yonesi taratibu lakini kitendo hicho ni kama kimempa nafasi ya kumwangalia zaidi usoni kwa ukaribu zaidi , sasa harufu ya kimwili ya Yonesi pamoja na ya hospitalini ilimfanya pua zake kuburudika.
Kitendo cha Hamza kumlisha akiwa kimya ilimfanya Yonesi kujihisi hali isio ya kawaida.
“Mbona huongei?”
“Kapteni leo Nimegundua ngozi yako ni laini mno bila hata ya kuigusa”Aliongea Hamza.
“Acha kuongea”
“Unatakiwa kuniacha nimalize kwanza kuongea na kisha ndio uniambie ninyamaze”
“Sitaki kusikia ujinga wako”
“Nimekusifia unaita ujinga”
“Haina haja ya kunisifia hivyo kwangu ni ujinga”Aliongea Yonesi lakini mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda kasi mno na kuanza kujiuliza nini kinaendelea kwanini anakosa utulivu mbele ya Hamza.
“Labda ni kwasababu tupo katika chumba kimoja wenyewe”Aliwaza Yonesi akijaribu kujipa sababu.
Upande wa Hamza wakati akiendelea kumlishaYonesi macho yake yalikuwa yamegota katika kifua cha mrembo huyo , ilionekana nesi ambae alimvalisha hakufanya kazi nzuri kiasi kwamba kwa juu kila kitu kilionekana kwa ndani.
Yonesi mara baada ya kumwangalia Hamza usoni aligundua ni wapi alipokuwa akiangalia na alitamani kumpiga lakini kwasababu hakuwa na uwezo huo kutokana na maumivu aliishia kung’ata macho kwa hasira.
“Endelea kuangalia tu kama sijayatoboa hayo macho yako”
“Umenidhania vibaya Kapteni , nilikuwa nikijiuliza nikusaidie kukufunga hicho kifungo vizuri , naona nesi hajafanya kazi nzuri kwenye kukuvalisha”
“Haina shida wewe jua mambo yako tu “Aliongea Yonesi huku akivumilia maumivu na kujiweka vizuri.,
Mara baada ya kushiba Hamza alimsaidia kuegamia kwenye kitanda lakini ni muda ule Yonesi alianza kukunja sura.
“Naomba uniitie nesi”Aliongea.
“Nesi wa nini , kuna shida yoyote?”
“Nenda niitie nesi maswali mengi ya nini?”Aliongea na kumfanya Hamza kutoka nje kwenda kumuita nesi.
“Mgonjwa kuna chochote unachohitaji nikusaidie?”Aliuliza Yule nesi.
“Nataka kwenda bafuni”Aliongea Yonesi na sasa kumfanya Hamza ajue shida ya Yonesi ni nini na kutamani kucheka.
Ilikuwa ni sahihi kuhisi mkojo maana tokea asubuhi alikuwa amelala na muda huo amepewa madawa pamoja na kunywa uji.
Yule nesi alimwangalia Hamza kwa maswali kadhaa , ni kama alimuona Yonesi na Hamza ni wapenzi lakini hata hivyo alikubali.
“Sawa ngoja nikusaidie , shuka taratibu taratibu ukiona unahisi maumivu niambie”Aliongea yule nesi hakuwa mrefu sana alikuwa na mita kama moja na nusu lakini Yonesi alikuwa na zaidi ya mita moja nukta saba.
Yonesi alipiga hatua kuelekea chooni lakini mwili wake wote ulikuwa umemlemea yule Nesi na kuonesha ni kwa namna gani alikuwa akipata shida kwani alianza kutetemeka.
“Arggh,,!”
Yonesi alijikuta akihisi maumivu na kuguna na yule nesi kutokana na kuchoka alijikuta akishindwa kumsaidia zaidi Yonesi na kumuombaHamza amsaidie.
“Kaka itakuwa vizuri ukimsaidia wewe , sina nguvu za kutosha na itakuwa hatari kama nikidondoka” “Haina shida nitaweza mwenyewe”
“Dada huna haja ya kujilazimisha sana ni hatari kwako , ngoja mpenzi wako akusaidie , mtu yoyote anaweza kuwa mgonjwa na kuhitaji mtu wa kumsaidia , haina haja ya kuona aibu”
Upande wa nesi aliamini kama Hamza sio mpenzi wa Yonesi basi ni mume wake maana ndio amemleta hospitalini na hata chakula ndio amemsaidia kumlisha na amekaa wodini tokea asubuhi.
Yonesi alitamani kumwelezea yule nesi kwamba sio vizuri kwasababu ni jinsia tofauti na hana mahusiano yoyote na Hamza lakini Hamza alikubali haraka.
“Ngoja nitamsaidia mimi”Aliongea Hamza na kumpokea yule nesi na ni kama alipata nafuu , alionekana kuwa bize hivyo aliondoka mara moja.
“Kapteni usiwe na wasiwasi naahidi sitokuchungulia kabisa “Aliongea Hamza akiwa siriasi.
Yonesi kwasababu mkojo ulikuwa umembana sana hakutaka kujizuia tena hivyo alikubali kusaidiwa.
“Sijasema chochote , nisaidie niingie”Aliongea na Hamza alikubali na alimsaidia mpaka ndani lakini mara baada ya kuingia ndani kulikuwa na tatizo lingine , alishindwa kuinama ili kushusha suruali chini kwani angejisababishia maumivu.
Alijikuta akikakamaa akishindwa kujua afanye nini , aliogopa kujikojolea pia kwa kuogopa aibu atakayoipata.
“Kapteni nitageuka nyuma halafu nitakusaidia kushusha suruali, nadhani hapo hutojisikia vibaya” “Sawa”Aliongea Yonesi maana hakuwa na jinsi.
Hamza alijikuta akigeuka nyuma huku mkono ukiendelea taratibu kushusha suruali ya Yonesi pamoja na nguo yake ya ndani kwa wakait mmoja.
“Taratibu usiniguse”
“Sawa”
“Huko unakogusa ni wapi wewe?”
“Sioni vizuri sasa , basi ngoja niangalie tu”
“Unajitakia kifo sio , ole wako ugeuke”
Mara baada ya kuteseka kwa sekunde kadhaa hatimae alifanikisha misheni ya kuishusha.
Yonesi alijiegamiza katika mwili wa Hamza huku akijitahidi kukaa katika choo , lakini bado alikuwa na wasiwasi Hamza atageuka na kumwangalia
“Usiwe na wasiwasi , kama nilivyosema siwezi kufanya chochote ni bora ujiachie hayo maji yakutoke haraka haraka kuliko kujikaza usitoe sauti”Aliongea
Hamza na kumfanya Yonesi kumwemwesa lips zake alitamani kumwambia Hamza atoke.
Halafu Kapteni ushawahi kuwa mwanajeshi inakuwaje unapata wasiwasi na jambo la kawaida kama hili”
“Kwahio kuwa mwanajeshi ndio nini?”
Aliuliza Yonesi huku akiona asijikaze tena na kuachia kojo limtoke , lilikuwa na presha kama vile bomba la maji limepasuka, isitoshe wote walikuwa kimya hakukua na alieongea.
Yonesi alikuwa na aibu mno ilikuwa afadhali Hamza hakuongea chochote mpaka anamaliza.
“Unaweza kuondoka tu”Aliongea Yonesi mara baada ya kufanikiwa kurudi kitandani.
“Usiwe na wasiwasi , isitoshe bado ni muda wa kazi na hata nirudi kwenye kampuni sitokuwa na chakufanya, kwa maelekezo ya Dokta unapaswa kupumzika kwa siku mbili”
“Siku mbili?”
“Umejiumiza sana na hutakiwi kujiingiza katika matatizo tena , halafu tena umenikumbusha imekuwaje mpaka ukajiumiza ni mbinu gani ambayo umeitumia?”Aliuliza Hamza.
Ukweli ni kwamba alikuwa ashashuhudia mbinu nyingi za mapigano lakini hakuwahi kuona mbinu ambayo mtu anajiumiza mwenyewe kiasi cha kutema damu , alijua lazima mbinu ya Yonesi sio ya kawaida, lakini licha ya kuuliza Yonesi aliendelea kubakia kimya.
“Niwie radhi , huna haja ya kujibu kama ni siri yako?”
“Ukweli ni kwamba hata sijui ni mbinu gani, siwezi pia kusema ni mbinu ya kuamsha nguvu ya ndani?”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Kuna kipindi wakati nikiwa chini ya kitengo kama mwanajeshi katika misheni maalumu katika Jangwa la Sahara niliweza kupata hii mbinu imeandikwa katika Notebook , mtu ambae aliandika nilimkuta akikaribia kupoteza maisha na alinikabidhi , nilimpatia Kapteni hio notebook lakini alisema haina maana yoyote , wakati nikiwa mafunzoni China nilimpa mkufunzi hio notebook na alitafsiri maandishi yale na kusema ni mbinu ya mafunzo ya kichawi ya kuamsha nguvu ya asili ya mwili lakini haijakamilika”
Kwahio uliamua kujifunza bila ya kukamilika kwake?”
“Mwanzoni sikupanga kujifunza ila niliamua kuhifadhi tafsiri yake kama ilivyo , lakini kutokana na maelezo yake yalivyo yalinipa shauku na kuanza kuitumia na wakati nikifanya hivo mwili wangu huwa najihisi ni kama vile unaungua na presha kupanda juu mno huku nikijihisi mwenye nguvu lakini viungo vya mwili huwa ndio vinauma mno, nilikuwa na wasiwasi ni mbinu ya nguvu za giza hivyo sikuendelea nayo sana , lakini mara baada ya kumuona yule Chekani na kutamani kumshinda kwa mbinu yoyote ile nilianza kufuata maelekezo ya hio mbinu na matokeo yake ndio kama ulivyoona”
“Yaani kitu hakikukamilika lakini ukaamua kujifunza?”
“Ndio, mwanzoni nilifanya kutokana na shauku lakini mara baada ya kujaribu yale mabadiliko yalinijengea shauku ya kutaka kujua zaidi , Master alikuwa sahihi kabisa hii mbinu sio nzuri”Aliongea na kumfanya Hamza kumwangalia kwa mshangao kidogo.
Kwanini unaniangalia hivyo?”
“Kapteni nimekusaidia kwenda chooni , vipi mimi unaweza kunisaidia kitu?”
“Niondokee hapa , kuna haja gani ya kurudish kumbukumbu za matikio yaliopita”
“Kukusaidia kwenda chooni inamaanisha wewe ni rafiki yangu mpaka hatua hii ndio maana naomba msaada kama rafiki pia”
“Kama unataka kujamba wewe jamba , huna haja ya kuongea sana”Aliongea Yonesi lakini Hamza alibadilika na kuwa siriasi zaidi.
“Unaweza kuniambia hio mbinu ilivyo?”
“Unataka kujaribu pia , inaweza kukusabishia matatizo?”
“Nataka kuijua tu , usiwe na wasiwasi siwezi kwenda mbali zaidi”
“Basi nitakuambia maana sio kama ni hazina ya maana mpaka nikufiche”
Yonesi mara baada ya kuona namna ambavyo Hamza alikuwa siriasi aliona amwelekeze tu maana ni kama ndio mara ya kwanza anamuona akiwa siriasi.
Fumba macho kisha tengeneza hisia za kusikiliza mapigo ya moyo wako yanavyodunda , iliruhusu nafsi yako kuitawala akili yako , endelea hivo hivyo mpaka uone giza katika macho yako linapotea , litafute jua katika nafsi yako mpaka liwe katika uhalisia wa macho yako kisha lipotezee , utafute mwezi katika nafsi yako na kisha upotezee na kwanzia hapo kila kitu kitajielezea chenyewe kwa kadri unavyoona ….”Yonesi aliendelea kuongea lakini baadhi ya maneno yake hayakueleweka kwani yalikuwa na rahaja ya mafunzo ya kimapigano ambayo mtu wa kawaida hawezi kuelewa.
Hamza aliendelea kuwekeza akili yake katika kile alichoona lakini ghafla alijihisi mapigo yake ya moyo yakizidi kwenda mbio kwa kile alichoona na alijikuta akitoka mara moja katika mawazo yale na kufumbua macho.
Na muda huo huo mlango wa wodi uifunguliwa na msichana mdogo ambae Hamza alimfahamu ni moja ya mlinzi katika idara ya Yonesi aliefahamika kwa jina la Joyce.
“Kapteni vipi hali yako , unaendeleaje?”
Joy unafanya nini hapa muda wa kazi?”Aliuliza Yonesi.
“Mkurugenzi kaniambia nije kumpokea Hamza , maana mimi ni mwanamke mwenzako hivyo ni rahisi kukusaidia”
Yonesi alijikuta akiona aibu kidogo lakini kwa wakati mmoja alijikuta akikasirika alitamani Joy angekuja mapema kabla ya kuaibika mbele ya Hamza.
“Mr Hamza Mkurugenzi anasema urudi makao makuu haraka haraka kuna vitu anataka kukuuliza”Aliongea Joyce na kumfanya Hamza kushangaa kidogo maana aliona kama ni kuuliza si angepiga tu simu, lakini hata hivyo hakuuliza zaidi na aliaga na kuondoka.
Hamza mara baada ya kuingia kwenye gari alijikuta akifikiria kile alichoona wakati wa kujaribu kufuatisha ile mbinu , alijiuliza kwanini aliona sura ya yule mwanamke aliekuwa akichomwa moto kwenye ile ndoto na ni kama alikuwa akimsubiria.
Hamza aliamua kupotezea kwanza swala hilo na palepale aliondoa gari mpaka katika makao makuu ya kampuni na mara baada ya kuegesha gari na
kwenda moja kwa moja katika ofisi ya Regina , alishangaa kumkuta Bibi Mirium akiwa ndani ya ofisi katika kiti chake cha Magurudumu.
Pembeni yake alikuwepo Regina alieismama kiadabu kabisa , hakuwa kabisa na ile hali ya kuwa bosi wa kampuni.
“Kwanini bibi amekuja mpaka huku , shangazi hayupo nyumbani?”Aliuliza Hamza mara baada tu ya kuingia ndani ya ofisi hio na kumfanya Bibi yake Regina kugeuka na kumwangalia Hamza.
“Nasikia umevunja mtu mguu alietumwa na familia ya Benjamini kwa teke moja tu licha ya kuwa na mafunzo ya hali ya juu , nikama nilivyoambiwa unaonekana sio mwepesi mwepesi nadhani ndio maana Regina anakupenda”Aliongea.
“Bibi, Simpendi mimi”Aliongea Regina kwa haraka akikataa.
“Bibi ngoja nikuambie ukweli , yaani tokea nijiunge na hii kampuni nimekuwa na mchango mkubwa sana
, siku nyingine ukija utazisikia sifa zangu tu”Aliongea Hamza
“Hehe,, nimekuja angalau kwa mara ya mwisho
katika hii ofisi ili niweze kuliangalia jiji la Dar kupitia hili dirisha , sidhani kama nitaweza kuja tena kwenye maisha haya. Ila uzee una mambo mengi sana nakumbuka kipindi na babu yako wakati tunasimama hii sehemu baada ya jengo kukamilika mandhari hayakuwa ni ya kuvutia kama ninavyoyaona leo, naona kama uzuri wake umezidi kuongezeka mara tatu zaidi”Aliongea huku akionekana kama vile ni mwenye kujutia.
“Bibi kwanini kila saa unapenda kuongea maneno ya kujikatia tamaa”
“Wewe mtoto sisi wote ni wafanyabiashara na ili ufanikiwe kama mfanyabiashara unapaswa kujifunza namna ya kuukabili uhalisia , haina haja ya kufikiria mambo yasiowezekana kwasababu tu uhalisia ni mgumu , mimi bibi yako siku zangu zinahesabika na nashukuru hata kuweza kufika hapa juu nikiwa katika kiti cha magurudumu , pengie inaweza hata kunisahaulisha kile ambacho nataka kuona kikitokea kabla ya kuondoka”Aliongea na kumfanya Hamza kumkubali huyo bibi aliona ni kama umri wake umemfanya kuzidi kuwa na busara.
Bibi unaonaje tukienda kupata chakula cha usiku katika hoteli kubwa ya kifahari , inaweza kuwa sehemu ya matamanio yako ya mwisho mwisho kutaka kufanya”
“Kuhusu hilo .. nadhani sio mbaya chagua hoteli nzuri kabisa tutaagiza mvinyo wa bei ghali kuliko yote inayopatikana nchini na kusherehekea”Aliongea kinyonge na kumfanya Regina macho yake kuanza kuwa mekundu.
“Nitamwambia Linda aweke utaratibu , vipi nialike na wazee wa kampuni”
“Washaondoka kuna haja gani ya kuonana nao , malizana nao kabisa ndio nitapata nafasi ya kwenda kuwaona , kwasasa sitaki kuwaona maana sidhani kama wana maana yoyote kwangu”Aliongea kikauzu na kumfanya Hamza kuishia kupumua tu kwa masikito aliona kabisa kuna uwezekano Regina karithi kila kitu kwa huyo mzee.
Muda huo huo mwanaume mzee wa miaka kama sabini na kitu hivi mwenye dalili ya mvi aliweza kuingia katika ofisi hio na kumfanya Regina kushangaa.
“Mzee Kibatala kwanini upo hapa?”Aliuliza Regina , Mzee Kibatala ndio aliekuwa mwanasheria mwenye umri mkubwa sana ndani ya kampuni yao na alisimamia maswala mengi tokea kipindi cha babu yake.
Ni moja ya wanasheria ambao walikuwa wakiheshimika mno ndani ya Tanzania nzima.
Kutokana na umri mkubwa aliokuwa nao alijichukulia kama vile amestaafu hivyo kazi nyingi za kampuni zilikuwa zikiwakilishwa na vijana waliokuwa katika ulingo wa sheria na yeye alionekana mara chache sana kwenye maswala ya kisheria ya kampuni.
“Mkurugenzi nipo hapa kwa maombi ya Madam ,
nimeleta wosia na nyaraka nyingine za kisheria”Aliongea.
“Wosia!!”
“Ndio”Aliongea na muda uleule alianza kutoa nyaraka katika mkoba wake wa Briefcase aliokuja nao , ilikuwa ni ile mikoba ya zamani kabisa na ilionekana ulitumika kwa kipindi kirefu mno.
Kwasababu Madam hawezi kusaini na karamu basi tutatumia alama ya vidole vyake , pia nitarekodi tukio zima kwa ajili ya ushahidi”Aliongea.
“Mzee Kibatala amefikiria vya kutosha na ameona huu ndio muda”Aliongea Bibi Mirium.
Muda uleule yule mzee alianza kusambaza nyaraka katika meza ya kioo iliokuwepo katika ofisi hio na kumpa nafasi ya Mirium kuweka kidole gumba katika kila nyaraka
Regina ambae alikuwa pembeni aliweza kuona kila kitu na mara baada ya kuona mwisho wa nyaraka hio alijikuta akishangaa.
“Bibi , unataka kunipa hisa zote?”
“Ndio lakini kama nilivyosema kuna
masharti”Aliongea huku akinyooshea mkono karatasi ya mwisho.
“Sharti langu ni wewe kuolewa , nikifariki bila ya kuona hujaolewa basi hisa zote kisheria zitaenda kwa baba yako”Aliongea na kumfanya Hamza kukunja sura na kujiambia huyu mzee ni mkatili mno kwa kutumia sababu hio kumfosi Regina kuolewa.
Lakini kwa upande mwingine aliona kama hisa hizo zitaenda kwa baba yake Regina basi kampuni inaweza kuwa ndio mwisho wake maana moja kwa moja hisa zote zitakuwa zinamilikiwa na Lamla.
Sasa kama Regina amefanya kazi kwa juhudi kubwa kuifikisha kampuni ilipo ataweza kuruhusu kuona kampuni inaangukia katika mikono ya watu wenye nia ovu.
Upande wa Regina aliona ni kama bibi yake anamuonea na kabla hajaweka kidole gumba katika karatasi yenye masharti alianza kulalamika.
“Lakini bibi mimi sitaki kuolewa nae”Aliongea na kumfanya Hamza midomo yake kucheza na kujiambia kwani amemkosea nini huyo mwanamke mpaka kumkataa waziwazi.
“Mimi sina shida , sio lazima uolewe na Hamza , mimi ninachotaka ni ndoa hivyo sijali nani unaoana nae”Aliongea na kumfanya Regina kuona wazo hilo ni baya zaidi.
“Bibi kwani lazima niolewe , ninao uwezo wa kuendesha kampuni bila ya kuolewa , sitaki mwanaume kabisa”
Huu ni wosia wa baba yako na wa kwangu pia na sifanyi hivi kwasababu sina sababu haya yote ni kwa ajili yako , na nishaweka alama tayari hivyo kama unataka kuilinda kampuni isiende kwa mwingine hakikisha unaolewa haraka iwezekanavyo”Aliongea na kisha alimwangalia Hamza.
“Ila kwa upande wangu nimetokea kumkubali Hamza zaidi kama utaolewa nae una baraka zangu zote”Aliongea na kumfanya mzee Kibatala kutabasamu.
“Madam mimi ninawaacha kazi yangu ishamalizika hapa”
“Asante sana na pole kwa usumfufu matumaini yangu hili swala utalifanya kuwa siri kwa muda”
“Usiwe na wasiwasi Madam”Aliongea na Bibi Mirium alitingisha kichwa kumuaga.
Muda ule hali ya Bibi ilianza kubadilika na kumfanya Regina kumpeleka mpaka chumba cha kupumzikia , ofisi ya Regina ilikuwa na chumba cha kulala na sebule kabisa , ilikuwa ni kama ofisi ndani ya Apartment.
Upande wa Hamza wakati akiwa akimsubiria Regina kutoka ujumbe kwenye simu yake uliingia na alipoangalia namba ni mpya na aliufungua ule ujumbe na alikuta sentensi ya neno’ I am Back – From 2F .
Hamza palepale alijua aliekuwa ametuma ujumbe huo ni Frida na alijikuta akishangaa kidogo na alitaka kuipiga ile namba palepale lakini simu yake ilianza kuita na aliekuwa akipiga ni Eliza.
“Babe naona unanipigia muda wa kazi , utakuwa umenimisi sana nini?”
“Hata sijakumisi , nimesikia Yonesi kalazwa ndio maana nimepiga kujua maendeleo yake”
“Kwahio unachojali ni Kapteni Yonesi tu na sio mimi?”
“Hamna bwana.. ukweli nimepiga kwa ajili yako , nataka kujua kama una ratiba usiku , kama huna unaonaje ukija nyumbani nikupikie chakula kitamu
kama ishara ya shukrani kwa ajili ya matibabu ya mama yangu?”
“Kwa leo haiwezekani , nishakubali kwenda kupata chakula cha usiku na bibi yake Regina”
“Oh… basi hata siku nyingine tu”Aliongea Eliza kinyonge.
“Babe ila usiwe na wasiwasi naweza kuja hata baada ya chakula”
“Sikufungulii mlango”
“Napitia dirishani”
“Halafu wewe .. sitaki kuongea na wewe”Aliongea na muda uleule simu ilikatwa.
Hamza mara baada ya kusikia sauti tamu ya Eliza moyo wake ulianza kuhisi majuto , na kuanza kujiuliza au baada ya chakula aende kwake kumfanyia surprise , pengine anaweza kupewa tunda.
Hamza mara baada ya kurudi katika ofisi yake ili kupoteza poteza muda ghafla tu mlango wa ofisi yake ulifunguliwa bila hodi na aliengia alikuwa ni Linda.
“Hamza”
“Kuna nini?”
“Bibi kazidiwa , wahi ukawashe gari
tunamshusha”Aliongea Linda na kumfanya Hamza muonekano wake kubadilika mara moja na kitendo cha kutoka aliweza kusikia sauti ya kilio cha Regina akimwita bibi yake aamke.
Comments