Hamza mara baada ya kuingia eneo la sebuleni aliweza kumuona Yulia alievalia blazia ya rangi nyeupe na jeans ya rangi ya bluu bahari na Regina upande wake alikuwa amevalia gauni la rangi ya bluu na visendo manyoya, wote walikuwa wamekaa ki upande upande kwenye masofa.
Kwa mwanaume yoyote angeburudishwa na muonekano wa warembo hao wawili , maana licha ya kuwa na rangi tofauti lakini walikuwa wakivutia macho mno.
Lakini upande wa Hamza ilikuwa akifikiria tofauti muda huo , kitendo cha kuwaona wanawake hao wamekaa sehemu moja aliona kuna kitu ambacho hakipo sawa.
Muda ule Yulia mara baada ya kumona Hamza akiingia uso wake ulipambwa na tabasamu mwanzoni na kugeuka kuwa hali ya mshangao kana kwamba ni mtu ambae hakutarajia kumuona hapo.
“Hamza unafanya nini hapa?”Aliuliza Yulia huku akishangaa.
Regina mara baada ya kusikia Yulia anamwita Hamza macho yake yalijawa na mshangao pia , alionekana kushangaa Yulia kumfahamu Hamza.
“Na wewe unafanya nini hapa?”Aliuliza Hamza huku akikunja ndita.
“Nimetoka kumtembelea leo Bi Mirium ni mfanyabiashara ambae namuheshimu , nafahamiana pia na Regina ndio maana nimekuja kumsalimia”Aliongea Yulia akiwa na utulivu.
“Yulia unafahamiana na Hamza?”Aliuliza Regina na Hamza alitaka kujibu hilo swali haraka lakini Yulia alimuwahi.
“Namjua ndio , nimekutana nae miaka saba iliopita nikiwa nje ya nchi na ndio alieniokoa kwenye mikono ya watekaji , siku kadhaa zilizopita nilikutana nae hapa Dar , kukutana kwetu kumenifanya nione imepangwa tuje kuonana tena”Aliongea huku akiwa na tabasamu zito.
Regina alikuwa akijua swala la wazazi wa Yulia kupoteza maisha wakiwa nje ya nchi baada ya kutekwa na katika tukio hilo aliesalia alikuwa ni Yulia pekee yake , sasa hakujua kwamba tukio la kipindi kile Hamza alihusika kwa kumsaidia mwanamke mrembo kama Yulia.
Isitoshe pia pengine wakati huo Yulia alimchukulia Hamza kama raia wa nje ya nchi, hivyo kukutana nae nyumbani hapa Tanzania lazima kuwe na hisia tofauti zilizojijenga kwake kama mwanamke , maana sio rahisi kupata msaada kwenye ardhi ya ugenini.
“Mbona hujawahi kuniambia?”Aliuliza Regina huku akimwangalia Hamza.
“Nilisahau ndio maana , kwangu halikuwa tukio kubwa sana kiviile ndio maana sikuona haja ya kuliweka wazi”Aliongea Hamza huku akilazimisha tabasamu.
“Tukio la namna hio unaliita dogo! , huwa najiuliza ni tukio lipi ni kubwa kwako?”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kumeza mate huku akiona aibu kidogo baada ya kuhisi kuna zaidi ya maana kwenye kauli ya Regina
“Regina unafahamiana vipi na Hamza ni rafiki yako au?”Aliuliza Yulia na kwa namna ambavyo alikuwa mpole utadhani ni mpole kweli kumbe ni mtukutu.
Regina aliishia kudharau ndani kwa ndani kwenye moyo wake , alikuwa na akili sana , ijapokuwa kihisia alikuwa slow haikumaanisha hakuwa akijua kinanachoendelea kwa Yulia.
Isitoshe Yulia hata yeye alikuwa na cheo kama chake ijapokuwa Yulia alitambulika kama Managing Director(MD) , yaani Mkurugenzi mtendaji na Regina kama Chief exucutive officer(CEO) yaani Afisa Mtendaji mkuu lakini wote ni wafanyabiashara wenye vyeo vinavyolingana kimajukumu kwa kiasi flani ndani ya kampuni wanazoongoza.
Ukweli ni kwamba mwanzoni Regina alikuwa akijiuliza kwanini Yulia Mkurugenzi wa makampuni ya Prima Tanzania kumtembelea hospitalini bibi yake na hata kuja nyumbani kwa ajili ya kumpa faraja.
Lakini baada ya ujio wa Hamza na namna ambavyo alikuwa akiongea ilimpa nafasi Regina ya kujua nia yake halisi ni ipi , alijua yote aliofanya Yulia ilikuwa kisingizio tu cha kutaka kumuona Hamza.
Katika moyo wa Regina alianza kushikwa na hali ya kupaniki , hakujua ni kwanini lakini alikuwa na wasiwasi Hamza anaweza kuwa na uhusiano wa ndani kabisa na Yulia.
Kama ingekuwa ni mwanamke mwingine pengine asingejisikia hivyo lakini Yulia , ukiachana na kwamba amemzidi kimwonekano na yeye kuwa na umri mdogo ,lakini hakuwa na kitu kingine cha ziada cha kujivunia , kwa ufupi ni kwamba alikuwa akijihisi amekutana na mtu anaeweza kumletea ushindani , ndio hisia alizokuwa akijisikia muda huo.
Muda uleule Regina alikumbuka maneno ya bibi yake akimuonya juu ya kutoruhusu Hamza kuondoka kwenye maisha yake na kuhakikisha kumbakisha hata kama ni kwa kumuigizia , maneno yale ni kama sasa yametoka kwa bibi yake na yanaanza kutafuta nafasi katika moyo wake na kujiambia kwa vyovyote vile hawezi kumuacha Hamza kwenda kwingine.
Sasa Regina anaanza kuelewa nini amabcho bibi yake alikuwa akilenga , kama Yulia alikuwa anafanya juhudi za namna hio kwa ajili ya kumkaribia Hamza hata kwa kujifanyisha mkarimu kwao basi ni mtu ambae ana kitu.
Mrembo huyo ni kama alianza kuchanganyikiwa , hakujua kama moyo wake ulikuwa ukitaka Hamza abaki kutokana na thamani ambayo inaweza kuwa mchangao kwake au moyo wake na hisia zake ndio vilivyokuwa vikimtaka Hamza kubakia upande wake.
Lakini kwa muda huo hakutaka kujali ni hisia gani ilikuwa kweli na ipi ni uongo, maamuzi ni kwamba Hamza hapaswi kuondoka kwenye maisha yake anapaswa kummiliki hata isiwe kimapenzi, kwanza tayari alikuwa na pete ya ukoo.
‘”Umekosea sisi sio marafiki Yulia”Aliongea Regina na kumfanya Yulia kushangaa kidogo.
“Oh! , kama sio marafiki ni bodigadi wako au Houseboy?”
Baada ya Yulia kuuliza vile, Regina alitoka kwenye Sofa na kusogea upande aliopo Hamza na kisha alipitisha mkono wake kwenye kiuno chake na kumwegamia.
“Hamza ni mume wangu”Aliongea.
Hamza alishitushwa na kauli hio na kumwangalia Regina kwa mshangao, ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia sauti ya upole na yenye heshima kutoka kwa Regina ikionyesha kweli walikuwa na mahusiano.
Sauti ya Regina ilifanya mapigo yake kwenda kwa kasi mno huku damu za kutosha zikimwagwa na moyo wake kushangilia kauli hio.
Regina hata yeye uso wake ulikuwa umepata moto kidogo lakini hakuwa amemuachia Hamza, muda huo alikuwa akimwangalia Yulia kwa namna ya kujivunia kuwa na mume kama Hamza na kumpa ishara kwamba hana nafasi na amechelewa.
“Sikujua kabisa kama CEO Regina ameolewa , kama ningejua ile siku tulivyokuwa kwenye gari tusing.. tusinge..” baada ya kufikia hatua hio alijifanyisha kuziba mdomo kama vile anajutia kutamka kauli hio.
“Regina naomba unisamehe , sijui nataka kuongea nini, nilikuwa najaribu kumaanisha kitu kingine…”
Regina aliishia kumwangalia Hamza , alikuwa na hasira ndani kwa ndani,huku akijiuliza inamanaa huyu mpuuzi tayari ashafanya kitu na Yulia.
“Siwezi kufikiria chochote kibaya , kwanza namwamini sana mume wangu , pia naijua tabia yako bosi Yulia”Aliongea Regina akimuwahi Hamza ambae alitaka kuanza kujitetea lakini hata hivyo asingeongea kile ambacho alimfanyia Yulia kule Bagamoyo.
Regina pia alijua huo sio muda wa kuanza kugombana, vinginevyo angempa Yulia ushindi, hivyo aliendelea kukazia.
“Honey utakuwa umechoka na mihangaiko ya siku, nenda kaoge na upumzike, muda umeenda”Aliongea Regina kwa namna ya kupembeleza.
Hamza alijiambia kama maneno ya Regina yangetokea moyoni basi angekuwa anajisikia ni kama anaogelea angani.
Lakini kwa wakati huo kwasababu alikuwa akijua anaigiziwa alianza kukosa utulivu na alichotaka kufanya ni kuondoka ndani ya hilo eneo haraka.
“Sawa Wife natangulia kwenda chumbani” Aliongea Hamza maana muda huo alijihisi kama ni kama Refa kwenye uwanja wa vita.
Regina aliishia kutoa tabasamu la kumkubalia kama vile alikuwa ni wanandoa wapya ambao wanatokea kula fungate.
Baada ya Hamza kuondoka ndani ya eneo hili hali ilirudi katika ukimya wake.
Yulia aliishia kushika shika nywele zale kimapozi ambazo siku hio hakuzisuka kama alivyozoeleka na kisha alisimama.
“Regina muda wangu wa kuondoka umewadia , naamini hotochukulia vibaya kilichotokea kati yangu na Hamza.”
“Wala usijali , najua hakuna kibaya kilichotokea , kwa cheo chako Yulia huwezi kujikosea heshima mbele ya mume wa mtu”Aliongea Regina akiwa na macho makavu.
Na kauli yake ile ilimfanya Yulia kumkazia Regina macho , muda huo ni kama wawili hao wanaonyeshana kwamba hakuna ambae yupo tayari kukubali kushindwa bali ni half time na raundi ya pili itaanza.
Yulia ndio aliekuwa wa kwanza kucheka kana kwamba kuna kitu ambacho amekumbuka.
“Regina , nadhani sasa naelewa kwanini umeamua kukubali kuolewa na Hamza, nikiri kwamba sikukujua vizuri lakini unaonekana kutokuwa mwanamke mwepesi”
Maneno yale yalimfanya Regina kidogo kuwa na wasiwasi lakini hakuuonyesha kwa macho.
“Asante kwa sifa , ila mimi najiona mwanamke wa kawaida tu ambae ni bosi kazini na mke nyumbani , najijua vizuri kuliko mtu yoyote yule, ukiachana na kuchukulia kama mfanyabiashara mzuri leo nimegundua upo vizuri pia kwenye maeneo mengine, nipo tayari kujifuza kutoka kwako”
“Oh kama nini vile?” Aliuliza na kumfanya Regina kuwa kimya kwa sekunde kadhaa.
“Kwa mfano Bosi Yulia unajua sana kuwa na shukrani kwa muda mrefu,nichukue nafasi hii kwa niaba ya mume wangu kukushukuru na na kukuombea siku zijazo usije kuingia kwenye mtatizo kama uliopitia”
“Nimefurahi kusikia hivyo , kwasababu Hamza anaishi hapa mjini naamini siku za usoni nitakapokuwa kwenye hatari hatokataa kunisaidia, naamini pia wakati huo Bosi Regina hutokataa kuniazima mume wako, najua ni ombi dogo ambalo huwezi kukataa, si kweli?”
Regina alijikuta akishindwa kujua namna hata ya kujibu , ilikuwani kama Yulia anamwambia muda sio mrefu ataingia kwenye matatizo na Hamza ndio mtu atakaekuja kumsaidia.
“Kuhusu hilo itategemea na tutakavyokubaliana na mume wangu”Aliongea Regina .
“Natanguliza shukrani zangu za dhati kwako Bosi Regina”
“Huna haja ya kunishukuru. Nadhani sina haja ya kukusindikiza, nakutakia Usiku Mwema” Aliongea Regina na Yulia alitoa tabasamu na kutoka nje.
Baada ya Regina kuhakikisha ameondoka na gari yake kwanza alisita kidogo lakini alirudi ndani na kupandisha mpaka juu na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha Hamza.
Dakika ambayo alitaka kugonga Hamza alikuwa ameshafungua mlango na alimwangalia kwa tabasamu.
“Regi Babe , kumbe una wasiwasi mno juu yangu , sikujua hapo kabla”Aliongea Hamza.
Regina alitaka kukataa lakini aliona haitokuwa vizuri , aliamini kufanya hivyo ni kama kumwambia Hamza aende kwa Yulia kitu ambacho hakutaka kitokee, hivyo haraka haraka alibadilisha topiki.
“Kwannini jana hukurudi?”
“Ah.. jana nilikutana na rafiki yangu wa kitambo , hivyo tulitumia siku nzima kusherehekea na kujikumbushia, sikukumbuka kukuambia , nadhani unajua ni kwa muda mrefu nimeishi peke yangu”
“Unaweza kuendelea na mazoea yako tu , isitoshe nina kazi nyingi za kufanya na napata amani zaidi ukiwa haupo”Aliongea na kumfanya Hamza kukamaa mwili baada ya kujihisi kumbe ni mzigo.
Muda huo hakuna aliongea neno na kufanya hali kuwa kimya , Regina aliishia kumwemwesa lipsi zake , hakujua cha kuongea lakini kwenye moyo wake bado alikuwa na wasiwasi juu ya Yulia.
“Regina bado una wasiwasi juu ya Yulia?”
“Nini kilichotokea kati yenu , haijawahi kutokea akajali kinachoendelea kwenye familia yetu , unaonaje ukinipa maelezo”Aliongea
“Anachopenda ni kuniona nikipigana , sina mahusiano yoyote nae, kwa mudu sasa alikuwa akinibembeleza niwe bodigadi wake , usimzingatie Yulia ni mwanamke mjanja sana na muda wote anapanga kutega watu na hajawahi kuona hasara yoyote ya kile anachokifanya hata kiwe kibaya ,ana mawazo juu ya vitu visivyowezekana hivyo usije kumruhushu akakuingia kichwani”
“Yulia familia yake anayotokea sio ya kawaida , ijapokuwa mpaka sasa hivi sijui kwanini familia yake imekuwa tishio sana lakini ni ngumu mwanaume wa kawaida kukubalika ndani ya familia yake , usianze kucheza cheza huko nje na kusababisha matatizo maana sitokusaidia”Aliongea kwa kuonya huku akiweka maneno ya kumtishia kidogo Hamza akitarajia ataogopa lakini baada ya kumwangalia usoni aligundua hakukuwa na wasiwasi wowote kutoka kwa Hamza
“Hii ni mara ya kwanza kuwa hivi , kwahio siku hizi unajali sasa ni mwanamke gani natoka nae , usiniambie unaona wivu?”Aliongea Hamza na Regina uso wake ulianza kuwa yai na kujiambia kwanini anapenda sana hizo topiki.
“Hamna .. siwezi kuwa na wivu nakutahadharisha tu… Ahhhh!.. unafanya nini”
Hamza hakutaka hata kumsubiria Regina kumaliza kuongea kwani alimshika kiuno na kumbeba juu juu na kumwingiza ndani ya chumba chake.
Baada ya kumfikisha bila ya kumjali kama ni bosi wala nani alimrushia kitandani na kisha kumpandia kwa juu huku akiwa amemshika mikono na kumzuia kurusha miguu kwa kwa miguu yake.
Akiwa ameinama walijikuta wakiangaliaana kwa jiuu na chini huku pua zao zikiwa zimepishana sentimita chache.
Regina aliishia kuchezesha kope za macho yake kwa haraka haraka akionekana kutetemeka , alijua ilikuwa ngumu kujichoropoa hapo kwa kutumia nguvu zake pekee.
Hamza aliishia kumwangalia mrembo huyo na tabasamu lililojaa nia ovu na alimsogelea sikioni na kumnong’oneza.
“Wife ongea ukweli wako , una wivu mimi kuwa na wanawake wengine”
“Sio wivu, niachie”
“Usipokubali kuongea sikuachii”Aliendelea kupigilia msumari huku akicheka kifedhuli akinusa shingo ya Regina.
“Wife umejipulizia marashi sasa hivi ni nini , kwanini unanukia sana”Aliongea Hamza lakini Regina muda huo aliona yanakwenda kumshinda.
“Hamza niachie bwana… sipendi hivyo…”
“Usifanye chochote” Aliongea Hamza huku akimsogezea uso wake karibu kabisa kiasi cha pua zao kugusana.
Kitendo kile kilimfanya Regina kuwa mwekundu kama yai huku macho yake akionekana kutaka kulia.
“Wewe endelea kunifanyia hivi.. nita.. nita …” Hakujua hata aongee nini.
“Unataka kuongea nini , unataka kusema utanikata mshahara , nikiendelea na ninachopanga kwa usiku huu mmoja sitojali hata unikate mshahara”Aliongea.
“Usiku mmoja!!?”Aliongea huku akili yake ni kama ukichaa uliopotea unaanza kumvaa.
“Unashangaa nini , sisi ni mume na mke kisheria , sidhani litakuwa kosa tukilala pamoja?”
“Kama tukiendelea nini kitatokea kati yetu?”Aliuliza.
Hakuelewa kwasababu alijua ndoa yao ni ya mkataba tu , pengine kwa kinachofanyika muda huo alipaswa kukasirika lakini alijishangaa alishindwa kabisa kushindana na Hamza.
Lakini muda huo ni kama wazo lilimwingia na kujiuliza au nimsikilize bibi kile alichoniambia , aliamini ili kuweza kumfanya Hamza kuwa upande wake kama bibi yake alivyomwambia basi anapaswa kulipa gharama hata kama ilimaanisha kuutoa mwili wake.
Muda huo aliiona jambo la msingi sio swala la hisia zake kwa Hamza wala mahusiano yao.
“Sipo tayari kumuona Yulia akimchukua Hamza”Aliwaza mwanake huyo,kwa haraka haraka alipima faida na hasra na kuona hata kama ikitokea akifanya kwa mara ya kwanza na Hamza isingeleta picha mbaya kwani licha ya mkataba wao lakini kisheria ni mume na mke.
Baada ya kufikiria kwa haraka juu ya jambo hilo aliamua kujilegeza na kuacha kushindana nguvu na Hamza na palepale alifumba macho yake kusubiria chochote kila kitakachomkuta kama tu ndio njia pekee ya kumbakisha Hamza kwake.
Lakini licha ya kusubiri kwa dakika mbili zote hakuweza kuhisi kitu chochote kinachoendelea na kumfanya afumbue macho yake na alijikuta akimwangalia Hamza kwa mshangao.
Lakini muda huo Hamza alikuwa akimwangalia mrembo huyo na macho yaliojaa upole.
“Wewe.. shida nini?”Aliongea Regina akionekana kushangazwa na Hamza mbona haendelei.
“Kaoge upumzike , naamini utakuwa umechoshwa na kazi”Aliongea Hamza huku akimwachia na kumfanya Regina awe ni kama haamini kama Hamza amemuacha salama.
“Kwanini?”Aliuliza kwa shauku , hakujua ni sababu gani ambazo zimemfanya Hamza kuishia njiani na alitaka kujua.
“Kwa kilichotokea kule chini nishajua tayari unanipenda ila unaona aibu ya kukubali, lakini bado unaonekana haupo tayari kwa hili maana ghafla tu umegeuka kuwa kama sanamu juu ya kitanda , hakuna ushirikiano wowote na siwezi kufanya kitu ambacho haupo tayari kufanya”
Regina aliona ilikuwa kweli maana hata yeye hakujua moyo wake ulikuwa katika upande upi kwa wakati huo , isitoshe hajawahi kupenda na hakujua kama hisia zake ni za mapenzi au ni hisia za kutotaka kuwa mpweke.
Lakini hata hivyo alijikuta akijisikia vizuri na kufanya damu yake kuchemka, ilionekana Hamza alikuwa akijali hisia zake kuliko kitu chochote, maana kwa mwanamke mrembo kama yeye mbele ya mwanaume katika mazingira kama hayo asingekuwa salama hata kidogo.
“Basi naenda kulala , pumzika mapema kesho jumatatu”Aliongea Regina na kisha alitoka ndani ya chumba cha Hamza.
Baada ya Regina kuondoka Hamza aliishia kujilaza kwenye kitanda kivivu akionekana kama mtu ambae anaweza, ukweli aliona alikuwa na safari ndefu kwa Regina , japo mwanamke huyo alionyesha hisia za wivu lakini haikumaanisha alikuwa akimpenda moja kwa moja na kujikabidhi kwake kwa hiari.
Isitoshe pia alijua Regina alikuwa mgonjwa na bado hakuwa na uelewa na ugonjwa wake ulivyo maana hakumuuliza, kutouliza sio kwamba hakutaka kujua bali aliamini ni Regina mwenyewe ambae anaweza kuchukua jukumu hilo la kumwambia.
Lakini kwa namna moja aliona Yulia ni mwanamke ambae muda wote anamtafutia matatizo , maana kama sio hivyo asingekuja nyumbani kwake kutangaza vita, ilikuwa bahati tu Regina hakuwa mwanamke wa kawaida la sivyo asingeweza kumshinda mwanamke mwenye hila nyingi kama Yulia.
Muda ambao Hamza anataka kuvua mavazi yake kwa ajili ya kwenda kuoga simu yake ilianza kuita na alishangaa kidogo maana muda ulikuwa umeenda.
Baada ya kuangalia namba inayompigia alishangaa kidogo maana ni muda hawajawasiliana.
Alikuwa ni Irene mwanafunzi wa Advance shule ya Alpha ambae alikuwa akimfundisha tuwisheni miezi kadhaa iliopita kabla ya kuacha, Hamza alishangaa kwanini msichana huyo anampigia ila hakutaka kujiuliza sana kwani alipokea palepale.
Kitendo cha Hamza kupokea simu tu alichoweza kusikia ni sauti ya kilio cha mwanamke.
“Irene kuna nini!?”Aliuliza Hamza kwa mshangao.
“Hamza where are you ? , I feel so terrible …”Sauti ya kike ilisikika huku ikiambatana na kilio.
“Nipo nyumbani , nini kinakufanya ulie?”Aliuliza Hamza huku akijaribu kumsikiliza kama msichana huyo anamtega kama siku zote.
“Sina pakulala…, Sina pakwenda Hamza”Aliongea na kumfanya Hamza kushangaa.
“Hebu nyamaza kwanza uniambie nini kimetokea , kwanini unasema huna pakulala wakati una nyumbani kwenu”
“Baba kamfukuza mama na mimi anasema hataki kuniona pia..”Aliongea mrembo huyo na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.
Ukweli ni kwamba tokea aanze kwenda nyumbanni kwa Mama Irene hakuwahi kukutana na baba yake Irene hata siku moja ila hakuwahi kuuliza pia.
Hamza alijua pangine ni mgogoro ya kindoa imeibuka, lakini bado hakumuamini Irene moja kwa moja , lakini hakutaka kupotezea pia, aliishia kujikuna kichwa huku aking’ata meno kwa uchungu wa kuharibiwa ratiba yake ya usingizi.
“Niambie uko wapi?”
“Nipo Masaki Karnitas Restaurant mkabala na CCBRT hospital’Aliongea na kumfanya Hamza kuanza kukuna kichwa tena maana kutoka Kigamboni mpaka Masaki ilikuwa mbali japo si mbali sana kwa usafiri binafsi.
“Kaa hapo hapo usiondoke nakuja” Aliongea Hamza na kisha hakujali kubadilisha tena mavazi alishuka mpaka chini na aliona akienda na usafiri wa uma angechelewa hivyo aliiba ufunguo wa Maybach ya Regina na kisha kuliwasha na kuondoka .
Muda huo na mvua haikuweleka imetokea wapi ghafla lakini ilianza kunyesha mfululizo.
Hamza alichukua maamuzi ya kwenda kwasababu ya Mama Irene , kipindi ambacho anaanza kumfundisha Irene alitendewa wema sana na mama huyo ikiwemo kumlipa hela kubwa tena hata kabla ya muda na hata kuacha kwake kazi ya kumfundisha Irene ni kwasababu ya heshima aliokuwa amejenga kwa mama yake , alijua msichana huyo alikuwa akimtega kimapenzi na hakutaka kumgusa kutokana na kuaminiwa na mama huyo.
Ilikuwa usiku wa saa tatu hivyo hakukuwa na foleni kubwa na ndani ya nusu saa tu aliweza kufika Masaki na kwa kutumia GPS aliweza kuufikia mgahawa wa Karnitas na kusimamisha gari pembeni.
Kulikuwa na mvua na Hamza hakutaka kushuka kwenye gari hivyo alimpigia simu na kumwambia atoke aingie kwenye gari.
Zilipita kama sekunde kadhaa Hamza aliweza kumuona msichana akitoka nje ya mgahawa ule , kulikuwa na magari kadhaa kando kando ya barabara ikiweo gari yake.
Irene alikuwa mwanamke mrembo mno , pengine kutokana na uzuri wa mwanamke huyo ndio maana Hamza aliachaga kumfundisha maana alijua asingewea kuhimili mitego yake.
Hamza alimwangalia tu namna anavyohangaika na kujiuliza kuna wazee ni wakatili wanafukuzaje mtoto wa kike nyumbani usiku usiku tena mzuri namna hio , si ni kama kumwambia aende akajiuze.
Hamza mara baada ya kuona Irene anashangaa shangaa ilimbidi kupiga honi huku akiwasha taa za gari na kufungua kioo upande wa dereva akimpungia mkono.
Mrembo huyo mara baada ya kuangalia gari aliokuja nayo Hamza ni kama alishikwa na mshangao , ilikuwa ni usiku lakini gari aina ya Mercedenz Benz Maybach ni chache sana barabarani kwa Tanzania na pengine hakuna kabisa hivyo mtu yoyote angeijua.
“Unashangaa nini unanyeshewa na mvua , ingia kwenye gari?”Aliongea Hamza , alijua kwanini msichana huyo alikuwa akishangaa , isitoshe tokea aache kwenda kwao maisha yake ni kama yamebadilika.
Irene mara baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida hakuongea kingine na aliingia kwenye gari huku akiliita jina la Hamza kana kwamba hakutegemea angekuja na kumkumbatia kwenye shingo huku akianza kulia kwenye kifua chake.
Na Hamza alivyomshika nguo zake aligundua alikuwa ameloa karibia nguo zote, ilionekana alikimbia kwao mvua ikiwa inanyesha.
“Irene tulia , nipo hapa kwa ajili ya kukurudisha nyumbani kwenu na si vinginevyo”Aliongea Hamza.
“Siendi nyumbani nyumbani hata kwa fimbo , baba hataki kabisa kuniona”
“Irene acha utoto ujue , mama yako alishawahi kuniambia ulitoroka nyumbani na kwenda kuishi Mwenge wewe kisa ulifokewa”Aliongea Hamza.
“Sitaki kwenda nyumbani wala kwa ndugu yoyote , haiwezekani makosa ya mama anibebeshe mimi kwa kuniita Mal*ya”Aliongea na kuanza kulia upya.
“Nini kimetokea !?”
“Mimi sijui ila Baba nimesikia akisema mama anamsaliti na jirani yetu ambae ni msanii wa Bongo Movie…Hamza sitaki kuzungumzia hili please naomba unipeleke unapoishi , sitaki kurudi nyumbani..”
Hamza mara baada ya kusikia ombi hilo hakutaka kuvuta picha muonekano wa Regina utakavyo kuwa , licha ya Irene kuwa mwanafunzi tu wa High School lakini asingekubali kirahisi wakae nyumba moja.
“Nyumbani ninapoishi hapana.. nitakupeleka hotelini”Aliongea.
“Hotelini!?”Aliuliza kwa mshangao na Hamza alitingisha kichwa akiwa siriasi huku akigeuza gari.
“Okey , nipo tayari kwenda popote , ili mradi isiwe nyumbani”Aliongea na Hamza alikubali na kuondoa gari.
“Nitakupeleka hoteli za karibu , shule unaendaje bila sare?”
“Tupo likizo, twende hoteli ya mbali’Aliongea na Hamza upande wake hakutaka kumwitikia kwa kila anachoongea ila alishachagua hoteli ya kumpeleka.
Dakika chache Hamza alikuwa ameshamfikisha Dosam V hoteli, hoteli ambayo ndio kwa mara ya kwanza alikutana na Regina , hoteli hio alikuwa pia akijua ni mali ya kampuni ya Dosam.
Baada ya kwenda mapokezi Hamza alitoa kadi yake ya benki, alikuwa na kitita cha kutosha alichopata katika mashindano ya Baskatball hivyo kwake kulipia chumba kwenye hoteli ya hadhi kama hio halikuwa tatizo.
Wakati Hamza anatoka mapokezi ndani ya hilo eneo kama angeongeza umakini angegundua kuna mtu aliekuwa akimfahamu alikuwa akimwangalia kwa macho ya mshangao na shauku.
Mtu huyo alikuwa ni mwanafunzi mwenzake , msichana ambae alimkataa baada ya kuziweka hisia zake hadharani kwenye kadamnasi ya watu, alikuwa ni Anitha na alitaka kunyanyuka kumkimbilia lakini alisita kufanya hivyo mara baada ya kumuona Chriss anasogelea eneo hilo.
Ki ufupi ni kwamba Chriss na Anitha walionekana kuwa wapenzi na wapo eneo hilo kula bata pamoja , Hamza angegeuza uso wake Chirss angemuona.
“Mbona umekodolea macho upande ule , kuna nini?”Aliuliza Chriss huku akiangalia upande ambao Anitha alikuwa akiangalia lakini aliishia kuona mgongo wa mwanaume ukitokomea kwenye lift na hakuweza kumtambua kama ni Hamza.
“Hakuna tu , kuna mtu nilidhani nilimfanananisha”Aliongea Anitha huku akijitahidi kulazimisha tabasamu.
“Huyu Hamza kwanini ajitokeze sasa hivi , ashanipotezea mudi tayari”Ndio kitu ambacho alikuwa akiwaza huku kwa namna moja akishangaa pia.
Ijapokuwa hakuwa mshamba wa kuingia hoteli za hadhi ya juu kama hizo lakini kwa Hamza ambae alimjua chuoni kama masikini sio mtu wa kuingia kirahisi na kulipia hapo tena akiwa na mwanamke mrembo na mbichi kuliko yeye.
Ndio Irene alikuwa mrembo kuliko Anitha na alionekana mbichi mno kuliko yeye ambae ashaanza kuvaa sidiria.
“Nenda kaoge sasa, nishamwambia mhudumu akusaidie upate nguo zingine za kubadilisha”Aliongea Hamza mara baada ya kuingia ndani ya chumba.
“Sawa”Aliongea Irene huku akimwagalia Hamza kwa macho ya kusita sita
“Lakini si huondoki , unalala hapa hapa?”Aliuliza.
Hamza alitaka kusema kwamba anaondoka lakini muonekano wa kutia huruma wa Irene ulimfanya aone pengine kubakia inaweza kuwa vizuri zaidi na asubuhi ampeleke kwao.
“Nipo usiwe na wasiwasi”
Baada ya kuongea kauli hio Irene ni kama alipatwa na uhakika wa jambo flani na kimya kimya aliingia bafuni na kumuacha Hamza akiwa amekaa kwenye kiti na kutoa simu yake ili kufanya mawasiliano.
Mpango wake ulikuwa ni kumpigia mama yake Irene ili kumpa taarifa alikuwa na mtoto wake ili asije kujibebesha kesi ambayo haimuhusu.
Hamza mara baada ya kupiga simu kwa bahati nzuri ilipokelewa na alimweleza Mama Irene juu ya binti yake na Mama huyo alionekana kushangaa sana huku akimlaumu mume wake kwa kusema hata kama alikuwa na hasira na yeye asingezitolea kwa Irene, aliishia kumshukuru mno Hamza.
Mama Irene alimwambia Hamza atawasiliana na shemeji yake yaani mdogo wake mume wake ili ikiwezekana asubuhi amchukue[DI1] Irene kwenda nyumbani kwake kwani yeye yupo Morogoro.
Muda huo alivyokata simu mlango wa chumba chao uligongwa na mhudumu alifika akiwa na nguo za aina tofauti ikiwemo za ndani na nje na Hamza alitingisha kichwa kuridhika na alipokea na kwenda kuweka kwenye mlango wa bafuni.
“Irene nguo nimekuwekea mlangoni vaa ukimaliza”Aliongea Hamza na Irene aliitikia na kumfana Hamza kurudi kwenye sofa na kuegamia.
Lakini dakika mbili mbele Irene alitoka bafuni akiwa hana nguo hata moja mwilini na kuja kusimama mbele ya Hamza, kitendo cha kunyanyua kichwa na kumuona hana alichovaa alijikuta akishangaa mno.
“Wewe unafanya nini?!”Aliuliza Hamza maana hakuelewa au hakutaka kuelewa na Irene muda huo alikuwa na aibu za kike ziliozoambatana na ujasiri,
“Ni.. nipo tayari”
“Upo tayari kwa ajili ya nini?”
“Inamaana huelewi , kwanini unaniuliza Hamza wakati wewe ni mwanaume”Aliongea na sasa Hamza alielewa kilichokuwa kikiendelea.
Kwa picha iliokuwa ikiendelea pengine Hamza angemrukia Irene na kufanya nae , ijapokuwa aliona kakomaa lakini hakuwa mwepesi hivyo kufanya mapenzi na mwanamke kisa tu amemkalia uchi mbele yake , kama ni hivyo angekuwa ashafanya mara kibao na Dina ambae usiku wa jana alilala nae akiwa nusu uchi.
“Kwahio ulidhani nimekuleta hotelini kwa ajili ya kufanya mapenzi?”
“Kama sio hivyo maana yake nini?”Aliongea.
Haikuwa mara yake ya kwanza kwa Irene kumkukalia uchi kama hivyo , wakati anamfunndisha ilikuwa hivyo hivyo kutegwa.
Muda huo hakujua alie ama acheke maana aliona ni kama msichana huyo bado hajabadilika na pengine hata kupiga simu na kutokwenda kwa ndugu hio ndio sababu.
“Hey! Nimekuja kukusaidia na sijafikiria mbali hivyo , au kwenye macho yako unadhani mimi ni mnyama nitakupalamia tu bila kufikiria, Irene nadhani nishakuelekeza mara nyingi juu ya hili”
“Lakini kipindi kile ulikuwa ukikataa kwasababu ni nyumbani na leo tupo wenyewe tu na umesema huondoki na kitanda ni kimoja… au nimekuelewa vibaya?”Aliongea na Hamza hakutaka kumwangalia zaidi akiwa uchi mbele yake na alienda bafuni na kuchukua zile nguo na kumpatia.
“Vaa kwanza nguo zako na acha kufikiria ujinga , nishakwambia soma kwanza umalize ndio mambo mengine yaendelee , kwanini huelewi tu?”Aliongea Hamza na kauli ile ilimfanya Irene machozi kuanza kujitengeneza kwenye mboni za macho yake alihisi ni kama anaonewa ilihali anajiona mtu mzima.
“Kama hutaki ungesema mapema , nimekuonyesha kila kitu kwnaini unanikataa?”
“Irene ukiendelea na ujinga wako nitakuacha ulale mwenyewe?”
“Wewe sema tu uvumilivu unaanza kukushinda kwa kuniona hivi?”
“Ni mara ya ngapi hii unanionesha. hebu nenda kavae nguo huko”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Irene kwa hasira kwenda kuvaa nguo na ndani ya dakika chache tu aliweza kurudi huku akiwa mwekundu , alikuwa mweupe kama mama yake.
“Nishaongea na mama yako,Uncle wako kesho asubuhi atakuja kukuchukua”Aliongea Hamza na Irene alimwangalia tu bila kuongea chochote, licha ya kukataliwa na Hamza bado hakukata tamaa.
“Sasa si uande kitandani au unataka kukesha kwenye hilo sofa?”
“Wewe huogopi naweza kugeuka Simba na kukurarua”Alitania Hamza.
‘Kama ningekuwa naogopa ningetoka uchi bafuni na kukuonyesha kila kitu?””
“Unaonekana bado upo bikra , kwannini unataka kupoteza ulichotunza kihasara hasara namna hio?”
“Kama Baba yangu Mzazi ananiita Kahaba na kunifukuza nyumbani kwanini nijali , si bora nikutafute wewe ambae naweza kukutegemea, Hamza nipo tayari kukupa chochote sio kwasababu mimi ni Ma*ya nakupenda ndio maana…”
“Sijasema wewe ni M*laya na hata baba yako hajamaanisha pengine ni hasira tu”Aliongea .
“Baba ana hasira kweli , kamfumania mama mara mbili na yule Mgosi, ila mara zote amesamehewa”Aliongea na kumfanya Hamza kushangaa kidogo ukweli hakuwahi kudhania Mama Irene anaweza kuchepuka , lakini hata hivyo alikuwa mwanamke haswa na bado hajazeeka ilikuwa sahihi kupata vishawishi , kingine kwa muda wote ambao alifundisha nyumbani kwake hakumuona mume wake ikimaanisha alikuwa mpweke kwa muda mrefu.
“Baba yako anafanya kazi gani?” Aliuliza Hamza.
“Baba anafanya kazi kitengo cha usalama wa Taifa , wakati ule unaanza kuja kwetu alikuwa Jamhuri ya Czech kikazi , sasa hivi amerudishwa Ikulu”Aliongea na kumfanya Hamza kuona ndio maana kagongewa,hakuna kazi ambazo zinawafanya wanaume kuwa bize kama za vitengo vya usalama.
“Hamza kama nikikupa bikra yangu siku moja si hautoniacha?”
“Nishakuambia ukiendelea kuongea ujinga nitaondoka”
“Unajifanyisha hunipendi lakini umekuja nilivyokupigia simu?”
“Nimekuja kwasababu wewe ni mwanafunzi wangu hakuna sababu nyingine , kama unataka kunitunuku maliza Form Six kwanza na faulu kwenda chuo nitakufikiria upya
“Jamani mpaka nimalize Form Six, mimi ni mtu mzima tayari , nina marafiki wana wanaume hadi watatu watatu halafu wewe unanina mtoto,unanikasirisha”
“Wewe ni mtoto kwa macho yangu , hebu lala huko?”Aliongea.
Hamza hakuwa na mpango wa kulala kitanda kimoja na Irene alimjua hashindwi kuamka usiku na kumkuta yupo bize na kiungo chake hivyo alijiegamiza kwenye sofa kuutafuta usingizi.
Asubuhi ilipoingia kilichomtoa Hamza usingizini ni mlango wa chumba kugongwa kwa nguvu na ilimfanya Hamza kushituka haraka haraka na kwenda kuufungua na mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni mhudumu wa kike nyuma yake kukiwa na mwanaume mrefu mweusi alievalia suti na alivyomuona ni kama alionyesha hali ya kushangaa kidogo.
“Irene yupo wapi?”Aliongea
“Kaka samahani , huyu baba anamtafuta binti yake na tumeshindwa kumzuia , tunaomba radhi..”Aliongea akianza kujitetea ila Hamza alimpa ishara asiwe na wasiwasi na anaweza kuondoka.
Comments