SEHEMU YA 65.
Wakati Hamza akiwa amembana yule mwanaume mlevi chini na mguu wake, yule mhudumu ambae aliwakalisha hapo aliingia kwa haraka huku akiwa na hisia mchanganyiko ilikuwa ni kama hakuwa ametegemea tukio hilo au hata kama alitegemea hakuwa na jinsi ya kulizuia kutokana na maagizo ya bosi wake.
“Samahani kaka , nini kimetokea?”Aliuliza yule mwanamke na Hamza aliacha kumminya na kumpiga teke.
“Huyu bwana amekuja hapa na mapombe yake na kutaka kumdhalilisha Meneja,hili eneo inaonekana lina usalama mdogo sana kwa watoto wa kike”
“Mr Hamza najua amekosea kweli , naomba umwachie kwanza”Aliongea yule mwanamke huku akimwangalia yule mwanaume wa miraba minne alivyodhbitiwa na Hamza na ilimfanya kuonyesha hali ya mshangao.
“Sio kirahisi, huyu mtu alitaka kumdhalilisha meneja na kwa ninachoona hapa pengine sio tukio la kwanza , hivyp napanga kupiga simu polisi waje hapa wafanye uchunguzi”.
Yule mhudumu mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akikakamaa , sio kwamba alikuwa akiogopa polisi, ukweli ni kwamba yametokea matukio mengi ya polisi kuja eneo hilo lakini hawakufanya chochote zaidi ya kuzuga, bosi wa hilo eneo alikuwa ameliweka jeshi la polisi mfukoni mwake, kilichomuogopesha ni kwamba swala hilo linaweza kumfanya kupoteza kibarua chake.
“Naona samahani kwa kile kilichotokea, lakini kabla ya kuwasiliana na polisi naomba kwanza niwasiliane na bosi wangu ili nione kama ananipa maagizo gani”Aliongea na kwa haraka sana alikimbilia nje kufanya mawasiliano.
“Vipi ushawahi kupitia tukio kama hili?”Aliuliza Hamza na El,iza alitingisha kichwa kukataa.
“Sijawahi nimeshangaaa Mr Laizer kupanga kitu kama hichi kwa ajili ya kutotaka kulipa”Aliongea Eliza.
“Kuna kitu hakipo sawa hapa , hata mimi sidhani yote haya ni kutotaka kulipa kama ni mfanyabiashara kwanini akatae kulipa”Aliongea Hamza.
“Unataka kumaanisha pengine kuna sababu nyingine zaidi ya kulipa deni?”Aliuliza Eliza.
“Kwasasa hatuwezi jua , lakini kwasababu nipo, wewe usiwe na wasiwasi , nina hamu ya kuona ni kitu gani wanapanga”Aliongea Hamza na muda huo yule mhudumu alirudi mbio mbio.
“Naomba mnifuate tafadhari bosi yupo vyumba vya ardhi kwenye Kasino”Aliongea na kauli ile ilimfanya Hamza kushangaa kidogo na kujiuliza inamaana hii sehemu ina vyumba vya ardhi.
Hamza alimpa ishara Eliza kutokuwa na wasiwasi na palepale alitoa tabasamu akimwangalia yule mhudumu.
“Hakuna shida tangulia tuelekee huko”Aliongea Hamza na yule mhudumu aligeuka na kuanza kutembea kuwapeleka vyumba vya ardhi.
Walitembea mpaka mwisho wa Korido na mwishoni kulikuwa kumejengwa kijumba kidogo kama kabati kubwa kilichopakwa rangi nyeupe , kwa kuangalia tu ungegundua ni kijumba ambacho hutumika kama mlango wa kuingilia kwenye lift kuelekea upande wa chini.
Eliza ndie ambaye alionekana kushangaa zaidi kuliko hata ya Hamza , katika eneo hilo kulikuwa na eneo kubwa mno ambalo katikati ya eneo hilo kulikuwa na ulingo takribani ukubwa wa mita sitini za mraba.
Ulingo huo wa mzunguko ulikuwa umezungukwa na viti virefu ambavyo vilikuwa vimekaliwa na wanaume , wanawake na hata watoto walikuwepo.
Kwa haraka haraka tu utaweza kusema watu hao wote ni wale wenye uchumi wa juu sana, yaani watu walioyapatia maisha.
Ililikuwa ni eneo la kushangaza mno tena kuwepo ndani ya ardhi ya nchi kama Tanzania.
Kitu ambacho kilimshangaza Hamza na Eliza ni kwamba watu hao wote waliokuwa hapo ndani walikuwa wamevalia vinyago usoni kana kwamba walikuwa wakiogopa sura zao kuonekana.
Ijapokuwa ni eneo ambalo lipo chini ya ardhi lakini mwanga wa taa za rangi tofauti tofauti zilimulika na kufanya eneo lote kuonekana kupendeza zaidi.
“Huu ni uwanja wa mapigano unaitwa NunguNungu ,Bosi yupo pale upande wa VIP , mimi naruhisiwa kuishia tu hapa”Aliongea yule mhudumu na kwa ukauzu aligeuka na kuondoka akiwaacha Hamza na Eliza.
Hamza na Eliza waliinua vichwa vyao upande ambao walielekezwa na yule mhudumu na waliweza kuona pande zote nne za steji kulikuwa na viti virefu , masofa na aina nyingine za thamani.
Kulikuwa na wanaume kadhaa ambao ndio pekee hawakuwa wamevalia vinyago na mmoja kati yao alikuwa ni bosi Laizer ambaye amevalia mavazi ya kitamaduni ya kimasai , alionekana kuwa na uso uliozeeka kidogo, licha ya umbali na mavazi yake ya kitamaduni lakini saa ya Luis Dantoni ya rangi ya almasi ilikuwa ikionekana.
Sekunde ambayo Hamza na Eliza walitaka kusogelea eneo lile sauti zilianza kusikika upande wa uliongo watu wanaopigana.
“Kill him , Kill him!”
Zilikuwa ni sauti za kingereza zilizokuwa zikitoka kwa watu, ilimpa Hamza uelewa kwamba inawezekana wengi wambao wapo ndani ya eneo hilo walikuwa ni wageni na sio raia wa Kitanzania, ni kweli kwamba kati ya watu waliovalia vinyago walikuwa wana ngozi nyeusi na za kizungu lakiini ilikuwa ngumu kuwatofautisha wala kuwafahamu.
“Tumia nguvu, Yess!, kata sikiio lake la kulia kwanza , yeah yeah safii”Zilikuwa ni kelele za kutisha na kwa jinsi ambavyo walikuwa wakiongea ni dhahiri kabisa watu hao wote walikuwa na roho za kikatili mno , yaani wanashangilia mtu kuulizwa kwa ukatili mkubwa.
Katika steji ya ulingo wa mapigano alionekana mwanaume wa miraba minne mweusi ambaye damu na jasho vilikuwa vimemloanisha na alikuwa amemshikilia mwanaume mwingine mwenye ngozi nyeupe shingo yake huku akiwa na kisu alichokielekezea shingoni.
Yule mwanaumne alieshikiliwa alionekana kujitahidi kuhangaika ili kujitoa katika mikono ya yule mwanaume wa miraba minne , lakini alikuwa ameshikiliwa vyema kiasi kwamba hakufurukuta.
Dakika ileile kilichosikika ni shingo ya yule mtu kuvunjwa na kupoteza uhai palepale huku akiwa hana masikio kwani yalishakatwa.
Kitendo cha bwana yule kuondoka chini na kupoteza maisha ilifanya kundi la upande wa kulia kuanza kushangilia kwa furaha kubwa.
“Tumeshinda , tumeshinda …!!”Ilikuwa ni kama wote wamepandwa na ukichaa na walianza kurusha maburungutu ya hela pamoja na vito vya thamani kwenye ulingo.
Jambo lile lilimfanyua Eliza kutetemeka kiasi cha kujificha nyuma ya Hamza.
“Hamza please naomba tuondoke , hii sehemu inatisha mno”Aliongea Eliza kwa sauti ya kuomba.
Upande wa Hamza alijua Tanzania pia kuna matukio ya ulimwengu wa giza lakini hakutegmea ingekuwa hatari namna hio, ukweli ni kwamba alishasikia tetesi za kitu kama hiki , kipndi ambacho alikuwa mtu wa kuperuzi sana mitandaoni alisikia malalamishi kibao kutoka kwa watu wakisema baadhi ya ndugu zao wamepotelea katika jengo hilo , sasa kile ambacho anaona ilionekana ilikuwa ni kweli kabisa, pengine waliongia hapo ndani waliingia kupigana na kilichowatokea ni kupoteza maisha na maiti zao kutoweshwa.
“Usiogpe Eliza ,ukiondoka si ndio kitu ambacho Laizer anataka kitokee, hili eneo linaonekana kuwa siri lakini kafanya makusudi kutuleta hapa ili tumuogope na uache kumdai”
“Lakini…”
Hamza ilibidi amtulize , ijapokuwa kwa mwanamke kama Eliza kwake eneo hilo lilikuwa likitisha lakini kwa watu wengine ilikuwa ni burudani ya aina yake na hata kuingia hapo pengine walilipia pesa nyijngi sana.
“Kama ushawahi kusikia Black Boxing Market ndio hii sasa , zipo nyingi duniani na zinaendeshwa kwa siri , ndio mahali ambapo matajiri wanatafuta msisimko wa furaha ya tofauti , haya matukio yote yanayoendela hapa yanarekodiwa na kuonyeshwa kwenye mtandao wa DeepWeb kama njia ya matangazo kujiingizia pesa zaidi , ndio maana hapa wentgi wanaonekana sio raia wa kitanzania”Aliongea Hamza.
“Lakini huu ni ukatili unaofanyika”Aliongea Eliza.
“Katika Dunia hii furaha inatafutwa kwa njia tofauti sana, kuwa na kila kitu hakumfanyi mtu kuwa na furaha ndio maana kuna starehe za namna hii, wewe nifuate mimi na tufanye kile kilichotuleta kisha tuondoke”Aliongea Hamza na kumfanya Eliza kumwangalia kwa macho ya kusita , kwa namna ambavyo Hamza alikuwa akijiamini aliona ni kama vile ni mtu ambae ashaingia kwenye maeneo kama hayo mara kibao.
Mara baada ya kufika eneo la VIP yule bwana alievalia kitamaduni alionekana kuwaona.
“Nimefurah kuwaona nyie wageni wetu wa heshima kutoka kampuni ya Dosam , mniwie radhi kwa kutokuja kuwapokea kwasababu ya ubize”Aliongea Laizer huku akifurahishwa na namna ambavyo Eliza alionekana kutetemeka.
“Mr Laizer tupo hapa kwa ajili ya kukusanya malipo ya mwisho ya tenda, lakini mazingira ya hapa yanaonekana kutokuwa mazuri kuongea”Aliongea Eliza
“Hili eneo ni zuri kabisa kuongelea maswala ya hela , hivi unajua wageni wangu wote unaowaona hapa wamelipia zaidi ya milioni mia kama kiingilio, kwasababu mmefika ngoja mliwekee baraka kidogo hili eneo”Aliongea na muda uleule alimwangalia mwanaume alievalia kinyago alionekana kama mhudumu na kumpa ishara ya kusogea.
“Leta mvinyo huo kwa ajili ya wageni wetu”Aliongea na Mvinyo wenyewe haukua mbali, mhudumu yule alimimina mvinyo kwenye glasi mbili na Bosi Laizer aliinua glasi yake juu kama ishara ya kuwakaribisha.
“Meneja mnapaswa kunywa huu mvinyo kama ishara ya heshima kwa ajili ya hili eneo”Aliongea na muda uleule alikunywa mvinyo uliokuwa kwenye glasi yake huku akitoa tabasamu lililojaa uovu.
“Samahani Mr Laizer situmii mvinyo wenye kilevi”Aliongea Eliza akijitetea.
“Kama nilivyosema sio swala la kunywa ama kutokunywa ni ishara ya heshima ndani ya hili eneo”Aliongea huku akiwa na muonekano usiokuwa na furaha.
“Macallan ni moja ya mvinyo bomba sana hasa huu wa miaka ishirini na tano , unaonaje nikinywa kwa niaba ya Meneja nadhani maana ni ileile”Aliongea Hamza.
“Unaonekana upo vizuri sana Mr Hamza likija swala la Mvinyo mpaka umejua jina lake”Aliongea Laizer na Hamza hakujali sifa zake, alichukua kile kilevi cha Eliza pamoja na cha kwake na kunywa vyote kwa mikupuo miwili.
“Mr Laizer tunaweza kusogea sehemu iliotulia, ili kwenda moja kwa moja kwenye lengo letu”Aliongea Eliza akiwa tayari ashatoa karatasi kutoka kwenye mkoba wake.
“Mbona haraka hivyo”
“Mr Laizer bado nipo kazini na nina kikao baada ya hapa , kwanini tusiongee haya makabidhiano ya hela kwanza , kampuni yetu…”
“Eliza..”Laizer alimkatia hewani asiendelee kuongea.
“Una hisa ndani ya kampuni ya Dosam?”
“Sijafanyakazi kwa muda mrefu ndani ya kampuni , ni vigumu kuwa na hisa”
“Kama hisa huna kwanini unafanya kazi kwa juhudi kiasi hiki, ni faida gani kubwa unapata tofauti na mshahara?”
“Haijalishji napata kiasi gani cha mshahata hii ni kazi na napaswa kuichukulia siriasi”
“Hivi katika dunia ya leo kuna sababu nyingine ya kufanya kazi kwa bidii tofauti na kupata hela?”Aliongea na muda huo alionekana kuchukua cheki kutoka kwenye mikono ya msaidizi wake.
“Nitakuandikia cheki ya milioni ishirini hapa na hela zinataingia kwenye akaunti yako binafsi , kuhusu malipo mengine mnaweza kunishitaki tu”
“Mr Laizer unajaribu kunipa rushwa?”
“Sio kukupa rushwa ninachofanya hapa ni kukununua”
“Kuninunua!?”Eliza hakuamini maneno ya Laizer na aliishia kukunja ngumi kwa hasira.
“Meneja wewe ni mwanamke mrembo sana , na nimekupenda ghafla tu , unaonaje ukichukua milioni ishirini na kuwa na mimi kwa mwezi mmoja, hii ni hela rahisi mno kuliko mshahara unaopata kwa jasho jingi”Aliongea na kauli ile ilimfanya Eliza kubadilika na kujawa na hasira na ukauzu kwa wakati mmoja , ni kweli ametokea familia ya kimasikini lakini hakuwa tayari utu wake kushushwa thamani.
“Mr Laizer ukiongea tena , nitakushitaki kwa kosa la unyanyasasi””
“Unishitaki .. hahaha.. huu ni utani ambao sijausikia kwa muda mrefu , mwanamke wa kariba yako ya kukutokuchangamka umewezaje kuwa meneja wa kampuni kubwa?”Aliongea huku akiendelea kucheka, aliamini mwanamke mrembo kama Eliza ili kuwa meneja lazima atumie uzuri wake na alitaka kutumia njia hio hio kumhonga.
Eliza alikuwa na hasira mno na kwa ilivokuwa ikionekana Laizer hakuwa na mpango wa kulipa na aliona swala hilo lishakuwa la kisheria tayari.
“Hamza tuondoke tu”Aliongea lakini Hamza alikataa palepale.
“Hatujapata hela tulioijia hapa , tunaondokaje kirahisi?”Aliongea na kumfanya Eliza kushangaa maana hakujua Hamza alikuwa akipanga nini.
“Kwahio unasema bila hela hapa huondoki?”Aliuliza Bosi Laizer.
“Mwanzoni sikuwa nikijali swala la hela na nilitaka kuona nini kinaendelea hapa ndani, lakini nimebadilisha mawazo”
“Nini kimekufanya kubadili mawazo?”Aliuliza Laizer.
“Hakuna sababu kubwa , cha kwanza umetufanya tusubirie muda mrefu na kisha ukatuma mtu wa kuja kutuogopesha , lakini sasa hivi unaanza kuongea uchafu wako kumtania meneja wetu , hatuwezi kupoteza muda wote huo tuliokuja hapa na kuondoka mikono mitupu , kingine nimekuja hapa kama mlinzi wa meneja , unadhani nitaonekana vipi ikisikika kwamba niliangalia tu bosi wangu akidhalilishwa?”Aliongea Hamza na kumfanya Bosi Laizer macho yake kuchanua.
“Hivi unajua muda mwingine muonekano wa mwanaume unaweza kumfanya kupoteza maisha hata kama hana kosa?”
“Acha kujaribu kuniogopesha , nakushauri tulipe kilicho chetu tuodoke kwa amani na sio kutupotezea muda , sisi wote ni watu wazima michezo kama hii ya kitoto ishapitwa na wakati”Aliongea Hamza huku akikaa chini kabisa na kauli yake ilimfanya Laizer kushangaa maana siku zote vijana ambao alikuwa akiongea nao walionyesha kumuogopa, palepale alijikuta akisimama na kuangalia mbele kwenye ulingo.
“Ukiangalia hili eneo lote ubunifu wake ni wa Kirumi, hii inakupa hisia gani?”Aliuliza akionyesha kuwa siriasi.
“Ninachoona hapa ni ushenzi tu unaendelea , muda mchache uliopita nimeona mtu akipoteza maisha kwenye ule Ulingo , huwa miili yao unapeleka wapi , vipi kuhusu waliojeruhiwa wanatibiwa wapi?”Aliongea Eliza.
“Meneja Eliza unadhani anaeingia ulingoni ni kwa ajili ya kutoka bila majeraha au kufa , hapa hakuna cha daktari ukiumia umeumia , ukifa umekufa”Aliongea.
“Hizi sio Karne zilizopita , hii ni Tanzania inayoendeshwa kwa sheria na haki za binadamu na watu sio watumwa wako , inakuwaje unawachukulia binadamu kama vile ni wanyama, sijawahi kuwaza ndani ya nchi yetu iliojaa amani kuna vitu kama hivi vinafanyanyika , huu ni ushenzi”Aliongea kwa kufoka lakini Laizer hakuonyesha kukasirika hata kidogo na alinyoosha kidole chake kuelekea ulingoni.
‘”Wale unaowaona pale nimewanunua kwa pesa nyingi na unajua alieniuzia ni nani? , hawa wote ni wafungwa wenye vifungo aidha vya maisha au wamehukumiwa kuonyongwa, wengine wamejileta wenyewe kwa ajili ya kutafuta hela , hebu chukulia wewe ni mfungwa adhabu yako ni ya kifo na kuna njia kama hii ya kuweza kupigana aidha kufa katika ulingo au kushinda na kupata hela na kisha kujiokoa na adhabu ya kifo ni kipi utachagua?, wewe utaniita kila jina baya lakini wao wananiita Mwokozi niliewapatia tumaini, hebu kwanza waangalie wanavyopigana , unadhani kuna wakulazimishwa pale?”Aliongea na kisha aligeukia wageni wake.
“Hebu angalia na watazamaji, angalia walivyocharukwa na akili kutokana na furaha , kukurahisishia ukishakuwa mfungwa muda mrefu na ukapewa nafasi kama hii , watazamaji hawatakuonea huruma , watakuona kama mambwa tu wanaojaribu kushindana ndio maana wanafuraha hio”
“Hawa watu ni kwamba tu huwezi kuona sura zao, lakini unadhani hawa wanatokea wapi , hapa kuna wanasheria , wanasiasa , wanajeshi, wajasiriamali wakubwa tu mpaka watu wa dini wapo hapa, ndio watu ambao wapo katika ngazi za juu kimaisha kwenye jamii zetu , watawala wetu, lakini wapo tayari kulipa mamilioni ya pesa kwa ajili ya kumuona Mfungwa akimuua mfungwa mwenzake kama sehemu ya starehe”Aliongea Laizer bila ya kubadilisha muonekano.
Eliza aliishia kukamaaa mwili bado hakukubaliana na maneno yake lakini alishindwa pia kujua namna ya kupinga.
Hakuelewa kwanini watu kama hawa ambao walionekana kuheshimika katika jamii na kuwa na elimu kubwa kuja kulipa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kumwangalia binadamu akimpiga mwenzake mpaka kufa na kisha kushangalia.
“Meneja inaonekana bado hujanielewa tu , mimi sio mkatili . unachokiona hapa ndio asili halisi ya binadamu akiwa nje ya sheria na haki , binadamu ni mnyama hatari zaidi ya wanyama wote tena zaidi ya mkatili ukimwondolea vifungo vya sheria, haya sio maneno yangu ni kutoka kwa mwanafalsafa mkubwa wa kihistoria Aristotle, na alikuwa sahihi maana unachokiona ndio uhalisia wa maneno yake”Aliongea Laizer na aliinama na kuchukua Whiskey na kupiga pafu mbili na kisha akaendelea.
“Hili eneo ndio sehemu pekee ndani ya Tanzania hii ambalo hakuna sheria , wala mfumo wa aina yoyote ile , Sheria ya msituni pekee ndio inatumika hapa, uwezo na nguvu ndio kitu pekee chenye maana hapa na mimi Laizer Kayole ndio mungu wa hili eneo”Aliongea huku akitoa tabasamu la kujivunia hasa pale alipomuona Eliza amekosa neno la kuongea lakini alishangaa kuona Hamza hakuwa na mabadiliko yoyote na macho yake yalionyesha ukauzu usiokuwa wa kawaida.
“Mr Hamza naona ni kama hujakubaliana na mim”
“Nafikiria kwanini unangea pumba zako kutupotezea muda na huna mpango wa kulipa”
“Kwahio unaona naongea pumba?”
“Ndio, unaongea pumba , nishasema unachokifanya ni mambo ya kitoto na huwa sipendelei michezo ya namna hii”Aliongea na kumfanya Laizer uso wake kucheza.
“Mr Hamza nimesikia umemuumiza kijana wangu aliekuwa amelewa , najua ana kiu ya damu lakini bado ni mtoto kwako lakini haogopi chui”
“Mini natokea ukoo wa farasi na nina uhakika wewe sio Chuii”Aliongea Hamza
“Haha.. kumbe unajua kuongea utani , sio mbaya nimependa kujiamini kwako , kama nilivyosema uwanja huu wa mapambano wa Nungunungu kinachoangaliwa ni nguvu pekee na uwezo , kama kweli unataka kuondoka na milioni mia nane zote basi onyesha kama uwezo unao”
“Oh , na ndio naonyeshaje sasa?”
“Hii sehemu ukiingia lazima ulipie kama sio hela basi ni mwili wako”
“Kwahio unamaanisha kama nikiingia ulingonni na kupambana kama mwanaume na kushinda ndio nitaweza kulipwa deni?”
“Hamza nini , hapana.. ni hatari sana tuondoke tu”Aliongea Eliza kwa kupaniki lakini upande wa Hamza alikuwa na tabasamu na kumwambia apunguze wasiwasi.
Upande wa Laizer aliishia kutingisha kichwa kwa tabasamu akionyesha kukubali.
“Haitokuwa fair sasa , sisi tupo hapa kwa ajili ya kukusanya madeni yetu na haina haja ya kupambana kwani ni haki yetu , kama nikipambana na nikishinda sitofaidika kwa chochote”Aliongea Hamza.
“Mr Hamza upo sahihi , unaonaje tukifanya hivi, kama ukishinda sitotoa milioni mia nane pekee mnazonidai bali nitatoa kiasi chote cha pesa kilichopatikana leo hii”
“Ndio shilingi ngapi?”Aliuliza na bosi Laizer alimgeukia bwana aliekuwa nyuma yake.
“Mpaka sasa tumeingiza milioni mia tisa bosi”Aliongea na kumfanya Hamza kushika kidevu , zilikuwa ni pesa nyingi mno kwa mahesabu ya Kitanzania ambazo zimeingizwa kwa siku moja tu.
“Deal!!”
Aliongea Hamza akikubali kuingia kwenye ulingo na kumfanya Laizer kutoa tabasamu la kikatili wakati huo Eliza akiwa na hofu kiasi kwamba mwili ulianza kumtetemeka , alijiuliza Hamza katoa wapi tamaa ya pesa kiasi hiko.
Baada ya kukubaliana na Hamza Laizer alionekana kujawa na furaha na alichukua maiki yeye mwenyewe na kisha kutoa tangazo.
“Mabibi na mabwana tunakwenda kuanza mechi ya kipekee ambayo mshindani wetu hatopitia raudi ya kwanza , tunaye Hamza hapa kutoka jijini Dar es salaam na ataingia kwenye ulingo moja kwa moja na kupambana na Maddog nambetia kiasi chote cha pesa kilichopatikana tokea asubuhi”Aliongea na kauli ile ilifanya watu washangilie kabla hata hajamaliza.
Muda huo Hamza alikuwa ashapanda kwenye Steji tayari na kufunguliwa mlango kuingia kwenye Arena na mara baada ya mashabiki kumuona mtu mwenyewe anaenda kupambana na Mad Dog walijikuta wakianza kumdharau.
“Huu ni utani , yaani hata hajatuna mwili anataka kupambana na Mad Dog”
“Mad Dog hajawahi kuwa na mpinzani tokea kufunguliwa kwa hili eneo, huyu binadamu anakwenda kung’atwa mpaka afe”
“Nitambetia kama ataweza kumshida Mad Dog”Aliongea mzungu mmoja alievalia kinyago na wengine walianza kubeti kati ya mpiganaji aliepewa jina la Mad Dog na Hamza , wengi walichagua upande wa Mad Dog kushinda.
Eliza mara baada ya kukaa chini na kuangalia kile kinachoendelea moyo wake ni kama ulikuwa umehama upande.
Hakujua imekuwaje hali ikafikia hatua hio , alitamani kupiga simu kuelezea kile kinachoendelea lakini tokea waingie hilo eneo simu zao hazikuwa zikisoma mtandao kabisa.
Muda huo kitu pekee ambacho aliona anaweza kufanya ni kumuombea Hamza kushinda na si vinginevyo.
Upande wa Hamza alikuwa na utulivu wa hali ya juu akimwangalia Eliza kwa namna ya kumtuliza.
Muda huo huo makelele yaliweza kusikika , kwa jinsi watu walivyokuwa wakishangalia utadhani ni michezo ile ya mieleka inayoonekana kwenye runinga , hata taa za manjonjo zilimulika eneo ambalo anatokea bwana ambae alijibatiza jina la Mad Dog.
Licha ya kwamba yanayofanyika hapo ni mambo ya kikatili lakini ukweli ni kwamba yalikuwa na msisimko mkubwa mno hasa namna ambavyo Mad Dog anaimbwa na watu kwa furaha kubwa.
Mwanaume huyo alikuwa amejengeka mno mwili kimazoezi, alikuwa sio mwafrika kama ambavyo Hamza alitegemea bali alionekana kuwa mzungu ambae amenyoa kipara huku akiwa amefunika uso wake na kinyago.
Mad Dog alionekana ni kama vile hakutaka kujulikana yeye ni nani kwa sura lakini licha ya hivyo watu waliendelea kumshangalia.
Ukimlinganisha Hamza na yule bwana ilikuwa ni kama vile ni mtoto na anakwenda kupambana na mtu mzima.
“Hahah… huyu mtoto hajaanza kujikojolea bado tu”
“Hey! Mad Dog kill him , nitakulipa dola laki tano ukimuua huyo dogo”
“Nitatoa Dolla laki sita Cash nikiona umeunyofoa mguu wake”
“Mimi nne ukinionyesha uume wake ulivyo kwa ndani”
Makundi ya watu kwa watu ni kama walikuwa wakishindana kuonyesha nani analipa zaidi lakini masharti yao yalikuwa yakikatili mno.
Kitendo cha Mad Dog kuahidiwa kiasi cha pesa ni kama mzuka ulianza kumvaa na licha ya kuwa na mwili mkubwa miguu yake ilianza kucheza cheza kwa wepesi, licha ya kwamba alikuwa amejifunika na kinyago lakini macho yake yalionyesha hali ya ukatili.
Mara baada ya kipenga cha pambano kuanza Mad Dog alimsogelea Hamza kwa spidi huku akiwa amekunja ngumi na alipomfikia aliirusha kumlenga eneo la kichwa.
Hamza kwa wepesi kabisa alisogea pembeni na ngumi ile ilipiga hewa kiasi cha kumfanyaMad dog akose mhimili na kutaka kudondoka maana alikuwa ametumia nguvu kubwa.
“Unatumia nguvu kubwa , unaendana vyema na jina lako la mbwa kichaa”Aliongea Hamza,
“Damn huyu chalii ana bahati , kama ile ngumi ingempata ingekuwa ndio mwisho wake”Mmoja ya watazamaji aliongea.
Mad Dog alianza kumshambulia Hamza kwa spidi kubwa , licha ya kuonekana kutumia nguvu kubwa lakini alionekana kuwa na mafunzo na hili kidogo lilimshangaza Hamza na kutaka kumuona sura yake.
Lakini licha ya Hamza kushambuliwa ilikuwa rahisi kwake kukwepa mashambulizi lakini alijua kama ni mtu ambae hana mafunzo ya uhakika basi ni rahisi kushindwa pambano.
Upande wa Hamza sio kama hakuwa akitaka kupigana , alikuwa akimkwepa Mad Dog huku macho yake yakiangalia watazamaji , kuna kila hisia zilizokuwa zikimwambia kinachoendelea hapo ni tukio ambalo limepangwa ili alifanye.
Ukweli hakuona kama kuna haja ya Laizer kupitia kampuni yake ya Dede kushindwa kulipa kiasi cha pesa wanachodaiwa na hata kama hawataki kulipa haikuwa haja ya kutengeneza uadui na wadeni wake na pia kutoa siri za uwepo wa hili eneo.
Hivyo Hamza aliamini lazima kuna mkono wa mtu mwenye nguvu zaidi ya Laizer katika swala hili na si vinginevyo.
Lakini kadri alivyokuwa akiangalia watazamaji hakuweza kumhisia yoyote na alijiambia pengine mtu aliepanga huo mchezo hayupo kwenye kundi la watu waliovaa Vinyago.
Hadhira hio ni kama ilikuwa na chuki ya muda mrefu na Hamza , walikuwa wakizunguka huku na huko wakimlaani Hamza na maneno ya kila namna, wakitaka apigwe .
Hamza alijikuta akisimama bila ya kusogea tena na palepale MadDog aliona hio ni nafasi adhimu ya kummaliza kabisa Hamza na alimsogelea kwa kasi akiwa amekunja ngumi lakini Hamza alikuwa amejiandaa kwani baada ya kukaribiwa palepale aliinua mguu na kumpiga Mad Dog kwenye makagari na kutokana na uzito wa teke Mad Dog alidondoka chini mpaka nje ya ulingo.
“Haaaaa…!!”
Hadhira ilijikuta ikishikwa na mshangao , kwasababu hawakutegemea Hamza angeweza kumshinda Mad Dog kwa shambulizi moja tu
Eliza alijikuta akifurahi mara baada ya kuona Hamza ameshinda , alikuwa na wasiwasi mno.
Mad Dog aliugulia maumivu ya kupigwa teke lile kwa sekunde kadhaa huku akijiuliza imekuwaje amepigwa kirahisi namna hio.
“Kama umeshindwa tayari , tuishie hapa”Aliongea Hamza kwa kingereza akimwangalia Mad Dog.
Mad Dog bado alionekana hakuridhika kushindwa na alitambaa na kurudi ndani ya ulingo.
“Kwenye ulingo wa Nungunungu ni swala la kifo au uhai , kama hujafa hutakiwi kushindwa , simama na endelea kupigana”Aliongea Laizer kwa kingereza kwa nguvu na Mad Dog mara baada ya kusikia kauli ile alisimama haraka.
Hamza aliishia kukunja sura , lakini kwa wakati mmoja akitaka kuangalia sura ya Mad Dog , dakika ileile bila kumpa nafasi ya kurudiwa na nguvu aliruka teke na kumpiga kifuani.
Bam!
Teke lile lilikuwa zito kiasi kwamba lilimchomoa Maddog kutoka kwenye ulingo na kwenda kudondokea mashabiki huku akitema damu nyingi , alijitahidi akasimama lakini ghafla tu alidondoka chini na kuzimia.
Lakini sasa teke lile pia lilimfanya kile kinyago chake kumtoka usoni na Hamza mara baada ya kumwangalia kwa umakini alijikuta akishangaa na kutabasamu kwa wakati mmoja.
Alikuwa ni yule mfungwa ambae inaaminika ndio kamuua Jongwe mgombea wa kiti cha uraisi kupitia chama tawala na kisha kutoweka.
Hamza aliishia kutabasamu na kujiambia ni kama alivyofikiria , hakuwa ameenda mbali lakini kumbe alikuwa amejichimbia ndani ya hili eneo.
Ilionekana hisia zake zilikuwa sahihi bwana huyo hakuwahi kukaa kwenye gereza ambalo halina fursa , ilionekana kipindi chote akiwa Gerezani hili ndio eneo lake la kujiingizia kipato na hata baada ya kumuua mtu mzito bado hakupanga kukimbia maana ni sawa kukimbia utajiri , kwa nchi kama ya Tanzania ilikuwa rahisi kwake kujitengenezea kipato bila ya kuwa na mshindani.
Hamza aliona mtu ambae alikuwa akimchezea alikuwa amefikiria mbali , pengine aliona ni bwana huyo pekee ambae anaweza kumletea ugumu katika uwanja wa mapambano ndio maana zikachewa hila mpaka kumfanya kupanda kwenye ulingo, aliishia kutoa tabasamu na kutaka kumjua adui yake.
Upande wa Laizer uso wake ulikuwa umejikunja kama vile amekula pilipili ya kuwasha sana , alikuwa na uhakika asilimia mia moja Hamza hawezi kumzidi Mad Dog na kujiamini huko kumetokana na kwamba Mad Dog kwa kipindi kirefu sana hakuwahi kuwa na mpinzani ndani ya hilo eneo na ndio mpiganani ambae amempatia pesa nyingi sana kwa kurekodi matukio yake na kuyauza kwenye mtandao wa Black Web.
Sasa alijiuliza inakuwaje Hamza kuwa na uwezo wa ajabu namna hio na kumshambulia kwa mapigo mawili Mad Dog na kisha kuzimia.
Eneo lote lilikuwa kimya , macho katika vinyago yalionekana kumwangalia Hamza kwa wasiwasi , zile dharau na kejeli zote zilikuwa kwisha.
Kwao kupatikana kwa mpinzani wa Mad dog sio tatizo , kilichowashangaza ni pale ambapo Mad Dog alishambuliwa na mashambulizi mawili tu mpaka kuzimia ili hali wamembetia kiasi kikubwa cha pesa kushinda.
“Takataka hii!1”
Aliongea Laizer kwa hasira akisahau ni zaidi ya miaka minne sasa tokea afungue hilo eneo ni Mad Dog ambae hakuwahi kupigwa, hata wapiganaji kutoka maeneo mengine duniani walifika kushindana nae na wote wakapigwa na kufanya watazamaji wengi kusafiri kuja kumuona.
Muda huo mara baada ya kuangalia uelekeo wa Hamza aligundua ni kama hakuwa na nia ya kurudi alipo ili kupata hela yake badala yake aliruka ulingo na kutokomea nyuma eneo ambalo Mad Dog alitokea.
“Anafanya nini?”Aliuliza Laizer.
“Inaonekana ameenda nyuma ya ukumbi”Aliongea kijana msaidizi.
“Pumbavu unadhani mimi ni kipofu , Seba hebu peleka mtu akaangalie anafanya nini”Aliongea Laizer na Seba kiongozi wa mabodigadi alikusanya watu kwa ajili ya kwenda kuangalia Hamza anafanya nini lakini muda uleule Hamza alionekana akirudi kupitia kwenye ulingo huku akiwa na utulivu wa hali ya juu.
“Kumradhi , nilienda toilet mara moja, Bosi Laizer nadhani umeshuhudia mwenyewe ushindi wangu , hivyo andika cheki ya pesa tuna njaa sisi “Aliongea Hamza huku akijifuta mikono yake kwa tishu.
“Umeumia , mbona unatoka damu?”Aliuliza Eliza na palepale aliishika mikono ya Hamza kuangalia kama alikuwa ameumia.
“Sijaumia sana nimejichubua kidogo tu”Aliongea Hamza huku akicheka lakini dakika hio meneja wa eneo la nyuma ya ukumbi alichomoka akija eneo la VIP huku akiliita jina la bosi wake..
“Bosi, bosi…”
“Nini kimetokea , mbona umepaniki?”
“Dakika hii huyu mtu amekuja kwenye vyumba vya wapiganaji wetu na kuwashambulia , zaidi ya wapiganaji wetu ishirini wamekuwa vilema”Aliongea
“Pumbavu, kivipi?”
“Ni kweli bosi , baada ya kuja alianza kutupiga sisi na kisha akafuatia wapiganaji “Aliongea huku akionekana anatetemeka.
“Hamza inamaana hiki ndio ulichofanya?”Aliongea Laizer huku hasira zikiwa zimempanda kiwango cha juu.
“Kama nilivyosema nilienda kutafuta choo lakini sikukiona lakini hao watu wako wakanizuia nisiondoke , sikuwa na jinsi zaidi ya kuwashikisha adabu”
Moyo wa Laizer ulikuwa ukivuja damu , milioni mia nane pamoja na mia tisa alizoahidi haikuwa kitu sana kwake, lakini hao watu ambao Hamza amewageuza viwete amewanunua kutoka magerezani kwa zaidi ya mamilioni ya hela , hata kama wakifa ulingoni angeendelea kujipatia hela lakini kama wakifa bila ya kuingia kwenye ulingo ni hasara.
Kwa mahesabu ya haraka haraka alikuwa amepata hasara zaidi ya bilioni ishirini .
Ili kupata wapiganaji kama hao kwake ilikuwa ni kama uwekezaji ,ilimbidi kwenda hadi nje ya nchi katika magereza kuangalia wafungwa ambao anaweza kuwaingiza kwenye ulingo , lakini hao wafungwa hata akiwapata hakuwachukua bure, lazima viongozi wa kisiasa walipwe kuidhinisha na kisha jeshi la polisi kuwaziba midomo , sasa kwa mlolongo wote huo zilikuwa ni pesa nyingi sana , alikuwa akinunua mpiganaji mmoja mpaka kufikia Dolla laki moja na nusu sawa na milioni mia nne na bado hapo hajawalisha virutubisho vya kutunisha misuli.
“Nadhani huwezi kunilaumu katika hili , isitoshe wapiganaji wako wamejaza misuli tu ila kupigana hawajui , hasara uliopata chukulia kama riba ambayo ulipaswa kuilipa Dosam kwa kuwazungusha muda mrefu na deni lao”
“Kwannini ulienda kupiga watu tena?”Aliuliza Eliza.
“Ni kheri kuwavunja miguu kuliko wakaingia kwenye ulingo na kuishia kupoteza maisha, wewe unaona kipi bora?”Aliuliza Hamza na kumfanya Eliza kushindwa kujua cha kuongea.
“Mr Laizer unapaswa kulipa maana haitokuwa taswira nzuri kwako ilihali watu kibao wamesikia kwa masikio yako ukiahidi”Aliongea Hamza na muda huo masikio ya Laizer yaliokuwa yametobolewa ni kama yamegeuka ya Sungura kutokana na hasira, aliishia kuchukua cheki na kisha aliandika kiasi cha pesa anachodaiwa na Hamza alichoshinda na kisha kwa kusaga meno alimkabidhi.
Tokea aanze biashara siku hio ndio mara ya kwanza kupata hasara kubwa namna hio.
Hamza mara baada ya kupatiwa cheki mbili moja alimkabidhi Eliza na ile yake alichukua na kuikagua kama masifuri yapo sawa na alijikuta akitoa tabasamu lililojaa uzembe huku akijiambia hajapoteza muda wake kuja ndani ya eneo hilo.
Eliza mara baada ya kushika ile cheki ya milioni mia nane alijikuta akishikwa na hisia mchangayiko , hakuamini deni hilo lingelipwa., sio kwamba hio ni pesa kubwa ambayo ashawahi kukamilisha , alikuwa akikamilisha madili ya zaidi ya bilioni kumi, kilichomfanya kushikwa na hisia mchanganyiko ni kutokana na kwamba alikuwa na hofu ya muda mrefu deni hilo haliwezi kulipwa na alijutia kuwahudumia Dede bila ya kulipa malipo yote.
“Asante sana Mr Laizer deni lako na kampuni yetu limeisha, sisi tunaondoka sasa”Aliongea Eliza huku akionyesha hamu ya kutoka hilo eneo.
Lakini sasa wakati wanataka kuondoka Seba akiwa ameambatana na kundi la wanaume waliovalia mavazi ya kibodigadi waliwazingira Hamza na Eliza huku wakiwa wameshikilia bunduki za shoti.
“Mr Lazer hiki ni nini tena ?”Aliuliza Hamza baada ya kugeuka
“Niliahidi nitakulipa lakini sikusema unaweza kuondoka hili eneo , tutakuacha uondoke baada ya kuchukua hizo hela , utalipia hasara uliosababisha”Aliongea Laizer.
“Mr Laizer huko ni kukosa aibu, huna thamani watu wanayokupa”Aliongea Eliza.
Laizer licha ya kuonekana anafanya biashara za kihalifu lakini alikuwa pia ni maarufu sana kwa watu , alikuwa amejenga shule kadhaa ambazo wanafunzi wanasoma bure na pia alikuwa akitoa misaada , licha ya kampuni yake kuhusishwa na skendo ambazo nchi haijawahi kudhithibitisha licha ni kweli baada ya Eliza na Hamza kushuhudia lakini aliheshimika na hata viongozi wakubwa walikuwa wakimwalika kwenye matukio makubwa makubwa Ikulu.
“Kimya wewe mwanamke , unadhani najali thamani watu wanayonipa , ninachojali ni biashara zangu kufanya vizuri na si vinginevyo.”
“Ni kheri kwanzia leo nimekujua tabia yako , siwezi kuwa gizani na kumpa mtu sifa asizostahili, kwangu wewe huna tofauti na jambazi”Aliongea Eliza na kumfanya Hamza kumwangalia Eliza kwa mshangao , alijiambia kumbe hata panya anaweza kung’ata akizidiwa.
“Mwanamke mpumbavu wewe usiejua nini uongee na kipi usiongee, Seba nataka kumuona huyo kijana akiwa chini na mwanamke anafaa sana kwa filamu za kutuingizia pesa”Aliongea
“Yes Sir!!”Yale majambazi ya Bosi Laizer yaliitikia kwa nguvu kama misukule na kumzingira Hamza kwa ajili ya kumshambulia.
…………
Dakika chache mbele wale mabodigadi wote walikuwa chini wakiugulia maumivu , Abasi ambae alikuwa ndio kiongozi wa mabodiadi aliishia kupiga yowe mara baada ya Hamza kutegua kiganja chake cha mkono na kudondoka chini.
Eliza ambae alishuhudia tukio zima alijikuta akikamaa mwili , alikuwa akitamani kutoa kilio kutokana na kile alichokuwa akiona , Hamza alimtia wasiwasi mno.
Hamza mara baada ya kugeuka nyuma aligundua Laizer alikuwa amekaa sakafuni kwa woga, tukio hilo lilimfanya kuhisi kudhalilishwa kwa karne na kwa muda huo hakuwa na mtu mwingine wa kumwambia apigane na Hamza kwani aliokuwa akiwategemea walikuwa chini wakiugulia maumivu.
Upande wa Hamza mpaka anakuja kupumua na kuona kundi la watu wakigalagala chini hata yeye hakujua amewezaje kuwashughulikia kwa dakika chache hivyo , maana hakutumia uwezo wa ziada kudili nao , ulikuwa ni uwezo wake wa mafunzo mbalimbali ya mbinuu za sanaa za kimapigano.
Hamza mara baada ya kutulia kidogo alimsogelea Mzee huyo wa kimasai ambae ni kibukta tu kilichokuwa kikionekana kutokana na rubega yake kupanda juu.
“Unataka nini kwangu?”Aliongea Laizer akijitetea maana hakujua Hamza alikuwa na mpango gani.
“Nataka hio saa , gharama za kumpiga mad dog ilikuwa ni milioni mia tisa, ukaniletea kundi la mabodigadi nipigane nao lazima niongeze hela kidogo , sitokufanya chochote wewe nipatie tu hii saa yako”
Wageni ambao walishuhudia tukio zima la Hamza kupiga mabodigadi mara baada ya kusikia hitajio la Hamza walijikuta wakiduwaa , ni kama sasa waliona Hamza anajaribu kujitajirisha kupitia Laizer.
“Unajua hii saa inauzwa shilingi ngapi?”Aliuliza Laizer huku akirudisha mkono wake nyuma.
“Najua ndio , imetengenezwa kwa madini ya platinum , mkanda wake ni wa ngozi ya mamba , kioo cha Yakuti , mashine yake lazima itakuwa ni CA, kama nitakuwa sahihi lazima itakuwa si chini ya dollar laki sita”Aliongea Hamza.
“Hizi saa zipo kumi na tano duniani , unadhani nakuogopa mpaka nikupatie kitu cha thamani namna hi?”Aliongea na kauli yake ilimfanya Hamza kuinama na kumwangalia bosi Laizer usoni kwa macho ya kichawi na ndani ya sekunde Laizer alijikuta akianza kutetemeka mwili mzima , alikuwa akihisi mtu ambae yupo mbele yake ni jini ama kiumbe ambacho hakuwahi kukutana nacho.
Hamza haikueleweka alimfanya nini na palepale alisimama na kumwangalia akiwa na tabasamu la uchokozi.
“Nitakuuliza tena , upo tayari kuivua mwenyewe au nikate mkono ndio niichomoe?”Aliuliza Hamza na kumfanya Laizer kuangalia watu waliokuwa wakimwangalia kupitia vinyago, aliona aibu mno lakini kutokana na kumhofia Hamza aliishia kuivua.
Hamza alimkwapua kwenye mikono yake na alisogea mpaka kwenye meza na kisha alichukua chupa ya mvinyo ambayo imebakia nusu na kuimalizia yote mara moja.
“Mvinyo mtamu sana huu , huwa muda wote nikinywa Wine namkumbuka mwandishi wa vitabu Willium Faulkner huyu jamaa alisema: ‘Human civilization starts with distilling technology’ kama unamjua Aristotle basi utakuwa unasoma soma vitabu na utaona sikudanganyi , kama mwanaume unapaswa kustaarabika hela unazo lakini unafanya vitu ambavyo fukara anafanya”Aliongea Hamza na Mzee Laizer hakuongea kitu , alijua Hamza alikuwa akimdhihaki ila hakuna kingine.
“Leo ilikuwa siku nzuri , nimepata hela , nimekunywa mvinyo wa bei ghali na nimechukua mazoezi kidogo , Mungu akijaalia Bosi Laizer pengine tutaonana tena , Binadamu sio milima”Mara baada ya kuongea alimshika Eliza mkono na kuingia kwenye lift.
Bosi Laizer mara baada ya Hamza kupotelea kwenye macho yake alisimama na kisha alimsogelea Seba ambae kamasi linamtoka kwa maumivu na kumpiga teke kwa hasira na kisha alisogelea mlango uliokuwa ni kama lift na alibonyeza, mara mlango ule ulipofunguka ilionekana eneo kama jukwaa la vioo , ukiwa kwa ndani unaona upande wa eneo lote la Ulingo ila kwa aliekuwa kwenye Ulingo hawezi kuona watu ndani ya eneo hilo.
Eneo hio walikuwa wakikaa VVIP yaani watu muhimu zaidi, yaani sio muhimu tu , wale muhimu zaidi ndio walikuwa wakikaa hapo ikiwemo wanasiasa wakubwa na wafanyabiashara wakubwa.
Sasa ndani ya eneo hilo kwenye Masofa alionekana mwanamke mrembo wa kuvutia sana akiwa ameketi kimapozi , alikuwa amevalia gauni la rangi ya bluu na viatu vya high heels.
“Madam Yulia , nadhani unapaswa kuniambia huyu Hamza ni nani haswa?”
“Mzee Laizer kwanini unaniuliza mimi?”
“Kwahio hata wewe hujui , kama ni hivyo kwanini uliniambia nimlete Eliza hapa na kumwandalia mtu wa kudili nae, inamaana mpango wako haukuwa Eliza bali Hamza kwasababu ulikuwa ukijua ni wapenzi?”
“Ndio , mwanzoni nilijua tutapata mkanda mzuri wa filamu lakini bahari haikuwa kwetu Hamza amekuja na kuharibu mpango mzima”Aliongea lakini Laizer alikuwa na hasira.
“Yuia unapaswa kunielezea vizuri , nimepoteza wapiganaji wangu na zaidi ya mabilioni ya hela , halafu unaniambia hujui chochote?”Aliongea kwa hasira lakini mwanamke huyo alionekana kutokuwa na hisia zozote , alisimama kimapozi na muda uleule alitoka kuwa mwanamke mrembo na kuwa mwanamke kauzu.
“Laizer nilikuambia udili na Eliza pekee lakini sio kutafuta ugomvi na Hamza , yaani hasara kidogo tu unabweka , wakati nakupatia kazi ulijaa ujivuni kwamba utaiweza lakini sasa hivi umeingia kwenye mikono ya Hamza unalalama , kwahio unataka nikulipe hasara uliopata?”Aliongea na kisha alimsogelea Laizer karibu kana kwamba anajaribu kunusa jasho lake.
“Kama shida yako ni pesa naweza kukuandikia cheki … lakini je ujasiri wakuipokea unao?”Aliongea kikauzu na kumfanya Laizer kugwanya , alikuwa na hasira mno wakati akija hapo lakini sekunde hio hio alikuwa akimuogopa huyo mwanamke.
“Sijamaanisha hivyo Madam , kwanini nikudai?”
“Unapaswa kujijua wewe ni nani , ijapokuwa kwa nje unaonekana mtu muungwana lakini wewe ni mhalifu namba moja ndani ya nchi hii , nikiamua huwezi kuliona jua tena, Mimi Yulia ndio mrithi wa nguvu ya familia yangu yote na hakuna mtu yoyote ndani ya taifa hili anaweza kuondoa mizizi yangu, kuja kwangu hapa unapaswa kujivunia , kwanzia sasa unapaswa kuanza kufikiria nafasi yako na sio kujilinganisha na mimi , aliekuwa anakupa kiburi nishamkata miguu na amekuwa joka la kibisa”Aliongea na kumfanya Laizer jasho kumtoka maana alielewa Yulia alikuwa akimaanisha nini.
“Nimekuelewa Madam , naomba unisamehe”Aliongea Laizer huku akiinamisha kichwa chake chini lakini kitendo kile kilimfanya Yulia kuanza kutoa kicheko , alikuwa akicheka vizuri mno na kufanya uzuri wake kuzidi kuonekana.
“Vizuri , napendaga mbwa mtiifu ..oh sorry namaanisha mtu mtiifu haha…”Aliongea na kisha alizipiga hatua kimaringo kutoka hapo ndani.
Laizer aliishia kumwangalia mwanamke huyo akiondoka huku macho yake yakiwa yamefunikwa na uovu mkubwa.
Comments