Mzee huyo alionekana kuwa na haraka , japo Hamza alikuwa hamjui lakini kuna kitu ambacho alikiona kutoka kwa huyo mwanaume , ilionyesha alikuwa akimfahamu japo hakujua kivipi.
“Daddy!!”
Sauti ya Irene ilisikika nyuma ya Hamza , ilionekana hata yeye alishituka baada ya mlango kugongwa na alimwangalia baba yake kwa macho yaliojaa hasira.
“Irene naomba unisamehe binti yangu , nimekukosea jana , Dadd amekosea na hatorudia tena ..”Aliongea huku akimpotezea hata Hamza na kwenda kumshika mikono Irene.
“Ulinifokea jana na kunitolea lugha chafu..”
“Nilikuwa nimechanganyikiwa na pombe zilinipanda kichwani…”Aliongea kwa kujitetea , ukweli kama mwanaume Hamza alimuonea huruma mwanaume mwenzake kusalitiwa.
Waswahili wanasema ‘kugongewa’ kusikie kwa jirani tu, halikuwa jambo jepesi na aliona hata kwa Irene ni swala ambalo litamuathiri sana.
Irene hakuwa na sababu ya kumkasirikia baba yake , isitoshe alikuwa akimpenda na alimchukia mama yake kwa kumsaliti baba yake na waliishia kusameheana.
Lakini ndio muda ambao mzee huyo alianza kushikwa na wasiwasi kama hakuna kitu kilichomtokea binti yake , Irene ilibidi amhakikishe hakuna kilichomtokea na alipatwa na ahueni japo sio kwa asilimia mia.
Ukweli licha ya kumfukuza Irene hakujua hata alimfukuza saa ngapi maana alikuwa amelewa chakali na alikuja kukumbuka asubuhi akimfukuza Irene na alivyoenda kuangalia chumbani kwake na kutomkuta ndio alipatwa na wasiwasi na mtu wa kwanza kumkumbua alikuwa mdogo wake , alijua Irene ataenda Bunju kwa mjomba maana ndio mtu aliemzoea lakini alivyopiga na kuambiwa yupo Dosam V Hoteli ndio alikimbia mkukumkuku huku akiwa na wasiwasi baada ya kugundua mvua ilinyesha sana jana, japo ya kupokea lawama kibao kutoka kwa mdogo wake hakujali tena.
“Mr Hamza asante sana kwa kumfanya binti yangu kuwa salama”Aliongea.
“Usiwaze mzee , Irene ni mwanafunzi wangu nisingemuacha ananyeshewa na mvua”
“Hivi ni kweli umekuwa mwalimu wa Irene , nimesikia leo ila sikuamini?”
“Ndio ila nilipatwa na ubize ndio maana sikuonekana tena”Aliongea na kauli ile ilimfanya bwana huyo kumwangalia Hamza kwa macho yaliojaa wasiwasi.
“Hamza nakushukuru kwa yote uliomfanyia binti yangu na kuhakikisha yupo salama , yalikuwa makosa yangu kumfukuza nyumbani hivyo siwezi kumlaumu mtu , lakini kwanzia sasa naomba ukae nae mbali , bado ana safari ndefu ya kimasomo…”Alitaka kuongea zaidi lakini Hamza alimzuia.
“Mzee kwanza kabisa niseme mimi nimeoa , pili hatuna ukaribu wala mimi sio mwanafunzi wako kiasi cha kutaka kuanza kunifundisha cha kufanya kilichotokea kuwepo hapa ni ukarimu tu na kujali usalama wa msichana mdogo kufukuzwa na baba yake nyumbani”
“Ah , kumbe umeoa?”Aliuliza huku akionyesha mshangao na Hamza aliishia kutingisha kichwa.
“Kama ni hivyo basi nimeridhika na maneno ya Irene , sisi wanaume ni waaminifu sana ndio hivyo tu , kwa mtu kama wewe unaefahamiana waziri Mulumbi sio mtu wa kukurupuka”Aliongea na kumfanya Hamza kujua sasa wasiwasi umetokana na nini.
Mulumbi ni Waziri wa ulinzi ambae alikutana nae jana wakati akiwa na Afande Himidu katika viwanja vya bata.
Upande wa Irene mara baada ya kusikia kauli hio ya Hamza kuoa uso ulijikunja na alimwangalia Hamza kwa macho yaliojaa machungu.
Ilikuwa ni Jumatatu hivyo Hamza aliagana nao haraka haraka na kuianza safari ya kwenda kazini.
Kutokana na foleni kubwa barabarani alichelewa kufika kwa zaidi ya nusu saa na mara baada ya kupeleka gari kwenye maegesho aliweza kuona Aud Q8 nyeusi na moja ka moja alijua Regina ashafika.
Hamza mara baada ya kuingia ofisini kwake hakupewa kazi nyingi sana kama mwanzo na ilimfanya kushangaa maana sio kawaida ya Linda na alijiuliza nini kimetokea mpaka mwanamke huyo kubadilika , sio hivyo tu hakuonyesha ile hali ya dharau aliokuwa nayo mwanzo bali ni kama alikuwa akimuogopa.
Asichokijua Hamza Linda alifokewa mara baada ya kumwagiza kwenda kudai mkopo makao makuu ya kampuni ya Dede.
Mchana ulipofika Hamza alishuka chini kwa ajili ya chakula cha mchana na aliweza kumuona Yonesi akiwa amekuja kazini na alikuwa amekaa sehemu yake ile ile ya siku zote.
Alikuwa amevalia suti nyeusi , rangi ambayo ndio sare kwa watu wa usalama ndani ya jengo hilo lakini kutokana na suruali yake kumbana ilifanya wanaume kumwangalia kwa macho ya tahadhari, walikuwa wakimtanani na kumuogopa kwa wakati mmoja.
Yonesi ni kama alikuwa ametarajia Hamza atafika kwenye meza yake maana hakuonyesha kushangaa zaidi ya kuinamisha kichwa chake chinni akiendelea kuwa bize na kula.
“Kapteni hatimae naona umekwisha kupona kabisa na ari ya kufanya kazi imerudi”Aliongea Hamza lakini Yonesi hakuongea kitu.
“Kapteni mbona kimya tena , leo sijakuchokoza ila kwanini unanipotezea?”
“Wewe ni mume wa bosi, hata kama wafanyakazi wote hawajui napaswa kujiweka mbali na wewe”Aliongea kwa kauli hafifu na hata bila ya kumaliza chakula chake alisimama akitaka kuondoka lakini Hamza alimzuia.
“Kapteni umeongea kitu ambacho hakipo sahihi , kwani kuna kosa lolote kukaa kama hivi , ukinikimbia kama hivi si itamaanisha kuna kinachoendelea kati yetu , Au Kapteni ushaanza kunipenda nini?”Aliuliza Hamza.
“Sijaanza chochote , unaongea ujinga gani?”Aliongea huku akishikwa na aibu na kugeuza uso wake pembeni.
“Hutaki hata kuniangalia usoni, najuaje kama kweli hujaanza?”
“Haya nimekuangalia sasa , umefurahi?”Aliongea Yonesi huku akimkodolea Hamza macho kwa hasira lakinni Hamza hakuchukulia upande wa hasira bali aliangalia uzuri wa mjeda huyo.
“Kama ni hivyo basi kaa chini , umalizie kula tena kama vipi uongeze kabisa maana umetoka hospitalini na kama mgonjwa unatakiwa kula ushibe”Aliongea na kweli Yonesi hakuwa ameshiba na kutokana na kwamba alikuwa mtu wa mazoezi alihitaji kula sana tofauti na wanawake wengine.
Baada ya kufikriia aliona hakuna kibaya ambacho amefaqnya na Hamza hivyo haitokuwa vizuri kuonyesha kana kwamba kuna kilichotokea , hivyo alikaa chini na kuendelea kula.
“Halafu nimekumbuka , hivi Afande Mdudu hajakusumbua tena?”Aliuliza Hamza na kumfanya Yonesi kumwangalia usoni.
“Kwannini unauliza?”
“Nina rafiki yangu jeshini ana cheo kikubwa kuliko Mdudu na nilimiomba amwambie Mdudu asikusumbue tena, ila sijajua kama kweli anaweza kumtii”Aliongea Hamza kawaida lakini kauli yake ilimwacha Yonesi na mshangao.
“Wewe ndio umefanya hivyo?”
“Nimefanya nini?”
“Jana mchana nilipigiwa simu kutoka nyumbani , ni mara ya kwanza kunipigia tokea nilivyokuja Dar”
“Oh, na wamesemaje?”
“Baba amesema hakuna ulazima wa ndoa na Mdudu tena maana wametengua posa”Aliongea na Hamza aliishia kutabasamu na kuona pengine Mdudu alikuwa mtu mzuri kama ameweza kutii mara moja kauli yake , aliona hayo yote ni kutokana na rafiki yake Himidu na pengine anapaswa kumtafuta na kumshukuru , isitoshe alikuwa akijua bado yupo mjini.
“Nadhani sio ishara nzuri kwangu , napaswa kuwa makini kwanzia sasa”Alitania Hamza.
“Ukweli nilijua baba alikuwa akinipigia kwa ajili ya kunifokea maana toka nikimbie hakuwahi kunipigia na kuniuliza chochot, lakini tofauti yake alianza kuniuliza maswali ambayo haya eleweki?”
“Amekuuliza nini?”
“Ameniuliza tu , yupo Dar huyo anaekutana na Mshauri mkuu?”
Baada ya kumaliza sentensi hio Yonesi alimwangalia Hamza kwa umakini mkubwa kana kwamba kuna kitu anakitafuta
“Kwahio nini cha kushangaza hapo?”
“Cha kushangaza kipo , nimeingia jeshini muda sana , lakini mpaka leo sijawahi kukutana na Mshauri mkuu , wanajeshi wengi wa vyeo vya chini hatukuwahi kumuona zaidi ya kumsikia tu”Aliongea na Yonesi alijua pengine Hamza ndio Mshauri mkuu.
Ki ufupi hata kwa Afande Mdudu kumjua Mshauri mkuu ni kwasababu alikuwa katika mfumo wa jeshi kitengo cha siri.
“Mshauri mkuu ni rafiki, naweza sema ni kama ndugu yangu”
“Mshauri mkuu amejiunga jeshi miaka sita iliopita na alipitia mafunzo makali na kushinda kwa maksi ambazo hazijawahi kufikiwa na mwanajeshi yoyote kihistoria na ndio ilivyokuwa rahisi kwake kupandishwa mpaka kufikia cheo cha Luteni Jenerali na inasemekana ametokea nje ya nchi kama wewe na ni mdogo kwa umri , ndio maana nikahisi niwewe”Aliongea na kumfanya Hamza aone kumbe rafiki yake Himidu amekuwa shujaa kwa mwanamke kama Yonesi, lakini hata hivyo hakupenda..
“Unaonekana kumkubali sana?”
“Kabisa , kipindi hicho kila mtu alipokuwa akimzunguzia hakuna ambae alikuwa akiamini , unapaswa kuelewa sio rahisi mwanajeshi kupanda cheo ndani ya miaka mitatu kutoka kuwa Meja mpaka kuwa Jenerali na hatimae kuwa mshauri mkuu”
“Mna mpa misifa kibao , unadhani kapanda cheo kwasababu ya juhudi zake tokea karudi , kama sio uzoefu wake aliokuwa nao nje ya nchi isingekuwa rahisi kiasi hicho mpaka kuwa mshauri mkuu , kapitia hatua za kawaida tu , alikuwa jeshini nje ya nchi na kuna ambao walikuwa wakimzidi vilevile , hebu acha kumfikiria sana kwangu ni wa kawaida sana”
Hamza sio kama alikuwa akimuonea wivu Himidu kuwa shujaa kwenye macho ya Yonesi , alikuwa akiongea ukweli mtupu licha ya kwamba ingeonekena kama ana wivu.
Yonesi pia aliliona hilo na kujiambia kwanini Hamza anaongea kama vile ana uchungu.
“Mbona povu wakati namuongelea Mshauri mkuu? , kwahio umekosa furaha kisa nimemsifia?”
“Kwannini nikose furaha wakati naongea ukweli , yeye ni mtu wa kawaida tu hivyo sikutaka uende mbali”
“Nimesikia ni mtaalamu wa levo ya mbingu , kwahio unataka kusema umemzidi?”
Hama alijiambia ndio Himidu yupo levo ya mbingu kama sio hivyo angewezaje kurudi bongo.
“Kama ni hivyo inawezekana vipi , maana huna nguvu za nishati yoyote ya mbingu na ardhi?”Aliendelea kuuliza Yonesi.
“Kwenye huu ulimwengu kuwa na nguvu sio kujifunza tu maswala ya nishati za mbingu na ardhi , kama umezaliwa na kipaji na uvumilivu , unaweza kuwa na nguvu hata bila ya kujifunza mbinu ya nishati ya mbingu na ardhi na ukamshinda hata mtu ambae yupo levo ya juu ya mafunzo hayo”Aliongea Hamza na kumfanya Yonesi kushangaa.
“Kama ni hivyo kwanini usinielekeze namna ya kuweza kuwa na nguvu?”Baada ya kusikia hivyo Hamza alijiona amekuwa mropokaji na kuongea vitu ambavyo hata hakupaswa.
“Basi tufanye hivi saa nane twende kwenye vyumba vya mazoezi na nitakufundisha kitu”Aliongea.
“Kwahio unaniambia naweza kuwa na nguvu bila ya kujifunza mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi?”
“Ndio , ila itategemea na jinsi unavyojifunza , ninachoweza kusema kama utazingatia nitakachokuelekeza , unaweza kuwa zaidi hata wavuna nishati”Aliongea Hamza na kumfanya Yonesi kushangaa.
“Wewe ni nani?, kwanini mtu ambae unafahamiana na Mshauri mkuu kuwa na mafunzo ya ajabu namna hio?”
“Kama unataka kujua , nikiss kwanza”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.
“Kafie mbali” Aliongea akionekana kuurudia uhusika wake , Hamza hata hivyo alimtania tu maana alijua ni ngumu sana kwa Yonesi kufanya hivyo.,
“Umeoa tayari , kuwa makini na mimi la sivyo nitaenda kumwambia mkeo ujinga wote unaofanya”Aliongea na palepale alichukua sahanu yake na kisha akaondoka.
Hamza mara baada ya chakula alichukua matunda kwa ajili ya kumpelekea Regina na kumsalimia pia , lakini alivyokumbuka ana siku nyingi hajamuona Eliza wala kuwasiliana nae aliona aanze kupitia huko kwanza na kumpelekea na yeye matunda.
Dakika ambayo alitaka kuingia ofisini kwa Eliza sauti ya Asha kutokea nyuma ilimwita
“Hamza unamtafuta Eliza?”Aliuliza huku akionyesha kuwa na ari kubwa.
“Ndio , yupo wapi?”
“Meneja ameomba likizo ya muda mrefu , hatorudi mapema”Aliongea na kumfanya Hamza kushangaa.
“Kwanini kaomba likizo ghafla tu?”
“Kuhusu hilo sina uhakika , lakini nadhani kuna kinachoendelea nyumbani kwao , pia nimesikia ameomba nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi kwenye kampuni tanzu , sijui sababu labda utuambie wewe Hamza”
Muonekano wa Hamza ulibadilika hapo hapo , alikumbuka mara ya mwisho alivyoachana na Eliza na wasiwasi ulimvaa palepale na kuanza kujilaumu kwanini hakumtafuta hata kwenye simu.
“Ngoja nitakucheki nikifahamu lolote”Aliongea Hamza na kukimbilia kwenye lift akipanga kwenda ofisini kwa Regina.
Regina alikuwa bize na tarakishi yake ikionekana kuna kitu alichokuwa akisoma , siku hio alikuwa amevalia shati la mikono mirefu kitambaa cha saatini na suruali ya kitambaa ya rangi ya pink.
Kwa kumwangalia kwa ukaribu usingedhania alikuwa CEO , alikuwa kama msichana wa miaka kumi na nane ambae anajiandaa na mtihani wa chuo , lakini usiriasi wake ulimfanya kuonekana mtu mzima.
“Mbona umeleta maboksi mawili , siwezi kumaliza yote”Aliongea Regina maana alishazoea Hamza ana utaratibu wake wa kumletea matunda.
“Regina nasikia Eliza ameomba kufanya kazi nje ya nchi , unajua kuhusu hili?”Aliuliza Hamza na swali lake lilimfanya Regina kuganda kabla ya kutingisha kichwa kukubali.
“Ndio nimepokea maombi yake kutoka ofisi ya rasilimali watu , kwanini nisijue wakati ndio naidhinisha”Aliongea.
“Tangu lini tokea atume hio barua,halafu kwanini hujaniambia?”Aliongea Hamza huku akionyesha kuwa na mawazo na ilimfanya Regina kuongeza usiriasi zaidi.
“Mimi ndio Mkurugenzi na yeye ni mfanyakazi wangu kama mfanyakazi katuma maombi napaswa kuwasiliana na Idara ya HR kwanini nikuambie wewe?”
“Regina unajua sijamaanisha hivyo , kama hili swala linatuhusu sisi napaswa kujua , huoni sio sawa kwa mtu ghafla tu kutaka kwenda nje ya nchi?”
“Kwahio unaona ambacho hakipo sawa kwake , kwangu ndio kipo sawa , kwanini kila kinachomtokea Eliza unahisi mimi ndio Mkandarasi mkuu nyuma yake?”
“Regina unajua sijamaanisha unachofikiria , ninachotaka kujua sababu ni nini basi”
“Kwahio unadhani nimekuficha makusudi sio ili kuwatenganisha , kama una wasiwasi sana kwanini usimtafute alipo na kumuuliza sababu niini , hujiulizi kwanini hajakwambia?”Regina alikuwa na hasira mno hasa baada ya kuhisi anasingiziwa kitu ambacho hajafanya.
“I was wrong , usiwe na hasira hivyo , nimekosea nilipaswa kujiuliza mwenyewe na sio kukuuliza wewe”Alijitetea Hamza.
“Halafu ukitoka hapa unaanza porojo ooh sijui ni wanandoa kisheria na ujinga mwingine huku unaempenda ni Eliza. At least on the surface, you should show me respect
Hii ni mara yako ya pili unanisingizia kitu cha namna hii , ushawahi kujiuliza najisikiaje?”Regina alikuwa na hasira kiasi kwamba kifua chake kilipanda na kushuka kwa kasi mno, huwa ni mara chache sana kumkuta akichanganya kingereza na kiswahili na akifanya hivyo ni kweli hasira zimemfika kooni.
Comments