Reader Settings

Hamza  mara baada ya kuona  Regina ameshituka  alirudi katika hali yake ya kawaida  huku akijifanyisha hakuna kilichotokea.

“Kumbe tushafika?”Aliuliza Regina huku akijivuta.

“Ndio  tumefika  na  nilikuwa nikijishauri hapa nikubebe au nikuamshe”

Muda ule  Regina  alijihisi ubaridi kwenye eneo lake  la kifua  na alijikuta akipeleka mkono  na kugusa na palepale  akikunja sura.

“Mbona nimeloa , haya maji yametokea wapi?”Swali hilo lilifanya uso wa Hamza kugeuka na kuwa wa bluu kama  mtu aliekosa oksijeni kwa muda mrefu.

Lakini  asingefanya chochote kwa wakati huo  maana Regina alikuwa ashagusa tayari.

Kilichomchanganya zaidi Regina alikuwa   na shauku ya kutaka  kujua maji  hayo yametokea wapi , hivyo mara baada ya kugusa  alipeleka  kidole puani na alijikuta akikunja sura kama vile amekula pilipili.

Licha ya  kwamba Regina alionekana kuwa mwanamke ambae hajui mambo mengi  lakini  alikuwa na akili ya kutofautisha  maji na mate., kunusa kidogo tu alijua  ni mate ya mtu.

“Wewe ..  wewe  umenifanyia nini .. kwanini unatabia  mbovu , hujawahi  kuona mwanamke  maisha yako  yote?”

Regina  alihisi  ukichaa ulikuwa ukimpanda na hakujua ni kwanini anamuamini  mwanaume mhenzi   kama Hamza.

“Wife  acha wasiwasi , mbona hakuna nilichokufanyia hebu angalia  nguo zako vizuri”Aliongea  Hamza na  alivyosikia neno wife akili yake ilikuwa ikichemka kwa hasira  na aliishia kumpiga Hamza na mkomba wake wa Hermes kwa hasira.

“Wewe  ni kichaa… mtu wa kawaida hawezi nifanyia huu ujinga , nitakuonyesha leo”Aliongea huku akirusha mkoba kwa nguvu  lakini kitendo kile kilimfanya kukosa  balansi  na kujikuta akitaka kudondoka kutoka kwenye Gari.

Hamza asingemuangalia tu mrembo huyo  akidondoka  na  kujipigiza kwenye mlango hivyo   kwa haraka alipiga hatua mbele na  kumzuia  asidondoke , lakini  kilichotokea mkono wake uligusa sehemu ileile iliokuwa imeloa.

Dakika hio ni kama muda umegandishwa  kutokana na ukimya uliotokea,  ijapokuwa  Hamza alitamani kuminya minya tena lakini alikuwa akiogopa Regina atakasirika zaidi  na pengine mpaka kufukuzwa   ndani ya hio nyumba.

“Regina  sija.. sio makusudi  , nimekuzuia usidondoke”Hamza alijikuta akigwaya huku akijitetea kwa kukosa  kujiamini.

Regina upande wake alijihisi  aibu  kubwa  alitamani kumpiga  lakini alishindwa kuchukua hatua.

“Hebu niachilie kwanza”

“Nakuachia ila usije kunipiga”

“Hata nikupige si utakwepa tu”

“Hehe.. ni kweli”Aliongea Hamza  na kumsimamisha vizuri.

Baada ya kutoka nje ya gari Regina uso wake ulikuwa umejaa aibu na hakutaka kabisa hata kumwangalia Hamza usoni kwani alitembea  haraka haraka kuingia ndani.

Hamza aliishia kupumua kwa ahueni mara baada ya msala huo kumpita na kujiambia  ni  kheri kutafuta hela kuliko kudili   na mwanamke kama Regina..

Hamza alijikuta akijitoa ufahamu na kujiambia kama  atalala nae kitanda kimoja je  ni raha  kiasi gani atajisikia.

Kitendo cha kupata mawazo hayo alijikuta  akitoa tabasamu  na kujiambia leo lazima atupie swaga  maana amechoka kula kwa macho , hivyo  haraka haraka  alipeleka  gari Gereji kwa ajili ya kuligesha.

Wakati  anaingia ndani alimkuta  Regina akiwa jikoni akichangula changula friji akionekana anatafuta kitu cha kula.

“Mke nimeagiza chakula muda  si mrefu  kitaletwa huna haja ya kula hio  mikate haitokushibisha””

“Halafu ni mara ngapi nakwambia  usiniite na hilo jina lako”

Regina  alijizuia tu kutomfanya chochote Hamza  licha ya kukasirika kuitwa mke maana alijua hana uwezo wa kumpiga.

“Regina bado tu una hasira  na mimi?”

“Kwanini niwe na hasira na wewe?”

“Kuna sababu nyingi za kuwa na hasira na mimi , swala la mimi kumuua mtu ,swala la Eliza  na  kilichotokea sasa hivi..”Aliongea Hamza akiona ni vizuri kuongea nae kuhusu hayo maswala.

“Mambo ya kuua mtu hayo ni maswala yako , wewe na Eliza kuwa wapenzi  halinihusu, sio kama  nina hasira  ila sijisikii tu  kujihusisha na wewe”

“Kivipi hutaki  kujihushisha na mimi ilihali kisheria sisi ni mke na mume , hata bibi yako amenipa pete  kwa ajili yako kama ishara ya  mambo yangu ni mambo  yako , haya ni mambo ya kifamilia”

“Hata kama bibi amekupa hio pete haimaanishi  kwamba kihisia  tutakuwa pamoja , karatasi ndio linasema hivyo lakini moyo wangu  hapana , acha kuwa mjinga kwa kuendelea kuona unaweza kuwa mume wangu”

“Kwahio unadhani niliamua kuandikisha ndoa kwa ajili ya kucheza  na wewe na kisha kila  mtu kuchukua hamsini zake?”

“Labda , nikuulize swali unajua nini kuhusu mimi?”Aliongea Regina  huku akionekana kuwa siriasi.

“Upande  upi?”Aliuliza Hamza maana kuna baadhi ya vitu  anajua na vingine hajui.

“Upande wote wa maswala ya  kuzingatiwa kabla ya  ndoa, unajua  nini napenda na kipi sipendi , unajua  napenda kula nini  na kipi sipendi kula,  unajua ni  aina  ya vitabu gani napendelea kusoma na vipi sipendelei , unajua  nimesoma wapi na kumaliza  wapi  , unajua  marafiki zangu wote, unajua  mtazamo wangu wa kimaisha  ukoje na ndoto zangu ni zipi ?”

“Nitajuaje hayo yote ilihali  hatuna  hata mwezi tokea tukutane?”

“”Ndio ninachomaanisha hapa , hatujajuana muda mrefu na unataka kulazimisha ndoa ya karatasi  iwe ndoa ya kihisia , huoni kwamba ni kichekesho?, ni mchana tu hapa   ulidhania  nimempa Eliza gari kwasababu ya  kutaka akuache  ili niwe na wewe , kama kweli ungekuwa unanijua usingekuwa na mawazo  kichaa ya namna  hio”

Hamza alijikuta akinywea , ilionekana Regina bado alikuwa na kinyongo juu ya kumsingizia kumpa  Eliza gari kwa ajili ya kumtuliza.

“Kwahio  mimi kwangu hata kama uue mtu au au  uwe mwizi siwezi kukasirika maana  kama ni kukutana tumekutana kikazi,  hivyo  kama usivyonijua mimi na wewe pia sikujui, mimi ulieniona ndani ya siku hizi tulizofahamiana pengine  sio mimi  , kwanini nikuambie na wewe unionyeshe wewe ni nani?”

Hamza aliishia kukosa neno ,   hata hivyo aliona maneno ya Regina yalikuwa sahihi , ukweli ni kwamba  hakuna anaemfahamu mwenzake na kwanini Regina ajali  kile ambacho anafanya yeye.

Licha ya kwamba kuna mambo kadhaa yalitokea kati yao lakini  yalikuwa katika msingi wa maswala ya mwajiri na mwajiriwa pekee na hakukuwa na hisia zilizohusika.

“Sikatai ni kweli umenisaidia mara kibao tokea tukutane   iwe ni mimi au kampuni  lakini  ndoa  ni swala  linalojitegemea , usidhani kwasababu ya  uwezo wako na koneksheni ulizokuwa nazo ndio  inakufanya ujione  una vigezo vya mimi kukubali, vipi kama ukanichukulia mimi kama mkeo kihisia na mwisho wa siku ukaja kugundua nilikuwa nikikutumia tu,utajisikiaje?”

Hamza alitaka kuongea neno lakini alikatishwa  na simu  yake ambayo ilianza kuita , alipoangalia aligundua ni mtu ambae alimwagiza kuleta chakula.

Hamza mara baada ya kwenda kuchukua delivety yake  na kufungua mbele ya Hamza ilionekana  aliagiza  Doughnut  za strawberry kwa ajili ya Regina.

Jambo ambalo lilimshangaza Regina maana hakutegemea kama Hamza angekumbuka kitu anachopenda   kiasi hicho.

“Wewe umeleta nini?”Aliuliza Regina  licha ya kwamba alikuwa ameona Hamza alikuwa ameagiza Dougnut.

“Licha ya kwamba tumeoana kikazi haimaanishi  siruhusiwi kukujali , nimeagiza kitu unachopenda”Aliongea Hamza.

“Kumbe unaweza kuagiza  hata Doughnut na kuletewa!?”

“Ulikuwa  hujui kama unaweza kuagiza , hio simu yako ni ya nini sasa?”

“Ni kwasababu sijawahi  kupata wazo la kuagiza  ndio maana sijui”

“Basi usijali , kwanzia sasa nitakupatia namba  ya mtu ambae unaweza kumuagiza  muda wowote ukijisikia  kula  ngoja nikuonyeshe  na akaunti yao ya instagram”Aliongea Hamza na alitoa simu yake na kwenda  mtandaoni na kumuonyesha  Regina picha za mgahawa ambao Doughnut zinapatikana.

“Nataka kula tambi”Aliongea Regina  mara baada ya kuvutiwa na namna tambi zilivyokuwa zikivutia katika picha.

“Unataka tambi na sio Doughnut tena”

“ Nataka kula vyote kwa pamoja unataka nilalie Doughnut?”Aliongea  na kumfanya Hamza kucheka kidogo.

“Kama unataka tambi  jaribu  kuagiza , huu mgahawa haupo mbali na hapa tunapoishi”Aliongea Hamza huku akimpatia Regina simu  yake.

Regina hajawahi kuagiza chakula  kwa njia ya mtandao ndio maana hakuwa mzoefu , hio yote ni kutokana siku zote  Shangazi anakuwepo.

“Nilivyokuwa kituoni,  kipindi ratiba ikiwa ni  ya kula tambi huwa tunakuwa na furaha  kubwa,  hapa nawaambia vipi wasiweke vitunguu”

“Hivi kwanini unachukia vitunguu namna hio?”

“Sipendi harufu y ake”Aliongea na kumfanya Hamza  kutingisha kichwa

“Mtumie meseji tu mwambie asiweke   asiweke vituunguu”

“Wewe  hutaki  tambi?”Aliuliza Regina  na Hamza  hakuona anaweza kula  hizo Doughnut na kisha kulala hivyo alitingisha kichwa na wewe awekewe oda yake.

Hamza aliishia kumwangalia tu Regina namna ambavyo alikuwa bize kuandika meseji akiagiza chakula.

“Mimi naona kuwa mke sio  kitu kibaya sana”

“Unamaanisha nini ?

“Licha ya kwamba hatujafahamina kwa muda mrefu , lakini   najua  unapendelea kula Doughunt kuliko kitu  chochote  , tena ambazo zina Strawberry, naendelea kukufahamu kwa spidi ya juu mno “

“Ni  kimoja katika vitu vingi ninavyopenda sioni haja ya kujivunia”

“Mtu na mtu hawawezi kufahamina   ndani ya muda mfupi , ni swala la  kufahamiana kidogo kidogo , unaonaje tukijipa muda  wa  kufahamiana  mdogo mdogo, nakiri kwasasa sikujui vizuri na pia wewe  una maswali mengi kuhusu mimi , lakini  sio  sababu  ya kutuzuia kuwa pamoja, huoni  muda mwingine  tulikuwa na furaha licha ya kutokufahamina”

“Unaongea nini , muda gani nilikuwa na furaha?”Aliongea huku uso wake ukiwa mwekundu.

“Sijui ila moyo  wangu unaniambia kuna  muda unaonekana kuwa na furaha kuwa  na mimi, halafu kama unakumbuka vizuri wewe mwenyewe umesema  huamini ndoa  sio kwasababu  hupendi kuolewa  bali ni kutokana na kuipa ndoa thamani ya juu , lakini  leo hii umekubali tuandikishe ndoa ya mkataba bila kunifahamu , hii inaonyesha mimi sio mtu mbaya kihiivyo,si ndio?”

“Hayo  ni mawazo yako peke yako , mimi nimeamua kukutumia kwa malengo yangu kwasababu  ulikuwa tayari kutumiwa”

“Ah!, kwahio  muda wote ulikuwa  unanitumia , kwanini huongea mapema sasa?”Aliongea Hamza huku akimshika  Regina kichwa.

“Acha ujinga basi , kwanini unagusa kichwa changu?”Aliongea Regina huku akigeuka kwa hasira.

“Sio tu  kukishika  nataka pia kukipiga, maana  kinafikiria sana  hata vitu ambavyo havina maana , tunaweza kuwa  hatufahamini  vizuri kwasababu sisi sio wapenzi halisi   lakini licha  ya hivyo haimaanishi kwamba haiwezekani,   kuna wenza kibao ndani ya dunia hii  ambao  wanapeana talaka kila uchao  unadhani hawafahamiani vizuri, hisia na kufahamiana ni vitu viwili tofauti , kwasasa tunaweza kuchukulia kama tumeruka darasa  kwanza kwasababu hatukuwa  na muda  na   tulishalimaliza hivyo  tunarudia  darasa la nyuma , ukiona unsjisikia  kunitaka   nitatakika”Aliongea Hamza

“Nikiona nakutaka , acha  kuota  nani  akutake?”Aliongea Regina huku akionyesha kukasirika

“Kwahio unamaanisha wewe unataka mimi ndio nikutak , kama  unataka nikutake nitakutaka kweli”

“Achana kabisa na hayo  mawazo, kama unataka kutaka watake  wengine , sitaki unisumbue na kunitaka kwako”Aliongea Regina na kuchukua Doughnut  na kwenda kujitenga mbali na Hamza .

“Hebu muone sasa , unaongea kwasababu unaona  wivu , mimi naona moyo wako ushaanza kunipenda”

“Unaongea kila  kinachokujia mdomoni kwasababu mshipa wa aibu huna, sasa wewe endelea kuongea ujinga uone hiki kisu nisipokididimiza kwenye mdomo wako”

“Basi wife yaishe , ngoja nikuwashie TV”

“Kwanini husikii , nishakwambia usiniite hivyo  wewe”Aliongea Regina  kwa ukauzu.

“Basi  nitakuita  Regina  usikasirike basi ukazeeka mapema”Hamza aliamua aache kumtania zaidi maana  aliona angeharibu , alijua kama Regina  atatokea kupenda kweli basi  itakuja kuwa ngumu sana  kwa Eliza kuendelea nae.

Lakini kwa wakati mmoja aliona kitendo cha  Bibi yake Regina kumlazimisha kumua Regina ilikuwa ni kama mtego kwake, licha ya kwamba  hakujua   alichokuwa akiwaza  Bibi Mirum ni nini lakini   hakuona ni jambo baya  kuwa na mwanamke mrembo kama Regina kama mke wake.

Hamza alijisikia fahari  kwani licha ya Regina kuonekana mgumu kuelewa lakini ilionyesha  anaanza kumwelewa taratibu taratibu.

Baada ya lisaa kupita   kila mtu aliweza kushiba tambi na Doughnut na kugawana vyumba  kulala.

Upande wa Regina usiku  alipata nafasi ya kufikiria tokea siku ambayo  amekutana na Hamza na matukio  yote mpaka kufikia siku hio , alijaribu kuhesabu siku  na kuona zilikuwa ni siku chache mno lakini ilikuwa ni kama mwaka  wamefahamiana , jambo hilo lilimshangaza  maana  hajawahi kumzoea mtu kwa haraka  hivyo  kiasi cha kugombana na kupatana  ndani ya muda mfupi, mrembo huyo  alijikuta akiingiwa na hisia mchanganyiko ambazo yeye mwenyewe hakuwa akizielewa vizuri , kutokana na kwamba ni kama mara yake ya kwanza kupatwa na hisia za namna hio.

*********

Aalto  ni nchi  inayozungukwa na safu za milima ya giza , ni mji  maarufu   zaidi kupitia jiji lake kubwa  la kila fursa la Zaburi.

Huu ni mji wa Aderon , mji wa watu masikini ndani ya nchi ya Aalto , jina langu naitwa  Luther  , kazi yangu ni mbeba mizigo sokoni lakini sasa hivi sina kazi kutokana na  kuugua muda mrefu.

Licha ya ufahamu wake kama Hamza ulikuwa ukifanya kazi  lakini  kwenye akili yake ni kama kuna  fahamu  mbili , fahamu moja ilikuwa ni ya  Luther  na ndio iliokuwa ikimwelezwa  wapi alipo, zilikuwa ni hisia kana kwamba alikuwa na uwezo wa kujua kila kitu ndani ya eneo  hilo asilolijua  kutumia akili nyingine iliokuwa katika akili  yake.

Hamza alijua yupo kwenye ulimwengu mwingine, ulimwengu  ambao unaonekana katika ndoto , alikuwa  akijua kabisa alikuwa akiota  yupo  ndani ya ulimwengu mwingine akiwa na sura tofauti,

“Huu ni ulimwengu mwingine , ulimwengu ambao  miujiza na maajabu ni vitu vinavyoonekana kwa macho”Aliwaza Hamza akijua kabisa yupo ndotoni lakini nafsi yake ipo sehemu  nyingine.

“Katika huu  ulimwengu  wanachoma watu  wakiwa  hai na moto wa ajabu”Aliendelea kuwaza muda huo akiwa katika kijumba ambacho alikuwa mwanzo baada ya kuachana na  watu ambao aliwafahamu ni ndugu  wa Luther  ambae ameiba mwili wake  kupitia ndoto.

Hamza  alijikuta  akijawa na  shauku  ya kujua vitu vingi kuhusu eneo hilo,baada ya kuingia kwenye chumba chake alisogelea maboksi ya mbao ambayo  yalikuwa yamepangwa kwenye kona ya  kijichumba hicho.

Licha  ya kwamba  akili yake ilimwambia yupo ndotoni , lakini alijihisi   njaa kali , alikuwa akihisi njaa kali , njaa ambayo ni kama inamwambia hayupo ndotoni bali yupo katika uhalisia.

Hapana  haikuwa akili yake iliokuwa ikimwambia  ana njaa , ufahamu mwingine ambao ni wa  Mzungu Luther ndio uliokuwa ukimwambia ananjaa  na  hata akili yake ilishindwa kufanya vizuri  na kuendeshwa na  njaa.

Mara baada ya kuchangula kwenye yale maboksi aliweza kuona kipande cha mkate uliokakamaa kama biskuti , aliangalia ndani zaidi na hakukuwa na kitu kingine zaidi ya sarafu zenye matundu katikati.

“Hizi ni sarafu kama zilizotumika  Karne  ya kumi na tano”Aliwaza huku akichunguza  zile sarafu kwa macho ya uchunguzi , licha ya kwamba   alikuwa ndotoini  lakini akili yake pia ilikuwa ikimkubusha sio wa ulimwegnu huo , yupo kwenye ulimwengu huo  kwa namna ya kutalii  kupitia mwili wa Luther.

Baada ya kushika ule mkate mkavu aling’ata kipande  ambacho kilianza kukatika mdomoni  kama  anakula mkaa ,akili yake ilikataana na ile radha  na kujikuta akitema chini.

“Nini hiki , mbona kama nakula  mkaa?”

Alijikuta akianza kuchunguza kile kipande kwa mara nyingine ili kuhakikisha ni mkate kweli .

Aliangalia kitu kingine kwenye lile  Creti la mbao na  aliweza kuona jiwe la kusagia(flint)  na hakuchelewa alichukua na kuanza kuponda ponda ule mkate mpaka ukalainika na kisha akapeleka  mdomoni na kuanza kula , lakini hakukua  na radha yoyote   na njaa ilikuwa kali.

“Hata kama nipo ndotoni  siwezi kula kitu kibaya kama  hiki ,  huu ni umasikini na siwezi kuishi  katika huu umasikini,  nataka kujifunza ile nguvu alioonyesha yule  askofu na kuwa   kama yeye , sijui kama nitafanikiwa ..  hapana ile nguvu siitaki yule mwanamke alivyokuwa akiniangalia lazima aliona  nina mafunzo ya kichawi katika uhalisia wangu licha ya kutokuwa katika mwili  wangu halisi , nikijipeleka kwa ajili ya kujifunza ile nguvu ni  kama kuwaambia wanichome moto”Aliwaza Hamza.

Licha ya kujihisi alikuwa kwenye ndoto  , lakini  moyo wake  ni kama unamwambia kwamba hawezi kurudi tena , maisha yake yanaendelea  kwanzia saa hio.

Wakati akijiwazia kwanini anaota ndoto ya namna hio katika uhalisia  aliweza kuona kijitabu kidogo kilichokuwa  pembeni ya  kitanda  na alisogelea na kukifungua ndani ili  kujaribu kusoma.

Lakini kilichomshangaza alishindwa kabisa  kusoma licha ya kwamba alikuwa akiona liugha ile ilikuwa ni ya kingereza,  ni kama uelewa wake wa lugha ya kingereza ulipotea ghafla.

Hisia zilizokuwa zikimwambia hajui kusoma  zilizidi kumuandama  na   kila  alipokuwa akijaribu kufikiria ni kama anaanza kupoteza ufahamu wake na ufahamu wa  Luther unamvaa.

Alijikuta akiacha kuwaza mara moja  kwa hofu na kukisogelea kitanda kwa ajili ya kulala , lakini kabla  hata hajapandisha miguu  miguu yake iliguswa na kitu kilichomshitua..

“Panya!!”

Aliwaza  mara baada ya kuhisi   sauti upande wa pili, uijasiri wa Uhamza ndani yake ndio uliomfanya asihangaike na ile Panya , lakini   muda huo huo  sauti  za panya wengi zilianza kusikika , ilikuwa ni kama vile  wamebanwa sehemu na kuanza kutoa  vilio , jambo ambalo lilimshangaza.

“Hapana  sitaki kuota  tena , ndoto isha mara  moja, cut!!”Hamza alijikuta akiongea kwa nguvu kutokana na hasira , alitaka kuondoka katika ndoto ambayo anaota lakini  licha ya kusema ndoto  iishe haikuwezekana

Baada ya  kutuliza hasira zake mara baada ya  kuona ndoto imeshindikana kuisha  alijikuta akisimama  lakini ghafla zile sauti za panya ziliacha kulia kama panya bali  sauti  ya kilio cha kwikwi kutoka kwa mwanamke kilisikika.

Kuna mtu analia , kuna mtu analia  tena usiku wote huu, alianza kujiwazia  huku  mapigo ya moyo yakienda mbio , licha ya kwamba alijihisi yeye kama Hamza  sio muoga lakini ajabu mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kweli , akili yake ilishindwa kudhibiti  mabadiliko ya mwili wake kutokana na woga aliokuwa akijisikia.

Hali hio ilimshangaza  na aliweza kugundua  licha ya kwamba alikuwa na ufahamu wa Hamza  lakini  alikuwa muoga , hakuwa jasiri tena , hii ndoto ni kama imemfutia baadhi ya uzoefu wake unaomfanya kuwa jasiri.

“Sio mimi ninaoogopa , ni huyu  Luther mzungu,  hapana  ni huyu Luther , mimi sio muoga”Aliongea huku akisikiliza upande kilio kile  kinapotokea , lakini licha kujifariji kwamba sio  muoga mwili ulikuwa ukitetemeka kwa woga.

“Nahisi uoga maana huu sio mwili wangu , acha kuwaza  huu sio mwili wako”Aliwaza  lakini  muda ule hakujua hata ni muda gani alikuwa ameshikilia kipande   cha mbao kwa ajili ya kujilinda.

Alijaribu kutafuta sauti inatokea wapi lakini  sauti ya kilio ilitokea  kila upande , ni kama  kila sehemu  kuna hio sauti,  sekunde chache mbele akizidi kuongeza umakini , ile sauti ilipotea na sasa  alichoweza kusikia  ni wimbo  ni kama kile kilio kilikuwa kimebadilika na kuwa  biti  la wimbo.

“Huu ni ulimwgnu wa  maajabu na uchawi , pengine hiki chumba kina mzimu  au msukule”Aliwaza Hamza  huku akitetemeka.

Alijaribu kutumia uwezo wake wote kujituliza kwa kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha  huku akiwa amefumba macho wakati akiwa ameusogelea mlango na sasa ni kama ile sauti aliweza kusikia vizuri ,  sauti  ilikuwa ni ya  yule mwanamke alieshuhudia akichomwa moto na  kilio chake ni kama kilikuwa kikimuita.

Hamza alifungua mlango  na sasa ni kama masikio yake  yalikuwa yakifuata upande ambao sauti ilikuwa ikitokea  na alizipiga hatua bila  ya kujali giza.

Kwa  alichoweza kufahamu  mwanamke ambae amechomwa moto alikuwa jirani yake  na sauti   ndio ilikokuwa ikitokea.

Ufahamu wa Luther  ni kama  ulikuwa ukimpigia makelele na kumwambia   yule mchawi alikuwa akiishi  hapa.

Hamza mara baada ya kusogelea eneo hilo alishangaa kwasababu eneo lote lilikuwa limechomwa  moto  na nyuma ya huyo mchawi ilikuwa imebobolewa na kilichoonekana ni kifusi cha  matakataka , lakini   sauti ya kilio  bado ilikuwa ikisikika.

Licha ya kwamba giza lilikuwa kubwa  nafsi yake ilikuwa na ujasiri kasoro mwili wake.

“Kama waliemchoma  ni yule mchawi kwanini nasikia sauti yake , au  hili eneo kuna  vyumba vya chini   ambavyo hawakuona?”Alijiuliza Hamza.

Ile sauti ghafla tu ilibadilika kutoka kuwa  ya kike na kuwa kama ya mwanaume kutokana na uzito wake , lakini muda huo sauti  haikuwa ikisambaa bali sauti ilikuwa  ikisikika kwenye ufahamu wake  tena kwa ukali mkubwa.

“Kama naota  na  huu mzimu ukiniua   pengine ndio njia ya kutoka ndotoni na kulala kwa amani”Aliongea Hamza akiamini kwamba  atatoka katika hio  ndoto kwa kushambuliwa na huo mzimu unaotoa sauti.

Kitendo cha kusogelea  karibu kabisa  ghafla tu  ile sauti ya kilio ilipotea  na kukawa kimya, Hamza akijua kile kilio kilipita ghafla tu alihisi sauti ile ikitokea  nyuma yake  kwenye chumba alichotokea na awamu hio ilikuwa na nguvu  kiasi kwamba ujasiri wa nafsi yake yeye kama Hamza ulimwambia usiogope lakini  mwili   mabao haukuwa wake  ulikuwa kwenye mbio huku  akipiga makelele.

“Jamani mzimu weee! ,  kuna mzimu , kuna Mzimu.!!!!!”

Hamza alikuja kugundua ambae alikuwa akiogopa sio yeye kama Hamza bali katika mazingira  kama hayo ni   Luther , alijitahidi kutokukimbia lakini nafsi ya Luther ni kama imeamka na mpaka anakuja kusimama  alikuwa mbele ya  geti la kanisa  na kuzuiwa na walinzi ambao walikuwa wakimshangaa kwa makelele yake.

Kilichomuogopesha zaidi  licha ya kufika  mbali na nyumba yake ni bado sauti ya kilio alikuwa akiisikia huku  ikiwa imeambatana na sauti za  mbwa kubweka.

“Unafanya nini hapa , kwanini unapiga makelele?”Swali kutoka  mlinzi , muda huo sauti yake ilikuwa imeamsha na majirani wengine.

“Mzimu , kuna mzimu kwenye ile nyumba ya mchawi”Aliongea  Luther huku yeye kama Hamza akijitahidi kutoonesha woga lakini alishindwa kutawala  mwili kuongea.

Muda huo mlinzi mwingine aliongezeka  , ilionekana alisikia  sauti za  kelele za Hamza,

Wale walinzi wote mara baada ya kusikia kauli yake , walionyesha kushikwa na wasiwasi pia na  kwa muonekano wa Luther wale  walinzi  ni kama walikuwa na wasiwasi wa kumuamini kama anaongea ukweli.

Yule  mlinzi  alimwangalia  Luther  kwa macho  ya wasiwasi na kisha alimwambia mlinzi mwenzake asubiri  akamwite mchungaji.

Dakika chache mbele  yule mlinzi alirudi akiongozana na mwanaume mwingine mzungu ambae   ana nywele nyeupe.

“Naitwa mchungaji Benjamini , niambie kilichotokea”Aliongea.

Wale walinzi waliishia kusimama   nyuma ya mchunganji huku wakiwa na wasiwasi   wamemsumbua tu mchungaji kutoka kwenye usingizi wake.

Hamza mara baada ya kuona anashindwa   kujidhibiti kuongea  aliona airuhusu akili ya Luther kuutawala mwili na palepale  kwa  msaada wake aliwezesha kusimulia kila ambacho alisikia.

“Umefanya vizuri , ujasiri wako unaonyesha ni  kwa namna gani  umejitoa kwa  Mungu”Aliongea yule mchungaji na kisha aliwageukia wale walinzi.

“Thompson   na  Gary waiteni  walinzi wengine  waliopo  hapa ,  huyu mchawi lazima atakuwa ni wa daraja la  chini hivyo haina haja ya kumhusisha askofu”

“Sawa  bwana wangu”

Hamza alijaribu kumfahamu  huyo mchungaji kupitia akili ya  Luther na aligundua  alikuwa ni mchungaji wa  daraja la  kati  na  alikuwa na uwezo wa kudili na mitego ambayo imeachwa na mchawi   wa  daraja la chini,kulikuwa na gepu kubwa kati ya mchungaji na  mchawi wa daraja  la chini kinguvu.

Yule mchungaji alimuuliza Hamza  jina lake , Hamza alitaka kusema anaitwa Hamza lakini mdomo ulikuwa mzito kuongea na alijikuta  akisema anaitwa Luther na sio Hamza.

Muda uleule  watu wengi walikuwa washatoka katika nyumba zao na kukusanyika mbele ya nyumba ya yule mchawi  wakiwa  na mienge ya  moto kama  vyanzo vya mwanga.

Hamza  muda huo ndio alikumbuka  kuangalia juu angani  na alijikuta akishangaa mara baada ya kuona mwezi haukuwa  mwezi wa kawaida , ulikuwa mwezi mwekundu  kabisa kama vile umejaa damu.

Licha ya  kuwepo  kwa watu katika eneo hilo   , ni yeye Hamza pekee ambae alkuwa  akisikia sauti  za kilio  cha yule mwanamke  na alijiuliza kwanini watu hao hawasikii chochote tofauti  na yeye

“Ndio  hapa kuna mzimu….”Aliongea yule mchungaji kanakwamba amejua Hamza ambacho anakifikiria.

 

Previoua Next