Regina mara baada ya kuulizwa swali hilo ni kama moyo wake uliingia katika hali ya mkanganyiko na akili yake , lakini mara baada ya kufikiria kwa umakini alionekana kupata jibu.
“Kabisa bibi, yaani simpendi”Aliongea na kumfanya Bibi Mirium kuonesha hali ya kukata tamaa.
“Hata iwe hivyo hakikisha huachani nae , ukihisi kutaka kuachana nae kumbuka maneno ya bibi yako , ukiona huko mbeleni umeshindwa kumpenda kabisa basi jifanyishe unampenda . mchukulie kama kete , mtumie kwa faida yako huku ukihakikisha haondoki”Aliongea Bibi Mirium na maneno yale yalimshangaza mno Regina.
“Bibi wewe….”Aliongea lakini muda huo Bibi Mirium alionekana kuwa siriasi na kile abacho anaongea.
“Mjukuu wangu unadhani mimi bibi yako ni kipofu na sionni kinachoendelea kati yenu , lakini sitaki kuongea sana kuhusu hayo , hakikisha unamshikilia hata kama huna hisia nae”
“Lakinni bibi kwanini…”
“Hakuna cha kwanini Regina , nataka uniahidi hutoachana na Hamza”Aliongea na kumfanya Regina kuishia kung’ata lips zake.
“Bibi nimekuelewa”Aliongea na kumfanya Bibi kucheka kicheko cha ahueni.
“Mjukuu wangu wewe ni mwanamke mrembo sana , umewazidi wengi kwa uzuri , ukiongeza mbinu kidogo tu unaweza kumfanya Hamza kufa kuoza kwako na kumfanya akutii kwa kila kitu , mimi bibi yako nakuamini sana”Aliongea na kumfanya Regina mwili wake kusisimka.
Alijiuliza inamaana ndoa hudumu kutokana na kudanganyana , Regina alijikuta akijihisi vibaya kwenye moyo wake , kadri alivyokuwa akiangalia swala hilo ni kama bibi yake alikuwa na sababu kubwa
Bibi Mirium alionekana kama vile ni mtu ambae amekuwa na amani ghafla na ki uchomvu sana aliegamia mto wake.
“Nimechoka sasa , nenda kamtafute Hamza , haina haja ya kuendelea kuja kuniona”Aliongea
Regina alijikuta akishikwa na huzuni baada ya kuona bibi yae anazidi kuwa mdhaifu , alijikuta pia akishikwa na mshagao akijiuliza kwanini bibi yake alionekana kuwa na ahueni lakini ghafla tu hali yake inabadilika.
“Bibi unajisikiaje , mbona ghafla tu umekuwa…”Regina alitaka kuongea lakini alizuwa na Shangazi Mariposa.
“Regina kwasasa nendeni nyumbani kwanza na umuache apumzike”
Regina licha ya kuwa na wasiwasi mwingi alijikuta akitii na kugeuka na kutoka nje , moyo wake ulikuwa mzito mno kuondoka.
Baada ya Regina kutoka Shangazi alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa ahueni na alinyoosha mkono wake na kushika mkono wa Marium na macho yake ni kama yamebadilika ghafla na kutoa miale kama ya jua.
Alimwangalia Bibi yake Regina kwa namna ambavyo ni kama anamsindikiza huko aendako.
*******
Regina mara baada ya kutoka nje aliweza kumkuta Hamza akiwa ameegamia boneti ya gari huku akionekana kama mtu ambae anafikiria kitu, aliishia kuangalia pete ambayo amevaa kidoleni kwa sekunde kadhaa na macho yake yalionyesha kutoridhika.
“Tunza hio pete vizuri , ni mali ya familia yetu”Aliongea na kumshitua Hamza.
“Unaonaje nikikuachia uitunze”
“Sitaki , kwasababu bibi ndio kakukabidhi kwasasa siwezi kukupokonya , isitoshe haina maana hata nikiichukua”Aliongea na kumfanya Hamza asijue alie ama acheke , ukweli ni kwamba alikuwa akiwaza kama kweli pete hio ni kama ambavyo anafikiria basi kuendelea kuivaa ni kujitafutia matatizo.
“Regina wapi tunaenda?”
“Naenda kumtembelea Yonesi hospitalini”Aliongea na kumfanya Hamza pia kukumbuka alimuacha Yonesi hospitalini , hivyo aliona sio mbaya kama ataenda kumuona pia.
Muda ambao Hamza anafika ndani ya hospitali ambayo Yonesi amelazwa alijikuta akimwangalia Regina na kujiangalia na kuona hawakuwa wamebeba chochote.
“Regina tunaenda kumuona mgonjwa lakini hakuna tulichobeba?”Aliongea na kumfanya Regina kushangaa na kuona ilikuwa ni kweli hakuna walichobeba.
“Ila tungebeba nini?”Aliuliza na kumfanya Hamza kufikiria kidogo na baada ya kugeuza macho upande wa kulia waliweza kuona kijana ambae anauza maua na kadi.
Hamza alisogelea na kisha alinunua ua na kadi ya kumtakia Yonesi kupona haraka na kisha waliongozana kuingia hospitalini upande wa wodi.
“Hili ua nikiliangalia vizuri naona kama linakufaa mno mke wangu”Aliongea Hamza.
“Halafu huelewi tu , nishakuambia usiniite hivyo”Aliongea huku akizidi kuongeza ukauzu lakini alikuwa akihema kwa nguvu kiasi kwamba alihisi kutokana na udogo wa lift Hamza atasikia mapigo yake ya moyo yalivyokuwa yakidunda.
“Acha wasiwasi , sina mpango wa kukupa zawadi ya ua”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kuzidi kuwa kauzu.
“Bora ufanye hivyo , siku ukijipendekeza na vimaua maua hupati mshahara”Aliongea na kumfanya Hamza kuishia kutingisha mabega, ilionekana Regina kutaja mara kwa mara neno mshahara ni kumkumbusha kwamba uhusiano wao ni wa kikazi pekee na hakuna zaidi.
Wakati Hamza akiwaza hilo lift ilifungukka katika wodi ya daraja la watu muhimu na walitembea mpaka kwenye wodi namba nne , kitendo cha kusukuma mlango na kuingia ndani Hamza alijikua sura yake ikikunjamana mara baada ya kuona ndani kuna mtu tena akiwa amevalia Kombati za jeshi zilizochafuka kwa vyeo.
******
Ni muda wa saa tisa za jioni alionekana Kanali Dastani akiingia makao makuu ya kitengo cha MALIBU, huku kwa kiasi flani hatua zake zikionyesha alikuwa na haraka.
Muda huo baadhi ya wafanyakazi walikuwa wakianza kutoka kazini wakipisha zamu za jioni.
Mara baada ya kuingia kwenye lift alibonyeza kitufe cha floo ya juu zaidi, floor ambayo ofisi za wakuu zaidi yake zilipatikana.
Yeye alikuwa akiendesha idara yake kama Kanali na ofisi yake ilikuwa floor ya kumi na tisa huku ya bosi wake ikiwa floor ya ishirini.
Kitendo cha kutoka katika floor hio mtu wa kwanza kukutana nae alikuwa ni Afande Msuya mkuu msaidizi wa kitengo cha MALIBU,licha ya kwamba kivyeo wote walikuwa ni makanali lakini Msuya yeye alikuwa ni mwandamizi hivyo Dastani ilibidi kumpa heshima yake.
“Jambo afande”Alisalimia Kanali.
“Dastani hivi unajua katika hiki kitengo wewe ndio unaonekana kuwa bize sana , nimeshauriana na Afande Doswe na kuona pengine tukupunguzie majukumu”Aliongea Msuya huku akionyesha hali ya kutoridhishwa na Kanali.
“Sio kweli Afande , nilikuwa nje ya ofisi kikazi ndio maana nimechelewa kuripoti”Aliongea
“Vizuri kama ulikuwa nje ya ofisi kikazi , sasa niambie ni kazi gani hio ambayo timu yako hata hawaijui”Aliongea na kumfanya Afande Dastani wasiwasi kumvaa.
“Dastani unanipotezea muda”Sauti nyuma yao ilisikika na kumfanya Afande Msuya bila kugeuka kukunja ndita.
“Nakuja afande”Aliongea na kisha alitoa ishara ya heshima kwa Msuya na kisha kupita huku akonekana kuvuta pumzi ya ahueni.
Ukweli ni kwamba licha ya Afande Msuya kuwa mkubwa wake kazini lakini hakuwa akimuamini ni moja ya Ma’Afande ambao walijaa rushwa na hata nafasi yake hio ya umakamu aliipata kutokana na kuwa mkwe kwa Makamu wa raisi.
Kwake mtu aliekuwa akimheshimu alikuwa Afande Doswe, lakini kutokana na mara nyingi kujihusisha na maswala mengi yanayomuhusu Mheshimiwa Mbilu, Kanali Doswe alikuwa akimuweka pembeni katika misheni nyingi na watu waliokuwa wakiaminiwa ni kama Amosi na wengineo.
“Jambo Afande”.
“Kaa chini Dastani, muda umeenda nina kikao sehemu nyingine”Aliongea kwa kuamrisha na Dastani alikaa chini.
“Nimeitikia wito Afande”
“Dastani naungana na Msuya , upo bize sana kama nisingekuwa na Siwalima katika idara yako mambo mengi yangekuwa hayaendi , kwasasa umegeuka kuwa Field officer tofauti na Command officer , kama unataka naweza kukuondoa ofisini”Aliongea Afande Doswe na kumfanya Dastani kuanza kukuna kichwa akikosa jibu.
“Nadhani umezipata taarifa za kifo cha Jongwe huko ulipokuwa umejichimbia mpaka simu yako kutopatikana hewani”
“Ndio Afande , nimezipata tokea jana usiku”Aliongea.
“Jana usiku ya saa ngapi?!!”Aliuza Afande Doswe huku akionyesha mshangao kidogo.
“Usiku wa saa tano kwenda sita hivi”Aliongea huku akionyesha hali ya kuchangahyikiwa kidogo.
“Mimi mkuu wa kitengo taarifa nimepatiwa saa nane usiku, wewe umezipata saa saa tano, kwanini hukutoa taarifa mapema?”
“Afande taarifa sikuzipata”
“Unamaanisha nini?”
“Nilikuwa eneo la tukio wakati ajali inatokea”Aliongea Dastani na kauli ile kidogo ilimshangaza Afande Doswe.
“Inamaana ulishuhudia wakati ajali inatokea , ilikuwaje mpaka ukawa aneo la tukio?”Aliongea na kumfanya Kanali kukuna kichwa huku akionyesha hali ya wasiwasi.
“Ongea kanali una dakika kumi tu za kunielewesha la sivyo nakubadilishia majukumu”
“Afande nilikuwa nikiendelea na uchunguzi wa kesi namba 99”Aliongea na kumfanya Afande Doswe sura kujikunja.
“Hii kesi si imetolewa chini ya idara yako na kupatiwa Amosi?, hukupaswa kuigusa mpaka tuhuma zinazokukabili kuthibitishwa , inamaana muda wote ulikuwa bize kuvunja utaratibu wa Kitengo?”
“Afande najua ni kweli nilikuwa nikivunja utaratibu lakini yote ni kwasababu ya faida ya Kitengo chetu”
“Faida kivipi?”
“Afande nadhani hata wewe unajiuliza mpaka sasa Amosi yupo wapi, kesi namba tisini na tisa ni nyeti sana na inahitajika kutafutiwa ufumbuzi wa haraka , lakini mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kutoka kwa Amosi , tokea mwanzo niliona hii ni kesi ambayo naweza kuitatua”Aliongea na kumfanya Afande Doswe kuvuta pumzi na kuzishusha na kisha akaangalia saa yake , ilionekana maneno ya Dastani yalikuwa na ukweli, mpaka muda huo Amosi hakujulikana alipo.
“Muda umeenda , niambie kwanini ulikuwa eneo la tukio?”
“Jana usiku wakati nikitokea Mpiji nilitumiwa ujumbe kwenye simu yangu ukinitaarifu Chendezi ametolewa Gerezani”Aliongea.
“Chendezi!”
“Ndio Afande , mfungwa wa kesi ya Ajenti Sedekia”
“Endelea”
“Wakati nikitafakati namna ya kudili na ujumbe huo nilipokea simu kutoka kwa Afande Norbert na kunipa habari juu ya ujumbe aliotumiwa na yeye”
“Unamaanisha Norbert na yeye katumiwa ujumbe kama wako?”
“Ndio katumiwa ujumbe lakini tofauti na wangu?”
“Wa kwake unasemaje?”
“Jongwe yupo hatarini”Aliongea na kumfanya Afande Doswe macho yake kucheza.
“Norbert aliniambia yupo hospitalini hivyo hawezi kutoka na alinipigia kuuliza maoni yangu juu ya ujumbe huo na nilimwambia kuhusu ujumbe wangu na ndipo tulipokubaliana mimi nifuatilie kwa undani kama ni taarifa ambayo ni sahihi”
“Kwahio ulianza kumfuatilia Jongwe”
“Ndio Afande”
“Baada ya hapo nini kilitokea?”
“Afande nilienda nyumbani kwa Jongwe baada ya kuambiwa yupo kwake lakini wakati nafika niliambiwa mheshimiwa alikuwa na kikao na Mzee Martini na kuambiwa kama nataka kuonana nae nije kesho, ila nililazimisha ni jambo muhimu sana nataka kuonana nae usiku huo hivyo nitasubiri , lakini baada ya kuonyesha msimamo wangu mtoto wa Mzee Jongwe alinipa taarifa mheshimiwa hana mgeni, bali ametoka kwenda kwenye kikao cha siri nyumbani kwa Mzee Martini , baada ya taarifa hio kuipata machale yalinicheza na haraka nilianza safari ya kwenda nyumbani kwa Mzee Martini , lakini wakati nakaribia kiwanda cha Binsulm ndio nilishuhudia gari ikilipuka”Aliongea Kanali na kumfanya Afande Doswe kupatwa na utulivu wa kutaka kusikia zaidi.
“Kama ni hivyo kwanini hukutoa taarifa?”
“Sikuwa na muda, mwanzoni sikujua gari ile ilikuwa ni ya mheshimiwa Jongwe , umakini wangu niliuelekeza katika pikipiki iliokuwa nyuma ya gari hio , kwa namna gari ilivyolipuka niliweza kugundua ni bomu mara moja kutokana na uzoefu wangu na mtu aliekuwa kwenye pikipiki nilimtilia mashaka kushika rimoti mara baada ya kuigeuza na kurudi alikotokea uzuri tulikuwa uelekeo sawa”
“Kwa maana hio ulianza kumfukuzia?”
“Ndio Afande”Aliongea na kumfanya Afande Doswe uso wake kucheza kidogo.
“Hilo lilikuwa swala la kutaarifu polisi na hata kama ulitaka kuhusisha kitengo ungempigia mkuu wa TISA, Wewe na Norbert kama mlipata ujumbe wa namna hio mlipaswa kuwasilisha makao makuu ili kuchakatwa, huo ndio utaratibu, Dastani huu nin muda wa kikao na sina muda wa kusikiliza mpaka mwisho , andika ripoti ya tukio zima na kisha unitumie kwenye barua pepe yangu, hata kama nikujirekodi fanya hivyo na unitumie kabla sijafika makao makuu ya TISA”Aliongea na kusimama.
“Ndio afande”.
“Usishahu na kuandika vifungu vya sheria ulivyovunja, asubuhi naitaka barua yako hapa na nitajua namna ya kudili na wewe”Aliongea akiwa kauzu na kisha alitoka ofisini.
Lakini kitendo cha kufungua mlango atoke alijikuta akisimama mara baada ya kuona sura aliokuwa akiitafuta.
“Amosi!!”
“Jambo Afande!!” Alisaluti Amosi.
Comments