“Kwa.. kwanini?”
Regina alitaka kujua sababu ya Hamza kumuua mtu , alitaka angalau kujua sababu pengine anaweza kujishauri, tokea siku ambayo aliweza kuona Hamza akiifahamu lugha ya kifaransa vizuri , siku ambayo alijua Hamza anafahamina na mshonaji nguo mkubwa alijua fika pengine kuwa mwanachuo , fundi na mwalimu ni namna ya kuficha ubini wake , lakini licha ya hivyo ilikuwa ngumu kwake kumvumilia kama kweli amemuua mtu bila sababu licha ya kwamba hakujua uhusika wake.
“Nimewaua kwasababu walistahili kufa”Aliongea Hamza
“Kwahio unajiona Mungu?”Aliuliza kwa hasira Norbert.
“Wame… inamaana sio mmoja?”Aliuliza Regina kwa mshangao.
“Huna haja ya kuniangalia hivyo , nilichofanya ni kama mwanajeshi kumuua adui , siwezi kuhesabika muuaji kwasababu nimemmaliza adui na kurudisha ushindi nyumbani , siwezi kuua bila sababu lakini ikitokea nipo hatarinni na watu wangu wa karibu kuwa hatarini ni sababu tosha”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha mbele ya adui yangu ninachukua uhusika wa mwanajeshi na kazi ya mwanajeshi ni kuangamiza adui , hivyo sio tu jana wala kesho adui ambae ni hatari kwa usalama wangu anastahili kifo”
“Unazunguka zunguka sana na maneno mengi , au ndio sababu inayokufanya unaficha ficha mambo yako mengi”Aliuliza Regina.
“Kuna zaidi ya sababu kwa kila ninachofanya”Aliongea “Wewe ni muongo..”Regina alitaka kuongea zaidi kihasira lakini alishindwa, aliishia kuondoka mbele ya Hamza na kuingia ndani ya hospitali.
Muda uleule mara baada ya Hamza kuondoka wale mapolisi walimzingira , ni kama hali yao ya kujiamini imerudi mara baada ya bosi Regina kuondoka.
“Mr Hamza kwanza kabisa nijitambulishe vizuri ,naitwa Kapteni Norbert Geza kutoka kitendo cha usalama wa nchi , lakini vilevile nafahamika kama Jino la Fisi, matendo yako yameweka usalama wa nchi katika sintofahamu na kwa kosa hilo rasmi sasa tutakukamata”Aliongea Afande Norbert huku akijiambia potelea pote wamesema waachane nae ni wao ila yeye anamkamata akamhoji.
“Kwahio kweli unataka kunikamata?”
‘Unataka kukataa , hii ni Tanzania , hivi unajua nini kitakupata ukitaka kushindana na sisi”Aliongea Afande Gamale.
“Natamani kuona kipi kitanipata”Aliongea Hamza. “Afande Gamale acha kujibishana na huyo mhalifu mfunge pingu”Aliongea Afande Kyombo.
Gamale hakutaka kuchelewesha na alimsogelea Hamza akitaka kumvisha pingu lakini wakati akitaka kufanya vile ni kama macho yake yaliingiwa na ukungu na ashindwe kumuona Hamza mbele yake wakati akili yake inakuja kukaa sawa alishangaa yeye ndio amefungwa pingu na alijikuta akibung’aa.
“F*ck you “
Kyombo kitendo cha Gamale kuvishwa pingu na Hamza aliona ni tusi kwa jeshi la polisi na kwa hasira alifyatuka na teke akidhamiria kumpiga Hamza , lakini kabla ya kumkaribia Hamza alibadilishana nafasi na Gamale kwa kumvutia aliposimama na kutokana na Kyombo kutumia nguvu nyingi alishindwa kuzuia shambulizi lake mara baada ya kuona linaenda kumpata Gamale. “Puuh!!
Gamale alijikuta akichwapwa teke na mwenzake na kwenda chini huku akigulia maumivu. “Kyombo umekuwa kichaa , mbona unanipiga mimi”
“Unauliza ujinga ,kwani nimekupiga makusudi?”Aliongea Kyombo huku akiwa na hasira nyingi.
“Nitalipiza , huwezi kunipiga teke kubwa hivi, umefanya makusudi”Aliongea Gamale kwa hasira huku akijaribu kusimama lakini kutokana na pingu alijikuta akirudi ardhini.
“Afande Kizito mfungue Gamale hizo pingu”Aliongea Norbert mara baada ya kuona timu yake inapaluana wakiwa wamesahau adui yao ni Hamza. “Sawa kapteni”
Niobert alikuwa akiongoza vichaa wenzake , ni kama wote walikuwa wakifanana tabia , mara baada ya Gamale kuondolewa zile pingu walimzingira Hamza na kuanza kumshambulia
Lakini mbele ya Hamza aliona ni kama ngumi za wanawake wanaojaribu kuwa na hasira mbele ya mwanaume wanaempenda hivyo alizikwepa kama anacheza Amapiano.
“Wewe mpuuzi hebu acha kutukimbia , ni mwanaume kweli wewe?”.
“Kama unadhani mimi sio mwanaume kamuulize mpenzi wangu”Aliongea Hamza.
“Niachieni huyu mimi namwendea na pigo za kijetilii , tuone kama atakwepa kwepa kama anacheza rede”Aliongea Kyombo na kuanza kurusha miguu , japo alionekana kuwa na stamina na mafunzo kiasi lakini kwa Hamza ilikuwa kichekesho maana alimuacha amsogele na kisha aliudaka mguu wake na kuusukuma na kumfanya adondokee makalio yake kwa nguvu.
Baada ya kuona Kyombo ameshindwa waliobaki wote walimsogelea Hamza na kuishika mikono yake wakitaka kuikutanisha kwa ajili ya kuifunga pingu lakini licha ya wote wawili kutumia nguvu kubwa walishindwa kuikutanisha kadri walivyokuwa wakiisukuma., walihihisi ni kama wanasukuma chuma kizito.
Upande wa Kapteni Norbert alikuwa pembeni akiangalia vijana wake wanachokifanya.
Baada ya kuona wameshindwa kuuipindishahata kidogo mikono ya Hamza alijikuta akishangaa.
“Hamza kama sikosei hio ndio mbinuu maarufu inayofahamika kama Joho la Chuma”Aliongea Norbert
“Kama unaijua basi utakuwa unajua pia namna ya kuishinda , acha kutegea wenzako fanya na wewe shambulizi”Aliongea Hamza.
“Nilikuwa najiandaa”Aliongea Norbert na muda ule alianza kuizungusha mikono yake hewani kana kwamba anajaribu kukusanya nguvu ya kiroho.
Upande wa Hamza alikuwa ameshikiliwa na polisi wawili , kama vile walikuwa wakitaka bosi wao ampige Hamza shambulizi la kifuani.
Norbet mara baada ya kujikusanya kwa sekunde kadhaa alifyatuka kwa spidi kiasi kwamba alisababisha hadi upepo kama vile ni gari ambayo ilikuwa kwenye spidi kubwa na kumsogelea Hamza kwa kasi , lilikuwa ni teke la tiktaka ambalo lilienda kutua katika kifua cha Hamza.
“Bam!!
Sauti iliosikika ni kama vile mtu anafungua mlango kwa teke na mlango ukagoma kufunguka
Polisi wale walijikuta wakipatwa na wasiwasi kutokana na ukubwa wa teke lile na kuona limemsababishia Hamza matatizo.
Lakini mara baada ya kumwangalia Hamza walishangaa akiwa amesimama na hakuwa na mabadiliko yoyote hata kidogo.
“Unaonekana umejifunza funza, Precelestial Kick sio mbaya , ila umetumia hisia nyingi sana kwenye hili teke”Aliongea Hamza
Afande Norbert alijikuta akibung’aa mara baada ya kukaa sawa na kumuona Hamza yupo vilevile kama jiwe , sio kwake tu hata kwa wenzake pia.
“Vipi kuna mwingine ana shambulizi ambalo anataka kunionyesha?”Aliuliza Hamza akiwaangalia kwa zamu.
Wale polisi waliokuwa wamemshikilia Hamza walijikuta wakianza kushikwa na woga na walimuachia na kurudi nyuma.
“Hamna uwezo hata wa kunipiga halafu mnataka kunikamata , sidhani hata mna vigezo vya kuongea na mimi , poteeni wakati nikiwa na roho ya kistaarabu”Aliongea Hamza huku akianza kutoa msisimko ulioanza kumtisha Norbert kiasi kwamba mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda mbio mno.
“Hii ni Tanzania nchi ya amani huwezi…”Alitaka aendelee kujibishana lakini Hamza alimsogelea na kumpiga kofi la kifuani na kumfanya adondoke chini kama mzigo .
“Kapteni!!”
Wale polisi walijikuta wakimkimbilia mwenzao wakidhani amekufa maana sio kwa uzito wa bao lile.
Walijikuta wakipatwa na ahueni kapteni wao alikuwa hai licha ya kutema damu , lakini upande wa Norbert aliona kama Hamza angetumia nguvu kidogo kwenye mkono wake basi kifo kingemkuta palepale.
Wale polisi mara baada ya kuona Kapteni wao hali yake si nzuri walimbeba na kumrudisha kwenye gari na safari ya hospitalini ilianza mara moja. *****
Hamza mara baada ya kuingia ndani aliweza kumuona Regina akiwa ameshika kile cheti cha ndoa mbele ya bibi yake , alikuwa na furaha , ule muonekano wake wa nje ulikuwa umepotea na ilimfanya Hamza kuvuta pumzi ya ahueni.
Bibi Mirium mara baada ya kumuona Hamza alitoa tabasamu hafifu huku akimpa Hamza ishara ya kumsogelea.
“Safi sana .. wewe ni mtoto mzuri”Aliongea Bibi Mirium.
“Bibi kuna kitu unataka tena?, niambie nitakamilisha”Aliongea Hamza. “Haraka iwezekanavyo mfanye Regina apate mtoto
, ndio njia ya kuifanya nyumba yako kuchangamka”
“Bibiii!!!” Regina aliongea , aligeuka mwekundu kwa aibu kiasi kwamba hakutamani kuendelea kubakia ndani ya wodi.
“Nimekuelewa bibi nitalifanyia kazi”Aliongea Hamza akitingisha kichwa kukubaliana nae
Bibi Marium alitoa tabasamu hafifu na kisha alifunika macho yake kana kwamba amekwisha kushoshwa na dunia na yupo tayari kuondoka.
“Regina unaonaje tukitoka nje kidogo , kuna vitu nataka kukuambia”Aliongea Hamza na Regina alisita kidogo lakini aliishia kugeuka na kutangulia nje.
Mara baada ya kufika mwishonni mwa korido haikuwa na mtu yoyote hivyo ilikuwa sehemu nzuri kwao kuongea.
“Vipi kuhusu wale polisi?”
“Wameondoka”
“Kwanini hawajakuchukua?”
“Mbona kama unataka nikamatwe ?”
“Ndio, umeua na unapaswa kuadhibiwa kisheria”
“Regina mrembo , mambo hayapo ‘simple’ namna hio, haiwezekani kufupisha maisha yangu yaliopita na neno kuua”
“Basi elezea vizuri nikujue wewe ni nani na ndio nifanye maauzi kama naweza kukuamini”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kukosa neno , aliona si vyema kumwambia chochote Regina , sio kwasababu anataka kumficha ila ni kwasababu akishamjua atakuwa hatarini.
“Ninachoweza kukuambia ni kwamba , unaweza kunijua ila sio sasa?”
“Mhh, kama hutaki kusema , vipi hiki nisichokijua kuhusu wewe, je kinahusiana na maswala ya kihalifu , kama kuua na kuteka nyara?, Aiu polisi walikuwa sahihi wewe ndio muuaji ulietangazwa kwenye vyombo vya habari?”
“Regina!!”
Hamza sauti yake ilianza kuwa siriasi kidogo.
“Unaweza kusema ndio nimemuua mtu lakini mimi sio mhalifu wala huyo muuaji muhuni muhuni . sijawahi kujihusisha hata na makundi ya kigaidi sio hivyo tu sijawahi kufanya kitu ambacho kinaifunga dhamiri yangu”
“Kwanini nikuamini kama huwezi kusema chochote?”
“Siwezi kukuambia kwasababu siri ninayoficha hapa , kama nikisema nikuambie utakuwa hatarini , nafanya haya kukulinda”
“Haina haja, hatujafahamiana muda mrefu hivyo huna haja ya kunilinda kwa staili hiii”
“Sekunde ambayo ulitia saini hiko cheti umebeba cheo cha mke wangu , unaweza usikubali lakini ni jambo siriasi kwa watu wengine”
“Unamaanisha hili karatasi , hivi unadhani kuna mwanamke duniani anaweza kukubali kuolewa na mtu asiemjua?”
Hamza alitamani kusema ndio ,isitoshe katika uzoefu wake ameshuhudia ndoa ningi zikifanyiika kwa ajili ya manufaa mbalimbali , wengine walifanya hivyo kupata uraia , wengine mali na kadhalika lakini hata hivyo aliona haitokuwa na maana mbele ya Regina.
“Hatutaachana mpaka niweze kuishikilia kampuni kwa asilimia kubwa , hivyo naomba usiambie watu chochote kuhusu ndoa yetu, una uhuru asilimia mia moja ya kutafuta mwanamke unaempenda na hata kuanza taratibu za ndoa , ikifikia muda wa ndoa nipo tayari kwenda kubatilisha hiki cheti”Aliongea Regina huku akitingisha cheti kilichokuwa kwenye mikono yake. “Regina unamaanisha nini kuongea hivyo?”
“Kipi ambacho huelewi , sina mpango wa kuwa mke wako kabisa ,haiwezi kutokea kihisia nikakubali kuwa mkeo , kitu kingine unaweza kutangulia nyumbani au kazini , nitakaa kidogo na bibi usinisubiri”
Mara baada ya kuongea hivyo aligeuka kikauzu na kisha aliingia ndani akimwacha Hamza akimwangalia kwa nyuma.
“Ningeililia ndoa kama kweli naitaka , lakini nipo kazini Regina”Aliwaza Hamza huku akitingisha kichwa , katika maisha yake pengine Regina ndio mwanamke wa kwanza kumuongelesha kwa tabia hio.
********
Upande mwingine katika moja ya hospitali ya jeshi alionekana Afande Norbert akiwa amelala kitandani huku uso wake ukiwa umepauka.
Timu yake ilikuwepo ndani ya chumba alicholazwa na walimwangalia kwa hali ya huzuni.
“Kapteni inamaana ndio tunakwenda kuachana na hii misheni?”
“Mnapaswa kuelewa sisi ni wanajeshi kabla ya kuwa polisi na yote ni kwa ajili ya kuikamilisha hii misheni , acheni kuwa kama walinzi , kuna watu wanamfatilia Hamza kwa ukaribu”Aliongea Kapteni.
“Norbert haina haja ya kuendelea kumfatilia Hamza tena”Sauti iliweza kusikika kutoka mlangoni na wote walijikuta wakikakamaa kwa mshangao wakimwangalia mwanaume aievalia gwanda za jeshi la ulinzi akiingia,alikuwa na vyeo vilivyochafuka begani mwake.
Hakuwa peke yake alikuwa ameongozana na wanajeshi wengine wawili .
“Kapteni Mdudu!!,”Aliongea Norbert kwa mshangao ni kama hakutegemea kumuona Mdudu ndani ya hilo eneo.
Afande Mdudu alikuwa ni Kapteni wa kikosi namba mbili kutoka kitengo cha uchunguzi cha
MALIBU.
Moja ya sababu kubwa ambayo ilimfanya Mdudu kuheshimika jeshini mpaka kupewa nafasi ya kukaa pamoja na wakubwa ni kutokana na kwamba ndio mwanajeshi ambae amepanda vyeo akiwa na elimu kidogo, kwa lugha nyepesi ndio mwanajeshi aliepanda vyeo bila ya kutegemea elimu zaidi ya mafanikio yake ya kijeshi.
Alionyesha uhodari wa namna yake kipindi alipokuwa katika mpango wa Umoja wa Taifa wa kulinda Amani nchini Sudani na Congo.
Mara nyingi MALIBU wanafanya uchunguzi wao kupitia jeshi la polisi , Norbert alikuwa ni mwanajeshi wa kitengo cha MALIBU ambae anaongoza timu namba moja aliepandikizwa ndani ya jeshi la polisi , hivyo alikuwa akipokea maagizo kutoka kwa mkuu wa polisi na pia vilevile alikuwa akipokea maagizo kutoka kwa mkuu wa kitengo cha MALIBU.
‘”Tumepewa maagizo ya kuja hapa , kwanzia sasa kikosi namba mbili ndio kitaongoza misheni ya kumchunguza Hamza, operesheni mlizofanya nyie kama kikosi cha kwanza hazijawaridhisha viongozi , mnaweza kuendeea na taratibu za kawaida kama polisi”
“Nini!, mbona niliwasiliana na mkuu mwenyewe na hajaniambia kuhusu hili”
“Kwahio Norbert nini ambacho huamini , angalia
hio karatasi kuna sahihi ya mkuu wa kitengo”Aliongea akimrushia karatasi kwenye kitanda na kweli kulikuwa na sahihi.
“Kwanini mnataka tuiachie hii kesi kwenu , bado hatujakamilisha kumkamata Hamza lakini vilevile hatujafanya kosa lolote”
“Norbert licha ya kwamba wakuu wanasifia uwezo wako lakini kwangu nakuona kama mjinga , kwanini hukujiuliza licha ya Afande mwenye cheo kikubwa kama Afande Yowe kuuwawa lakini bado viongozi wakakuambia uachane na Hamza , lakini angalia ulichokifanya ukajaribu kumkamata na sasa upo hapa hospitalini , viongozi hawakuridhishwa na namna yako ya kukosa utiifu na wamesikitishwa sana na hili ndio maana tumepewa jukumu la kumchunguza Hamza na kumjua kwa undani”
“Nimefanya vile kama polisi , sikuona haja ya
kumwangalia mhalifu anafanya anavyotaka”Aliongea Norbert na kumfanya Mdudu kutoa tabasamu la dharau.
“Tulichokifanya ni kujaribu uwezo wake kwa kumtishia kumkamata , timu namba mbili mnataka kuchukua crediti zetu wakati misheni inaendelea vizuri”Aliongea Kyombo.
“Norbert wewe ndio uongee , unadhani tunakuibia sifa zako?”Aliuliza Mdudu.
“Kyombo kaa kimya” Aliongea Kapteni Norbert na kumfanya Kyombo kunywea.
“Norbet una timu ina watu vilaza kweli…”Aliongea mwanajeshi aliekuwa nyuma ya Afande Mdudu lakini alizuiwa asiendelee maana angeibua ugomvi.
“Norbert uliwaambiwa viongozi kwamba hisia zako zinakuaminisha Hamza ndio muuaji anaeua wanawake ndani ya jiji la Dar es salaam , lakini kwanini umeshindwa kujiuliza swali jepesi , kwanini Bounty hunters kutoka Samar wamesafiri kutoka
Ufilipino mpaka Tanzania kwa ajili ya kumtafuta Hamza , nadhani unawajua vizuri hawa wawindaji hawatumiki sehemu ambayo haina hazina”Aliongea Mdudu.
“Ni hazina gani ambayo Hamza
anashikilia?”Aliuliza Norbert huku kidogo akiona ni kweli kuna mahali amekosea.
“Huna haja ya kuuliza maswali , tokea mwanzo ulikuwa ukitafuta kitu sehemu ambayo sio sahihi , lakini usijali mimi na timu yangu mapema tu tutaweza kujua ni kitu gani wale wawindaji wamekijia Tanzania na ndio namna tutakavyomjua Hamza kwa undani zaidi na hakuna atakaepata majeraha kama yako”
Mara baada ya Mdudu kuongea hivyo aliwapa ishara wenzake na kisha waliondoka .
******
Saa mbili kamili za usiku Hamza alikuwa ndani ya eneo la kijichi akilisogelea lango la kuingia katika mgahawa wa Dina.
Mara baada ya kuingia aliweza kuona Mercedenz s Class ikiwa imeegeshwa na Lau alionekana kuilinda gari ile.
Hamza alikuwa hapo kwa ajili ya kutii wito wa mrembo Dina mara baada ya kumpa agizo la kufika hapo bila ya kukosa.
“Bro umewahi mno , ungenipigia simu nije kukuchukua kabisa”Aliongea Lau kwa bashasha. “Mbona hii gari ipo hapa,Dina anapanga kutoka?”Aliuliza Hamza.
“Ndio , anaelekea Club”
“Club!!”
“Ndio kila mwisho wa mwezi vigogo na watu wazito wazito hukusanyika katika club moja , ni kama tukio maalumu , sio lazima kwenda lakini kutokana na kwamba wengi ya wanaohudhuria ndio wateja wetu wakubwa haina jinsi kwenda”Aliongea Lau.
Muda huo wakati wakiongea Dina aliweza kutoka akiwa amevalia amependeza.
“Nilijua utachelewa”
“Siku kwenye mudi nzuri ndio maana nimekuja, nimeambiwa unaenda Club, nitakusubiri mpaka utakaporudi”
“Nilikuambia uje leo kwasababu nataka unisindikize”Aliongea Dina.
“Lakini hujaniambia ni club ya aina gani” “Nitakuambia tukwia tunaeekea huko , ingia kwanza kwenye gari, umesema huna mudi club ndio sehemu inayokufaa”Aliongea huku akitangulia kuingia ndani.
Hamza aliishia kutingisha kichwa na paepale aliona sio mbaya kutokana na mudi yake kuwa mbaya ni kheri kidogo akapunguze mawazo huko Club.
Comments