Hamza akiwa ndani ya gari na Dina alimwambia kile ambacho kimetokea mpaka namna alivyojiandikisha na Regina na kuwa wanandoa kisheria.
Ijapokuwa Dina alikuwa mtulivu wakati wa kumsikiliza Hamza , lakini mara baada ya kusikia Hamza alikuwa amesajili ndoa na mwanamke mwingine alijikuta akishikwa na huzuni.
Lakini hata hivyo aliona haiwezekani yeye kuja kuwa mke wa Hamza kwani hakuwa na vigezo hivyo.
“Kwahio kwanzia sasa utakuwa chini ya ulinzi wa mke wako na kuwa ngumu kwetu kuonana , sijui mimi Dina nimekosea wapi katika ulimwengu huu”Aliongea na kumfanya Hamza asijue alie au acheke.
“Hapo ndio unapokosea , kasema licha ya kuandikisha ndoa niharakishe kutafuta mwanamke na ataachana na mimi baada ya nafasi yake katika kampuni kuimarika”Aliongea Hamza
Dina mara baada ya kusikia hivyyo alijikuta akimuonea huruma na kumdharau kwa wakati mmoja Regina.
“Regina ni mwanamke asiejua ana bahati kiasi gani lakini anachezea, kuolewa na mtu kama wewe ni zaidi ya faida ya vizazi na vizazi”Aliongea Dina.
“Dina huwezi kurahisisha mambo , kwa nafasi yake huwezi kumlaumu yeye sio kama sisi tuliozea kuona damu , nadhani baada ya kugundua nimeua mtu jana ameona hata swala la kuandikisha ndoa amekurupuka”Aliongea Hamza lakini upande wa Dina alimuona Hamza kama anatafuta sehemu ya kulalamikia.
“Naona unafikiria sana , sio kawaida yako, kwa haraka haraka unaonekana kumpenda, ni kitu gani cha pekee ambacho kimekuvutia kutoka kwake?”
“Ushaanza kujilingansha sasa , hebu acha kufikiria mbali kwangu mimi wewe ni mtu muhimu ambae siwezi kukupoteza.. Regina sijafahamiaa nae kwa muda mrefu na kuna uwezekano pia naweza nisiendelee kuwa nae muda wowote lakini angalau najua wewe huwezi kunikimbia”Aliongea Hamza na kumfanya Dina kujisikia utamu.
“Sawa , ila acha sasa kufikiria maswala ya Regina , mimi naamini anakupenda pia na muda wowote atazielewa hisia zake , leo ngoja ukapoteze mawazo yako Club”
“Ni Club gani tunaelekea?”
“Tanganyika Club ushawahi kuingia?”Aliuliza Dina.
“Naionaga sijawahi kuingia”
“Sasa Tanganyika ndio moja ya Club ya kifahari hapa nchini yenye kila aina ya starehe kuna hadi sehemu ya kujifunza kutumia bunduki halisi kulenga shabaha, kiingilio cha chini kwa mwezi ni milioni therathini na tano na pia lazima upendekezwe na mwanachama, wanaoingia humo ni wa hadhi ya juu mno”
“Mbona kama unapanga kunipeleka kulenga shabaha na bunduki?”
“Ni mpango wangu pia, nimekuona mara kadhaa ukipigana lakini sijawahi kukuona ukitumia bunduki , nataka nione kama unanizidi”
“Dina unajua unazidi kuwa tofauti na wanawake wa kawaida kutokana na hobi zako”
“Kwahio unamaanisha hupendi.. kama ndio hivyo turudi”Aliongea Dina na Hamza aliishia kutingisha kichwa chake kukataa na kuendelea kuendesha gari.
Dakika kadhaa mbele waliweza kufika Posta na kuingia kwenye jengo kubwa ambalo halijaenda sana hewani , lilikuwa limejengwa kwa kuigiza muundo wa meli , sehemu hio ndio ilikuwa ikipatikana Club na hoteli maarufu ya matajiri ya Tanganyika.
Licha ya Club hii kuwa ndani ya Tanzania lakinni ni asilimia kumi tu pengine pungufu zaidi ya walioingia ndani ya Club hio kuwa watanzania, ukiachana na kwamba matajiri wa kibongo huingia ndani ya club hio ila ni wachache sana, raia wengi wa Kigeni ambao walikuwa wakiingia nchini kwa ajili ya kufanya anasa lazima wafikie katika hio Club , ilikuwa maarufu Afrika mashariki na kati yote.
Taarifa ambazo hazikuthibirishwa ilisemekana inamilikiwa na familia moja ya kitajiri kutoka Scotland maarufu kama Keswick kupitia asset zao ndani ya Mandarlin oriental luxury
hospitality,Uwekezaji huo mkubwa ulitekelezwa
kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Mgweno.
Mara baada ya kuingia ndani ya lango la hoteli na Club hio Hamza alikabidhi funguo kwa Valet na kutokana na Dina pia kuwa moja ya wanachama ndani ya Club hio alikuwa akiruhsiwa kuingia na tafiki.
Mara baada ya kuingia katika Korido ndeefu Dina alikunja kulia kwake na kuhamia katika Korido nyingine na hapa ndio Hamza alijua ni kipi kinaendelea , ndani ya eneo hilo kulikuwa na skrini zilizofungwa ukutani kama TV na zilikuwa zikionyesha kila aina ya Bunduki inayopatikana kwa ajili ya kulengea shabaha.
Kila mtu alikuwa na starehe yake na hili lilizingatiwa ndani ya hoteli hio , wengine starehe yao pengine ni kuzima shauku zao katika matumizi ya siraha na sio kuishia kuziona kwenye filamu tu na hiki ndio kilichokuwa kikipatikana ndani ya club hio , ukitaka kuwa Mdunguaji ama kujifunza kuwa Mdunguaji basi hio ndio sehemu yenyewe.
Upande wa Hamza kila bunduki alioweza kuona alikwua ashaitumia hivyo ni kama hakuwa na ile shauku kubwa.
“Dina!!”
Ghafla tu sauti ya kiume iliita kutoka nyuma yao na kufanya wageuke.
Alikuwa ni bwana mmoja mwenye muonekano wa kipole alievalia suti nyyeupe pamoja na miwani. “Huyu mwanaume ni nani , usiniambie ndio boyfriend wako?”Aliongea mara baada a kuwakaribia na alimwangalia Hamza kwa macho yasiokuwa na ishara ya urafiki, alikuwa hajapenda kabisa namna ambavyo Hamza na Dina walivyoshikana mikono.
“Robert umekuwa na shauku ya kumjua , huyu sasa ndio mpenzi wangu”Aliongea Dina na kisha alimtambulisha Hamza.
“Hamza huyu ni Robert mtoto wa Eliasi mheshimiwa raisi anaemaliza muda wake, ni Mbunge na msimamizi mkuu wa mahoteli yote ya Tanganyika”Aliongea Dina.
“Hello Mr Robert!”Aliongea Hamza na kunyoosha mkono kusalimiana nae.
“Sijaona ubora wowote uliokuwa nao tofauti na mimi , ukiachana na muonekano wako wa kuchanganya rangi, nimemfuatilia Dina kwa mwaka sasa lakini kila siku ananikataa , nataka kujua ni kipi ambacho kinakufanya kuwa bora zaidi yangu”Aliongea Robert na kumfanya Hamza kucheka.
“Sijajua anachonipendea labda ni kwasababu mimi ni handsome zaidi kuliko wewe”Aliongea na kumfanya Dina kumpiga Hamza na kiwiko akimwambia atulie.
“Haiwezekani , kinachokubeba ni huo muonekano wako wa kuchanganya rangi lakini kimavazi na kila kitu nimekuzidi “
“Labda nikwasababu namridhisha kwenye sita kwa sita wanawake hawajawahi kueleweka wanachopenda kwa mwanaume”Aliongea Hamza.
“Hebu acha kuongea , unamaanisha nini?” Dina hakutaka Hamza aendelee kuongea maana alijikuta akishikwa na aibu.
“Dina kwahio ndio sababu ya kunikataa , kwanini usingeongea tu , niko vizuri pia kwenye sita kwa sira na kama usingeridhika ningetumia hata mkongo kwa ajili yako”
“Robert usimsikilize Hamza anakutania tu , sijakukataa kwasababu huna vigezo ni kwasababu kazi yangu haieandani vyema na kazi yako na ya baba yako, sidhani pia kama natosha kwako , isitoshe hili ni swala la kihisia zaidi”
“Hilo sio tatizo Dina , nilikupenda siku ya kwanza nilipokuona ndani ya mgahawa wako…”
“Robert naomba unisamehe lakini sitaki kuendelea na haya mazungumzo mbele ya Hamza”Aliongea na kumfanya Robert kuonekana kutoridhika hasa alipomuangalia Hamza.
Upande wa Hamza aliona huyo bwana anafurahisha , alikuwa ni kama mtoto ambae amekasirika baada ya kunyimwa hitajio lake , kariba ambayo kwa bahati mbaya haikuendana na Dina kabisa.
Muda huo Wenza wengine waliingia ndani ya eneo hilo na kumfanya Hamza kuwashangaa baada ya kuwajua .
Alikuwa ni bosi Side Mkrugenzi wa Vodocum Tanzania alieambatana na Salma ambae alidhalilika mbele ya Fellini wa kamapuni ya kimavazi ya Zara..
“Mr Hamza?”Aliita Saidi.
“Bwana Saidi kumbe na wewe ni mhudhuriaji hapa?”Aliongea Hamza huku akitoa tabasamu la utulivu.
“Side unamfahamu?”Aliongea Salma akijifanyisha eti hamjui Hamza.
“Ndio namfahamu , mbona kama na wewe unamjua?”Aliongea Saidi na kumfanya Salma mwili wake kukakamaa , alihitaji kujizuia kadri awezavyo asije kuongea upuuzi kama wakati ule.
“Ndio nilifahamiana nae katika harakati za kazi”Aliongea Salma.
“Kumbe mnafahamiana ne , Hamza huyu ni Side rafiki yangu , Salma ni mpenzi wake na rafiki yangu pia”Aliongea Robert na kumfanya Hamza kuishia kujisemea Side hakuonekana mzembe , Salma alikuwa mwanamke matawi pia na mrembo na kwa kuangalia tu ilionekana Salma ndio kapenda zaidi ya Side.
“Robert si ulisema ulimfukuzia Dina kwa zaidi ya
mwaka , inamaana huyu ndio mtu aliekubia?”Aliongea Salma hakukoma tu.
Hata kwa Side aliweza kuona ukaribu uliokuwepo kati ya Dina na Hamza na alizidi kujawa na hisia mchanganyiko , siku ile Prisila alimtambulisha kama mpenzi wake lakini leo hii Hamza yupo na Dina , wanawake hao wote kwake ni ngumu kuwapata licha ya cheo chake kazini .
“Salma haina haja ya kusema hivyo , bado sijakubali kumpoteza Dina , lazima nimuonyeshe mimi ni zaidi ya Hamza”Aliongea na muda uleule alimgeukia Hamza.
“Si mmekuja upande huu kulenga shabaha na bunduki , kwanini tusishindane , kama kweli wewe ni mwanaume tucheze pambano moja na atakae shinda rasmi atatoka kimapenzi na Dina”
“Robert!, mimi sio tuzo kwamba nitajikabidhi kwa yoyote anaeshinda , kwanini unanigeuza kuwa kifaa?”
“Dina usinifikirie vibaya , nadhani utanipa nafasi angalau ya kukupigania , kama wasemavyo huwezi kuona ubora wa kitu pasipo ya kukilinganisha na kingine , siwezi kukubali kushindwa bila ya kuijua sababu”
“Lakini mimi sitaki kushindana”Aliongea Hamza
“Wewe sema hujui kutumia bunduki acha kuzunguka, Dina ni mwanamke anaeweza kulenga shabaha kwa kiwango kikubwa unaweza vipi kuwa mpenzi wake kama hata kutumia bunduki hujui?”
“Najua lakini sitaki kushindana”Aliongea Hamza akionyesha kukereka.
“Kama unajua tushindane acha kuwa mwanamke , jiamini bro kama nikishinda utaachana na Dina kama ukishinda nitaacha kumsumbua Dina , unaonaje hapo?”
“Robert huwezi kuzipangia hisia zangu nani wa kumpenda kupitia mashindano?”AliongeaDina akionekana kuanza kukasirika lakini Hamza alimzuia huku akitoa tabasamu lililojaa kejeli. “Sio mbaya muda mwingine wanaume kwa wanaume kushindana japo huwa sipendelei , kama hili ni swala la kuonyesha nani mwanaume zaidi kati yetu basi nipo tayari”
Hamza hakutaka kuonekana mdhaifu mbele ya Dina hivyo alitaka kuuonyesha Robert nini maana ya kulenga shabaha.
Side na Salma walioneysha hali ya dharau kwa Hamza , walikuwa wakimjua Robert Eliasi likija swala la kulenga shabaha alikuwa fundi kuzidi hata wanajeshi wa vikosi maalumu.
“Hamza upo tayari kushindana na Robert kweli! , ngoja umpoteze bosi Dina kwa Robert”Aliongea Salma.
“Hatujaanza kushindana lakini ushaanza kuleta dharau zako kama siku ile?”Aliongea Hamza na kumfanya Salma kupandwa na hasira, bado alikuwa na kinyongo na Hamza kwa kumsababishia kukosa ushirikiano wa kibiashara kati ya Kampuri yao ya S Corporation na Zara Group kwa Hamza kuleta habari zake za Mshona nguo kutoka Ulaya.
“Dina usiwe na wasiwasi , huwa sijawahi kushindwa”Aiongea Hamza akimtoa wasiwasi.
Dina hakuwa na cha kumfanya Hamza kutokana tayari ashaafanya maamuzi , licha ya kwamba alionekana kama anatania lakini aliamini Hamza hawezi kufanya kitu ambacho hajiamini nacho.
Wote kwa pamoja walisogea mpaka eneo la Shooting Range.
“Tutatumia bastora ya Smith & wesson toleo la tatu , yenye uwezo wa kuachia risasi ukubwa wa Kaliba arobaini na tano, kila mtu raundi kumi , mita hamsini kutoka kwenye shabaha , tutashinda kwa kuangalia nani ana maksi kubwa”Aliongea Robert na kumfanya Hamza kuchukua bastora na kuanza kuipima uzito wake na aligundua ilikuwa ni orijino kutoka kiwandani kabisa na sio feki na alijiambia hii hoteli sio ya kawaida.
Eneo hilo lilikuwa na soundproof kiasi kwamba hata ukifyatua bunduki sauti yake inamezwa na haiwezi kufika floor za juu kwenye makasino na vyumba vya kulala lakini pia bunduki nyingi zilikuwa na mfumo wa Suppressor wa kuzuia makelele.
“Hakuna shida, nani anaanza?”
“Yoyote yule , mimi niko freshi”
“Kama ni hivyo wewe anza”Aliongea Hamza na Robert hakujali zaidi ya kutoa tabasamu lililojaa kejeli na aliijaza bunduki na risasi na kisha akaiweka katika usalama na kuanza kulenga shabaha za duara zilizokuwa mita hamsini umbali.
“Bang , Bang , Bang..”
“Bahati mbaya kwako umenikuta nikiwa na hali nzuri ya kulenga , alama hizi ni karibia na alama zangu za juu katika ulengaji , kama utaamua kukata tamaa mapema naweza kukuelewa”
Alikuwa ameweza kulenga duara namba nane na namba saba , kwa umbali wa mita hamsini ana uwezo wa kulenga kiganja cha mkono wa mtu , ni uwezo wa juu ambao mtu wa kawaida hawezi kufikia kabisa, lazima uwe na mafunzo ya miaka mingi , maana msukumo wa nguvu inayokurudisha nyuma ulikuwa mkubwa mno bila kusahau bastora aliokuwa akitumia ina mdomo(Calliber au Kaliba) mkubwa hivyo kuwa na msukumo mkubwa.
Dina hata yeye aliingiwa na wasiwasi , licha ya kwamba uwezo wake wa kulenga shabaha ni mzuri lakini ilikuwa ni mara chache sana kufikia alama alizopata Robert kwa kufyatua risasi mara kumi mfululizo na aliona Hamza anaweza asimfikie.
Hamza hakuongea neno na taratibu alichukua risasi moja moja na kuijaza kwenye bunduki.
Ni kweli aliona Robert alikuwa na uwezo mzuri wa kulenga kwa kugusa duara namba 8 na 7 , wasiwasi wake mkubwa ni kupata maksi za juu kabisa ambazo sio za kawaida na kufanya hao watu kumshitukia.
Baada ya kuwaza hivyo aliona kidogo aonyeshe ubinadamu kwa kujikosesha.
Bang , Bang , Bang
Hamza aliishikilia bunduki kwa mikono miwili kana kwamba alikuwa akimuigiza Robert lakin ukweli ni kwamba hakuangalia hata anapolenga, kwa umbali huo aliiona anaweza kupata maksi mia ya mia hata kama amefumba macho yake.
Mara baada ya kukamilisha mizunguko kumi , haraka sana Robert alibonyeza kitufe cha kuonyesha alama Hamza alizopata.
“”Nane .. tisa ,,, nane , nane , nane!!”Robert alijikuta akishikwa na hasira huku akisaga meno akiwa haamini macho yake
“Samahani mkuu nimeshinda”Aliongea Hamza.
“Wewe .. unaonekana kuwa na bahati sana”
“Kwahio bado hujakubali nimeshinda”
“Turudie tena , tufanye iwe mbili kwa tatu”Aliongea Robert akionyesha kutokukubali kushindwa.
“Tulikubaliana atakaepata maksi kubwa ndio mshindi lakini sasa hivi unaanza kubadilisha sheria, siwezi kushindana na mtu ambae anaenda kiunyume na ahadi yake”
“Sio hivyo…”
Kilichomfanya Robert kukasirika ni kwasababu alijua angekosa nafasi ya kuombata tena tunda kutoka kwa Dina.
Salma alimwangalia Saidi na kisha alimgeukia Hamza na alionekana kuna kitu alichokiwaza.
“Mnaonaje tukifanya hivi, kama marafiki Saidi atashindana kwa ajii ya Robert , akishinda tutafanya shindano la mwanzo ni suruhu”Aliongea huku akishika mkono wa Saidi akiupangusa kwa mapozi.
“Side naomba umsaidie Robert , naona kama haki haijatendeka”Aliongea lakini Side alionekana kutofurahishwa na alichosema Salma.
“Hili ni wazo zuri Salma , vipi upo tayari kupambana na saidi?”Aliongea Robert akimwangalia Hamza
“Bado hatujamaliza tu hili na mnataka tena, sidhani kama kuna faida yoyote”Aliongea Hamza lakini Side alionekana kulifikiria lile wazo.
“Unaonaje tukifanya hivi kama nikishinda, pambano kati ya Hamza na Robert ni batili na kama Hamza akishinda nitampatia dola laki moja , Robert chukulia hio hela kama ufadhili wangu kwenye uchaguzi wa kutetea jimbo lako”Aliongea Side.
“Haha… Side ndio maana nakukubali sana rafiki yangu , hili limepita”
Hamza alijikuta akiishia kutingisha kichwa kwa masikitiko , ilionyesha Side alitaka kushindana nae kwa kiasi kikubwa mpaka kuweka rehani kiasi kikubwa hivyo cha pesa.
“Kuwa makini , Saidi uwezo wake wa kulenga shabaha sio wa kawaida , ndio mwenye rekodi ya juu tokea kuanzishwa kwa hii club, huwa hashuki chini ya pointi tisini”Aliongea Dina lakini Hamza wala hakujali.
“Unaonekana kuwa na nia ya dhati kabisa kupambana na mimi hivyo sio vizuri kukukatalia , tuanze mechi”Aliongea Hamza na Side alitingisha kichwa na kisha alisogea na kuanza kuload risasi na kuanza kushuti.
Baada ya awamu kumi kuisha Side hata hakujali kuangalia matokeo kwani alisogea pembeni na kazi hio ilifanywa na Robert.
“Side umevunja rekodi tena , umepata pointi tisini na nane umekosa mbili tu”Aliongea Robert ikimaanisha amelenga kwenye duara namba kumi mara nane na tisa mara moja.
“Babe upo vizuri sana ndio maana nakupenda”Aliongea Salma akimwangalia Side na macho yaliolegea.
Dina alimwangalia Hamza na aliona ni ngumu kwa Hamza kuzidi hizo maksi mbili tu ambazo Side alikosa.
“Unaweza kukubali kushindwa hakuna atakae kucheka”Aliongea Side.
Hamza aliona yupo kwenye hali ngumu na hawezi kuigiza tena , isitoshe iwe tisini na tisa au mia hakuna ambae ataona kama anadanganya.
“Usiwaze , ngoja nijaribu na mimi”Aliongea Hamza na kisha alisogea na kuanza kujaza bastora na risasi na kisha aliinua mkono mmoja wa kushoto na kuanza kupiga , hakupumzika hata kwa sekunde ilikuwa ni mfululizo wa risasi kutoka.
Dakika ambayo Hamza aliweka bunduki chini , kwa haraka sana Robert aliangalia matokeo na mara baada ya namba nyekundu kuonekana wote na Dina ambao walionekana kuwa na shauku macho yaliwatoka , huku Side na Salma wakimwangalia Hamza kwa mshangao mkubwa.
“100!?”
Robert alikuwa akiangalia namba hio kwa muda mrefu kana kwamba alidhania macho yake yanamdanganya.
“Wewe ni binadamu kweli!?”Aliuliza Robert maana hakuamini mfuatano wa risasi zile zote zimegonga shabaha kwa asilimia mia.
“Leo inaonekana nina bahati sana”Aliongea Hamza akicheka , ijapokuwa watu wote waliokuwa wakimwangalia hawakuwa wajinga , lakini ilikuwa ni uhalisia Hamza hakutumia uwezo wake wote.
“Kupoteza ni kupoteza tu , ikitokea mtaalamu zaidi yako utaishia kushindwa , Hamza nitajie namba za
akaunti yako ya benki nikuingizie kiasi nilichoahidi”Aliongea Saidi.
“Potezea , Side sisi sio wageni kwetu , chukulia kama tulikuwa tukicheza”Aliongea Hamza hakutaka kufanya mambo kuwa magumu kwa
Saidi.
“Huwa sichukulii kiwepesi ahadi zangu , nikisema ni laki ni laki , nimekubali kushindwa hivyo usinifanye kwenda kinyume na ahadi” “Babe nitampatia mimi”Aliongea Salma.
“Haina haja”
Salma alionekana kujutia kupendekeza shindano lile na kumfanya Saidi kuingia hasara na aliona hasira ya Side kabisa, lakini alipendekeza vile kwani hakuamini kama Hamza anaweza kumzidi
Saidi.
Hamza mara baada ya kuona Side anataka kukasirika aliona asiikatae ile hela.
“Dina mtajie akaunti yako ya benki akuingizie hela , chukulia kama malipo ya siku zote nilizokula na kunywa bure kwenye mgahawa wako”
“Ni hela yako hio , sioni kama ni vizuri kuitumia kama malipo”Aliongea Dina lakini hata hivyo alimtajia Saidi akaunti yake ya benki na alichukua sekunde kadhaa muamala ulisoma milioni mia mbili hamsini, ijapokuwa aliahidi atalipia kwa dola lakini alilipa kwa hela za kitanzania na baada ya hapo alionekana hakuwa hata na mudi kwani aligeuka na kuondoka na kumfanya Salma kumkimbilia.
“Side inaonekana kakasirika, sio kwasababu ya kupoteza hela ila kwasababu ya kushindwa”Aliongea Robert
Wewe vipi hujakasirika, siku nyingine unapaswa kutimiza wajibu wako wa kutumikia wananchi na sio kumsumbua mpenzi wangu”
“Nimekubali kushindwa Bro , kama nilivyoahidi nitatekeleza’Aliongea Robert kisha alimsogelea Hamza na kumpatia mkono.
“Hamza unaonaje tukishikana mikono kama ishara ya kuwa marafiki kwanzia sasa?, natumaini utamfanya Dina kuwa na furaha”Aliongea na kumfanya Hamza amuone kweli bwana huyo ni mwanasiasa lakini hata hivyo aliishia kunyoosha mkono kumkubalia.
Upande wa maegesho ya magari mara baada ya bosi Side kuingia ndani ya gari yake Audi R8 aliweza kumuona Salma akiwa ameshaingia tayari.
“Shuka!”Aliongea kikauzu na kumfanya Salma kutia huruma.
“Side naomba unisamehe mpenzi wangu , sikujua kama Hamza angekuwa na bahati kiasi kile , naomba usikasirike”
Eti bahati , kuna bahati ya namna ile mtu kuweza kulenga shabaha eneo moja kwa mara zote kumi au unaongea upuuzi?”
“Lakini kwanini upo hivi Side , kuna kingine tofauti na hiki kilichotokea , tumekuwa wapenzi kwa zaidi ya miaka minne sasa na nimeamua kurudi kwa ajili yako , lakini kwanini kadri siku zinavyosogea unazidi kuwa mkali kwangu?”
“Kama unadhani nimekuwa mkali kwako , basi rudi China ukaendelee na mambo yako sikukuambia urudi kwa ajili yangu”
“Sirudi tena China, awamu hii nimerudi ili unioe”
“Nani kasema nitakuoa , hebu toka kwenye gari yangu kabla sijakufanya kitu kibaya”Aliongea na kumfanya Salma kuzidi kuona Side anamkosea na alishuka kwa hasira na kuondoka lakini hata hivyo Side hakujali , mara baada ya kuingia katika gari yake alianza kutafuta majina katika simu yake na kuweka sikioni ikionyesha anapiga simu.
“Side , naona leo umepata muda wa kunipigia?”Sauti ya kike ilisikika.
Lea hebu acha maneno yako , kuna kitu nataka unisaidie nitakulipa hela”
“Kila unapoongelea hela ujue una stress , haya niambie ni kipi unataka nikusaidie?”
“Leo nimegundua siri ambayo Hamza anaificha , nataka umwambie Prisila…”Aliongea Saidi huku akiwa na tabasamu lililojaa uovu.
******
Upande mwingine ndani ya makazi ya mrembo na Daktari , Frida Franklin katika chumba cha Master alionekana mrembo huyo akiwa amejilaza na kukoroma kabisa , alionekana alikuwa amechoka kwa namna alivyokuwa amelala.
Taa ya kitandani ilionekana haijazimwa na pembeni yake kuna kitabu kilichokuwa kimefunguliwa , ikionyesha alipitiwa na usingizi wakati akiwa anasoma.
Zilipita sekunde chache tu muda ule hali ya hewa ya kile chumba ilibadilika , ilikuwa ni kama upepo umeongezeka na kumfanya Frida kuanza kujinyoosha kitandani.
Mara ghafla tu chumba kile kilirudi katika hali ya utulivu wa hali ya juu na kumfanya Frida kujigeuza na kulala chali , lakini utulivu ule uliambatana na maajabu yake kwani ghafla tu kilionekana kivuli kikitokea kwenye pembe ya chumba hicho.
Ajabu ni kwamba kifizikia ili kivuli kitokee kinahitaji mwanga lakini kivuli hicho kilitokea bila ya kuwa na chanzo cha mwanga.
Kile kivuli kilikuwa na umbo la mtu lakini kwa namna moja ama nyingine kama ni mtu katika uhalisia basi angekuwa akitisha kutokana na eneo lake la kichwa kukosa mpangilio mzuri.
Wakati Frida akiwa hana hili wala lile mkono wa kivuli kile cha mtu wa ajabu ulinyooka ni kama ulikuwa ukirefuka kutoka eneo kilipo mpaka kwenye kitanda , mkono ule ukimlenga Frida katika shingo yake.
Ghafla tu ni kama Frida alishituka lakini alianza kurusha miguu kama mtu ambae amekabwa
shingoni , alijikuta akirusha Miguu huku akijitahidi kuvuta hewa.
Lakini mwanamke mrembo huyo alionekaa kushindwa kabisa kupambana na mkono ule wa Kivuli cha mtu na ulionekana ni kama umedhamiria kumuua.
Frida alijikuta kadri sekunde zinavyoenda ndio ambavo alikuwa akikosa nguvu kutokana na kutoweza kuvuta pumzi ,aliishia kurusha rusha miguu huku akionekana muda wowote atakata roho.
Comments