“Kazi yangu nyingine , kwanini ghafla tu unaniuliza kitu kama hicho?”
“Najua utadanganya lakini nimesikia taarifa unafanya kazi chini ya mtandao wa kihalifu wa Chatu”Aliongea Prisila na pale sasa Hamza alielewa ni kipi kilikuwa kikimfanya mrembo huyo kuwa na wasiwasi.
“Unaujuaje mtandao wa Chatu?”Aliuliza Hamza.
“Niambie ukweli kama unafanya kazi kwenye mtandao huo au hapana , napatwa na wasiwasi maana mimi ndio nimekukutanisha na bosi Regina”Aliongea .
“Prisila huna haja ya kuwa na wasiwasi hivyo , sio kama unavyofikiria ni kwamba tu nina ukaribu na bosi wa huo mtandao lakini haimaanishi kama nafanya hizo kazi , lakini pia huo mtandao sio wa kihalifu kama unavyofikiria wewe”Aliongea Hamza.
“Najua habari juu za huo mtandao na imekuwa moja ya topiki kwenye kampeni za viongozi wa chama cha wapinzani, najua pia kiongozi unaemzungumzia una ukaribu nae ni Dina , mwanamke Smrembo, kwahio wewe ndio mpenzi wake ndio maana mnafanya kazi pamoja?”Aliuliza na kumfanya Hamza asijue acheke ama alie.
“Nani kakuambia hayo yote”
“Nime mfollow Instagram ana wafuasi kibao , wengi wanamjuia japo haijulikani kama ndio mmiliki wa mtandao wa Chatu, baada ya kusikia una ukaribu nae nikajua moja kwa moja mnafanya wote kazi , wasiwasi wangu sio wewe kufanya kwake kazi maana siwezi kukupangia , kama yanayozungumzwa ni sahihi basi hupaswi kuwa karibu na Bosi Regina, chochote kitakachomtokea mimi ndio nitalaumiwa kwa kutokuwa makini”Aliongea huku akionekana kuwa siraisi.
Hamza hakujua nini Prisila aliambiwa na nani lakini alijua kwa mwanamke kama huyo anajali sana kitu kinachoitwa sheria.
“Unaonaje tukifika Dar twende wote ukajionee mwenyewe na ndio utajua kwanini nashirikiana nao”Aliongea Hamza , aliona ndio namna pekee ya kuondoa wasiwasi wa Prisila na mambo mengine yaendelee.
“Wewe niamini mimi tufika twende wote?”Aliongea Hamza mara baada ya kuona Prisila anasita na kutokana na msisitizo wa Hamza Prisila aliamua kukubali, hata hivyo aliona kama Hamza ni mhalifu kwanini atoe kiasi chote kile cha pesa kwa ajili ya kusaidia watoto Yatima, ukweli ni kwamba tokea aambiwe juu ya hilo swala alikuwa na wasiwasi na alitamani kumwambia Regina lakini aliona ni busara kuongea na Hamza kwanza.
Baada ya masaa mawili kupita hatimae waliweza kufika mjini Dar es salaam na Hamza alinyoosha moja kwa moja mpaka Kijichi unapopatikana mgahawa wa chai wa Dina.
Hamza mara baada ya kusimamisha gari alishuka na Prisila na kuingia ndani na mhudumu alivyomuona Hamza alitingisha kichwa kumkaribisha kwa adabu.
Muda huo waliweza kusogelewa na Lawrence ambae alionekana kuwa na haraka.
“Bro karibu sana ila Madam ameenda kwenye kikao tokea asubuhi ila naamini atawahi kurudi”Aliongea Lawrence na kumfanya Hamza kushangaa kidogo.
“Kwenye kikao?!”
“Ndio , ni juu ya lile swala la usiku ule”Aliongea Lawrence na kumfanya Hamza kuelewa.
“Hii sehemu nilikuwa napita tu , sijawahi kuelewa wanachouza hapa”
“Wanauza Chai”
“Sehemu kubwa hivi wanauza chai tu?”
“Sio chai ya kawaida Prisila, ni chai inayotumia aina nyingi ya mimea , ushawahi kusisikia Gisaeng tea?”Aliuliza Hamza akiamini Prisila atakuwa anaangalia filamu za kikorea.
“Ndio nishawahi kuona kwenye filamu wakorea wanashabikia, unasema na hapa wanauza!!?”
“Sio Gisaeng tu , hapa wanauza kila aina ya chai maarufu zote duniani ikiwemo Panda Dung kutoka China , Gyokoro , Yellow Gold na aina nyingine nyingi za chai”Aliongea na kumfanya Prisila kushangaa na alishangaa baada ya kuona kuna wateja wengi tu wakionekana kufurahia chai.
Hawakuchukua muda mrefu kuwa peke yao Dina aliweza kurejea na alishangaa kumuona Hamza akiwa na mwanamke mwingine , tena mrembo.
Upande wa Prisila pia alishangaa kumuona Dina kwa urembo wake , ijapokuwa Prisila alikuwa amemzidi Dina lakini muda huo mwonekano wa kujiamini wa Dina umemfanya kuona amezidiwa vitu vingi.
“Hamza huyu msichana mrembo ni nani , mbona hunitambulishi?”Aliongea Dina huku akiwa na wasiwasi.
“Huyu anaitwa Prisila ni mfanyakazi mwenzangu lakini vilevile nimegundua leo ni rafiki yangu wa utotoni”Aliongea Hamza na kauli ile ilimfanya Dina kujiona mdogo mbele ya Prisila maana licha ya kwamba alikuwa amevalia mavazi ya kawaida lakini alikuwa ni mrembo haswa.
“Hello ! Naitwa Dinaq , ndio bosi wa hapa”Aliongea.
“Nimefurahi kukuahamu Dina”Aliongea Prisila huku akimpatia mkono lakini alionyesha hali ya wasiwasi.
“Prisila unaonaje sasa , huyu Dina unaemuona anafanana na mtu mhalifu?”Aliuliza Hamza lakini upande wa Prisila ni kama alianza kukosa utulivu , ukweli ni kwamba alikuwa akizidi kujiuliza inakuwaje Hamza anakutana mara kwa mara na wanawake warembo warembo na wote wanaonekana kana kwamba wanampenda.
Dina mara baada ya kusikia kauli ya Hamza ni kama sasa alielewa kwanini amekuija na mrembo huyo hivyo alichukua nafasi ya kujielezea.
“Prisila , ijapokuwa kwa nje tunaweza kuonekana kama wahalifu lakini biashara zetu hazihusiani na maswala ya kihalifu, tofauti ya biashara zangu na za kawaida ni kwamba tunamalizana na wateja wetu kibiashara bila kuhusisha sheria”Aliongea.
Prisila alimwangalia Dina kwa wasiwasi , lakini tabasamu la Dina lilimfanya kushindwa kujizuia kumuamini.
“Ni kweli?”Aliuliza.
“Unadhani nakudanganya, kama kweli sisi ni wahalifu unadhani ingekuwa rahisi kwa serikali kutuangalia tu bila kuchukua hatua yoyote , ijapokuwa wapo wengi wanaotusemea mabaya kama wahalifu lakini tunacheza nafasi kubwa ya usalama ndani ya nchi hii, kama huniamini mimi unaweza kumuamini Hamza , unadhani ni mtu mbaya ukimwangalia?”Aliuliza Dina na kauli yake ilimfanya Prisila kukumbuka Hamza muda mchache uliopita alikuwa ametoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya watoto yatima, tena wakati ambao kituo hicho kilikuwa kikihitaji msaada kwa kuwa nje ya bajeti.
Walikuwepo matajiri wengi ambao walikuwa na uwezo wa kuchangia zaidi ya milioni mia tisa lakini wengi wao michango yao haizidi hata milioni mia nne , isitoshe kwa mwonekano wa Hamza alionekana kama mtu ambae anauhitaji wa hela , kama sio hivyo kwanini akubali kuajiriwa na Regina kwa ajli ya mshahara wa laki saba .
Baaada ya kufikiria hayo yote aliona wasiwasi wake ulikuw bure tu na hakupaswa kumshuku hata kidogo.
Dakika ile ile ni kama sasa ndio anaanza kumuona Hamza kama rafiki yake wa utotoni ambae alikutana nae kituoni ,ile furaha ya kumjua Hamza kama mtu aliepotezana nae ilianza kuchipua.
“Hamza Sorry kwa kukushuku , ningejua nisingemsikiliza Lea na ujinga wake, wote mnaonekana kuwa watu wazuri”Aliongea Prisila.
“Lea ndio nani na kwanini akuambie mambo yangu ?”Aliuliza Hamza akiwa amekunja sura.
“Lea ni jirani yetu na ni kama rafiki yangu wa muda mrefu , alikuja nyumbani na kuniambia alikuwa Tanganyika Club na aliwaona wewe na Dina mkiwa pamoja , amesema wewe ni mhalifu hivyo nichukue tahadhari”Aliongea na kumfanya Hamza kumgeukia Dina.
“Ile siku kulikuwa na mwanamke yoyote alieitwa Leah?”Aliuliza.
“Sijasikia jina la Leah , halafu ile siku ilikuwa ni tofauti na watu wanazopendelea kuja kuchukua mazoezi hivyo hatukutana na watu wengi”Aliongea Dina .
“Prisila nadhani umejionea mwenyewe licha ya kwamba ni kweli Chatu inachukuliwa kama mtandao wa kihalifu , sio swala la kumfanya mtu awe na aibu kama sheria zinafuatwa hivyo usiwe na wasiwasi sasa”Aliongea na kumfanya Prisila mzigo wa wasiwasi kuutua
Maana swala hilo lilikuwa likimuumiza kichwa sana , kama mwajiri aliona amemwingiza bosi wake kwenye hatari na kutafuta namna ya kumuondoa kwenye hatari lakini baada ya kuongea na Hamza na kuonyeshwa hali halisi wasiwasi ulimtoka.
“Haya yameisha sasa , Prisila unaonaje tukiwa dadaz , njoo nikuonjeshe radha ya chai tofauti tofauti”Aliongea Dina kwa furaha huku akiagiza chakula pia maana Hamza alikuwa na njaa.
Dakika chache mbele walijikuta washazoeana na kuanza kupiga soga na kucheka.
Prisila alijua vitu vingi sana kuhusu chai na faida zake mwilini na mwisho wa siku aliona ni kheri kunywa chai kama njia ya kujichangamsha kuliko mvinyo uliojaa pombe.
Dina alidhamiria kumfanya Prisila rafiki yake pengine ni kwasababu ya Hamza na ili kukazia alimwalika Prisila kwenda nae kwenye sherehe ya uzinduzi wa Albamu ya msanii maarufu , Dina alikuwa amealikwa hivyo alimchagua Prisila kwenda nae , kwasababu Prisila alikuwa akijua juu ya uzinduzi huo alikubali.
“Naona amani imerudi sasa maana ulikuwa ukiniangalia kwa wasiwasi mno?”Aliongea Hamza wakati akimsindikiza Dina kuelekea nyumbani.
“Wasiwasi wangu haukuwa wewe kufanya wapi kazi , wasiwasi wangu ulikuwa juu ya Regina na Kampuni”
“Unamjali sana Regina , sijui kama na yeye anakujali kama unavyomjali?”
“Sina mashaka kabisa na Regina , alivyosiriasi utadhania hajali lakini ukimiuona anaweka hisia zake wazi kukuonyesha kujali huwa inagusa sana , nimekuwa nae namjua vizuri”Aliongea na Hamza hata yeye alijua hilo maana hata Eliza aliongea.
“Vipi yule mtoto mwenye mashavu kule Morogoro niliekutana nae miaka zaidi ya ishirini iliopita?”Aliuliza Hamza na kumfanya Prisila kuona aibu ilionekana udhaifu wake ni kuambiwa alikuwa na mashavu makubwa akiwa mdogo.
“Wakati nikiwa mtoto nilitelekezwa na mama kule kituoni kwa Baba Hizza na sikuwahi kumuona mpaka leo”Aliongea Prisila na kauli ile ilimshangaza na kumgusa Hamza.
“Mama yako alikuacha kule kituoni , ilikuwaje?”
“Ni stori ndefu ila nikipindi ambacho baba alikuwa nje ya nchi kwenye mafunzo ya kijeshi , mama alionekana kutompenda baba , pengine ilikuwa ni kutokana na kusafiri safiri kwake ndio maana alipoteza hisia na baba mpaka akaamua kunitelekeza kituoni , Baba Hizza ni ndugu wa baba upande wa bibi , baada ya baba kurudi nchini ndio aliambiwa nipo kituoni na kuja kunichukua”
“Na mama yako sasa hivi yupo wapi?”
“Mama sijui alipo mpaka sasa , ila tetesi zinasema itakuwa anaishi nje ya nchi maana alikuwa na mahusiano ya siri na mtalii, sijui labda baba anajua anapoishi ila sijawahi kumuuliza”Aliongea na kumfanya Hamza kumuonea huruma.
Kila mwanamke aliekuwa nae alikuwa na matatizo upande wa mama lakini ilionekana Prisila alikuwa na uchungu zaidi , kutelekezwa lazima itakuwa anajihisi mama yake hakumpenda.
Hamza wakati akifikiria namna ya kumfariji muda huo wakiwa mkabala na chuo cha TIA walisimamishwa na Traffic.
Dakika hio hio baada ya Hamza kusimamisha gari pembeni, gari mbili ziliongezeka kutoka nyuma yao na mbele yao moja kati ya hizo ikiwa ni Diffenda ya kijeshi jambo ambalo lilimfanya akunje sura na kujiambia kumekucha.
Wapita njia pia walivutiwa maana ni mara chache sana kuona jeshi la ulinzi kuzingira gari mbele na nyuma kama kwamba wanakamata mhalifu maana wengi walizoea kazi hio hufanywa na jeshi la polisi.
Muda ule mlango wa gari aina ya Jeep ulifunguliwa na alitoka mwanajeshi alievalia kombati za jeshi , alikuwa ni Afande Mdudu akitanguliwa na wanajeshi wengine na wote walizingira gari ya Hamza huku wakimwamrisha atoke.
Prisila alijikuta akitetemeka mno kutokana na tukio lile na alimwangalia Hamza na kushangaa alikuwa katika hali ya utulivu.
“Hamza nini kinaendelea?” Mrembo huyo aliuliza huku akiamini pengine ni kutokana na Hamza kujihusisha na mtandao wa kihalifu.
“Prisila usiwe na wasiwasi najua wanachotaka ngoja nitoke wewe utatangulia nyumbani tutawasiliana”Aliongea Hamza lakini kauli yake haikutosha kumtoa Prisila kwenye wasiwasi na Hamza baada ya kutoka na yeye alitoka.
“Afande Mdudu nini tena tatizo?”Aliuliza Hamza mara baada ya kutoka nje ya gari.
“Hamza Mzee , Naitwa Meja Mdudu , kapteni kikosi namba mbili kitengo cha usalama wa nchi , rasmi kwanzia sasa hivi upo chini ya ulinzi kwa tuhuma za mauaji , kusababisha Ghasia na Utekaji”
Baada ya kuongea hivyo alitoa nyaraka na kumuonyeshea Hamza mbele yake, ilionekana kweli ni nyaraka ya kukamawa kwake iliosainiwa na wakubwa.
Hamza macho yake yalisinyaa , ilionekana hawa wanajeshi walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu na hawakutaka kumkamata mbele ya Dina wakijua kuna uwezekano angemkingia kifua ndio maana wakamuwekea mtego wa kumkamatia njiani.
Japo Hamza hakupenda kukamatwa mbele ya kadamnasi ya watu na mbele ya Prisila ambae ndio kwanza anatoka kumtoa hofu ili aendelee kumuamini lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kutii shuruti.
“Naona mnaniwinda sana kama mizimu”Aliongea na kumfanya Afande Mdudu kucheka kwa furaha.
“Unadhani nilikuwa nikikuogopa , kabla ya kuwa mwanajeshi mimi ni raia wa hii nchi na kabla ya kuchukua hatua lazima niwe na ushahidi wa kisheria , kwa mtu hatari kama wewe ushahidi wa uhalifu wako ninao hivyo ninakukamata”
“Kwahio unajiona raia unaetii sheria , lakini sio wewe juzi ulietaka kumfosi mwanamke kwenda kumuoa , na hio pia ni sheria ya hii nchi?”Aliuliza Hamza na kumfanya Kamanda kunywea
“Haina haja ya kubadilisha topiki , nipo hapa kikazi na sina muda wa kuongea ujinga na wewe , kama unajua kuwa mtii na tuondoke pamoja”Aliongea Kamanda Mdudu maana alijua kama Hamza akitaka kuwakimbia wanaweza wasimzuie , lakini mbele ya mwanamke kama Prisila walijua ndio njia rahisi ya kumkamata na kumfanya atii shuruti , ulikuwa ni mpango.
Hamza aliishia kutoa tabasamu la uchungu na aliona Mdudu alikuwa na akili kidogo kwa kutaka kumkamatia mbele ya Prisila.
“Hamza..!!”
Prisila alitaka kuongea neno lakini jicho alilokatwa na wanajeshi hao lilimfanya kukosa nguvu ya kujiamini.
“Sikia Prisila usiwe na wasiwasi na usifikirie mbali, nitakupigia simu hili likishaisha nakuhakikishia sijafanya kosa lolote hivyo hawatonifana chochote”
“Mhalifu hebu acha majigambo kujsafisha mbele ya mwanamke uwe umefanya au hujafanya sisi ndio tunajua”Aliongea Mdudu
Kwa jinsi wajeda hao walivyokuwa siriasi Hamza aliamua kutii amri na alimwangalia Prisila kwa macho ya wasiwasi.
“Nitakupigia simu , nakuahidi nitakupeleka kwenye sherehe aliokuwahidi Dina mimi mwenyewe”Aliongea Hamza.
“Hio ni ahadi??”
“Ndio ni ahadi , hivyo acha wasiwasi”Aliongea Hamza na kishingo upande Prisila alikubali na kumfanya Hamza kuvuta pumzi.
Mdudu palepale alitoa ishara kwa mwanajeshi mwenzake na Hamza alaivishwa pingu na kuingizwa ndani ya gari na kuondolewa kwa spidi kuelekea mjini”
Comments