Hamza hata hakujua ndoto iliisha saa ngapi na saa ngapi alipata usingizi lakini kitu ambacho alikuwa akikumbuka usiku aliota na katika ndoto aliishia akiwa anamwita mchungaji kwa ajili ya kudili na mzimu.
Alijikuta akikaa kitandani na kufikiria juu ya uhalisia wa ndoto , ukweli ni kwamba ashawahi kusikia aina za ndoto ambazo mtu huota huku wakati akijua kabisa alikuwa akiota , ndio kilichokuwa kikimpata Hamza , alikuwa akiota yupo ulimwengu mwingine huku akijua kabisa alikuwa akiota.
Maneno ya kile kimemo ambacho kiliachwa kwake juu ya ndoto hizo kilikuwa kikijirudia rudia katika akili yake.
“The history of your past life in onother world has already begun to echo , if you fail to inherit your history ,it will be the end of your life in this world , your greatest enemy has already awakened”
Hamza alijikuta akikumbuka maneno hayo , lakini ajabu licha ya kwamba ni swala ambalo lilikuwa likimpa wasiwasi kwa kiasi flani lakini alijikuta akianza kupatwa na hamu ya kujua kinachoendelea , kwake ilikuwa ni kama anaangalia sinema ya karne za kumi na tano katika nchi za Ulaya.
Hamza kabla hajatoka kitandani aliona siku hio anapaswa kwenda kuonana na Frida , sababu ya kutaka kuonana nae ni kwamba alikuwa na uwezo wa kuota bila kutumia mshumaa wa nuru ambao alipewa , alikuwa akitaka maelezo kama kuna shida yoyote ya yeye kuota bila ya mshumaa huo , maana ukweli ni kwamba katika maisha yake ya nyuma hakuwahi kuota ndoto za maajabu namna hio , zimeanza muda mfupi tu baada ya kufahamiana na Regina.
Kwasababu alikuwa na namba ya Frida aliamua kumtafuta muda uleule na simu yake ilipokelewa na alimwambia waonane siku hio na Frida upande wake ni kama alikuwa akiisubiria simu ya Hamza kwa hamu zote.
Alikuwa na mpango wa kwenda sehemu mbili kwa wakati mmoja mpango wake wa kwanza ilikuwa ni kwenda kuonana na Frida na kisha achukue safari ya kuelekea Morogoro..
Kwasababu alijua ilikuwa ngumu kwa Regina kupika chochote alitoka na kwenda jikoni.
“Jiandae nataka twende wote kwenye kampuni”Aliongea Regina baada ya kumaliza kifungua kinywa.
“Leo ni jumamosi na kazini sina kazi hivyo sitoenda”Aliuongea Hamza maana alikuwa na mipango yake kichwani tayari.
“Sio huna kazi ni kwasababu hujatafuta kazi ya kufanya , unataka kwenda wapi kama huendi kazini?, au ni chuo si likizo inaendelea?”
“Sio chuo , kuna maswala yangu binafsi naenda kuyafuatilia”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumwangalia na muonekano usiosomeka na alionekana kuna kitu anataka kusema lakini anasita.
“Jana usiku umesema tupeane muda wa kufahamiana na kuelewana , nimefikiria kwa umakini na nimefanya maamuzi , mwanzoni sikutaka kuolewa lakini kwasababu tushafunga ndoa naamini tutakuwa na mwisho mzuri , sitaki yanayomkuta baba yangu kunikuta na mimi wala kuwa kama mama yangu ambaye ameishia kuwa mpweke…”Aliongea Regina na kauli ile ilimfanya Hamza kufurahi mno.
“Upo sahihi , kwanzia sasa hivi tunapaswa kufikiria mazuri yenye uelekeo mmoja”
“Umeongea ki usahihi hivyo naamini utaanza kufanya kazi kwa bidii na kupunguza uzembe , najua una koneksheni kubwa jambo ambalo ni zuri lakini hii ni Tanzania, nataka siku ambayo nikikubali watu wakujue kama mume wangu nijivunie kwa kile ambacho unafanya na sio kuongelewa vibaya na watu”
Hamza alielewa alichokuwa akimaanisha Regina na aliishia kukuna kichwa na hakujali kabisa msisitizo wa huyo mwanamke.
“Regina wewe mwenyewe unanijua vizuri , kwasasa nasoma lakini mpango wangu nikimaliza hata nisiwe na cha kufanya ili mradi niwe na hela ya chakula basi , sitojali watu wanachoniongelea”
“Sawa unaweza usijali lakini vipi kuhusu mimi, siwezi kuwa na mwanaume ambae hana malengo wala ndoto za kukamilisha , wanaume ambao hawana malengo wanachukiza zaidi ya wanaume wachepukaji”
Regina alikuwa siriasi , alionekana hakuwa akitania hata kidogo , alithamini sana Career yake hivyo alihitaji mtu ambae atakuwa sambamba nae.,
“Vipi kuhusu Eliza sasa , unaweza kukubali niendelee nae bila kuleta shida?”
“Inamaana hukuelewa pointi yangu au unajitoa ufahamu?”Aliongea huku hasira zikianza kumvaa.
"Hivi kwenye kichwa chako wewe malengo yako ni wanawake na sio kitu kingine , wanaume wengi wa umri wako wanafikiria namna ya kutengeneza pesa , kuanzisha biashara na kufanya kazi kwa bidii , ukiachana na wanawake ni kitu kipi kingine unataka kufanya au kukamilisha kwenye maisha yako?”Aliongea Regina akiwa siriasi.
“Kufanya kazi kwa bidii na kupata hela sio malengo yangu kwasasa naona ni kama kujishughulisha tu , kama ni hela tunazo za kutosha , kwani unataka kuwa na shilingi ngapi ili uridhike?”
“Unakwepa majukumu yako, hela zangu sio zetu , halafu wewe si ndio jana ulisema mwanaume anapaswa kujua kuwajibika , kwahjio kutofanya chochote na kupoteza muda ndio unaita uwajibikaji?”
“Regina kwanini unaweka vigezo vikubwa hivyo, mimi nipo mwaka wa mwisho chuo na sasa hivi umenipa kazi kama mfanyakazi wako wakati wewe ukiwa ndio CEO , kazi zote ninazopewa kufanyia kazi nazifanya kwa usahihi na nazidi kuwa bora siku hadi siku , nimeweza kushinda tuzo kwa ajili ya kampuni na mengineyo , kipi kingine napaswa kufanya?”
“Ninachomaanisha sitaki mwanaume anaeridhika na kitu kidogo au wewe unadhani hela ulizopata zinakutosha kabisa?”Aliuliza na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la uchungu.
“Labda ndio zinanitosha , nimepitia mengi mpaka kufika hapa na malengo yangu ni kuishi maisha ya amani na utulivu na kuwa na furaha”
“Umepitia mengi!, unamaanisha kuua watu?, mimi nataka kujua ni mafanikio gani umefanikisha , kama ni kupitia mengi kila mtu anapitia hayo mengi , wewe baada ya kupitia mengi mafanikio yako ni yapi?”
“Sijasema mafanikio yangu ni kuua watu na sio kweli kama nimeaua watu?”
“Kama sio hivyo ni mafanikio gani unayo?”Hamza alijikuta akishindwa kujibu swali lile.
Mwingine angeona Regina ana masharti makubwa lakini ukweli ni kwamba alikuwa ni bosi wa kampuni kubwa ambayo imeorodhshwa katika masoko makubwa ya hisa dunani , kama ataolewa inamaanisha na mume wake atakuwa katika rada za watu.
“Najua unashindwa kuongea , wewe ni mwanaume usie na malengo na uliepoteza tumaini , nenda kapoteze muda huko unakoenda , mimi naenda kazini”Aliongea na kisha kwa hasira alishika mkoba wake na kutokomea nje.
Hamza aliishia kuvuta pumzi tu na hakuongea chochote , sio kwamba hakuwa na mafanikio , alikuwa nayo lakini hayakuwa yakielezeka.
Yeye alijichukulia kama mtu ambae ameishuhudia Tsunami tayari na hawezi kuogopeshwa na mawimbi madogo madogo.
Lakini hata hivyo alijiambia sio muda sahihi wa kumwambia Regina chochote , isitoshe licha ya kwamba ni kweli alitamani maisha ya amani ambayo hayana usumbufu , lakini vilevile alikuja Tanzania kwa lengo moja tu , lengo la kumfahamu Mzee ni nani.
Siku zote wanawake wanajivunia kuwa na mwanaume ambae ana mafanikio kumzidi , hilo Hamza alielewa lakini aliona sio muda sahihi wa kumuonyesha chochote Regina, isitoshe sio yeye tu kama sehemu ya familia yake.
Kwasababu alikuwa na mzunguko mrefu hakuchelewa kuondoka nyumbani na hakutoka na gari bali aliona atumie usafiri wa uma , isitoshe Regina alimnanga vya kutosha hivyo hakutaka kushobokea magari yake.
Ilimchukua dakika kama arobaini hivi kufika Madale kwa ajili ya kuonana na Frida.
Na baada ya kugonga ni Frida ambae alitoka kuja kumfungulia mlango .
“Mlinzi wako leo hayupo?”Aliuliza Hamza.
“Kwasasa sina mlinzi, uliemkuta kipindi kile amerudi nyumbani kwao Singida”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa.
Frida alikuwa mwanamke mrembo lakini Hamza aliweza kuona mabadiliko Frida alionekana kupungua mwili.
“Naona umepungua mwili , ndio kutokana na adhabu nini?”Aliuliza Hamza maana alijua mara ya mwisho wakati alipoongea na Frida alimwambia alikuwa akienda kuhojiwa.
Kitendo cha Frida kumsikia Hamza akimwambia amekonda alijisikia faraja , japo ukweli ni kwamba sababu za kukonda ni juu ya kazi yake na misheni yake kwa Hamza.
“Niliweza kutoka bila ya kupatiwa adhabu ndio maana nimewahi”Aliongea huku akimkaribisha ndani.
Eneo la sebuleni kulikuwa na makatarasi kibao pamoja na vitabu , ilionekana mwanamke huyo alikuwa bize kusoma kama sio kuandaa ripoti.
“Oh !, nilikuwa bize kidogo na ripoti ndio maana unaona makaratasi mengi”Aliongea.
“Wana taaluma hamjawahi kupumzika, kila saa mpo na mavitabu mnasoma na kufanya uchambuzi”
“Watafiti wa kisayansi hawajawahi kupata usingizi kwa muda mrefu , hata wakati wakulala tunawaza kile kilichokwama, ukiachana na kutambulika kutokana na kukamilisha kitu kikubwa lakini haya yote tunafanya kwa ajili ya faida ya dunia”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha kichwa kumwelewa.
“Nina safari ya Morogoro , hivyo sitaki kukaa hapa muda mrefu”Aliongea Hamza.
“Ukweli ni kwamba nilitaka kukutafuta pia leo tuonane kama nilivyokuambia kwenye simu , nianze mimi au uanze wewe kuongea sababu ya kutaka kuonana?” Aliongea Frida.
“Nitaanza mimi”Aliongea Hamza na Frida alitingisha kichwa akimpa ishara ya kuongea.
“Kilichonileta ni swali moja tu , wakati unanipatia ule mshumaa ulisema umetoka kwa Dokta Genesha na kazi yake ni kuamsha ndoto, je una kazi zaidi ya kuamsha ndoto?”Aliuliza Hamza na swali lile kidogo lilionekana kumshitua Frida lakini alijizuia.
“Kwanini unaongea hivyo , kuna kitu kingine ambacho kimekutokea kwasabu ya Mshumaa?”
“Hakuina kilichonitokea , ukweli ni kwamba sijawahi kuutumia tokea unipatie , ila katika kipindi chote nimekuwa nikipatwa na ndoto kama kawaida, kama mshumaa ni wa kuamsha ndoto na naota bila ya kutumia mshumaa kuna haja ya kuutumia?”Aliuliza Hamza na swali lake lilimfanya Frida kupumua kwa ahueni.
“Unachokiona kupitia ndoto sio ndoto kama ndoto bali ni uhalisia wa kumbukumbu zako, kuna kitu nilisahu kukuambia kuhusu mshumaa , licha ya kwamba ni kweli kazi yake ni kuamsha ndoto lakini pia ni kuifanya akili yake isichukulie kile ambacho unakiota kama ndoto”Aliongea na kumfanya Hamza sura kuchekza kidogo .
“”Unamaanisha nini?”
“Umesema unaonta ndoto kama kawaida, kama umeota zaidi ya mara mbili au mara tatu lazima kuna tofauti ambayo umeweza kuona?”Aliongea Frida na kumfanya Hamnza kushangaa.
“Umnejuaje kuna tofauti?”
“Umesahau mimi ni mwanafunzi wa Dokta Genesha, ukiachana na Profesa Frola rafiki yako”Aliongea na kumfanya Hamza kukunja ndita.
“Unamfahamu Dr Ronicas kama mwanafunzi wa Dokta Genesha?”
“Kila mtu anamfahamu Dr Ronicas , najua pia alikuwa hapa nchini Tanzania , wakati nikiwa kama Ajent miaka saba iliopita niliweza kumfahamu Dr Ronicas lakini ni kupitia maandishi tu”.Aliongea na Hamza hakushangaa sana maana mzunguko wa Dokta Genesha haukuwa wa kawaida.
“Licha ya kwamba ndoto zote utakazoota una husika moja kwa moja wakati wa matukio lakini utofauti unakuja pale ambapo unaota lakini hujui unaota na muda mwingine utakuwa unaota huku ukijua kabisa unaota”Aliongea Frida na kumfanya Hamza kutngisha kichwa.
“Upo sahihi mara ya kwanza niliota bila kujua naota , lakini jana nimeota huku akili yangu ikiniambia nipo ndotoni”
“Ndoto unayoota unajiona kuwa na sura ya tofauti si ndio?”Aliuliza .
“Hivi nilikusimulia , mbona ni kama unajua kila ninachoota?”Aliuliza Hamza na kumfanya Frida kutabasamu.
“Kwasababu wewe ni mteja wangu wa tano”
“Unamaanisha kuna watu wanaota kama ninavyoota mimi?”
“Ndio wapo licha ya kwamba kuna utofauti lakini wote wanaota wakiwa na sura tofauti , ni kama wamezaliwa katika miili mingine kwenye ndoto zao , utofauti ni kwamba kwa maelezo ya Dokta Genesha wewe ndoto zako zina upekee”
“Upekee! Unamaanisha nini ?”
“Sina maelezo ya kutosha, ninachojua unachoota ni kitu cha kipekee ambacho kitakufanya kutafsiri Lugha iliowashinda binadamu kutafsiri”Aliongea na Hamza alikuwa akielewa Frida alikuwa akimaanisha nini kuhusu lugha.
“Kwahio ni ipi sahihi , kuota nikiwa najua naota ama kuota nikiwa sijui naota?”.
“Swali lako nikilirudia naweza kuliweka hivi , je ni ndoto ya aina ipi unaweza kusahau haraka, kati ya ndoto ambayo unajjihisi unahusika moja kwa moja au ndoto ambayo unajua unaota?, jibu la swali hili kitaalamu ni kwamba ndoto ya kawaida ambayo hujui unaota ndio ambayo haisahauliki haraka , lakini kwa swala lako wewe ndoto yako sio kama ndoto zingine , ubongo wako sio wenye kutengeneza matukio ambayo unaona kama msingi mkuu wa ndoto bali unachoota ni koneksheni ya kimawasiliano baina ya Dimension mbili tofauti hivyo kwa swala hili unapaswa kujua unaota lakini pia uwe na uwezo wa kukatisha ndoto muda wowote”Aliongea Frida.
“Kwa kukuelewesha kwa urahisi wakati ukiwa ndotoni si unajua unaota, lakini ghafla ukakutana na tukio la kutisha na kutamani ndoto iishie palepale na ikaisha hapo utakuwa umefanikiwa , kati ya wagonja wangu ambao nishawahi kupata wengi walikuja kwasababu wanaota vitu vya ajabu ambavyo vinawafanya kushindwa kulala,hakuna dawa ya kumpa mtu kuzuia ndoto bali namtengenezea mazingira ya kuifunga ile ndoto na njia pekee ni kumfanya aote wakati akijua anaota kwa njia ya hypnosis”
“Kwahio napaswa kutumia mshumaa kama njia ya kunifanya niote wakati nikiwa naota si ndio?”
“Ndio , unapaswa kuota wakati ukijua unaota na wakati huo hisia zako zote zikiwa katika ndoto , hata baada ya ndoto isitokee ukasahau kitu chochote kile ambacho unaota , kama nilivyosema unaota ukiwa umetawala mwili mwingine, lakni nafsi ya mwili huo bado inafanya kazi, mshumaa wa nuru utakusaidia kuwa na uwezo wa kutumia akili yako na ya mtu ulietawala mwili wake kwa wakati mmoja na kila unachoota hakitasahaulika hata baada ya ndoto”Aliongea Frida.
“Kwahio unaamini kwamba kupitia hii ndoto nitaweza kutafsiri kitabu alichoniachia Dokta Genesha”
“Ndio kwasababu kupitia hio ndoto utajifunza lugha mpya ambayo hukuwahi kuijua hapo kabla na itaendana na lugha ambayo binadamu tumeshindwa kuitafsiri”
“Kuna uhakika gani kwamba nitaweza kujifunza lugha mpya na je ninachoota mnajuaje kama ni sahihi au ni ndoto tu ambazo hazina mpangilio”Aliongea Frida na kumfanya Frida kutabasamu kidogo .
“”Nadhani ni muda wa kukuambia na mimi kwanini nilitaka kuonana na wewe . ndio njia rahisi ya kujibu swali lako”Aliongea Frida na kisha alimwambia Hamza asubiri anarudi.
Dakika moja tu alitoka chumbani akiwa ameshikilia picha na kumpatia Hamza.
“Hii ni picha ambayo aliniambia nikupatie Dokta , huwezi kuita picha ni kwasababu ni mchoro tu lakini nadhani umebeba maana ambayo utaweza kuitambua”Aliongea Frida na Hamza aliingalia ile picha na macho yake yalichanua .
“Red moon!!”Aliongea Hamza akimaanisha mwezi mwekundu.
Comments