“Sijui kuhusu katiba yao inachosema , ila nina uhakika mgombea Mwenza ndio atachukua nafasi, kwanini unauliza?”Aliuliza tena Dina maana alijua Hamza hakuwa mtu wa siasa.
“Nawaza kuna mchezo unaochezwa hapa na kuna nguvu mbili kubwa za kisiasa , nataka kujionea mwenyewe”Aliongea Hamza na Dina alitingisha kichwa , kwasababu Hamza alitaka kwenda hakuona haja ya kumzuia , isitoshe ilimpelekea kujiamini zaidi kudili na hali kama hio.
Upande wa Dina alijua lazima kuna mchezo unaofanywa na kama Mzee Seif atakubali kuhusika moja kwa moja itaaminika mtandao wake ndio umekamilisha swala hilo , jambo ambalo hakautaka litokee.
Nyumba ya Mzee Seif ilikuwa Kigamboni Mbutu B na gari mbili ziliendeshwa kuelekea huko ya mbele akiwemo Hamza na Dina na ya nyuma ilikuwa Noah iliowabeba Lawrence na kundi lake.
Kitendo cha kufika eneo la tukio waliweza kuona watu walioizingira nyumba ya Mzee Seif , jambo ambalo liliwashangazwa hakukuwa na uwepo wa polisi hata mmoja ni kama Hamza alivyotarajia.
“Mbona sio polisi kama taarifa ilivyosema?”Aliuliza Dina kama kwamba Hamza alikuwa na majibu.
Hamza alichunguza eneo lote hasa wale watu walioshikilia siraha na alijikuta akikunja sura mara baada ya kuona wazungu wawili ndani ya eneo lile wakiwa ni sehemu ya watu waliozunguka nyumba hio.
“Ni kama nilivyotarajia kuna kinachoendelea hapa”Aliongea Hamza.
“Lakini kama kweli walikuwa wakimshuku Mzee Seif kulipua gari ya mheshimiwa Jongwe kwanini hawajaja polisi?”Aliuliza.
“Tutapata majibu yote mara baada ya kuongea nao”Aliongea Hamza huku akitangulia kutoka nje ya gari.
Wale watu kama walinzi walioshikilia siraha wakiwa wamezingira nyuma hio waliongeza umakini kwa Dina na kundi lake.
“Kama tabia yako ya siku zote, Dina mrembo wa kujiamini , naona umekuja na watu wachache mno tofauti na nilivyotegemea”Sauti ya mwanaume ilisikika kwasababau ilikuwa kuna giza hawakumuona vizuri na mara baada ya kusogelea taa za mwanga wa gari ndio Dina aliweza kumuona.
“Pancho!, unafanya nini hapa?”Aliongea Dina na muda huo ni kama sasa alishaanza kupata picha ya kile kinachoendelea.
“Nimekuja kukusalimia kwa mara nyingine mara
baada ya kukataa pendekezo ya dili
nono”Aliongea na muda ule alitoa ishara na baada ya kupita dakika mmoja tu wanaume wanne walitoka katika nyumba hio na moja wapo ya wanaume wale alikuwa ni Mzee Seif alieshikiliwa na wanaume wawili weusi waliojazia mwili , mtu wa mwisho kutoka alikuwa ni Mzungu- Mjapani , yaani mtu aliechanganya rangi ya mjapani na Mzungu.
Kilichomfanya Dina kuanza kupandwa na hasira alijua mpango wote huu ulisukwa na Pancho.
Pancho alikuwa ni moja ya wasimamizi wa mtandao wao upande wa Congo na siku kadhaa nyuma Dina alipokea dili kupitia kwa Pancho kutoka kwa Wacanada ambao walitaka kuingiza siraha za kivita Congo kupitia Bandari ya Mtwara.
Dili hili liliungwa mkono na Mheshimiwa Mgweno lakini Dina aliona halikuwa na maslahi na kama angelikubali ni kama kujipiga risasi mguuni, ikizingatiwa siraha hizo zilipaswa kufikishwa kwa kundi lingine la waasi ndani ya Congo tofauti na lile ambalo wanashirikiana nalo kwa muda mrefu. “Mzee Seif nini kimetokea , kwanini taarifa nilizopokea ni wewe kuhusika na kumuua Mzee Martini na mheshimiwa Jongwe?”Aliuliza Dina akimpotezea Pancho.
“Hawa ndio wahusika , wameiteka familia yangu na wanataka nikiri kuhusika kwa kushirikiana na wewe kumuua Jongwe au turejee mezani na kuanza mazungumzo ya kuingiza siraha Tanzania kwenda Congo”Aliongea Mzee Seif aliekuwa na hali ya hofu na kumfanya Pancho kutoa tabasamu.
“Pancho unajaribu kufanya nini , nani yupo nyuma yako?”
“Dina hakuna ambae yupo nyuma yangu?”Aliongea Pancho kwa kejeli.
“Kwa kumuua mgombea wa uraisi kupitia chama tawala, unasema hakuna ambae yupo nyuma yako?”Aliongea Dina kwa hasira na kumfanya Pancho kutoa tabasamu la kifedhuli.
“Nilitaka hili swala angalau ulichukulie kwa uzito wake, ushahidi wa wewe kuhusika katika shambulizi la kulipua bomu gari ya mgombea wa uraisi kupitia chama tawala upo , unaweza ukawa wa kutengeneza lakini jeshi la polisi lipo tayari kuuamini na kama likitoka uraiani , kitengo cha TISA kitakufanya mbuzi wa kafara, lakini huko kote ni kujisumbua kama upo tayari kuchagua chaguo zuri kati ya matatu alioongea Mzee Seif?”
Hamza muda huo alikuwa akiangalia mazingira yalivyo na watu wote waliokuwa hapo walikuwa na siraha za bunduki na haraka haraka kwa sheria ya Tanzania ilikua ngumu kwa watu hao kumiliki hizo siraha labda iwe kuna mtu ndani ya serikali ambae alikuwa akihusika.
Isitoshe safari yao kutoka kijichi mpaka kufka hapo , kama kweli jeshi la polisi lilikuwa sirasi kukamata watu hao waliomsababishia ajali mgombea wa kiti cha uraisi basi wangeshafika labda tu iwe kuna maagizo ambayo yamewafanya kuchelewa.
“Hizo siraha mnaotaka kuingiza Tanzania mnazitoa wapi?”Aliongea Hamza.
“Oh!, ahsante kwa kuuliza bwana mdogo , kidogo tu nimesahau kumtambulisha bosi wetu hapa , huyu ni Bosi Keita na ndio msingi wa haya maungumzo , kuhusu wapi siraha zinatoka ni juu yake”Aliongea Pancho kwa kujigamba.
“Pancho kama nilivyosema mtandao wetu haudili na maswala ya siraha bila ya utaratibu maalumu, kama unataka dili hili lipite lisimamie wewe mwenyewe na hela zako na sio za mtandao wa Chatu”Aliongea Dina na yule bwana mwenye asili ya kizungu na Kijapani alimpa ishara Pancho ya kuongea yeye.
“Miss Dina kama alivyoongea Pancho tunaweza kulimaliza hili swala kimya kimya na kusiwe na athari zozote kwa kila upande”Aliongea kwa Kingereza.
“Unamaanisha unaweza kuzima kesi ya kulipua gari ya mgombea wa Uraisi pamoja na Martini?”Aliuliza Lawrence.
“Itategemea na maamuzi ya Miss Dina?” “Kwanini nahisi hata waliompendekeza Jongwe kupeperusha bendera ya Chama ni kama wanashangilia kifo chake?”Aliongea Hamza huku wakati huo Dina akiwa ametulia.
“Tunafanyaje?”Aliuliza Dina akimegemea Hamza , isitoshe ndie aliesema wasije na watu wengi.
“Wana siraha na hata kama tukishambuliana bila siraha hatuwezi kushinda bila kushitua raia , hawa watu wana mafunzo ya mapigano”Aliongea Hamza na kumfanya Dona kuwa na wasiwasi.
“Usiwaze hili naweza kulimaliza kwa amani na kisha utadili nao kujua nini kinaendelea kuhusu mgombea wa uraisi kulipuliwa”Aliongea Hamza na japo Dina alikuwa na wasiwasi aliamua kumwamini Hamza.
“Bwana Keita kwa ninavyojua huwezi kudili na siraha pasipo kuwakilisha shirika la giza unalotokea”Aliongea Hamza akitaka kujua Black Association ambayo Keita anatokea.
“Jungle Army Merchant ndio ninatokea”Aliongea bila ya kusita sita.
“Kumbe ni Jungle , hebu subiri kwanza nipige simu, nikimaliza utaamua cha kufanya”Aliongea.
“Umpigie nani?”
“Utajua nikimaliza’Aliongea Hamza.
“Mr Keita haina haja ya kupoteza muda na hawa watu , swala ni moja tu wachague chaguzi moja kati ya tatu tumalizane”Aliongea Pancho akionekana kukosa uvumilivu.
“Kimya! , sitaki unifundishe namna ya kufanya biashara”Aliongea Keira kwa kingereza na kumfanya Pancho kukaa kimya , isitoshe alikuwa akijua Jungle Army Merchant walikuwa wafanyabiashara wakubwa ndani ya Black Market kwa kuuza siraha za kila namna.
Muda huo Hamza alikuwa ashapiga simu tayari bila ya kuwa na wasiwasi kabisa.
*****
Magneto, Las Vegas- USA
Ni ndani ya jiji la Las Vegas , jiji ambalo kwa wacheza kamari hawakuhesabu muda , Usiku ni kama mchana na Mchana ni kama usiku tu ndani ya hili jiji.
Katika moja ya hoteli ya kifahri ya nyota tano ndani ya chumba cha hadhi ya raisi , alionekana mtu bonge mweusi mwenye kitambi akiwa amelala chali.
Alikuwa mrefu wa mita kama moja nukta tisa hivi , vidole vya mikono yake vilikuwa vimevishwa pete za madini ya almasi , Dhahabu na madini mengine ya thamani , shingoni alikuwa amevalia mikufu ya bei ghali.
Mtu yule bonge alijikuta akitandaza miguu yake vizuri huku akifumba fumba macho na
kuyafumbua , katikati ya eneo la mapaja yake alionekana mwanamke mzungu mwenye nywele nyeupe(blonde) akiwa bize kumhudumia.
“Mr Mamen are you comfortable?”Aliuliza yule mwanamke kwa sauti tamu huku akiinua kichwa chake akimwangalia kwa macho malegevu , akimuuliza Big kama ni mwenye kuifurahia huduma.
Mwanaume yule bonge udenda ulikuwa ukitaka kumwagika kutoka kwenye midomo yake , alionekana alikuwa kwenye ulimwengu mwingine wa raha.
“Comfortable..!?, Deeper the better .”Aliongea akimaanisha azame chini zaidi ndio itakuwa vizuri.
“You’re so annoying , I’m realy tired ..”Aliongea yule mwanamke akimwambia anachukiza kwani amekwisha kuchoka.
Bonge yule mweusi kama msanii RickRoss alifungua droo ya meza pembeni na kitanda chake na kuchomoa maburungutu ya pesa za dola na kumtupia.
“Hakikisha najisikia vizuri mpaka kisogoni , nitakupa kiasi chochote cha pesa unachotaka”Aliongea Big na yule mwanamke uchomvu uliisha palepale na alijkuta akiongeza mashambulizi ya kuhakikisha Big anajisikia vizuri.
Dakika hio hio simu yake ilianza kuita , hata simu yake tu ilikuwa imetengenezwa kwa housing ya madini ghali sana na kuifanya ionekane kama kitu kisichokuwa cha kawaida kutokana na uthamani wake
“F*ck , kama ningejua ningeizima hii simu , nani ananipigia muda huu”Big alilaani huku akichukua ile simu na kuipokea maana namba ilikuwa mpya tena haikuwa ya taifa hilo
“Big naona kama kawaida yako sasa hivi unaringa , kwahio unaona sipaswi kukupigia hata kama ni swala linalohusu vita ya tatu ya dunia”Sauti ya kiume ilisikika katika simu ya Big.
Kitendo cha Mameni kusikia ile sauti mwili wake ulitetemeka na macho yake yalibadilika na kuwa mekundu na hata ule msisimko aliokuwa akisikia ulipotea.
Yule mwanamke aliekuwa bize kuhakikisha Big anafurahi alijikuta akipiga kelele mara baada ya kadudu kabig kupotea na kuwa kabamia.
“Boss!! , ni wewe kweli , naona hatimae umenipigia , nimekumisi sana”Aliongea Big huku sauti yake ikiwa imebadilika.
“Unafanya nini hapo , lazima utakuwa na m*laya kitandani , yaani ndio kwanza kunakucha wewe unahangaika na wanawake , kuna siku utafia kwenye kifua cha mwanamke”
“Hehe..Bosi wewe mwenyewe unanijua vizuri , isitoshe wewe ndio mtu pekee ulievunja rekodi yangu”Aliongea. “F*ck you!”Alitukanwa.
“Bosi nasikia upo Tanzania , habari za siku nyingi , vipi naweza kuja huko?”
“Nina mambo mengi ya kufanya siku hizi tutaona kama unaweza kuja , nyie watu ni wasumbufu sana mkisikia nipo mahali mnataka kuja tu , sitaki usumbufu wenu nahitaji kutulia kwa sasa”
“Bosi kwa uwezo wako na ushawishi wako unaweza kuomba chumba mapumziko Ikulu na ukapatiwa na warembo kabisa , hayo sio mapumziko ila ni kujitia stress tu , mapumziko ni yale wafariji wanakuwa wanabadilika badilika kila siku kwenye kuusisimua mwili”
“Sterehe za kutumia hela hizo nishazichoka , hata nikikuambia ni namna gani nafurahia maisha ya sasa hivi hutonielewa Big”
“Kama ni hivyo bosi kwanini umenipigia simu , kuna dili jipya?”
“Hakuna dili lingine , nishastaafu hayo mambo”
“Sababu ni ipi sasa Bosi , au kuna sehemu nimekosea?”Aliuliza Big kwa upole.
“Kwenye biashara zako unamfahamu bwana anaefahamika kwa jina la Keita?”
“Ndio mwaka juzi niliingia dili na kundi moja linalofanya shughuli zao ndani ya Afrika kuiba madini Adimu na kuyauza kwenda kwenye moja ya kampuni ya maswala ya kiteknolojia nchini Ufaransa , linaongozwa na bwana Keita”Aliongea Big.
“Huyu bwana wako naona ana juhudi mno , muda huu nimeelekezewa mitutu ya bunduki ndio maana nimekupigia simu kuthibitisha , Big kwahio sasa hivi umeshaanza kuwa mkubwa kiasi cha kunisaliti kisa tu nnimetoka kwenye uringo?”
Big mara baada ya kusikia kauli hio kutoka kwa Hamza alijikuta mikono ikimtetemeka kiasi kwamba simu ilitaka kudondoka.
“Bosi , subiri kwanza , nitampigia simu sasa hivi , naomba kwanza nimfokee baada ya hapo unaweza kumuua”Aliongea Big na dakika ileile alikata simu na kuitafuta namba ya Keita.
“Mamen Babe! , unafanya nini sasa mbona imepotea!?”Yule kahaba wa kizungu aliongea lakini Mameni alimpotezea na mara baada ya kuipata namba ya Keita aliipiga palepale.
Mara baada ya Hamza kumaliza kuongea na simu hakuongea neno na alitulia akiangalia matokeo.
Ijapokuwa Keita hakujua Hamza alikuwa akiongea na nani kwenye simu lakini alihisi kuna kitu hakipo sawa.
Dakika ileile simu yake ilianza kuita na alisogea pembeni na kupogea lakini muda huo huo alianza kuonyesha ishara za kupaniki.
Upande wa pili ilikuwa ni sauti ya Big kutukana kimarekani kwa mara nyingi mfululizo kadri alivyoweza.
“Bosi nimefanya kosa gani?”
“Unataka kumuua nani sasa hivi?”
“Bosi umejuaje nataka kuua mtu?”
“Unaetaka kumuua ni bosi wangu”
“…”
Keita alijikuta akikosa neo , alishangaa mno kwa zaidi ya sekunde kumi , ni kama alikuwa akisharabu yale maneno.
“Ah!”
Alijikuta hofu ikimwingia na vigoti vya miguu yake vilianza kumlegea na alijikuta akigeuka na kumwangalia Hamza.
Upande wa Hamza alikuwa akimwangalia Keita tu kwa mbali na kwa jinsi alivyoonyesha kupaniki na woga alitamani kucheka.
“Mr Keita , Mr Keita , what happened?”Pancho aliuliza mara baada ya kuona mabadiliko.
Dina macho yake yalichanua alijua kabisa mabadiliko ya Keita ni kutokana na Hamza alipopiga simu na kwake aliona mwanaume Hamza alikuwa akimshangaza kila siku.
“Nini tatizo Mr Keita , mbona huongei?”Aliuliza Pancho kwa wasiwasi
“Hivi unajua mimi na vijana wangu tutakufa sasa hivi kutokana na ujinga wako na wale wanasiasa wapuuzi?”Aliongea kwa hasira.
“Unamaanisha nini Mr….”
Keita hakuchelewa alichomoa Desert Eagle kutoka kwenye kiuno chake na kumchapa risasi tatu Pancho palepale.
Mpaka Pancho anadondoka chini muonekano wake ulikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini Keita anamshambulia.
Keita mara baada ya kumalizana na Pancho alitoa maagizo kwa vijana wake kuwashambulia watu wa Pancho na walionekana kuwa shapu kweli kwani ndani ya sekunde wote walikuwa chini.
Baada ya Keita kuituliza hali alijikuta akimdondokea Hamza kwa magoti huku akiwa na wasiwasi mwingi akitia huruma.
“Prince Rich.. Bosi wangu ameniambia kila kitu , naomba unisamehe kwa ujinga wangu , sikubahatika kukutana na wewe ana kwa ana zaidi ya kusikia habari zako ndio maana nimekukosea…”
Kitendo kile kiliwashangaza mno Dina , Lawrence na wenzake , waliishia kujiuliza Hamza ni nani mpaka bwana yule kuwa na hofu namna ile kiasi cha kupiga magoti.
“Nipe bastora yako”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Keita kukakamaa mwili lakini alimpatiia.
‘Tafadhari naomba uwaache vijana wangu waondoke , walikuwa wakifuata maelekezo tu kutoka kwangu na wanazofamilia zinawategemea”Aliongea Keita lakini Hamza hakumjali na muda ule aliinua ile bastora na kujielekezea kwake kana kwamba anataka kujipiga risasi.
Tukio lile lilimshangaza kila mtu wakishindwa kuelewa Hamza anataka kufanya nini
“Hamza unataka kufanya nini , usipaniki..”Aliongea Dina lakini kabla hata hajamaliza Hamza alikuwa ashaachia risasi.
Bam!
Mlipuko ule wa bunduki ulimuogopesha mpaka Keita na wote walimwaangalia Hamza kwa mshangao na walishangaa zaidi baada ya kuona hakuna kilichotokea.
Risasi ambayo ilitoka katika ile bunduki ilikuwa katika vidole vya Hamza , haikueleweka amefanyaje lakini ilionekana aliikamata kabla ya kumfikia, tukio lile lilimfanya Keita kushindwa kuendelea kupiga magoti na kukaa chini kwa kunyoosha miguu huku mapigo yake ya moyo yakidunda kwa kasi.
“Kabla sijafanya chochote nataka muelezee kila kilichotokea… sababu ya kwamba umepiga magoti sio kwasabau ya bosi wako bali ni kwasababu yangu hivyo nataka majibu”Aliongea Hamza.
“Serafii.!!, nipo tayari kuongea”Aliongea Keita huku akipiga kichwa chini kiasi cha kutoka damu kwenye paji la uso.
“Anza kuelezea , kwanini kifo cha Mgombea wa uraisi na nani kahusika”Aliongea Hamza.
“Hatujahusika katika kumuua mtu , tupo hapa nchini kwa ajili ya mazungumzo ya biashara ya kupitisha Siraha Kwenda Congo kupitia bandari ya Mtwara , kitu pekee ambacho nafahamu kuhusu muhusika tulipewa kazi ya kumtorosha hapa nchini kupitia boti yetu”Aliongea na kauli ile ilimfanya Dina kusikiliza kwa umakini.
“Imekuwaje mkajiingiza , sitaki kuuliza maswali mengi elezea kila kitu ninachotaka kujua?”
“Mara ya mwisho nilivyokuja hapa nchini niliweza kukutana na mstaafu Mgweno kwa ajili ya kuingia dili la kupitisha siraha , lakini kutokana na usafirishaji wote wa Kimagendo kuwa chini ya Chatu hakutoa maamuzi badala yake aliwasiliana na Miss Dina ambae mara baada ya kuelekezwa kuhusu dili hili alikataa, Mstaafu baada ya ombi hili kukataliwa alituambia hana namna ya kutusaidia kwani njia pekee ya kupitisha siraha hizo ni moja tu ambayo ni Mtwara kutokana na bandari zote kuwa chini ya mwekezaji”
“Nini kiliendelea”
“Wakati tukifikiria namna ya kutafuta njia nyingine ya kukamilisha dili hili nilipokea simu kutoka kwa mtu ambae alijitambulisha ni msaidizi wa raisi”Aliongea.
“Unamaaniisha Mheshimiwa Eliasi Mbilu?”
“Ndio na alisema anataka kuonana na sisi kwa ajili ya mazungumzo ya namna ya kukamilisha kile tulichokuwa tukihitaji , kutokana na kuwa na haraka ya kufanikisha hili dili nilikubali na kupitia msaidizi wake alinipa maelekezo niwaache vijana na boti yetu nchini Tanzania kwa muda na nikutane nae jijini Kual Lampur nchini Malaysia ndani ya tarehe alionitajia wakati akiwa ziarani”
Tokea tuzungumze kuhusu hili dili imeshapita mwezi miwili , inamaana huu mpango ulikuwa wa muda mrefu?”
“Inawezekana Miss Dina , kabla ya siku moja ya tarehe kufika , niliweza kufika Malaysia na nilikutana na mheshimiwa kwa siri sana kupitia msaidizi wake na nilitambulishwa kama mwekezaji”Aliongea Keitani kwa kutetemeka.
“Alitaka kuongea nini kwa siri namna hio?”Aliuliza Dina , ijapokuwa Keitani alijua alikuwa akitoa siri kubwa lakini hakuwa na jinsi.
“Aliniambia siku ya leo saa nne kamili za usiku mgombea wa kiti cha uraisi kupitia chama chake atafariki kwa ajali ya gari na atakaesababisha ajali hio napaswa kumtorosha nje ya nchi na kama ikishindikana nimuue kabla ya kukamatwa na polisi, kisha nitumie ushahidi feki wa tukio hilo kuhakikisha nakamilisha dili la kupitisha siraha”
“Ushahidi feki ni kutusingizia sisi ndio wahusika, si ndio?” ‘Ndio”
Ameenda mbali mpaka kutengeneza ushahidi feki
, yeye anafaidika nini katika hilo?”Aliuliza Lawrence.
“Kila kitu kipo wazi , naamini Jongwe sio chaguo lake na pili alitaka kujitengenezea njia za kupata maslahi hata akiwa amestaafu kupitia hili dili”Aliongea Hamza.
“Ndio , alitaka asilimia ishirini ya faida itakayopatikana na wakati huo huo Mgombea wa uraisi akiwa ni chaguo lake baada ya chaguo la Mgweno kufariki”Aliongea keita na kumfanya Dina sura kujikunja
“Mgweno na Eliasi wanataka kupinduana , madaraka huwa ni matamu sana”Aliongea Dina lakini upande wa Hamza hakujali nani anampindua nani.
“Vipi kuhusu muuaji ni nani?”
“Kuhusu mfungwa hatuna taarifa nyingi kuhusu yeye , tulipatiwa picha pekee na tuliambiwa ni mfungwa wa kidiplomasia aliefungwa kwa muda mrefu kwa siri”
Yuko wapi kwasasa?”Aliuliza Hamza.
“Ametoweka mara baada ya tukio, tunaamini alikuwa na mpango wake binafsi wa kujitorosha baada ya kukamilisha misheni”Aliongea na kumfanya Hamza kuvuta pumzi.
“Picha yake ipo wapi”Aliuliza Hamza na Keita alimpa ishara bwana moja wa kizungu na alimsogezea Hamza simu na ilionekana picha ya mfungwa kwenye kioo cha simu na mara baada ya kuiangalia alijikuta macho yake yakichanua.
“What the f*ck!!”
Hamza alijikuta akitoa tusi na kumfanya Dina kusogea kuangalia picha hio ili kujua kwanini kashangaa.
Comments