Dina alipata ahueni mara baada ya kuona Hamza hajakasirika , alifika hapo akiwa na hofu mno, baada ya kushusha pumzi hatimae aliwageukia wale watu waliomchukua Hamza kwa kujifanyisha ni polisi.
“Nimewaambia nini kuhusu kutojihusisha na maswala ya uhalifu hasa kipindi hiki cha uchaguzi?”Dina alifoka kweli
“Boss sikujua kama unafahamiana na huyu Hamza , kama ningejua ni Braza nisingeenda mbali na kupokea maagizo ya Zefa haha..”
“Nani kasema mimi ni Braza kwako …”Aliongea Hamza lakini bwana aliefahamika kwa jina la Kidula hakutaka kujali kauli yake , bado alikuwa na chembe za dharau kwa Hamza , ilikuwa ni kama anajiamini bosi wake hawezi kumfanya lolote.
“Boss ni kweli kabisa sikuwa nikifahamu kama unamjua Hamza , tunaomba ututambulishe ili swala kama hili lisije kujirudia?”Aliongea Kidula , wakati huo Zefa alikuwa kimya tu akiwa na wasiwasi.
“Hakuna hata mwenye thamani kati yenu wa kumjua hapa”Aliongea Dina kwa dharau.
Ukweli ni kwamba huyo Dina mwenyewe hakuwa akimjua Hamza ni hisia zake tu ndio zilikuwa zikimwambia sio mtu wa kawaida ambae nchi ndogo kama Tanzania inaweza kudili nae.
“Hamza , unataka tulimalize vipi hili swala ?”Aliuliza Dina.
“Hawa watu wako sina shida nao , hakikisha siku nyingine hawajitokezi mbele yangu , kuhusu huyu nataka akiondoka hapa sio
mwanaume”AliongeaHamza akiwa katika hali utulivu na kauli yake ilimshitua Zefa.,
“Mr Hama naomba tulimalize hili swala , kama ningejua mapema nisingekuchokoza , nipo tayari kukupatia kiasi chochote cha pesa , naomba tusiende mbali”Aliongea Zefa.
“Sina shida na hela zako , watu wa aina yenu hamtakiwi kuwepo uraini kama sio kufa basi ni kifungo cha maisha, lakini hayo yote nimeyasamehe kwa kukupa adhabu ndogo”Aliongea aliongea na kumfanya Zefa kuzidi kuwa na wasiwasi.
“Dina.. Madam boss , hebu fikiria mara mbilimbili, kundi lenu hili ni la kihalifu na mzee ni moja ya watu ambao wanafumbia macho uhalifu uneondelea, ukinigusa mimi jua umeigusa serikali , najua jana nimekosea lakini tunaweza kulimaiza kwa pande zote kutokuathirika”Aliongea Zefa.
“Haha.. haha….unasema nikikugusa nagusa serikali ..haha”
Dina alicheka kicheko cha ajabu kweli na ilikuwa ni ghafla tu ashatoka aliposimama na kwa spidi kubwa alipiga hatua mbele na kilichofuatia ilikuwa ni Kidula kushika shingo yake huku akianza kutetemeka na ishara ya damu kumtoka eneo la shingonni zilionekana..
Ki ufupi ni kwamba alikuwa amekatwa eneo la shingoni na hata haikueleweka mrembo huyo alitoa wapi kisu lakini miondoko yake ilikuwa ni ya kuogofya mno.
“Nimerudia zaidi ya mara tatu sitaki kusikia swala la uhalifu , hasa kipindi hiki cha uchaguzi lakini hakuna anaelewa ninachomaanisha kwa maneno , nadhani hii ndio itaonyesha ni kwa namna gani nipo siriasi”Aliongea Dina na muda uleule Kidula aliondoka huku akianza kuchezesha miguu yake akipambania uhai.
Dina licha ya kuuwa hakuonyesha ishara ya hatia hata kidogo , ilikuwa ni kama mtu alieua kuku.
Vijana wote waliokuwa ndani ya hilo eneo walirudi nyuma huku hofu ikionekana katika macho yake.
“Hivi umesema baba yako ni nani vile..?”Aliuliza Dina huku akiangalia kisu kilichokuwa mkononni kwake , ilikuwa ni kama anaangalia kuona kama kuna damu yoyote imebakia lakini hakukuwa hata na doa ikionyesha spidi yake ya kuua ilikuwa ya juu mno.
Kisu hicho kilikuwa kidogo mno kama vile vya kufanyia upasuaji , pengine ndio maana hakikuonekana mkononi kwake mpaka pale alipoua mtu.
Zefa alianza kutetemeka huku akirudi nyuma kwa hofu, ule ujasiri wake wote ulimpotea mara baada ya kuona namna ambavyo Kidula alikuwa akitapatapa kupambania uhai wake.
Dina hakuwa mwanamke mrembo tena , alikuwa ni muuaji mwenye sura ya kirembo ambae huficha matendo yake kupitia biashara ya kuuza chai , sasa Zefa anajua kwanini mrembo huyo alikuwa akiogopeka na kufanya kundi la chatu liwe na nguvu.
“Rudia kauli yako , umesema nikikugusa nimegusa nini…?”Aliuliza Dina mara baada ya Zefa kushikiliwa na moja ya mwanaume aliekuwa nyuma yake asizidi kurudi nyuma.
“Naomba unisamehe ,nitafanya chochote kile , naomba usiniue…”Zefa mara baada ya kuona hakuna dalili ya huruma kwenye macho ya mwanamke Dina aliamua kupiga magoti na kupasha viganja.
“Hamza naomba unisamehe , sitomsumbua tena Eliza , mkiniachia nitaenda kujisalimisha polisi kwa nilichomsababisia mama yake…”Mwanaume alipasha viganja na muonekano wa Zefa ni kama sasa ulimridhisha Dina.
“Naweza kuonekana mwanamke mrembo na mlaini laini, lakini hiko ndio ninachowapa walimwengu kuona , huku uhalisia wangu ukibakia siri, unadhani baba yako ana nguvu ya kuizima nguvu yangu hapa nchini, kama ni hivyo tutaona hilo kuanzia leo”Aliongea Dina na kisha alisimama.
“Kama hamtaki yawakute kama yaliomkuta mwenzenu kiukeni maagizo yangu tena, hakikisheni haondoki na korodani hata moja na mtupeni barabarani kisha nisiwaone hapa wote muwe chimbo mpaka nitakapotoa maagizo mengine”
“Sawa Madam boss”
Vijana wale angalau hali ya ahueni iliwapata mara baada ya kuona wamesamehewa na hawakutana na kifo kama ilivyokuwa kwa Kidula.
“Nadhani mnajua cha kufanya juu ya huu mwili , hakikisheni mnasafisha kwa kufuata itifaki”Aliongea na kisha aligeuka na kumwangalia Hamza.
Upande wa Hamza hakuonyesha mshituko wowote , ilikuwa ni kama anaangalia kitu cha kawaida , pengine watu kwake kushuhudia kifo ni swala la kawaida ndio maana muonekano wake haukua na mabadiliko.
“Kwahio hili ni kwasababu ya yule mwanamke tena…?”Aliongea na swali hilo lilimfanya Hamza kushangaa na hakuelewa muda huo Dina alikuwa na hasira au na furaha ilikuwa ngumu kuelezea muonekano wake.
“Ni bahati mbaya tu ilionifanya kukutana nae , ndio maana…”
“Huna haja ya kujielezea naelewa”Aliongea huku awamu hio akiwa na sura ya huzuni na kisha alimpita Hamza na kuliendea gari lake.
Hamza alikosa neno lakini hata hivyo aliona anapaswa kumpeti peti mrembo huyo, hivyo alimfuata haraka haraka katika gari yake ya Mercedenz Benz S600
Gari hio ilikuwa ya thamani , japo sio sana lakini kwa mazingira ya Tanzania ni moja ya gari za bei ghali , uzuri wake zaidi ni kwamba hio gari vioo vyake havikuwa vya kawaida , ilikuwa kama gari za mercedenz zinazoingia nchini lakini ilikuwa imetengenezwa kwa mfumo wa ki usalama wa hali ya juu.
“Dina usiwe hivi , mimi na Eliza sio kama unavyofikiria”Aliongea Hamza, alishajua mrembo huyo ana taarifa zote kuhusu Eliza ndio maana hakutaka kujizuia kumtaja jina lake.
“Huna haja ya kuongea , kunikataa kwako kote kule kumbe kuna mtu ambae ushampenda tayari , haishangazi , moyo wako umejaa ndio maana nimekosa nafasi”Aliongea na kumfanya Hamza kuvuta pumzi.
“Dina sababu ya wewe kukosa nafasi ni kwasababu tayari ushaujaza moyo wangu muda mrefu tu”Kauli ile ilimshangaza sana Dina.
“Kweli!!?”Aliuliza akiwa kama hajategemea kauli hio.
“Ni kweli , kama isingekuwa hivyo unadhani kwanini asubuhi nilikutumia ujumbe wa maandishi juu ya kufuatiliwa na watu wako, ningekuwa sikujali nisingehangaika ningewaua wote , lakini nikafikiria na kuona vipi kama nitawaua wote utajielezea vipi mbele ya Umoja , ki ufupi ningekuingiza matatizoni na ungepokonywa uongozi”.Aliongea na kumfanya Dina kufikiria hilo na kuona inaleta maana na alijikuta akitabasamu.
“Mimi na yeye nani mzuri zaidi?”Ilikuwa zamu ya Hamza kushangazwa na swali hilo.
“Bila shaka wewe ndio mrembo zaidi”Aliongea
Hamza huku akimkonyeza kichokozi lakini ilimfanya Dina kucheka vizuri na kwa jinsi alivyokuwa akionekana utadhani sio yeye alieua mtu dakika chache zilizopita.
“Unachojua ni kunichokoza tu muone, kama kweli unanipenda kama unavyyosema , kwanini hutaki hata kulala usiku mmoja kwangu kama ulivyofanya kwake?, Au mimi sikuvutii kama yeye?”
“Naona umefanya uchunguzi wa kutosha mpaka ukajua nimelala kwake”
“Nani kakuambia unipotezee , unadhani nitakaa chini
tu bila kufanya chochote , nilitaka kujua ni mwanamke wa aina gani huyo amekuteka”
“Sijakupotezea Dina unajua nikwasababu…”Alisita.
“Sababu gani?”
“Ni kwasababu sina malengo makubwa ya kimaisha , nilichotaka ni maisha ya amani kuishi maisha ya kawaida , kuwa na wewe moja kwa moja maisha yangu yatabadilika”Aliongea lakini kauli ile palepale ilimfanya mrembo huyo kubadilika.
“Ondoka mbele yagu”Aliongea kwa kufoka
“Nimekosea nini?”
“Nimesema ondoka mbele yangu, sitaki kukuona tena”
“Dina kama nimekosea sema , acha kukasirika basi”
“Achana na mimi , kwahio kwa macho yako unaona kuwa na mimi kutakufanya ukose amani kiasi cha kuyabadilisha maisha yako,Hamza umeniangusha sana leo”Baada ya kauli hio palepale mlango ulifungwa kwa nguvu na gari iligeuzwa na ikatolewa nduki.
Hamza aliishia kuvuta pumzi na kuzishusha huku akiwa ameshika kiuno, hakujua kauli yake ingemkasirisha mno Dina , eneo hilo lilikuwa mbali na muda umeenda na aliona hata kipindi kishampita.
Aligeuka na kuangalia namna ya kuondoka hapo ndani lakini ile gari ya Corolla iliokuwepo hapo ndani ilikuwa imepakia ile maiti kwenye buti pamoja na Zefa aliekuwa amepoteza fahamu.
Hakutaka kuingia ndani ya gari hio , hivyo alitoka na kuanza kutembea wa mguu akiamini angepata usafiri wa daladala kurudi.
Kitendo cha kufika kuipita Bar iliofahamika kwa jina la Jiteketeze tu gari aina ya subaru nyeusi ilisimama pembeni yake na kioo kilishushwa na bwana mmoja mweye muonekano wa kihindi.
“Wapi Braza nikupe lift?”Aliuliza yule bwana na kumfahya Hamza kutabasamu.
“Haina haja ya kujifanyisha wakarimu , wakati ni wiki nzima sasa tokea muanze kunifuatilia, hamchoki tu?”Aliongea na kauli ile ilimfanya yule Mhindi kutoa tabasamu na aligeuza uso wake nyuma kana kwamba kuna mtu anamwangalia ndani ya gari hio.
“Uko vizuri , hatukujua kama ushatufahamu , unaonaje ukiingia ndani ya gari tukiongea kidogo?”
“Haina tatizo , nilikuwa nikitafuta lift hata hivyo?”Aliongea Hamza na bila ya kujiuliza mara mbilimbili alifungua mlango na kuingia ndani na hapo ndipo alipoweza kuona watu wengine wawili wakiwa siti za nyuma , mmoja alikuwa ni shombeshombe(Colored) mwenye nywele ndefu kama rastafarians na mwingine alikuwa ni mzungu.
“How did you discover us?”Aliongea kwa kingereza yule mweusi mwenye rasta.
“Kuna hata haja ya kuuliza , mlilipa hadi vijana waanze kunifuatilia huku wakijifanyisha kucheza pooltable karibu na ninapoishi , hii gari ndio iliokuwa ikinifuatilia juzi nilipokuwa Morogoro road, kwa rafudhi yako inaonekana umeishi sana visiwa vya Samar, kama sikosei kwa Tattoo hio kwenye mkono wako mnatokea katika kundi la wawindaji la Waray kutoka mji usionekana wa Biringan”
Kauli ile ilimfanya yule bwana aliesuka rasta kushangaa kidogo na kuonyesha kuridhishwa na Hamza..
“Ni kama tulivyosikia sifa zako za kutokuwa binadamu wa kawaida, haishangazi ndio maana una urafiki na mtu mkubwa kama Dokta Genesha” Hamza mara baada ya kusikia neno Dokta Genesha ni kama sasa ashajua nini kilichowaleta Tanzania kutoka Ufilipino.
“Sijali mnachotafuta wala mnachopanga , lakini hamtakiwi kuwepo Tanzania”
“Umoja wetu wa wasionekana unamtafuta Dokta Genesha dunia nzima , ndani ya maabara ya Trishaza tulikuta taarifa zako zote ikiwemo sehemu unayoishi kwasasa , kitendo cha Trishaza wa Tembo kuwa na taarifa yako inaonyesha ni kwa namna gani mna
ukaribu , swali letu ni wapi alipo Trishaza wa
Tembo?”
“Nadhani kila mmoja anajua Dr Genesha alishafariki , hii sio siri na hata kwenye vyombo vya habari ililiripotiwa”
“Unachosema ni kweli , lakini hapa tunamzungumzia Dr Genesha ambae ni Trishaza Wa Tembo , lolote linawezekana”
“Narudia tena mnaemtafuta alishakufa tena sio kufa ameuliwa”Aliongea Hamza na wakati huo sauti yake ilionekana kuwa siriasi.
Jamaa aliefamika kwa jiina la Mendoza , huyo mwenye marasta alimeza mate na palepale ni kama mwili wake ulianza kutuna na nguvu isioonekana ambayo haikuwa ya kawaida iliongezeka.
“Kama kweli amekufa , tunataka kujua kitabu cha ufunuo wa Njiwa Juu Ya Mti Wa Uzima kipo wapi .
je unajua alipokificha kabla hajafariki au kama alikuambia itakuwa vizuri ukituambia?”Aliuliza bwana mwingine ambae alikuwa mzungu , huyo aliitwa Dodo.
“Mnachotafuta ni hadithi ya kufikirika tu na hakuna ukweli wowote kuhusu uwepo wa hicho kitabu na sidhani kama kweli kuna huo ufunuo wa Njiwa juu ya mti wa Uzima”
“Acha porojo , taarifa tulizopata ni kwamba kabla ya kufariki kwa Dokta Genesha alitoa kauli kwamba ya ‘wanachokitafuta hawawezi kukipata’ , unadhani alikuwa akimaanisha nini? , moja kwa moja tunaamini kuna mtu aliemuachia urithi na urithi huo ni juu ya kitabu hiko cha Ufunuo”
“Nadhani hamuelewi na mnataka kulazimisha vitu ambavyo havipo , kwa hiari yenu niachieni hii gari, nitahesabu mpaka tatu , sitaki kuona mtu ndani ya gari”Aliongea Hamza kwa sauti ya kibabe.
“Moja…, Mbili..”
“Tunaondoka”Aliongea Mendoza Rastamani na aliwapa ishara wenzake na kushuka katika gari.
Mara baada ya wote kuondoka Hamza hakuchelewa aliushika usukani na kuondosha gari hio kwa spidi.
“Dokta Genesha sikutaka kukuamini tokea mwanzo juu ya ulichoniambia, ila kama sio shida yangu ya kutaka kumfahamu Mzee nisingeendelea kubaki na kitu ambacho kinanifanya niwe shabaha ya watu wengi.
Kazi imeanza , maisha ya utulivu nishayaishi ni muda sahihi wa kuanza kumtafuta Mzee , nitafuata ushauri wako , kama kuna ukweli wa simulizi ya Njiwa juu ya Mti wa Uzima basi malengo yangu yatafanikiwa”Aliwaza na muda huo alifanikiwa kumkwepa mtoto aliekuwa akiendesha gurudumu barabarani na kumfanya mawazo yake yarudi katika uhalisia.
Dokta Raphaeli Genesha ndio jina lake, ni raia wa Ureno ambae amechanganya rangi kwa kuzaliwa na baba wa kijapani na mama wa kireno.
Kabla ya kutambulika kwake kama mwanasayansi aliewaacha wanasayansi wenzake mdomo wazi alikuwa ni muumini mtiifu sana wa kanisa la kikatoliki.
Mara baada ya kuishi katika misingi ya kiimani kwa miaka mingi ndipo aliposhikwa na shauku na shauku yake ndio ambayo ilimtambulisha leo hii na pengine kumsababishia kifo chake.
Huyu ndio mwanasayansi ambae alitoka hadharani na kusema kwamba Spirituality is real na anao uwezo wa kuthibitisha hilo.
Kauli yake hio iliinua mijadala mingi sana kwa wanasayansi wengi duniani huku wengi wakienda mbali kwa kusema hilo ni swala ambalo haliwezekani kwani sayansi msingi wake ni majaribio na majaribio hayo sio juu ya namna kitu kinavyofanya kazi bali ni sababu ya kitu hicho kufanya kazi kwa kufuata mchoro wa tabia husika.
Ukweli ni kwamba hata huo uthibitisho hakuwahi kuuweka wazi lakini baadhi ya watu walianza kumuunga mkono bila ya kuona ukweli husika , huku wale waliokuwa wakimuunga mkono ni kulingana na hisia zao tu juu ya matukio yaliowapata yasioelezeka.
Miaka miwili mbele baada ya Dokta Genesha kutangaza msimamo wake kama mwanasayansi ambae anaamini uwepo wa nguvu za kiroho hatimae alikutwa na umauti na ushahidi wa juu ya ukweli aliokuwa akizungumzia hakuweka wazi na stori yake ikaishia hivyo.
Ni sawa leo hii atokee mtu aseme anao ushahidi wa kisayansi wa kuthibitisha uwepo wa Mungu, ndio iliyokuwa kwa Dokta Genesha.
Sasa kuhusu kuwa na ukaribu na Hamza haikueleweka ilikuwa vipi na historia yao ipoje mpaka kuja kufatiliwa na kundi la wawindaji kutoka visiwa vya Samar.
******
Dakika kadhaa mara baada ya Hamza kuondoka , wale watu wote watatu walisogea upande wa barabarani na kuingia katika gari aina ya Toyota Crown nyeupe , ndani ya gari hio kulikuwa tayari na mtu mwingine na ilionekana walikuwa wakimwambia kilichotkea.
“Umesemaje ,unamaanisha alikuwa akijua uwepo wetu tokea muda mrefu?”Aliuliza , alikuwa na sauti ya kike hivyo ikiashiria ni mwanamke na mkononi alikuwa ameshikilia picha.
“Mbona anaonekana wa kawaida sana , inawezekana amewapiga mikwara kuwaogopesha tu”
“Haiwezekani, anaonekana sio wa kawaida kabisa na ni mtaalamu, nilikuwa karibu yake lakini kila nilipo jaribu kuamsha uwezo wangu wa kichawi pumzi zilikuwa zikiniishia, anaonekana kuwa na mwili dhaifu mno lakini sio wa kawaida, hisia zangu zimeniambia kama nitamshambulia kuna uwezekano wa kutopona”
“Uwezo wako unachukuliwa kama wa juu ndani ya umoja , haiwezekani awe amekuzidi?”Aliongea yule mwanamke.
“Kwahio vipi kama akiwa na uwezo wa juu , ijapokuwa umoja wetu unachokuliwa kama daraja B lakini kazi hii sisi ndio tumepewa kwasababu ilionekana tunao uwezo wa kuikamilisha , Tanzania inaonekana kama nchi tulivu sana ila kuna mambo mengi yasioyakawaida yanaendelea , tunapaswa kuwa makini hasa nyakati za usiku”Aliongea Mendoza.
“Ila sidhani kama itakuwa rahisi kupata uelekeo juu ya kitabu hiki kilipo, mtu ambae ana urafiki na Dokta Genesha hawezi kuwa wa kawaida”
“Mbona kama tunaogopeshana , sisi ni wawindaji na sifa ya muwindaji hawezi kuacha kitoweo kupita mbele yake kirahisi , Tumekuja mpaka Tanzania kwasababu ya kazi na tunapaswa kuimaliza ili kuwa na maelezo ya kutosha mbele ya wakuu wetu”Aliongea Dodo.
“Kwahio ni hatua gani tuendelee nayo , ashatuona tayari hivyo atakuwa ni mwenye tahadhari”
“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi , kwasasa kitu pekee tunachoweza kufanya ili kupata taarifa kutoka kwake ni kupitia watu wake wa karibu”
“Unamaanisha nini Huda?”Aliuliza Mendoza akimwangalia mwanamke aliekuwa mbele yake , alifahamika kwa jina la Huda.
“Mendoza umeshanielewa ninachomaanisha”
“Sidhani kama ni wazo zuri ila kwasababu hatuna namna na tunahitaji matokeo tuendelee kumfuatilai kwa ukaribu , Udhaifu wake utaonekana na tutautumia vizuri”Aliongea yule Mhindi na kauli yake iliungwa mkono.
***
Hamza mara baada ya kutoka hapo aliona haina haja ya kwenda chuo na kwasababu alikummbuka Regina alimpigia simu alijua kabisa alikuwa akihitaji arudi nyumbani hivyo moja kwa moja aliona aelekee huko lakini kabla ya hapo aliona kwanza arudishe gari aliokuwa akiendesha.
Gari hio ilikuwa na nembo ya kampuni ya kukodisha magari ya DriveUs na Hamza aliijua fika kwani ashawahi kukodi gari katika kampuni hio ,ilikuwa na makao yake Posta lakini Hamza hakuona haja ya kupeleka gari hio Posta kwani wenyewe walikuwa na mfumo wa kufatilia magari yao pale aliekodishwa asiporudisha.
Dakika kadhaa tu alikuwa ashafika Kigamboni na alitafuta eneo na kuegesha gari hio katika megesho ya moja ya supermakert, alitembea mpaka zilipo bodaboda na kisha alitoa maelekezo ya eneo analoelekea na alichukuliwa kuelekea huko.
Alikuwa na uhakika wa kumkuta Shangazi nyumbani hivyo hakuwa na wasiwasi.
Dakika kumi na tano zilimtosha kufika kabisa , ukweli ni kwamba hakuwa hata na haja ya kupanda pikipiki kutokana na ukaribu wa mji wa Egret lakini kwasababu kulikiuwa na jua kali hakutaka kutembea.
Baada ya kushuka tu kwenye pikipiki na kubonyeza kitufe cha kengele hatimae aliweza kusikia sauti ya furaha ya shangazi kutoka ndani.
Mfumo wa nyumba wa kengele ulikuwa umeunganishwa na kamera na kifaa cha kusafirishia sauti na muda uleule mlango wa geti la kuingilia ulijifungua na akazama ndani.
“Hatimae umerudi nyumbani , nilikuwa na wasiwasi mno “Aliongea Shangazi ambae alionekana kuwa na furaha kabisa kumuona Hamza amerudi na mapokezi hayo yalimfanya kujihisi kuwa mwenye hatia , kwani Shangazi alimchukulia Hamza kama mwanafamilia ilihali alikuwa akiujua ukweli yupo hapo kwa muda tu .
Lakini sasa wakati Hamza anataka kuingia ndani sauti ya mwanamke anayoifahamu ilimwita.
“Hamza!,Unafanya nini hapa?”
Hamza alishangaa maana hakutegemea , aliinua kichwa chake na mara baada ya kuangalia eneo la sebuleni ndio sasa aliweza kumuona Eliza akiwa amekaa kwenye sofa.
Comments