“Sogea uone kama sitochangua ubongo wako”Aliongea Mdudu huku akiwa hana ishara ya utani kwenye macho yake.
Regina na Yonesi mara baada ya mara baada ya kuona Hamza kawekewa bunduki kwenye paji la uso mioyo ilitaka kuwatoka,
“Hamza naombeni tuishie hapa , Mdudu haina haja ya kwenda mbali hivyo”Aliongea Yonesi kwa namna ya kubembeleza.
“Huoni kama sio vizuri kutoa siraha eneo la hospitalini ?”Aliongea Regina.
“Kwahio ikiwa hospitalini ndio nini , ninaweza wa kumuua hapa na hakuna wa kufanya chochote”
“Kapteni kwanini tusimkamate tu na kumpeleka kituoni?”Aliongea Afande Diksoni ambae muda wote alikuwa ametulia pembeni.
“Upo sahihi , huyu tunaondoka nae hapa pamoja na Yonesi , nitakuwa nimepiga ndege wawii kwa jiwe moja”Aliongea Mdudu mara baada ya kujifikiria kwa dakika chache, lakini dakika ambayo anamaliza kauli hio bunduki yake ilikuwa ishachukuliwa kiustadi kabisa na kutua katika mikono ya Hamza na ilichukua dakika chache tu risasi zote kutolewa na Hamza na kumwagwa chini.
“Umeitunza vizuri hii bastora”Aliongea Hamza huku akiichunguza chunguz.
Mdudu na mwenzake walikuwa wameshikwa na butwaa maana hawakujua ni kwa namna gani Hamza aliweza kuchukua hio bastola , kilikuwa kitendo cha spidi sana kutokea.
Hamza mara baada ya kuhakikisha bunduki hio haikuwa na risasi hata moja alimrushia Afande Diksoni ambae aliidaka.
“Mnaweza kuondoka sasa , hapa ni hospitalini na panapaswa kuheshimiwa , kama hutaki ugomvi na mimi basi acha kumsumbua Kapteni”
Wajeda hao walijihisi kudhalauliwa kwa kile ambacho kimetokea , yule bwana ambae alikuwa ameambatana na Mdudu alionekana mtu wa shari kwani palepale kwa hasira alimsogelea Hamza kwa nia ya kumshambulia, lakini hata hivyo mbele ya Hamza ilikuwa ni kujitafutia matatizo tu kwani sekunde ambayo ngumi yake inamkaribia Hamza alishadakwa mkono na kilichosikika ni mifupa ya mikono yake kupishana.
Lakini licha ya maumiivu makali alionekana alikuwa na uwezo mkubwa wa kuyavumilia kwani aliinua mguu wake kutaka kupiga teke na buti la kijeshi lakini Hamza alikuwa mwepesi kwani alimkwepa na kumpiga ngumi ya mbavu iliomfanya kudondoka chini kama gunia kutokana na maumivu.
Mdudu mara baada ya kuona mjeda mwenzake ameweza kudhibitiwa na Hamza kwa mashambulizi mawili tu hali ya hofu ilimvaa palepale na aliona ilikuwa bahati kwake hakumshambulia.
Muda huo Yonesi na Regina walijikuta wakishangaa na kufurahi kwa wakati mmoja.
“Sogea , si ulitaka kuondoka na kapteni , ukinishinda nitakuruhusu kuondoka nae”Aliongea Hamza akimpa ishara Afande Mdudu , lakini bwana huyo aliishia kumeza mate mengi huku akionyesha hali ya kusita .
“Nitakuchunguza kwa umakini na kukujua wewe ni nani na baada ya hapo nitakukamata kulingana na sheria”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka.
‘Yamekuwa maswala ya kisheria tena, sekunde chache nyuma ulikuwa ukiongea kana kwamba hujali sheria lakini sasa hivi unaonekana kutii”
“Sitaki kuendelea kubishana na mtu kama wewe”Aliongea akionyesha kabisa amenywea na muda ule alimgeukia Yonesi.
“Yonesi wewe ni mchumba wangu ukubali ukatae na ni swala la muda tu utakuwa mke wangu”Aliongea kwa hasira na kumpa ishara mjeda mwenzake na kuondoka.
Mara baada ya wajeda hao kuondoka hatimae hali ya ukimya ilirejea , Regina na Yonesi walimwangalia Hamza huku wakiwa na mwonekano usioelezeka.
“Mbona mnaniangalia hivyo kama ndio kwanza mnaniona?”
“Ni bora kama usingenisaidia , Mdudu namjua vizuri ni mtu wa kuweka chuki moyoni na kwa sapoti ya cheo cha baba yake utamsababishia tu matatizo mkurugenzi”Aliongea Yonesi.
“Yonesi usiongee hivyo , ijapokuwa ni kweli Hamza ni mtu wa kukurupuka lakini nisingeweza kukuangalia tu ukichukuliwa kwa nguvu,maana haina tofauti na kutekwa”
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , nakuhakikishia hakuna matatizo yoyote yatakayotokea , halafu Kapteni unaonekana umeshapona tayari , kwanini usiende kukaa kwenye apartment za kampuni ili isiwe rahisi kwa yule mtu kukusumbua”
“Namfahamu Mdudu kwa muda mrefu tokea tukiwa kambini , kwa kilichotokea leo hatokuja kunisumbua tena mpaka apate mbinu ya kudili na wewe”Aliongea lakini Hamza haikufanya kuwa na wasiwasi kabisa.
“Yonesi nadhani itakuwa vizuri kama ukiwahi kurudi kazini , usifanye mazoezi magumu , nikikuona kazini itakuwa rahisi kwangu kutokuwa na wasiwasi”Aliongea Regina na Yonesi alitingisha kichwa kukubali.
“Regina hujawahi kuniuliza chochote kuhusu familia yangu au hutaki kujua?”Aliuliza Yonesi huku akionyesha kusita sita.
“Hata nijue ama nisijue haimaanishi kwamba nitabadilisha maamuzi yangu wala kukataa ukweli kwamba tumekuwa marafiki kwa muda wa miaka mitatu , ila kama unataka kuniambia nipo tayari kusikiliza”Aliongea Regina.
“Usiwe na wasiwasi, nyumbani kwetu Kongwa natokea familia ambayo inaheshimika kwa mchango mkubwa jeshini, niliondoka nyumbani kuja Dar kwasababu ya kuepuka usumbufu wa Mdudu na maswala yake ya ndoa maana simpendi, hivyo usiwe na wasiwasi familia yangu haiwezi kukuletea shida”
“Nakuamini Yonesi , isitoshe wewe ni msichana jasiri ambae unapenda haki sijapata ona”
“Usiseme hivyo mkurugenzi , ni kwasababu tu sipendi kuonewa”Aliongea Yonesi huku akitabasamu kwa furaha.
Ukweli licha ya kwamba muonekano wa Yonesi na Regina ni kama wanalingana ki umri lakini Yonesi alikuwa akimheshimu mno Regina , pengine ni kutokana na tabia zao kuendana.
Upande wa Hamza aliishia kukunja sura tu , kuna kitu alihisia na kujiambia kuna uwezekano Yonesi ni mtoto wa mwanajeshi mwenye cheo kikubwa kama anavyohisi kwa Mdudu..
****
“Damn it”
Kitendo cha Mdudu kuingia kwenye Jeep ya jeshi alijikuta akigonga usukani kwa hasira.
Diksoni mjeda mwenzake ambae alikuwa ametenguliwa mkono na Hamza aliishia kujikaza kisabuni ili aweze kufika hospitali ya jeshi kwa ajili ya matibabu .
“Kapteni huyu Hamza anaonekana sio wa kawaida kabisa , ndio maana Norbert licha ya uwezo wake ameweza kudhibitiwa kirahisi”
“Wewe ni mjinga ndio maana umepigwa kirahisi , ole wako uruhusu taarifa ziwafikie watu wengine kwenye kikosi changu”Aliongea huku akisugua meno kwa hasira na kumfanya Job kutulia.
Muda huo huo Mdudu alionekana kupokea simu kutoka kwa vijana wake.
“Afande taarifa kutoka TISA wale wawindaji kutoka ufilipino wameingia nchini”Sauti ilisikika upande wa pili na kumfanya Afande Mdudu macho kuchanua.
“Wameingia nchini lini ,mmeweza kupata uelekeo wao??”
“Ndio Afande wameingia jana nchini na wamefikia katika hoteli ya Sunset Kigamboni , wana Visa kama watalii lakini taarifa kutoka kwa majasusi ubalozi wetu Ufilipino wametuhakishia ndio wenyewe”
“Lazima wapo hapa nchini kwa ajili ya kufuatilia kupotea kwa wenzao , hakikisha hawaondoki kwenye rada zetu , hii ndio njia rahisi ya kujua walikuwa wakitaka nini kutoka kwa Hamza”
“Sawa Afande”
Kitendo cha Afande Mdudu kukata simu tabasamu lilichipua kwenye uso wake , tokea tukio la Hamza kuua kundi lile kikatili kule Bagamoyo , kitengo cha Malibu kikiongozwa na Afande Msuya walikuwa katika uchunguzi wa kutaka kujua walifuata nini nchini Tanzania mpaka kujaribu kumteka Regina.
“Kapteni hii ni njia nzuri ya kukamilisha uchunguzi wetu”
“Haha..hili lazima lifanikiwe , njia pekee ya kuja kufanya kazi hapa makao makuu ni kuonyesha uwezo wa juu kuliko Norbert, isitoshe pia nina hamu ya kujua ni kwasababu ipi kundi kama hili linatoka mbali hivyo kwa ajili ya Hamza tu”
*******
Upande wa Hamza aliishia kushika simu yake akiendelea kuperuzi wakati Yonesi na Regina wakiongea kwa kucheka, kwasababu stori hazikuwa hazimhusu hakushiriki katika maongezi.
Baada ya kuachana na Yonesi, Hamza na Regina walianza safari ya kruudi nyumbani maana muda ulikuwa umeenda, ilikuwa inakarbia saa moja na nusu za usiku.
Regina baada ya kuingia kwenye gari alionekana hakuwa na mudi ya kuongea kwani aligeukia kioo na kuangalia mandhari ya usiku ya mji.
Hamza alijua lazima Regina bado atakuwa na hasira juu ya swala la Eliza hivyo hakutaka kumsumbua na kuendesha gari kimya kimya huku akiwaza namna ya kumchangamsha.
Ambacho hakujua , Regina alikuwa akiyawazia maneno ya bibi yake, na kujiuliza au bibi yake ameongea vile kutokana na ugonjwa wake wa akili au kuna maana nyingine Zaidi .
Regina hata hivyo aliona kama ni swala la shida yake ya akili ni kwa muda mrefu sana hajaugua na kuna siku alikuwa akisahau kumeza mpaka dawa na hakuna shida yoyote iliokuwa ikimpata.
Kwake aliona sio sababu ya bibi yake kumwambia kumshikilia Hamza hata kama hampendi.
“Nitaenda kuonana na Dokta , pengine anaweza kuwa na ushauri mzuri Zaidi”Alijiwazia Regina mara baada ya kuona akili yake ni kama imechoka kufikiria , isitoshe kwanzia asubuhi alikuwa akifikiria mpaka muda huo, kutokana na uchomvu alijikuta akipotelea usingizini.
Hamza mara ya kufika nyumbani na kuegesha gari na kugeuka nyuma ndio alikuja kugundua Regina alikuwa amelala muda mrefu na kujikuta akianza kukuna kichwa.
Hamza aliona ni swala la kumbeba na kumpeleka ndani , hivyo alishuka na kufungua mlango mwingine , lakini wakati anataka kumpakata udenda ulianza kumtoka mara baada ya kuona lipsi nyororo ya Regina kwa ukaribu Zaidi.
“Hivi jamani si nimefunga nae ndoa huyu , inamaana siruhusiwi hata kumkiss japo kidogo”Alijiuliza Hamza swali la kipuuzi akijisahaulisha yupo kazini.
Kulikuwa na kasauti kalikuwa kakimwambia anaruhusa kwa asilimia mia moja na aache uoga la sivyo atadhalilisha uanaume wake.
Kitendo cha kuweka pua zake karibu na kupatwa na harufu nzuri kutoka kwa mrembo huyo pumzi yake ilianza kuwa nzito.
“Huu ni ufala , ngoja nipige hata kakiss kakuibia ibia”Alijiwazia huku akianza kuinamisha mdomo wake kuzisogelea lipsi za Regina.
Lakini sasa kabla hata hajazifikia Regina usingizi ulimzidia na kutaka kudondokea upande mwingine , sasa ile Hamza anamzuia ili asidondoke mdomo wake uliojaa udenda ulivamia nyonyo la Regina ambae alikuwa amevaa blauzi nyepesi tu.
Shida haikuwa mdomo wake kugusana na nyonyo la watu , tatizo ni kwamba mate mengi yalimtoka na kuloanisha ile sehemu .
Hamza macho yalimtoka lakini alipatwa na ahueni mara baada ya kuona Regina bado hajashituka.
“Bro endelea hapo hapo acha woga..”
Hamza hakuelewa sauti hio ya ushawishi inatokea wapi lakini aliamu kuitiii na kujaribu tena huku akifurahia marashi ya mrembo Regina.
Hamza hisia zilianza kumpata kwa kiwango cha SGR , na kutokana na kukosa tendo kwa muda mrefu ilimfanya ashindwe kujizuia na kutoa ulimi kama paka.
“Arghhh..!”
Regina alijikuta akishituka mara baada ya kuhisi kitu kikimuwasha upande wa kulia wa kifua chake.
Comments